Monday, 10 October 2011

Mjamzito, Kazini Moto nyumbani hakuna mapenzi, Nifanyeje?

"Habari dada Dinah,
Hongera kwa kazi kubwa unayoifanya ya kutuelimisha, ubarikiwe sana. Mimi nina umri wa miaka 28, ni mama wa mtoto mmoja na kwa sasa ni mjamzito.

Dada Dinah ninapitia kwenye kipindi kigumu kwani baba mtoto hanijali kabisa yaani hajishughulishi kunisaidia kitu chochote na anapachukia nyumbani. Hana mapenzi na mimi na nimeacha kazi baada ya manyanyaso kazini.

Maisha yangu yamekuwa na huzuni kubwa, najiona nina bahati mbaya nasijui nifanyeje? Mume wangu hana muda wa kuongea na mimi, nashindwa hata kula chakula vizuri. Naombeani msaada wa mawazo na namna ya kumfanya mume wangu anijali na kunionyesha mapenzi kipindi hiki cha ujauzito."

Dinah anasema: Pole sana, kwakweli ni kipindi kigumu kwani sasa najua mtu unavyojisikia unapokuwa mjamzito. Ni ngumu kuamini mume anaweza kumfanyia mkewe vitendo hivyo.

Nashindwa kujizuia kuuliza maswali hili:-
Kabla hujashika Ujauzito huu wa pili mliwahi kujadili suala la kuzaa mtoto wa pili au mimba imetokea tu bila kupanga?

Mimi nakushauri uzungumze na Mama mkwe wako kuhusu tabia/vitendo vya mume wako na yeye anaweza kuzungumza na mwanae (lazima atamsikiliza mama yake) na wakati huohuo zungumza na mama yako mzazi wa ndugu yeyote wa karibu kutoka upande wako na wote kwa pamoja wanaweza kuitisha mkutano/kikao.

Ikiwa mumeo ataendelea na tabia yake baada ya kikao cha familia zote mbili, usilazimishe sana na badala yake wewe tafuta namna ya kurudi nyumbani kwenu/kwa wakwe (inategemea na taratibu za huko uliko olewa) kwajili ya mapumziko mpaka utakapojifungua.

Ujitahidi kula vizuri na kujitahidi kuondoa mawazo ili usiharibu afya yako na ya mtoto tumboni. Baada ya kujifungua utakuwa na nguvu ya kukabliana na mumeo uso kwa uso na kujaribu kurekebisha tofauti zenu.

Sasa hivi jitahidi ku-focus kwenye afya yako na afya ya mtoto alafu hayo mengine yafuate baadae. Mungu akutie nguvu, akupe amani na ujasili ili uweze kujifungua salama.

Kila la kheri!

4 comments:

Anonymous said...

Pole na matatizo.
Maelezo yako nilipo yasoma bado nimeshindwa kukupata umeeleza kuhusu nini ili tuwe na maelezo ya kukusaidia.unasema ujauzito kazini kuna uhusiamo gani kati ya kazi yako na ujauzito ulionao? Kwanini unyanyaswe kwa ajili ya ujauzito? au je! Kazi unayo fanya kwakawaida haifanywi na wajawazito?
Towa maelezo kwa kina ili tukusaidie kitu kinacho elewka.Pili unasema mume wako hakusaidii napenda kujua akusaidii nini ? Hakupi mahitaji yako ya maisha au akusaidii kazi za nyumbani akusaidii nini mbona ujafafanua.. Mume aongei nawewe kwamba hayuko karibu nawewe nivyema kabla huja ona tatizo la mwenzio tambua kwanza tatizo lako anawezekana ukirekebisha matatizo yako inaweza kuwa jibu la kurekebisha matatizo ya mumeo malanyingine inawezekana kauli zako,mapokezi yako na jinsi ya unavyojiweka bila kusahau heshima yako kwa mumeo yawezekana haijakaa vizuri pia yawezekana upendi kuelekezwa na mumeo vile anavyo taka yeye.unajua hayo ndiyo mambo ambayo mara nyingi sisi wanaume uwa inatu boa sana kama mwanamke haeleweki inasababisha kukata stimu ya story na mapenzipia.

Lakini wewe dada unaonekana unayo hali ya kujihisi kukataliwa. Inayo kufanya kuto kuwa karibu na watu pia watu wamesha kusoma unaweza kujiisi una gundu au mikosi au laana kumbe siyo niwewe tu kubadilisha mtazamo uanze kuwa na mitazamo chanya kamo watu wengine unao hii wanakuxchukia.unajua Mungu alikuumba kama mche ambao haujakamilka unaitaji kumwagiliwa maji na kuwekewa mbolea ili uke na kusitawi,kazi ya kumwagamaji na kuweka mbolea ni yakwetu sisi wanadamu na wakwanza kuifanya kazi hiyo kwa uzuri zaidi ni mume wako kwahiyo usijifanye kutaka ushaui wa wana blog tu na wakati unashindwa kusikiliza ushauli wa mumeo.Wewe dada mtunze wakwako ili akutunze usidanganywe sisi tulimaliza kuku shauli tunaenda kukaa na wake zetu mabusu kwa sana na mambo yote yanayo fanyika kwenye chumba cha kuta nne yanakuwa yametulia.
Usifanye chumbanikwako na kitandachako kuwa mahakama ya kisutu utamkosa mume ujue mahakamani hakuna mapezi niheria zina somwa na adhabu zake.
Pole dada kwa yote yanayo kusibu mimi sielewi sana mambo yanayo kusibu lakini niko katika harakati za kutoa mitazamo yangu kama mojawopo lita kugusa panapo husika usisite kulifanyia kazi nakuta kia maisha mema na mumeo.

Anonymous said...

Kwa maelezo yako dada, naona Rekebisha matatizo yako kwanza. Halafu huu upumbavu wa watu kukimbilia huku kwenye blogs kutafuta solutions ipo siku utazicost ndoa za watu. Jamani, msikimbilie huku, 1st step ni kukaa na mwenzango mzungumze, pia jirekebishe tabia zako huenda ikawa ndio chanzo cha matatizo unayohisi mwenzako anakufanyia.
Jamani, jamani, jamani! Nawaasa, msikimbilie mitandaoni kuomba ushauri, huku ni hatua ya mwisho. Ongeeni na wandani wenu , ikishindikana ndo anza michakato mingine. Ushauri wa mtandaoni unahitaji hekima kubwa. anza. Halafu huu upumbavu wa watu kukimbilia huku kwenye blogs kutafuta solutions ipo siku utazicost ndoa za watu. Jamani, msikimbilie huku, 1st step ni kukaa na mwenzango mzungumze, pia jirekebishe tabia zako huenda ikawa ndio chanzo cha matatizo unayohisi mwenzako anakufanyia.
Jamani, jamani, jamani! Nawaasa, msikimbilie mitandaoni kuomba ushauri, huku ni hatua ya mwisho. Ongeeni na wandani wenu , ikishindikana ndo anza michakato mingine. Ushauri wa mtandaoni unahitaji hekima kubwa.

inzo said...

maelezo yako hayajitoshelezi,
ila kuachakazi ni makosa sana
lazima utafakari kwa nini huyo mumeo anakupotezea labda
1. unahasira
2. unamjibu vibaya
3. nyumbani hakuvutii kuchafu, vitu vipo hovyo hovyo
4.mtoto mlienae kelele za mtoto
5. kawaida yake kutokuwepo nyumbani
ongea naye umsikie anasema nini

Anonymous said...

lo watu mliochangia mada hamna hata huruma...... inaonekana nyote ni wanaume na hamjui how it feels to be pregnant. kama hamna cha maana cha kusema si msichangie mada? dada pole kwa matatizo mi naona mwambie mumeo shida ni nini na kama hakuisikilizi jiondokee uende kwenu