Monday, 1 August 2011

Kitu kidogo tu anitishia kuachana, nimuache kweli au?-Ushauri

"Habari yako dada Dinah???
I hope upo pouwa sana and well, thanks for everything you have been taught us and may God Bless u always...

My name is (dinah kahifadhi jina) am Tanzanian but currently am in Malaysia studying, I am having a problem with my GirlLover and I completely dont understand her! My girllover lives in Tanzania and am here (in Malaysia). Every end of the year I go to Tanzania to see her, I have no other reasons for me to go there apart from seeing her.

Anapenda sana kunitishia kuniacha yaani kitu kidogo tu atanuna na kunitumia msg'z kama "maisha mema na usinipige simu wala kuni text" tena kwa kosa dogo sana ambalo liko juu ya uwezo wangu, kosa lenyewe ni kutopokea sms zake kwavile network ilikuwa inamatatizo.

Pia nikifanya kosa bahati mbaya basi atanuna wiki moja au mbili, yaani nisimsemeshe. Lakini yeye akifanya kosa kama nililofanya mimi na akiomba msamaha ni hapo hapo umsamehe na usimpomsamehe hapo on the spot ataanza kunitishia kuwa "basi kama huwezi kusamehe on the spot tuachane" na kosa hilo hilo nilikifanya mimi naweza kuomba msamaha kwa wiki mbili mfululizo lakini hanisamehei and it's annoying.

Nampenda sana na nimeshamtambulisha home na yeye ameshanitambulisha kwao na familia zetu ni friends lakini hii tabia yake inaniboa sana, pia hivi vitisho vyake vya "tuachane" vinanifanya nisisome kwa raha yaani performance inashuka.

Nampenda sana na I can't afford to loose her... sasa nifanye nini ili aache kunitishia hivo vitisho au njia ni kuachana nae na nikiongea nae sometimes anakubali kuendelea na mimi but kitu kidogo anarejea hiyo tabia.

Naomba ushauri jamaa, ni kuachana nae au njia ni ipi hasa?"

26 comments:

Amos Bwire said...

If you can't afford losing her, then there is no better advice to you than to tell you "hang on." Otherwise, truth of the matter is...people who behave that way are people who usually got better alternatives. I mean, it seems like you're not alone, someone else is doing a better job to her than you do. So you better amp your game or pack and go. She doesn't feel you the way you think she does and she can afford losing you.

Anonymous said...

Pole kaka, huwezi amini mimi pia nakumbana na tatizo kama lako, nikimkosea kidogo atanuna tena unakuta ni kuchelewa kujibu txt au sikupokea simu yake! Mara nyingi tukizinguana ataniambia "kama unaona huniwezi tuachane" uwa ananifanyia mambo ambayo yanahitaji uvumilivu wala uwa sikasiriki namchukulia poa! Ila nikimfanyia same thng km alichonifanyia atanuna wiki nzima. Nimewahi kujaribu kumwacha alilia tena akadai ananipenda sana. Sasa mpk leo simuelewi, sijui nmuache kweli

Anonymous said...

pole sana .wawili nyie need to do something ambacho kitawaweka sawa kabla ya ndoa.u know ndoa ni kitu kingine tofauti na mapenzi ya kawaida ,kwa maana hiyo sasa vitisho kama hivo havitatakiwa mkishakuwa na familia.so ushauri wangu mimi naomba mtizame mbele zaidi na zaidi kwa wakati huu ambao bado hamjaingia katika ndoa iwapo mnatarajia kuoana.na kitu kingine,elimu yako ndo kitu cha kwanza so cha msingi hapo jitahidi sana mambo ya mapenzi na masomo viwe viwili tofauti otherwise u may loose in both sides.NI USHAURI.

Anonymous said...

kaka mungu ndiye anayotoa mke muombe mungu akupe mke ambaye atakuwa faraja kwako wakukuchukulia mapungufu yako katika maisha yenu ya ndoa

Anonymous said...

No one is perfect under the sun. Unachotakiwa kuangalia ni mmetoka wapi na mnaenda wapi utaachana nae and at the end utakuja kumpata mtu utasema afadhali ya yule.afu ictoshe wanaume sometym tunapenda kuwapotezea wakna dada zetu mda bila sabb toka mwanzo mlikubaliana kuwa una utakuwa na future nae so ukimuacha unadhan itakuwaje?think twice bro haya mambo sio ya kukurupuka unatakiwa kuangalia mbele hvo vitsho vckuogopeshe kikubwa its if u had a real luv with her and km nae kwel anakupenda and she is commited to u!mi nakushauri ucmpotezee mda dada wa watu we endelea nae tu,nadhan nawe una mapungufu fulani lakn anakumilia. All the best bro. Its Kev mmetoka wapi na mnaenda wapi utaachana nae and at the end utakuja kumpata mtu utasema afadhali ya yule.afu ictoshe wanaume sometym tunapenda kuwapotezea wakna dada zetu mda bila sabb toka mwanzo mlikubaliana kuwa una utakuwa na future nae so ukimuacha unadhan itakuwaje?think twice bro haya mambo sio ya kukurupuka unatakiwa kuangalia mbele hvo vitsho vckuogopeshe kikubwa its if u had a real luv with her and km nae kwel anakupenda and she is commited to u!mi nakushauri ucmpotezee mda dada wa watu we endelea nae tu,nadhan nawe una mapungufu fulani lakn anakumilia. All the best bro. Its Kev

Anonymous said...

akikuambie muachane this time act like ..its okey lets break ata mi nimechoka na huu uhusiano wa kutishiana kuachana ...uone atavyorudi akiomba msamaha..cause huyo kuna mawili la kwanza inawezekana kapata bwana huku bongo?!
au anatishia nyau

Anonymous said...

well pole sana kaka kwanini anakuzingua hvyo pole sana.nitakachokushauri na wewe tikisa kiberiti anagalau mara moja aone kuwa uko criaz....akikunyamazia chukua kifaa kingine hayuko peke yake.

Anonymous said...

Tulia na shule kijana, wanawake wako wengi wenye nia njema na wenye usataarabu wa kutosha. Dalili ya mvua ni mawingu ma siku njema huonekana tangu asubuhi.

Yaani wewe mwanaume mzima unakubali ushuke kimasomo kwa sababu ya demu?? Inawezekana na wewe hujiamini ndo maana huyo bibie anakutesa kihivyo.

Akisema tuachane mwambie hola hola halafu uone kama kweli anakuacha.Au la sivyo ana mtu mwingine anamzingua huko Bongo.Si unajua tena wasichana wakifika mahali fulani hukosa msimamo hasa kama ni mtu mpenda hiki na kile basi kila kukicha ni kudandia pale na pale.

Ninachokushauri leo ni kwamba weka jitihada yako kwenye shule achana na upuuzi huo ambao hauna maana kabisa.Watoto wa kike wamezagaa wakisaka wanaume wa ukweli wajenge nao maisha mema wewe unahangaika na mwenye roho nyeusi? Eti nashuka kimasomo,huenda ulizaliwa mwanaume kwa bahati mbaya wewe?

Rik Kilasi said...

Mie nakushauri soma kwanza hayo mambo ya mpenzi sijui girllover achana nayo kwasasa.Elimu ndio ufunguo wa maisha kama ni wasichana ukishakua na elimu yako utapata tena wa ukweli (In case huyo atakua ka move on).Suluhu ya mapenzi siku zote ni kuongea mwambie vile hupendezwi na yale anakufanyia na wala usijidanganye na hio kutambulishana watu wana engage tena kwa party kubwa na wazazi wote wanataarifiwa lkn mwisho wa siku kila mmoja anachukua 50 zake kwasababu zisizo eleweka.Kwa sasa kazana na kusoma kwanza kwani mtaka yote hukosa yote chagua moja na vile umesema wasoma basi chaguo bora ni shule.Mtazamo wangu tu huo.

Anonymous said...

Wacha nikuambieni nyie wa kaka.hao magrilover wenu bila kuficha kila mmoja anampango wake wa kando .Ukweli mwenye upendo wa kweli kwako hawezi kufanya hilo analofanya.Siku moja akikuambia tuachane mwambie sawa hata mimi ndivyo nilivyokuwa nataka uone kama alikuwa anakutisha atakupigia magoti .Angalia usije fanywa speare tail.Wasichana wa miaka hii kutunza ahadi ni ngumu sana .wewe soma utakapomaliza utapata mtu mwenye mapenzi ya kweli .Nakwambia huyo utakapomuoa utajuta kwa kifupi hapo umekosea kabisa usijari kutambulishwa .wala hutajuta maishani.Huyo mwanamke atakusumbua sana kumbuka dalili ya mawingu ni mvua funguka kaka yangu.

Anonymous said...

mmh pole kaka,huyu mdada inaonyesha anamtu anamchetu kwa sasa ndo maana anajidai kukutishia kukuacha.wewe jaribu kusema tu unamuacha walau kwa wiki u,uone atakavyoomba msamaha mana na huyu jamaa alienae akijua umemuacha nae atamuacha alafu ndo atakapoona umuhimu wako kwake.kwahiyo asikupe presha buhre GPA yako ikashuka.siwajua wanake wakidanganywa na viadventur vidogo wanaona wanapendwa kumbe nii style tu yakumpata for a nightstand na baada yahapo twasepa.

smokeless said...

Pole kijana hiyo ndio tabu ya kupenda wanawake wa kichaga, piga chini atarudi mwenyewe.

Anonymous said...

Naona wengi waliotoa ushauri kwenye hii issue ni wanaume, anyway me ni msichana na sishangai sana kwani pia nina tabia kidogo kama za huyo dada, na sio kama simpendi mpenzi wangu Nampenda sana tena sana na wala sina mwanaume mwingine na sihitaji mwingine zaidi yake, mara nyingi majibu ya hivyo huwa tunayatoa kama njia ya kujihami lakini hatumaanishi ndo mana mtu anapokwambia ok poa na tuachane una haha

Anonymous said...

we kaka hebu jichunguze vizuri,hawa dada zetu wana akili sana na ni welevu pia,hivi kweli mtu ana akili zake timamu na alikupenda kwa hiyari awe anatishia kukuacha bila sababu za msingi? kuna vitu vingi vibaya unamfanyia na amevijua na huenda unavirudia rudia ndiyo maana kafika kote huko,siku zote sisi wanaume ni dhaifu sana kuna makosa umeshamkosea mara nyingi,na kwa kuwa siku zote mkosaji huwa haoni uzito wa kosa lake ndiyo maana unachukulia na kusema vikosa vidogo vidogo,na huenda mmeshakaa na kutatua shida hizo ila kwa demu akishagundua unamsaliti inataka busara sana kumweka sawa hasa kwa madem wenye misimamo na wasiyoangalia kitu kingine zaidi mapenzi,broo kuna mahali unachemka ila hujajishitukia, shituka utakuwa wa kutishiwa kila siku na inawezekana hakutishi amedhamiria ila atakuwa anakumbuka mlikotoka ndiyo maana anakuwa na wewe mpaka leo.

Anonymous said...

sijui nisemeje mdogo wangu mtoto wangu maana sijui unaumri gani elewa tu ya kwamba dunia ya sasa kitakacho kusaidia ni elimu sina uwakika kama hutakuwa na elimu hata huyo mwanamke atakutaka maana utakuwa huna mbele wala nyuma wewe wekajitihada zako zote katika elimu kwa muda huu kwani elimu ndio mkombozi wa mambo yote wasichana wako wengi sana na wanaendelea kuzaliwa wengi tena wazuri tu sio ajabu wakwako bado hajazaliwa wewe zingatia masomo dunia ya leo bila ya elimu ya uwakika ni bure tu huyu msichana anakutingishia kiberiti nadhani anajua jinsi unavyompenda ndio maana anakutishia embu jaribu kukaza roho uwache mawasiliano naye hata cm yake usipokee umpotezee kwa mda kama vile humjui kama hakuhanyahanya kwani huyu dada ulizaliwa nnaye kwani kwa mfano tu wala simwombei mabaya ila natakusema tu mungu sasa hivi akimchukua hutaishi au na wewe tajiuwa hembu mtoto wa kiume usipende kujishusha kwa ajili ya wasichana ambao hawana msimamo na wala wajui maana ya kupendwa usipoteze muda wako bure na watu wenye matisho ya kishamba

Anonymous said...

pole kaka yangu ni kawaida kwa sisi kina dada kutafuta asurence hivyo onesha ukweli wako kwamba kweli unamaanisha but jitahidikukaza but shule ukichemka atakukimbia speed 200

manyagag said...

kiukweli huyo dada hakupendi japo unaonyesha unampenda kwelikweli.i have experience with ladies wengi wakianza kukutishia hivyo ujue kuna mtu tayari anampa kiburi mtaan.nimewahi kuambia kua
(wengi wananitaka huko nje na pesa zao alafu wewe unanidengulia kisa sikutuma vocha)its a normal thing kaka angu cha muhimu kaa nae mueleze hisia zangu na juu ya tabia yake ya kukutishia kua atakuacha.mwambie ukweli juu ya inavyokuumiza na nn hatima yake.huenda akakusikia itategeamea pia hali utakayo kua nayo wakati unamwambia.jitahidi kuonyesha hali ya kutojali hata kama mkiachana although najua itakua ngumu.

ni mtazamo tu from manyagag@gmail.com

Anonymous said...

Huyo anapenda kubembelezwa.Kwa hiyo unavyomuomba msamaha anasikia raha sana.Halafu wanawake tunapoona mapungufu ya mtu ndio hapo hapo tunapo take advantage.Ameshajua huna jeuri mbele yake ndio maana anakusumbua na amejihakikishia kumuacha huwezi ndio maana anakuzinjgua tu.Nafsini mwake anakupenda sana.Siku nyingine akikwambia nakuacha mwambie hata mimi nilifikiri iwe hivyo maana nimechoka kutishiwa.

Anonymous said...

Mie ni msichana pia,swala hli limenigusa.kaka pole kwa hlo.kuna kitu kimoja kikubwa sana tunakisahau katika mapenzi,nacho ni KUWA MKWELI NA MUWAZI,endapo mwenza anakubore kwa namna 1 ama nyngne basi mwambie kuwa hki na hiki kinanikwaza.kama tunavojua no one is perfect but unapoambiwa ur mistake jaribu kutorudia.realy hamna kitu kinachokera kama kurepeat the same mistake.na girl wako anapokuambia hvo yan ujue she is tired of tht somthn na may b humpi sababu za kueleweka tht z y.She might b real to u tht z y anakuaanajihami hvo ajue stability yako kwake na hataki kupotezewa muda.Remembr mpenzi akisema hamtaki mwenzie ujue kuna mwngne anawaza atampata lini.Sio wanaume au wanawake WOTE wanaomaanisha katika mapenzi yao nwdays ila t z better muambizane ukwel nakutatua wote kwa pamoja b read and accept weakneses ili muweke mambo sawa.
Lastly,wapenzi kutatua tatizo si kuyakimbia mana huko unapoenda wawezajuta nakusema aheri nlipotoka and when u turn back wakuta keshafanya uamuz mwngne hapo ndo kitauma zaidi,mapenz si kutishiana.!!ni hayo tu.

Anonymous said...

Kijana nakuomba soma. Huyu binti atakufanya ufeli shule au upate pass tu or gentlemen pass. Cha msingi kwako ambacho utakaa nacho milele ni elimu yako na utazikwa nayo. Mke, rafiki, kazi, mpenzi, mchumba, ndugu, etc utaachana navyo siku moja. Umekiri mwenyewe kuwa kama ukiwa na tatizo na binti hata ufaulu wako unashuka, it is obvious. Tatizo umeshalifahamu, ni huyu binti. Hebu tulia, acha mawasiliano naye mawazo yote shule. Mke au hata rafiki mwema hutoka kwa Mungu.

Pili, kama anathubutu kukutamkia kuwa muachane wakati wa urafiki.uchumba wakati hata hamjaishi pamoja ambapo hapo ndo the true colours zinaonekana jua kabisa ukifunga naye ndoa hamtadumu, expect talaka. Pole sana ila zingatia ushauri wa wadau hapa.

Anonymous said...

Kweli binadamu tunapitia mambo yanayoendana, mimi nina shida kama yako ajabu mimi ni msichana. Kuna kaka mmoja nimeanza nae urafiki kama mwaka hivi sasa, yeye akitaka chake ni hicho kiwe kizuri au kibaya kina faida au hasara... ukimbishia tu utaambiwa goodluck with your life, dont text, dont call na maneno mengine ya kuudhi.... hapa kwenye simu yangu kwa mwaka huu tu nna meseji za kuniacha hata 20 zinafika. Siku moja alivyosema tuachane nikamwambia poa, hata nami nimechoka, kwaheri......wee baada ya nusu saa nasikia gari nje... am soorry nilikasirika...sasa hivi tunaheshimiana.
Mi nakushauri, usimkwaze makusudi, na upime akma kweli ulilokosa linawarrant kuachana, kama sivyo basi mwambie sawa tuachane nami nimechoka na uhusiano usio na amani. Kama kweli anakupenda alikuwa anatingisha kiberiti atakuomba msamaha lakini kama kweli anakusudia asemacho basi mtaachana kweli. Hapo ujue ana mwanaume mwingine anayempenda zaidi yako.

Anonymous said...

mh. mtingishie kiberiti uone jeuri yake itafika wapi. mie ni mwanamke nilikuwa na mwanaume wa vitisho vya kuachana. ukifanya kitu kidogo week nzima kanuna. came to find out ana demu mwingine. i got fed up, so mara ya mwisho alivyosema tuachane nilifurahi sana. najua alikuwa anatingisha kiberiti but hiyo time nikakutana na jamaa mpya, by the time ana-realize mie i was gone for good. anajuta maana hata yule demu mwingine naye hamtaki!

Anonymous said...

trust me, mungu ana sababu zake na anakuepusha na janga so achana naye huyo asiye na msimamo!

Anonymous said...

pole kaka yangu mm ni mwanamke ila hayo maisha nilishapitia yaan ilikuwa kitu kidogo tu anadai bac tuachane smtymz nipo kazin nashindwa kupokea cm nipo na boc amenisimamia nifanye kazi yake faster lakin ht ukimweleza hawezi kunielewa, mm ni customer care smtyz naongea na wateja kwa cm ya oficn na kiukweli siruhusiwi kuwa busy na sim yangu na yy hilo analijua ila kila ck nisipopokea lazima atishie tuachana, ilifikia hatua hd mama yake mdogo aliniambia niachane nae kwanza si mwaminifu ht kidogo so akirudia kukuambia muachane mwambie ulishachoka kila mtu ashike njia yake na mpotezee kweli ht kwa muda utaona matokeo, mm ss ni wa kupigiwa magoti na kuombwa msamaha ila naweka ngumu kuonyesha msimamo wangu, kuwa makin bro

Anonymous said...

Mi nnachojiuliza, hivi watu hupenda nini? Sura? au umbo la aina fulani? Au sauti?

Manake haiingii akilini kwamba mtu unakukera na bado unasema unampenda---kinachokufanya umpende ni nini? Kama kipo kitu cha msingi kilichokufanya umpende, na kitu hicho bado kipo intact, then hicho kitabia cha kutokusamehe kitakuwa siyo issue kwako, na maisha yataendelea

Arusha Computers! said...

Duh! Pole sana ila ninge kushauri ukae nae utafute sehemu private uzungumze nae juu ya relationship yenu wote muone kama kuna kusonga mbele au msimamo wa mwenzako kwa ujumla kuliko kutishiana maana kama umejaribu kutengeneza upande wako lakini yeye hatoi ushirikiano wowote sasa hapo inabidi mzungumze na mfikie muafaka ili wewe na yeye muweze kusonga mbele na maswala mengine ya maendeleo na sio kuishi roho juu juu. Hatakama anamtu mwingine mwambie asem ili ujuwe moja vinginevyo mtapotezeana muda alafu mwishowe yakawa masikitiko na majuto wakati sasa hivi ndio vema mkajuwa muafaka wenu.