Tuesday, 16 August 2011

Asaliti ndoa yetu usiku asubuhi anaenda kuhubiri neno la Mungu-Nimfanye nini?

"Mimi ni mwanamke ambae niko kwenye ndoa miaka minne sasa. Ila ninatatizo naomba mnipe maoni na ushauri. Mume wangu ambae nilimpenda kupitiliza nimegundua amekuwa akitoka nje ya ndoa yetu pale nilipoanza kumufatilia sana ingawa alikuwa mjanja sana.

Kinachoniuma saaana huyo mwanamke aliekuwa akitoknae nilianza kumuhisia kipindi hatujafungandoa, kila siku nilikuwa nikiona msg zake akimtukana mtu fulani ila nikijaribu kumuuliza mume wangu anasema kuwa ni mambo tu ya kazini. Lakini kila nilipokuwa nikiona msg nahisi kusutwa!

Hivi sasa tuna watoto wawili na nilikuwa muamini zaidi mume wangu nakila ninapo shitukia ishu kuwa labda anatoka kusaliti ndoa yetu na kumhoji kama ni kweli, mume wangu anakasirika na kuniomba nipige magoti nisali na kuomba Msamaha.

Nilikuwa nikifanya hivyo na hata yeye kuomba pamoja nami huku maombezi yake yakiwa Mungu atupe tuweze kuaminiana. Hajawahi kupunguza mapenzi kwangu wala kuonyesha ila siku moja nimekamata msg nyingine nikajifanya mimi ni mume wangu na hapo ndipo nilipogundua mwanamke huyo anavyo enjoy na mume wangu.

Kinachoniumiza sana alikuwa akitumia rafiki yake huku mara nyingi nyingi kujifanya kuwa ni mgonjwa anahitaji kwenda hospitoli anadai asindikizwe na mume wangu kumbe ilikuwa njia yakumtoa tu. Akitoka asubuhi kusaliti ndoa yetu anahubiri Kanisani kama kawaida na huku akisukuma Injili.

Yaani nikifikiria hapo nahisi kumchukia, hata mida mingine sijisikii kumpikia kutokana na ahadi nyingi tele tele na huku akionya watu wengi kuhusu ndoa. Naombeni jamani mniambie nifanye nini kumsamehe sijamsamehe ila aliishaomba msamaha nakunieleza kuwa kila nililoligundua ni ukweli! ninaumia sana.

Nilimwambia asubiri nitampa jibu. Sasa mawazoni mwangu najiandaa na nikipata kazi nitamuacha kwani nikifanya uamzi mapema naweza kuumia sijuwi niko sahihi au nakosea?

Hii yote ni kwasababu hakuna njia nyingine ya kumuamini hasa pale anaponiambia yote "tumkabizi Mungu" nahisi hata hilo jina asiwe analitaja. Nikiwa mbali na yeye ninajihisi kufurahi nikimuona nahisi kujinyonga sasa jamani mnasemaje hapo naombeni ushauri wenu. Asante"

18 comments:

Anonymous said...

Mmmmmmmmmmmhhhhhhhhh! Pole sana dada yangu!! Mimi ni mwanaume,yaani kweli nimecheka kisa chako lakini huku nikiumia na kusikitika sana kwa zengwe hilo.Yaani sijaamini hasa paliponitoa jasho ni hapa nanukuu.."Anatoka kusaliti ndoa na asubuhi anatwanga injili"

Kwa kuwa amekiri yote, please msamehe na mwambie akirudia utamsemea huko Kanisani hadhrani.
Kosa si kosa bali kurudia kosa.Chukua muda kutafakari na kumhurumia yeye pia kwa dhambi hiyo kwani kuna kutenda kwa kuzingirwa.Tamaa huponza wengi.Mhurumie kwamba hajajijua katika hilo na uone jinsi mnavyoweza kuanza ukurasa mpya wa kuaminiana.

Usimhukumu kwa hilo tu maana umesema anakujali na hajapunguza upendo,huyo ni shetani tu kamzidi kete.Hata wewe una makosa japo hujaambiwa nini na nini unakosa.Hutakujwa kupata malaika asiyekosea. Na abda utakujapata mbaya zaidi ya huyo.

Samehe saba mara sabini na ndoa yako itadumu na kurekebika sana.Ukichukua uamuzi wa kumchukia na kumkimbia utapata mabaya zaidi kwa sababu suluhisho la tatizo ni kukaa ndani ulishughulikie.Ukitoka nje unaongeza ugumu wake zaidi.

Pole dada najua inaumiza sana lakini ndiyo hivyo ulikiri kuwa naye katika shida,huzuni,furaha nk.

Anonymous said...

I afraid to say ur husband can be hard to change his behave. Duuh! Huwa anahubiri, halafu anasaliti! Sijuwi utafanyaje! Najaribu kuvaa viatu vyako nione maumivu yake bt naona hayapimiki kwakweli!

Anonymous said...

Samahani najua Mungu anaweza yote, lakini huyu mmeo ni malaya aliyekuhubu, yaani kweli anaweza kutoka kulala na mwanamke tena akaenda kuubiri injili ya Bwana. Hapo dada sitapenda kukuzidishia machungu lakini mmeo anakuwa akikufanyia mind's game. Anajua unamwamini Mungu na kwa hivyo ukimhisi tu anakwambia eti mpige magoti mmwombe Mungu. Yaani huyo ni chui ambaye madoa doa yake hatokaa yatoke hata kama atajipaka matope mwili mzima, matope yakikauka tu basi utayaona madoa doa yake, naona umenielewa. Asikwambie mtu ndoa ni yako, kwa hiyo bibie fwata roho yako na pia hao wanao baada ya miaka 2 tusije wakuta mitaani omba omba eti kwa sababu mmoja ya wazazi wao alishindwa kuzuia tamaa za mwili. NI HAYO TU MAMIE.

Anonymous said...

Achana nae,hata biblia inasema msiachane isipokuwa kwa dhambi ya uzinzi,kama amekudhibitishia kweli anatoka nje ya ndoa,wa achana nae,Mungu atafanya njia.
Na kwa taarufa yake,mwambie Mungu hajaribiwi wala hadhihakiwa,huo unafiki anaofanya kwa Mungu wakati sio mkweli,atakufa haraka sana,we mwombee tu Mungu atajibu.

Anonymous said...

Jamani jamani wanandoa na hata wasio na ndoa,wanaume naomba msomee hii kwa makini na mkatafakari.Mnajua kwa nini kuna wajane wanawake wengi kuliko wanaume?sababu mojawapo ni pamoja na wanawake wengi kuwa tunalia na kulaani vitendo vichafu wanavyofanya waume zetu,matokeo yake Mungu anafanya kweli.Wanaume mmekuwa ni sababu ya wanawake wengi kulia kila wakati,mtu huna raha n kuwaza tu Mr leo ametoka na nani,mtu unampokea mnasex huku unawaza sijui amebeba virusi huko,sijui kuma aliyotomba ilikuwa na kisonono,ma usaha au,yani mambo mengi kichwani,unahamua kumwachia Mungu.Yani kila mwanamke ni kilio na mumewe,na kinywa kinaumba,the more unamlalamikia Mr the more the chance of laana.Ok sijui nimeeleweka,anyway tuwaombee tu mema maana mabaya tunayowaombea matokeo yake ndio tunabakia wajane.Mungu anisamehe maana hapa nimekasirika sana,hata wangu nae ni matatizo tu,kununa kwa kwenda mbele,mtu unarudi wewe usiku wa manane halafu unanuna ili tu nisikuulize,wanawake pia tunanyege jamani,tukitoka nje ya ndoa wote itakuwaje,aah,inaboa sana

Anonymous said...

Bibie pole kwa mksa huo!! Lakini una bahati kwamba huyo mumeo anamjua hata Mungu, hivyo ni rahisi mno kumrudi japo amepotoka kidogo.

Unachohitaji kufanya ni kuwa mvumilivu na pia ujue kusamehe maana usiposamehe sijui wewe utakuwa mwanadamu wa namna gani kwa sababu hata wewe una makosa japo hayajabainika wazi.

Msamehe mumeo na mwambie siku ya siku akirudia makapi utampeleka mbele ya kanisa zima ili limjue kuwa anawahubiria uongo.Ni muhimu chukua biblia halafu mwite kaa naye na muulize ni wapi pameandikwa utoke nje ya ndoa yako? Halafu mwambie kuanzia leo nimekusamehe kabisa,na usirudie.kama K yako ameichoka akuambie nini kinapungua ili ukiboreshe na wala si kubemenda nje.
Kumbuka hasira hasara,ukizidi kumshupalia na hasira utamfanya aendelee kufikiria kupata lishe hiyo huko nje,kwa hiyo mkaribishe na mlishe chakula kitamu yaani ongeza manjonjo katika mchezo, maana inaelekea labda hata wewe hujui kujishughulisha kitandani unabaki kulalama tu.

Kusamahe na kusahau ni muhimu na ndipo ndoa itadumu.

Anonymous said...

Hata me ningewaza kuondoka, nina moyo mwepesi sana na si mvumilivu na nikisema nivumilie ntakonda na kunyong'onyea mpaka ulimwengu wote ujue mume wangu kanisaliti na sizani kama naweza kusamehe wala kusahau. Hakuna kitu kinauma kama kusalitiwa na mpenzi au mume huwa najiuliza wale wanaosalitiwa zaidi ya mara moja na wanajua wanawezaje kuyabeba na kuendelea na hizo ndoa au mahusiano na hao wanaume. kwani hata kwenye biblia ruksa kuvunja ndoa kama mmoja atazini nje ya ndoa.Nakushauri fanya kile ambacho moyo wako unakutuma kwani wewe ndo unaebeba uzito wa jambo hilo

Anonymous said...

duuh pole sana dada naelewa kabisa unavyofeel,pole mami.lakini kuondoka sio solution kwa sababu una watoto na utawatesa viumbe wale,,bwana wanaume ndivyo walivyo ukimwamini sana siku ukisikia utatamani kujinyonga kweli,lakini dada vumilia,mwombe mungu ambadilishe,,wala hakuna kuondoka unakomaa hivyohivyo

Anonymous said...

Kama humtoshelezi unategemea afanya nini ili ndoto yake mapenzi itimie?

Kwani wewe huna makosa kiasi kwamba umemchukia kiasi hicho licha ya kukuomba msamaha?

Kama anahuburi huyo ndiye mzuri sana kwa sababu anajitega mwenyewe hivyo ni rahisi sana kumtegua na akarekebika na ndiyo maana amekuomba msamaha kirahisi.Wanaume ni wagumu kuomba msamaha.lakini wa kwako amekiri yote na kukuomba msamaha, sasa ulitaka afanye nini zaidi ya hilo?

Yaani wewe unaona hilo ndiyo kosa kubwa hasa kuliko yamkini makosa unayofanya wewe? MSAMEHE MUMEO MAISHA YAENDELEE!! usidhani kumkaushia utatatua tatizo labda ndo utaendelea kumfukuzia mbali zaidi.

Pole lakini maana inaumiza,ila kumbuka kuwa kukosa ni kila mtu anakosea muhimu ni kurekebisha, na lazima ujiulize kwa nini kaenda huko nje,labda wewe ndiye kikwazo.

Ukishindwa kutunza wa ndani watakutunzia wa nje.Wewe utabaki kutunza ndoa wakati wenzio wanakutunzia penzi.

Anonymous said...

dada nakushauri usamehe mumeo kwa ajili ya watoto wenu bado wadogo. pia nenda kwa wazazi wake uwaeleze na aombe msamaha mbele yao wanaume baba yao mmjoa wote wanafanana utamwacha utapata mwingine ndio itakuwa balaa bora unayemjua na amekiri na kuomba msamaha imeandikwa samehe mara saba sabini

Anonymous said...

JAMANI STORY YAKO INATIA HURUMA ILA MWOMBE MUNGU AKUFUNGULIE NJIA MAANA HAKUNA WANAUME WAKWELI SIKU HIZI NI KUCHOREKA TU KILA KONA. LAKINI AFADHALI HAPA NAJUA SIO MIMI TU NINA HAYO MATATIZO KWELI MUNGU ATUNUSURU WANAWAKE.

Anonymous said...

Pole dada kwa matatizo magumu yanayo umiza moyo wako. Kwanza namshukuru yule ambae amepata wazo la kuendesha ukurasa huu wa mahusiano.mimi ni mwanaume nina mke na ninaheshimu ndoa yangu ingawa pia inamengi magumu lakini najitaidi kuyatafutia ufumbuzi chanya.nimedumu kwenye ndoa sasa ni miaka ishirini.na sijawai kutoka nje ya ndoa.pamoja na hayo sijisifu bali ni kwa uwezo wa Mungu.kitu ambacho ningependa kukuambia nikwamba ndoa nisafari ndefu ya kufikia Lengo la maisha ya kuishipamoja kwa amani,furaha na upendom lakini yote hayo yata fikjwa endapo nyote wawili mtashirikiana kuyatafuta kwa bidii,gharama na kutumia muda wa kutosha. Tambua kwamba huyo ni mume wako nasiyo wa mtu mwingine wewwe ndiye unapaswa kumlinda kumjali na kumsaidia katika kila jambo baya au zuri.kama wewe utashindwa kumsaidia katika udhaifu alionao niwazi kwamba hakuna mtu ambae ataweza kumsaidia mumeo,kumchukia na kuto kumpikia sio jibu la kutatua shida,kitendo cha mwanaume wako kuwa na uhusiano wa nje inaonyesha udhaifu ulionao wakuto kuwa karibu na mumeo na kujua mahitaji yake bila shaka mumeo kuna kitu ana kitafuta katika uhusiano wa nje ambacho anafikiri hakipatikani kwako.jitahidi kwa akilizako zote kujua hitaji la mumewako kuliko kutumia muda mwingi kuchunguza mahusiano ya nje ya mume wako.utaumia sana kwa kuchunguza matatizo lakini uta uponya moyo wako na ndoa yako ka utajua jisi ya kuifanya ndoa yako iwe bora zaidi.kumbuka asilimia kubwa ya wanaume wana matatizo hayo cha msingi sio kuachana nae kwani hutapata mwanaume unae mtaka kwakuwa ujui yuko wapi sijui ukiweza kuumba mwanaume unae mtaka wewe.kaa na huyo mwanaume niwakwako mpende jitahidi kuvutia muonekano wako na kauli zako mbele yake ziwe zenye mvuto wa kike (mahaba)ukitangatanga usipotunza chakwako ukimwi uta wamaliza pia ni haipendezi kuolewa kila mara na kuzaa watoto wenye baba tofauti

Anonymous said...

Mleta mada nimesoma ujumbe wako kwa uchungu mkubwa sana na machozi yananitoka kwa sababu nami nina mume ambaye anajidai ni mlokole kumbe ni malaya wa kutupwa. Ana miaka 54 ila ana malaya wa umri wa watoto wake na wake za watu. Nyumbani amejaza CD za kwaya za nyimbo za injili, eti hanywi pombe na kanisani anakaa kiti cha mbele na kuwa miongoni mwa wazee au viongozi wa kanisa. Anafanya biashara ambazo hazieleweki na hata siku moja huwezi kukaa mpange mipango ya mapato na matumizi maana njia zake za pesa ni za giza. Wachungaji kanisani wanamuona mume wangu kama muumini safi ambaye anachangia huduma za kanisa kwa pesa ambazo huwa ninajiuliza hivi kweli wachungani hawa wangejua source au chanzo cha hizo hela wangezipokea? Anatumia sana dini/ulokole kuficha madhambi yake.
Nimeshamfuatilia sana hadi sasa nimechoka, sina mpango naye kabisa tena na sasa najitahidi kujenga makazi yangu ili nijiandae kuanza maisha mapya. Suala la tendo la ndoa nimesimama kwa sababu sitapenda niache wanangu yatima. Mungu alinisimamia nikawa na nguvu ya kwenda kupima HIV hatua ya awali ni salama, nasubiri nirudie mara ya pili wiki ijayo ili kupata uhakika wa afya yangu then nimpe uhuru afuate hao malaya wake kabisa milele. Nimeshamvumilia sana,ameomba msamaha mara nyingi sana huko nyuma ila mara ya mwisho (mwaka jana 2010 Septemba) alimpata tena binti wa mwaka 1991 muuza duka la nguo na nilipomuuliza alinijia juu hadi kunikaba. Nimemlaani kwa Mungu hata kaa afanikiwe chochote milele. Mungu ataniwezesha mimi kuwatunza watoto kwa kazi yangu na biashara zangu ndogo. Yaani aliiba hadi jewelery zangu (almasi, dhahabu, tanzanite, etc) anaenda kuhonga na kuuza ili apate hela za kuhonga nakupanda ndege kufuata malaya. Kuna mchangiaji amesema pengine unashindwa kumtimizia mwanaume ndo maana anatoka nje,nasema hapana, ni tabia na hulka zao tu kwa maana huyu mume wangu ameishi na wanawake ndani mimi ni wa nne na hakuna aliyeweza kuishi kuvumilia mateso yake hata kwa miaka mitatu, mimi nipo naye miaka saba ya uvumilivu na mateso na nilikuwa namfanyia huduma zote anaonekana barabarani, chupi yake siku zote inaonekana mpya, chakula safi, kumsaidia biashara zake kimawazo maana Mungu amenipa nafasi na uwezo au upeo mkubwa kielimu na kufahamu mambo. Yote hayo sasa nimeacha na sitakaa kabisa kujishughulisha na maisha yake. Kwa hiyo jamani wanume mtakaosoma hii habari ninaomba sana wapendeni wake zenu kwa ukweli, tunaumia jamani mkitusaliti. Mimi nina muda mrefu sijui tena mboo ya mwanaume wangu na wa nje naogopa magonjwa na si tabia yangu kutembea nje.Naumia sana kisaikolojia, nalazimisha nature. Nami nisaidieni jamnani.

Anonymous said...

Anon wa 12.41 pm, umeadika kwa hisia sana, umetugusa wengine, na kwa ushauri wako tumedhamiria kubadilika

Anonymous said...

mi naona wanawake wote tuingie kwenye maombi kuwaombea waume zetu waweze kutii kiapo cha ndoa.Na katika maombi yetu tumwambie Mungu kabisa huu mwaka ndio uwe mwisho wa wanawake kunyanyasika kimapenzi na waume zetu,kuanzia mwakani basi Mungu amwondoe duniani kila mwanaume au mwanamke anaeenda nje ya ndoa,this is serious,yani mi nitaanza maombi haya ya kumponya au la kumlaani anaumiza roho ya mkewe au mumewe kwa kwenda nje ya ndo.NA HAKIKA WATU WASIPOBADILILI WANAUME MTAKUFA WENGI!

Anonymous said...

Ann wa 5:36.00pm

mama nakupa pole sana kwa kisa chako!!

Mimi kama mwanaume, nimesoma maelezo na vitimbwi vya mumeo hadi nimelia kwa kuziona tu hisia zako kimaandishi jinsi ulivyosimulia.

Kwa kweli nashindwa hata nikushauri nini bibie maana hapo ulipofikia naona umeishakata tamaa na mumeo.Moja tu dada, MUOMBEE naamini hajitambui wakati fulani unaweza kulaani mtu usijue kilichomshika huko akilini.

Nimefurahi sana kwa dada mmoja ambaye amepiga mbiu ya kufanya maombi kutuombea wanaume. Ila sikubaliani naye kabisa anaposema ataomba wengine wafe au waangamizwe.Kama Mungu angekuwa na hasira kiasi hicho sisi sote tusingeishi hadi leo kwa makosa mengi tulimtendea. Pia hata wewe mwenyewe si ajabu ni mama wa ajabuajabu maana mtu unamhukumu kwa maneno ya kinywa chake.

Kosa katika ndoa haliko moja tu la kutoka nje ya ndoa, bali yako makosa mengi yanayoambatana na hilo.Muhimu ni kama ulivyosema kuombeana ili Mungu aingilie kati katika kunyoosha mioyo ya wana ndoa.

Lakini nisema pole sana kwa wamama wote ambao waume zenu ni jeuri ya chama.Kusema ukweli inaumiza, ni sawa na mwanaume naye anaposikia mke wake anatembea na mwanaume fulani huko nje. Poleni wadada zetu ndiyo msalaba wa ndoa jaribu kumuomba sana Mungu anweza kuingilia kati.

Anonymous said...

dada ann wa 5:36:00

Umenigusa sana na kilio cha mumewe ambaye umesema umemvumilia sana na sasa umeamua tangu mwaka jana asiguse kuma yako.Pole sana mwaya.Ndoa ni ndoana kweli!!!

Ila usahihishe usemi wako wa "Nimemlaani asifanikiwe" kama utashupalia usemi huo na fikra hizo hata wewe utazidi kulaaniwa na yeye atazidi kubarikiwa.

Kama ulijua alishindwa kuishi na wanawake watatu waliotangulia, ilikuwaje wewe ukaingia kichwa kihwa hapo?Ulidhani wewe utambadilisha kirahisi kama hivyo?

Je mara ngapi umeshauriana naye na hata ungempeleka kwa hao wachungaji wake wakakusadia kutatua tatizo lako kwa sababu ni mzee wa kanisa kuliko kulia kilio barabnarani na kuamua kumnyima chakula cha usiku wakati na wewe una njaa.
Mimi kama mwanaume nakupa ushauri, nenda kwa mchungaji wenu mweleze kila kitu na umuombe msaada wa kukaa na mume wako. Ukichukua nafasi ya kumlaani haitakusaidia hata kidogo.Kama Mungu angehesabu maovu yetu sisi sote ni wakosaji japo makosa yetu yanatofautiana.Muombee mumeo usimlaani kihivyo kwani mlipendana na ndiyo maana mkaoana na mlikiri kuvumiliana katika tabu na huzuni na katika raha pia.

Ann wa 12:41 usiwe muongo, wanaume hawatangulii kufa eti kwa sababu ya vilio vyenu??? Wewe ni nani hata useme hivyo?nani kakuambia hivyo?Hivi unajua kuwa wanaume wanaoa wake walio na umri mdogo kuliko wao?Unategemea mtakufa siku moja? Hujui kuwa wanaume wanaumiza sana vichwa katika mahangaiko ya maisha na kazi za suluba nyingi?

Vilio vya wanawake havina uhusinao na vifo vya wanaume na kuacha wajane.Je kama ni hivyo ni wanawake wangapi wanapenda kubaki wajane na kuwaombea waume zao wafe?

Waombeeni waume zenu kwani hata ninyi mna makosa mengi sana ambayo yanawafanya waume zenu kuwakimbia.

Msome sana Ann3:22:00pm ameongea mambo ya maana sana na ushauri wa maana sana utawasaidia mkizingatia kuliko kelele zenu hizi na hasira hazitawasaidia kamwe.

Anonymous said...

majitu mengine bwana yaani yanaijificha kazini huyo sijui moto wake utakuwaje ,pole mama kapime kwanza virus ndo ukate shauri