Monday, 4 July 2011

Wazazi na jamaa wanasema nitafute msomi kama mimi, does it matter?

"Pole na kazi dada Dinah, kwanza nitangulize shukrani zangu kwa watu wote wanao toa ushauri na kutuelimisha mambo mbali mbali katika hii blog. Mimi ni mwanamke mwenye umri miaka 25, nimekuwa na boyfriend wangu kwa muda wa miaka 6, nilianza mahusiano nae nikiwa namalizia kidato cha nne, ila kwa sasa nipo chuo nachukua masters degree.

Mimi na boyfriend wangu huyu tunapendana sana, na pia namsaidia mambo mengi sana ya kifedha na hata yakimaisha (nikimaanisha ushauri), kwani kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia, elimu yake ni ya kidato cha nne.

Hiyo yote ni kutokana na Wazazi wake kutojishughulisha nae tokea zamani, hawakujali suala la elimu, kutokana na hili alipitia maisha magumu saana kiasi cha kumfanya aanze kufanya dili mbalimbali ili apate hela za kuendesha maisha, na pia aliweza hata kupanga chumba akawa anaishi mwenyewe na kununua assets mbalimbali za nyumba.

Kwa ujumla ni mtu ambae anajipenda na anapenda maisha mazuri tatizo ni uwezo tu na kazi ya maana ambayo itakidhi mahitaji yake yote. Pamoja na hili anasaidia hata ndugu zake pia. Hivi karibuni mambo hayamuendei vizuri kabisa japo hajakata tamaa.

Anajitahidi hivyo hivyo, kwa sababu hii mara nyingi ananiomba mimi nimsaidie kifedha kwa sababu nampenda inabidi nimsaidie nimpe hela za matumizi na muda mwingine hata za kulipia nyumba. Na fanya hivyo kwasababu nampenda, na yeye ananipenda, yupo tayari hata kesho kuishi na mimi.

Swali langu lina kuja hivi, mimi nimesoma nategemea kupata master degree yangu miezi kadhaa ijayo, kwa ujumla namshukuru Mwenyezi Mungu ninamahitaji yangu yote, ila tatizo huyu boyfriend wangu, hajasoma ila ni mtu ambaye anajitahidi hivyo hivyo sio mvivu anapenda maisha mazuri, ila watu wanasema hatutadumu kwa muda mrefu kutokana na tofauti zetu, je mnasemaje kwa hili?

Swali la pili ni hili, tumejuana kabla hata sijaanza chuo, kwa kipindi chote hicho tulikuwa pamoja mpaka sasa nategemea kumaliza masters tupo pamoja, na pia ndio boyfriend wangu wa kwanza sijawahi kuwa na mwingine, je mnanishauri vipi hapa?

Kwani baadhi ya watu wananiambia nitafute mtu aliesoma kama mimi kwani tutaelewana zaidi kimaisha. Kuhusu suala la wazazi, wazazi wake wananipenda saana, ila tatizo lina kuja upande wa wazazi wangu wanataka nitafute msomi mwenzangu, ila kwa mimi siko tayari kwani nampenda huyu nilionae.

Kwasasa haijalishi kwani nipo tayari kumsaidia kwa lolote ili tu awe na maisha mazuri. Je hii ni sahihi? Naombeni ushauri wenu, je kuna future hapa kweli au tunaforce mambo tu kwa muda kwani yatakuja nizidia huko baadae kama asipo pata kazi au biashara ya maana.

Naombeni ushauri wenu na mtazamo wenu.

Dada K".

Dinah anasema:Asante mdogo wangu, natumaini kuwa umefanyia au unaendelea kufanyiakazi maelezo mazuri kutoka kwa wachangiaji, yasome yote kisha uyachanganue alafu uchanganye ndio ufanye uamuzi.

37 comments:

Anonymous said...

Wewe mdada uwe makini ELIMU ni moja ya vitu vyenye kuleta tofauti kubwa sana kwenye mahusiano.Endapo una nia ya dhati ya kuishi na huyo jamaa mpige shule kwanza.Halafu hakikisha ana ari ya kweli ya kusoma usije lazimisha ng'ombe kunywa maji ! My take kama mnakubaliana kuishi kwa yeye kujiendeleza basi mpe muda na support ya kutosha huku, mambo mengine yakiendelea taratibu.Usikimbilie kuingia kwenye shimo usilojua kina chake.Jitahidi sana kuushinda moyo wako ,Kwani utakuja kumjutia nani yatakapokufika?
Kusoma wala siyo kufanikiwa kinyumba ni factor tu mojawapo ya msingi ili ku balance.Nawe ujue Masters degree yako siyo kila kitu,Jipange zaidi na zaidi kujiendeleza na kutafuta kile ambacho unaamini katika mafanikio yako.Ushauri wa wazazi siyo wa bure pia lipo jambo wanaloliona .Jaribu kukaa nao na kushauriana nao kuhusu hatima ya maisha yako pindi watakuwa hawapo.Nakutakia maisha mema na shukrani kwa fikra pevu na endelevu za kutafuta ushauri kwanza kabla ya kuamua. BRAVO

Amos Bwire said...

Binti...ushauri ntakaokupa unaweza kuwa mgumu, lakini unatoka moyoni na ni wa kiuzoefu zaidi. Kwanza pole sana kwa dilemma ulilonalo. Ni dilemma lililozoeleka sana kwa watu wengi wa umri na elimu kama yako. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kuna mambo mengi sana yanabadilika mara wawili wanapooana na kuanza kuishi kama mke na mume...Mazuri na Mabaya. Lakini kubwa na la msingi sana sana ni lile la wawili nyie kuwa na amani ya kweli ndani ya nyumba yenu. Sasa katika mambo ambayo hubomoa kirahisi sana amani ya ndoa na hata ndoa yenyewe, ni lile la mwanaume kuishi kwa kutojiamini. Kuna sababu lukuki za mwanaume kutojiamini ndani ya ndoa...sintapoteza muda kuzitaja nizijuazo lakini tu moja ninayoijua, na ambayo nimeiona kwa wanaume wengi-wengi mno ni hiyo uliyoitaja mwenyewe! Ni rahisi kwa sasa kutoiona tofauti yenu na hata kutoona dilemma alilonalo mpenzi wako, maana bado hamko committed kwa lolote la maana, lakini mara mtakapoingia kwenye ndoa ndipo maigizo yatapoisha na shughuli halisi ya "kisaikolojia" itakapoanza kufanya kazi yako. kuna mistakes za kawaida kabisa utafanya, na elimu yako itaonekana ndio sababu! Rafiki zako wasomi watakapowatembelea home na kuanza kuongea kisomi...mumeo atatoka sitting room na kuingia bedroom, au atakaza macho kwenye TV, au ataaga kabisa na kutoka nje. Utakapo-challenge idea zake fulani ukitumia elimu yako ku-reason...shughuli! Yani kwakweli ni ngumu saaana kwa mwanamke msomi kukaa na ku-share mambo mbalimbali yanayohitaji taaluma ku-analyze, pamoja na mume asiyesoma. Watu wengi wana-overlook swala la elimu kwenye mahusiano, lakini asikudanganye myu...ni la msingi kupindukia(with very minor exceptions!) Kwa kirefu ni kwamba, ni ngumu saaaana-saaana kwa mwanaamke mwenye degree moja tu kuishi na mwanaume alieshia form six(sasa wewe Masters degree na form four leaver?) Kama mumeo atakuwa tayari kurudi shule na akatafute walau degree moja ya uzeeni, hapo itakuwa vyema sana(kwake.)..au walau basi awe mpiganaji wa ukweli atakaekuwa na uwezo wa kulea na kuilinda nyumba yake na kuweka PAMBA ZA CHUMA masikioni! Hapo wote mtakuwa na AMANI. Lakini kama mtakuwa kama ninavyofikiri sasa, mh, Inakubidi uwe na MAAMUZI, BUSARA UVUMILIVU na HEKIMA ZA HALI YA JUU ili uweze kuishi na huyo mume, vinginevyo ndoa yako itakuwa ya machungu na vurugu kabla hata ya kufikisha miaka mitano! Nina mifano zaidi ya 10, tena mingine ya ndugu na jamaa wa karibu, walioingia kiujasiri sana kwenye ndoa lakini wakaishia kusambaratishwa na baadhi ya mambo niliyotaja hapo juu, kabla hata ya kuota meno ndoani! Sio Rahisi kabisa, unless you're truly a woman from Venus and your man comes from Mars!!!

Anonymous said...

mapenzi hayaangalii pesa ila maisha bila pesa in this age ni balaa..mie ushauri wangu ni hivi..dada kama unapesa ya kutosha kwanini usimsaidie ajiendeleze anweza fanya pepa ya form six coz kwa hiyo form 4 kupata kazi almost ni impossible unaweza usione sasa kwani love is blind ila baadae maisha mkipata watoto life burden ikiongezeka utaona tabu..bora atafute kujiendeleza kielimu sio kwa ajili ya mapenzi tu hata yeye pia ili awe na kauhakika ka kzi

Anonymous said...

.. dah! Sist. Dina umeleta mjadala mzuri sana, ..hivi kwanini wanawake hamwapendi wanaume kama walivyo-mnadhamini sana fedhaeh!

... kama unajimudu na umepiga shule ya ukweli kwanini usikae na mpezio ukapanga naye mikakati ya kujikwamua kimaisha- sasa nini maana ya kusoma kwako?

kidato cha nne ni kikubwa na mnaweza kukaa na kuanzisha biashara au hata miradi kwa kutumia elimu yako. Kama kweli unampenda na anakupenda tofauti za vidato si kigezo chamsingi sana. Ndio wakati sasa wa kuonuesha upendo wako kwake.

Wakina baharesa na bilgate hata master hawana na wanatesa duniani...hahaha! ACHA MAPEPE DADA ETI KISA MASTER. WATU WANA PHD, UPROFESA na wameoa au kuolewa na darasa la 7.

mama 2 said...

Mshukuru Mungu kwanza kwani huyo Boyfriend wako siyo mvivu na anajituma. Na vipi ana uelekeo wowote wa kujiendeleza kielimu? kama anapenda kujiendeleza kielimu basi shule zipo msaidie. Na kama hana uelekeo wa kujiendeleza,Kaeni angalieni biashara gani anaweza akafanya ikawatoa, mpatie mtaji ili aendelee yeye kusimamia biashara wakati wewe unaendelea na kazi yako. Mapenzi siyo elimu, ni jinsi ninyi mnavyopendana mamaaa, usiwazikilize hao wanakushauri upate msomi mwenzako, unaweza ukampata na usi-enjoy love. Mapenzi kitu kingine mdogo wangu, kuwa na maamuzi yako binafsi.

Anonymous said...

Kwa maelezo yako inaonyesha dhairi unampenda kupita kiasi huyo boyfriend wako..Mimi ninapenda kukupa ushauri kwa mifano zaidi,kuna watu ambao nawafahamu mwanamke ana Masters kama wewe na mwanaume alikuwa dereva ingawa sasa alipokuwa anafanyia kazi amepunguzwa kazi na wameoana kwa ndoa kanisani na wanaishi maisha mazuri mwanamke ana pesa nyingi na wanamagari ya mizigo mwanamme ye ni dereva ndo anayasimamia,mwanamke ni mtu wa kusafiri sana nje ya nchi...maisha safi kwa sisi tunaowaangalia nje cjui ndani ya ndoa yao ni siri.....Ila nakushauri usilazimishe kuolewa nae ila jaribu kuwashawishi wazazi wako waridhie hilo kwani baadae ikikuletea matatizo watapata cha kuzungumzia..

Anonymous said...

Kwa maelezo yako inaonyesha dhairi unampenda kupita kiasi huyo boyfriend wako..Mimi ninapenda kukupa ushauri kwa mifano zaidi,kuna watu ambao nawafahamu mwanamke ana Masters kama wewe na mwanaume alikuwa dereva ingawa sasa alipokuwa anafanyia kazi amepunguzwa kazi na wameoana kwa ndoa kanisani na wanaishi maisha mazuri mwanamke ana pesa nyingi na wanamagari ya mizigo mwanamme ye ni dereva ndo anayasimamia,mwanamke ni mtu wa kusafiri sana nje ya nchi...maisha safi kwa sisi tunaowaangalia nje cjui ndani ya ndoa yao ni siri.....Ila nakushauri usilazimishe kuolewa nae ila jaribu kuwashawishi wazazi wako waridhie hilo kwani baadae ikikuletea matatizo watapata cha kuzungumzia..

Anonymous said...

mie nakushauri uendele nae huyo huyo,ulie mpenda na alie kupenda.Kuolewa na msomi mwenzio sio tija, unaweza kuolewa na msomi akakuweka mashakani au matatizoni, ukajuta. Kwanza wanaume wasomi wanajifanya wajanja na wanaakili sana, na wanapenda kumiliki mwanamke, wajeuri, hawana abadu, upenda nyumba ndogo nyingi nyingi, na kukesha kwenye maba na starehe. Utajuta. Mbaya zaidi wanunue machangu ndoa sababu wanahela za kutosha na wakuambukize ukimwi.

Mapenzi ya kweli ndio yanayo dumisha ndoa na sio elim wala kipato. Wazazi na jamaa zako wanazani huyo jamaa atakuchosha na kukutegemea wewe. Sasa hapo inabidi uwe na mawazo strong ya kumpata mpenzi wako ajiendeleze kielim na kipato ili awe na maisha mazuri ya kujitaftia mwenyewe kwa nguvu zake. msaidie kipesa ili ajielimishe tu,sio umlipie kodi ya house na furniture. Kwani ana age gani? watu wanasoma hata akiwa na miaka 50, akili yake tu. Baada ya miaka 5 nae anaweza kuwa msomi vile vile

Anonymous said...

Nimesoma story yako ikanifurahisha. Binti watu wengi wanapenda sana ready made. Ila kijana huyo huyo anaweza akajakusoma hata akawa na zaidi ya masters kama yako ila maisha ni mipango tu. La msingi umeshasema unampenda so that is it. You don't have to hear from your parents je ukampata msomi na akaanza kukunyanyasa utafanyaje. Mtu umekaa nae miaka sita yote, na bado unafeel kuwa nae mpenzi nakushauri waeleweshe wazazi wako kuwa huyo kijana anaweza kujiendeleza sana tu maisha yenu yakishasettle.

All the best.

Anonymous said...

Pole dada K. kwa hali iliyokukuta mimi pia nipo kwenye situation kama yako hivyo hivy nina mpenzi ambaye 2napendana sana ila tatizo limekuwa ni kwamba mimi nina elimu kumzidi kitu ambacho baadhi ya marafiki zangu wanapingana nacho wananishauri nitafute mtu ambaye nitaendana naye ambaye 2takuwa 2melingana kielimu na angalau tunatoka kwenye familia zenye uwezo sawa (my family is somehow well ukilinganisha nayakwake). Wazazi wangu nao wamekuwa wakipingana na uhusiano wetu huo ambao nao una miaka 6 kama wa kwenu. Kwa sasa nimeamua kufanya ibada na kufunga ili Mola aweze kunionyesha ni njia gani nifuate kwa sababu mimi siamini kama elimu na mali ni vigezo vya kuwafanya watu wasiwe pamoja. Dada K, nikushauri 2 mwenzangu tusimamie misimamo yetu tuafute furaha za mioyo yetu kwani unaweza kupata bwana msomi lakini ndo hivyo moyo wako wala haupo kwake. Ikiwezekana omba DUA.

Anonymous said...

Mimi napenda jinsi ulivyo honest na loving! ila kuna mfano mingi kua watu kama hawa, utamsaidia ahalafu mukaoana lakini itakifika wakati, huyo bwana atakuacha tuu, hata kukifanye je, mimi nawajua wanaume wanamna hii, ila if you love him, just try! but do not regret later!

Anonymous said...

my dia nakushauri uufuate moyo wako unachopenda kwani watu hawaelewi unachopata, mapenzi siyo elimu wala pesa bali thamani ya moyo wako.

Anonymous said...

Binti K, Kwa kukuangalia harakaharaka tu kutokana na rafudhi ya uandishi wako,nimebaini kuwa kusoma masters hakujakuongezea kitu chochote cha kuzidi ubinadamu uliokuwa nao tangu mnaelewana na huyo mpenzio.Ulichoongeza ni mjina la kuitwa nina ninasoma masters.

Kisomo ni cha kwenye makaratasi,lakini utu na heshina ya mwandamu haiko katika kisomo alichonacho. Kisomo kama umekitumia vizuri kitakuongezea heshima na ujuzi zaidi,lakini hakiwezi kukkutenga na upendo ulio ndani ya utu wako ambao ndio umewaunganisha na jamaa yako.

Ni rahisi kwa wengi kufikiria kuwa kisomo ni kila kitu,lakini kumbe sivyo. Kama kweli umesoma basi naamini unaweza kuwa chachu tosha ya kumchachua mpenzio ili aumuke na yeye aende mbele kielimu.

Ni sawasawa na aliyeoplewa na mtu tajiri.Utajiri utadumu iwapo huyo tajiri atachukua fursa ya kumwelimisha mwenzake namna ya kutunza mali nk.Hivyo kwa kuwa mpenzio kafika f 4 una nafasi kubwa kumfanya na yeye aendelee mbele.

Hata ukiolewa na msomi mwenzako usidhani ndiyo kuimarisha ndoa, wakati mwingine inaweza kuwa ndo kuvunja ndoa kwa kuonyeshana umahili wa usomi wenu.

Ndoa isifaninishwe na vitu tunavyoweza kuvichuma au kuvipata kama elimu au mali.ndoa hubarikiwa na Mungu.Ni maisha ya milele kwa wapendanao.Na upendo huvumilia sana (Soma hapa kama wewe ni Mkristo, Ikor 13:1-13).

Digrii zenyewe za siku ni za ku-copy na ku-paste wala hazina tija watu wanajivunia vyeti ukutani lakini kaangalie kichwani hakuna kitu.Hapa naaminisha digrii haina nafasi katika suala la upendo kwa umpendaye tena umeanza naye miaka na hajawahi kukudanganya.

Haya bibie tafakari zaidi usije ukaacha mbachao kwa msaala upitao. Leo huyo huyo utamuona hivi lakini hujui kesho atakuwa wapi,hivyo usikubali kumwa-undermine mtu kwa hali aliyonayo sasa kwani hujui Mungu kamwandikia nini siku zijazo.

Anonymous said...

ndugu yangu pole kwa hayo mapenzi ni uamuzi wako mwenyewe kama unampenda kwa dhati endelea na msimamo wako

Anonymous said...

dada k,story yako imenitouch...ukweli jamaa anakupenda kwa dhati,unaweza kupata msomii mwezako asikupende kwa dhati ukabakii kuumizwa kila siku na kujutia,after all jamaa ni mpambanajii.wangapi hawajasoma ilaa wanamaisha mazuri yenye upendo katika ndoa zao.usisikie ya watu kama unampenda stick nae

Anonymous said...

dada k,story yako imenitouch...ukweli jamaa anakupenda kwa dhati,unaweza kupata msomii mwezako asikupende kwa dhati ukabakii kuumizwa kila siku na kujutia,after all jamaa ni mpambanajii.wangapi hawajasoma ilaa wanamaisha mazuri yenye upendo katika ndoa zao.usisikie ya watu kama unampenda stick nae

Anonymous said...

Hello Dada K! Pole sana kwa yote.. Lakini kitu kimoja tu naomba nikwambie na kukushauri katika mapenzi kitu cha msingi ni upendo, na kukiwa na upendo ndani yake kutakuwa na amani icho ndio kitu cha msingi. Kama wote mnapendana na mmeanza tangia zamani na adi leo hii bado mnapendana basi usisikilize maneno ya watu kwasababu wewe ndio utakaye ishi na uyo jamamaa ktk maisha yenu yote.(Wazungu wanasema follow your heart). Uyo mwanaume unaweza kumsomesha kuanzia certificate mpaka akafika juu kama wewe na ata mkafanya biashara yoyote as long as umesema uyo jamaa yako yupo smart. ni kiasi tu cha kujipanga na kuamua.unaweza ukamchagua msomi mwenzako ikaja ikakupa shida kwasababu utakuwa ujampenda kutoka moyoni mwako na ndani ya nyumba mkawa amuelewani eti kwasababu ya usomi . Mapenzi ni kupendana na kuelewana na cha mwisho usisikilize maneno ya watu kwasababu awajui mmetoka wapi watu wengine awapendi kuona wenzao wakipendana.

Anonymous said...

Elimu yako isaidie mkumbeba asiye na elimu ili na yeye apate elimu.Ndiyo maana kuna mwalimu anayewafanya wengine baadaye wawe waalimu na wajuzi.Upendo wako ndiyo utakaofanikisha kumwinua huyo jamaa hadi watu washangae.

Mimi nina ndugu yangu ambaye alimzaliza darasa la saba.Alitokea kumpenda sana binti mmoja ambaye alikuwa amehitimu kidato cha nne.ndugu wa binti huyo ni wenye nafasi nzuri kiuchumi,hivyo walimkataza sana huyo binti asiolewe na huyo mwenye elimu ya chini ambaye pia ametoka familia maskini na bahati mbaya baba yake alikufa miaka mingi.

Yule msichana aligoma kabisa akasema huyo ndiye nampenda na yeye ananipenda nitaolewa naye. Kweli yule binti alifanikiwa kuolewa naye.Amini usiamini, yule jamaa yangu alianza mwenyewe kujipandisha kusoma, akafanya mtihani wa f 4 akafaulu akaenda chuo, akamaliza.Mungu si athumani akapata kazi na kanisa.Na kazi hiyo ikampa nafasi ya kufahamiana na wakubwa serikali hapo Dar.Yule mke wake akawa anafanya vibarua tu kazi ya maana hakupata.Huyu mumewe akamtafutia kazi benki ya exim.Huyo jamaa yangu kapata nafasi kwenda nchini Marekani kusoma miaka miwili, Akarudi Bongo, kaendelea kufanya kazi na baada ya miaka mitatu kapata nafasi kusoma nchini Norway kwa miaka miwili. Akarudi nchini na sasa ana nafasi nzuri na mke wake ana nafasi nzuri Exim Bank.Kumbuka aliyemtafutia kazi hiyo ni huyu mumewe ambaye ndugu zake walimuona hana elimu na ni maskini,leo ndiye mkombozi mkubwa wa binti yao.

Maisha wanayoishi ni mazuri, wana magari mazuri kila mmoja ya kutembelea,nyumba nzuri, na wamejaaliwa watoto wao watatu wazuri.Nimekusimulia kisa hiki ili kikusaidie kuchekecha mambo,kwa sababu umetuambia kwamba huyo mpenzi wako anajua sana kujishughulisha,hiyo ina maana ukimuwezesha atageuka baadaye kuwa almasi kwako.Mpe nafasi utakapokuwa umeolewa naye au hata kabla muongoze njia,na mpe uwezo utaona matokeo yake.

Nakutakia kila la heri.Hakuna lisilowezekana palipo na nia pana njia pia.Kumbuka kinachowakalisha watu kwenye ndoa ni upendo wenye kustawisha amani, furaha, mawasiliano na maelewano.Ndoa haiimarishwi na elimu, mali au ufahari wa aina yoyote ile.Kuna watu wameolewa kwenye familia za kifahari, pesa nyingi, vyeo vingi, na elimu za kumwagalakini wanaishi kwa kuishiwa Upendo, amani na furaha.Chunga kilico moyoni kwani kipendacho moyo ndiyo dawa.

Anonymous said...

Mimi nachoona wanaokushauri utafute msomi mwenzako wanakupoteza,kwanini usimuenedeleze shule taratibu afikie level yako,hilo ndio la msingi,

Anonymous said...

maisha ya ndoa ni maisha tofauti kabisa na maisha mnayoishi sasa. ndoa inaitaji uvumilivu kati yenu na sio elimu ya darasani au madegree. kama kweli unapendana basi lazima kila mtu hamkubali mwenzake kwa mapungufu yake. Maisha ya ndoa ni kuvumiliana kwa kila hali na kujitoa kwa ajili mwenzi wako bila hivyo hakuna ndoa.

Anonymous said...

Dada, wala usithubutu kufanya kosa la kuolewa na mtu ulomzidi elimu kwa kiasi hicho.. itakusumbua wewe na yeye pia baadae...been there done that tumeishia kutengana, mana ilikuwa kila kitu''unajifanya msomi kunizidi unanidharau....''
nenda kwa wanasheria au mahakimu uliza factors zinazosababishaga divorce kwa sasa ivi..hiyo ni among them..at least mwanaume ndiye angekuwa amesoma isingekuwa tabu...think twice...

Anonymous said...

Final decision unayo wewe dada yangu What if umpate msomi anayekunyanyasa.Ila wanaume wengi hawapendi wanawake wasomi.But kiukweli love haichagui!!

Anonymous said...

hivi wewe dada mimi naona huyo jamaa humpendi kidhani, kwa sababu ungekuwa unampenda kweli kweli hata usingetaka kutafuta ushauri ila wewe upo katika gatigati, una wasiwasi kwa maneno unayoambiwa na watu, sasa kama mtu ushakaa nae miaka 6 na tabia zake unazijua vizuri na umeridhika nae, sasa kinakusumbua kitu gani. Mimi ninaekupa ushauri nina jamaa pia tunajuana kwa muda wa miaka mitano na nusu, na yeye elimu yake ni ndogo kuliko yangu, na pia hata baadhi ya ndugu zangu na rafiki zangu huwa wanasema kuhusu kabila lake. lakini yote hayo sikuyajali ninampenda na akipenda Mungu tutaoana, kama kumsaidia kimaisha nimemsaidia sana mpaka kakaa sawa na wala sioni shida yoyote na sijamwambia yoyote na kuhusu kumsaidia hajui yoyote isipokuwa wewe. sasa usiwe na wasiwasi GO AHEAD KAMA UNAMPENDA KWELI KAMA UPO TAYARI NA AKUOE.

Anonymous said...

My dear kwa mtazamo wangu ni kwamba wewe binti umeongea tuu kwa upande wako na tena kwa kuonyesha kuwa unaforce mambo na pia hujiamini, Ukweli ni kwamba huwezi kuuzuia moyo isipokuwa je uko tayari kumuheshimu maisha yako yote? Sasa hivi umejaribu kumtetea sana huyo jamaa kwasababu kwanza wewe bado mwanafunzi hujashika hela i.e mshahara na pia bado hujakutana na wasomi wenzako huko ofisini kweli utamuheshimu tena huyo mpenzi wako wa sasa? kupenda maisha mazuri sio sababu coz hata vichaa wanayapenda ni kwamba hawajayapata tuu suala ni heshima baada ya mafanikio itakuwepo? Wasiwasi wangu ni kwamba utakapoanza kupokea millioni kadhaa na kukutana na msomi mwenzio ambaye nae salaryslip yake inasomeka vema and u both speak the same language kweli will u turn back na kuangalia all those six yrs u spend with him kwa shida na raha? please think twice and follow ya dream!

Anonymous said...

Maisha hayafanani hata kidogo.Na watu wote wamezaliwa na kulelewa na wazazi na ndugu tofauti kwa kabila na mazingira tofauti.Kwa hiyo mimi ningekushauri uangalie moyo wako, naamini hadi hivi sasa kama ni wasomi umeishakutana nao tangu unasoma kidatu cha sita, chuo kikuu, hatimaye unasoma masters naamini una wenzako darasani unasoma nao masters ungewapenda hao kama kiegezo ni elimu.

Usifikirie mambo ya mbele ambayo huyajui kabisaaaaaa.Fikiria kitu kilicho karibu na wewe na kukijengea MISINGI NA MIPANGO YA MAANA KWA MANUFAA YA MBELENI.

Siku hizi kila mtu ni mwelevu hata kama hajaenda sana darasani kuna njia mbalimbali ambazo zimewafanya watu wawe wajuzi wa mambo mengi kutokana na utandawazi.Unaweza kushangaa sana kwamba huyo jamaa yako akajua mengi yanayozunguka jamii na dunia kwa ujumla kuliko wewe unayekariri mambo ya darasani kufaulu mitihani yako.Mambo ya darasani ni finyu sana ukilinganisha na mambo unayoweza kuyapata nje ya darasa. Mimi niko Ughaibuni.Nilipofika huku nilijikuta kama hata shule sijaenda hata unaingia darasani unaona kama ndo kwanza unaanza darasa la saba kwa sababu mazingira yanayokuzunguka ni elimu tosha kukufikirisha na kukufungua mind yako.

Umesema unasoma Masters, unaweza kuambiwa andika tu ka-proposal fulani ka page kama 5 tu ikawa ishu kama si kwenda kudesa.Lakini mtu mwingine hajaingia hata digrii anaweza kukaa chini akaweka vitu vyake chini vikaeleweka zaidi.

Wengi wametoa mifano mingi ya watu waliolewa na wasio kuwa na kisomo na wako vizuti na maisha. Kwa kuwa umempenda mwenyewe jitahidi kuutafakari upendo wako kwake kama umethibitika basi huyo ndiye mume wako.

Amos Bwire said...

Sorry Dinnah! Have to say this kwa kweli...Yaelekea siku hizi watoto wengi wa sekondari wanachangia mada zako! Hakuna uwezekano wa ku-control hilo? Duh!

Anonymous said...

Amos umeongea point....Tigo wazima wasalimie

Anonymous said...

kabisa annon #1apo katika elimu yani ata km mwapendana vipi,jamani wanaume wengi wana viranga balaa apo badae!!sijui kama na uyu tumuweke katika lile kundi la wanaume 2% tu ya waelewa...

Anonymous said...

amos bwire very well said,mie ni mwanamke na i agree with u kabisa yani,ata mie nna mifano kama 5 ya ivo na izo ndoa wameachana wengine baba kitanzi kooni basi maigizo tu.wanaume wana kitu cha tafauti sana vs wanawake kukubaliana na hali ya kuwa mwanamke anaweza kuwa juu kimaisha na amakupenda lzm vijisababu vitaanza tu...WATCH OUT SANA DADA WITH AN EAGLE EYE ABT THAT

Anonymous said...

maamuzi ya mwisho ni yako mpenzi,ila ndoa ni makubaliano ya wapendanao na baadae uaminifu na heshima basi!!mengine ni ya ziada sana
ila yana msingi mkubwa sana ktk relationship yenu mkiwa ndoani mf,kazi,elimu,mtoto ata kama watu wanasema haya si chochote ila UKWELI unabaki palepale ni vitu vya ziada sana ila vina-play a big role ktk maisha ya binadamu!!omba Mungu aje kuwa mume mwenye busara na wewe uwe mke mwenye hekima ndipo mtaweza ishi ata mkiwa na iyo tafauti ya elimu nk nk
aza

Anonymous said...

Its Complicated dear. Suala la mapenzi ni gumu sana kuomba ushauri coz unaweza ukakubali ushauri kumbe ukakuingza motoni! Na unawea ukaukataa lkn baadaye ukajutia.
Ishu ya mapenzi inahitaji HEKIMA. Hekima ni utajiri mkubwa sana ambao ni wachache mno wameejaliwa kuupata. Ni mtu mmoja ktk mia ndio anaweza kuwa na hekima. So, kwa elimu yako, ni lazima ukubali kuwa mwanamke, na ni lazima ukubali kuwa below a man na mume awe kiongozi na wewe uwe mshauri, na mwisho HEKIMA ni bora zaidi.
Halafu, Maisha sio lazima shule, play ur role, mpe ushauri wa biashara then mpe support ya mtaji kidogo kidogo FINALY mtakuwa sawa interms of ur cashflows.

Pretty girl with edu. said...

Yaani mimi ndo kwanza ninakatafuta hako ka degree , mwenzangu ni form six nimejuana nae almost five years past, haishi kuwa na wanawake , kejeli kila sku eti ooh , unajifanya msomi, ooh hata ukiwa na degree kumi huwezi kunizidi kwa lolote, yeye ana uwezo kidogo na muda mwingine huwa anani support financially hasa kwenye mambo ya shule, and now kazaa dada fulani, according to my experience iz that hata kama utaishi nae huyo mtu jua atakuja kukufanyia kitu ambacho kitakuuza lengo lake ni ku compasate hiyo elimu yako uliyoihangaikia and sio kwamba atakuwa hakupendi no, bali atakuwa anatafuta comfidence over u, YAANI UKIAMUA KUISHI NAE UWE MWANAMKE WA SHOKA HASWA , UKUBALI , KULIA, KUUMIZWA, KUDHALILISHWA etc 2Me am on my way leaving the guy coz nimevumilia mengi saaana , saana.
Lol uwanja ni wako, kusuka au kunyoa, by they way,kwenye maisha kuna wakati inabidi UKUBALI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, ITS BETTER UULIZE WTU AMBAO WENYE SITUATION HIYO NDO WANAOJUA REALITY BILA CHENGA, HAWA WANAO BASE KWENYE MAPENZI WATAKUPOTOSHA MAPENZI HUISHA, LOVE IS NOT CONSTANT ITS DYNAMIC IT VARIES TIME TO TIME.,,
a hako ka degree , mwenzangu ni form six nimejuana nae almost five years past, haishi kuwa na wanawake , kejeli kila sku eti ooh , unajifanya msomi, ooh hata ukiwa na degree kumi huwezi kunizidi kwa lolote, yeye ana uwezo kidogo na muda mwingine huwa anani support financially hasa kwenye mambo ya shule, and now kazaa dada fulani, according to my experience iz that hata kama utaishi nae huyo mtu jua atakuja kukufanyia kitu ambacho kitakuuza lengo lake ni ku compasate hiyo elimu yako uliyoihangaikia and sio kwamba atakuwa hakupendi no, bali atakuwa anatafuta comfidence over u, YAANI UKIAMUA KUISHI NAE UWE MWANAMKE WA SHOKA HASWA , UKUBALI , KULIA, KUUMIZWA, KUDHALILISHWA etc 2Me am on my way leaving the guy coz nimevumilia mengi saaana , saana.
Lol uwanja ni wako, kusuka au kunyoa, by they way,kwenye maisha kuna wakati inabidi UKUBALI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU, ITS BETTER UULIZE WTU AMBAO WENYE SITUATION HIYO NDO WANAOJUA REALITY BILA CHENGA, HAWA WANAO BASE KWENYE MAPENZI WATAKUPOTOSHA MAPENZI HUISHA, LOVE IS NOT CONSTANT ITS DYNAMIC IT VARIES TIME TO TIME.,,

Anonymous said...

Pole mrembo kwa kutwa na dilema.lakini nirahisi. kama mdau wa kwanza alivyotangulia kusema (anonymous wa 4:06:00), ningekushauri kama huyo mchumba wako aengeeda shule kwanza, kama anania ya kusoma muendeleze halafu mengine yatafuta taratibu.umuhimu wa elimu ni muhimu sana. nipo kwenye ndoa na ninaelewa umuhimu wa elimu.
anonymous wa kwanza kabisa nimependa sana ulivyomjibu BRAVO
ahsante

Anonymous said...

Kinachomatter ni kupendana kwa dhati na hizo tofauti msizifirie sana bali kaeni na mpange namna ya kusonga mbele kimaisha. Mimi nina degree ya kwanza na wife wangu ana Phd na tunapendana fresh na mtoto wetu mmoja. kama watu mnapendana vyeti vinasaidia nini? mimi nafanya biashara na tunasaidiana coz hakuna changu wala chake bali tunatafuta kwa ajili ya familia. I love my wife.

Anonymous said...

Tusidanganyane kuwa kwenye kuolewa mtu aangalie penzi tu. Yes penzi linatakiwa liwepo na mengine ni muhimu ili penzi liweze kudumu. Kama walivyochangia wengine sisi wenye experience na ndoa ni kuwa ndoa siyo tambarare kuwa kila siku kutakuwa na same level ya penzi. Sasa utaja jutia uamuzi wako na kumuona mumeo kama ana ghubu na mzigo. Mwanaume awe na elimu sawa na wewe au akuzidi au ukimzidi basi iwe wote mna level ya degree meaning na yeye anaweza ongeza digrii nyingine any time t. Kumwendeleza mtu wa form four mbona kazi. Akija kumaliza shule si umeshazeeka?? Muwe waangalifu kabla ya kupenda. Mimi nilikuwa napenda kwa malengo. SI malengo ya pesa lakini nilishasema mume wangu lazima awe degree holder hence nilifall kwa mwanachuo mwenzangu na nisingeweza kamwe kuokota mtu mtahani asiye na elimu nimpeleke kwa wazazi. Mnawaumiza wazazi wenu

Anonymous said...

wewe msomi achaujinga kusoma na mapenzi ni vitu tafauti mimi nilishamwona jamaa mmoja mwanamme ni std seven mkewe ana degree msomi wa chuochikuu wanaishi wanapendana wamezaa watoto na huyo mwanamme ni mchaga wamejenga nyumba.nimipangilio tu

Anonymous said...

Dada fuata ileki2 moyo inataka.as long there is true love in between you 2people.kuhusu kaz kaz zipo nyingi.na kma ulivyo sema ni mchapa kazi iyo cyo problem tenaa