Monday, 4 April 2011

Nikimhitaji mume wangu kimwili ananishushua, nifanyaje....


"Hallo dada Dinah pole kwa shughuli hasa hii ya kutuelimisha sie wanawake. Asante sana.

Mimi nina swali, nina mume asiyejua mapenzi japokuwa nahisi anaelewa ila ananisoma tu,hivyo najizuia sana kumfanyia na kumuonyesha mapenzi kwa sana kwani naogopa atanidhania mhuni.


Pia hapendi kufanya mapenzi mara kwa mara, ukweli ni kuwa anakaa mbali nami lakini nikimwomba niende anadai yupo busy! nina wakati mgumu sana kwa hilo,anadai nifanye kazi yaani kuchakarika na life nisiwaze hayo mambo ya mapenzi,eti ooh "huna kazi nini"?

Naomba ushauri pia ktk hili".

3 comments:

Anonymous said...

Kama hakuwa hivyo tkea zamani, mchunguze atakuwa na kimada huyo. I had the same experience nilipokuwa na ujauzito. Eti alikuwa ananambia ananihurumia, hata nibembeleze vipi, sipati. Basi nikakubali matokeo. Kumbe jamaa alikuwa na kimada sasa mimi nilikuwa makini ndo maana nilimgundua ndani ya muda mfupi. Ila alinambia (baada ya kumbana kuwa alikuwa ana ni ignore kwa sababu ya kimada) alikuwa anaogopa kuniambukiza ukimwi mimi na mtoto. SO baada ya kujifungua tulipima, maisha yanaendelea. In short I was thankful for his consideration kwani imagine anatoka nje alafu anakuja lala na wewe, a pregnant woman na magonjwa haya. wanandoa tusali jamani, maana huyo kimada nilipata e cards alizokuwa anamtumia hubby nilichoka, full kujikomba, yaani its like my hubby wanted a one night stand and the lady was begging for the continuity of the dirty relation. Bad thing is I now know the lady and it is making me sick. People out there are hunting for our husband girls, lets be careful. Wana kamsemo kao wanaume ni wachache kuliko wanawake. I don't agree with that, what they want is men with money. Wanashindwa jua kuwa tulipooana hatukuwa na kitu. Wanasubili wenye pesa ambao tayari wameshaoa.

Well msijesema mume wangu alinipa cards nisome, ni upelelezi wangu wa ki-intelligensia ndo uliniwezesha ku-access his emails.

Anonymous said...

huyo anakucheat tu kwanini akuzuie kwenda huko pia asijidai hana haja ya mapenzi sasa alikuoa wa nini kama kufua au kumpikia si angetafuta house girl au boy yaani haya mambo ya wanaume yananitia hasira kila ninapoona jinsi wanavyowasababishia wanawake maumivu usiwe bwege dada yangu kuna wakati wa kazi na wakati wa kufuraia na mumeo fanya upelelezi utagundua ikibidi nenda kwa siri uko anakokaa bila taarifa umpeleleze tena usifikie kwake ili kufanya uchunguzi
hawa viumbe hawana shukrani ata umpendeje utakuta bado anakucheat tu,

Anonymous said...

Hiyo hali unatakiwa uifanyie uchunguzi wa kina na wamakini sana. Kwa sababu wanaume hatulingani kwenye suala la ngono (nadhani hata wanawake).
Wapo wanaume wanahitaji ngono kila saa! wengine kila siku
wengine kwa wiki mara mbili au moja, wengine kila baada ya wiki mbili, wengine mara moja tu kwa mwezi!!!! na kuendekea.

Halafu wapo wanaume ambao wakipata nje ndani hawahitaji tena, (kumbuka wapo wanaofanya nje na akija nyumbani anafanya pia)

Halafu wapo wanaume pia ambao wanaweza kufanya ngono hata kila siku, but wakiwa na shuhuli fulani iwe ya kutafuta maisha, masomo, au wakiwa wanafuatilia jambo fulani kwa makini kama vile mpira etc, huwa wanapoteza kabisa wazo la ngono.

Mimi nina rafiki yangu hajaoa na ni na mhuni sana,almost all day lazima afanye. But ni mpenzi sana wa mpira hasa timu za ulaya, ikifika kipindi cha zile mechi za ulaya hashuhuliki tena na mambo ya ngono na mademu wake wanalijua hilo.

Katika uchunguzi wako zingatia Je hali hii ni toka mwanzo au ni ya hivi sasa tu? je katika kipindi cha kuwa naye je kuna siku ambazo mlifululiza kufanya ngono angalau siku mbili au tatu?

Baada ya uchunguzi wako ongea nae. Mweleze hisia zako ( na mzoeshe kumweleza hisia zako) Usijizuie kumwonesha mapenzi, ukijizuia vicheche vitamwonesha tahamaki hutamwona tena. Na hili naomba nisisitize watu wengine wanaona aibu kuongea mambo ya ngono na wenzi wao, matokeo yake mwanaume mitindo yote anaenda kuifanyia hukoo kwa machangu na mwanamke naye anaenda kujitosheleza na mitindo tofauti tofauti hukoo...... Halafu jioni wakikutana kila mtu anajifanya hajui kitu.

MWAMBIE UNAHAMU YA KUFANYA NGONO NA YEYE, KAMA HUJATOSHEKA UNASEMA, KAMA KUNA MTINDO UNAHITAJI UNASEMA.

Mapenzi ya ngono wakati mwingine yanahitaji kujengwa kwa kuambiana hayaji hivi hivi tu.

Ukigundua kwa tabia yake si mtu wa kufanya ngono kila siku zipo appetizer za kitandani zitumie. utaona zile frequence za sex ninaongezeka day after day then finally anacope na wewe.

Naomba fanya hivyo na wengine wajifunze kutoka kwako.