Nianzie wapi Kisheria kumtaliki mume wangu?-Ushauri

"Kwanza napenda kukupongeza kwa kazi yako nzuri, pili mie nilitoa malalamiko yangu kuhusiana na mume wangu ambae hataki kunipa Talaka dada dinah, naomba unielekeze wapi naanzia kwenye vyombo vya Sheria maana issue nataka pia atoke kwangu.

Kuna baadhi ya watu wananiambia Mahakamani hawavunji Ndoa na wengine wananiambia inaweza pelekea hata Miaka miwili kila siku unapigwa Tarehe tu, sio siri dada Dinah ni kama naishi na Chui ndani ya nyumba, kwamba muda wowote anaweza akanibadilikia na kunila nyama"

Comments

Anonymous said…
Dada yangu.
Mimi ni mwanasheria. So, fuatilia ninachokuashauri.
Unaweza kumtaliki mumeo kwa kwenda mahakamani kuomba talaka. Ni mahakama tu ndio yenye mamlaka ya kutoa talaka kisheria-kama utataka mambo yako yaendeshwe kisheria na kwa kirahisi. Talaka ya kiislamu haina nguvu ya kisheria na hata akikupa hiyo haitaweza kupelekwa mahakamani kama talaka. Labda itatumika tu kama uthibitisho kwamba ndoa imevunjika bila uwezekano wa kurekebishika, na hivyo mahakama itoe talaka ya kisheria. Lkn hii sio route nzuri.

Sasa basi:
Ili mahakama itoe talaka inatakiwa ithibitishwe kuwa NDOA IMEVUNJIKA NA HAITAREKEBISHIKA TENA i.e The marriage has broken down irreperably. Na sheria ya ndoa ya 1971 inabainisha sababu TATU TU (3)za kuweza kutolewa talaka. Hizi zikithibitishwa basi mahakama ndio hufikia uamuzi kuwa ndoa imevunjika kwa kiasi nilichoeleza hapo juu. Sababu hizo ni:
(1) Uzinzi (adultery). Ukiweza kuthibitisha kuwa mwanandoa amefanya uzinzi. Mtoto wa nje ya ndoa anaweza kuwa ni uthibitisho mzuri. Lkn zipo namna nyingi eg fumanizi, etc.
(2) Ukatili (cruelty). Hii ni pamoja na kupigwa, kunyanyaswa kwa namna mbalimbali. Ukatili hata wa kisaikolojia unakubalika. So, ukatili ni neno pana
(3) Kutelekezwa (dessertion). Kama mwenzio amekutelekeza. eg kwa kuondoka bila kujua aliko, au bila kuitunza familia na kutokomea. Pia kunaweza kuwa na kutelekezwa hata kama bado yuko ndani ya nyumba. e.g kama anagoma kuzungumza kabisa na pengine kuhama chumba. in short mnakuwa kama nyumba 2 ndani ya 1.

NB:
1) Mahakama yoyote ina mamlaka ya kutoa talaka. Kuanzia mahakama ya mwanzo, ya hakimu mkazi/wilaya au mahakama kuu.

2)Kabla ya kwenda mahakamani kuomba talaka LAZIMA upitie kwanza baraza la usuluhishi la ndoa (marriage conciliation board). haya mabazara yameanzishwa kwa mujibu wa sheria na yapo mengi sana. Mara nyingi misikitini na makanisani utayapata. Pia ofisi za ustawi wa jamii watakuwa na orodha yake. Mnatakiwa muende huko kwa usuluhishi na kama watashindwa kuwasuluhisha wataandika taarifa kuwa wameshindwa. Hii itahitajika mahakamani kwa ajili ya maombi ya talaka. Bila kuanzia huko mahakama haitapokea maombi yako.
NB Kama ndoa ni ya kikristu ukienda baraza linaloendeshwa na kanisa wanaweza wasikuandikie hiyo taarifa ili ukavunje ndoa. Kumbuka ndoa zao hazikubali talaka, kwa hiyo watafanya kila jitihada kuinusuru.

Ushauri.
talaka sio jambo jema sana hasa kwa watoto. Inakuja na implications nyingi sana-nani akae na watoto, vipi walelewe, matunzo etc. na mbaya zaidi ni kuwaathiri kisaikolojia. kama unaweza kuiepusha tafadhali fanya hivyo.
Pia ujue talaka inatoka tu kama kuna ndoa halali yenye cheti. Hauwezi kuvunja kitu ambacho hakipo. kama mnaishi tu kama mahawara (concubines) au masuria huwezi kuomba talaka. Ila kama mmekaa miaka angalau 2 na jamii inayowazunguka inawachukulia kama mke na mume, basi ukienda mahakamani kama hivi mahakama itadhania (presume) kuwa kuna ndoa (presumption of marriage) kwa lengo tu la kuweza kuwagawia mali mlizochuma pamoja.

Naamini nimekupa mwanga. Unaweza kwenda kwa wanasheria wanaotoa msaada wa kisheria wakakusikiliza wakakupa ushauri. Wako Kituo cha sheria na haki za binadamu, NOLA, TAWLA, Chuo kikuu dsm, Kipo pia pale parokia ya msimbazi centre. etc.
Anonymous said…
Ni kweli Mahakama hawavunji ndoa, itapelekwa hata miaka mingi tu. Kikubwa ikiwa umechoka kukaa na mume tengana nae wewe uhame angalau upate peace of heart and mind kuliko kundelea kukaa na huyo chui.
Anonymous said…
pole mdada..mambo ya ndoa magumu hasa kwenye migogoro...

mie sio mtaalamu wa masuala ya sheria au kuamulia hasa ukizingatia am single..

labda niulize..je ndo yenu ni ya dini gani?...kama ni ya kikristu basi waone viongozi wa dini mnapoendaga wakupe ushauri pia na wazazi wote hasa wazazi wake mwanaume kama mnaelewana...

sijajua chanzo cha wewe kumtaka aondoke yaani nini tatizo maana kujua tatizo nayo inasaidia kujua jinsi ya kutoa ushauri...

pia kama ni ndoa ya kiislamu ni rahisi u just see wazazi wa pande zote waeleze matatizo yenu na sema unataka kuondoka..wakikupa go ahead then huyoo..

Ila watoto kama mmezaa aisee ni issue kubwa sana..u better ishi nae same house for sake of kids japo kila mtu anaweza kulala kivyake...family 1st..

anyways inakuwa ngumu kushauri kwavile sijajua dini yako na ugomvi wenu ni wa aina gani...

swali je yeye si anakupenda na anataka muwe wote ...if yes give second chance and see if he can get back to those days ...ha haaa

Gluv ..gluv100@yahoo.com
emu-three said…
Swali kubwa la msingi, ulifungia wapi ndoa? Kwani ulipofungia ndoa ndipo unaweza kwenda kuivunja hiyo ndoa!
Mimi naona ajabu kabisa ndoa mnafungia kanisani au msikitini, lakini talaka mnatoleana mahakamani, mahakama ndio Mungu? Ndoa inashikamana na imani ya dini yako au wahatever, labda kama ulifungia bomani, basi ni halali kwenda hukohuko!
USHAURI: Ndoa ina mitihani, na ni vyema talaka ikawa ndio suluhisho la mwisho , kwasababu huenda tatizo hilo lililopo linaweza likawa sababu ni wewe mwenyewe, kwahiyo omba ushauri, omba wakuu wa dini yako waje mkutanishwe, ili huenda mwisho wa siku mkapendana saana. Lakini ikishindikana basi utafanyaje...!
Anonymous said…
Eleza vizuri anakufanyaje ili tunapochangia tujue pa kuanzia. Sikiliza Binti" huruhusiwi kutoa taraka kwa mumeo mpaka kama vitu vifuatavyo huvipati.
1) Hupati Ndoa anakunyima Unyumba makusudi.
2) Kawa Hanithi Mboo yake haisimami tena.
3) Mboo yake ni kubwa sana
anakuumiza anapokupa unyumba.

Mbali na sababu hizo hurhusiwi kutoa taraka. sasa sema anakufanyaje?...Kizito!!
Anonymous said…
Dada Dina umekuwa kimya sana. Mzima wewe. Tunamiss comment za blog yako