Thursday, 24 March 2011

Baada ya kutendwa ndoani, nachukia wanaume wote....nifanyeje?

"Pole na kazi ya kushauri,kuelimisha n.k jamii. Kwanza napenda kukupa kheri ya mwaka mpya dada DINAH. Mimi ni mwanamke wa miaka 29 ingawa mapema sana this year natimiza 30. Nilipokua na umri wa miaka 24 nilibahatika kupata mchumba na hatimaye kuolewa na kupata mtoto wa kiume, Kwa sasa nimeachika. Wakati wa Uchumba na mwanzoni mwa Ndoa Mume wangu alikua mchaMungu wa kweli kiasi kwamba tulikua tunagombana nisipo swali[ni waislam] Hali ya kimaisha niliyomkuta nayo mume wangu haikua nzuri, ikabidi Baba yangu atusaidie mimi na mume wangu. Hivyo mambo yakawa mazuri tena sana kwani tulianzisha Biashara zetu ambazo kiukweli zilitukubali. Baada ya mambo kuwa mazuri, mwenzangu akaanza kubadilika akawa mlevi,wanawake ndio usiseme! Nilipokwenda nyumbani kujifungua, huku nyuma akawa anaingiza wanawake kila siku tena kwa kuwabadilisha. Niliporudi nikapewa habari zile nikamuuliza akakataa. Basi nikaanza kuchunguza na Mungu aliniwezesha nikabaini ukweli niliyokua nikiambiwa. Kwavile nilibaini mwenyewe,nilikua na vielelezo nilipompatia alikua mpole na kukiri ni kweli akaomba msamaha nami nikamkubalia. Ila kumbe hakua ameacha tabia yake. Nikawaeleza wazazi wake wakamuita na kumsema hakusikia. Tukapelekana BAKWATA akaitwa akasemwa na wakamwambia kwavile amekua mchafu wa tabia kwanza tukapime afya lakini yeye akakataa na kusema kama ni hivyo bora anipe Talaka yangu. Mimi tangu nitoke kujifungua sikua nimeshiriki nae tendo la ndoa na hata baada ya kumsamehe pia sikutaka kushiriki nae kwani nilikua nikimwambia tukapime ndio tushiriki. Kinachonifanya niombe ushauri ni kwamba kwa sasa simuamini mwanamme yeyote naona wote ni wadanganyifu. Niliwahi kupata mwanamme ila aniponitamkia kunioa nikamchukia na kuachana nae. JE,NIFANYEJE?" Dinah anasema: Heri ya mwaka mpya kwako pia, asante sana kwa kuniandikia na kwa uvumilivu, vilevile nakupa pole kwa yote uliyokabiliana nayo katika umri mdogo. Hongera sana kwa kuwa na msimamo wa kugoma kushirikiana nae kimwili mpaka mkapime afya zetu....well technically afya yake yeye mwenye tabia chafu. Hakika, ukiumwa na Nyoka mara moja lazima utaogopa sana hata ukiguswa na jani. Unahitaji muda kuweza kumuamini mwanaume na hiyo ni hali ya kawaida kabisa, wala usihisi presha kutoka kwa Jamii inayokuzunguuka kuwa una mkosi au huwezi kuolewa tena(Hakuna kitu kibaya kama kufungandoa ili kuridhisha Ulimwengu, kumbuka walimwengu hawana wema na huwezi kufurahisha kila mtu kwenye jamii yako). Kitendo cha kuanza kutoka na wanaume wengine kinaonyesha umeanza "kupona" maumivu aliyokupa Mumeo wa ndoa, lakini linapokuja suala la kuwa na uhusiano wa kudumu unashindwa kuji-commit kitu ambacho kinaeleweka. Nini ch akufanya: Usiwe na haraka na usijali wasemayo Walimwengu kuhusu ndoa ya awali au lini utaolewa tena, nenda taratibu na tumia muda wako vema huku ukifurahia maisha kama mwanamke anaejitegemea na mwenye uzoefu (ndoa yako iliyopita ichukulie kuwa ni uzoefu unaokufanya ujue utakacho maishani mwako na sio Mkosi). Ikitokea tena umemdondokea mwanaume kimapenzi, hakikisha unakuwa muwazi kabla uhusiano haujaota mizizi. Mueleze mpenzi huyo nia yako(kwamba huna haraka sana kufunga ndoa). Unatakiwa kuwa a bit smart unapoliweka hili suala wazi kwani kamamwanaume ni mjinga-mjinga anaweza kudhani kuwa unataka akuchumbie kumbe wee huna mpango huo. Sasa unatakiwa kujiwekea malengo, mfano:- Napenda kutekeleza hili na lile kabla sijaamua kutulia na kujenga familia n.k. Natumaini maelezo ya wachangiaji na haya yangu yatakuwa yamesaidia kiasi fulani kujua nini chakufanya, ila kubwa zaidi ya yote ni kujipa muda na kufurahia maisha kama Mdada/mwanamke/single.....kumbuka umeolewa ukiwa na miaka 24, huu ndio u mri wa kufurahia "uanamke"....kwamba wewe ulitoka kuwa Binti wa moja kwa moja na kuwa mke wa na Mama wa.....hujawahi kuwa wewe bila kuwa chini ya.... Kila la kheri.

12 comments:

Anonymous said...

Pole rafiki.
Ni kweli inakuwa ngumu kuamini wanaume wengine lakini wewe ni binadamu na utapenda tu siku moja.
Mi nna historia mbaya kwenye mapenzi ila nadhani na mwenyewe nachangia pia.
Niliolewa nikafanyiwa vimbwanga wewe mwenyewe nikabwaga manyanga. Nikapata mwingine nikaolewa, huku mambo kidogo hayakuwa kama yale ila na kwenyewe hakukua shwari sana, ila nikang'ang'ania weee pamoja na yote mpaka mume wangu akafariki dunia kwa ajali. Sasa ndo nna kimbembe.... nawaza usaliti na hili la kufiwa nalo linaingia humo humo, naogopa kupenda ntatendwa, na hapohapo naogopa kupenda atakufa aniache mpweke tena, basi nipo tu......!

Anonymous said...

Mh pole sana Dada. Ndoa zina mambo mengi ndani yake.Kwa hali ulifikia katika ndoa yako ni sahihi kuchanganyikiwa. Hata hivyo pamoja na tabia hiyo ambayo wanaume wengi tunayo sikuungi mkono kuwachukia wanaume wote. Bado kuna wanaume waliotulia na kwa umri wako wamiaka 29 jipe moyo utampata mwingine japo hutakiwi kukurupuka.Jitahidi kusahau yaliyopta . Pole sana

Anonymous said...

Pole sana. Usijali utapata mwingine ambaye atakustahi na kukulinda.Maisha ndivyo yalivyo hutakiwi kukata tamaa

Anonymous said...

Pole sana bibie. Naamini umepata mshtuko mkubwa juu ya wanaume kwa sababu ya mumeo uliyemwamini kukutenda kihivyo.

Nimeshangaa kwamba ulipata mtu tena muungwana anayetaka kukuoa ukamtupilia mbali? Nakuomba ubadilishe moyo wako kwani si wanaume wote wako hivyo.Kuna wanawake pia wenye tabia mbaya, lakini wanaume hatujawajumlisha kihivyo na tunazidi kuwakubali.

Usiliweke tatizo la mmoja kuwa ni tatizo la woteeeeeeeeeeee!! Anza kupenda wanaume kwani wapo wenye nia na heshima nzuri kabisa.Mimi niandikaye hapa ni mwanaume na niko single hadi nimetamani ningekufahamu hata kesho ningefika karibu nawe ili tupeane mawili matatu tuone ni jinsi gani tunaweza kutoana hizo BP tuanze ukurasa mpya wa maisha.

Nakutakia maisha mema na ya baraka.

Anonymous said...

Kwanza, pole sana kwa mkasa huo. Pili, nakushauri ushikilie msimamo wako huo huo: hamna unyumba bila kupima afya. Tatu, mnaweza kutengana ili kumpa muda afikirie kama bado yuko serious na ndoa na mtoto wake au la. Kama bado yuko serious na atakubali kutulia basi lazima akubali masharti ya ndoa mliyoyaweka wakati wa nikaha. Kama bado anataka kuendelea kuwa kiruka njia, basi kubali tu huyo hakufai na focus kwenye maisha yako na ya mtoto wako. All the best.

Anonymous said...

Mtoa ushauri wa kwanza, Pole sana na kutendwa.Pia POLE SANA NA KUFIWA NA MUMEO WA PILI.

uMEONGEA KITU KIMEGUSA SANA MOYO WANGU NA UNAONEKANA NI MWANAMKE MWENYE STAHA NA HESHIMA SANA KWA JINSI NILIVYOKUPATA KWA LUGHA NA MAELEZO YAKO.

Nakuombea Mungu akutulize sana na kukuumbia moyo wa ujasiri na kusahau yaliyopita ili uangalie mbele.

Naamini Mungu atakuponya na majeruhi hayo.Ingekuwa tunataja na anwani zetu humu ningewasiliana na wewe kwa kufahamiana zaidi kwani umenigusa sana dada.POle sana!! Nina mengi ya kuongea na wewe kama kutakuwa na namna ya kuwasiliana moja kwa moja nawe.

Anonymous said...

pole sana dada yangu kwa matatizo yaliyokufika. maumivu ya mapenz yanahtaji utulivu wa mwili na akili ili kulinda kudhohofisha v2 hvyo viwili muhimu.
Kwanza ningekushauri ujipe mda wa kujiweka mbali na mazingira yatakayotengeneza mahusiano yakimapenz kabla ya kipindi ulichojiwekea na uhakkshe umeweka mda wa kutosha. Pili ucweke akilini kuwa kila mwanaume ni sumu ya mwili na akili yako icpokua utambue kwamba utulivu na kujiamini kutakufanya umpate mwanaume ambaye atakufaa kimaadili na kimaisha pia. Kumbuka kwamba leo umetendewa ww mwanamke lkn kesho utalckia tatizo hilo hilo kwa mwanaume akilalamika, nayeye 2mshauri achukie kila mwanamke? HAITAPENDEZA!!
Huo ni mtazamo wangu kwa ufupi lakini yote kwa yote unatakiwa umweke mungu mbele ktk iman yako utafanikiwa. Kila la kheri.
jcaustical@yahoo.com

Anonymous said...

Asante sana anonymous wa saa 7:32 PM.
Tumia sdobogo@yahoo.com kuwasiliana nami.
Siku njema.

Anonymous said...

jamani anonymous saa 1:34:00 pole dia umenitia simanzi sana let ur self luv again hakuna mtu aliyezaliwa na bahati mbaya ni maisha tu

nunu said...

nawashukuru sana wote mlionishauri ukiwepo dada dnnah mwenyewe mungu awabariki sana kwa kunitia matumaini mapya.Nawaahidi nitayafanyia kazi.Na kwa wale wanaotaka kunipa ushauri zaidi naomba watumie nunu_ibrahim@yahoo.com

nunu said...

Nawashukuru sana

nunu said...

nawashukuru sana wote kwa kunipa moyo na ushauri wenu mzuri.Kwa wale ambao wangependa kuendelea kunipa ushauri watumie nunu_ibrahim@yahoo.com. Dada Dinna nakushukuru sana mungu akubariki.