Sunday, 6 February 2011

Natafuta njia ya kushika na kubemba mimba-Nifanyeje?

"Dada Dinah, umri wangu ni miaka 33 miaka miwili tangu nimefunga ndoa nilibeba mimba lakini kwa bahati mbaya iliyoka baada ya miezi mitatu tu, mpaka leo sijashika tena mimba. Nimeenda Hospitali zaidi ya mara moja kwa ajili ya uchunguzi lakini nimeambiwa sina tatizo lolote.

Vilevile nimejaribu kutumia dawa za Kienyeji lakini sijafanikiwa kushika mimba mpaka leo, je kuna njia nyingine yeyote inayoweza kunisaidia kushika mimba tena bila kunywa dawa za Clomid? Naomba mnisaidie....

Nimefurahi sana kupata email yako.

Asante."

10 comments:

Anonymous said...

Hilo ni tatizo ambalo hata mimi ninalo dawa za hosp. nimekunywa ingawa madaktari wanasuma mimi na mume wangu hatuna tatizo lolote, za miti shamba nimekunywa sasa iliyobaki tunasubiri miujiza ya Mungu tu.sijui ni mavyakula tunayokula au mahusiano yanyuma tuliowahi kuwa nayi ndio yanatutesa(ex boyfriend ans ex girlfriend wameenda kwa wataalamu kuzuia mimba zisishike) lakini penye wangi hapaharibiki neno tuwaachie wachangiaji watatuambia jipya tusikilize.

Anonymous said...

JARIBU KUNYWA VIDONGE VINAITWA FOLIC ACID, UKITAKA MAELEZO ZAIDI I GOOGLE THEN USOME MAELEZO YAKE.

Anonymous said...

Ulishashika mimba ikatoka na hospitali wamekuambia huna tatizo, dada stress pia inaweza kukufanya usishike mimba. Ondoa mawazo kuhusu kushika mimba na ukiwa unafanya mapenzi jitahidi juweka mandhari ya kimapenzi kama vile ndiyo wapya mnaonana.

Punguza pombe pia kama ni mywaji na angalia vyakula unavyokula, pata mapumziko ya kutosha.

Anonymous said...

pole dada yangu kwa maswaiba yako nakushauri ufanye yafuatayo, ukianza kubleed hakikisha unahesabu siku ya kwanza hadi ifike siku ya kumi na nne then do na jamma yako utapata mtoto. pili hakikisha kabla ya siku ya kumi na nne mmme wako anakula vizuri hasa vyakula vya protein.

Anonymous said...

Pole sana kwa tatizo lako, lakini mimi nakushauri acha kabisa kutumia dawa hizo za mitishamba ,kwasababu ilishashika mimba kwa mara ya kwanza basi ni dhahiri kwamba huna tatizo, na sijui shida yako ni nini mbona umeolewa juzi tu, watu wanakaa hadi miaka kumi ndo wanapata watoto wewe juzi tu unaanza kuhangaika na miti shamba. Ni vema ukijua kwamba sio kila tendo la ndoa linaweza kukupa ujauzito, inategemea na mzunguko wako wa mwezi upoje. Nakushauri rilax,wala usihangaike haitaisha miezi sita utapata ujauzito.
Wakati mwingine dawa hizi za uzazi wa mpango zinaweza kufanya uchelewe kubeba ujauzito hata kama umeacha kwa kipindi cha miezi nane dawa inakuwa na nguvu mwilini.

Anonymous said...

kushika mimba kunachangiwa na vitu vingi. Sina hakika ulipokuwa unameza clomid ulikuwa unalenga nini?
kwa kifupi ili mimba ishike miongoni mwa mambo muhimu ni pamoja na uzima wa kizazi cha mama pamoja na uzima wa mbegu za mume wake. Kingine ni tarehe za kukutana na mwanamme, kwa sababu hata kizazi kikiwa kizima na mbegu za mwaname nzima sio tarehe yoyote mimba inaweza kushika. Kitalaamu kama hamuwezi kulenga zile tarehe za kushika mimba basi unatakiwa angalau mkutane mara nne au tatu kwa wiki.
Lakini pia umesema kuna mimba iliwahi kutoka. Hivyo yawezekana lile tatizo lililofanya mimba ikatoka ndio hilo ambalo linazuia usishike mimba, au wakati mwingine mimba iliyotoka imeacha madhara ambayo hayajatibiwa na haya madhara yanachelewesha kushika mimba. Jingine wanawake wa umri wako ambao hawajapata watoto huwa wanakabiliwa na matezi ya kizazi (fibroid)Matezi hayo yanaweza sababishwa na kutokupata mimba mapema lakini pia yakisha tokea nayo yana tabia yakuzuia mimba kushika. Nenda hospitali pamoja na mumeo mkachunguzwe kwa pamoja. Msikate tamaa. Waweza pata ushauri zaidi. Email- hiishkamili@yahoo.com

Anonymous said...

Niliwahi kukutana na mwanamke aliyepewa talaka kwa kuwa hazai ingawa alikuwa na mtoto kabla ya ndoa na mumewe alikuwa na watoto kabla ya ndoa. Ilinigharimu shs. elfu kumi tu kumsafisha na kumpachika mimba heshima yake ikarudi. safisha na siku ya 14 pigwa mboro utashika mimba

Anonymous said...

Niliwahi kukutana na mwanamke aliyepewa talaka kwa kuwa hazai ingawa alikuwa na mtoto kabla ya ndoa na mumewe alikuwa na watoto kabla ya ndoa. Ilinigharimu shs. elfu kumi tu kumsafisha na kumpachika mimba heshima yake ikarudi. safisha na siku ya 14 pigwa mboro utashika mimba

Anonymous said...

@anonymous wa 10.06am, ulimsafishaje uyo dada akapata mimba haraka hivyo? embu tuelimishe basi wengi wanahitaji watoto na wana matatizo km huyu dada, clomid haijasaidia....sasa solution ni nini?

Anonymous said...

Sina tatizo la kizazi, sijapata siku zangu huu ni mwezi wa pili sasa nikipima mimba naambiwa negative. sielewi nifanyaje nishauri ndungu yangu