Monday, 27 December 2010

Mpenzi aninyanyasa kisa Umasikini, sasa ataka ndoa, je atabadilika?

"Habari dada Dinah, Mimi ni msomaji mkubwa wa Blog yako na ninapenda Posti kwani zimetusaidia wengi. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 natokea Mkoani Tanga lakini kwa sasa naishai Zanzibar na mpenzi wangu alienichukua nyumbani.

Ninamshukuru Mungu kwani mpenzi wangu ananijali na kunitimizia mahitaji yangu ikiwemo na kuwasaidia wazee wangu nyumbani. Lakini huyu mpenzi anasema kwa kila mtu alie karibu nae kuwa kwetu ni masikini na sote tunamtegemea yeye. Hali hii huzidi hasa tukiwa na ugomvi.

Nimewahi kumwambia mara kadhaa kwamba sipendi tabia yake hiyo, lakini bado hana dalili yeyote ya kuachana na tabia hiyo. Ikitokea ananigombeza basi huwatusi mpaka wazee wangu jambo ambalo hunitia uchungu sana.

Zaidi ya yote anasema hafurahii sana ladha ya tendo la ndoa kwa hiyo anataka tufanye kinyume na maumbile, kitu ambacho mie siwezi kuthubutu kukifanya.

Kwa bahatimbaya au nzuri nimekutana na Kaka mmoja Mzanzibari ambae anadai kuwa ananipenda sana na yupo tayari kufunga ndoa nami nikamwambia kuwa ninampenda lakini kuna mtu ninaishi nae.

Kusema ukweli ninampenda huyu Mkaka niliekutana nae, aliomba akanitambulishe kwao lakini mimi nikamuomba akanitabulishe kama rafiki kwani sikutaka wajue kutambulishwa kama mpenzi wakati niko kwenye uhusiano na mtu mwingine japo sina amani.Familia yake walionyesha kunipenda.

Tatizo linalonisumbua ni kuwa huyu mpenzi ninaeishi nae ametangaza ndoa, lakini mie sitaki kuolewa nae kutokana na tabia zake za kinyanyasaji, sasa sijui nimueleze mama yangu ukweli wa mambo ili nipate mawazo yake au nikubali kuolewa nae kwa kuamini kuwa atabadilika!!

Au nitafute njia ya kuachana nae ili niwe na Kaka wa Kizanzibari alienitambulisha kwao kama rafiki lakini nia yake ni kufunga ndoa nami?

Naombeni ushauri
Asante"

Monday, 20 December 2010

Nifanye nini ili nidumu na Kimwana?-Ushauri


"Habari wanablog, mimi ni mwanaume na nimejaaliwa kuwa na mpenzi wangu ambae anaonekana sio mzungumzaji sana mbele yangu lakini nina uhakika kuwa ananipenda kwani huwa anazungumza na watu wake na watu hao kuniambia mimi kiasi gani ananipenda.


Tatizo ni kuwa sina ile hali ya kujiamini kwani huwa napatwa na hisia kuwa muda wowote mpenzi wangu anaweza kunitoka. Sasa nifanye nini ili niweze kudumu nae?


Asanteni."

Huu unaweza kuwa Ugonjwa wa Bawasiri?-Msaada!

"Habari za leo Dada na wadau wote wa hapa, nimekuja hapa kupata msaada wa kimawazo na ushauri. Kuna hali ambayo huwatokea watu sijui niite ugonjwa! Ni kwamba kule kwenye njia ya haja kubwa kunakuwa kama kuna utumbo unajitokeza kwa nje.

Je nini sababu ya tatizo hilo na je kinga yake ni nini? Pia kama unatatizo hilo tiba yake ni nini?

Natanguliza shukrani zangu.

Asante."

Dinah anauliza: Sina uhakika kama unachozungumzia ni ugonjwa wa Bawasiri (Piles au Haemorrhoids), tafadhali kama unaweza naomba utupatie dalili anazokuwa nazo mhusika/mwenye tatizo ili uweze kupata ushuri wa yakinifu.

Saturday, 11 December 2010

Vita kati ya Mpenzi wa Bagamoyo na Arusha, mie napenda Arusha-Nifanyeje?

"Shikamoo dada Dinah! mimi ni Kiajana kutoka Arusha lakini kwa sasa niko Chuoni hapa Dar. Ni mtembeleaji mzuri sana wa Blog yako. Leo dada naomba ushauri wako kwani umewasaidia wengi kimawazo.

Nimewahi kuwa na mpenzi kutoka Bagamoyo lakini sikumpenda, baada ya muda nikapata mwingine kutoka Arusha ambae ninampenda na hivyo kuanza mahusiano kabla sijamwambia yule wa Bagamoyo kuwa sitaki kuendelea nae, nilikuwa natafuta jinsi ya kumwambia ukweli.

Baada ya wiki mbili na nusu tangu nianze uhusiano mpya, nikagundua kuwa mpenzi nimpendae wa Arusha anajuana na yule nisie mpenda wa Bagamoyo kwani walisoma wote na hata kuchangia chumba bwenini. Baada ya kugundua hili nikaamua kumwambia wa Bagamoyo Ukweli kuwa sivutiwi nae na kwamba sitoweza kupanga mipango ya kimaisha ya mbeleni na mtu ambae sijampenda kutoka Moyoni.

Nikamwambia kwa sasa ninampenzi mwingine (nikamtajia yule wa Arusha) yeye akadai hadhani kama huyo wa Arusha ananipenda kwani alikuwa anajua uhusiano wetu yaani mimi na yeye huyu wa Bagamoyo.

Sasa juzi hapa(tarehe 5) kamtukana sana mpenzi nimpendae wa Arusha na huyu mpenzi wa Arusha anatishia kuniacha, kiukweli nampenda sana na hata kuanza kupanga nae mipango ya kimaisha kama mtu na mpenzi wake, lakini shida ni huyu Mbagamoyo.

Tafadhali dada na wadau wengine naombeni ushauri kwani nina mawazo mengi mpaka nashindwa kuzingatia masomo.

Nifanye nini?"

Friday, 10 December 2010

Mpenzi anapenda ning'ae wakati wa tendo, je nitumie nini?

"Kabla ya yote naomba kukushukuru Dinah na wadau wote wa Blog hii, Kwa hakika michango yenu imenifunza mengi sana sana. Hapa Dinahicious nimejifunza mengi na ninazidi kujifunza masuala mbali mbali ya Ngono na mahusiano jinsi siku zinavyozidi kwenda. Mbarikiwe wote.

Nikija kwenye swali langu, hivi karibuni natarajia kufunga ndoa, mimi namchumba wangu tumekuwa tukishirikiana sana kwenye suala hili la ngono ili kila moja wetu afurahi nakuridhika na kwa kweli nafurahi kusema kuwa sote tunafurahia.

Nilikuwa natabia ya kutazama Picha za Ngono kabla sijakutana na mchumba wangu, nilikuwa nahusudukuona vile actress wa picha hizo wanavyo ng'aa wanapofanya ngono nadhani ni mafuta lakini sina uhakika. Sikuwahi kufanyia udadisi wala kujaraibu kutokana na sababu kadhaa.

Sasa nimegundua kuwa mchumba wangu nae anapenda nipake ili mwili wangu ung'ae lakini mimi sijui kama ni mafuta au ni aina ya maji yanayong'aa. Kama kuna yeyote anajua naomba mnisaidie kwa kunieleza ni bidhaa gani ile, je ni mafuta na kama ni mafuta yanaitwaje?

Asanteni sana."