Thursday, 25 November 2010

Mimba ya kwanza iliharibika, kila tukijaribu tena sishiki Mimba-Nifanyeje?

"Habari dada Dinah, Mimi ni mwanamke wa miaka 26 na nimeolewa mwezi wa 9 mwaka huu. Tatizo langu kubwa ni kwamba, mwaka jana nilipata Ujauzito lakini mimba iliharibika baada ya miezi mitatu kwani nilikuwa natokwa damu nyingi sana na hivyo kupelekea kusafishwa.

Baada ya hapo nikawa nasumbuliwa sana na maumivu ya tumbo ya vichomi. Nilikwenda tena Hospitali na wananiangalia kwa Utrasound lakini hawakugundua tatizo ni nini! Nimefanya vipimo vya magonjwa mengine pia inaonekana niko salama.

Hivi sasa najitahidi kushirikiana na mume wangu kimapenzi lakini sina dalili yeyote ya Mimba. Mume wangu inaonyesha kuwa anatamani sana kupata mtoto kwani hata mtoto. Je dada na wachangiaji wengine mnanipa ushauri gani kuhusiana na tatizo langu hili.

Nifanyeje mwenzenu ili nishike mimba? Hapa nilipo sina raha kabisa, nazidi kuwa na machungu kila nikiona mwanamke ana mimba. Naombeni ushauri wenu, nifanye nini?

Dada A-Moro"

Thursday, 18 November 2010

Baada ya miaka 2 nimegundua kuwa mimi ni The Other Woman~Nifanyaje?

"Hi Dada Dinah na wachangiaji wengine, asante na pole kwa kazi ya kutushauri maana wadada kilakukicha hatujambo kwa maswali. Mimi ni mwanaama wa miaka 27 mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Nimekuwa na uhusiano na Kijana mmoja wa miaka 25 kwa muda wa miaka miwili, sikufichi ananipenda sana na kunijali.Kijana huyu anashughuli zake binafsi kwani amejiajiri.

Sasa kipindi chote hicho tumekuwa pamoja ni hivi karibuni tu ndio nimegundua kuwa kumbe mwenzangu alikuwa na msichana mwingine na wamejuana kwa muda wa miaka 5. Baada ya kugundua tulikorofishana na alikuja kuniomba msamaha na mimi bilakujijua nikakubali na kumsamehe na hii imetoeka mara chache mpaka nahisi kama vile Jamaa ana dawa ya kunifanya nisamehe haraka.

Mpenzi huyu amekwisha enda nyumbani kujitambulisha kwa mama, kiukweli jamaa ananifikisha na kunijali pamoja na mwanangu ingawa hatuishi pamoja. Lakini ninapofikiria kuwa nina mwenzagu huwa nakosa raha na wakati huohuo sielewi huyu jamaa ana nia gani na mimi.

Swali la Kwanza: Unadhani huyu jamaa anampango gani na mimi?

Swali la Pili: Je niendelee kuwa nae au niachane nae?

Kama ni kumuacha nimejaribu mara nyingi lakini kila akirudi nakuniomba msamaha najikuta nasamehe tu, pia anatabia ya kunitumia pesa nyingi kama hana akili nzuri ikiwa nitamchunia.

Naomba mnishauri wana Dinahicious,
Asante."

Wednesday, 10 November 2010

Nikifanya tendo nachanika na kutokwa Damu kama Hedhi-Help!!

"Pole na kazi mamii, mimi ni mwanamke wa miaka 32. Ninatatizo ambalo nimeshindwa kupata tiba yake hata bada ya kwenda kumuona Daktari. Mimi na mpenzi wangu tumekuwa pamoja kwa muda wa miaka miwili.

Mwanzo tulikuwa tukitumia Condom tunapofanya mapenzi lakini mimi nilikuwa napatwa na maumivu makali sana na wakati mwingine kutokwa na damu kama vile niko kwenye siku zangu za Hedhi.

Baada ya muda nikaja kugundua kuwa nilikuwa nachanika kidogo kidogo ukeni, basi tukakubaliana kuacha kutumia Condoms. Pamoja na kuacha kutumia Condom bado hali hiyo iliendelea kila ninapofanya mapenzi na Boyfriend wangu.

Nilipokwenda kwa Daktari, nilishauriwa niwe nabana sehemu zangu za siri kama vile navuta pumzi, nikajaribu kufuata ushauri huo lakini wapi! Sasa nimeanza kupatwa na mawazo je kuchanika huku chini kunaweza kunisababishia Cancer, labda sitoweza kushika mimba na kuendelea kuchanika zaidi na zaidi.

Naomba ushauri wenu wee Dada Dinah na wasomaji wengine. Asante"

Monday, 8 November 2010

Ushuhuda: Asanteni kwa Ushauri!

"Hi da Dinah na wanablog wanzangu, nimewahi kuja na swali “"Ex ananirudisha nyuma kihisia, nami nataka ndoa-Ushauri" Nashukuru kwa ushauri wenu kwa ujumla umenisaidia na namshukuru Mungu kwa kuwa mvumilivu na kuyafanyia kazi mawazo yenu.

Nimejitahidi sana hadi nimefikia hap, kwa ufupi nimefanya kama mlivyo nishauri kwani niliona anazidi kunifatilia nilichofanya nilinunua line mpya nikamtumia x-boyfriend wangu na kumwambia kwa upole kabisa kua hii line ndio yangu ya sasa. Ile ya zamani usiitumie nimempa Mother atumie hivo ukitaka kunipata tumia hii ya sasa.

Hivyo ametumia kuwasiliana kupitia hii ya sasa na kunitaka tuonane lakini kila siku nikawa namdanganya kuwa kuna kazi kidogo imenibana anisubiri baada ya wiki kama nne hivi nitakua free then tutaenjoy nae akakubali.

Baada ya kuona amekubali nikarudi kwenye line ile ya zamani na kuanza kuitumia hii mpya nikaitupa hivo akawa anashindwa kunitafuta kupitia ile ya zamani kwani nilishamwambia kua ipo na Mother.

Nafikiri amesubiri hadi mwisho amekata tamaa akaacha kunitafuta na kitu cha kushangaza zaidi njiani hatukutani kama zamani, kwa sasa naishi maisha safi raha mstarehe na mpenzi wangu hakuna anaenisumbua wala nini.
Nawashukuru sana".

Dinah anasema:Nafurahi kuwa umefanikiwa kufanya uamuzi na sasa unaendelea vema na mpenzi wako ambae unataka kufunga nae ndoa. Lakini mbinu uliyotumia sio nzuri na nitakuambia kwanini?

Umekosea sana kumpa matumaini ya kukutana na ku-enjoy nae wakati huna mpango huo. Mwanaume sio mtu wa kukata tamaa kirahisi hivyo hasa kama anakupenda, ikiwa atakukosa kwenye Line uliyotumia anaweza akajaribu kupiga au hata kutuma ujumbe kwenye namba yako ya zamani ambayo ndio unayotumia sasa.

Siku moja mpenzi wako ulie nae sasa anaweza kukutana na ujumbe kutoka kwa Ex wako huyo na hivyo kutaka kujua ukweli wa nini kinaendelea kati yako na huyo Ex. Sidhani kama ungependa hilo likutokee.

Pamoja na kuwa kwa sasa hamkutani mtaani haina maana jamaa amehama Mji au eneo hilo, ipo siku atarudi na mtakutana, je utamueleza nini kuhusianana ahadi uliompa?!!

Unachotakiwa kufanya ni kumwambia jamaa ukweli ulio wazi kuwa humtaki na sasa uko kwenye uhusiano mwingine na usingependa uhusiano wako huo uharibuke kwa sababu yake. Kama mtu mzima atakuelewa na kukubali kuwa hawezi kuwa na wewe kwa vile tayari una mtu mwingine.

Kila la kheri!

Wednesday, 3 November 2010

Fungus zimenimalizia hamu ya NNgono-Ushauri!


"Pole na kazi Dada Dinah, mimi ni mwanamke wa miaka 22, ninampenzi wangu ambae tunapendana sana na tumedumu kwenye uhusiano kwa miaka 5. Tatizo langu ni kwamba nimeishiwa na hamu ya kufanya mapenzi na huu sasa ni mwezi wa nne.


Ikitokea nafanya mapenzi basi nitajitahidi mzunguuko wa kwanza tu na baada ya hapo K inakuwa kavu na kupata maumivu makali ukeni. Tatizo hili limefanya mpenzi wangu ahisi vibaya kuwa labda nina mpenzi mwingine anaeniridhisha nje ya uhusiano wetu.


Ukweli ni kuwa nina Fungas ambazo zinanikosesha raha (nawashwa sana) najitahidi kuzitibu lakini hali haibadiliki mpaka sasa nimeanza kukata tamaa, hili ndio nadhani kuwa ni tatizo linalosababisha niumie wakati wa kufanya ngono.


Naomba ushari wenu kuhusu tatizo hili, linasababishwa na nini na nitumie dawa gani ili nipone? Asante"