Wednesday, 29 September 2010

Mume aki-cheat na mwenye umbo tofauti na lako anaweza akawa bado anakupenda kama zamani?

"Dada Dinah mie naomba kuuliza,hivi kweli mumeo akitembea nje ya ndoa na mwanamke ambae hamfanani kabisa ikimaumbile anaweza akawa bado anakupenda?

Nimeuliza hivyo kwa kuwa mimi ni size 12 though kabla sijajifungua nilikuwa navaa chini saizi 14 juu saizi 12 kwa sasa nimepungua sana (na nimependa mwenyewe kupungua). Mwanamke ambae mume wangu alikuwa na affair nae for almost two months (kama ni mkweli) ni wale ambao ni ngumu hata kupata saizi dukani, yaani ni bonge la mtu lakini ni namba nane.

Inanifanya nisijue mume wangu anapenda miili gani? That is why I am not feeling like staying married to someone that am not sure anymore that he still loves me. Na wakati mwingine tukiwa kwenye gari wakipita wanawake wakubwa wenye namba nane huwa namcheki anavyowaangalia japo kwa wizi sana. Ingawa hata mimi huwa sometimes nawashangaa wanawake wenzangu. Sasa sijui nina wivu na sina Imani kwa sababu ameshani-cheat au ni normal"?

Naomba mnipe ukweli, je mume wako akitoka nje ya ndoa yenu na mwanamke ambae ni tofauti na wewe na baadae kukubali makosa na kurudi kwenye ndoa, je ataendelea kukupenda?

Asante".

Monday, 27 September 2010

Mkwe anataka nimuache mwanae ni Hanithi, lakini tumesha-do mara kibao na yuko sawa-Nifanyeje?

"Habari Aunt? Mimi ni mwanamke wa miaka 24,nina boyfriend wangu ambae tumedumu kwa miaka mitatu na plan yetu ni kufunga ndoa. Alipanga kuleta Posa baada ya Mwezi wa Ramadhan lakini cha ajabu mama yake aliwafuata mama zangu wakubwa na kuwaambia kuwa huyo boyfriend wangu si mwanaume, kwamba ni hanithi.

Pia mama yake alinifuata mimi na kunambia kuwa mwanae hana uwezo wa kiume. Lakini mimi na boyfriend wangu tayari tumekutana kimwili mara kadhaa na mimi namuona yuko sawa ila huwa anapiz nje kwa kuwa tulipanga tusizae nje ya ndoa.

Siku nyingine Mama yake kanambia kama siamini basi nijarbu kumtega kwa kumwambia kuwa anipe mimba, nilipomwambia boyfriend wangu anipe mimba alinijibu kuwa yeye yuko tayari. To be honest nampenda kutoka moyoni na yeye ananipenda pia.

Hivi sasa niko njia panda kwani pande zote mbili wanataka niachane nae lakini mimi sijaona tatizo au mapungufu ya mpenzi wangu yako wapi. Kwangu mimi ngumu kuachana nae kwa kuwa tunapendana na tuna plans nyingi tulizopanga na ni za muda mrefu.

Naomba watanzania wenzangu mnisaidie kwa hilo niko njia panda.

Asante."

Dinah anasema:Habari ni njema tu lovey, asante sana kwa ushirikiano. Pole kwa misukosuko ya soon to be mother in law, hapo ni sawa na kujitukana na kujidhalilisha mbele ya wazazi wenzie. Yeye amejuaje kama mwanae hawezi au hana uwezo wa kuzaa? Hata kama huo ni ukweli yeye anahusika vipi na maisha yenu ya ndani ninyi wawili kama wapenzi?

Anyway, Kama walivyo akina mama wengi wenye watoto wa kiume hupenda sana kupata mjukuu pale wanapotaka wao, wengine hutumia neno "sitaki kufa kabla sijaona mjukuu) hivyo hufanya kila jambo ili mtoto wa kiume kuzaa iwe kabla au baada ya ndoa.

Utagundua kuwa, kuna baadhi ya kina mama wakishajua mtoto wao wa kiume anauhusiano utasikia anataka kijana huyo afunge ndoa (hata kama hayuko tayari) na ikitokea akafunga ndoa kutokana na matakwa ya mama, soon baada ya ndoa mama mkwe ataanza kudai mjukuu, akipata wa kike, atataka wa kiume n.k yaani ni kama vile wana-control maisha ya watoto wao wa kiume.

Huyu mama anaposema mwanae ni Hanithi anamaanisha mwanae ni Tasa (hana uwezo wa kuzaa), labda kwa vile kila msichana alietoka nae kabla yako hakushika mimba kwa vile Mwanae alikuwa mwangalifu au hakutaka kuzaa kabla ya ndoa.

Vilevile inawezekana Mama mkwe huyo anadhani wewe ni Tasa kwani umekuwa na mwanae kwa muda mrefu bila kushika mimba (si unajua wazazi wetu wao walitumia Majira na hivyo waume zao walikuwa wanamwaga ndani tu hakuna cha nje wala Condoms)huenda anajiuliza "kulikoni hawa watu hawapeani mimba miaka yote hii" hivyo anataka ushike mimba kabla mwanae hajakuoa.

Sasa huyu mama anachojaribu kukifanya hapa ni kutaka wewe uwe forced na wazazi wako kushika mimba kabla ya ndoa ili ukifunga ndoa baada ya muda mfupi wewe na mumeo mmpatie mjukuu. Kumbuka amekuambia kama "huamini mwambie akupe mimba".

Alafu kwanini wazazi wako wakatae kupokea posa wakati sio wao wanaokwenda kuolewa na huyo Kijana, kwa kawaida binti ndio huwa na uamuzi huo. Kwamba mtu akija kuchumbia kwenu wazazi wanasema watamjibu baada ya muda fulani, then unaitwa alafu unaambia kinachoendelea na wewe kukubali au kukataa (kizamani).

Kisasa wengi tunakuwa tunawajua wachumba (vishwa Pete) kabla ya posa hivyo hata posa ikipelekwa wewe unakuwa wa kwanza kujua na huenda ukawaambia wazazi kuwa wazee wa kadhaa wa kadhaa watakuja kuposa n.k. hivyo wazazi kukataa Posa kwa sababu ya majungu ya mzazi mwenzao sio haki.

Nini cha kufanya:
Hebu kaa chini na mama yako mazazi na uwaambie ukweli kuwa Mchumba wako anauwezo wa kufanya mapenzi kwani tayari mmekwisha fanya mara kadhaa ndani ya miaka 3.

Mwambie "tunapendana na niko tayari kufunga nae ndoa. Sielewi mama mkwe(sijui unamuitaje) anataka nini kutoka kwetu kwani hivi majuzi (itaje siku) alinifuata na kuniambia nimtege mchumba wangu ili anipe mimba, inamaana huyu mama anadhani ukoo wetu ni Tasa?!!"

"Mimi sitaki kushika mimba kabla ya ndoa na ndio maana nimekuwa mwangalifu na kujikinga kwa miaka yote mitatu" (hii trick ya kujifanya victim huku unatoa CHOZI siku zote hufanya miujiza).

Enedelea "Mama naomba mkubali posa ya mpenzi wangu kwani ni mwanaume pekee ninae mpenda na tumepanga kufanya mambo mengi kwa ajili ya maisha yetu na familia zetu, nisingependa kumpoteza mwanaume anaenijali, mwenye nia njema nami na mwenye upendo wa dhati".

Mama yako anakupenda, hakika atakuelewa na atafikisha ujumbe kwa Baba. Ikiwa bado wanashupalia uachane nae basi uamuzi ni wako, Funga ndoa na Mchumba wako bila ya kuwaharifu wazazi wenu na baada ya ndoa ndio wapewe taarifa.

Fanyia kazi maelezo ya wachangiaji wengine pia,
Kila la kheri!

Wednesday, 22 September 2010

Mume wangu hawezi tena, natafuta mpenzi wa pembeni

"Dada dinah asante sana kwa blog yako hii ambayo tunaipenda sana. Mimi ni mdada wa miaka 35 na ninaishi nchi mojawapo ya Scandnavian, mume tuliyeoana hawezi tena kufanya mapenzi na amenipa uhuru wa kutafuta mwenzangu ambaye atanipa starehe ninayoitaka kimapenzi.

Tuna watoto na anatuhudumia wote kama kawaida. Tatizo ni hilo tu kuwa hata uboo wake hausimami tena na hata hajafikisha 60yrs. Nimekaa zaidi ya mwaka sijaonja hiyo kitu, naogopa UKIMWI kama nini.

Kama kuna mwanaume ambaye yuko single na atapenda tu enjoy na pengine future life na anaishi Scandinavian anitumie email yake kwa kutumia mtandao huu nitamtafuta. Only awe serious si vinginevo. Dada Dinah na wanablog naombeni ushauri wenu pia nisije ingia matatani au mkenge, nitathamini sana mchango wenu.
Mdau"

Dinah anasema: Mpendwa nashukuru sana kwa mail yako, nasikitika kusema sito-publish emails za Mkware yeyote atakae taka kuwa na wewe kwa vile tu mumeo hawezi tena kukuridhisha kingono. Nakushauri utafunte njia nyingine ya kuwapatia wanaume wa namna hiyo.

Nia na madhumuni ya kuweka mail yako hapa ni kwa vile hapo chini umeomba ushauri ili usije ingia mkenge na ni matumaini yangu waungwana watakushauri vema kuhusiana na suala zima unalikabiliana nalo kwenye ndoa yako.

Kuna wanaume wengi sana wanamatatizo ya kusimamisha na hivyo kushindwa kufanya mapenzi tena na wake zao, lakini kwa bahati nzuri kuna aina nyingi za dawa ambazo zinaweza kumsaidia mwanaume kufanya mapenzi kama kawaida.

Huyu mwanaume anahitaji support kubwa sana kutoka kwako wewe kama mkewe (kumbuka kiapo chenu cha ndoa unless otherwise wewe sio Mkristo), unapofunga ndoa na mtu mnahaidiana kuwa pamoja no matter what! magonjwa na afya ni tunakumbana navyo zaidi maishani mwetu....sasa mumeo hapa amekumbwa na tatizo la kiafya, ulitakiwa kuvumilia wakati unampa ushirikiano wa kwenda kumuona Daktari na hatimae kupata matibabu kwani yapo hasa kwa Ulaya ndio rahisi zaidi.

Tatizo kubwa ni kuwa wanaume wengi hawpaendi kuliweka wazi hili kwa Daktari kwa vile wanadhani ni kujidharaulisha mbele ya mwanaume mwenzio, kitu pekee kinachomfanya mwanaume ajiamini kuwa yeye ni kidume ni uwezo wa kufanya mapenzi. Sasa ikiwa kuna tatizo litakalomfanya ashindwe kufanya hivyo hakika hujiona kuwa sio mwanaume tena au ni mwanaume lakini hajakamilika.

Huenda hisia hizi za kutokujiamini tena ndizo zilizopelekea yeye kuamua kukupa uhuru wa kutoka nje ya ndoa yenu ili uridhishwe kingono, kama mwanamke mwenye kujali, mwenye Imani na mwaminifu ulitakiwa kumshawishi mumeo kufanya mambo mengine yahusuyo ngono bila yeye kuku-penetrate.

Kuna njia nyingi tu za kufanya ngono bila yeye mwanaume kukuingili na bado ukaridhika, yeye akawa anaridhika Kisaikolojia zaidi kwa vile wewe unaridhika na hivyo wote wawili kuridhishana kwa mtindo huo. Baada ya kumuona Daktari nakumpatia matibabu (dawa za kusaidia uume kusimama) mumeo then ataweza kukuingilia kama kawaida.

Mimi kama Dinah sipendezwi na watu wanaotoka nje ya ndoa/mahusiano, ikiwa tatizo ni kubwa sana na huna jinsi siku zote nashauri watu waachane na wahusika kabla ya kuanzisha uhusiano mwingine ili wawe huru zaidi na kuwapa nafasi Ex zao kusonga mbele na maisha yao bila kuumizwa kihisia.

Kwa case yako sidhani kama itakuwa vema wewe kuanzisha uhusiano mwingine wakati bado uko kwenye NDOA na baba wa watoto wako, vilevile ni mfano Mchafu kwa watoto hao vinginevyo umeamua kuwaambia ukweli kuwa baba yao hawezi kufanya mapenzi na wewe tena ndio maana unatoka na "Uncle" au umeamua kumtaliki baba yako kwasababu hizo!!

Jaribu kurudisha heshima ya ndoa, fanyia kazi tatizo analokabiliana nalo mumeo kwa kumpa ushirikiano kwa kubadilisha lishe na mtindo wa maisha, kuacha pombe kama ni mnywaji sana, kuanza kufanya mazoezi na kumtembelea Daktari kwa msaada wa kitibabu zaidi.

Samahani kama nitakuwa nimekukwaza, lakini kama nilivyojieleza hapo juu, nia na madhumuni ya mimi kuanzisha Blog hii ni kudumisha mahusiano ya kimapenzi na ndoa, sio kuharibu.

Wachangiaji wengine wataendelea......
Kila la kheri!

Friday, 17 September 2010

Shukrani kwa Maoni, ushauri na Mawazo yenu, sasa nimejitambua!

"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipo mshukuru muongozaji wa blog hiimy sister DINAH, shukrani zangu pia ziwaendee wale wote ambaowalisoma, au kuchangia katika ujumbe wangu ulio rushwa katika blog hii pendwa tarehe 18/08/2010 (Bofya hapa).

Kwa heshima na taadhima nawashukuru sana tena sana, sababu amini msiamini mmenionesha mwanga. Wapi nielekee. Nakubali kusema kuwa nilipoteza muelekeo ila kwa mchango na mawazo yenu na ushauri wenu kupitia hapa nimefanikiwa kufanyia kazi yote kutoka kwa kila mdau.

Kulinganana majibu hayo sasa nimejitambua, nasema hivyo kwasababu nilijaribu kumuomba tukae chini nijue kipi kinamsumbua akashindwa kutokea mahali ambapo tuliekubaliana zaidi ya mara mbili that means kweli hana mapenzi ya dhati kwangu.

Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na masomo yangu ya Ualimu, kwa wale ambao walishindwa kufahamu kama ninasoma ama la. Mimi ni mwanachuo wa Diploma ya Ualimu mwaka wa pili sasa.

Dada dinah pamoja na wale wenye mapenzi ya dhati na nia njema ktk blog hii Mungu awabariki sana."

Thursday, 16 September 2010

Nimegundua mume wangu kampa mimba mwanamke wa nje-Ushauri

"Habari dada Dinah, mimi ni moja ya wadau wa blog yako. Nieolewa na ni mama wa mtoto mmoja ana miaka 3+ na ninakaribia kupata baby no.2 panapo majaaliwa mwishoni mwa mwaka huu.

Mwenzenu nina matatizo ambayo naomba wadau wanisaidie kunipa ushauri nini cha kufanya maana nimejaribu kufikiria sioni njia ya kutatua matatizo yangu. Mimi na Mume wangu tangu tumejuana tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo, lakini cha kushangaza hivi karibuni nilimuona kabadilika sana kiasi kilichonifanya nianze kuchunguza kulikoni?

Mbona mambo hayaendi sawa kama zamani! baada ya kuanza uchunguzi niligundua mume wangu kuna watu anawasiliana nao sana bila kutaka mimi nifahamu wanawasiliana kwa ajili ya issue zipi. Hapo nilijawa na wasiwasi zaidi nikaamua kutega baadhi ya number kwenye simu ili msg zikitumwa asizione kwenye inbox ila ziingie kwenye folder tofauti.

Nilipokuja kufungua lile folder nilikuta msg nyingi za mdada mmoja ambaye ni mpenzi wake na alikuwa akilalamika kuwa hamtumii msg wala kumpigia simu nakuwa amepunguza kumjali na yeye ni mjamzito na ameamua kuitoa hiyo mimba kisa hamjali sababu hampigii simu.

Nilipoona hizo msg nilitamani kufa hapohapo! maana sikutegemea kama mume wangu angekuwa na mwanamke nje ya ndoa yetu ambayo bado changa. Nikaamua kumuuliza mume wangu akasema hana mwanamke nje na hategemei kuwa na mwanamke nje ya ndoa.

Nami kwa kuonyesha kuwa hamna msg niliyoona nilikaa kimya kwa muda wa wiki mbili bila kumuuliza kitu. Baadae nikakuta msg nyingine ya huyo mwanamke akimuuliza mume wangu anaamuaje kuhusu ujauzito alionao?

Nikaamua kuhamishia ile msg kwenye inbox na kumuomba mume wangu aisome ile msg na anieleze kuna kitu gani kinaendelea. Chakushangaza mume wangu akasema haijui hiyo msg, basi nikamwambia tupige hiyo simu tukiwa wote nae akakubali yule dada alipopokea akaanza na maneno yanaonyesha wao ni wapenzi wa siku nyingi.

Mumue wangu akajidai kumfokea yule dada lakini haikuleta maana yeyote, nikaamua kuchukua ile namba na nikaipigia mimi mwenyewe nikimuomba tukutane kwani nina shida nae, yule dada akakubali lakini hakutokea na simu yangu hapokei tena.

Huku mume wangu hajawahi kulala nje ya nyumba yetu hata siku moja na siku zote yeye huwahi kurudi kutoka kazini kabla yangu maana mimi huwa narudi kuanzia saa kumi na moja na kuendelea na yeye hurudi kuanzia saa nane mchana.

Hapo naomba dada Dinah na wachangiaji wengine mnisaidie kimawazo, nifanyeje maana nimepunguza sana upendo kwake kila nikimuona mume wangu namuona kama ni muuaji maana kama ameweza kufanya mapenzi nje ya ndoa tena bila ya kutumia kinga si anataka kuiteketeza familia yetu?!!

Asanteni"

Wednesday, 8 September 2010

Wenzangu mnafanya nini mpaka nakubaliana kufunga ndoa na wapenzi wenu?

"Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32, ninafanya kazi hapa Dar es Salaam. sasa tatizo lililonileta hapa leo ni kwamba ningependa sana kuolewa na ninaomba Mungu anipe Mume mwema. Nimekuwa na mahusiano mazuri tu na wanaume lakini inapofikia wakati ukigusia masuala ya ndoa inakuwa sumu.Yaani tunakorofishana mpaka kufikia hatua ya kutishia kuwachana.

Kwa sasa nina mwanaume na tumekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja sasa, lakini nikimueleza masuala ya ndoa ndio inakuwa ugomvi na anaona kama vile namghasi nainafikia hatua tunakorofishana kabisa.

Zake ni kunipiga danadana tu nakuniambia nimpe muda, mimi umri unaenda si unajua tena mwanamke? Yaani hanishirikishi kwenye mipango yake hivyo nashindwa kuelewa. Nikiuliza Muda upi unahitaji? na kwanini tusishirikiane kimawazo?

Nafikiria kuachana nae lakini najiuliza nitaachana na wangapi? Yaani ninapata wakati mgumu sana na ninashindwa kuelewa, je inakuaje mwanamke anaweza kukubaliana na mwenzie vizuri hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa?

Au labda mimi napata wanaume ambao hawako tayari kuwa ndani ya ndoa? Naomba mnishauri nifanye nini ili niweze kujua kama ana nia ya kweli au ndio nimechemsha tena!"

Dinah anasema: Niliwahikuzungumzia issue hii kitambo kidogo, kuna dadaz kama wawili wamefanikiwa kufunga ndoa baada ya kusoma Makala yangu hii, huwezi jua huenda na wewe ikafanikiwa, kwa kuanzia wakatiunasubiri ushauri kutoka kwa wengine hebu Bofya hapa na hapa alafu malizia hapa.

Kila la kheri!

Friday, 3 September 2010

Nilichanika hadi kwenye O wakati wa kujifungua, sasa nahisi hewa inapita ukeni-Ushauri

"Mimi naitwa Anita na ni mfuatiliaji wa Blog yako tangu mwezi wa tatu. Nafurahia unavyowasaidia watu namatatizo kupitia Blog hii. Mimi nimejifungua mtoto wa kiume Mwezi wa Tano mwishoni .

Wakati mtoto anatoka alinichana vibaya kiasi kwamba mchano ulipitiliza hati kwenye njia ya haja kubwa, nadhani walinishina vibaya kwani nahisi huku chini kuko wazi sana maana natoa hewa sana sehemu yangu ya Uke.

Nimeenda Hospitali mara tatu ila bado wananiambia kuwa kupo sawa lakini mie nahisi kuko wazi hivyo naogopa hata kufanya mapenzi na baba mtoto kwavile nahisi kama vile atapwaya. Naomba wadawau wenye uzoefu mnisaidie kwa ushauri na kunielekeza nini chakufanya au kutumia ili nihisi huku chini kunabana kama zamani, maana baba mtoto alikuwa anapenda jinsi ilivyokuwa tight?

Vilevile kama kuna mtu anamjua Kungwi mzuri atakaeweza kunifunda kwenye masuala ya ngono anielekeze kwani sio mzuri sana kwenye hiyo department.

Asanteni"