Friday, 28 May 2010

Tutadumu au ananipotezea muda tu-Ushauri!

"Habari dada Dinah! Pole na majukumu.
Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri kwenye blog yako. Mimi ni mwanamke wa miaka 25, nina mtoto wa miaka 3.

Kwa sababu zisizozuilika nimeachana na baba wa mtoto karibu mwaka na nusu sasa. Baada ya hapo sikujihusisha na mwanaume yeyote yule hadi mwanzoni wa mwaka huu nilipotokea kupendana na kaka mmoja.


Penzi letu limekua kwa kasi sana lakini from the beggining nilishamwambia situation niliyokua nayo kabla sijakutana na yeye. Mwanzo ilimsumbua kwasababu hakutegemea,but after few days aliniita tukazungumza na tukakubaliana kuendeleza mapenzi yetu kwa kuwa my baby sio kipingamizi.


Mtoto wangu namhudumia mwenyewe kila kitu after all mimi nakaa kwa wazazi wangu ila yeye anakaa peke yake. Kinachonipa shida ni hiki MOJA -nakosa amani pale ninapoona anawachangamkia watoto wa majirani lakini wangu hamchangamkii kivile. Huwa ananiambia niende nae kwake kwavile weekends nashinda kwake kwakua wote hatuendi kazini.

Dinah anasema: Natambua kuwa ungependa mpenzi wako amchukulie mwanao kama mtoto wake lakini hiyo itakuwangumu kidogo hasa kama yeye mwenyewe hana mtoto, kwamba hana uzoefu wa kuwa baba.

Nadhani ni mapema sana kwa mpenzi wako kuanza kujenga mazoea na mtoto wako nahivyo kupelekea mtoto huko kumuita yeye baba, vilevile huenda anaogopa kuzoeana na mtoto huyo kwa vile hana uhakika na uhusiano wenu kwa maana kuwa ikitokea anamzoea mwanao kama mwanae na siku moja mkaachana ni wazi ataumia sana na pia mtoto ataumia kwa vile hawatopata nafasi ya kuonana tena.

Sidhani kama anachuki na mtoto wako ila inaweza kabisa inampunguzia ile hali ya kujiamini kutokana na ukweli kuwa kunamtu mwingine alifanya mapenzi na wewe na matunda ya mapenzi yenu ni huyo mtoto. ngumu sana kwa mtu yeyote kumchangamkia mtoto ambae sio wake.

Kumbuka kuwa mmekuwa pamoja miezi michache tu, na katika kipindi hicho kifupi sidhani kama ni haki kwakwe mpenzi wako au mwanao kuzoeana. Unatakiwa kuheshimu hisia zake na wewe kupunguza hali ya kujishitukia.

Yeye kuchangamkia watoto wengine zaidi kuliko mwanao haina maana kuwa hampenzi mtoto wako, kumbuka hao watoto wa jilani hawahusiani na wewe, hawakuzaliwa na wewe, hivyo anavyowachangamkia haina uhusiano wowote na mwanao, anawachangamakia na kuwapenda kama watoto.

Kama ambavyo sote tunapenda watoto wote bila kujali wazazi wao ni akina nani, lakini linapokuja suala la mtoto wa Ex wa mpenzi wako kidogo inakuwa tofauti, na ukikuta mtu anaonyesha kumpenda mtoto/watoto wako ndani ya kipindi kifupi tangu mkutane ujue kuna kitu nahitaji kutoka kwako na njia pekee ni kujipendekeza kwa watoto/mtoto wako.


MBILI -Siku zote za weekend ninapopika chakula nikiwa huko kwake, after eating he never says thank you au chakula kizuri/kibaya yaani ha-comment chochote. Sometimes nikitoka kazini nikimnunulia kitu cha kuvaa au hata take away sababu yeye hapiki na anarudi usiku he never says thank you.

Dinah anasema: Hii ni tabia ya mtu ambayo imejengeka kutokana na mazoea (inategemeana na mazingira aliyokulia) au kasumba iliyojengeka kutokana na mfumo dume, kwamba chochote kinachofanywa na mwanamke ni haki yake au ni wajibu wa mwanamke nahivyo hakuna sababu ya kushukuru.

Kuonyesha shukurani ni kitu muhimu sana kwenye uhusiano wa kimapenzi, na asante hiyo sio kwenye chakula, zawadi, ngono tu bali kwa kila jambo unalofanyiwa na mwenzio, hata ile hali ya yeye mpenzi kukujali unatakiwa kumshukuru, lakini kwa baadhi ya wanaume wetu wa Kitanzania inakuwa ngumu kwa vile hawajui.

Wakati wanakua baba zao (wazee wa Mfumo Dume) hawakuonyesha shukrani wala heshima kwa mama zao na hivyo wao kama watoto wa kiume wakadhani kuwa ni kawaida. Hivyo wajibu wako hapa ni kuweka wazi suala hili ili ajue kuwa unayomfanyia sio wajibu wako na wala sio haki yake bali ni mapenzi na hali ya kumjali, ni vema akaonyesha shukrani, akakuambia kama chakula kizuri au kibaya ili ujue wapi pa kuboresha au nini cha kuongeza, nini ununue na nini ukiepuke n.k.

TATU - Nikivaa nguo nzuri au nikipendeza hanisifii, yaani hana ile kusifia chochote changu.
Sasa napata mashaka why he is like this?au mimi ndio na-complicate mambo? kwangu mimi nahisi kuwa tabia yake sio normal.

Dinah anasema: Tabia yake ni ya kawaida sana kwa wanaume wengi tu hapa Duniani, kama nilivyosemahapo juu tabia hujengwa na mazoea sasa kama mazingira aliyokulia yalikuwa ya mfumo dume kwamba mwanamke haeshimiwi wala hathaminiwi inakuwa ngumu sana kwake kujua nini aseme kuhusu mwanamke, anachojua yeye ni kuwa mwanamke yuko pale kwa ajili yake, ampikie, amsafishie nyumba, amjali na kumridhisha kingono.

Zungumza nae na kuweka wazi hisia zako, alafu siku hadi siku anza kumsifia yeye na siku akivaa ovyo mwambie ukweli kuwa hajapendeza na bora abadilishe avae hivi au vile....hii itamsaidia kuelewa umuhimu wa kukusifia unapofanya jambo zuri au unapopendeza.

NNE, according to him anasema ananipenda, kuhusu future yetu pamoja hatujawahi zungumzia in deep but tuliongea one day. Kutokana na kuachana na baba wa mtoto wangu, naogopa sana kuwa na mwanaume lakini ndio hivyo mtu huwezi kuishi mwenyewe milele na ninampenda sana mpenzi wangu huyu wa sasa.

Lakini tatizo ndio hivyo simuelewi au niseme ni mimi ndio ninacomplicate things na kukosa amani.
Asante na naombeni ushauri nifanye nini, tatizo, ni langu au mwenzangu? Je kuna uhakika wa maisha ya mbele kama wapenzi?."

Dinah anasema: Asante sana kwa ushirikiano na uvumilivu wako, nimejaribu kutoa maelezo kwa kila swali hapo juu na hapa nitakupa maelezo kwa ujumla. Melezo yako kwenye kipendele cha nne yameonyesha kuwa wewe ni mdada mwenye uwezo mzuri wa kuchanganua mambo, umegundua kuwa tatizo ni wewe na sio huyo mpenzi wako japokuwa na yeye anavijitabia fulani ambavyo vinaongeza uzito kwenye tatizo ulilonalo wewe kama wewe.

Baada ya kuumizwa na hatimae kuachana na baba mtoto wako, umepoteza ile hali ya kujiamini na pia umekuwa ukifanya vitu kwa tahadhari kubwa (unajishitukia) kwa vile husingependa kilichotpokea kitokee. Hali hii inakufanya utamani au utake uhusiano ambao ni secure na commited au hata ndoa. Ni hali ya kawaida kwa mtu yeyote alietendwa na kuumia sana.....sasa hili ndio tatizo lako.

Uhakika wa maisha ya mbele hakuna mtu anaujua hata mtunzi wa kalenda hajui lakini siku zote sisi kama wanadamu huwa tunajitahidi kumuomba Mungu atupe uzima na aongeze baraka ili mahusiano yetu yasimame imara. Pamoja na kumtegemea Mungu pia sisi wenyewe kama pea (wapenzi) tunatakiwa kufanyia kazi ili mahusiano hayo yaendelee kuwa mazuri na yadumu kw amuda mrefu.

Kwa maana ninyingene najaribu kusema kuwa, kama unataka uhusiano wako uendelee na uwe na afya njema ni vema ukajitahidi kugundua tofauti za hisia za upendo kwa mwanao ambae ni sehemu ya mwili wako na mapenzi kwa mwanaume ambae sio sehemu ya mwili wako lakini anaumuhimu kwenye maisha yako.

Jifunze namna ya kuzungumza na mpenzi wako, namna ya kuwakilisha hoja zako, kujua mipaka kati ya mtoto wako na mpenzi wakoa ambae sio baba wa mtoto huyo (epuka kumzungumzia mtoto unapokuwa na mpenzi wako) ukiwa unamzungumzia mtoto kwa mpenzi wako itakuwa kama vile unamzungumzia Ex wako. Ni ngumu lakini jitahidi.

Umekuwa na mpenzi huyu mpya kwa takribani miezi mitano, mimi nakushauri upunguze speed kidogo ili u-enjoy maisha yako kama mama lakini pia ni binti mdogo wa miaka 25, kwani inaonyesha unaharaka sana hali inayoweza kuharibu uhusiano wenu usipokuwa mwangalifu kwani jamaa anaweza kuingia mitini kwa vile unampeleka-peleka, kumbuka wanaume wanapenda amani, hawapendi kulazimishwa wala kusukumwa-sukumwa.

Pamoja na kuwa umemhakikishia kuwa Ex hayupo tena kwenye maisha yako lakiniukweli utabai kuwa ni baba wa mtoto wako na mtakuwa na uhusiano fulani kwa ajili ya mtoto wenu kwani huwezi ukamkataza mtoto kuwasiliana na baba yake au baba yake kuwasiliana na mtoto wake.

Sasa wewe kuwa na mtoto ni headache kwake tayari kwani anaweza kuhofia mambo mengi kama vile....itakuwa vipi kama siku moja ikitokea jamaa anataka kurudiana na wewe kwa kisingizio cha mtoto wenu? huenda anafikiri kuwa itakuwa rahisi kurudiana kwa vile tayari mnamtoto......umewahi kufikiria hili, kujiweka kwenye nafasi yake ili ujue ni vipi anajisikia?!!

Mpaka sasa anajua kuwa wewe unamtoto na amekwisha muona au huwa anamuona mara kwa mara, wakati unajaribu kuhimarisha uhuaino wako vema kama utapunguza mawasiliano kati ya mtoto nampenzi wako, unapokwenda kwake kwa ajili ya weekend usiende na mtoto, nenda peke yako ili mtumie muda wenu kama wapenzi wakati mtoto atakuwa na bibi yake.

Acha kucheza kamchezo ka "a little family" kwa maana kuwa mnapokuwa pamoja ninyi watatu basi wewe unapata amani kuwa ninyi ni familia, ni mapema sana kwa hilo...mpe muda Mpenzi wako.

Ni rahisi kwa watu kusema ukipenda Boga penda na Ua lake, lakini wanasahau kuwa upendo kati ya mtoto amabe sio wako na mpenzi unatofautiana, Upendo unahitaji muda, upendo huwa haulazimishwi, upendo ni hisia na kama hisia hizo hazipo hakutakuwa na upendo....suala muhimu ni kwa yeye kumchukulia mtoto wako kama watoto wengine tu hapo jirani na kuheshimu nafasi ya mtoto kwako kama mama yake.

Natumaini umenielewa,kama kuna mahali nimekuchanganya tafadhali usisite kuniandikia nami nitafafanua. Jaribu kutembelea Makala za nyuma na baadhi ya maswali ili uweze kujifunza zaidi namna ya kuishi kwenye uhusiano na kuufanya uhusiano uwe na maendeleo na hatimae kuwa wa kudumu.

Kila la kheri!

Wednesday, 26 May 2010

Nataka Muziki Munene(uume Mkubwa), nifanyeje?

"Napenda kukupongeza kwa dhati kabisa juu ya kazi yako unayoifanya ya kuelimisha jamii hususani katika hili suala zima la kimapenzi ambalo ndilo linalochukua nafasi kubwa katika jamii zetu hapa duniani.

Mimi tatizo langu ni kukuomba dada yangu unisaidie kama ninaweza kupata dawa ya kuongeza uume wangu, maana nina inchi 5.8 sasa naona ni ndogo sana. Maana hata nikijilinganisha na wenzangu wakati wa kuoga naona ya kwangu ni ndogo kiasi kwamba naoana hata aibu wakati mwingine.

Na nimekuwa nikifanya mapenzi na wasichana mbali mbali na hakukuwa na tatizo lolote, mpaka siku moja nilipokutana na dada mmoja ambaye aliniambia "mbona maumbile yako ni madogo"? mimi nikamjibu ni kawaida kwani cha muhimu ni kusimamisha na kuweza kufanya kazi sawa sawa.


Lakini nikabaki na kujiuliza sasa huyu inawezekana amezowea zile kubwa. Sasa kwa hii tabia ya hawa dada zetu kupenda uume kubwa ndio imesababisha vijana wengi kutafuta dawa za kuongeza maumbile.

Ombi langu kwako na wadau wote wa hii blog ni kuomba msaada wa kufahamishwa sehemu au mtu ambaye anauza dawa za kuongeza uume na pia nitazipataje kwa kuwa ninazihitaji sana hasa ukitilia m aanani wakati wa kuoa sasa unafika na hivyo nisije jikuta nikaumbuka humo ndani ya nyumba.

Napenda niwe na ile kubwa ya wastani na nene ambayo itanisaidia kufanya tendo langu kwa kujiamini zaidi. Maana sasa hivi naogopa hata kutongoza demu kwa sababu ya hii kitu ndogo. Msaada tafadhali dada yangu. Natanguliza shukrani."

Dinah anasema: Nadhani wanaume wamekupa majibu yakinifu kabisa, mimi binafsi naamini kuwa mwanamke yeyote anaekuambia kuwa wewe una uume mdogo ni wazi kuwa yeye ndio mwenye uke mpana kuliko.

Uume wa wastani ambao kwa kwaida inasemekana ni Inchi 4.5-6.5 unauwezo kwa kumridhisha mwanamke yeyote bila matatizo yeyote unless otherwise amejaaliwa kiasi kwamba haridhiki unless mwanaume awe na uume kama mkono wake. Suala la udogo au ukubwa wa uume kusema ukweli huwa halitusumbui sana sisi wanawake bali wanaume wenyewe katika suala zima la kujiamini au kutaka kuwa kama Porn star artist.

Kama wewe ni mtazamaji wa picha za ngono ni wazi kuwa utatamani kuwa kama wale wanaume unaowaona ukiamini kuwa wanawake watafurahia kitu kubwa lakini ukweli ni kuwa sio wanawake wengi hasa wa kiafrika ambao wanapenda Miziki minene.

Wanawake wa Kimagharibi kutokanana mitindo ya maisha yao wengi inasemekana huwa na K kubwa na hivyo kushindwa kuridhika na uume wa kawaida (inchi 4.5-6.5 na hivyo kuhitaji Kubwa hali inayo sababisha waume/wapenzi wao kwenda kufanyiwa Upasuaji ili kuongeza ukubwa huo wa uume namatokeo yake wengi hupeteza hisia na hivyo kushindwa kufurahia tendo.

Uume wako wenye ukubwa wa Inchi 5.8 katika hali halisi unatosha kabisa kuridhisha mwanamke yeyote, as long as unauwezo wa kwenda mwendo mrefu, unajua kuutumia na vilevile mpenzi wako huyo anajua kujituma wakati wa tendo.

Unachotakiwa kufanya ni kuongeza bidii na utundu ili umuonyeshe huyo mwanamke alie jaaliwa uke mkubwa kuwa Inchi 5.8 ni zaidi ya Inchi 9 ni wanaume wachache sana wanafikia hiyo(na sidhani hata hiyo itamtosha....Lol)

Nasikitika kusema sina uhakika na dawa za kuongeza ukubwa wa uume.

Kila la kheri!

Saturday, 22 May 2010

Miaka 3....Happy B'day Dinahicous!


Dinahicious ni Blog ya kwanza inayozungumzia Ngono kwa undani na uwazi zaidi, imefanikiwa kwa kiasi kubwa, inajulikana zaidi kuliko miaka 3 iliyopita, inazungumziwa kwenye mitaa, sherehe na kwenye mikusanyiko mbalimbali.
Bila wewe Dinahicious isingefikia hapa, napenda utambue kuwa nathamini sana Ushirikiano wako kwa kutembelea, changia, kuuliza, kuizungumzia na kuiweka Blog hii kwenye Tovuti yako.
Katika kuadhimisha miaka 3, ningependa kukupa nafasi wewe mpenzi mtembeleaji, Msomaji na Mchangiaji (kwa kuuliza au kushauri) kutuambia umefaidika na nini hasa tangu tumeanza kukumbushana, fundishana, ambizana, shauriana, elekezana kuhusiana na masuala ya Kimapenzi, Ngono na Mahusiano?
Nakupenda sana!

Friday, 21 May 2010

Uchoyo/ubahili wake unanipa hofu kama tutafunga ndoa-Ushauri

"Mambo Dinah mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 27, ni mfuatiliaji mzuri wa Ushauri wako nina mpenzi yapata mwaka mmoja hivi sasa. Tumepanga tuje funga ndoa Mungu akijaalia.

Huyu mpenzi wangu sijui niseme ni mbahili, mchoyo au nimwitaje, maana kila wakati huwa analalamika hana hela hata tukitoka dinner anatanguliza kusema "yaani sasa hivi sina hela kabisa" hapo sijamuomba.

Kwa kawaida sina kawaida ya kumuomba hela yaani hata ninapokuwa nimepungukiwa au ninashida huwa namwambia anikopeshe halafu nitamrudishia baada ya muda Fulani lakini bado anasema hana hela.

Wote ni mfanyakazi na yeye anakipato kikubwa zaidi yangu. Naomba ushauri nifanye nini? nimsaidie vipi maana baadae asijekuwa mbahili hata kwa watoto wake."

Dinah anasema:Asante sana kwa ushirikiano na hongera kwa kuwa mmoja kati ya wanawake wachache wanaojitahidi kujitegemea kiuchumi. Ikiwa wewe una miaka 27, napata hisia kuwa mpenzi wako atakuwa kwenye miaka ya thelathini na kitu.


Kwa mwanaume yeyote kipindi hiki ndio pekee ambacho hudhani ni muhimu kujiweka sawa kimaisha kwa maana ya kufunga ndoa, kuwa na mahali pake pa kuishi, kuanzisha miradi ya kujiendeleza n.k. hilo moja.


Pili, inawezekana anamajukumu mengine kama ilivyo kwa sisi waafrika wote, kama wewe ni mkubwa kwenye familia yenu na umefanikiwa kupata kazi basi unachukua majukumu fulani kutoka kwa familia yako, inaweza kuwajengea wazazi, kusomesha wadogo zako n.k


Sababu ya tatu ninayoweza kuifikiria kwa haraka haraka ni Muda/wakati. Katika kipindi cha mwaka mmoja ni mapema sana kwake yeye mpenzi wako kuanza kukushirikisha kwenye kila jambo alifanyalo sio kwamba hakupendi bali hana uhakika kama yuko tayari kuweka wazi mambo yake binafsi labda kwa kuhofia kuwa utamkimbia kutokana na uwingi wa majukumu yake au utaendelea kuwa nae kwa kutegemea kupata kitu kwake na sio mapenzi ya dhati.

Pamoja na kugusia yote hayo hapo juu, inawezekana kabisa kuwa mpenzi wako ni mbahili, na hii inategemea na asili yake au jinsi alivyolelewa.


Nini cha kufanya: Kabla hatujampa hukumu ni vema tukajua ukweli wa mambo, je ni mbahili kweli? kuna jambo anafanya lakini anadhani ni mapema sana kukushirikisha? au kuna majukumu mengine ya kifamilia yanam-bana?


Ndani ya mwaka mmoja lazima utakuwa unajua kama jamaa anandugu ambao wanamtegemea ama la! Inawezekana kabisa ulidhani kuwa ni kitu ambacho hakikuhusu, lakini ni muhimu sana kujua watu wa karibu wa Mpenzi wako, sio lazima urafikiane nao au kuwafahamu kwa karibu bali kujua tu kuwa anawadogoz ake 3, anaishi na wazazi wake, kuna binamu n.k.


Ingekuwa mnaishi pamoja ingekuwa rahisi zaidi kwani mngegawana majukumu na kwa vile yeye anakipato kikubwa, angechukua jukumu la kulipia Nyumba na Bill ya umeme, wewe ukawa unashughulikia Bill ya maji, chakula na mahitaji mengine madogo madogo ya nyumbani na senti zinazobaki kwa pande zote mbili zinahifadhiwa kama akiba au inaenda kufanya jambo la maendeleo...kama mnajenga n.k.


Lakini kwa vile kila mtu anaishi kwake basi njia pekee ya kujua ukweli ni kutafuta muda mzuri wa kuzungumza nae kuhusiana na maisha yenu ya baadae kama wenza, tena ni rahisi zaidi kwa vile tayari mmepanga kufunga ndoa Mungu akijaalia. Wee anzisha maongezi haya kwa kuonyesha kuwa wewe ni "mama maendeleo" na hakikisha kila unalosema linauwingi kwa maana ya wewe na yeye.

Unaweza kuwakilisha hoja yako kwa utani Mf: mnatoka kwa ajili ya mlo wa jioni alafu yeye anasema sina hela.....cheka kisha muulize..."hivi kwanini wewe kila siku huna hela wakati wote tunafanya kazi? anaweza kukupa jibu la moja kwa moja kama kweli anamajukumu mengine au anaweza kusema "siku ikifika utajua kwanini huwa sina hela".....asipokupa jibu usijali kwani litabakia kichwani na atalifikiria jiono hiyo na usiku mzima na kukupa jibu atakapo kuwa tayari.

Au mpe kitu cheupe moja kwa moja....kwa upole na upendo lakini kwa kumaanisha, mwambie yote yalioujaza moyo wako, hali ya kujitegemea kiuchumi (kama ulivyosema hapa), mipango ya baadae, hofu yako juu ya maisha yenu na watoto hapo baadae n.k.

Maongezi hayo yatasaidia mpenzi wako kufunguka na kukuambia ukweli kama anasomesha ndugu zake, au anatunza hela kwa ajili ya kufunga ndoa, anajenga n.k. sasa ukipata ukweli kama ni mbahili au anamajukumu mengine tafadhali usisite kurudi tena hapa ili tujue namna gani tunaweza kusaidia kutokana na tatizo husika.

Kila la kheri!

Thursday, 20 May 2010

Wifi na Shemeji walinishawishi nimuache mdogo wao, sasa najuta!-Ushauri

"Pole dada Dinah kwa kazi ngumu, mimi ni mwanablog wako wa muda mrefu. Nimesoma kisa cha dada Rhoda wa Mwanza aliye sex na shemeji yake na mimi imenitia moyo kusema ya kwangu ambayo na dhani ya kwake ni trailer sinema kamili iko kwangu.

Naomba nisitaje jina langu ila mimi ni mwanamke wa Kichaga nilikuwa na boyfriend wangu miaka ya nyuma ambaye wakati nakutana naye alikuwa anasoma Chuo kimoja hapa Dsm na mimi nilikuwa nasoma Chuo cha mambo ya Hoteli.

Tulikuwa tunapendana sana na kwa kweli yeye ndio alinitoa usichana wangu na kuniingiza katika ulimwengu wa mapenzi. Jamaa alikuwa ni mtu wa mazoezi so alikuwa fit everywhere kitandani. Mammbo yalienda vizuri mpaka kufikia maamuzi yakufungandoa atakapo maliza chuo na kupata kazi.

Kimsingi jamaa alikuwa ananitomba vizuri na alikuwa fit na mpaka niandikapo mail hii sijawahi kutombwa hivyo. Wakati jamaa anasoma alikuwa akiishi kwa kaka (baba zao ni mtu na mdogo wake)yake ambaye alikuwa ameoa na ni mfanyakazi Serikalini.

Lakini kwa bahati mbaya mke wa kaka yake alifariki wakati ambao mchumba wangu alikuwa amemaliza Chuo anatafuta kazi. Namwita mchumba kwa sababu process zote za kutambulishana tulikuwa tumekwisha zifanya.

Baada ya kaka mtu kufiwa na mke wake Wifi ambaye ni tumbo moja na kaka yake mchumba wangu akaanza kunishawishi nimwache mchumba wangu ambaye ni kama mdogo wake ili niolewe na kaka yake ambaye amefiwa na mke.

Kakamtu na dada yake (wifi na shemeji yangu) wakawa wanafanya kampeni kubwa ili mimi nimwache mchumba wangu ambaye ni mdogo wao kwa baba mdogo ili niolewe na kaka yake. Ikafikia mpaka kunidanganya kwamba mama yake mchumba wangu ambaye ni mama yao mdogo ni mchawi.

Nikaanza visa kwa mchumba wangu na baadae nikiamwacha ingawa alikuwa aninipenda sana na yeye alifikiria nimemwacha kwa sababu hana kazi kwani wakati huo alikuwa bado hajapata ajira. Nikaanza mapenzi ya siri na kaka yake bila yeye kujua na mchumba wangu huyo baada ya kunishawishi kwa muda mrefu turudiane akakata tamaa na kutafuta mchumba mwingine na alipopata kazi wakaoana.

Kwa bahati nzuri alihamishiwa Arusha kikazi ndipo mimi na kaka yake tukapata wasaa mzuri wa kuwa huru hapa Dsm na kuatangaza uchumba wetu. Kaka mtu alitumia nguvu nyingi sana kuhalalisha uchumba wetu ingawaje alipata vikwazo vingi sana kutoka kwa ndugu na jamaa waliokuwa wanafahamu kwamba mimi nilikuwa mchumba wa mdogo wake.

Kwa sababu ni mtu mzima (amenizidi miaka 12 kiumri) na ni mtu mwenye uwezo nyumba na magari hakupata vipingamizi vyovyote tukafanya bidii tukafunga ndoa.

Tatizo.
1.
Baada ya ndoa nimekuja kugundua mume wangu huyu hana nguvu za kiume na hii inatokana na uzito mwingi na kunywa pombe kupita kiasi. Mwanzoni wakati tunaoana nilidhania ni tatizo dogo kwa sababu tulikuwa hatuishi wote ila baada ya kunioa mwanume anakaa hata mwezi mboo haisimami.

Nimejaribu kuvumilia nimechoka, nimetamani kwenda nje ya ndoa lakini naogopa kwani mwanaume huyu anawivu na ananichunga sana. Nikikumbuka mchumba wangu wa mwanzo ambaye ni mdogo wake alivyokuwa aninitomba naatamani nimwache nimrudie ila jamaa hataki hata kuniona.

Nimejaribu kumtega hategeki na anaiambia hawezi kuingia kwenye shimo(kaburi) ambalo alishaingia akaokoka au ananiambia hawezi kuingia kwenye shimo moja na kaka yake. Mume wangu ananipa kila kitu nyumbani, chakula, magari, biashara ila mwanamke sitombwi nakaa hata miezi mitatu mume hajui kama nina kuma au sina.

Naombeni ushauri nifanyeje jamani kuachana tunashindwa kwa sababu ya nguvu tuliyo tumiaa kuahalalisha uchumba wetu na ndoa baada ya mimi kumwacha mchumba wangu ambaye alikuwa mdogo mtu.

Dinah anasema: Sahau Ex wako ambae ni mdogo Mume kwani umechelewa hivi sasa na yeye tayari anamke wake hivyo muache aishi kwa amani na hakikisha unadumisha heshima na thamani ya ndoa kw akutoingilia ndoa hiyo ili uwe mfano bora kwa vijana wengi ambao hawajafunga ndoa.

Huyu ni mume wako sasa, iwe uwezo wake wa kungonoka na mdogo au haupo kabisa haibadili ukweli kuwa ni mume wako ambae ulikula kiapo Mbele ya Mungu kuwa utakuwa muaminifu kwake, utaishi nae kwa uzima na maradhi.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa Pombe ni sababu kuu ya yeye kushindwa kukuridhisha kimapenzi, kwani pombe inapunguza nguvu za kiume kwa kasi ya ajabu hasa kwa wanaume wenye umri zaidi ya miaka 35.

Sasa wewe kama mke wake ni jukumu lako kuhakikisha jamaa aishi maisha yenye afya ili kuepuka matatizo mengine ya kiafya sio ngono pekee. Zungumza nae kuhusiana na tatizo lake la ulevi, nakuhakikishia akipunguza kunywa pombe uwezo wake wa kungonoka utakuwa mzuri tu.

Vilevile wewe unatakiwa kutuliza mawazo na akili yako juu ya huyo Mumeo na kuwa mbunifu zaidi na kumfundisha mbinu nyingine za kukuridhisha kingono na hivyo kuwa na uhusiano bora wa kingono ambao utawasogeza karibu zaidi na hivyo kuibua hisia za kimapenzi keati yenu...kumbuka ni Mumeo huyo.

2.Watoto aliozaa na mke wake wa kwanza ambaye ni marehemu wameisha kuwa wakubwa na hawanipendi na huwa wananiita Malaya kwa kuchanganya baba yao na baba yao mdogo hivyo ni ugomvi kila siku kwani walipokuwa wadogo walikuwa wanajua mimi ni mchumba wa uncle wao. Nikimwambia baba yao watoto hawaniheshimu anashindwa kuwakemea kwa sababu anawapenda sana.

Dinah anasema: Sio watoto tu wanaokuvunjia heshima nina hakika sehemu kubwa ya familia ya huyo Mumeo wanahisia mbaya sana juu ya uamuzi uliochukua. Huna haja ya kushitaki watoto kwa baba yao kwani wewe mwenyewe ulishindwa kujiheshimu siku ile ulipokubali kuwa mpenzi wa Shemeji yako.

Watoto hao sio tu anawapenda pia kuna huruma ndani yake, watoto kuendesha maisha bila mama yao hapa duniani ni ngumu tayari, sasa kwanini makosa yako mwenyewe yawaongozee ugumu wa maisha?

Jitahidi kuwa mvumilivu na siku ukiweza, jaribu kuweka wazi ni nini hasa kilitokea, waambie watoto hao ukweli kuwa wewe hukutaka kuolewa na baba yao bali baba yao na shangazi yao ndio waliokushawishi uachane na Baba yao mdogo kwa sababu ambazo mwenyewe na mumeo mnazijua. Hii itasaidia watoto hao kuelewa ukweli wa mambo na kupunguza attacks kwako, lakini haitorudisha heshima kwako.

3.Wifi yangu ambaye ndio alinishawishi niachane na mdogo wake niolewe na kaka yake amekuwa adui yangu mkubwa baada ya kuona maslahi aliyokuwa anayapata wakati anafanya kampeni niolewe na kaka yake hayapati tena baada ya mimi kuolewa ananiita mimi opportunist imefata mali za ndugu yake.

Dinah anasema: Mawifi wengi Duniani hivyo ndivyo walivyo, iwe wameshiriki kuharibu au kufanikisha siku zote mke wa kaka yao utakuwa adui tu. Achana nae na focus zaidi kwenye maisha yako na mumeo.

4.Shemeji yangu ambaye alikuwa mchumba wangu amezidi kuwa Handsome na mwili wake wa mazoezi namtamani mpaka namwota usiku anaitomba najaribu kumshawishi angalau anifanye chochote anachotaka mradi anitombe hata mara moja tu amegoma, amejaaliwa uume mkubwa, mgumu na mweusiiii ambapo mume wangu hata ikisimama hamfikii nusu kwani uume wake ni flabby and lazy.

Dinah anasema: Mamaa P hiyo ngono ya mara moja itabadilisha nini? Sana sana hizo dk 20 mpaka ufike kileleni zitamharibia jamaa ndoa yake ambayo sidhani kama angependa iharibike na ndio maana hashawishiki, kwa kifupi baada ya kutendwa na wewe sidhani kama atakuwa na nguvu za kumtenda mkewe na mtu aliemtenda....sijui unanielewa! Hivyo achakupoteza muda wako kumfirikia shemeji yako.

Of cause Ex wako utaendelea kumuona anavutia na anapendeza zaidi, ulimpenda na ulimuacha ukiwa bado unampenda. Mwenyewe umedai jamaa alikuwa fit sasa kama mkewe anamuangalia vizuri na kuhakikisha jamaa anaendelea kupendeza na kuvutia.....utalaumu kweli? Hilo ndio jukumu letu kuu kwenye ndoa....kuwatunza waume zetu kama wao wanavyotutuza sisi...hivyo na wewe fanya the same kwa mumeo. Kama ulikubali

Msinitukane jamani naombeni ushauri.

Ni mimi

P
Dsm. "

Dinah anasema: Asante sana kwa ushirikiano Dada P, nadhani wachangiaji wengi wamegusia points muhimu na hakika umezifanyia na somehow kusaidi kuanza kufanya uamuzi wa busara.

Hapo kuna mawili, Moja baki kwenye ndoa yako na jitahidi kumsaidia mumeo kuacha pombe ili uwezo wake wa kungonoka urudi na vilevile mfundishe/elekeze mbinu nyingine ili ajue namna ya kukurishidha kingono kwa kutumia njia nyingine ili kuongeza ukaribu wenu na kuibua hisia za kimapenzi.

Au, Mtaliki mumeo na kuendelea namaisha yako kama wewe, Mungu akijaali utakutana na mwanaume mwingine na ku-share maisha yenu. Lakini kamwe na ni marufuku kujipendekeza kwa Mume wa mtu, ulipewa nafasi ya kuwa nae lakini ukaichezea na kuipoteza, mwingine kaipata nafasi hiyo hivyo haiwezi kurudi tena kwako......waswahili walisema "Bahati haiji mara mbili".

Bibi yangu alisema " Jenga heshima kwa Ndugu na rafiki wa mumeo ili na wao wakuheshimu, kamwe usirafikiane nao kwa vile tu umeolewa na Ndugu yao"

......sentesi hii inamaanisha kuwa kinachoepusha hisia za kimapenzi kati yako na wanaume/wanawake wengine kwenye familia mbili tofauti ni HESHIMA.

Kila la kheri!

Saturday, 15 May 2010

Ukikongonoka na aliye keketwa au mwenye govi Unajisikiaje?

"Je wanaume wanafeel vipi wakifanya ngono na mwanamke alokeketwa? And wanawake wanafeel vipi wakifanya na mwanamme mweny govi?"

Dinah anasema:Asante kwa swali lako ila ni fupi mno! Nadhani inategemea zaidi na ukeketwaji aliopokea mwanamke husika, kukeketwa kunatofauti Barani Afrika, kule Somalia wanaondolewa kila kitu ukeni na pale ambapo uume/mtoto anatokea hushonwa kidogo hivyo basi wanawake hawa hupata maumivu makali sana wanapoingiliwa kingono unless otherwise wakafanyie upasuaji ili kuachanisha lile kovu pale ukeni.

Baadhi ya Makabila Afrika magharibi, Masharini na Kunisi wanakeketa wanawake kwa kuwaondoa kisimi na mashavu yake(zile nyama zinazoshikilia kisimi) lakini uke pale kwa chini unaachwa kama ulivyo hivyo mwanamke huyu akiingiliwa kingono hakutokuwa na tofauti na mwanaume yeyote ambae hajakeketwa.

Tofauti kubwa itakuwa kwenye kupata kilele cha nje/juu kupitia kisimi, kwamba mwanamke alie keketwa hatoweza kusikia utamu wa ngono kwenye kisimi kwa vile hakipo lakini bado damu itakuwa ikimiminika kwenye eneo zima la uke kila naposisimka kingono (akiandalaiwa vizuri) na mwanamke huyu anaweza kufurahia ngono zaidi kwenye maeneo mengine ndani ya uke.

Mwanaume mwenye Govi hana tofauti na yule ambae amekatwa kwa sababu uume ukisimama vema "ulemkono wa sweta" (govi) huvutika kwa chini na huwezi kujua kabisa kama jamaa hajatahiriwa. Shughuli itakuwa pale unapotaka kumpa mdomo kabla hajasimamisha.....itabidi ufanye kama vile unamenya ndizi au...au?

Nadhani maelezo yangu yatakuwa yamejibu maswali yako ki-logical zaidi.
Kila la kheri!

Thursday, 13 May 2010

Nimegundua Mpenzi alizaa kabla, sina amani-Ushauri

"habari dada dinah na pole kwa kazi ngumu ya kuelimisha jamii, mimi nimekuwa mfatiliaji wa hii blog yako kwa muda mrefu na leo nina swali , Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21 sijaolewa ila nina mchumba ambae ana malengo mazuri na mimi lakini dada nina tatizo moja.

Mchumba wangu huyu tangu niwe na uhusiano nae ni mwaka umepita sasa, kwa kweli ananipenda na mimi nampenda tena sana tu na ananihudumia kwa kila nitakacho yani kama mke wake. Huwa hanifichi kitu! lakini nimekuja kugudua kuwa yeye ana mtoto mmoja wa kike na ni mkubwa, kwanza alikataa kuniambia kwa kudai ni mapema mno baada ya kumbana akaniambia kweli kuwa anamtoto ambaye alizaa na mwanamke mmoja kabla ya kuwa na uhusiano na mimi.

Alidai kuwa anamuhudumia yule mwanamke sababu wazazi wa yule binti wamembana ahudumie, pia amesema yeye anampenda mtoto tu na sio mama yake kwani hakutaka kuzaa nae ila ilikuwa bahati mbaya!

Sasa dada mimi Moyo wangu umeingia chuki sana baada ya kusikia hivyo lakini mwenyewe anadai anampenda sana mtoto wake kuliko kitu kingine, mimi hapo ndio sielewi je anampenda kuliko mimi?

Dada naomba ushauri, huyu mwanaume nampenda na ndiye anayenisomesha Chuo mpaka sasa na huduma zote ananipa ila tatizo ni chuki iliyoniingia ghafla nashindwa kuelewa ni kwa nini naomba msaada wako! kwani nataka nafsi iwe na amani."

Dinah anasema: Asante sana kwa mail na uwazi wako, Habari ni njema sana tu namshukuru Mungu. Vipi wewe? pole kwa kutokuwa na Amani moyoni. Kuna mchangiaji kafafanua vema kuwa hisia hizo sio chuki bali wivu nami nakubaliana nae kani ni ukweli.


Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke/mwanaume yeyote mwenye mapenzi, unapogundua mpenzi wako anazungumza na Ex wake na siku zote huwa tunawakataza wapenzi wasiwasiliane na Exes.....sasa ndioitakuwa Ex ambae wametengeneza mtoto pamoja kama sehemu ya mapenzi yao....mmh?!! Ni ngumu sana tusichukulie juu-juu tu.

Mchumba wako ni Kaka mwema, ni kweli anakupenda na amedhihirisha hilo kwa kutokuambia mapema kuwa anamtoto ili asikupoteze, muda ulipofika kaweka wazi kila kitu na hata kusema kuwa anahudumia mama mtoto wake. Hii yote inaonyesha kuwa Mchumba wako ni mmoja kati ya wanaume wachache waaminifu, wakweli na wawazi.....Mshukuru Mungu kwa hilo.

Nadhani kinachokuumiza zaidi ni Mchumba wako kumhudumia mama mtoto wake na sio mtoto, kama Mchumba wako hana uhusiano na mwanamke huyo ni wazi hapaswi kumpa huduma yeyote yule mwanamke bali mtoto wake tu.

Mtoto huyo ametengenezwa na watu wawili, yaani yeye na huyo mwanamke hivyo wote kwa pamoja wanatakiwa kukusanya nguvu na kumhudumia mtoto wako sio Mchumba wako kumhudumia mwanamke huyo kwa kisingizio cha mtoto kwani mwanamke huyo hamhusu kwa sasa.


Wazazi wa yule Binti wanachokifanya sio haki na kisheria hakitambuliki, Mchumba wako anatakiwa kuhudumia mtoto wake tu na si vinginevyo. Ukipenda unaweza kuongea na Mchumba wako sasa au kusubiri mpaka mtakapo funga ndoa wewe na mume wako (waakati huo) itabidi mjipange na kwenda kuonana na wanasheria wanaojihusisha na masuala ya watoto na familia (zamani walikwa pale Mnazi mmoja) huko watampa ushauri na nyaraka zinazoelezea haki yake kwenye maisha ya mtoto wake na sio mama wa mtoto huyo.


Alafu mchumba wakoa naweza kuwakilisha ishu hiyo Mahakamani (Mahakama ya Wilaya na omba kuonana na Hakimu moja kwa moja, Hawana matatizo kabisa) na ajieleze huku akiwakilisha yote aliyopewa kule kwenye kitengo cha Sheria kinachojihusiaha na maswala ya watoto na familia ili wazazi na huyo mama mtoto waambiwe kuwa kisheria Baba mtoto (mchumba wako) anatakiwa kuhudumia mtoto wake tu na kwanini, pia Hakimu atasema wazi ni kiasi gani kitatolewa na baba kwa mwezi kwa ajili ya mtoto.


Ni kweli anapenda mtoto wake na upendo huo ni tofauti na alionao kwako, mtoto wake ni damu yake hawezi kuikimbia unless otherwise DNA test iseme vinginevyo. Wewe ni mpenzi wake na anakupenda sana tu pia anampenda mwanae kuliko kitu chochote....hiyo haina maana kuliko wewe.

Mchumba hajui namna gani ya kuwakilisha maelezo kwako ili kukuhakikishia kuwa anakupenda zaidi ya mtu yeyote hapa Duniani lakini pia anampenda mtoto wake kuliko kitu chochote hapa Duniani. Katika hali halisi hawezi kulinganisha upendo wake kwako na kwa mtoto wake kwani ni hisia za upendo za aina mbili tofauti ndani ya moyo wake.

Kama kweli unampenda huyo jamaa na unakwenda kufunga nae ndoa inakubidi ukubali mzigo alionao, kwa maana kubali kuwa kuna mtoto aliezaliwa kabla wewe hujamjua Jamaa na hivyo mtoto huyo ni sehemu ya familia yenu.

Waswahili wanasema ukipenda Boga penda na ua lake, lakini wanasahau kuwa upendo haulazimishwi. Unaweza ukapenda lakini usipendwe hivyo suala muhimu ni kuchukulia mambo kama yalivyo na kujengeana heshima ili kuishi kwa amani.


Huitaji kumpenda wala kumchukia mtoto huyo bali mchukulie kama ambavyo utamchukulia mtoto yeyote utakaekutana nae, hakuna haja ya kujilazimisha au kujipendekeza ili uwe kama "mama yake" kwani kwamwe huwezi kuwa mama yake, hakikisha Mchumba wako hamlazimishi mtoto huyo kukuita wewe "mama" akuite atakavyo yeye as long as hakutukani...MF anawezakukuita jina lako au Antie, lakini ikitokea mtoto kajisikia kukuita mama that will be fine.


Mthamini kama mtoto wa Mchumba wako, mpe ushirikiano wako kila atakapohitaji bila kuwa na hisia zozote mbaya juu ya mama yake as long as Mchumba wako anaweka kila kitu wazi kama anavyofnaya sasa, hakikisha anaendelea kukushirikisha kila anapofanya mawasiliano na mama mtoto wake huyo.

Kamwe tena ni marufuku kumwambia mchumba wako kuwa ni vema mtoto ahamie kwenu kwani siku zote mtoto wa kike anapenda kuwa na mama yake, kitendo cha kumtenganisha na mama yake hata kama ni kwa nia njema bado mtoto anaweza kukichukulia vinginevyo na hivyo mtoto huyo kuathirika.

Ni vema mtoto akaamua mwenyewe kuja kukaa nanyi moja kwa moja au kukaa kwa muda mfupi kila baada ya miezi kadhaa n.k. ili kujenga uhusiano mzuri na pia kupata nafasi ya kufahamiana.

Nini cha kufanya: Kwa vile mchumba wako kaweka kila kitu wazi, unachotakiwa kufanya ni kuacha kuhoji kuhusu upendo wake kwa mtoto wake au hata kujilinganisha kwa kusema kuwa "najua unampenda mtoto wako kuliko mimi", badala yake anapomzungumzia mtoto mpe ushirikiano na ikiwezekana ushauri wa kujenga na sio kubomoa ikitokea kaomba ushauri kutoka kwako. Hiyo Mosi.

Pili, Ondoa shaka juu ya uhusiano wa mchumba wako na mtoto wake, chukulia uhusiano wake huo na mtoto wake ni mfano mzuri kwako kujua yeye ni baba wa namna gani na atawapenda vipi watoto wako mara baada ya kufungandoa.

Tatu, hakikisha unaulizia mtoto mara kwa mara ili kujua anaendeleaje hii itampunguzia mzigo na itampa furaha akijua kuwa wewe pia unajali kuhusu mwanae.

Nne, zingatia masomo yako ili ufanye vema kwenye mitihani yako ambayo ni ndio msingi wa maisha yako ya baadae kama mwanamke anaejitegemea.

Ni matumini yangu kuwa maelezo ya wachangiaji na haya yangu yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuelewa zaidi njisi ya kukabiliana na wivu ulionao kati yako na mama mtoto wa Mchumba wako.

Nakutakia kilala kheri kwenye Masomo yako, Uchumba wenu na maisha yenu ya baadae kama mke na mume.

Tuesday, 11 May 2010

SmS imezaa Penzi linalonichanganya-Ushauri

"Shikamoo dada Dinah, pole na majukumu.Mimi nimfuatiliaji mzuri wa blog yako na nimeona niombe ushauri kupitia blog yako. Naitwa Angel nina miaka 23, ni mwalimu wa Sek├Ândari moja hapa Mbeya.

Stori yangu inaanzia hapa; Mwaka 2007 Septemba nikiwa nasoma Diploma ya Ualimu huko Dodoma, kunakaka mmoja alikosea namba kwa kutuma vocha kwenye namba yangu. Mimi bila hiana nikamrudishia ile vocha na kumpigia kumwambia kaka umekosea namba.

Basi kwa kuwa nilikuwa mstaarabu kwake, kesho yake alinipigia akaniomba niwe dada yake kwani watu hufahamiana kwa njia tofauti. Nilimkubalia natukaanza mawasiliano kama kaka na dada. Yeye alikuwa Mwanza.

Baadae 2009 mwanzoni akaniomba tuwe wapenzi na kwa kuwa nilikuwa sina boyfriend kwa kipindi hicho nikamkubalia, tukawa wapenzi ingawa badohatujaonana. Nikawa naongea na ndugu zake kama shemeji yao nae akawaanaongea na ndugu zangu.

Tuliahidiana mambo mengi sana ambayo tulipanga kuyafanya mara baada ya kuonana. Mara nyingi nilipenda kumuuliza je atanipenda the way nilivyokwa kuwa mimi kwani ni mnene na wanaume wengi hupenda wanawake wembamba akawa akinijibu alichompa Mola hawezi kukikataa kwani ameamua yeye hivyo hakuna kitakachotutenganisha.

Hatimaye mwaka huu mwezi wa Nne nilienda kwake Musoma alikohamishiwa kikazi. Nampenda zaidi ya mwanzo kabla sijamuona, siku mbili za mwanzo niliienjoy kuwa nae. Tatizo likaja akawabusy sana na simu yake akichat na wanawake tofauti tofauti, sms za mapenzi na nilipokuwa nikishika simu yake alikuwa mkali kweli akidai kuwa eti namchunguza.

Usiku akilala ndio nachukua simu na kusoma zile sms,asubuhi akienda kuoga akawa anaficha simu yake. Baada ya wiki kuisha nikaongea nae kumwambia anavyofanya sivyo kabisa na kama hanipendi aseme tu kwani tulishakubaliana kuwa endapo mmoja watu hajaridhika na mwenzie aseme tu kwa uwazi.

Akasema hayo ya kutonipenda nayasema mimi yeye hana mawazo hayo kabisa, kwa kweli hatukufikia muafaka tuligombana kweli usiku ule na nikamuomba kesho yake akanikatie ticket niondoke.

Kweli baada ya siku mbili niliondoka, Nilivyofika Mbeya siku mbili za mwanzo tuliwasiliana vizuri kabisa, baadae nikawa nikimtumia sms hajibu na nikimuuliza kama kuna tatizo anadai hakuna na anaomba tuache kuwasiliana kwa muda then atanitafuta. Nikamwambia kama anataka tuachane aseme tu , lakini hakujibu na alikata simu.

Kitendo hicho kiliniumiza sana kwani nashindwa kabisa kufundisha wanafunzi kwangu kila nikiwaza promise tulizopeana mwanzo na vituko anavyonifanyia sasa nashindwa kabisa ku-concentrate na kazi zangu.

Nampenda saaana tu ila nashindwa nifanyaje ili nijue anawaza nini kuhusu mimi na hisia zake kwangu zikoje?naomba ushauri.
Asante, Madam Angel-Mbeya"

Dinah anasema: Angel asante sana kwa ushirikiano, ni matmaini yangu kuwa maelezo kutoka kwa wachangiaji yatakuwa yamesaidia kwa kiasi fulani kujua nini cha kufanya ili kupana amani na hivyo iwe rahisi kuendelea na maisha yako.

Huyo mwanaume (kutokana na maelezo yako) hana mapenzi na wewe alitaka kukutumia kama anavyotumia hao wanawake wengine, na usikute anatumia mtindo huo wa kutuma sms kwenye simu za wanawake ili kuwapata kiurahisi kama alivyofanikiwa kwako.

Na mara baada ya kupata alichokitaka ndani ya siku mbili ulipokwenda kumtembelea alihamisha hisia zake kwenye simu yake, Mshukuru Mungu kuwa mwanaume huyo alionyesha wazi tabia yake ilivyo ukiwa nae karibu imagine ni mangapi anafanya ukiwa Mbeya?

Huyu mwanaume kama walivyo Players wote huwa hawataki kuonekana kuwa wao ndio chanzo ya uhusiano kufa ili wakiishiwa huko waliko waweze kurudi kwako na kuomba uhusiano wenu uendelee kwa madai kuwa wewe ndio ulimuacha lakini yeye hakufanya hivyo.

Player yeyote akiona uko serious na uhusiano atakuambia "nitakutafuta" kwa maana nyingine anasema "usinisumbue na nikihitaji huduma yako nitakuambia"......hii inamaana kuwa mwanaume huyo hakufai na ukiendelea kutegemea siku atakutafuta utakuwa unajipotezea muda wako bure na kujipa maumivu ya moyo juu ya mtu ambae hathamini utu wala effort yako kwenye uhusiano husika.

Najua unahisia kali za mapenzi juu yake na hii inaweza kuchangiwa na umri wako kuwa mdogo na hivyo unashindwa kutofautisha hisia za kikware (last) na zile za kimapenzi (love) zote zinafanana sana kwa kuanzia lakini moja hudumu na nyingine huisha....sasa alichokuwa nacho huyo mwanaume juu yako ni Ukware na sio mapenzi.

Vievile nahisi kuwa kutokuwa ulikuwa na matarajio makubwa/mengi juu ya uhusiano wako na mwanaume yeyote kukutaka kwa vile unahisi kuwa umekamilisha mahitaji kimaisha isipokuwa mume, kwamba umemaliza masomo, unajitegemea kwa kufanya kazi na kinachokosekanakwenye maisha yako ni mtu wa ku-share nae maisha yako.

Huna haja ya kujua anawaza nini juu yako kwani amekwisha liweka wazi hilo kuwa hakuna mwanamke yeyote anaemthamini na kila mwanamke kwake ni "sanamu" la kuchezea na fashion ikipita anatupilia mbali na kwenda kununua the latest one.

Badili mawasiliano yako ili asiweze kuwasilianana wewe, pia futilia mbali namba yake ili usishawishike kuwasiliana nae unapojisikia mpweke (we all have those days), jaribu kubadili mtindo wa maisha yako hasa kwa kufanya mazoezi mepesi nakubadili ulaji wako kama unadhani kuwa ukubwa wa mwili wako ni kitu ambacho kinakukwaza.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umejiongezea hali ya kujiamini zaidi kama mwanamke mdogo, mrembo, alieenda shule na mwenye kujitegemea kiuchumi. Tumia muda wako mwingi kuongea/kujichanganya na watu wanaokujali nakukupenda (ndugu, jamaa na marafiki).

Hakikisha unajiweka busy na jitahidi ku-focus zaidi kwenye Taaluma yako ili usijepoteza kazi kutokana na utendaji wako mbaya unaosababishwa na mawazo juu ya mtu amabe hana umuhimu wowote kwenye maisha yako.

Mungu atajaalia na siku moja utakutana na kijana mwema, mwenye kuheshimu na kuthamini mwanamke, mwenye upendo wa dhati na kwa pamoja mkapendana na hatimae kufunga ndoa. Yote hayo yanawezekana kwani Angel wewe bado ni mdogo na una muda mwingi wa kujipanga upya na kufurahia maisha yako kama mwanamke anaejitegemea kabla hujajikita kwenye masuala ya kimapenzi na mahusiano nahatimae kuwa Mke na mama kwa watoto wako.

Kumbuka ukiwa mke na mama hutopata muda wa kufurahia maisha yako wewe kama Angel bali mke na mama kwa watoto wako.....maisha yako yatabadilika in good way, lakini itakuwa great kama utakuwa ume-enjoy uanamke wako kabla hujawa na majukumu mengine ya Mke na mama.

Kila lakheri!

Friday, 7 May 2010

Mke wangu haeleweki, sijui kwa vile sina kitu?-Ushauri

"Habari dada Dinah, pole sana na kazi nzito uliyonayo ya kutusaidia kimawazo na kutuelemisha,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 31. Nilioa miaka mitatu iliyopita na kubahatika kupata mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka 2 sasa.Huyu mke wangu ni mke ndugu kwani wazee upande wa bibi zetu mzaa baba ni ndugu waliotoka sehemu moja. Baadhi ya ndugu upande wa mke wangu hawakutaka tuoane lakini kwa sababu sisi tuliamua na kusimamia uamuzi wetu walikubaliana na mawazo yetu na tukafunga ndoa.


Tumeishi na mke wangu kwa mapenzi na kusikilizana sana na kushaurina katika kila jambo. Baada ya miaka 3 ya ndoa mke wangu alikutana na rafiki yake mmoja na kumueleza kuwa anahitaji amsaidie kutafuta kazi nyingine kwani kazi aliyokuwa nayo mwanzo ilikuwa haina maslahi kwake.Rafikiye alimpa namba ya mzee mmoja na alimkutanisha nae na hapo alianza kumtafutia kazi. Kazi iliyopatikana ilikuwa nje ya mji na yeye alikubali kwenda kwa kudhani kuwa huko angeweza kubadilisha maisha yake.Aliitwa kwenye usaili uliyofanyika Tabora na mara aliporudi kutoka huko kuna mtu mmoja aliejitambulisha kama Boss wake mpya, huyo Boss mpya walianza mawasiliano ya karibu sana na kutumiana msg mpaka saa nane za usiku.Nilipohoji nilijibiwa kuwa hawezi kumjibu vibaya kwani huyo ndiyo mtu pekee ambae angweza kumpatia kazi, nilikaa kimya lakini baadae ikawa imezidi sasa bila ya uoga jamaa alikuwa akipiga simu na mke wangu alikuwa akitoka nje na kuzungumza na nilipokuja juu nilijibiwa "sizungumzii nyumbani kwako ndio maana nimetoka nje", Duh, hali ilikuwa mbaya.Siku moja nilimuuliza wife juu ya msg yeye aliondoka kwa hasira saa 9 usiku eti amechoshwa na makelele yangu, kumbe kesho kutwa yake ndio alikuwa anaenda huko kwenye makazi mapya bila ya kuniambia chochote.Mimi nilienda kwa dada yake na kumshitakia lakini dada mtu alikuja juu akaniambia nimuache kwani anaenda kazini. Nilitoa Talaka kwa mke wangu huku nikiwa bado nampenda sana, niliumia but nikafanya hivyo na yeye akaenda huko kwenye makazi mapya na alikuwa na mahusiano na huyo Boss wake huko.


Baada ya miezi miwili kupita nilipokea simu kutoka kwa aliekuwa mke wangu na kuniomba msamaha kwa yote yaliyopita huku akitoa kisingizio kuwa mtoto wetu anakosa mapenzi ya baba na kuniambia kuwa yeye ameamua kuachana kabisa na huyo bwana kwani amegundua kuwa amekosea sana.Nilimsamehe mke wangu na kwa sababu eda ya Talaka ilikuwa haijaisha basi nilienda Shinyanga na kukutana nae na hivyo tukaamua kurudiana tena na tukasameheana kabisa. Baada ya muda yule boss aliacha kazi pale nadhani walikuwa hawaelewani na kesi zao zilifika mpaka makao makuu ya Organization yao na akaamua arisgn.
Tatizo la mke wangu ni kwamba siku hizi amebadilika sana, Mimi naishai Dar na yeye yupo Shinyaka kikazi lakini amekuwa hataki mawasiliano na mimi na nikimpiga ananiambia nimuache kwani yeye kwa sasa hataki kuwa na mwanaume masikini kama mimi.Kiukweli mimi kwa sasa sina kazi ya kuajiriwa, lakini nina biashara ndogondogo ambazo zinanipatia kipato kidogo sana, sasa kumtumia hela yeye inaniwia vigumu sana. Yeye amekuwa akinitaka niachane nae na ninapozidi kumng'ang'ania basi yatanikuta makubwa au naweza kufa kwa UKIMWI.Pia ndugu zake hawafurahii kabisa mahusiano yetu kwani hata wao wanaujua nampenda huyu mwanamke na kikubwa nilikuwa sipendi kumtesa mtoto wangu kwa kulelewa na mama au baba wa kambo.


Sasa wadau nipo njia panda niendelee kuwa na huyu mwanamke au niachane nae? Ila kiukweli nampenda sana huyu dada,

Soprano- Dsm"

Dinah anasema: Soprano kaka wachangiaji wamejitahidi na wamekupa maelezo yaliyojitosheleza. Kutokana na maelezo yako Mkeo sio muaminifu na anathamini pesa kuliko utu/ndoa yake, vilevile ndungu zake wanampa "kichwa" kwa ku-support tabia yake chafu badala ya kumuonya ili adumishe ndoa yake.

Inavyoelekea mkeo aliamua kufunga ndoa na wewe kwa sababu nyingine, kwa vile huna hela ni wazia lifunga ndoa na wewe ili kuondoa "mikosi", kujijengea heshima kwenye jamii kuwa na yeye anandoa na mtoto mmoja lakini hakuwa na mapenzi ya dhati kwako.

Huyu mwanamke hajabadilika, isipokuwa amechoka kuwa mtu mwingine. Amechoka kuwa yule mwanamke uliempenda na kuamua kufunga nae ndoa. Aliamua ku-act ili aipate hiyo ndoa. Mwanamke mwenye mapenzi ya dhati na aliefunga ndoa kwa sababu ya mapenzi kamwe hawezi kukutenda the way mkeo kakutenda?

Ni kweli kabisa ukiendelea kumng'ang'ania kwa jina la mapenzi hakika utaondoka Duniani mapema na mtoto wako atabaki bila baba na hivyo kuishi maisha ambayo wewe usingependa mwanao apitie.

Yeye ni mtu mzima na anafanya kazi, kwanini a-demand pesa kutoka kwako wakati anajua kipato chako ni kidogo?!! Mwanamke anaejitegemea kiuchumi akijua kuwa mumewe uwezo wake ni mdogo siku zote atakusanya nguvu zake na kuchanganya za mumewe ili wafanye jambo moja la kimaendeleo kama familia.

Sasa kaka yangu, fanyia kazi yote uliodhani kuwa ni muhimu kutoka kwa wachangiaji alafu ongezea na yangu...ukimaliza, fanya hivi:-

Mtaliki huyo mwanamke haraka uwezavyo kwani ukiendelea kusubiri kwa kutegemea kuwa ni "mke wangu" na Mungu atamrudisha hakika utakuwa unajipotezea muda na kujikoseshea bahati. Utakapofanikiwa kuachana nae kwa amani (ili wote mpate nafasi ya kumuona mtoto wenu) basi ujitahidi na ku-focus zaidi kwenye shughuli zako za kimaisha ili uweze ku-provide kwa mtoto wako.

Kuna kinadada wengi wenye kujiheshimu, kudhamini tu zaidi ya mali lakini hawajaolewa, hivyo basi ukiwa huru na kubadili mtindo wa maisha yako hakika utakutana na mdada mwema atakaekupenda kwa dhati.

Kila la kheri!

Thursday, 6 May 2010

Tunafunga soon lakini story za Ex wake zinaniudhi-Ushauri

"Dada Dinah pole na kazi.
Nashukuru kwa ushauri wa ukweli kuhusu relationships,to be honest nafanyia kazi kila ushauri as I apply by reflecting kama mimi ndio muuliza swali. Naomba wadau nisaidieni kwa hili linalonotatiza.

Nina miaka 30 na nimepata mchumba mwaka mmoja sasa, tunatarajia kuoana hivi karibuni na tumekwisha gawa kadi za mualiko hivyo jamii yote hapa wako aware na plan zetu. Tatizo ni moja, huyu mchumba wangu ana umri wa miaka 23 alikuwa na jamaa yake kabla hajakutana na mimi.

Wakati ninaanza nae aliniambia kuwa huyo kaka ndio aliyem-bikiri na akawa anamsifia sana kwa vile ni jasiri, yaani akawa anarudia rudia sana haya maneno. Nilimwambia kuwa mie sipendi kujua yaliyotokea kabla yangu akawa anaelewa lakini naona amekuwa anashindwa kujizuia kwani bado anarudia hii bad story.

Imagine tumeshaamua kuoana na vikao vinaendelea ila najisikia vibaya sana huyu mwenzangu kukumbuka issue ya Msukuma wake wa zamani (jamaa aliekuwa nae ni Msukuma)Je ni kweli kuwa mtu aliyem-bikiri msichana huwa ni kumbukumbu ya maisha?

Na kama ndio hivi,najua kuna wasomaji ambao wameoa mabinti waliokuwa tayari wamepitiwa,wamewezaje kuishi vizuri katika scene ya hii concept ya mtu aliyebikiriwa na mwanaume mwingine?

Naomba msaada ili nimshauri huyu mwenzangu, najua ananipenda nami nampenda sana tu ila inapokuja kwenye kunipa story za Msukuma ndio kama naformat issue za mapenzi na yeye. Nifanyeje jamani na mda si mrefu huenda tukapeana ahadi za maisha.
Jerry."

Dinah anasema: Jerry asante sana kwa ushirikiano. Ni kweli yule mtu aliyekuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi na ngono (aliekubikiri ) hubaki akilini kwa muda mrefu hasa kama tendo lile lilifanyika kwa wakati muafaka na kwa mapenzi. Hiyo haina maana kuwa Mchumba wako anampenda Msukuma, hapana!

Yeye kukusimulia kuhusu Msukuma ni kuonyesha kuwa alitoka na mwanaume mmoja tu na kwake hiyo ni sifa, kwa kifupi anajaribu kukuhakikishia kuwa wewe ni mpenzi wake wa pili na wa mwisho as mnakwenda kufunga ndoa ila hajui namna ya kuliwakilisha hili kwako.

Mwambie hivi " nimekwisha kuambia kuwa sitaki kujua kilichotokea kabla yangu kwani kinaumiza hisia zangu juu yako, najua mimi ni mpenzi wako wa pili na ninajivunia sana kuwa na mpenzi amabae hajapitiwa na wanaume wengi. Sasa mpenzi nikisikia tena unamzungumzia Msukuma nasitisha ndoa"......Mikwara sometimes inasaidia!
Jaribu hiyo uone....
Kila la kheri!

Tuesday, 4 May 2010

Mpenzi ni Mbabe, kosa lake mimi ndio niombe radhi-Ushauri

"Habari dada dinah,
Pole na hongera kwa kazi yako nzuri kwani tunajifunza mengi.

Dada dinah, mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 na nina BoyFriend wangu ambaye niko nae takribani miaka 6 japo hatujaoana kwani yeye bado anasoma. Kwa ufupi tulisoma wote ila kutokana na sababu mbali mbali nimemtagulia na sasa nafanya kazi.

Mahusiano yetu yamekuwa ya vuta nikuvute kutokana na sababu mbali mbali za hapa na pale japo tatizo kubwa ni WIVU na UBABE alionao BoyFriend wangu, mara nyingi amekuwa mgumu sana yeye kuomba hata samahani pale anaponikosea badala yake hugeuza kosa kuwa la kwangu.

Ili kuepuka ugomvi na mambo yaishe naishia kuomba mimi samahani. Niseme ukweli tunapendana na ktk upelelezi wangu sijawahi kusikia hana mtu nje zaidi yangu japo siwezi jua mambo ya wanaume.


Mara kwa mara amekuwa akidiriki kusema maneno ya fedhea na hata kunitukana. Pia mkipanga appointment muda fulani tukutane yeye anachelewa sana na anaweza akafika baada ya masaa hata 3. Kwakweli huwa nashindwa kuzificha hasira zangu na kujikuta nachukia (kununa). Nimuulizapo hunigeuzia kitabu lakini hawezi kusema samahani, Mimi hiki kitu kinanikera sana.

Siku moja alikuja chumbani akitaka mambo fulani, kama kawaida ya wapenzi kutaniana basi alitaka kufunga pazia nikamkataza na baadae aliporudi kitandnani nikamwambia kafunge. Kwa hasira alinyanyuka na kutaka kuondoka.

Nilipoona hivyo nikamvuta nikamwamia "hutaniwi"! Cha ajabu alinisukuma na kuniburuza nikiwa NAKED huku akielekea kufungua mlango wa nje na kisha akaondoka zake. Kwa kweli iliniuma sana n akuaibika kama pale nje kungekuwa na mtu.

Baada ya muda nilimtumia msg kuwa ktk mahusiano yetu amenionyesha picha halisi yeye ni mtu namna gani. Wadau hakujibu na tulichuniana takribani wiki 2 mpaka pale mimi nilipomwambia aje home. Tukiirudia topic ile lakini kama kawaida yake hakuomba samahani na kuniuzia kesi mimi.

Siku nyingine tulikubaliana tukutane Town ili nichukuwe pesa fulani kwani yeye alinisisitiza kuwa anashughuli nyingi hivyo niwahi. Ni kweli nilijihimu mida ya saa moja nikawa nimefika. Nilipompigia simu alidai bado amelala. Honestly niliumia na kwa hasira niliondoka nikarudi home. Wadau huyu mpenzi hakusema lolote wala samahani mpaka leo, baadae alinipigia simu mida ya saa 6 akiuliza niko wapi. Nilimjibu niko home.

Kutokana na tabia hii, nipatapo nafasi ambapo tukio kama lake linaweza kufanyika basi na mimi humlipiza ili aone uchungu wake. Huwezi amini huja juu na kulalamika kuwa ni kwanini nafanya vile, hapo ndipo ninapopata nafasi ya kumuliza je ni vibaya? Na je wewe uliponifanyia hivi uliona ni sawa?

Dada dinah, yeye huishia kusema niache kulipiza kisasi, Hata mimi humwabia kama hutaki kutendewa basi jirekebisha. Niliamua kuliweka hili suala mezani na tukalijadili kwa kina kama wapenzi lakini alihishia kusema atabadilika japo mpaka leo sioni mafanikio.


Nimechoshwa na hii tabia, yaani nimekuwa mtu wa kulia na kuumwa vidonda vya tumbo sababu ya hasira. Imefikia hatua anatoa maneno yake ya kejeli eti mimi na yeye nani mwanaume?anadai tutashindana mpaka lini?

Kununa nuna ndio haswaa, kwani hasione nina marafiki wakiume hata akiwa mfanyakzi mwenzangu. Kafanya juu chini niachane na nabest zangu wanaume ila nimegoma. Imefikia hata hatua tukienda kwenye fuction yoyote kama harusi basi mambo huko hayaendi tutanuniana mpaka tunarudi nyumbani, kisa watu wamenihug.

Dada dinah na wadau wote nisaidieni kwani nimechoka, mara nyingine nawaza kuachana nae ila naogopa magonjwa na kutengeneza CV za wanaume. Nifanye nini jamani? Naamini hakuna kitu kizuri kama kubembelezana na kuombana msamaaha pale mwenzi wako anapokukosea. Pia nimechoka kuona natendewa mimi na nishiwa mimi kupiga magoti kuomba samahani.

Nishaurini wadau kwani hayo ni machache tu."

Dinah anasema: Asante sana mpendwa kwa kuniandikia na kwa ushirikiano, kutokana na maelezo yako nadhani huyo jamaa hakulelewa kwenye mazingira ya nidhamu kwamba hajui kusema asante wala samahani.

Watu waliokulia kwenye mazigira hayo ni vigumu sana kwako kujua umuhimu wa shukrani na kuomba radhi, vilevile jinsi wanavyokuwa na kuwa na wapenzi huwa ni wagumu sana kusema "nakuepnda", "nimekukumbuka" "ninafuraha sana kuwa nawe" na wengine kuwa wabinafsi linapokuja suala la ngono.

Miaka sita kama wapenzi bila ndoa ni mingi mno yaani mmezoeana kupita kiasi na hivyo kulichukulia uhusiano wenu kama kitu mlichokizoea na mnashindwa kujitoa pamoja na kuwa wakati mwingine mnahisi kabisa kuwa " sasa basi, huyu mtu hanifai" lakini mnashindwa kufanya uamuzi na kusonga mbele kila mmoja wenu na maisha yake. Hilo moja.

Pili, mpenzi wako bado ana-elements za Mfumo Dume, yeye kuwa shule na wewe kufanya kazi (kuwa na kipato) n wazi anatishika nakuhisi kuwa haeshimiwi kama mwanaume na ndio maana amekuwa na maneno ya kashfa na hata kukuuliza wewe na yeye mwanaume ni nani? hii inaonyesha ni kiasi gani anahofia kupoteza "Uanaume wake".

Nini cha kufanya: Tangu umechoshwa na tabia ya huyo Mpenzi wako ningependa uondoe hofu ya kutengeneza CV ya wanaume kwani ukijipa muda wa kutosha wa kupumzika kutoka kwenye uhusiano wa muda mrefu na huyu Kijana wa sasa ni wazi utakutana na kijana mwingine na mkapendana nakuishi vizuri tu kama wapenzi na hatimae mkafunga ndoa.

Uoga mwingine ulionao ni "ugeni" wa kuwa single tena baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, hujui namnagani ya kujichanganya na hata nini cha kujibu ikiwa mtu atakutokea n.k., lakini ukijipa muda wa kutosha hakika utakuwa ok na utafurahia maisha yako wewe kama wewe.

Bado binti mdogo, unajitegemea kiuchumi na unajua nini mapenzi (umeonyesha wazi kwa kuishi na mtu mmoja kwa muda wa miaka sita na kuvumilia yasiyovumilika).....you can do better than that baby Girl.

Kila la kheri.

Monday, 3 May 2010

Akichomoa kubadili mtindo kitu hakiingii tena-Ushauri

"Habari dada dinah pole sana na majukumu ya kila siku ya kuwaelimisha wanajamii!! Mimi ni mfatiliaji mzuri wa hii blog yako na nimeelimika na masuala mengi ya kimapenzi kwa kweli nashukuru.

Dada dinah, mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22 nina mpenzi wangu na ana malengo ya kuja nyumbani hivi karibuni. Nimekuwa na uhusiano nae yapata mwaka mmoja na nusu sasa ila tatizo langu linakuja pindi tukianza kufanya mapenzi tukifika katikati huwa naumia sana na raha ya mapenzi siipati tena lakini navumilia na kuendelea tu kufanya kumfurahisha.

Huwa namwambia ukweli kuwa naumia na yeye anajitahidi sana kunichezea na kulainika sana akianza kuingiza mboo na kubadilisha style tu napata maumivu yanayosababisha mchubuko na kufanya nikose hamu ya kufanya mapenzi tena.

Akitaka mzunguuko wa pili huwa nakataa kuofia maumivu maana hata nikienda kukojoa huwa kama nimechanjwa na viwembe, yeye ana uume wa kawaida na weza kuumudu ni mkubwa lakini anajua kuutumia wakati mwingine huwa anafika mbali sana. Nikimwambia anajitahidi kuelewa tatizo langu na kufanya taratibu.


Wakati mwingine nakuwa na hamu sana ila nikiwaza tu maumivu nakosa amani kwani naishia bao la kwanza maana najua la pili kulitafuta ni kazi sasa ndio hapo kazi inapoanza, sijui nifanyeje naomba ushauri dada yangu mana anataka kunioa.

Najua tukifunga ndoa atataka kila siku nitamudu vipi na mimi ndio hivyo tena salama yangu bao moja tu la pili nikifika kati tu hakuna ute wote unakauka tunaanza upya yaani akisema atoe nje kidogo tu tubadili style kosa anaingia kwa tabu upya!
ahsante dada naimani utanisaidia"

Dinah anasema: Shukrani sana kwa ushirikiano wako, nadhani tatizo hapo ni kutokuwa tayari vya kutosha kabla ya tendo na kutoshirikishwa wakati wa tendo linaendelea. Pamoja na kuwa mpenzi wako anakuandaa na pengine kunyevuka (kulowa) haina maanakuwa uko tayari kupokea Uume. Mpenzi wako na wewe mwenyewe kwa pamoja mnatakiwa kuendelea kuchezeana kwa muda mrefu zaidi na kisha yeye mpenzi wako kutumia kidole iki kuichangamsha misuli ya uke kujiachia tayari kwa kitu kibwa zaidi ya kidole. Pia inawezekana wewe una uwezo mdogo wa kungonoka...hilo moja.

Pili, wakati mnaendelea kungonoka mpenzi wako anatakiwa kusubiri mpaka wewe utakapofika kileleni ndio abadili mikao yake, kufika kwako kileleni kutaongeza unyevu na hivyo kuepusha ukavu utakao sababisha mikwaruzo na maumivu.

Vilevile anapotaka kubadili mkao mwambie hatakiwi kutoa uume nje, anatakiwa kukugeuza uume ukiwa ndani.

Tatu, unaweza kubadili mtiririko wenu wa kungonoka kwa maana kuwa mnaaza na mikao anayoipenda yeye na kumalizia ile inaokufanya wewe uwe Comfy.....Mf. yeye anapenda sana "mbuzi kagoma" ambayo mara zote husababisha ukavu.....anzeni na hiyo kisha malizia "wewe juu".....n.k.

Nne, hakikisha mnakuwa na vilainishio/vilainisho karibu....kama vile KY jel, kamwe usitumie aina yeyote ya mafuta kwani huganda ukeni na hivyo kusababisha maamubiko.

Kila la kheri!

Saturday, 1 May 2010

Najua simridhishi nifanye nini ili aridhike-Ushauri

"Pole kwa usumbufu wa kutuelimisha wadau wako,
mimi nina girlfriend wangu yapata mwaka mmoja lakini cha ajabu katika tendo la sex
inavyo onekana simridhishi kisawa sawa maana yake nikimuuliza anakaa kimya tu, je nifanyeje ili nimridhishe asije akanikimbia akaenda kwa mwingine kwani bado na mpenda sana na Mungu akijalia katika malengo yangu awe my wife.


Swali jingine ni hivi, je nikitaka nichelewe kukojoa or wenyewe wanaita kupiga bao. Nifanye kitu gani kwani nikikutana na girlfriend wangu nusu saa haifiki nisha kojoa na nikikojoa basi hamu inaisha mpaka yapite masaa 2 ndio hisia za kufanya mapenzi zinarudi tena.

Naomba nisaidie ushauri wako, kazi njema kila la kheri anae kuchukia wewe na atengwe na wanaBlog woooote!
Ni mimi Salim"

Dinah anasema: Kutokana na kuwahi kwako kukojoa chini ya Nusu saa ndio linakufanya ujishtulie kuwa humridhishi, sio? Ikiwa mpenzi wako anakojoa ndani ya Nusu saa au saa nzima ni wazi hatokuwa na jibu la kukupa ikiwa umemaliza ndani ya Dakika chache.....ataamini kuwa unajua kuwa hajaridhika na hivyo wewe kama mwanaume utafute mbinu nyingine ya kumridhisha.

Mwanamke anafikia kileleni ndani ya dk10 mpaka dk45....inategemea ni kilele cha wapi (juu au ndani), hivyo ni vema Salim kama utakuwa mbunifu zaidi na hivyo kumpa utamu mpenzi wako kabla hujamuingilia....nikiwa na maana tumia kidole, midomo na ulimi wako ili mpenzi wako afike kabla yako na mara tu akiishafika muingilie ukeni na fanya mambo.

Kutokana na utamu utakaokuwa ukiendelea Kisimini utamfanya afurahie zaidi uwepo wako kule ndani ya uke wako na hakika atakupa tabasamu mwanana la "nakupenda mpenzi".

Kuhusu kuchelewa kukojoa tafadhali tembelea Topic yangu ya mwaka 2007 inayokwenda kwa jina la "kupizi haraka a.k.a one minute man" soma Comments kwani kipindi kile nilikuwa najibu kama Comment.

Kila la kheri!