Friday, 30 April 2010

Ndoa inamwaka mmoja mume wangu tayari katoka nje mara 3-Ushauri

"Habari za kazi Dada Dinah,
pole na majukumu ya kutushauri na kutuelimisha sisi tusiokuwa na watu wa kuongea nao. Mimi ni mdada wa miaka 28 nimeolewa na ndoa yangu ina mwaka 1. Nilianza kuishi na huyu mume wangu kabla ya kufunga ndoa ila kwa wakati huo tayari alikuwa ameshajitambulisha na mipango ya mahari na ndoa ilikuwa inaendelea.


Dada hii siku sitaisahahu maishani mwangu, ilikuwa wiki 2 kabla ya mahari nilipogundua mume wangu anatembea na housegirl wetu ambae alikua akitusaidia kazi ndogo ndogo pale tunapokwenda kazini.

Iliniuma sana nilipombana msichana akaniambia ukweli wote na kuniomba msamaha. Nilimsamehe ila nikamwambia aondoke ili inisaidie kusahau machungu na kuniwezesha kuendelea na mipango ya kufunga ndoa.

Nilitamani kusitisha mipango yote lakini ningewezaje kuiambia familia yangu ambao tayari walikuwa busy na maandalizi ya mahari na vikao vya harusi? tuliongea na mume wangu na akaniomba msamaha nikamsamehe nikijua atajirekebisha na kama ni ujana labda ataacha tukishaoana.

Tulifunga ndoa salama na maisha yakaendelea kama kawaida bila tatizo. Baada ya miezi 6 nikagundua mume wangu ana mwanamke mwingine this time sio yule house girl tena ila alikuwa ni binti umri wa mdogo wangu wa mwisho ambaye amezaliwa 1988!! Sikuona haja ya kugombana na mtoto mdogo kama huyu ila nilimpigia simu nikaongea nae friendly tu nikijifanya kama ni dada wa bwana wake (mume wangu).

Baada ya kujua kila kitu ndio nikamwambi yule binti kwamba HUYO BWANA WAKE NI MUME WANGU WA NDOA. Yule msichana alishtuka na kuniomba tuonane ili ahakikishe, kweli nilikwenda hadi kwao na picha za harusi ndio binti na mama yake wakaamini.

Akaniomba msamaha kwamba yeye hakujua kwa sababu huyo mwanaume alimwambia yeye ni bachelor na pia hakumtajia jina la ukweli na alikua akivua Pete kila wanapoonana. Baada ya wiki moja mume wangu aligundua nimeonana na mwanamke wake na aliponiuliza sikumficha nilimueleza ukweli na nilivosikitishwa na hiyo tabia.

Kwa mara nyingine aliniomba msamaha kama kawaida yetu wanawake, nilimsamehe ili kuiokoa ndoa yetu changa. Maisha yakaendelea ila haikupita hata miezi 3 nikaona mwenzangu amebadilika tabia, kuyachunguza zaidi nikagundua kwamba bado wanaendelea na yule msichana na worse enough ameanzisha mahusiano mengine na ex-girlfriend wa rafiki yake.

Dada hapo ndio nimezidi kuchanganyikiwa naiona ndoa chungu! Sikuishia hapo nikaamua kuongea nae kwamba tabia anayofanya sijaipenda this time alikuwa mkali na kusema kwamba nisimuingilie kwenye life style yake kwasababu kila kitu amenipa na mimi ndio mke wake hao vimada niwaache kama walivyo.

Dada ni kweli huyu mwanaume amenipa kila kitu hadi gari la kifahari ameninunulia na pesa za matumizi sio tatizo kwake yaani nakula ninachotaka navaa ninachotaka lakini tatizo langu kubwa sio pesa wala chakula na wala sio wivu kama wengi watavodhania bali sina uhakika kama huyu mwanaume ananipenda kweli au la??

Pia mwenzangu haogopi magonjwa na kila nikijaribu kuongea nae kuhusu magonjwa hanielewi, je nifanyeje?? naogopa kupeleka hili swala kwa wazazi nahisi kama ni mapema mno kuanza vikao vya mashitaka ukizingatia ndio kwanza tuna mwaka mmoja na bado nampenda mume wangu ila simuamini tena.

nisaidieni nifanye nini?

ni mimi dada B wa DSM.

Dinah anasema: Asante sana Dada B kwa ushirikiano wako, kwenye maelezo yako hakuna mahali umezungumzia kumpenda huyo mumeo au yeye kukupenda kitu ambacho kinanifanya nihisi kuwa ninyi wote wawili mmefunga ndoa kwa sababu nyingine tofauti na mapenzi. Vilevile umegusia kuwa mumeo anakujali nakukupa kila kitu lakini hujasema kama anakuridhisha kimapenzi na wewe unamridhisha kimapenzi!

Ninachokiona hapa ni kuwa wewe na huyo mumeo mwenye tabia chafu mlimfunga ndoa kwasababu za "kijamii zaidi" na sio mapenzi. Ikiwa kweli kulikuwa na hisia za kimapenzi sidhani kama ungekubali kuendelea na mipango ya ndoa mara tu baada ya kugundua jamaa anatoka na mwanamke mwingine.

Katika hali halisi ulitakiwa kusitisha mipango ili kujipa muda wewe na uhusiano wenu, ili kuona kama mumeo atabadilika baada ya kuomba msamaha. Lisingekuwa tatizo kuwaeleza wazazi wenu tatizo lililojotokeza na huenda some how ingesaidia mumeo kuendelea na tabia yake chafu ya "kugawa umasikini" nje ya ndoa yenu. Lakini inaonyesha wewe uliitaka sana ndoa kuliko usalama wa maisha yako (kupata maambukizo ya VVU).

Mumeo amerudia kosa, tena sasa kalirudia na wanawake wawili tofauti kwa wakati mmoja.....hakika huyu Jamaa ama hana mapenzi na wewe au anakupenda lakini humridhishi kingono.

Badala ya kupoteza muda na kufuatilia wanawake hao na kuwahakikishia kuwa wewe ndio mke wa jamaa na vilevile kumwambia mumeo tabia yake huipendi, ungemuweka chini na kumuuliza "mume wangu ni kitu gani hasa unakosa kwangu, kitu gani kinakufanya uwe na wanawake nje?"....kupata ukweli wa kitu gani anakitafuta huko nje ndio ingekuwa njia rahisi ya kuokoa au kuimaliza ndoa yenu.

Nini cha kufanya: Mwaka mmoja wa ndoa ukijumlisha na muda wote mliokuwa pamoja kabla ya ndoa inatengeneza miaka fulani tangu mmekuwa pamoja kama wapenzi. Wewe kama mwanamke, mpenzi na mke umejitahidi kuongea na mumeo lakini inaonyesha ama hapati ujumbe au anaupata lakini kwa vile akitakacho huna au hakipati kutoka kwako, anashindwa kujizuia kwenda kukitafuta huko nje.

Huu ni muda muafaka wa kuliwakilisha tatizo hili kwa Wazazi wake, tena bila kutuma wawakilishi. Lipeleke wewe mwenyewe ukiwa na mumeo na hakikisha unaweka wazi yote yalioujaza moyo wako kwa heshima na kistaarabu lakini uwe firm ili wajue kabisa kuwa ndoa hiyo ni muhimu kwako kwa vile unampenda sana mume lakini kama mume hatobadilika basi uko radhi kutoa Talaka (Sasa hivi Tanznaia mwanamke anaweza kumtaliki mwanaume Kisheria sio kidini).

Kumbuka wewe bado Binti mdogo sana, ndoa mwaka mmoja tu hivi sasa ukijazaa watoto na kuwa humo ndoani kwa miaka 15 itakuaje? pengine hotofikia huko kwani utakuwa umeshapewa VVU.

Kama wazazi wake watasaidia na Mumeo kuomba msamaha na kuahidi kubadilika then utapaswa kusimama Imara kama mwanamke...haya mambo ya "ananipa kika kitu" haya ndio hutumaliza tukiamini kuwa tunapendwa, mtu akikupenda atajali afya yako, hisia zako nakwamwe hatoziumiza, atakuthamini na kukuheshimu....hata siku moja hatokwenda kungonoka na watu wengine bali wewe pekee anaekupenda.

Jua haki na majukumu yako kama mke na mwanamke kwenye ndoa yenu, hakikisha unamkumbusha mumeo kwa vitendo majukumu yake kama mwanaume na mume kwenye ndoa hiyo, kumbuka wanaume ni kama watoto wakati wmingine wanahitaji kuongozwa/kuelekezwa.

Wekeaneni rules na kuanzia siku hiyo mtakayoamua kuendelea na ndoa yenu ni vema kuelewana nakuwa na uhusiani/ndoa iliyo wazi zaidi na kushirikaina kwa kila jambo, usimpe uhuru na muamini lakini usijisahau! Kama hakieleweki yaani akirudia tena tabia yake hata baada ya wewe kumpa ngono ya kutosha na kumchosha.....basi mdada anza mbele!
Kila la kheri!

Thursday, 29 April 2010

Nini jukumu letu kwenye ndoa?, hebu tuwekane sawa!

"Dinah pole na shughuli hizi za kutuelimisha, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Inaonekana ndoa nyingi zina matatizo ya ajabu na sasa Dinah inabidi utoe mada mpya zinazowafanya wanandoa wajue majukumu yao, huenda mwanaume unakuwa hujui kwa nini umeoa tuelekezane hapa tujue majukumu yako na familia yako.

Mke ajue kwa nini ameolewa na amsaidie mume wake kwa kiasi gani maana inaonekana wanawake wakisaidia sana nayo ni tabu pia sasa tuishije katika ndoa zetu ili kupunguza haya matatizo?

Tuongeaje na wapenzi wetu ili tusigongane? pia imeonekana kuwa wanaume wa sasa wana tabia za kununa na hapo inakuwaje? zimekuwapo kasumba kuwa wanawake wakiwa na uwezo kiuchumi ni shida ktk familia lakini mjue kuwa wanawake wengi sasa wana kazi nzuri au sawa na wanaume je tusiwaoe?

Hebu tupeni na uzoefu nyie wanaume wenye wanawake wanaowasaidia sana hapo nyumbani muwe wawazi bila kuweka ile ya uanaume au kuona aibu. Mimi kwa kifupi nimeona wanawake wengi wakiwa msaada mkubwa kwa familia ikiwa baba ana upendo na anamjali mkewe na akiwa mwaminifu hapo matatizo hayapo.

Mie nayashangaa haya matatizo ya ndoa kila siku humu mpaka naona kama ni shida kuoa, nioe mwanamke wa aina gani du!"

Dinah anasema: Shukrani sana kwa kuwakilisha hili suala, hakika hali iliyopo hivi sasa inakatisha tamaa sana. Ndoa zimekuwa zikifungwa kwa kasi ya ajabu na zinavunjika haraka kuliko ilivyokuwa miaka ile ya bibi na babu zetu, mama na baba zetu. Watu wengi wamepoteza imani na baadhi hawaheshimu wala kuthamini ndoa.

Matatizo yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika yanatofautiana kwa kiasi kikubwa(nitaelezea jinsi ninavyoenda mbele), vilevile sababu zilizowafanya hao wanandoa kufunga ndoa pia zinatofautiana(nitaelezea jinsi ninayoendelea).

Sababu kuu ya kufunga ndoa ni mapenzi, japokuwa enzi za babu na bibi zetu hali ilikukuwa tofauti kutokana na mtindo wa maisha wakati ule na vilevile mfumo dume, wanawake na wanaume wengi walifunga ndoa bila mapenzi, yaani mapenzi hayakuwa sababu ya wao kutaka kushi pamoja bali Familia zao, umri, kuepuka aibu, kufaidika kiuchumi kutoka familia tajiri, ndoa n.k.

Ndoa hizo zilidumu kwa muda mrefu kwa sababu ya watoto, kuepuka aibu, kuachika ni kama kufukuzwa kazi kwavile enzi zile ndoa ilikuwa kama sehemu ya ajira, kwamba mwanamke kuolewa ni mwisho wa matatizo. Sasa ukiachwa ni wazi kuwa familia "watakufa njaa" na wewe hutoolewa tena kwani jamii ilikuwa inaamini kuoa mwanamke alieachwa ni mkosi.


Kutokana na maisha tunayoishi sasa wengi tunapata nafasi ya kupendana kwanza kabla ya kufunga ndoa, lakini baadhi hufunga ndoa kwa sababu zilizowafanya bibi na babu zetu kufunga ndoa which kwa maisha ya sasa ni sawa na kujipa kifungo/mateso ya maisha kwani ni ngumu sana kuishi na mtu usiempenda maisha yako yote.

Nitakuja kumalizia hili midaz........

Wednesday, 28 April 2010

Unene wa Mikono unanikosesha raha...nitaipunguzaje?

"Habari dada dinah pole na kazi ngumu uliyo nayo ya kuielimisha jamii. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mada zako ila sijawahi kuleta swali leo nimena na mimi nijitokeze kwa swali ili nipate msaada.

Nilikuwa sijajua tatizo langu nilipeleke wapi, nilisoma mada ya mazoezi na nikaona tu tangazo la jinsi ya kupunguza mikono minene kwa wanawake lakini sikuona maelezo ya kutosha ya nini hasa mtu anatakiwa kufanya.

Nilijitahidi sana lakini sikuona, naomba msaada wako wa maelekezo ya kufanya hayo mazoezi ya kupunguza unene wa mikono, kwani ni tatizo linanikosesha raha na ninashindwa hata kuvaa nguo za mikonoo mifupi au wazi kutokana na unene wa mikono yangu.

Mimi bado ni mdogo naomba msaada wako dada dinah, nategemea majibu yatakayo nipa furaha na nakuomba samahani kwa usumbufu."

Dinah anasema: Habari ni njema tu mdogo wangu, hujambo wewe? Asante kwa mail yako, sasa unaposema wewe bado mdogo unamaanisha ni chini ya miaka 21? Ni kweli kuna mazoezi ya kupunguza unene wa mikono kama unene wa mikono hiyo umesababishwa na unene wa sehemu nyingine ya mwili wako.

Mf kama sehemu nyingine ya mwili wako ni nyembamba lakini mikono pekee ndio minene basi utambue kuwa hili ndio umbile lako lakini kama sehemu ningine za mwili wako ni nene kama vile mapaja, kifua, kiuno, makalio n.k. ni wazi kuwa unene wa mikono utapungua ikiwa sehemu nyingine za mwili wako zitapungua yaani mwili wako ukipungua basi na mikono nayo itapumngua kwani ni sehemu ya mwili wako.

Inawezekana kabisa kuwa umeridhika na unene wa sehemu nyingine za mwili wako isipokuwa mikono....kumbuka huwezi kupewa/pata vyote hivyo kama unapenda maeneo mengine yabaki kama yalivyo itakubidi ukubali unene wa mikono yako na kuipenda kama ilivyo.

Kama asili yako (umbile lako) ni juu mkubwa ni wazi mikono yako itakuwa mikubwa tu, lakini bado unaweza kuifanya ipendeze nakuvutia na ukubwa wake sio unene tena kwani ukifanya mazoezi ya kupunguza unene/mafuta ukubwa wa mikono yako utakuwa umejengwa na misuli zaidi ya mafuta.....hivyo basi miko yako itakuwa firm na kujirudi kiasi nahivyo wewe unaona kuwa imepungua.

Ukiniambia umri wako then nitakuelekeza namna ya kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya mikono yako ili kuepuka ukomavu, mana'ke ukifanya mazoezi haya wakati bado mwili wako unabadilika (chini ya miaka 21) ni wazi yatakufanya uonekane mkomavu.

Nasubiri jibu kutoka kwako...
Asante.

Tuesday, 27 April 2010

Mpenzi nampenda lakini vijimambo vyake mmh-Ushauri

"Mambo Dinah, mimi ni mpenzi mkubwa wa hii blog yako, kwa mara ya kwanza nimeamua kukuandikia ili na mie nipate ushauri. Mimi ni mwanamke wa miaka 27 nina mpenzi wangu ambae tumekua pamoja kwa muda miezi 10 sasa.

Bado tunazidi kujuana si unajua tena! huyu jamaa yuko tayari kuwa na mimi na baadae tumeamua kama penzi letu litakua mswano tutafunga ndoa na yuko tayari kwahilo ila tunataka kujuana zaidi. sasa kuna baadhi ya vijimambo mie sivifagilii kwa kweli kuhusu huyu jamaa na vitu vyenyewe ni kua anatabia ya kuchukulia vitu vidogo vidogo kuwa vikubwa that stresses me alot.

Tulikaa chini nikimwambia kuhusu hilo tatizo lakini anasema "mimi niko the same tangu mwanzo tulipokutaka ni wewe umebadilika" yaani mimi ndio mwenye matatizo kitu ambacho sikubaliani nacho lakini najaribu kustahimili .

Wakati mwingine nafikiria kuwa its too much hatujaona sasa akiamua kunioa mambo yatakuwa haya haya sasa sijui nifanyaje? nahisi labda nimbwage but naona ninampenda na yeye anasema amenifia na kweli ananionesha kama ananipenda ila pia nahisi bado nataka more and more naona kama haitoshi jinsi anavyonipenda.

So hapo ni mimi nina matatizo au inakuaje? please naombeni ushauri nimechanganyikiwa.
Mimi Waridi lisilo miba."

Dinah anasema: Mambo poua tu, vipi wewe Waridi? Mapenzi ni kitu cha ajabu sana sio tu kwavile hujui lini utamdondokea mtu kimapenzi pia hujui wapi wala nani hasa utapendana nae na je huyo utakaempenda atakuwa na kasoro/tabia gani? Kama tungekuwa tunajua ni wazi watu wengi tusingekuwa kwenye mahusiano achilia mbali ndoa.

Unapokutana na pea/wenza wanaopendana sana kwa kuwaangalia tu unajua hawa watu wanapendana kweli kweli lakini kama ungejua wanayokumbana nao huko ndani kutokana na tofauti zao (ndio tunaziita kasoro) unaweza ukashangaa. Mapenzi sio mteremko, kwamba umependa na yeye kakupenda basi utapenda kila kitu.....hapana, kuna vitu huwa tunajitolea mhanga na kuamua kuishi navyo....unadharau au unachukulia kawaida.


Hujasema kwa uwazi au hata kutoa mifano miwili ya vitu hivyo "vidogo vidogo" ambavyo yeye anachukulia kama vikubwa, je ni wewe kutumia muda wako mwingi na "marafiki" wa kiume? Kuchat/pigiwa simu mara kwa mara na wanaume/wanawake asiowajua, kwenda baa na mashoga sijui shosti bila yeye? masuala ya kingono? kutumia vibaya pesa anazokupa? wewe kumuomba senti mara kwa mara? Ulevi? kutokusafisha nyumba/chumba chako (Uchafu labda)?n.k.....hivi vyote nilivyotaja ni vikubwa kwa mwanaume yeyote anaekupenda?


Kitu kizuri ulichokifanya hapo ni kuwa wazi na kuwakilisha hoja yako kwake japokuwa yeye kakataa, kwasabau yeye ndio mwenye tatizo haoni kuwa ni tatizo isipokuwa wewe mtu wa pili. Lakini tatizo lake linaweza kuwa limesababishwa na tatizo lako yaani kw akifupi tofauti zenu kama watu sio wapenzi mwanamke na mwanaume.

Kwavile wewe unadharau vitu au mambo fulani kwa kudhani ni madogo kwake yeye ni vikubwa. Kumbuka ninyi ni wati wawili tofauti sio tu kijinsia, kimalezi, uwezo wa kufikiri, uelewa, mazingira mliyokulia n.k......sasa hapa unatakiwa kujifunza na kugundua ni vitu gani hasa ambavyo wewe kwako ni vya kudharau lakini kwake ni vikubwa? na kuvichukulia anavyovichukulia yeye au hata kuepuka kuvifanya.

Kutokana na maelezo yako ni kweli mnapendana na sababu uliyoitoa sio muhimu ya kukufanya wewe uachane na huyo Mpenzi, kama unafikiria kumuacha mtu kwa vile tu mnapishana kidogo kutokana na tofauti zenu kama individuals.....je ukimkuta kakunja mwanamke mwingine utafanya nini?

Kumbuka moja kati ya nguzo muhimu za kuimarisha mahusiano ya kimapenzi ni kuelewana, ukimuelewa mpenzi wako na kujitahidi kuepuka kufanya vitu vidogo kwako lakini kwake ni vikubwa, hakika mtaendesha maisha mazuri yenye amani.

Lazima kuna kitu au vitu ambavyo havipendi na vinamuudhi lakini kwa vile anakupenda anavifumbia macho, so why dont you do the same? Umuhimu wa uhusiano kabla ya ndoa (ni kinyume na maadili ya Imani zetu za Dini though) ni kuwa unapata nafasi ya kujifunza kuhusu mwenzio kila siku na hivyo kujipa nafasi ya kuyazungumzia na kuelewana ili kuandaa maisha yenu ya baade kama mke na mume.

Kila la kheri!

Monday, 26 April 2010

Mchumba ni mvivu au mapozi tu? ananikwaza-ushauri

"Pole na kazi, mimi nina mchumba wangu na nilishamwambia kua nataka kumuoa na tukakubaliana. Ukweli nampenda ila anatatizo moja ambalo mimi naona ni kubwa sana.

Yeye hawezi kuja kwangu mpaka mimi nimfuate nikamchukue na hata anapokuja kwa zaidi ya mambo mambo ya kitandani hakuna kitu kingine anachotaka kufanya, anaweza kukaa kwangu siku tatu hata chumbani hafanyi usafi mpaka msichana wa kazi afanye. Siku nyingine tukimaliza kufanya mapenzi tunalala nakesho yake akiamka ni kuoga na kuondoka, yaani hata kutandika kitanda hatandiki.

Sasa hapa sijamuoa anashidwa kuonyesha hata kaunafiki kadogo, tukiona si itakua balaa jamani! naombeni minishauri maaana hata wakati mwingine akikuta nguo zangu chafu nikimwambia anisaidie kufua anasema yeye kufua hapendi.

Sasa sijui atakua mke wa aina gani au mimi ndio nitakua nafua na kumfanyia usafi maana hata kuosha mwiko kwake ni kazi, ukimuuliza anasema mimi ndio nifanye hivyo kwa kweli ananikwaza naomba ushauri kabla sijaamua kumwacha dada dinah,
best rgds"

Dinah anasema:Asante sana kwa ushirikiano, unaposema mchumba wako unamaanisha kuwa umejitambulisha kwao na kumaliza taratibu zote zinazotakiwa, au ni "mchumba" kwa vile umemwambia utamuoa na yeye akakubali?

Kama unajulikana kwao na yeye anajulikana kwenu ni vema ukalipeleka hili suala kwa watu wa karibu na yeye kama vile Dada zake, Shangazi au Dada/wadogo zako ambao unajua kabisa wanajua wajibu wao kama wanawake wa Kitanzania....well mwanamke yeyote Duniani kwani hata Ulaya mwanamke asipojua majukumu yake hakika anasumbua unless otherwise unamahela ya kuajiri mtu ambae at the end anakuwa mke mwenzio.

Kabla hatujaenda mbali sana, kama ulikuwa na mpango wa kuoa mwakani basi ongeza miaka mingine wiwili vinginevyo utaoa mzigo.

Huyo Binti ni mmoja kati ya wale Masista duu ambao wanadhani kutokujua kufanya shughuli za nyumbani kama hizo ulizozitaja ni "uzungu" au "usasa" lakini ktk hali halisi ni ujinga, uzembe na aibu kubwa kwa wanawake wengi.

Inawezekana hali hiyo ni kutokana na malezi, kwani kuna baadhi ya wazazi wanaweka wasaidizi wa k azi tangu watoto ni wadogo mpaka wanakuwa wanawake, nakumbuka sisi tulipokuwa na wasaidizi nyumbani kwetu walikuwa wanajishughulisha zaidi na watoto (wadogo zangu) lakini kazi nyingine tulikuwa tunafanya wote na actually tulikuwa tunafanya zaidi kuliko wale mabinti ambao walikuwa wanalipwa......nakumbuka siku moja nilidai kulipwa lakini nikaishia kufinywa katikati ya mapaja...lol! anyway....

Sisemi kuwa afanye kila kitu hapo ndani kwavile tu ni mwanamke bali mwanamke yeyote anatakiwa kuwa msafi sio wa mwili tu bali na mazingira yanayomzunguuka, mazingira anayotumia n.k. Kama mwanamke na "mchumba" hiyo ndio trial yenu ili kujuana nani mchafu, nani mvivu na kusaidiana, elekezana na kusaidiana ili iwasaidie baadae mtakapokuwa tayari kufunga ndoa.

Huwezi tu ukamuacha mpenzi unaempenda sana kwa sababu ya kasoro moja ambayo inarekebishika na wewe ni mtu pekee mwenye uwezo wa kufanikisha hilo kama kweli unataka kuwa na mke mwema hapo baadae. Kumbuka moja ya nguzo kuu za kuimarisha mahusiano ya kimapenzi ni kuelekezana/fundishana.

Nini cha kufanya: Haitokuwa vema kumtimua Binti msaidizi wa kazi hapo nyumbani kwani ni wazi unamsaidia kiuchumi kwa kumlipa kutokana na kazi anazokusaidia, lakini ni vema ukatengeneza utaratibu na ukaweka mipaka kwamba Msaidizi wako wa kazi anafanya kazi maeneo mengine ya nyumba lakini sio Chumbani.

Huko chumbani ni sehemu pekee ambayo hapaswi kugusa/safisha na hiyo sehemu itasafishwa na niyi wawili yaani wewe na "mchumba wako", sasa siku muibukie huko kwao kama kawaida ila sasa nenda mapema. Mtakapo fika nyumbani mpe kitu cheupe tu kuwa kuwa leo ni siku ya usafi na hivyo unaomba yeye akusaidie kuufanya huo usafi huko chumbani......atakuambia "kwanini usimwambie msaidizi wako" hapo sasa weka wazi kuwa umeamua kugawa majukumu kwani huyo msaidizi sio mpenzi wako na usingependa aingie chumbani kwenu kusafisha, tandika kitanda wala kufua mashuka tunayotumia.

Suala la yeye kukufulia nguo zako liwakilieshe hivi; ukienda kumchukua mwambie kama ananguo chafu aziweke kwenye gari na mkifika kwako kwa mapoja mfuliane....yeye kukufulia wewe ni mapema sana kwenye level ya uhusiano mlionayo hasa kama huyo Mchumba mwenyewe ni wale wadada wanaojiona ni wa hali ya juu, mdada wa mtaani/wa kawaida/uswahilini yaani yule alielelewa kwa maadili ya Kitanzania wala usingekuja hapa kuomba ushauri kwani tunakuwa tukifunzwa kila kitu kama wanawake.

Mapenzi ni kutoa na kupokea, sasa suala la wewe kumfuata yeye kwao mara kwa mara sio sahihi na wala sio mapenzi bali kutumikishana, ni vizuri kama na yeye mara moja moja atakuwa anakuja hapo kwako bila wewe kumfuata.

Siku nyingine akiomba umfuate, mwambie umechoka au unajisikia vibaya hivyo basi achukue basi au taxii na aje kwako moja kwa moja. Asipokuja na wewe mchunie......she needs to learn the hard way!

Siku zitapita napengine atakupigia simu uende ukamchukue kwao, hapa sasa mwambie wazi lakini kwa upole lakini a bit fir.... kuwa wakati mwinginme unahisi kama vile unajipendekeza au wewe ndio mwenye shida sana na penzi lake wakati yeye hana habari. Mwambie mapenzi ni 2 ways na sio one way.

Vilevile ni give and take sio take-take-take ongeza mapenzi ni sisi/sote na sio mie/mimi......kwa sababuni Duu ataleka kaubishi na maringo fulani hivi.....hapo muulize "hivi mpenzi ni nini hasa napata kutoka kwako zaidi ya ngono??!!......sioni mapenzi kabisa kutoka kwako, je unauhakika kweli unataka kuwa na mimi au unanipotezea muda tu?

Ninakuhakikishia maelezo hayo yatambadilisha na asipobadilika ujue anakutumia kwa vile tu unaishi mahali pazuri, unachoma mafuta ya gari kila siku kwa ajili yake na hakuna haja ya kusaidia kazi kwani unamsaidizi.

Kila la kheri!

Sunday, 25 April 2010

Ushuhuda!!

"Habari Dinah,
Mimi ni yule mwanamke niliyetuma ujumbe kuhusu msg tata niliyotumiwa na mwanamke kuhusu mume wangu na namna mume wangu alivyomisbihave. Nashukuru Mungu kwani ile siku nilichanganyikiwa sana lakini zifuatazo ni step nilizopitia nataka na wanablog wengine wa D’HICIOUS wasome nao ikitokea wana shida kama mimi wafanyeje.Pia nashukuru wachangiaji wengi kwa comments zao nyingi zikielekeza vizuri . Mtarejea maelezo yangu ile siku, mchana nilimtumia msg mume wangu nikamwambia majibu aliyonijibu asubuhi na mwenendo wake ni dhahiri kuwa anamwanamke mwingine na nikamwambia kuwa kama hatajirekebisha na kutulia na familia yake Mungu wa mbinguni atakwenda kumpa adhabu hapa hapa duniani.Huwezi amini alituma msg ya kushuka na kuniomba kabla sijarudi home tukutane mahali tulivu tuongee. Akanambia kuwa yeye hana uhusiano na mwanamke mwingine isipokuwa anaomba msamaha kwa yale aliyosema akidai aliropoka kwa vile mie nilimfokea na kumwambia lazima kuna kitu anaficha.Anasema hakupenda ile tabia na ndio ikamuipress aseme vile, tukarekebisha tofauti zetu na amezidisha mapenzi zaidi ya yale ya mwanzo. Anawahi kurudi kama kawaida, muda mwingi tunazungumzia mipango ya maendeleo yetu.Namshukuru Mungu kwani nilikuwa nimeanza kufikiria kuondoka zangu maana maneno yale yalikuwa mazito.

Ushauri: Ndoa inahitaji uvumilivu, kuna mambo yanarekebishika, unaweza kuamua kudivorce kumbe ilitokea bahati mbaya. Tuvumilieni. Nawashukuru sana kwa mawazo yenu."

Thursday, 22 April 2010

"watu wanangonoana na baba zao sembuse mimi" Shemeji aniambia!-Ushauri!

"Dada Dinah pole na kazi. Nimeona nishee na wewe jambo moja linaloniumiza moyoni. Miaka kama minne hivi huko nyuma nilikuwa naelewana na kaka mmoja kama rafiki wa karibu tu, hatukuwa wapenzi.

Kwa kweli he was nice, good and heart caring guy, mimi na huyu kaka tulikuwa tunaelewana sana kiasi kwamba wakati mwingine tulikuwa tunatembeleana, kuwa na chakula cha pamoja hatakutoka mara moja moja.

Siku moja katika mazoea yetu hayo nilialikwa kwake nikakaa sana mpaka usiku tukakubaliana kuwa nilale hapo kwake. Nikalala naye kwenye kitanda kimoja tukikumbatiana na kubuasiana, lakini hakunitia kwasababu siku hiyo nilikuwa nipo kwenye siku zangu lakini kama isingekuwa hivyo sikuona kuzuizi kwanini nisifanye.

Nakumbuka kama tulichezeana mambo ya kushikana shikana na punyeto mpaka akakojoa.Baadaye kila mtu akaendelea na maisha yake. Huyo kaka akaondoka zake kwenda kusoma nje na mimi nikaenda kuongeza ujuzi.

Hatukuwa na mawasiliano yoyote! kwa kifupi tulisahau nini kilitokea kati yetu na kila mtu akachukulia kuwa ule usiku ulitokea tu (kama bahati mbaya) na hatukujuta wala hatukufikiria kuwa kuna siku tutahitaji kufanya kweli. Yaani naweza kusema ilikuwa kama tai kwenye suti.

Baada ya muda kupita nikawa nimepata mwanaume ambaye nampenda kimapenzi na tuna mipango ya kudumu,yaani tumeamua kuoana na tumefanya process zote za mahari, kutambulishana kwa wazazi na ndugu.

Kwenye zoezi hili la kutambulishana kwa ndugu ndipo nilipogundua kuwa yule kaka niliyelalanaye siku ile (alikuwa bado nje wakati huo) kuwa anaundugu na mchumba wangu. Kwa kweli nilitetemeka kwani mmoja ni mtoto wa baba mkubwa na mwingine baba mdogo.

Baadaye tukaongea kwenye simu (Mimi na yule kaka niliyelala naye kitanda kimoja) tukakubaliana kuwa tusimwambie kabisa mchumba wangu na tujifanye hatukuwahi kufahamiana kabla.

Na kweli nilijifanya simfahamu huyo ndugu yake, na yeye akiambiwa na nduguye juu ya mchumba wake yaani mimi alijifanya hanifahamu kabisa. Sasa balaa limenitokea hivi karibuni, mchumba wangu yupo Dar kikazi na mimi nipo Mwanza (naishi huku).

Huyo shemeji yangu kaja Mwanza kwani ana mchumba wake huko St. Augustine. Wakati anaondoka Dar ndugu yake kamsisitiza "hakikisha unamtembelea shemeji yako", na akanipigia na kunipa habari hiyo ua Ugeni wa mdogo wake kuwa “yule kaka yangu aliyekuwa shule anakuja huko,utakuwa muda muafaka wa wewe kumfahamu”.

Nilihofu sana lakini sikuwa na jibu la haraka nikasema na mkaribisha na nitafurahi kumfahamu. Basi bwana huyo shemeji yangu kafika, baada ya shughuli zake hapa mjini akaja kwangu ninakoishi.

Nikampokea vizuri kama desturi ya mwanamke wa kitanzania chakula na maongezi na uchangamfu. Akanilaumu kwanini naolewa na ndugu yake wakati tayari tulikaribiaku-do, nikajitetea sikujua ni ndugu yake.

Baadaye kulikuwa na program kwenye komputa nahitaji kuelekezwa, nikawanimekaa kwenye kiti na yeye ameinama kutoka nyuma yangu ananielekeza. Ghafla nikajikuta kama mwili unatetemeka, mate yananikauka mdomoni. Baadaye akashika mouse pamoja na mkono wangu, nikahisi msisimko na mwili ukawa unanitetemeka.

Akagundua hilo, akaniuliza kama naogopa,nikasema ‘hapana,’ akaniuliza “sasa nini?” nikasema “hakuna kitu”,baadaye akaleta mkono kifuani kama vile anapima mapigo ya moyo, moyo ulikuwa unanienda mbio wakati huo, akaniuliza “unataka’’? Kwa kweli sikuwa na uhakika kama namhitaji au laa!

Lakini kilichofuata ni kuwa nilijikuta navua nguo na shemeji akanitomba vizuri sana wote tukaridhika. Kama mwanzo wote tunahesabu ni bahati mbaya tu, halitatokea tena. Sasa shida yangu mpaka nakuja kwako ni hii.

Najua kuwa kitendo nilichofanyasio kizuri, najuta na ninajua nini cha kufanya, yaani natakiwa kuaacha mara moja uhusiano na huyu shemeji yangu. Lakini shida nitawezaje kujizuia isitokee tena?

Nahisi roho yangu inatamani penzi lake, nahisi na yeye anatamani kuendelea kula uroda na mimi? Kwani alinambia wala nisijutie kuna wanawake wengi hapa duniani wanatembea na shemeji zao kabisa wengine mpaka baba wakwe zao sembuse yeye shemeji wa mbali.

Naomba ushauri wako, baada ya Ndoa yetu nitahamia Dar ambapo shem ane anaishi baada ya kumaliza masomo yake, sijui itakuwaje masikini wa Mungu, nimechanganyikiwa na sielewi.

Ni msomaji wa blog yako.
Rhoda, Mwz"

Dinah anasema: Mpendwa Rhoda, kutokana na maelezo yako ni wazi huyo kijana ambae sasa umegundua kuwa ni "shemeji" alikuwa anahisia za kingono (alivutiwa na wewe kingono) na wewe tangu mwanzo ila tu hakupata nafasi ya kuweka wazi hisia hizo kwako.

Hakukupenda na wala hakuwa na mpango na wewe kama mpenzi wake na ndio maana alikubari haraka kuchukulia kuwa "hakuna kilichotokea" baada ya usiku ule uliompa Nyeto na alikata mawasiliano na wewe, kama angekuwa na nia njema au hata kukupenda tu ni wazi angeichukulia siku ile kama "special" na angebaki kwenye mawasiliano na wewe. Sio mpaka ukutanishwe na "mchumba" ndio mfufue mawasiliano.

Kosa kubwa ulilolifanya ni kumpa nafasi ya kuutumia mwili wako huyo "shemeji" asie kuwa na adabu, heshima wala utu, ni wanyama peke yao ambao wanatiana na watoto wao, kaka, shemeji n.k. kwasababu hawana "utu" ambao Mungu ametupendelea sisi wanadamu. Huyo "shemeji" hana tofauti na muuaji kabisa......kilichotokea ni kosa kubwa na aibu sio tu kwa Mchumba wako bali kwako pia, familia yako na kwa jamii nzima inayokuzunguuka.

Kichonisikitisha zaidi na kunifurahisha at the same time unauhakika kabisa kuwa hutoweza kujizuia kungonoana na huyo "shemeji" yako, sasa kama utafunga ndoa ni wazi utakuwa unangonolewa na ndungu katika hali halisi ni uchafu kuliko maana halisi ya neno hilo.

Mchumba wako afanya taratibu zote za uchumba na sasa ni maandalizi ya kufunga ndoa, kama ukweli ndio huo ambao wewe mwenyewe umekubali au niseme unadhani kuwa huwezi kujizuia ni vema basi ukasitisha shughuli za ndoa na jamaa akarudishiwa Mahari yake ili aweze kusonga mbele na maisha yake.....lakini kabla unatakiwa kuliweka wazi suala linalokufanya ukatae kuolewa na huyo Mchumba wako.

Wewe na huyo "shemeji" yako mkifanya siri ni wazi kuwa huyo Kaka mtu atabembeleza ili ukubali kuolewa nae, familia yako na yake watatafuta namna ya kuwapatanisha ili mfunge ndoa....lakini ukiweka wazi kuwa kinachokufa ukimbie ndoa na huyo Mchumba ni kwasababu unahisia na mdogo wake.

Kumbuka huyo "shemeji" yako hana mpango na wewe na ndio maana anajitahidi ku-justfy tabia yake chafu kuwa "kuna wanawake kibao wanalala hadi na baba zo ndio itakuwa Shemeji" ni wazi kuwa anataka kuendeleza uchafu na sio kwamba anataka uache kaka yake ili yeye achukue jumla, anataka kaka afunge ndoa na wewe ili yeye ajipatie vya chee!

Nini cha kufanya: Waambie wazi wanafamilia wa pande zote mbili kuwa wewe na Shemeji yako mlikuwa marafiki wa karibu na ulipochumbiwa hukujua kama huyu Mchumba anaundugu na Rafiki yako (mdogo wake) nahivyo mkaficha siri kwani mliwahi kukaribiana na kuonana mkiwa watupu.

Eleza kuwa alipokuja kukutembelea Mwanza kama shemeji yake hisia ziliwarudia ghafla na kusaliti wapenzi wenu na huyo Jamaa kusaliti Kaka yake na mchumba wake, hilo tukio limekufanya ugundue kuwa huna hisia kali kwa Mchumba wako kama ulizonazo kwa "rafiki" amabe sasa ni Shemeji yako.

Malizia kwa kuwaambia kuwa unauhakika kuwa hutoweza kujizuia kuwa karibu kimwili na "shemeji" yako hata kama utafunga ndoa......hii itawafanya familia yako na familia yake(mchumba wako) watambue kuwa hata kama watalazimisha au tafuta suluhisho ili ndoa iendelee bado haitakuwa na mafanikio.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa haukuwa tayari kufunga ndoa ulikuwa unakwenda kufunga ndoa kwa sababu ulidhani unahitaji kufanya hivyo lakini haukwa tayari kihisia. Hili ni moja kato ya makosa mengi yanayofanywa na watu wengi na hivyo ndoa zao kuwa na matatizo mengi na hatimae kuvunjika.

Baada ya kumaliza uchumba na jamaa, jitahidi kadri ya uwezo wako kuendelea na maisha yako wewe kama Rhoda, zingatia shughuli zako za kimaisha, kuwa karibu na familia yako na furahia maisha yako. Siku moja utakuwa tayari kwa ajili ya kuishi na mwanaume mmoja maisha yako yote.

Utampenda na atakuwa mwanaume pekee unaetaka kungonoana nae, hisia zako zitatulia juu yake nakwamwe hutoweza kushawishika wala kutamani mwanaume mwingine bali mpenzi wako. Wote kwa pamoja tujitahidi kurudhisha thamani ya Uchumba na Ndoa, hii kitu (ndoa) ni muhimu kwenye maisha yetu, maisha ya ndoa ni mazuri/raha ikiwa tu umefanya hivyo ukiwa tayari.

Kila la kheri.

Tuesday, 20 April 2010

Uongozi wa Dini umenaharibu, je niendelee kumsubiri?

"Hi Dinah!
Naitwa a.k.a Doctor nikiwa hapa Dar. Nina mpenzi ambae anasoma Chuo kimoja hapa nchini, mwanzoni tulipendana sana hadi ikafikia tukapanga tuoane atakapomaliza masomo yake mwaka 2012.

Lakini alipoanza tu Chuo 2009, wiki mbili zikapita akakata mawasiliano ghafla! Nimeonana naye tena mwezi uliopita baada ya kurudi kutoka Chuo na akasema anataka uhusiano wetu uishe kwani anataka kusoma na amechaguliwa kuwa kiongozi kwenye kikundi cha Dini.

Hivyo anahitaji muda mwingi wa kufanya shughuli hizo. Kwa kweli simwelewi kabisa huyu binti, maana siku nyingine ukimpigia simu ili kupanga mihadi ya kuonana anakuja vizuri tu, siku nyingine ukimpigia simu ananikatia.

Yaani simwelewi au nimpige chini kabisa, nitafute mrembo mwingine maana nahitaji binti wa kuishi naye ifikapo 2011 au 2012. Naomba maoni ya wadau. Nipo katikati ya bahari na sijui wapi pa kuanzia!!!!!!"

Dinah anasema: Doctor asante kwa ushirikiano wako, kuzungumzia na kukubaliana kuwa siku moja mtafung andoa sio tiketi ya mtu kubaki na wewe, kama kweli uko serious unatakiwa kuchumbia kwa vitendo (jitambulishe kwao nakufuata taratibu zote) nadhani huyu Binti ameamua kuzingatia masomo yake kwanza bila kuchanganya mapenzi na wakati huohuo kaamua kubadili mtindo wa maisha yake na kumtumikia Mungu ktk hali halisi ni jambo jema sana hasa ukilichukulia kwa upande mwingine.

Mf: Badili kabao wewe uwe kaka wa huyo binti, kwambatufanye ni mdogo, hivi angekuwa na mpenzi ambae wewe kama kaka unaona kabisa kuwa "jamaa" ataharibu maisha ya kimasomo ya mdogo wako hata kama atamuoa (which sio guarantee as hajachumbia kwenu)......alafu kwa bahati nzuri mdogo wako huyo wa kike kachaguliwa kwenda Chuoni na ghafla akaamua kuachana na "jamaa" ili azingatie masomo yake Chuoni.....ungejisikiaje kama kaka?!!


Kama nia yako ni kufungandoa mwakani au mwaka unaofuata haimfanyi huyo Binti kutaka kuolewa muda huo pia, lakini kama mlipokuwa pamoja na mkajadili suala la ndoa muda huo na alipojiunga na Chuo/Uongozi wa Dini akaomba uhusiano wenu ufe ni wazi kuwa Imani yake ya Dini kama zilivyo nyingine zote hasikubaliani na mahusiano ya kingono kabla ya Ndoa.

Mimi nadhani ni vema kuheshimu uamuzi wake na kumpa muda ili azingatie masomo yake(huenda atabadili mawazo), usijenge hasira/chuki na ikiwezekana endeleza urafiki na mawasiliano ya mara kwa mara mpaka utakapokutana na mwanamke ambae atakuwa tayari kuolewa na wewe kipindi ulichojipangia bila kuwa na majukumu ya Kimasomo wala Dini.

Kila la kheri.

Friday, 16 April 2010

Mapenzi pasipo yananipeleka pabaya-Ushauri

"Habari Dinah!!
pole na majukumu, mimi nina tatizo moja hata sijui nianzaje kukueleza? Nilikuwa na mpenzi nilimpenda sana kwa kweli aliyonitenda ni mengi siwezi eleza yote ila kwa kifupi alinitenda na niliumia sana mpaka nikakonda kama kijiti.

Nilikuwa sina la kufanya isipokuwa kuachana nae. Baada ya muda nikapata kaka mwingine ambaye nilianza nae mahusiano lakini sikumpenda kama yule wa mwanzo lakini niliamua kumkubali ili kujifariji tu kwa yaliyonikuta.


Lakini yeye alikuwa na mapenzi ya dhati kwangu akataka kuleta posa kwetu nilikubali lakini sikuwa na love nae, wakati kaleta posa huku watu wanaendelea kupanga mahali nikakutana na kijana mwingine ambae alionyesha kunipenda na mimi nikampenda sana tu. Tukanza mahusiano ya siri baadae nikamwambia ukweli kuwa mimi nimechumbiwa, akasema hakuna taabu kwani hata yeye ana mke.


Tuliendeleza mahusiano ya siri hadi baada ya mimi kufunga ndoa, nikashika mimba ya mume wangu wa ndoa na nikajifungua vizuri . Mtoto alivyofikisha miezi mitatu mimi na yule Kiajna wa nje tukaanza tena uhusiano.

Wakati wa ujauzito huyu Kijana aliwahi kuniomba tigo(tako) nikwambia subiri njifungue baada ya kujifungua akakumbushia nikakubali tulifanya kama mara 3 au 4 nilifanya kwa kuwa nampenda tu ila sikufuraha kabisa lile tendo.

Sasa namkatalia kuwa sitaki kuendelea tena na mchezo huo basi ananchukia yaani zinapita hata wiki 2 hapigi simu na akipiga anaulizia tigo tu, Mimi tigo sitaki tena nambembeleza tufanye kikawaida lakini namuona haridhiki anasex kama picha tu yani haoneshi kuridhika. Kwa kifupi mapenzi yamepungua na mimi bado nampenda kuliko ata mume wangu.

Nafikiria kumuacha lakini sina uhakika wa nini ch akufanya kwani yeye ni msaada mkubwa kwangu coz kipato cha mume wangu kiko chini namtegemea sana yeye kuliko mume wangu na anajua nampenda. Lakini kabadilika kwani zamani alikuwa anipigia simu mara 7 au sita now days zinapita ata wiki mbili na akipiga anaulizia sex.

Nifanyaje mapenzi yaamie kwa mume wangu yaani nimpende kama yeye?? Yote haya yamefanya nipoteze kazi ambayo nilikuwa nafanya kwenye kampuni ya mke wake hapa Arusha na ndio tulipokutana huyu bwana mkubwa alikuwa ananikuta pale ofisini kwa wife wake. Mkewe alipogundua uhusiano wetu alinifukuza kama mbwa na akaja kumwambia mume wangu yaani lilikuwa timbwili la asha ngedere.

Yeye akanambia nisijali ataniajiri kwake au atanipa hela ya mtaji lakini hanipi akinipa ni elfu 50 ambazo ni matumizi tu uwezi fanyia biashara yeyote. Sio kuwa hana hela anazo sana tu na nikimuuliza kuhusu hilo ananiambia "usijali nakumbuka mambo mengi tu ila swala lako nafanyia kazi "na muda ndio unazidi kwendaa ni mwaka sasa unakatika.

Nishaurini wapenzi nifanyaje????
Eve"

Dinah anasema: Eve mdada, ulikosea mwanzo kabisa kwa kuolewa na mtu ambae hukumpenda sasa kitu gani kilikufanya ukubali kuzaa nae huyo mumeo? Mpaka umeamua kuzaa nae ni wazi mlikuwa mnafanya mapenzi.

Mwanamke yeyote aliekamilika huwa ni ngumu sana kufanya ngono na mwanaume ambae hana hisia za kimapenzi hata kidogo unless otherwise ufanye hivyo ukiwa umelewa kidogo, lakini kama unaakili zako timamu ni ngumu sana kwa hiari yako kumvulia mwanaume na kumpa mwili wako wakati huna hisia kabisaaa.

Hilo ni kosa umelifanya na ni ngumu sana kwa mimi kama Dinah kukushauri namna ya kumpenda mumeo kama wewe mwenyewe unakili kuwa humpendi, lakini kama kunahisia fulani ambazo zinakufanya utakekumpa mwili wako nahatimae kuzaa nae then naweza kusaidia hapo.

Kosa kubwa kuliko yote ni kujiharibia kazi/maisha yako kwa kutoka na Mume wa boss wako.....jamani?!! ulikuwa unafikiria nini? Ndio kuchanganyikiwa, Hasira? au kukata tamaa?

Huyo Mume wa mtu mpenda Tigo anakutumia kimwili na wewe ulikuwa unamtumia kiuchumi. Unachotakiwa kufanya ni kujiheshimu, kuheshimu ndoa yako hata kama humpendi mumeo kisha jaribu kutafuta utaratibu wa kuomba talaka mapema ili uweze kumpa nafasi mumeo ya kusonga mbele na maisha yake ili na wewe uendelee na yako lakini sio na mume wa mtu.

Ninaamini kabisa unazo hisia juu ya huyo mumeo lakini hisia hizo hazina nguvu labda kwa vile ulikuwa nae kama "wakujipoozea tu" hukuweka mapenzi yako yote juu yake, au kwavile yeye mumeo kutokujua namna ya kuonyesha mapenzi ili umpende.

Mapenzi hayalazimishwi lakini kama kuna hisia kati yenu kwa pamoja mnaweza kuweka effort kwenye vitu vichache na hivyo hisia hivyo kuwa na nguvu na hatimae kundondokeana kimapenzi kila siku.

Inaonyesha unataka kuendelea kukaa kwenye ndoa na ndio maana umeomba ushauri wa namna gani utahamishia mapenzi kwa mumeo, ni jambo zuri lakini kurudisha mapenzi ambayo hayakuwepo ni ngumu.....ni kama vile unataka kufunzwa namna ya kupenda mtu kitu ambacho hakiwezekani kwasababu mapenzi ni hisia na mpaka hisia hizo ziwepo kati yenu basi penzi linaweza kuibuka.

Kitu cha kwanza kabisa ni wewe Eve kujipumzisha kwenye masuala ya kupenda/nani atanipenda/simpendi n.k. alafu badilisha tabia yako chafu ya kutoka nje ya ndoa na kuiba mume wa mtu mwingine.

Pili, zingatia mema na mzuri ya mume wako, maisha yenu kama familia na mshukuru Mungu kwa hilo, kama mke hakikisha unatumia muda wako mwingi kuwafanya mambo ya kizalishaji kama vile kujisoema, kujifunza mambo vitu vipya va kimaisha, kujifunza mbinu mpya za kuanzisha biashara n.k. badala ya kufikiria mapenzi na ngono (kwa sasa) wakati tunatafuta suluhisho, sawa mama!.

Tatu, jitahidi kutafuta kazi (ni mwiko na marufuku kwenda kuomba kazi kwa Mpenda Tigo wala mkewe) na hakikisha unajiweka busy na shughuli za kuboresha maisha yako ya ndoa na familia, kumbuka hivi sasa unajukumu la kuhakikisha kuwa mtoto wenu atakuwa na maisha mazuri na comfortable hapo baadae.

Nne, badili mtindo wa maisha yako (hasa mavazi na chupi)......hii itakurudishia hali ya kujiamini kama mwanamke na kufuta kumbukumbu za mpenda Tigo. Ongeza mawasiliano kwa mumeo, onyesha mapenzi ya vitendo kwa mumeo ili kuwa karibu zaidi nje ya kitanda. Kwa kufanya niliyogusia hapo juu (rejea hatua ya pili) itasaidia wewe kupata mambo vitu vya kuzungumzia unapokuwa na mumeo.

Vilevile itakuongezea uelewa zaidi na hivyo kufanya mambo tofauti na ulivyofanya awali na hivyo kutokurudia makosa na kuishi maisha yenye amani, upendo na furaha. Hili ni suala gumu sana na hatupaswi kulichukulia juu-juu, hali kadhalika yote niliyojaribu kukueleza hapa yatafanikiwa ikiwa tu utatilia maanani, utakuwa tayari kufanyia kazi na kujipa muda.

Kwavile wewe ndio mwenye kutaka ndoa yenu iendelee ni wazi kuwa unapaswa kuweka nguvu zako zote kuhakikisha hilo linafanikiwa, kumbuka kuwa jitihada zako zote utakazo ziweka hutakiwi kuharakisha mambo, upe muda uhusiano wenu uweze kukua, ipe muda ndoa yenu kuwa na nguvu, zipe muda hisia zetu kuwa na nguvu zaidi.

Pole sana kwa maneno makali kutokana na watu kushindwa kuzuia hasira zao, ukichukulia hasira zao kama challenge na ukatumia mawazo yao hasi (negatives) ili kufanya mambo chanya (positives) ni wazi utafanikiwa zaidi.

Kila la kheri!

Thursday, 15 April 2010

Nataka kuacha Mpenzi lakini naonea huruma watoto wangu-Ushauri

"Mambo vipi dada Dinah
Pole na kazi na hongera sana kwa kazi hii ya kutoa ushauri.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ninaishi na mwanamke ambaye ninae kwa miaka nane sasa na tumebahatika kupata watoto wawili mmoja wa kiume na mmoja wa kike.

Mwanzo wa maisha ki ukweli tulikuwa tunaishi vizuri tu lakini kadri miaka inavyozidi kwenda mambo yamekuwa yanabadilika na tatizo kubwa naweza sema limekuwa sugu, nasema hivyo sababu ni tatizo la muda mrefu na nimejaribu kuliongelea lakini naona hakuna mabadiliko yoyote na hakuna sababu za msingi anazotoa .

Dada Dinah huyu mwanamke swala la kunipa unyumba kiukweli limekuwa ugomvi yaani hataki na hatoi sababu za msingi kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Sasa nimechoka sana na nafikiria mambo mengi sana moja kubwa ni kuachana naye lakini nikifikiria watoto wangu nakosa raha.

Nafikiria katafuta mwanamke wa nje ambaye tutatimiziana hayo mambo hapa pia dada naogopa sana UKIMWI, siku chache zilizopita nilifikiria kupiga punyeto na nilivyofanya hivyo kwa kiasi fulani ilinipunguzia hamu lakini nitaendelea kufanya mapenzi na mkono wangu hadi lini?

Dada naomba ushauri nifanyeje?
Asante
J.M. KURASINI."
Dinah anasema: JM mpendwa asante sana kwa ushirikiano. Sasa kaka yangu umekaa na huyo dada miaka 8 na kakuzalia watoto wawili bado hujatangaza ndoa na inaonyesha huna mpango huo, yeye kama mwanamke hiyo hamu ya kungonoana na wewe kila utakapo ataitoa wapi?

Kama mwanamke hasa wa Kibongo hapo umemharibia maisha, kwanza kazaa watoto wawili (hakuna mwanaume atataka kuoa mwanamke mwenye mzigo), pili amekuwa nje ya "soko" kwa muda mrefu na hivyo itakuwa ngumu sana kwake kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi na mtu mpya.....miaka nane sio mchezo!

Kitu kikubwa ni kuwa umempotezea hali ya kujiamini na inaelekea wazi kabisa wewe huna hisia za kimapenzi nae (kwenye maelezo yako hakuna mahali umegusia kumpenda) tena bali uko nae hapo kwa ajili ya Ngono ambayo sasa huipati na inakufanya utake kutoka nje na watoto. Kinachokuzuia kutoka nje au kumsaliti ni UKIMWI, vinginevyo unekuwa na kimada.

Huyu dada kisheria ni ana haki zote kama Mkeo kwa vile mmeishi pamoja zaidi ya miaka 2, lakini hiyo haitoshi mpaka hatua zote kijamii zitakapofuata na kufunga ndoa kama wanavyofunga wengine.......kama alivyogusia mchangiaji, hicho ni kitu pekee huyu mdada anakitaka kutoka kwako.

Inaelekea alifanya yote ili kukufanya utangaze ndoa lakini hukufanya hivyo, akaamua kushika mimba mara mbili na kufanikiwa kuzaa wewe bado huna habari na ndoa, amendelea kuishi na wewe na sasa ni miaka nane (muda mrefu kuliko wanandoa wengi) lakini wewe ndio kwanza una-demand Ngono badala ya kutafuta tatizo ni nini hasa.

Huyo ni mwanamke, na ndoto ya mwanamke yeyote ni siku moja kufunga ndoa na mwanaume ampendae, huenda kwa wanaume hili ni suala la kijinga lakini kwa mwanamke ndoa ni kitu muhimu sana kwenye maisha yake.

Nini cha kufanya: Rudisha hisia za mapenzi kwenye uhusiano wako (kwani inaonyesha wewe umejisahau na yeye amekata tamaa kama sio kachoka), Muonyeshe huyu mama ni namna gani unampenda, onyesha kuwa bado unavutiwa nae japokuwa amezaa watoto wawili kwani mwanamke anapozaa mara mbili na zaidi mwili wake hubadilika.

Hivyo "Kisaikolojia" anaanza kuamini kuwa havutii tena na vilevile uke wake hauko vile ulivyokuwa awali na hivyo kujishtukia kuwa hatoweza kukuridhisha (anaweza kuwa na aibu pia), sasa kwa vile wewe hujui au hujali unadhani yeye anakunyima lakini ukweli ni kuwa humpi ushirikiano na wala huonyeshi kuwa bado unavutiwa na umbile lake.

Fanya yale yote ambayo ulikuwa ukimfanyia mwanzo wa maisha yenu kama wapenzi, unapohisi kutaka ngono usimuombe kama vile "haki yako" au "jukumu lake" bali itake ngono kwa kuonyesha mapenzi, kwa kumshika nakucheza na mwili wake, jitahidi kumfanya ajisikie kuwa anapendwa.....akielekea endelea lakini akigoma basi usimlazimishe na badala yake muulize kwa upole na upendo tatizo ni nini?

Usilalamike, bali tafuta ukweli kutoka kwake....."kitu gani nakosea mpenzi", " asali wa Moyo kwanini hutaki tufanye mapenzi?"....."naomba uniambie kama nimekosea nijirekebishe".....alafu mmwagie misifa (kulingana na kile unachokipenda na una uhakika anajua kuwa ni kweli).

Jinsi siku zinavyozidi kwenda ongeza kuonyesh amapenzi kisha tangaza ndoa(ndani ya mwezi mmoja), mchumbie mama watoto wako na mfunge ndoa. Nina kuhakikishia utaona mabadiliko na kila kitu kitakuwa sawa mara tu baada ya huyu dada kuwa na uhakika kuwa mnakwenda kufunga ndoa.

Hakikisha unafunga ndoa kiukweli,
Kila la kheri!!

Wednesday, 14 April 2010

Nahisi naibiwa, je niamini hisia zangu au?-Ushauri

"HABARI DADA DINAH,
POLE SANA KWA KAZI NZITO YA KUELIMISHA JAMII.
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 29 ,NINAMPENZI WANGU SASA YAPATA MIAKA MIWILI TANGU TUANZE MAHUSIANO, ILA NINAHISI KAMA VILE YUKO NA MSHICHANA MWINGINE.

HUWA HAPENDI NIENDE KWAKWE AKIDAI KWAMBA ANAHOFIA WADOGO ZAKE ANAOISHI NAO, MARA NYINGI HAPENDI TUWEPAMOJA MFANO WIKIENDI MUDA MWINGI ATASEMA YUKO NA RAFIKI ZAKE.

YAANI NAHISI KUNA JAMBO ANALOLIFICHA NA NAHISI ANAMWANAMKE MWINGINE ZAIDI YANGU, DADA NAOMBA USHAURI JE NIAMINI HISIA ZANGU AU NIFANYE NINI?
MAGDALENA
DAR ES SALAAM"

Dinah anasema: Magdalena mpendwa, dalili ya kwanza kabisa kuwa mtu anakupenda ni kutumia muda wake mwingi na wewe, kutambulishwa kwa ndungu, jamaa na marafiki zake ni dalili ya pili kuwa kafika kwako, kuwa wazi na huru kuwa na wewe au kukuonyesha kwa watu wake wa karibu ni dalili ya tatu, Mpenzi kutokuthamini mtu mwingine yeyote (rafiki zake) bali wewe na kama kuna shughuli/sherehe basi utakuwa wa kwanza kujulishwa na kushirikishwa kabla ya rafiki na jamaa wengine.

Haya yote hufanyika kwenye hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wa mtu yeyote, miaka miwili ni mingi sana kwa mtu kuendelea kukufanya wewe "mpenzi wa siri" kwa wadogo zake.

Natambua suala la yeye kukutambulisha au kukupeleka nyumbani ili kuepuka vishawishi kwa wadogo zake hasa kama wako kwenye umri wa kushawishika (kubalehe), wanaweza wakadhani kuwa na girlfriend/boyfried na kumpeleka nyumbani ni kawaida kwa vile kaka anamleta wake hapa.

Lakini vilevile inawezekana anahofia wadogo zake kuuliza kuhusiana na mwanamke mwingine ambae labda wanamfahamu, ili kuondoa utata jamaa inabidi akatae wewe kufahamu nyumbani kwake n.k.

Mpenzi anapokuwa na tabia ambayo wewe unadhani kuwa sio kawaida au hajawahi kuwa nazo kabla hukupa maswali na hofu, vilevile kama unabahati pia unaweza kupata hisia fulani ambazo huwa zinawatokea watu wachache, zinajulikana kama "the sixth sense" inakuwa kama "maono fulani hivi", kama kuna kitu kinatokea behind your back you just know.

Lakini kabla hujakurupuka na kumshutumu mtu kuwa anafanya maovu, unatakiwa kufanya uchunguzi wa karibu ili kuwa na uhakika ili kufanya uamuzi wa maana.

Nini cha kufanya:Punguza ulalamishi kwamba usimuulize wala kulalamika kuhusu tabia yake ya kukukwepa na punguza mawasiliano na huyo Boyfriend wako. Ikiwa unajua mahali anapoishi basi fuatilia kwa karibu ili kujua nini kinaendelea pale nyumbani, je kuna mke(mwanamke mwingine n.k.).

Badilisha mtindo wako wa kimaisha kwa kuwa mwanamke mmoja anaevutia kuliko kawaida, hakikisha unajipenda na kujijali zaidi, vaa mavazi yanayokukaa vema kulingana na umbile lako (usilifiche) ili uvutie zaidi.

Ukiomba kuwa nae mwisho wa wiki na yeye kudai kuwa anakwenda kutumia muda wake na rafiki zake, kuwa calm na muulize kwa upendo ni wapi huko anakoenda? ukijua kona anazopenda kutembelea basi ibuka huko bila yeye kujua, ukifika hapo mahali endelea na starehe zako lakini hakikisha kuwa amekuona.

Baada ya kufanya haya utakundua ukweli na hivyo itakusaidia kufanya uamuzi wa busara ili uweze kuendelea na maisha yako hasa kama kweli ni cheater na pengine kukupa nafasi ya kuweza kukutana na mwanaume atakaejali hisia zako, atakae kuthamini, kukupenda kwa dhati, mwanaume atakae kuweka wewe juu/wa kwanza kabla ya rafiki zake.

Ikiwa umegundua kuwa ni mwanaume mwema lakini hajui namna ya kumpenda mwanamke then itakubidi umfundishe, umuelekeze namna ya kujali na kuthamini mpenzi, kuweka wazi hisia zako na kumwambia ni namna gani unapenda kutumia muda wako mwingi na wewe. Mueleze kuwa hupendezwi na siri na usingependa uhusiano wenu uwe siri, ungependa "Dunia" ijue kuwa ninyi ni wapenzi.....ukianzia na wadogo zake, ndugu, jamaa na marafiki.

Kila la kheri kwenye umauzi utakaoufanya kutokana na matokeo utakayo yapata.

Tuesday, 13 April 2010

Babu kicheche! lakini ananisomesha, nimpendae ni Kijana ambae.....

"Habari dada Dinah, natumaini wewe mzima, First and foremost thanks for the advice najua sijawahi kuuliza but seems like we all face the same problems.

Mimi ni mwanamke wa miaka 27 niko njia panda na sina mtu wakunisaidia zaidi yako. Niko kwenye relationship na watu wawili nasijui nifanyeje? Sitajali kama watu wakinishambulia kwasababu nahitaji msaada.

Nimekuwa kwenye relationship na baba mmoja mwenye umri wa miaka 60 kwa muda wa miaka 5, huyu baba amekuwa akinisaidia kwa kila kitu ukichukulia mie sifanyi kazi. Amenisomesha chuo cha bei ghali, ananijali na kunipenda kwa kweli lakini tatizo ni hili hapendi nifanye kazi japokuwa ndio namaliza degree yangu mwaka huu.

Hapendi niwe na marafiki na ikitokea nimetoka na marafiki nikirudi anakuwa hayuko happy, nikienda mahali ambako anakujua basi atanifuata kwa kisingizio cha kuja kunichukua. Hapendi ni-have fun like going to the disco or any activity.

Ajabu for the last few years ambayo tumekuwa pamoja amekuwa na wasichana wengi since anasafiri sana na kila mahali anakokwenda analala na wasichana but yote nimevumilia na sikuwahi kummuuliza kwasababu naogopa kukatishiwa huduma.

Miaka miwili iliyopita tulihama Tz na sasa tuko Australia still ananipenda na kunihudumia na bado akiwa anasafiri ana-sleep na wanawake wengine. Anapenda kuzungumzia mambo ambayo mimi sina mpango wa kuyafanya.

Kwa muda wa miaka minne amekuwa akiniomba tigo lakini nimekuwa nikikataa pia huwa anataka 3some na marafiki zangu na tukiwa tunasex anataja majina ya marafiki zangu na siku hizi tunaweza kukaa bila sex hata miezi miwili ila blow jobs nampa karibia every other day.

In a positive side yaani tunapatana, kuelewana na ananisaidia na mambo mengi sana ya kimaisha lakini tatizo hatujaoana na mie sijajijenga japokuwa nina vipesa bank bt sio vingi ki-hivyo, also nikiwa na idea za kufanya vitu au kutafuta kazi ana-ni turn down.

Ki-ukweli mie niko very bright na nikiamua na kupata mtu atakayenipush hapa na pale nitafika mbali, huwa najiuliza je akifa leo nitafanyaje kwa kuwa sina chochote na yeye hawezi kuniachia chochote kwasababu ana watoto na watoto wake hawajui hii relationship yetu, yaani hata ndugu zake pia hawajui isipokuwa ndugu yake mmoja tu ndio anajua.

Basi nikiwa huku nikakutana na mkaka yeye ana 38yrs, nilimsumbua 4 a year but akawa mvumilivu thereafter nikajikuta niko nae nikamdanganya kuwa that old man ni baba yangu, this guy ananipenda ajabu, amenitambulisha kwa rafiki zake wote na anatarajia kunipeleka nchini kwao kunitambulisha.

He’s so sweet yaani tuna-click big time na niko huru ku-speak my mind sex is great,ananijali,I’m in love & happy with him. Sijawahi kujisikia like this all my life, yaani naamini ananipenda for sure. Nikimwambia idea zangu anazikubali na ananipush nitafute maisha yangu, although sijamwambia relation iliyoko between me na this old man.

The problem is he’s married na hajanificha he has 5 kids all I know there’s a tension between yeye na mkewe for sometime now & he’s not happy with her.

Dada Dinah na walimwengu nifanyeje?what I have planed ni kuwa nikimaliza degree yangu at the end of ths year nitafute kazi nchi nyingine nihame niwaache wote nianze maisha upya as mimi? Kwa abilities nilizonazo naamini nitafika mbali sana.
Samahi kwa email ndefu,
Ahsante
Ni mimi PP"
Dinah anasema: PP asante sana kwa ushirikiano na maelezo yako. Babu anakutumia kama ambavyo wewe unamtumia (kwenye maelezo yako umesema anakupenda na mnaelewana, hujasema unampenda). Ikiwa mnapitisha miezi hata miwili bila ngono ni vema hasa ukizingatia kuwa anakuchanganya na wanawake wengine hun ajinsi ya kumkataza wala kulalamika kwa vile unajua wazi ukifanya hivyo atasitisha huduma hasa ile ya Kielimu.

Sio kwamba na-support kuwa na mwanaume bil amapenzi ili kupata unachokitaka (kumchuna) bali kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa life haiko sawa nyumbani na ndio maana unasomeshwa na huyo babu mzungu, wee sio wa kwanza.

Wapo kina dada wengi tu hapo Dar, huondoka na vijibabu vya kizungu na hata kufunga navyo ndoa kwa sababu za ikuchumi lakini hakuna mapenzi, so ugumu wa maisha na tamaa ya kuendesha maisha ya juu inafanya Mabinti wadoo wengi kufanya unachokifanya, ikiwa sasa una miaka 27 na umekuwa na huyo babu kwa miaka 5 ni wazi umekuwa nae ukiwa na miaka 22.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha unajua nini ulikuwa unakifanya na kukitaka......Elimu na maendeleo yako kimaisha, sasa ukifanikisha hili ni vema kufanya kama ulivyosema kuhama nchi na kuanza upya.

Nini cha kufanya: Wakati unaendelea na haratati za kumalizia Digrii yako hakikisha unaachana na huyo mume wa mtu na jitahidi kutumia kinga kila mara huyo kibabu anapotaka ngono na wewe ili kujilinda.....kama unaweza usimpe kabisa mwili wako kwa kutafuta sababu atakazoziamini.

Kwa vile ni babu na mzungu haina maana kuwa hapati Ngoma, Australia wanapima Ngoma wageni lakini watu wao hawawapimi Ngoma wanapotoka na kuingia hivyo wanapokwenda Afrika au nchi nyingine na kungonoka ovyo uwezekano wa kuukwaa UKIMWI ni kuwa kuliko unavyofikiria. Kuwa mwangalifu, usipoteze maisha yako ktk umri mdgo ulionao.

Baadhi ya mabinti wanaoondoka nyumbani na vibabu vya Kikoloni (kizungu) huishia kufanya sex slaves (watumwa wa ngono), wengine hulazimishwa kuwa makahaba, wengine huteseswa na baadhi huishia kuuwawa.

Baadhi ya Wazungu bado ni wabaguzi, na wanapopata nafasi ya kumiliki binti wa Kiafrika huishia kufawafanyia maovu na mabaya mengi (kuwangonosha na wanyama, kuwafanya watumwa, kuwauza kwa Wazungu wenzao ambao hawajawahi kutomba wanawake weusi ambao wengi wanaamini kuwa ni watamu,kuwafanya mande n.k), kuweni waangalifu mnapojichanganya na hawa jamaa wanaokuja kutembea Bongo kwa ajili ya Ngono (Sex tourists).

Ni matumaini yangu Post hii ya PP itakuwa imesaidia mabinti wengine wanaibabaikia Wazungu wanakuja kutembelea Tanzania wakidhani ni mwisho wa matatizo, baadhi bado wanaunyama miyoni mwao dhidi ya Muafrika.

Kila la kheri kwenye masomo yako na katika kuhama makazi.

Monday, 12 April 2010

Nitajuaje kama kafika kileleni bila yeye kusema?

"Hello,
Natumaini unaendelea vizuri na kazi.

Nina imani sana na maelezo yako kwa vile yamesaidia sana ku-improve maisha ya familia nyingi japo baadhi ya watu wasio na mtazamo sahihi wa maisha wanayaona kama yanapotosha jamii. Ukweli ni kwamba haya mambo yapo na njia sahihi ya kuyashughulikia ni kushirikiana (to share) uzoefu kutokana kwa jamii tunamoishi.


TATIZO LANGU:
Ndoa yangu haijaingia mashakani ila nahisi naweza kufika huko endapo sitaelewa mambo yafuatayo:


Wakati wa kujamiiana na mwenzangu, kawaida yeye huwa ananiambia kuwa amefikia kileleni, ukweli ni kwamba mimi sijui ni jinsi gani ya kuitikia zaidi ya kuendelea tu. Pia mimi nikifikia kileleni huwa simwambii ila nadhania anakuwa anajua.


Pili, napenda kuelewa ni mbinu gani naweza kuitumia katika kujamiiana ili mwenzangu atoe maji (majimaji) mengi? Maana naona inakuwa vigumu kufanya hivyo mara nyingi. Nakuomba sana uifikirie hii email na unipe majibu yatakayoweza kuniongezea ujuzi katika eneo hili la maisha ili ndoa yangu/yetu iendelee kuwa yenye furaha.


Nasubiria kwa hamu sana kutoka kwako.

D"

Dinah anasema: D asante sana kwa ushirikiano. Nadhani mkeo ni mmoja kati ya wale wanawake wachache wanaopenda kuwasiliana/ongea wakati wa kufanya mapenzi, anapokuambia kuwa amekojoa ni kama kukupongeza kwa kwazi yako nzuri, kwamba umemfanya vizuri na amefika kileleni hivyo usimsubiri/usijizuie wewe jiachie tu na ukojoe.

Mf:- anakuambia nimekojoa/nimefika kileleni....wewe mwambie "oh yeah, jitahidi ukojoe tena basi" au "napenda unavyokojoa/fika kileleni" au "namimi nakaribia kukojoa"....au unaweza kumpa denda la kimahaba ambalo linaweza kumrudishia nyege na hivyo kupiga bao la pili kwenye mzunguuko mmoja.

Utajuaje kuwa amefika kileleni: Mwanamke anapofikakileleni mawili au yote kati ya haya hutokea....ute unaongezeka ukeni, utahisi uume wako kama vile unavutwa kwa ndani kutokana na misuli ya uke wake kubana na kuachia, mapigo ya moyo wake yatakuwa ya juu, kuhema kwake kutakuwa deep, atakaza misuli ya mapaja....alafu utahisi kila kitu kimetulia isipokuwa misuli ya uke kwa ndani itaendelea "kukonyeza"......ukichomoa uume wako utaona mashavu ya uke wake na kisimi vimetuna/vimba.....hapo ujue amefika kileleni.

Mkeo kutoa maji mengi inategemea na maumbile lake, kama ameumbwa hivyo basi wala huitaji kutumia nguvu bali kutumia uume wako kuchezea kisimi na sehemu iliyo kati ya tundu la mkono na kisimi, namna ya kufanya hivyo tafadhali bofya hapa kama hatotoa majimaji mengi utakayo basi ujue mkeo ni mmoja kati ya wanawake wengi ambao hawajaumbwa hivyo.

Kama unaweza kumridhisha kwa kumfikisha kileleni, mshukuru Mungu kuwa unamfikisha kwani wapo wanaume wengi hawawezi kuwaridhisha wake zao.
Kila la kheri!

Friday, 9 April 2010

Wapenzi 4, Uzoefu wa miaka 4, lakini sijawahi kupata utamu wa Ngono!

"Habari dada dinah? Pole na shughuli nzito ya kuelimisha jamii.
Mimi ni dada mwenye umri wa miaka 28 na nia uzoefu wa miaka kama nane hivi kwenye ulimwengu wa mapenzi na nimewahi kuwa na maboyfriend 4 lakini dada sijui kitu kukojoa kwangu, wala sijawahi kusikia utamu hata mara moja.

Naitamani hiyo raha dada ila ndio kwanza imenipitia kushoto. Wakati wa sex huishia tu kusikia viraha vya kuzungusha mboo tu. Nimewahi kuwa na Boyfriend ambaye tukianza gemu hataenda hata karibu saa nzima, ninachoambulia ni pale mwanzo na baadae huanza kuhisi maumivu.

Nimefikia hata hatua ya kuwa namdanganya boyfriend wangu kuwa nimekojoa kumbe lah. Hata yeye kitu hicho kimekuwa kikimkwaza hata kufikia mahali na kuniuliza wakati wa sex nakuwa nawaza nini?

Dada dinah na wadau nisaidieni kwani staili nyingi nimefanya na kujituma lakini wapi? Kuna wakati nasikia kitu kama mkojo unataka kutoka lakini inakuwa kama nimebanwa mkojo ule wa kawaida na mwishowe hautoki.

Wadau au sijui kukojoa ni nini? Ebu basi nielezeni huo mkojo unatokea wapi kama ni njia ile ya kawaida au kwenye tundu inapoingia mboo? Je unakuwa unafananaje?

Nisaidieni nami nipate hio raha ya sex mnayoisema nyinyi humu kwani inaniuma.
Anitha."

Dinah anasema: Asante kwa ushirikiano Anitha, Suala la kufika kileleni halina uhusianow owte na uzoefu wa kuwa na wapenzi wengi bali wewe mwenyewe na mpenzi husika. Unaweza ukabahatika ukawa na mpenzi wako wa kwanza na wote kwa mapoja mkawa willing kujifunz anakujaribu na pia kufundishana na kusaidiana mpaka wote mnafurahia au hata kujua kwanini hasa mnafanya hilo tendo.....kuwa karibu kama wapenzi na kupata utamu wa miili yenu.

Kuna mambo mengi ambayo yanaweza kusababisha wewe kushindwa kufik akileleni na moja kubwa kuliko yote ni wapenzi wako kutojua au kutojali hisia zako za kingono, ubinafsi kitandani ambao wanaume wengi wanao, uvivu, kutokujuana (miili yenu), yeye na wewe kutokujua vipele vya "utamu", uoga, hofu ya kukutwa (inategemea mlikuwa mnafanya ngono hiyo wapi?) n.k.

Ili mwanamke uweze kufika kileleni unatakiwa kuwa na mapenzi/hisia juu ya huyo mwanaume, ku-relax, kuujua mwili wako na kuzingatia tendo (hamishia akili na mawazo yako yote kwenye tendo linalofanyika), kama huna hofu ya kushika mimba au kupata HIV ni wazi kuwa hutoweza kufika kileleni.

Ili kujua utamu wa ngono ulivyo nakushauri ujipe mkono/jichue(soma topic hapo chini kama hujui) utasikia raha na hatimae utamu, sasa utamu huo ukiuongezea kama mara 5 hivi ndio unaopatikana kwenye uke kwa ndani wakati mwanaume ameingiza uume (anakufanya), lakini iliufanikiwe kupata utamu huo kwa ndani ni vema mpenzi wako na wewe mwenyewe mkajua namna ya kufanya mapenzi.....bonyeza topic ya tofauti za utamu wa ngono kwa mwanamke hapo chini.


Topic zangu za mwanzo kabisa (2007) zina maelezo mengi ambayo yalisaidia wengi na nina uhakika yatakusaidia wewe pia, tafadhali tembelea Topic kama "kilele na mwanamke", Uwazi kwenye mapenzi/ngono", "Ngono ni sanaa", "kuita kilele", "haki kwenye mapenzi, "nyeto kwa mwanamke", "tofauti za utamu wa ngono kwa mwanamke" na nyingine nyingi ili ujifunze zaidi.

Kila la kheri!

Saturday, 3 April 2010

Wakatiwa tendo anatoa maji mithiri ya Mtindi,Ni nini?

"Habari da Dinah pole na majukumu uliyonayo na pia hongera kwa kuchukua muda wako kutupa elimu na ufafanuzi wa mambo ya mahusiano na mapenzi. Mimi nina mpenzi ambaye tunapendana sana tatizo ni kwamba mara zote tunapotiana yeye hutoa maji yafananayo na maziwa ya mgando.

Pia huwa hajisikii vizuri anapoona ile hali na mara zote hulalamika kwa kusema amenichafua. Nimekuwa nikifatilia kujua nini kinamsumbua je ni ugonjwa au ni kawaida kwa wanawake kutoa aina hii ya maji ukeni wakati wa kutiana japo hasikii maumivu na yuko kawaida tu?.
Naomba Da dinah na wachangiaji mnisaidie kuhusu hili ."

Dinah anasema:Asante sana kwa mail yako, nashukuru kwa uvumilivu as nimechelewa kutoa maelezo hii ni kutokana na ufinye wa muda. Ni wazi kuwa mpenzi wako haujui mwili wake wala kinachotokea mwilini mwake na ndio maana Utoko unapojitokeza hujisikia aibu/vibaya kuwa amekuchafua, lakini sio ugonjwa unless "mtindi" huo unarangi ya pink-ish, nyekundu, njano, kahawia(brown) the itakuwa tatizo, kwamba ukeni kuna maambukizo.

Huo ni ute ambao tunauita Utoko, ni ute ambao ni muhimu kwa afya ya uke wa mwanamke lakini unapofika ukeni unatakiwa kuondolewa. Kwa kawaida utoko huteremka wenyewe lakini huchukua muda mrefu hivyo mwanamke anatakiwa kuusaidia utoke kwa kujisafisha.

Umewahi kusikia watu wakisema "mwanamke usafi" hawamaanishi kuoga au kujiremba au kusafisha nyumba na kuiremba, bali kujiswafi na kuondoa Utoko kila anapooga au angalau mara moja kwa siku (kila asubuhi) hii ni kwasababu Utoko huzaliana kwa wingu usiku na hutoa harufu zaidi kuliko ule unaojitokeza mchana/jioni.

Tafadhali rejea.....kulia kwa juu tafutaTopic iitwayo "jinsi ya kujiswafi/safisha uke"

Kila la kheri!

Thursday, 1 April 2010

Sikuwa tayari kwa ngono wakaniacha, sasa nimekua wananitaka-Nifanyeje?

"hi dinah, I'm MJ, a girl aged 21yrs bado niko Chunoni. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mada zako na napenda kukupongeza kwa kazi nzuri kwani umenielimisha kwa kiasi kikubwa. Tatizo langu ni kwamba nimeanza kuingia kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi nikiwa bado mdogo yaani nilikuwa na miaka 16 na nimekuwa na wanaume 7 kwa nyakati tofauti na kila uhusiano uliisha vibaya.

Yaani kwa kuachwa na machoz! to tell you the truth dinah, sijawah kusex na hao wavulana na ndiyo sababu kubwa wamekuwa wakiniacha! sasa nimekua baadhi yao wameanza kuniomba msamaha na kutaka nirudiane nao,
nifanyeje?"

Dinah anasema:Hello MJ, asante kwa kufuatilia mada zangu za awali na ninafurahi kuwa umejifunza vijimambo na hakika vitakusaidia hapo baadae utakapokuwa mkubw ana tayari kwa haya masuala.

Hao wote walikuwa wanataka uzoefu wa kingono kutoka kwako na sio mapenzi ya dhati hasa ukizingatia umri mdogo uliokuwa nao then. Kama walivyokushauri wengine ambao naungana nao ni kuwa usijali usumbufu wao hao wote wajinga-wajinga ambaoo walikuwa na wewe kutaka ngono na sio urafiki wa kusaidiana kimasomo au urafiki wa kawaida wa kugundua ujinsia bila ngono.

Ushauri wangu kw akifupi ni kuwa achana nao, piga kitabu hapo Chuoni, mapenzi na masomo kwa pamoja vinaweza kukuchanganya na hata kuwa hatari kwani vyote vinahitaji muda, attention na kufanyiwa kazi, lakini masomo ni muhimu zaidi kwako kwa sasa kuliko mapenzi, kwasababu mapenzi yapo na yataendelea kuwepo which means ukimaliza masomo utayakuta.

Lakini masomo uliyonayo hivi sasa, hayaendelei milele, itafikia mahali utahitajika kufanya mitihani ambao itakusiaidia kwenda kwenye level nyingine ya kimaisha. Ukicheza sasa kwa kuchanganya mapenzi ni wazi kuwa utakuwa umeharibu sehemu muhimu ya maisha y ako.

Hongera kwa kugoma kutoa mwili wako kwa hao jamaa na endelea na msimamo wako huo mpaka siku utakapokuwa tayari na kuwa na uhakika kuwa unampenda huyo Kijana na yeye anakupenda kwa dhati, ili kuifanya siku hiyo kuwa extra special.

Kila la kheri kwenye Masomo yako na uamuzi utakaufanya.