Friday, 29 January 2010

Nataka kuchumbua ila majibu yake mmh-Ushauri.

"Naitwa Michael miaka 25 ni mara yangu ya kwanza kwenye libeneke kuomba ushauri. Kuna binti anaitwa Joy ana miaka 23 ambaye ningependa awemchumba wangu, lakini nakuwa katika wakati mgumu kutokana na majibu anayonipa nikiwasiliana naye kupitia simu. Wakati huu hatukuwa karibu.

Majibu anayonipa hasa kwenye story za kawaida tunazopiga yanaonyesha uelekeo wa yeye kunikubali lakini nikimuuliza kuhusu mimi na yeye kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ananiambia muda wake wa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi bado, na nikimuuliza lini atakuwa tayari kasema "ni katika kipindi cha miaka 3 ijayo".

Nilimuahidi kumsubiri lakini akakataa kwa kisingizio kuwa asingependa kuniumiza wala mimi kumuumiza yeye.Tumekuwa karibu sana katika kipindi cha miezi 3 ya mawasiliano kupitia simu kiasi cha yeye kuniambia mambo mengi kuhusu familia yake na mengine yangehitaji mtu wa karibu sana kuyajua.

Mambo kuhusu boyfriend wake wa kwanza na jinsi walivyoachana, sifa za mume ambaye anamhitaji na zote ziliniangukia.Nilipomuuliza kama ananipenda na kunihtaji alisema ananipenda lakini kunihitaji hakuwa na jibu kamili.

Sasa wakati mgumu nilionao ni je niendelee kumbembeleza au nimuache? nikitaka kufanya hivyo roho yangu inasita kwani kwa jinsi anavyokuwa mgumu ndio nazidi kumpenda. Nifanyeje? Michael"

Dinah anasema:Mike hebu kuwa mkweli, unauhakika ktk umri wa miaka 25 uko tayari kumuoa huyo binti au ni gia tu ya kumpata kimapenzi? Kama kweli unauhakika na unania ya kumchumbia na kuja kufunga nae ndoa nasikitika kusema kuwa yeye kwa sasa hayuko tayari kwa ajili hiyo na amekuwa wazi kwako, kuwa anakupenda lakini hayuko tayari labda baada ya miaka 3...hapo uamuzi ni wako ku-take risk na kumsubiri au kuendelea na maisha yako.

Uamuzi wa kumsubiri unaweza kukupa matokeo mawili tofauti moja ni chanya au hasi, kwamba akawa nawe kama mpenzi/mchumba au akawa na mtu mwingine....ndio maana nikasema take risk.

Kitendo cha huyu binti kukuambia vitu vingi ambavyo wewe unadhani anapaswa kuambiwa mtu wa karibu zaidi kama vile mpenzi, ni kwa sababu anakuamini kama rafiki yake. Inawezekana kabisa hata upendo alionao ni wa kirafiki na sio wa kimapenzi na ndio maana anakosa jibu unapomuuliza suala la yeye kukuhitaji wewe kama mpenzi.

Katika hali halisi ni Binti mdogo ambae tayari amewahi kuwa kwenye uhusiano, kama mpenzi aliyekuwa nae alikuwa ndio mpenzi wake wa mwanzo ni wazi kuwa itamchukua muda mrefu kidogo kama hajaingia kwenye uhusiano mpya na mwanaume yeyote sio wewe tu.

Kutokana na maelezo yako nahisi kuwa huyu binti bado anahisia na yule ex, hisia zinazomfanya ashindwe kufanya uamuzi kwa vile hana uhakika kama bado anampenda yule au la! Inawezekana pia kajiwekea hiyo miaka mitatu kuweza kujua hisia zake ziko wapi.

Kitu ambacho kimepelekea yeye kukuambia kuwa asingependa kukuumiza au wewe kumuumiza, pale ulipoahidi kumsubiri ndani ya miaka mitatu ambayo kwa mujibu wake ndio atakuwa tayari kuingia kwenye uhusiano.

Nimependezwa na uwazi wa huyu Binti, kajaribu kuwa mkweli ili kukusaidia wewe kufanya uamuzi na kuendelea na maisha yako lakini wakati huohuo uendelee kuwa rafiki na mtu wake wa karibu.

Mimi nakushauri umuache (kwani kubembeleza kukizidi huwa kunaudhi sana) lakini endelea kuwa pale kama rafiki, msikilize, mshauri, msaidie na yote muhimu kwa marafiki. Ukionyesha kuwa umeheshimu "msimamo" wake lakini bado unaendeleza urafiki ni wazi atakuwa comfortable na wewe na pengine baada ya hiyo miaka mitatu wewe ukawa the one.

Kila la kheri.

Thursday, 28 January 2010

Niache mke ni we huru au niendelee kuteseka!-Ushauri!

"Pole na kazi za kutuelimisha dada dinah,
nahitaji ushauri kutoka kwako na wachangiaji wote. Mimi ni kijana miaka 26 nimeoa miaka mitatu iliyopita. Mke wangu kabla yangu alikuwa na bwana'ake aliye mtoa bikra, inasemekana walipendana sana lakini wakaachana baada ya mwanamke (mke wangu sasa) kumfumania jamaa yake na kila mtu kuanza maisha mapya.

Mimi nikaoa yule dem na baada ya jamaa kusikia akaamua kwenda kwa Waganga wakienyeji na kuua nguvu zangu za kiume na kuni haribia maisha yangu ilinisiwe na mbele wala nyuma, hii yote ni kwa sababu ya huyu mwanamke ambae ni mke wangu.

Jamaa nasikia anasema nikiendelea kuwa na mke wangu huyu basi hali itakuwa hivyo hivyo labda ni muache ndio nitarudi katika hali yangu ya kawaida. Sasa dada dinah naomba ushauri wako ktk hili.
Niache mke ili niwe huru au niendelee kuteseka?"

Dinah anasema:Asante kwa kujali (pole yako nimeipokea). Kaka pole sana kwa yanayokusibu ila mimi siamini katika urozi, lakini kama Mkristo natambua kabisa kuwa kuna nguvu za giza na majaribu ya Shetani.

Mimi binafsi sijui kudanganya hivyo basi sitokuambia nendeni mkaombewe ili mapepo yatoke na muendelee na ndoa yenu, mtajikuta mnzeeka mkiwa mnapambana na huyo mpenzi wa zamani wa mkeo kiimani na hakuna kitakachotokea (haya madhehebu ya siku hizi wachanganya uchawi na Mungu).

Pamoja na kusema hivyo sina maana kuwa usiamini Mungu, ni muhimu kumrudia Muumba wako na kuhakikisha kuwa unamhusiha ktk kila jambo.

Kuna sababu nyingi kwanini watu tunafunga ndoa lakini naamini nia na madhumuni ya kufunga ndoa ni kuishi kwa upendo, furaha na kufanya tendo la ndoa bila mipaka ili kuridhishana na kuzaliana, wewe umeoa na hupati hata moja kati ya hayo......sasa nini faida ya hiyo ndoa?

Naamimi kuwa hakuna mwanadamu anaweza kuzuia riziki ya mwenzake hivyo hali mbaya ya kimaisha inawezekana ni kutokana na msongamano wa shida za kimaisha (mawazo), hofu, majuto, kutokujiamini nk hali inayoweza kupunguza kasi ya utendaji wako wa kazi au ukashindwa kuwa "mpiganaji" kwa vile unapata hisia hasi kuwa wewe sio mwanaume kamili kwa vile tu huwezi kusimamisha.

Kuhusu mkeo, nakubaliana na wote waliosema uachane nae. Kama huyo Mlozi kasema ukiacha mkeo unakuwa huru basi fanya hivyo Kaka, kujiwekea mikakati na mipango imara ya maisha mapya na yanayomhusisha Mungu zaidi.

Wewe bado kijana mdogo sana (uliwahi tu kuoa) na nina uhakika kuwa utakutana na binti mwingine mzuri ambae atakufaa maishani na utaishi nae maisha ya raha mustarehe na yaliyokutokea yatabaki kuwa Historia.

Nakutakia kila la kheri, Mungu akuongoze utakapo kuwa unafanya uamuzi, pia akubariki kwenye kila jambo unalokwenda kulifanya kama kijana mpya.

Wednesday, 27 January 2010

Nikipiga bao lakwanza nakuwa mvivu kwa Dk 30, ni kawaida?

"Hi Dinah, vipi hali yako bila shaka umzima wa afya,
nina maelezo kidogo na nadhani unaweza kunisaidia kiushauri. Nlikua natafuta kwenye web ndio nikaona blog yako na unayoyaelezea mimi ndio hasa natayatafuta ili nitatue matatizo yangu.

Mimi nina umri wa miaka 30, nimeoa miaka miwili na nusu iliyopita na nina watoto wawili, tatizo langu mimi hua nakua na hamu sana ya sex baada ya kujiandaa vizuri kwa maromance lakini nikiingia uwanjani sichelewi kabisa kupiga bao na nikishapiga bao moja mwili unakwisha nguvu nakua mvivu sana.


Siwezi kuendelea na mboo haisimami mpaka ipite labda nusu saa ndio naweza kurudia tena mchezo au bao la pili, sasa nashindwa kuelewa hivi ni ujuzi wangu mdogo katika maswala ya kujamiana au kitu gani?

Wakati mwingine nashawishika kutumia Viagra lakini sijui umuhimu wake wala madhara yake kwani sijawahi kugusa maisha ni mwangu, namshukuru Mungu sisumbuliwi namatatizo ya kiafya japokuwa nina uzito wa Kg 96.

Kuna watu wengine huwa wanasema ati sababu ni chakula sio fresh tunachokula tofauti na kule nyumbani Africa, huku sisi kila kitu chatoleawa kimegandishwa sio kutoka shambani, kwa mvuvi au buchani moja kwa moja, lakini hili tatizo ninalo muda mrefu sana toka hata kabla sijaoa.
Tafadhali naomba ushauri wako na hapo nina uhakika kwa uzoefu wako ushafahamu tatizo langu.

Thanks a lot
Farid wa muscat.

Dinah anasema: Si bora wewe unapumzika Dk 30, kuna wanaume wengine wakipiga hilo moja ndio inakuwa imetoka hiyo mpaka wiki ijayooo! Hebu mshukuru Mungu kwanza alafu tuendelee! Duh! nimepitiwa, Farid kaka hujambo? hali yangu ni njema kabisa, asante kwa ushirikiano na kwa uwazi wako.


Wewe huna tatizo kabisa kwani wanaume wote wakipiga bao na kumaliza mzunguuko wa kwanza huitaji kupumzika kwa muda ili kukusanya nguvu za kuendelea na mzunguuko wa 2, 3 au mara zote ambazo mkeo atamudu.


Kuna sababu ya Kibaiolojia inayokufanya wewe mwanaume utake kupumzika kidogo mara tu baada ya kumwaga (bao), japokuwa utundu wa mwanaume unaweza kukufanya usimamisha haraka mara tu baada ya kumwaga....Mf unamwaga anakuacha kama Dk kumi hivi alafu anaanza kukuandaa tena kwa kucheza na kona muhimu za kukuhamasisha kingono.


Lakini pamoja na kuwa wanaume wote huitaji kupumzika kwa muda baada ya kumaliza mzunguuko wa kwanza haina maana huwa wavivu bali huishiwa nguvu (inategemea na ufanyaji wako ulivyokuwa na kuchelewa kufika kwa mkeo), kama ulienda kwa muda mrefu ukijaribu kumfikisha mkeo ni wazi akipata bao lake atakakuw akajichokea


Mwanaume kuwa na Kg 96 sio tatizo japokuwa inategemea uzito huo ni wa mafuta au misuli? Kama ni mafuta basi ni vema kama utanza kufanya mazoezi ili kupunguza mafuta na kuwa na uzito wa kawaida tu, lakini kama uzito wako ni wa misuli hakuna haja ya kupunguza uzito wako.

Inawezekana kabisa kuwa uchovu unaosuikia baada ya bao la kwanza unasababishwa na "unene" (kama uzito wako ni wa mafuta) wako na hivyo ukipunguza uzito ni wazi utakuwa unapumzika dk chache zaidi kuliko hiyo nusu saa ya sasa.

Ni matumaini yangu kuwa wachangiaji na nyongeza ya maelezo yangu yatakuwasaidia katika kufurahi maisha yako ya ndoa na yale ya kingono ili kujenga familia bora yenye furaha, Kwamba wewe ukiridhika na mkeo akaridhika mnakuwa na furaha au?.....

Kila la kheri.

Tuesday, 26 January 2010

Ujauzito umeongeza nyege lakini mume hataki-Ushauri

"Dada Dinah pole sana na hongera kwa kazi ya kutuelimisha kuhusu masuala ya kuboresha mahusiano yetu katika ndoa. Nimekuwa nikisoma na kuchangia kwa kutoa maoni kwa watu waliouliza maswali.

Leo na mimi yamenifika. Ninaomba tu wanablog mnisaidie. Yaani hapa nilipo nimetamani hata kumpigia simu dada Dinah ili tuonane uso kwa uso anisaidie zaidi, ila sina namba. Naomba tu dada Dinah ujitahidi kuutoa ujumbe huu mapema na ninaomba mawazo/maoni yenu. Dinah unaweza pia kuanza kudokeza machache wakati wachangiaji wanaendelea.

TATIZO NI HILI
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 29, nimeolewa na nina miaka 8 kwenye ndoa yetu ambayo imejaaliwa watoto watatu na sasa nina mimba nyingine ina miezi mitano, Mtoto wetu wa mwisho, inshallah!.


Imetokea mume wangu akapata serious infection kwenye mkojo. Daktari aliyemtibu kwa kuwa anatujua amemwambia kuwa kwa sababu mimi ni mjamzito na wajawazito hupata maambukizo haya kwa urahisi (ambayo hata hivyo hayajitokezi mapema) basi mimi nitakuwa nimemwambukiza.

Alipokuja na maelezo hayo sikumbishia na ilibidi na mimi nikapime. Kwa hakika sikukutwa na infection zaidi ya Viprotini kidogo ambavyo ni vya kawaida kwa mama mjamzito yeyote. Alitahadharishwa kwamba tusifanye kabisa ngono hadi atakapopona ili tusimwambukize mtoto.

Niliona ni wazo jema na nilijua kwa kuwa ni ugonjwa unaotibika poa tu. Sasa ni miezi miwili tangu alipoambiwa hivyo na ameshapona lakini "ananiogopa nitamwambukiza tena" na wala hana mpango wa kufanya ngono tena na mimi, sijajua hali hii itaendela hadi nitakapofungua au!

Tukilala kila mtu kivyake, haniwekei hata mkono kunikumbatia. Mwanzoni alikuwa analalamika mwili ni dhaifu, anajisikia vibaya sana, nimwache alale nisimusimbue. Sasa ni zaidi ya mwezi tangu amepona lakini bado mambo ni kama mwanzo.

Hapa nilipo yamenifika shingoni. Ninatamani hata kukunwa tu na nimejaribu kumchokoza anakuwa mkali, kama defensive mechanism hivi. Wakati mwingine anazua ugomvi ili tusiwe na mahusiano ya karibu.

Ninakuwa sina la kufanya ila ni kunyamaza tu, maana Condom pia alishakataa kutumia (na sijui kama ni nzuri pia kwa wajawazito!). Kwa kweli inaniumiza na ninajisikia vibaya. Nyege zimenikaba sina jinsi. Nimejaribu kujishika mwenyewe sisikii raha na ninatamani ningeguswa hata kwa kidole tu. Nadhani jamani mmenielewa.
Nahitaji ushauri wenu wapenzi.

JOKE: Nilikuwa nasoma ujumbe wa aliyeamua kulipiza kisasi hata nikashawishika kusema, wakati mwingine inabidi. Ila kutokana na hali yangu siwezi thubutu, ningetafuta hata wa kunishikashika kisimi tu (jamani msinielewe vibaya sijawahi hata mara moja - niliolewa bikira na bado ni bikira kwa mme wangu tu).

Ninaomba mnisaidie, nifanyeje? Na pia, je, mume wangu ameathirika kisaikolojia au? Nitamsaidieaje?

Mind You: Mume wangu pia huwa ni "mvivu" kwenye ngono. Ni kama amepata pa kuponea. LAKINI hili halizuii kutafuta mbinu. Nipeni ushauri wenu ndugu zangu."

Dinah anasema: Asante kwa ushirikiano na uvumilivu wako. Inapendeza kuona baadhi ya wachangiaji wamejitahidi na kuzungumzia uzoefu wao ambao hakika umesaidia kulichukulia suala lako kivingine na pengine kukuongezea mawazo au hofu zaidi.

Lakini kumbuka kuwa tatizo la kingono linapojitokeza kwenye uhusiano sio mara zote kuwa mwanaume anajinafasi nje na mwanamke mwingine, wakati mwingine inakuwa ni mawazo, hofu, hatia, ugonjwa, utu uzima n.k. ndio maana huwa nashauri watu kufanya uchunguzi wa kina nakuwa na uhakika wa nini kinasababisha tatizo lililojitokeza kuliko kujaji na kufanya uamuzi ambao mara zote huwa sio wa busara.

Kutokana na maelezo yako ya hapa na private nahisi kuwa mumeo inawezekana kabisa anasumbuliwa na tatizo la kiume a.k.a Upungufu wa Nguvu za Kiume, tatizo ambalo liko tangu na tangu lakini wanaume huwa hawapenzi kulizungumzia wala kwenda kupata ushauri namatibabu. Tatizo hili linatibika ikiwa mwanaume hana matatizo mengine ya kiafya.


Sasa mwanaume yeyote anapohisi kuwa uwezo wake wa kungonoka umepungua au hana kabisa nguvu za kufanya tendo la ndoa huwa anapoteza hali ya kujiamini kama mwanaume. Mwanaume hapa atatumia kila mbinu ili usigundue tatizo lake ambalo kwake ni aibu.


Njia mbazo mwanaume mwenye tatizo la Ukosefu wa Nguvu za Kiume wengi huzitumia ni kukimbia tendo, kutumia pombe, kubadilikakitabia na kuwa mkali, kusingizia kuwa wanaumwa/choka napengine kukusingizia wewe unatoka nje ya ndoa kama sio kuwa "humvutii" tena na wengine huamua kutoa Talaka kabisa, hii yote ni kuzuia "siri ya kiume" kutoka ambayo ni wazi inaweza kukufanya wewe mwanamke utafute namna hasa kama ngono uhusiano wako kwako pamoja na mambo mengine muhimu umeegemea zaidi kwenye ngono (unapenda Ngono).

Mwanaume anapokuwa kwenye hali hii anahitaji ushirikiano, matumaini na uelewa wa mwanamke kuliko wakati mwingine wowote wa maisha yake, lakini kutokanana hali yako ya ujauzito ni wazi wewe pia unahitaji ushirikaino na support yake.

Pea nyingi hupoteza ndoa zao kwa uzembe unaosababishwa na wote wawili kutokuwa makini na kuwa wabinafsi zaidi. Mumeo hapa ameonyesha ubinafsi ili kutunza Ego yake, wewe inawezekana mumeo akahisi kuwa umekuwa mbinafsi kwa kudai tendo wakati mwenzako hawezi kukupa pale unapotaka kutokana na matatizo ambayo ameamua kukuficha......katika hali halisi ungejua tatizo ungejitahidi kuwa mwelevu na wote kwa pamoja mkashirikiana na kupeana support ili kuondokana na tatizo linalokabili ndoa yenu hivi sasa.

Mambo mazuri hayataki haraka, natambua sana kuwa ujauzito umekuongezea hamu zaidi ya kungonoka na mumeo analijua hili lakini kwa sasa hana namna ya kukuridhisha utakavyo hivyo basi anajitahi kukupa ikiwa siku hiyo mambo ni mazuri (anahisi kuwa anaweza kusimamisha kwa muda fulani) au pengine katumia dozi ndogo ya Bluu au Viagra.

Isije kuwa kuwa anatumia aina fulani ya dawa za kuongeza nguvu ila hataki wewe ujue kwani anahisi kuwa utamdharau na kumuacha ukigundua kuwa hawezi tena kusimamisha bila "msaada".

Wewe na mumeo kwa mara nyingine mnahitaji kuongea kwa upendo lakini wewe kuwa a bit firm ili akuelewe vema na hivyo kukubali tatizo lake na kwenda kupata msaada wa kitibabu.

Samahani msomaji,
nitaishia hapa kwani ninaendelea na msaada wa moja kwa moja na mhusika.

Thursday, 21 January 2010

Nataka kurudi kwenye Kalenda kuzuia mimba baada ya kutumia Dawa-Ushauri

"Mambo dinah,
naomba unisaidie hili tatizo langu. Nina umri wa miaka 25, sijaolewa ila nina boyfriend ambaye tunaishi mbali mbali. Yeye yupo nchi nyengine na mimi nipo nchi nyengine, tatizo ni hili, toka naanza kufanya mapenzi huwa natumia kalenda kujikinga na mimba kwa sababu sikai na mwanaume kinyumba.


Ila kutoka na umbali uliopo kati yangu na boyfriend wangu huwa inabidi niwe naenda kumtembelea kila ninapopata nafasi na huwa nakaa si chini ya wiki mbili, na yeye mambo ya kuzuia mimba hataki wala kusikia kwahiyo anafanya kila njia anitundike moja. Kwahiyo nimekuwa natumia vidonge kisiri siri bila ya yeye kujua.


Sasa nataka niache kutumia vidonge kwasababu nakuwa mnene sana, nataka nirudi kwenye kalenda kama zamani kwa ajili ya kuzuia mimba kwahiyo nikiwa naenda kutembea niwe naenda siku ambazo nipo salama ili nisishike mimba.


Nilisikia hapo nyuma kwamba ukiacha tu kutumia vidonge unapata mimba, hivi ni kweli? na ili nisiweze kupata mimba natakiwa nisifanye mapenzi kwa muda gani? najua wewe sio dactari ila kwa uzoefu wako na mawazo unaweza kunisaidia kwa hili kwani sijui nafanyaje.
Warda"

Dinah anasema: Poa sana Warda, vipi wewe? Mzima kabisa? Kweli mimi sio Daktari na sina uzoefu na utumiaji wa dawa za kuzia mimba either, ila inasemekana kuwa ukiacha kutumia dawa za kuzuia mimba na kurudi kwenye njia ya kawaida unakuwa kwenye hatari ya kushika mimba haraka au kutoshika kabisa kutokana na mkanganyiko wa homono uliosababishwa na dawa ulizokuwa ukitumia. Huwa unaingilia mzunguuko wako wa hendi.

Nijuavyo mimi mtu yeyote anaetaka kurudi au kuanza kutumia njia asilia kuzia mimba anatakiwa kufuatilia mzunguuko wake wa hedhi kwa muda wa miezi sita angalau ili kuwa na uhakika kuwa mzunguuko wako umejirudia, kwamba unakwenda siku 28 tu kwa muda wa miezi sita. Kama ambavyo mwanamke yeyote ambae hajawahi kutumia dawa za kuzia mimba bali condom /kutolea nje lakini sasa anataka kutumia njia asilia ( kalenda) kuzia mimba.


Ushuari wangu ni kwenda kwa Daktari aliyekupa aina ya dawa za kuzuia mimba na kuzungumza nae na yeye akupe ushauri wa kitibabu zaidi since umekuwa ukizuia mimba kitibabu.

Kabla sija maliza ningependa utambue hili, Suala muhimu na la msingi unachotakiwa kuzingatia ni kutokufanya jambo lolote litakalo kuathiri wewe au kubadilisha mwili wako kwa sababu ya mtu mwingine hata kama unampenda kuliko unavyojipenda wewe.

Kama uhusiano wenu sio serious, Condom ndio njia pekee na salama kutumia kuzia mimba na maradhi mengine ya Zinaa. Wote wawili mnapaswa kuchukua jukumu la uzuiaji wa magonjwa na mimba na sio wewe peke yako as mwanamke.

Kama yeye anataka kukumimba kama jaribio kuwa yeye ni "rijali" na wewe sio Tasa ili atangaze ndoa basi ni vema akaliweka wazi hilo ili wote wawili mkaangalie afya zenu za uzazi na wataalam wa masuala hayo.....sio anajiamulia tu kuwa "nataka kukutia mimba" wakati wewe mwenyewe huna uhakika kama uko tayari kuwa mama....

Mpenzi wako ni mbinafsi sana, kutokanana maelezo yako yeye anataka kukutundika mimba na sio "nataka tuzae".

Kila la kheri!

Tuesday, 19 January 2010

Achojoa na kuniacha nimchezee, hataki uhusiano wala ndoa.....

"Pole sana dada Dinah kwa ushuri, Mimi nimepanga chumba kwenye nyumba moja hivi na huko nilimkuta dem ambaye tulizoeana sana,alianza taratibu mwenyewe kunichezea na kunivulia nguo na kunionyesha mapaja na aina ya chupi aliyovaa.

Ili nisionekane kama sifanyi kazi nikaamua kuomba kutomba, akakataa eti hanipendi pia eti tupo vyumba jirani!!! Lakini akija tunachezeana kama mtu na mpenzi wake. Akiona nimekolea na kuomba zaidi anakimbia eti hanipendi, huwa namvua nguo na kubaki na chupi na kumnyonya maziwa nk.

Lakini mimi huwa hapendi nivue, nimemwambia kama hataki kutombwa na kuachwa basi akubali tufanye mipango ya ndoa!!!!!!!Anasema hanipendi na hawezi kuolewa na mimi. Lakini nikichelewa kurudi nyumbani anapipiga simu mara kibao akiniulizia nikowapi? na mambo mengine mengine.

Akisikia naongea kwenye simu anakuja kusikiliza kama akihisi anayeongea upande wa pili ni mwanamke tunaongea mambo ya biashara, huyu demu yeye ni ugomvi tu.
NAOMBA USHAURI WENU HUYU DEMU NI VIPI??, SIMUELEWI KABISAA!
NI MIMI WA KAWE."

Dinah anasema: Huyu binti ni mdogo na ninadhani yupo kwenye kile kipindi cha ukuaji ambacho ni kigumu na kinachanganya sana, kwamba anajaribu kuujua ujinsia wake. Kipindi hiki wote tunakipitia lakini kutokana na malezi/mazingira wengi huwa hatupati nafasi ya kufanya anayofanya huyu binti kwani yeye yuko huru na anafuata hisia za mwili wake zinavyomtuma na hivyo kufanya hayo afanyayo kwako......huu ndio mwanzo wa mwanamke kujua kuwa yeye anavutiwa na wanaume (ujinsia wake).

Ndio maana miaka 3 ya mwanzo baada ya Binti kuvunja Ungo mabinti wengi hupewa ulinzi mkali nakupigwa marufuku kukaa karibu na wanaume/watoto wa kiume na kwa baadhi ya makabila binti huwekwa ndani(mwali) au kuchumbiwa ili asishike mimba na kuwapa wanafamilia aibu.

Inawezekana kuwa hana uhakika kuwa anakupenda au hakupendi kwani yeye mwenyewe hajui anataka nini japokuwa anafurahia na kauridhika kuchezewa na wewe ila hayuko tayari kungonoka. Hii pia inawezekana ni kutokana na uoga wa kupata HIV au mimba au vitisho kutoka wa wazazi.

Mimi nakushauri usimruhusu tena kuingia chumbani kwako na kuanzia sasa achana nae na tumia muda wako mwingi kuzingatia shughuli zako za kibiashara na kujenga maisha yako ya baadae na ikiwezekana kuhama nyumba hiyo.

Kuwa muangalifu utakapokuwa unafanya uamuzi huu kwani kwa hasira binti huyu (ambae inaonyesha anasumbulia na homono za ukuaji) anaweza kukufungulia kesi ya kumnyanyasa kijinsia au kutaka kumbaka na watakusweka ndani, si unajua Bongo tuna Sheria zinazomlinda mwanamke? Japokuwa ktk hali halisi yeye ndio anaekunyanyasa wewe kijinsia, lakini ukweli ni kuwa linapokuja suala la ngono mwanamke huwa "hana nguvu".

Kumbuka anaweza kuwa na ushahidi as anakuja kwako na kukukoleza, anaweza kuchukua picha kwa kutumia kamera ya simu.

Kila la kheri.

Monday, 18 January 2010

Nahisi Mke mtarajiwa hataki ngono tena-Nifanye nini?

"Heri ya mwaka mpya Dinah. Kwa pamoja tumshukuru Mungu kwa kutufikisha salama 2010, Muongo mpya kama ulivyosema. Pili nikushukuru wewe kwa shule nzuri ndani ya blog yako. Bado tuna matumaini makubwa sana kutoka kwako ndani ya muongo huu mwingine.

Ingawa najua kuna Makala nyingi sana zimeandikwa hapa kuhusu namna ya kulianzisha kwa pande zote mbili, uzoefu wangu kwa mpenzi niliyenaye ni kuwa kama sikuanzisha mie basi tutakaa hata miezi 6 bila kungonoka.


Huyu mwenzangu tunaishi naye na tuna mtoto mmoja. Mtoto ana miaka 3 sasa na tuna mpango wa kufunga ndoa karibuni. Je hili ni tatizo la kila mwanamke au kuna kitu kinamfanya asiwe na hamu ya kufanya ngono na mimi?

Je kuna mapenzi hapa au tunazinguana? Mara kadhaa amekuwa akisema kuwa hafiki kileleni. Nimejaribu kuongea naye yeye husema kuwa kabla ya kungonoana basi lazima nimwandae, sasa kama yeye mwenyewe hana hata wazo je huku si ndio husababisha kumwandaa kuchukue muda?

Nitafurahi kama wadau watasaidia nao kuelezea uzoefu wao kwenye ngono.
Taza."

Dinah anasema:Heri ya Mwaka Mpya nawe pia Taza. Hakika ni jambo la kumshukuru Mungu kutuwezesha kuingia kwenye Muongo huu mpya. Mwanamke kushindwa kufika kilelenia u hata kulianzisha kuna weza kusababishwa na mambo machache ambayo nimekwisha wahi kugusia kemye Makala za mwanzo.

Sina uhakika mpenzi wako alikuwa vipi kabla hamjapata mtoto, yaani yeye kuzaa (maelezo zaidi yangesaidia). Mwanamke kushika Mimba na kuzaa ni wazi kuwa mwili wake unabadilika kwa kiasi kikubwa.

Kama binti huyu hakuwahi kupata/sikilizia utamu wa ngono na kabla hajakaa vizuri kitu na box(mimba) ni wazi kuwa imemuondolea ile hali ya kutaka kufanya tendo na wewe kwa vile hajawahi kulifurahia, hivyo anahisi kuwa ni wajibu zaidi kuliko "mapenzi".

Kutegemeana na "uponaji" wake pia ushirikiano kutoka upende wa pili (mwanaume) inaweza kumchukua muda mrefu mwanamke huyo kabla mwili wake haujatengemaa na kuwa kama ulivyokuwa awali (Kabla ya kuzaa) japo kuwa kuna mabadiliko mengine ambayo ni ya kudumu lakini wewe kama mpenzi wake unaweza kumsaidia na akakubali kuwa hiyo ni hali halisi na hivyo kuzoea mabadiliko hayo.


Suala la mwanamke "kulianzisha" sio rahisi kwa wanawake wengi wa wa kibongo, kwa vile wanahisi aibu/Umalaya. Vilevile inawezekana mpenzi wako ni mmoja kati ya wale wanawake wenye kasumba kuwa Ngono hutakiwa na wanaume tuna wao wako pale kuwapa wanaume hao kila wanapotaka kungonoka.

Kitu kizuri mpenzi wako amejitahidi na kuwa wazi na kukuambia kuwa hafiki kileleni, hivyo ni wajibu wako wewe kama mwanaume kutafuta mbinu za kumfikisha kileleni na siku akifanikiwa kufika kileleni nakuhakikishia mpenzi wako atalipenda tendo hili na kulitaka mara kwa mara.

Njia rahisi ya kumfanya mpenzi wako apate kujua utamu wa ngono ni kumfanyia Katerero ya Uume au Ulimi, kwamba unachezea uke na "vitongoji vyake" kwa kutumia Uume au Ulimi wako (Tafuta topic ya katerero na ile ya kumshukia mwanamke), raha ya mtindo huu unaweza kuutumia kama "maandalizi" na tendo.

Kwamba akifika kileleni kupitia kisimi ute utaongezeka (ile cum) na kukurahisishia wewe kuingia ukeni bila taabu, sasa kwa vile tayari kasikilizia utamu na mara ukaingia all the way ndani na kuendelea kupiga takozi taratibu kwa mapenzi yako yote hakika utampa raha ya pekee na ukiwa na bahati anaweza kupata bao la pili huko ndani (inategemea zaidi na ufanyaji wako pia yeye kujituma).

Pia jaribu kuandaa mazingira kwa ajili ya tendo pia tumia muda mwingi kumuandaa, onyesha kuwa unaupenda mwili wake kwa kuuchezea, shika, lamba, busu na kuunyonya.

Taza, anza kumpa ushirikiano mpenzi wako, onyesha mapenzi ya kihisia zaidi mara kwa mara, onyesha kuwa unampenda mpenzi wako na unataka sana kufunga nae ndoa, hakikisha anajua kuwa unavutiwa na kila kilicho juu ya mwili wake (kuna uwezekano kapoteza hali ya kujiamini baada ya kuzaa na kunyonyesha).

Hakika tumbo lake litakuwa na ukubwa fulani hivi, na matiti hayapo kama yalivyokuwa miaka michache iliyopita kabla hajazaa,........pia Kisaikolojia uzazi umemfanya aihisi kuwa havutii tena kama mwanamke na hana uwezo wa kukuridhisha kingono.

Kama mmekuwa pamoja kwa muda kiasi na sasa mnamtoto wa miaka 3 na wewe bado hujachumbia na wala huna dalili yakufanya hivyo kama sio hamzungumzii suala la kufunga ndoa, hii inaweza kuongeza mzigo wa mawazo kwa mama huyu kuhusiana na maisha yake ya mbele......fanyia kazi hili pia.

Mengine ni ya kike zaidi na hata nikikueleza wewe hutoweza kuyawakilisha ipasavyo kwa mpenzi wako. Kama unaweza basi muelekeze kwangu ili nipe ile 1-2-1 ili nijue tatizo ni nini na kumpa hizo mbinu za kike ili wewe na yeye kufurahia maisha yenu ya ndoa kama kweli unakwenda kufanya hivyo.

Nakutakia kila la kheri.

Saturday, 16 January 2010

Mume ataja jina la binti yetu wakati wa Tendo!-Ni kawaida?

"Dada dinah habari ya mwaka mpya natumaini mwaka umeuanza vizuri. Mimi ndio mara yangu ya kwanza kutuma swali langu lakini ni mpenzi wa blog yako.


Mimi nimeolewa na ndoa yetu imejaaliwa mtoto moja wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, mimi na mme wangu tumekuwa pamoja kwa miaka mitano sasa. Jana (1/01/10 ndio ilikwa mwaka mpya hatukutoka tulikuwa tu home kwavile nchi tuliyopo ni baridi sana na snow kwa kwingi sana.


Hivyo tuliamua kukaa home na fungua mwaka mpya home, ilipofika saa sita kufunga mwaka na kufungua mwaka tulifungua champagne na kunywa kwa furaha tukakaa mpaka saa saba usiku ndio tukaanza kufanya mapenzi, yaani mwanzo ilikuwa poa sana mara katikati ya mapenzi ndio mme wangu akataja jina la mwanangu badala ya jina langu katikati ya mapenzi.


Tulivyo maliza mavitunzi ndio nikamuliza kuhusu kuita jina la mwanangu katikati ya mavituzi, akasema amezoea kuita hilo jina all the time ndio maana amejisahu na kuita hilo jina. Dada dinah naomba uniambie kama hii ni kawaina na kama imewahi kutokea kwa watu wengine hapa.
Naombeni michango yenu.
Ni mimi Samatha"

Dinah anasema: Samatha asante kwa email yako, lakini naomba kuuliza kidogo kabla sijakupa maelezo na pengine itasaidia watu wengine kukupa michango ya uhakika zaidi. Je hilo jina la mtoto ni nani alichagua? Mumeo na wewe ukakubali au wewe na yeye akalikubali? Je jina la mtoto na lako linafanana kwa mbali Mfano Dinah na Daniela, Maria na Marian/Mariam n.k....inawezekana ni jina la Ex n.k.

Huenda alitaka kukuita mama____(jina la mtoto) na akaishia jina la mtoto akasahau "mama".

Asante Samatha kwa nyongeza ya maelezo (nenda kwenye comments), naungana na mchangiaji aliyehoji Uraia/Makuzi ya mumeo, hakika sio ubaguzi lakini sio watu wa mataifa mengine tu wanawarudi watoto wao. Hapa Tanzania wapo wengi tu lakini kutokana na kulinda "heshima ya familia" watu hukaa kimya nakutunza siri.


Natambua inaumiza kumfikiria mumeo jinsi ambavyo watu wengine wanamdhania, lakini mimi nakuomba ufanye ushunguzi bila kumuuliza binti wala baba yake. Kuwa karibu zaidi na binti yako ili kuondoa wasi wasi. Samahani kama maelezo hayo yatakuwa yamekukwaza. Inawezekana hajawahi kumuingizia wala hana mpango huo ila huwa anamchezea-chezea.


Ujue watoto wa kike huwa tunakuwa karibu sana na baba zetu, lakini kutokana na mazingira yetu hapa Bongo inakuwa ngumu sana kuwa that karibu na baba, yaani baba hapewi nafasi ya kubadili nepi ya mtoto wa kike achilia mbali kumuogesha.

Lakini kwa watoto wa nje ya Tanzania huwa karibu zaidi kutokana na mazingira baba hulazimika ku-baby sit wakati mama anaenda kazini n.k. hivyoinawezekana kabisa mtu akaibua a sick tabia ya kumchezea mwanae wa kike ktk harakati za kutafuta namna ya kumbembeleza n.k.

Kuna babaz wanawazoesha kuwachezea watoto wao wa kike na kuwapandikiza imani kuwa "baba anakupenda ndio maana anafanya hivi". Wengine wanaimani za kishirikina, ili kufanikiw abasi mudi mwanao, baadhi hulazimika kuwarudi watoto wao kama sehemu ya Mila....wenyewe wanaita Suna!

***************************MUNGU APISHE MBALI!

Tendo la ndoa ni tamu, ni takatifu linawafanya wote wawili kuwakaribu zaidi in a way mtu mwingine yeyote hawezi kujua achilia mbali kuhusika. The moment na utamu wake, mihemo na sauti za mahaba, harufu za majimaji ya miili yenu na namna mnashikana n.k hakika HUWEZI kabisa kulopoka jina la mwanao au la mtu mwingine yeyote unless otherwise umewahi ku-share the momet like that with au u r willing to do so!


Haijalishi unapata utamu kiasi gani au wewe mwanamke ni mlopokaji kiasi gani, huwezi kabisa-kabisa kumtaja baba yako au mtoto wako wa kiume. Katika hali halisi wanaume ni wagumu sana kulopoka-lopoka wakati wa tendo na wanapofanya hivyo ni wazi kuna uhusiano mkubwa kati ya jina na tendo (amewahi/anafanya ngono na mtu mwenye jina hilo).


Kama jamaa ni mbongo na anakuita mama nanihii time 2 time ni wazi alikusudia kukuita hivyo il akasahau neno "mama", pia inawezekana kabisa kuna mtu alimkaa sana kichwani (alimpenda kupita kiasi) na utamu alioupata siku hiyo ulimkumbusha huyo mtu mwenye jina linalofanana na mtoto wenu.

Kutokana na uzoefu wangu, wanaume wanatabia ya kuita binti zao majina the last Ex b4 mke aliemuoa hasa kama walipendana sana enzi zao ila mmoja hakuwa tayari kuendelea mbele. Kuna Njemba moja iliwahi kuniambia "Dinah hata kama tukiachana, nikioa nakubalikiwa kuzaa mtoto wa kike lazima nimuite Dinah"......which kafanya hivyo!


Pia inawezekana ni character kwenye Porn movies ambayo mumeo anaipenda namlipokuwa mkifanya akili yake ilikuwa ikimfikiria huyo mtu wa kwenye Kideo, lakini ktk kujitetea ikabidi aseme kuwa alimtaja mtoto kwa vile anamuita na kumtaja kila wakati ili kulinda hisia zako.

Sasa Samatha, kama ni jina la Ex au Porn star basi let it go kwa sasa, akirudia tena kutaja jina hilo ni wazi mtahitaji kuzungumza kuhusu hilo Jina kwa undani zaidi.

Amos, amegusia kitu muhimu sana kwa jamii yetuya Kibongo, baba kuchagua jina la mtoto wa kiume na mama kuchagua jina la mtoto wa kike.

Kila la kheri mdada.

Friday, 15 January 2010

Nikiiingiza tu analia, huwa namuandaa vizuri, tatizo ni nini?

"hi its me mick Please ma sister naomba unishauri kwasababu mpenzi wangu kabla ya tendo huwa namuandaa vya kutosha namyonya kila kona siachi sehemu mpaka anakataa mwenyewe lakini kinacho nishangaza nikianza kuingiza tu huwa analalamika anaumia mpaka analia sasa mie nashindwa kumuelewa. tatizo ni nini?"

Dinah anasema:Hello Mick, asante kwa ushirikiano. Kuna machache yanayoweza kusababisha mpenzi wako kulia na la kwanza ni hili, huenda wewe ndio unaamini kuwa unamuandaa vya kutosha labda kwasababu wewe unakuwa tayari kama sio kuwa umechoka kwa vile unazingatia maeneo unayoyajua wewe na sio yale "yanayoibua" hisia za mpenzi wako.

Pili, kama baadhi ya wachangiaji walivyogusia, inawezekana maumbile yako ni makubwa kwa mpenzi wako na hajayazoea (inachukua muda kidogo mpaka aizoee).

Tatu, Kunauwezekano kuwa mnafanya ngono mara chache, kwasababu mwanamke akikaa muda mrefu bila kufanya ngono uke wake "husahau" na siku akifanya ngono hupatwa na maumivu mwanzoni lakini baada ya muda kidogo huku wewe mwanaume ukifanya taratibu na kumpa matumani kuwa unafanya polepole huku unamfanya ki-passionate maumivu huisha na kila kitu kinakuwa safiii mpaka mwisho.

Nne, huenda mnafanya kwa wizi (kama bado ni mwanafunzi, anaishai kwao na mnafanya ngono kwa washkaji n.k), hamtumii kinga (hofu yakushika mimba/magonjwa ya zinaa), sumu ya utamu wa ngono kwa mwanamke ni kuifanya ukiwa na hofu, hakika hutoweza kuwa tayari (kuandalika).

Tano, isije kuwa ukihisi ute ukeni wewe unadhani yuko tayari. Mwanamke kuwa na ute ukeni sio dalili kuwa unawez akuingiza, unatakiwa kuendelea mpaka uhisi ule ute unakuwa kama unadondoka hivi au kama una haraka sana basi tumia kidole chako kuingiza nakumchezea mpaka uone anatoa mihemo ya "give 2 me" alafu ndio ingiza uume na wakati unaendelea na tendo hakikisha unanyonya chuchu zake, kula denda, tafuta shingo, ulimi sikioni, kumshika hapa na pale ili kuongeza raha na kuufanya mwili wake usisahau kile kinachoendelea.

Na mwisho kabisa, aliyemtoa bikira hakufanikiwa kuingia ndani hivyo basi misuli yake ya uke haiko tayari kupokea kiungo chako, kama nilivyosema tena hapo awali itachukua muda kiasi na mnachotakiwa kufanya ni kufanya Ngono mara nyingi zaidi (kama inawezekana) kila mnapokutana.

Mfano kama mzunguuko wa kwanza anadai anaumia, jitahidi kufanya ki-passionate na hakikisha siku hiyo mnafanya hata mara tatu nakurudia tena siku nyingine in the same week so mtakuwa mmefanya mara sita ndani ya wiki moja......kama inawezekana, usilazimishe.

Kilala kheri!

Wednesday, 13 January 2010

Nilishika mimba 2008, sasa natokwa maziwa!-Ushauri

"Mambo Da dinah
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23, sijaolewa na sijawahi kuzaa, sasa tatizo linalonisumbua ni hili:

Siku hizi natokwa na maziwa kwenye chuchu wakati zamani haikuwa hivyo, Alhamis this week tukiwa tunapeana mapenzi na my boyfriend aligundua kua chuchu zangu zinatoa maziwa japo kwa wakati huo hakuniambia mpaka tulipomaliza game na kukaa kwa muda ndipo akaniambia kua amegundua chuchu zangu zinatoa maziwa na kweli nilipozibinya maziwa yalitoka.

Niliwahi kupata ujauzito mwaka jana japo nilipewa dawa nikameza na siku yangu ya period ilipofika nilibleed kama kawaida bila kuona tofauti yoyote, mimba hiyo sikuitoa hospital isipokua nilimeza dawa tu tena nilipewa vidonge viwili tu na nikaambiwa nitapata period kama kawaida na ndivyo ilivyokua.

Niliendelea na mapenzi japo sikuwahi kutokwa na maziwa katika chuchu zangu, sasa nauliza je? hii ni kawaida au? sielewi kwa ufupi nachanganyikiwa.
Asante dada.
Mourine."

Dinah anasema: Mourine mpendwa naomba unipe majibu kwa maswali yangu haya ili uweze kupata ushauri wa kutosha. (1)-Ulikunywa dawa hizo kwa nia ya kuizuia mimba isiendelee kukua (kutoa mimba ikiwa changa) sio? Mara nyingi Nesi/Daktari) hutoa maelezo ya kutosha kuhusiana side effects za dawa yeyote wanayokupa hata kama ni ya kutibu Maralia. Je unajua side effects za dawa ulizokunywa?

Mourine: ni kweli nilimeza dawa ili nisiendelee kuwa mjamzito lakini niliambiwa zile dawa madhara yake ni endapo ningeendelea kuzitumia mara kwa mara zinapunguza aina fulani ya homon, baada ya kutimiza lengo sikuzimeza tena.

(2)-Unatumia aina yeyote ya dawa za kuzuia mimba?

Mourine: Sijawahi kutumia dawa zozote za kuzuia mimba.

(3)-Ni mpenzi wa kula nyama za kuku na ng'ombe, Nguruwe wa kisasa (wananenepeshwa/kuzwa kwabla ya wakati kwa madawa)?

Mourine: Huwa nakula lakini napenda zaidi nyama ya Nguruwe.
asante da Dinah.

Dinah anaendelea: Mourine asante kwa kunipa majibu haraka. Mwanamke akishika mimba mwili wake hubadilika ili kuwa tayari kupokea mtoto, sasa kwa vile wewe ulisitisha ukuaji wa mimba ambayo ilikuwa imeandaa mwili wako tayari kwa mtoto.

Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa tangu uumesitisha ukuaji wa mimba ni mwaka mmoja katika hali halisi mwili wako utakuwa bado unakabiliana na mabadiliko hayo ili kurudia hali yake ya kawaida, kwa mama aliyezaa na kufanikiwa kunyonyesha mabadiliko hayo hutoweka ndani ya miezi tisa mpaka miaka miwili (inategemea na mwanamke husika), hivyo basi na wewe unapaswa kuwa mvumilivu na baadayamuda mwili wako uta-settle na hutopata tatizo ulilonalo.

Punguza au acha kabisa kula nyama nyekundu (mbuzi, Nguruwe, Ng'ombe, Kondoo) ili kujipunguzia protini inayosemekana kuwa ni muhimu ktk utengenezaji wa maziwa kwa ajili ya mtoto.

Vilevile kuna tetezi kuwa Nyama hizo nyekundu na kuku wa kisasa hukuzwa kwa mchanganyiko wa madawa ya kuzuia mimba (madawa hayo yana homono nyingi) hivyo ukila mara kwa mara unajiongezea homono bila mwenyewe kujua.

Badala ya kula nyama hizo nakushauri ujitahidi kula zaidi mboga-mboga, samaki na mboga jamii ya Kunde (dengu, maharage, kunde, mbaazi n.k.natambua jamii ya kunde ina mchanganyiko wa virutubisho vingi muhimu ikiwa ni pamoja na sehemu kidogo ya protini) mpaka mwili wako utakaporudia hali yake ya kawaida.

Tumia Condoms ili kuzuia mimba, kusitisha ukuaji wa mimba ni kutoa mimba ktk lugha nyepesi. Tafadhali jitahidi wewe na mpenzi wako msirudie kosa hili tena.
Kila la kheri!

Thursday, 7 January 2010

Mpenzi karudi Ulaya na kukata mawasiliano je nimeachwa?

"Dada Dinah pole na hongera sana kwa kazi nzuri.
Mimi ni msichana wa miaka 28, Naomba ushauri kama ifuatavyo. Nina mpenzi wangu wa muda mrefu nampenda sana, alikuwa Ulaya kwa miaka 3 na tulikuwa tunawasiliana vizuri sana.

Akarudi hapa bongo kurenew Visa yake na tulikaa pamoja vizuri kipindi chote hicho, siku moja nikamuuliza je vipi kuhusu maendeleo ya uhusiano wetu? akasema kwa sababu kazini kapewa wiki tatu tu za kuwa hapa Bongo hatutaweza kufanya lolote.


Akaniahidi kuwa ikiwa atanyimwa kibali cha kurudi huko Ulaya basi tutaendelea na mambo yetu na akifanikiwa kuongezewa muda basi ataenda Ulaya halafu atanitumia mwaliko, akaniambia nimsaidie kusali apate kwa sababu akikosa itamchukua muda mpaka atafute kazi hapa Tz.


Mimi nikasali, na kweli Mungu akatusikiliza alivyoenda Ubalozini akapata Visa na akarudi zake Ulaya, November mwishoni 2009, tukawasiliana siku tatu tu, mara mawasiliano yakakata nikamtumia sms nikimuuliza vipi mbona siku hizi kimya sana? hakujiibu, na mara akawa hapokei simu na wala hajibu email wala sms kwa mwezi sasa.

Hapa nimebaki nashangaa nini kinaendelea tena?wakati tulikuwa ok kabisa. Kinachoniuma ni kwa nini hataki kuongea na mimi? kwa nini hapokei simu?na ni kwa nini hakuongea nami kuhusu mipango yake alipokuwa hapa?
Nifanye nini?naombeni ushauri.
Pne"

Dinah anasema:Asante sana kwa mail yako na pole kwa maumivu ya moyo na hofu kuu uliyonayo juu yampenzi wako, isije kuwa mpenzi wako kapatwa na masahibu makubwa huko aliko. Hebu kwa kuanzia tu ili kupata amani moyoni, check na ndugu au jamaa zake wa karibu kujua kama Mpenzi ni mzima huko aliko alafu tunaendelea na mengine nikirudi......

Mungu apishe Mbali!

Wednesday, 6 January 2010

Jamani nijuzeni, nahisi kupunjika kingono!

"Hello dada Dinah,
Pole na kazi na mambo ya uelimishaji jamii, dada sijatembelea blog yako kwa muda. Nimeingia hapo juzi nikaona mambo ya kusisimua sana. Yaani nimebloo! hongera!

Ila nimetatizwa na kuchanganywa sana na shauri moja lililopita hapo kuhusu mwanamke kukojoa. Yaani nimechanganyikiwa na kupagawa na ninaomba msaada wa kujua mambo wawili matatu maana napenda sana ngono yaani na nataka niifaidi haswa maana nahisi kupunjika.

Dinah anasema:Hongera kwa kuipenda ngono, ili ufurahie tendo hili ni lazima kwa ulipende. Ni matumaini yangu kuwa unaipenda ngono pale unapoifanya na mpenzi wako ulienae kwenye uhusiano.
**************************************************

Nini maana ya G-spot na U-spot na ninawezaje kujistarehesha nayo mwenyewe ili niione hiyo raha yake? pia nataka kujua kama nikitiwa kidole/vidole vya huku tigoni, ni kweli nitasikia hiyo raha inayoongelewa hapa na kufikia hicho kilele???

Dinah anasema: G-spot haina maana halisi ila G ilitokana na jina Ernest Grafenberg ambae alikuwa ni Gynaecologis wa Kijermani ambae ndio aliigundua kona hiyo ya kumpa mwanamke utamu wa ngono, yeye hakuiita G-spot bali jina lingine la kingono-ngono ila vijana wa kizazi kile ndio wakaibuka na G-spot kama sehemu ya kumuenzi Mtaalam huyo(kama ilivyo kwa magonjwa na Tiba kupewa majina ya wagunduzi wake).


Kutokana na uzoefu wangu G-spot husisimka kwa haraka zaidi ikiwa uume unafanya kazi huko ndani ya uke, vilevile Kipele G kinasisimka kwa kutumia kidole lakini sina uhakika kuhusu kidole chako mwenyewe mwanamke as mimi sijawahi kujiingizia kidole kwa nia ya kupata raha ya ngono bali kujisafisha.

Utamu wa mahali hapa ukipatiwa kwa kutumia uume ni hauna mfano! Yaanii bao lake ni la nguvu mno na linaweza kukufanya upoteze fahamu kwa sekunde chache (mimi huwa naita kuzimia), Utamu wa kipele G hudumu kwa muda wa dk5.

U-spot ipo katikati ya tundu la mkojo (chini kidogo ya kisimi) na uke (pake uume unapoingia au damuya hedhi inapotokea) au kwa kukurahisishia wacha niseme hivi; ipo chini kidogo ya tundu la mkojo (chini ya kisimi) na juu kidogo ya uke (unapoingia uume).

Utamu wa mahali hapa ni wa kawaida tu ukilinganisha na ule wa kipele G, baadhi ya wanawake wakichezewa vema kona hii kwa kutumia kidole, ulimi au kichwa cha uume (a.k.a Katelelo/Katerero-inategema unatoka wapi) basi hukojoa kama wanaume japokuwa sio manii bali ni mkojo like usio na harufu.

Maana ya G-spot au U-spot haikusaidii wewe kufurahia ngono, kujua wapi hizi kona zinapatikana na namna ya kuzifanyia kazi ndio muhimu zaidi na Amos Bwire amejitahidi kuelezea wapi kipele hicho cha G kinapatika.


Dinah anasema: Kuna raha fulani unayoipata mwanamke ikiwa utatiwa dole sehemu ya nyuma kama sehemu ya kuandaliwa, japokuwa inasemekana kuna wanawake na mwanaume wakipigwa dole wakati anakaribia kufika basi hufika haraka ila sina uhakika as mimi sio mmoja wa hao waliojaaliwa kupata raha ya Tigoni.

Nisaidie dada, naona blog yako imechangamka sana kwa haya masuala. Duniani kuna mambo lol! natanguliza shukrani za dhati,
Anna."

Dinah anasema: Hi Anna, asante kwa ushirikiano. Natumaini maelezo ya wachangiaji yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuhusiana na swali lako kama kawaida mimi nimeongezea machache yaliyokosekana kwenye maelezo hayo hao juu kutokana na maswali yako.

Mwisho napenda tu niweke wazi kuwa utamu wa ngono kwa mwanamke sio kama "kutaka kukojoa" utamu wa ngono hauna mfano na huwezi kufananaisha na kutaka kukojoa mkojo kutoka kwenye kibofu......ingawaje unaweza kuhisi kuwa unataka kukojoa kwa vile kibofu chako kimesumbuliwa wakati tendo linaendelea sasa ukiachia mkojo + utamu halisi wa ngono inakuwa bomba.

Inawezekana utamu wa ngono kwa wanaume huwa kama wanataka kukojoa (manii yanatoka utapotokea mkojo) ndio maana wanaume wengi hudhani kuwa na sisi wanawake ni hivyo hivyo ukweli ni kuwa utamu wa ngono kwa mwanamke ni wa ndani kwa ndani na sio lazima sana upate atokeo ya nje "kukojoa".......

Endelea kuwa mtundu na jifunze zaidi kuhusu mwili wako, ukiujua vema mwili wako na ukawa wazi kumuongoza mpenzi akufanyie nini na wapi, hutohisi kupunjika tena, utaridhika na utaendelea kulipenda tendo hili takatifu.

Kila la kheri!

Tuesday, 5 January 2010

Mpenzi kajaaliwa, je Uke wangu uko hatalini?-Ushauri

"Habari za leo dada dinah!
Nimerudi tena kwako nina suala ambalo linaniumiza akili, na sijui kama linaukweli au la! Dada dinah mie nina umri wa miaka 28, nina boyfriend ambaye maumbile yake kwa kweli kajaaliwa yaani nikingonoana nae wakati anaingiza uume wake hauingii mpaka apakae Gel kibao.

Tumekuwa pamoja kwa miezi karibia 7 sasa hali ndiyo hiyo hiyo japo kwa sasa hapaki Gel ila ndio inapita kwa taabu japokuwa huwa naenjoy kwani huwa ananiandaa vya kutosha mpk aiingie mie nimeshakojoa hata mara3. Kweli anajua hasa mwanamke anahitaji nini kitandani, wakati mwingine inafikia mpaka huwa sijitambui kwa hizo raha lakini kesho yake ndio nasikia maumivu ukeni ambayo hudumu kwa siku mbili na kuisha.

Sasa dada dinah kwa kawaida huwa nikijisafisha ukeni hata kidole huwa kinapita kwa taabu hasa kama nina wiki sijakutana na mwanaume, ila sasa hivi naona mabadiliko yani ni
kijisafisha kinapita tu tofauti na mwanzoni.

Nimejaribu kuwauliza baadhi ya marafiki zangu wananambia kwa kuwa huyu bwana ana maumbile makubwa na kwamba nitaharibika kwani huku chini kutatanuka na hata baade nikiwa na mtu mwenye uume tofauti na huo atakuwa anapwaya tu. Basi kinaninyima usingizi yani nawaza kuharibika sehemu zangu za siri halafu nikija kuachana nae itakuwaje?

Kumpenda nampenda, raha anazo nipa sitaki kuziacha yani hata sielewi. Hebu nisaidieni kama hili jambo lina ukweli na kama lina ukweli nitumie nini? au nifanye nini jamani? Uke wangu ubaki kama ulivyo."

Dinah anasema: Tafadhali tembelea Topic isemayo "Ngono inazeesha" kwa uelewa zaidi kuhusu uhusiano wa maumbile ya kike na ngono. Nafurahi kusema kuwa sehemu kubwa ya majibu na maelezo ya wachangiaji yametosheleza na hakika utakuwa umeridhika na kuondoa hofu ya maumbile yako.

Kila la kheri.

Friday, 1 January 2010

U've made it! Heri ya mwaka Mpya!!

Hongera kwa kumaliza Mwongo (Decade) na Kila la kheri unapokwenda kuanza mwingine. Nakutakia afya njema, maisha ya Ndoa/Kimapenzi mazuri, marefu na yenye mafanikio zaidi ya 2000-2009.
Akupendae na kukujali,
Dinah.Xxx