Monday, 27 December 2010

Mpenzi aninyanyasa kisa Umasikini, sasa ataka ndoa, je atabadilika?

"Habari dada Dinah, Mimi ni msomaji mkubwa wa Blog yako na ninapenda Posti kwani zimetusaidia wengi. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 natokea Mkoani Tanga lakini kwa sasa naishai Zanzibar na mpenzi wangu alienichukua nyumbani.

Ninamshukuru Mungu kwani mpenzi wangu ananijali na kunitimizia mahitaji yangu ikiwemo na kuwasaidia wazee wangu nyumbani. Lakini huyu mpenzi anasema kwa kila mtu alie karibu nae kuwa kwetu ni masikini na sote tunamtegemea yeye. Hali hii huzidi hasa tukiwa na ugomvi.

Nimewahi kumwambia mara kadhaa kwamba sipendi tabia yake hiyo, lakini bado hana dalili yeyote ya kuachana na tabia hiyo. Ikitokea ananigombeza basi huwatusi mpaka wazee wangu jambo ambalo hunitia uchungu sana.

Zaidi ya yote anasema hafurahii sana ladha ya tendo la ndoa kwa hiyo anataka tufanye kinyume na maumbile, kitu ambacho mie siwezi kuthubutu kukifanya.

Kwa bahatimbaya au nzuri nimekutana na Kaka mmoja Mzanzibari ambae anadai kuwa ananipenda sana na yupo tayari kufunga ndoa nami nikamwambia kuwa ninampenda lakini kuna mtu ninaishi nae.

Kusema ukweli ninampenda huyu Mkaka niliekutana nae, aliomba akanitambulishe kwao lakini mimi nikamuomba akanitabulishe kama rafiki kwani sikutaka wajue kutambulishwa kama mpenzi wakati niko kwenye uhusiano na mtu mwingine japo sina amani.Familia yake walionyesha kunipenda.

Tatizo linalonisumbua ni kuwa huyu mpenzi ninaeishi nae ametangaza ndoa, lakini mie sitaki kuolewa nae kutokana na tabia zake za kinyanyasaji, sasa sijui nimueleze mama yangu ukweli wa mambo ili nipate mawazo yake au nikubali kuolewa nae kwa kuamini kuwa atabadilika!!

Au nitafute njia ya kuachana nae ili niwe na Kaka wa Kizanzibari alienitambulisha kwao kama rafiki lakini nia yake ni kufunga ndoa nami?

Naombeni ushauri
Asante"

22 comments:

Anonymous said...

Achana na hili levi, hata badilika hata chembe. Na kasha anza kuomba mambo ya nyuma huyo si mtu mwenzangu. Ushauri wangu rudi kwanza kwenu kwa amani then huyo mkaka wa zanzibar kama kweli anakupenda aje akufuate kwenu. Mana ukihamia nyumba moja kwenda nyingine isije ikawa taaaaaaaaaabu badae kuwa oh huna muamana ulimuacha mpenzi aliyekuleta huku kisa mie. Aje kwenu alipe nauli na mahali kama inawezekana na mara shoga ukienda uwe umeolewa kuliko kupelekwa kama kimada tu. Wewe ni msichana umri mdogo tu usikimbilie kuolewa na mume mnyanyasaji ukitegemea akikuoa mambo yatabadilika. Kwanza akikuoa ndo manyanyaso yatazidi kuwa umekubali kuolewa naye sababu ya dhiki.

Huyu mwanaume tena si wa kuendelea naye unaweza ukawa umelala ndani ya nyumba akakufanyia kitu mbaya. Rudi kwenu huyo mpenzi mwingine aje akupatie kwenu na ndoa kabisaaaaaaa. Usikubali kubebwa tu

Anonymous said...

Kwanza pole dada kwa kuwa na kijanaume chenye jeuri kiasi hicho, unajua umaskini hukuumbiwa wewe na yeyote hapa duniani aweza kuwa maskini kutegemea na umaskini wake ni wa nini!!! Huyo mchumba wako jeuri inaonyesha ana umaskini wa kifikira na automatically he is not good for you, usije ukafanya makosa kufanya maamuzi unayositasita yataja kukuta makubwa kwa huyo jamaa. Maamuzi ni yako wala si ya mtu mwingine, kupenda na kupendwa ni nafsi ya mtu na si kundi la watu, wazazi ndugu nk sana sana hao wataishia kukushauri tu tena kwa kukuangamiza ama kufanikiwa kutegemea na maslahi binafsi. Sasa basi, ushauri wangu kwako ni kuwa kama kweli umempenda huyo kaka mzanzibari na hakuna kipingamizi chochote na wadhani kweli moyo wako umeridhia na umeshamfahamu please nenda uolewe naye na haihitaji kuhofu na kuogopa maana hayo ni maamuzi yako na ni uhuru wako kuamua kufanya hivyo. Huyo mchumba wako wa kwanza anayetaka hata kukuingilia kinyume na maumbile ikitokea kakuoa na kakuweka ndani sidhani kama kweli atabadilika na kuwa mwema kwako, anaweza hata kukuwekea madawa ya usingizi ili akuingilie kinyume na maumbile wakati unajua kabisa dini zetu haziruhusu kitu kama hicho na ni dhambi isiyosameheka mbele ya mwenyezi Mungu. Ni hayo tu.

Anonymous said...

Ingawa watu husema wanawake hatupendani, ushauri ninaokupa ni kwa vile nakupenda kama mwanamke mwenzangu. Nimevaa viatu vyako na kuvisikilizia. Ushauri wangu ni kuwa achana na huyo bwana mwenye manyanyaso na kuhitaji kinyume cha maumbile. Si mstaarabu na wala usitarajie atabadilika. Kama leo hii tu wewe si mke anakutenda hivi unafikiri akishakumiliki atabadilika? Tena ndiyo atakuwa mbaya zaidi. Dada hata kama hujapata mtu mwingine achana na huyu maisha yako yatakuwa ni yakunyanyasika na lazima atakubaka kupata kinyume cha maumbile. Huyu si mme wa kuolewa naye, kimbia kabisa. Pili sioni kama kuna ubaya ukimshirikisha mama yako kwa hili.

Jamila said...

Oooh swittie ! pole sana mdada , ila nakushauri huyo kijana achana naye coz atakuumiza sana baadae uje juta ! Mi yalishanikuta ila kwa mkaka ambaye alikuwa hana pesa tunategemea kwetu ila siku "akizishika ni full kashfa " tukaoana ,nikampa mtaji alipowini majivuno na akasahau kila kitu mwisho akanitaliki miaka mitano iliyopita ! Hapa nna 30 yrs na kazi nzuri sitaki hata kusikia neno mwanaume for 5 yrs na naamini ntaweza zaidi !

Jamila said...

Oooh swittie ! pole sana mdada , ila nakushauri huyo kijana achana naye coz atakuumiza sana baadae uje juta ! Mi yalishanikuta ila kwa mkaka ambaye alikuwa hana pesa tunategemea kwetu ila siku "akizishika ni full kashfa " tukaoana ,nikampa mtaji alipowini majivuno na akasahau kila kitu mwisho akanitaliki miaka mitano iliyopita ! Hapa nna 30 yrs na kazi nzuri sitaki hata kusikia neno mwanaume for 5 yrs na naamini ntaweza zaidi !

Anonymous said...

ni heri nusu shari kuliko shari kamili! usithubutu kufunga ndoa na huyo mwanaume au la uwe umejitayarisha kwa masononeko na vilio vya milele for as long as mtakuwa katika hiyo ndoa. yaani utalia hadi utakoma mdogo wangu, ninaelewa ninachokuambia, mwanaume mnyanyasaji (emotion abusive husband)ni mbaya kuliko nyoka wa porini! achana naye kabla ya hiyo ndoa please! usijejuta wakati u real knew from the beginning. akili kichwani kwako

shushu hot said...

pole sana dada kwa masahibu yanayokukuta, mbona hapo jibu liko wazi tu! huyo unayeishi nae hakufai! anaonekan ni mnyanyasaji sana wa kijinsia mpaka kifedha, yani me ningekuwa wewe siku nyingi ningeshawaambia kwetu kuhusu tabia zake na ningekuwa nimeshaachana nae, na kuhusu huyo kaka mwingine aliekutambulisha kwao kaa nae umchunguze kwanza usitake kukimbilia kuolewa ukajikuta umeruka kojo ukatimba nyesi!

shushu hot said...

pole sana dada kwa masahibu yanayokukuta, mbona hapo jibu liko wazi tu! huyo unayeishi nae hakufai! anaonekan ni mnyanyasaji sana wa kijinsia mpaka kifedha, yani me ningekuwa wewe siku nyingi ningeshawaambia kwetu kuhusu tabia zake na ningekuwa nimeshaachana nae, na kuhusu huyo kaka mwingine aliekutambulisha kwao kaa nae umchunguze kwanza usitake kukimbilia kuolewa ukajikuta umeruka kojo ukatimba nyesi!

Anonymous said...

Shosti mbona unataka kujichanganya mwisho wa yote waweza kukosa vyote ukarudi kwenu Tanga. Anyway, sitaki kukulaumu kwani sababu ya yote ni huyo bwana unaeishi nae, mara nyingi unapokosa amani kwenye ndoa yako au kwa mpenzi wako, moyo unakuwa mwepesi sana anapotokea mtu mwingine wa kukuonyesha care. Ila kama hayo uliyoongea ni kweli kuhusu huyo unaishi nae kukutukania umaskini wa kwenu tena kwa watu mana ni bora angekuwa anakutukana wewe tu lakini kufikia kukusema hadi kwa watu wa nje huo ni udhalilishaji mkubwa sana, kifupi hafai nakushauri na kukusapoti 120% uachane nae hata kama kwenu hawata kubali mana pengine wanaweza kuwa wameshalewa na hizo senti wanazosaidiwa na huyo bwana kwahiyo watataka kukuwekea pingamizi usimuache, shosti usikubali kimbia tena bila kujishauri mana huko mbeleni itakuwa balaa zaidi ukizingatia anataka na nyuma ya maumbile, inaonyesha ni jinsi gani alivyo mchafu wa roho na mwili. Hafai muache haraka.

Huyo bwana mwingine nakushauri endelea nae, ila uamuzi wa kumuacha huyu unaishi nae uufanye haraka sana ili usijepoteza vyote, wanaume huwa hawapendi kuwekwa kwenye dilema, so ukimkawiza sana unaweza kumkosa.

Ila mwisho wa yote wewe ndo muamuzi wa Mwisho, fata roho yako inavyokutuma.

Anonymous said...

Pole dada,kwa mawazo yangu naona mshirikishe mama kwanza kabla hujaamua chochote,kuhusu huyo unaeishi nae tabia haina dawa anaweza kujifanya kajirekebisha baada ya ndoa ndo itakuwa balaa zaidi.muombe mungu akuongoze kwa imani yako.
Mama daxin

Anonymous said...

Mwombe Mungu atakuonyesha maana hata huyo unayempenda yawezekana ni vile tu hujaishi nae. Wanaume huwa hawaonyeshi ukikaa nae ndio utajua matatizo yake wewe jenga kumuheshimu huyo mpenzi wako na endelea kumweleza juu ya hali yake ya kueleza mambo ya ndani kwa watu.

Anonymous said...

dada wewe unachotakiwa kufanya ni kutazama mbele zaidi,cz kama mtu anakuonyesha vitendo hivo kabla ya ndoa ,mimi nahisi baadaye ndio itakuwa mbaya zaidi.kuwa na msimamo wa maisha yako hata kama hauna uwezo wa kutosha.

Anonymous said...

Hauja tulia. Haustairi kuolewa. Na utaendelea kunyanyaswa hivo hivo hadi kufa kwako, sababu sio muaminifu. Unaishi na mtu alafu una mapenzi na mwingine. Toba. Mpenda wengi uitwa malaya daima. Na itakuwaje kijana wa watu achumie familie yako, kwani wewe biashara ya wazazi wako? wakuuze kwa mwanamme ili wapate ela ziwasaidie? Kama ndio hivo, basi utaendelea kunyanyasika daima, pole. Tumia akili yako ujitegemee na usaidie wazazi wako mwenyewe. Hapo hamna mwaname atakunyanyasa. Samahani kwa kukuvamia na maneno lakini sio vizuri kufanya hivo

Anonymous said...

kwa nini usitafute chako?badala ya kukaa na kutegemea hao wanaume?na huyo mpya nae baadae atachoka tu,hapo ni mwanzo mwanzo.mwanamke jishughulishe,usitegemee sana vya kupewa

Anonymous said...

Pole dadangu. Usikubali kuolewa na huyo mtu ikiwa hayo usemayo wasema kweli. Narudia tena USIKUBALI kuolewa na huyo mtu hata kama wazazi watakulazimisha kwani umekwishamfahamu vyema tabia yake. Hakika huyo ni FIRAUNI.
Wanaume mara nyingi hujivika ngozi ya KONDOO na hali wao ndani ni Mbwa mwitu!! Hivyo usiparamie ndoa na huyo kaka wakizanzibari hakika hivo ulivo mtazama sivyo alivyo!!! Msubiri umtambue vema mapungufu yake uone kama yanavumilika. Haya yote ni kwa faida yako dadangu mpenzi. Usikubali kuwa mtumwa kwasababu ya umasikini wako labda Ungekuwa umezama kwenye dimbwi la mahaba.

Anonymous said...

Atabadilika? Lini? Tunafanya makosa sana pale tunapofikiri tunaweza kubadilisha hulka ya mtu....! Habadiliki huyo, hivi unataka uambiwe lugha gani uelewe hakupendi " hafurahii ladha ya mapenzi anataka kinyume cha maumbile " Hee na bado unafikiri atabadilika..........!
Usije ukafanya ujinga wa kutembea na mwanaume mwingine wakati unaishi na mwanaume mwingine, na pia acha papara za kutoka kwenye uhusiano mmoja na kukimbilia mwingine...utalia kila uchao. Tulia, achana na huyo kwani yaelekea humpendi ila wapenda hizo pesa zake zinazoitunza familia yako, naye kakujua atakuchezea apendavyo....

Anonymous said...

Pole sana. Huyo mpenzi wako usitegemee kama atabadilika. Kubadilika ni ndoto za alinacha. Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni kuamua.

Anonymous said...

ni bora umuache kwanza ni mtu wa aina gani! kila siku kukutukania wazazi wako na kukusimanga na umasikini. hakuna mtu aliezaliwa tajili hapa ulimwenguni. kama alizaliwa tajili mbona alizaliwa akiwa hana nguo toka kwenye tumbo la mama yake.Ni bora kwa sasa umwangalie huyo mzanzibar. na kwanza anataka akuanzishie tabia yake chafu wewe usie itaka. mwache atafute mwengine mwenye tabia hiyo chafu kama ya kwake

Anonymous said...

wewe huna lolote kinachokusumbua ni tamaa tu hapo. utampendaje mtu humjui eti umekutana naye tu kakupenda umempenda..ama cuz hakuna neno la kiswahili "i like u" ndio unamananisha u like him? and he like u too? make it open what do u mean? he do love and u too and since when u've dating each other? unazani mapenzi yote ni marahisi? mapenzi mwanzo ni matamu na huyo mzanzibar wako anataka kitu toka kwako ndio mana kaficha makucha yake. akikuzoea atakuonesha uchafu wake. lakin nasikitika kuona msichana kama we unashindwa kuwa mvumilivu mpaka sasa unamcheat bf wako. amua moja kuwa na huyo old one na uvumilie one day yataisha. ila kama unamuona mzanzibar wako bora kuwa naye then utatupa feedback hapa wananet. mdau toka german

Anonymous said...

Pole sana dadaangu lakini hiyo ndio mitihani ya mwenyezi Mungu.Sasa swali langu ni hili,je huyo mkaka wa kizanzibar umeshavuunja nae ukimya?(Means umeshatembea nae),na kama ndio,nae amesemaje kuhusu Ladha yako?,kwa maana usiwe unaruka mkojo then ukakanyaga mavi,coz huwa tunackia hao wazanzibar wanapenda sana ufiraji so ni bora ukatulia na huyo wa kwanza ambae ushamjua tabia zake nyingi na umekubaliana nazo isipoikuwa hiyo 1 tu inayokukera ambayo nauhakika anaweza kubadilika in a long run,kuliko kwenda kwa mtu mgeni ambae huzijui tabia zake kabisaaaaa.Ni hayo tu dadaa

Anonymous said...

we mdada narudia tena. huwezi kusema mzanzibar anakupenda na wakati humjui. mie mpaka hapa nilishatembea na wanawake 30 na ninamiaka 23 tu. na kila mwanzo wa uhusiano wangu wanawake walikuwa wanajua mie ni msitarabu sana. mpaka kutulia nilikuatana na huyu mjeruman wangu kila kituko anavumilia. matusi. kufumaniwa na hata kumpiga. yote alivumilia mpaka nikaamua kutulia kabisa na nimetulia mpaka leo hii na sitaki kusikia wanawake wengine na namheshimu vibaya sana. ni mwaka wa 2 sasa tuko wote, sasa mie nakushangaa unashindwaje kumvumilia mwenzio, na utampendaje mtu mzanzibar wakati bado unampenda huyo old wako? na kama humpendi old wako kwa nini bado unaishi naye? anakutukana cuz umeweka makalio tu hujishughulishi. hangaika kuwa na chako uone kama atakuzarau. otherwise we utakuwa mtu wa kutukanwa tu daima milele..badilika mwanamke we

Anonymous said...

Sikiliza mdada wakitanga. Binadau ana akili nyingi sana aliyopewa na mwenyezi Mungu lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kutumia hata Robo ya akili tuliyopewa. unaowaona matajiri leo ujue wametumia akili yao kuwa hivyo nina maana huwezi kutoka kundifurani la maisha kwenda kundi lingine kwa kusaidiwa! ni lazima utie bidii mwenyewe kwa akili uliyopewa na Mungu wako.
Tuje kwenye hoja yako. Rudi nyumbani kwenu kajipange upya utampata wa kukufaa.Mungu hugawa Riziki kwa kila mtu........Kizito!!