Monday, 8 November 2010

Ushuhuda: Asanteni kwa Ushauri!

"Hi da Dinah na wanablog wanzangu, nimewahi kuja na swali “"Ex ananirudisha nyuma kihisia, nami nataka ndoa-Ushauri" Nashukuru kwa ushauri wenu kwa ujumla umenisaidia na namshukuru Mungu kwa kuwa mvumilivu na kuyafanyia kazi mawazo yenu.

Nimejitahidi sana hadi nimefikia hap, kwa ufupi nimefanya kama mlivyo nishauri kwani niliona anazidi kunifatilia nilichofanya nilinunua line mpya nikamtumia x-boyfriend wangu na kumwambia kwa upole kabisa kua hii line ndio yangu ya sasa. Ile ya zamani usiitumie nimempa Mother atumie hivo ukitaka kunipata tumia hii ya sasa.

Hivyo ametumia kuwasiliana kupitia hii ya sasa na kunitaka tuonane lakini kila siku nikawa namdanganya kuwa kuna kazi kidogo imenibana anisubiri baada ya wiki kama nne hivi nitakua free then tutaenjoy nae akakubali.

Baada ya kuona amekubali nikarudi kwenye line ile ya zamani na kuanza kuitumia hii mpya nikaitupa hivo akawa anashindwa kunitafuta kupitia ile ya zamani kwani nilishamwambia kua ipo na Mother.

Nafikiri amesubiri hadi mwisho amekata tamaa akaacha kunitafuta na kitu cha kushangaza zaidi njiani hatukutani kama zamani, kwa sasa naishi maisha safi raha mstarehe na mpenzi wangu hakuna anaenisumbua wala nini.
Nawashukuru sana".

Dinah anasema:Nafurahi kuwa umefanikiwa kufanya uamuzi na sasa unaendelea vema na mpenzi wako ambae unataka kufunga nae ndoa. Lakini mbinu uliyotumia sio nzuri na nitakuambia kwanini?

Umekosea sana kumpa matumaini ya kukutana na ku-enjoy nae wakati huna mpango huo. Mwanaume sio mtu wa kukata tamaa kirahisi hivyo hasa kama anakupenda, ikiwa atakukosa kwenye Line uliyotumia anaweza akajaribu kupiga au hata kutuma ujumbe kwenye namba yako ya zamani ambayo ndio unayotumia sasa.

Siku moja mpenzi wako ulie nae sasa anaweza kukutana na ujumbe kutoka kwa Ex wako huyo na hivyo kutaka kujua ukweli wa nini kinaendelea kati yako na huyo Ex. Sidhani kama ungependa hilo likutokee.

Pamoja na kuwa kwa sasa hamkutani mtaani haina maana jamaa amehama Mji au eneo hilo, ipo siku atarudi na mtakutana, je utamueleza nini kuhusianana ahadi uliompa?!!

Unachotakiwa kufanya ni kumwambia jamaa ukweli ulio wazi kuwa humtaki na sasa uko kwenye uhusiano mwingine na usingependa uhusiano wako huo uharibuke kwa sababu yake. Kama mtu mzima atakuelewa na kukubali kuwa hawezi kuwa na wewe kwa vile tayari una mtu mwingine.

Kila la kheri!

8 comments:

emu-three said...

Ni kweli kama alivyolonga dada Dinah, ukweli na uwazi kwenye mapenzi ni jambo jema, na mkweli wakati wote ni mpenzi wa mungu!

Anonymous said...

Bibie, niliposoma kuwa umeufanyia kazi ushauri nikadhani ulitumia mbinu sahihi na wazi kumwambia mlimbwende wako wa zamani, lakini kumbe ulitumia njia ya kipuuzi kabisa, naita ya kipuuzi kwa sababu hujatatua tatizo bado kwa sababu ulidanganya.Ujue kuwa mzigo upo palepale bibie hiyo uliofanya ni danganya toto.

Mwambie kuwa mambo yaliisha yaliisha na sasa upo kwenye uhusiano mpya na hutorudia matapishi PERIOD. Eti ulibadilisha line, na ulimwahidi muonane ili mu-enjoy!! hufai kabisa wewe!! ole wako mpenzi wako aikute sms humo.

Mwanaume gani atakukatia tamaa kihivyo?? wembe uleule bi dada atakutafuta tu na atakupata.Ahadi ni deni!! Asante dada Dina kwa kumweleza ukweli huyo bibie.

Anonymous said...

Mmhhhhhhhhhhh hapo umeongeza tatizo juu ya tatizo mama!!!

jamaa anajipanga namna ya kukudaka kiulaini.Umepewa ushauri mzuri wewe unaenda kufanya udanganyifu tena? Tena udanganyifu wa kipumbavu kabisa eti uliahidiana naye mka-enjoy?? kweli ndivyo tulivyokushauri?Huoni ulijiingiza tena kwenye mtego zaidi?

Asante Dina kwa kumpa vidonge vyake akaponee huko hospitalini.

Anonymous said...

dinahicious mimi ni mpenzi wa glob yako sana unafanya kazi nzuri ktk kushauri watu ktk ndoa zao na hata wapenzi kwakuwapa mbinu mbalimbali jinsi ya kudumisha ndoa yao wengi wamefaidika kupitia hii blog yako nawengi wanaendelea kufaidika kupitia blog yako kazi nzuri sana na uwendelee hivyohivyo na mungu akubariki mimi ninaswali moja ambalo limekuwa likinisumbua kidogo swali lenyewe ni hivi hivi katika maandiko ya dini iwe ya kislam au kikristo maandiko yanasemaje juu ya mwanamke kukzidi umri mwaume kuna ubaya wowote nazungumzi ktk vitabu vya dini naomba kama kuna mwenye kujua mstari anijuze pls ni hayo tu kazi njema

Anonymous said...

jamani hapo dada umechemsha umwambie ukweli huyo jamaa coz anyways anaweza akajaribu siku moja kutuma sms coz ni rahisi kujua kama unadanganya how can u give ua 4n card to somebody else?simu zina program ya caller blocker unaweza kumblock msumbufu yeyote.its better that than wat u did

Anonymous said...

Naomba uniwie radhi nikisema wewe si mjinga bali ni mpumbavu maana ungekuwa mjinga kwa jinsi watu walivyokushauri ungeelimika na kufanya mambo yanayoeleweka.Wewe unashindwa nini kumweleza mtu ukweli kama humtaki tena mbaya zaidi unampa promise ya kujirusha naye.Wewe hata ukiolewa utakuwa si mwaminifu kwenye ndoa eti umebadili line kwa muda nani kakuambia mwanaume anakata tamaa kama anakutaka kweli?

Anonymous said...

The truth will always set you free...
bora usingeandika upuuzi ulioufanya maana hujatatua tatizo. Mimi ningetumia same old number kumweleza it was over nina mtu mwingine so stop bothering me, halafu namfungia madirisha. Umemu entertain kwa kujibu msgs kupokea simu, kusimama kumsikiliza maongezi yake etc etc so ana hopes na wewe hadi kesho! mama ukilikoroga utalinywa mwenyewe wachumba hawapatikani siku hizi shauri lako!!!

Anonymous said...

eeeh mi kweli namuunga mkono huyo alekwta mpumbavu,,,,kip kinakuzuia ww kumwambia humtaki tena, unaenda kuanzisha familia wht kund of mama r u going to be????huna mcmamo unapelekeshwa pelekeshwa tuuuu,, em STOP IT!!!!! zinduka, umeamua kua na huyo bc kua nae na umpende kweli, nyie nd wamam mnaoleta ukimw kwenye ndoa zenu!!! mwambie humtak, au kama huwez, m'block acweze kukupgia. Thats all heee, una2tia aibu.