Thursday, 18 November 2010

Baada ya miaka 2 nimegundua kuwa mimi ni The Other Woman~Nifanyaje?

"Hi Dada Dinah na wachangiaji wengine, asante na pole kwa kazi ya kutushauri maana wadada kilakukicha hatujambo kwa maswali. Mimi ni mwanaama wa miaka 27 mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Nimekuwa na uhusiano na Kijana mmoja wa miaka 25 kwa muda wa miaka miwili, sikufichi ananipenda sana na kunijali.Kijana huyu anashughuli zake binafsi kwani amejiajiri.

Sasa kipindi chote hicho tumekuwa pamoja ni hivi karibuni tu ndio nimegundua kuwa kumbe mwenzangu alikuwa na msichana mwingine na wamejuana kwa muda wa miaka 5. Baada ya kugundua tulikorofishana na alikuja kuniomba msamaha na mimi bilakujijua nikakubali na kumsamehe na hii imetoeka mara chache mpaka nahisi kama vile Jamaa ana dawa ya kunifanya nisamehe haraka.

Mpenzi huyu amekwisha enda nyumbani kujitambulisha kwa mama, kiukweli jamaa ananifikisha na kunijali pamoja na mwanangu ingawa hatuishi pamoja. Lakini ninapofikiria kuwa nina mwenzagu huwa nakosa raha na wakati huohuo sielewi huyu jamaa ana nia gani na mimi.

Swali la Kwanza: Unadhani huyu jamaa anampango gani na mimi?

Swali la Pili: Je niendelee kuwa nae au niachane nae?

Kama ni kumuacha nimejaribu mara nyingi lakini kila akirudi nakuniomba msamaha najikuta nasamehe tu, pia anatabia ya kunitumia pesa nyingi kama hana akili nzuri ikiwa nitamchunia.

Naomba mnishauri wana Dinahicious,
Asante."

15 comments:

Anonymous said...

Pesa pesa pesaa .........sabuni ya roho! Kwa maelezo yako humpendi jamaa, unapenda hela zake. Kama huwezi kujikimu, inabidi uwe mpole tu maana bongo jua kali. Kama una uwezo mmwage, dudumizi anakula watu sio mchezo! ukishindwa mwambie mkapime na kama hawezimwacha huyo mwingine basi akija aje na ndomu vinginevyo hakuna game. Ni wewe mwenye uamuzi, ni uhai wako, ni mtoto wako, ni mtoto wenu.

MM

Anonymous said...

Pesa ndio sababu ya wewe kuwa slave wa mapenzi. Huyo jamaa nia yake ni kukumega as long as he can.

Kama ana true love na wewe kwanini awe na wawili, na kumbe mwenzio bado alikutangulia. Zungumza naye in details about this na yeye, angalia kama any his defence makes senses, otherwise move on.

Na pili, kama dada umeamua kuachana nae, you have to consider other options like changing your phone number ili kukata mawasiliano kama unaweza pia hama mtaa.

Anonymous said...

Pole sana dada, nachoweza kukushauri ni kuongea na huyu mpz wako ujue ana msimamo gani na wewe, alafu pia hata ukimwacha tayari una mtoto nae huoni kwamba mtoto atakosa malezi ya baba? Cha msingi msisitize muende kwa wazazi mkajitambulishe muanze taratibu za kufunga ndoa. mpige stop kuhusu huyo mwanamke mwingine.

auntie nancy said...

pole sana ndugu kwa mkasa uliokupa mpndwa.1 inavyoonekana ww ndo uliyeingilia pnz la watu ukiangalia na muda wako ww na mwenzako.pia age wise inaonekana kuwa huyo kijana ni mdogo sana so bado hajafikia hatua ya kutulia.
kingine ni kwamba mtazamo wako ktk mpnz ni kwasababu yy huwa anakuhudumia ww na mtoto wako so kumwacha itakuwa ngumu kutokana na mawazo kwamba ukimwacha ww na mtoto wako mtapata shida coz mmeshazoea huduma na pesa anazowapa.
kwa ushauri kama huna kazi basi bora utafute kazi itakayo kuingizia kipato kitakusaidia amini ukiweza pata kazi bac utaacha kuwa tegemezi na itakusaidia kujiamini na kuwa na kiburi na ckazi yako coz inakuingizia na kumsahau huyo jamaa itakuwa rahisi coz utakuwa huna kitu kitakacho kubabaisha tena.

Anonymous said...

Mimi naichukua hiyo Sentensi ya mwisho "pia anatabia ya kunitumia pesa nyingi kama hana akili nzuri ikiwa nitamchunia" Hiki ndicho kinakufanya umsamehe kila akitenda ndivyo sivyo.Acha pesa zake! kaa na maisha yako. Mungu atafungua milango mingine utapata utapata Riziki yako kupitia mikononi mwako mwenyewe!!...............Kizito!!

Anonymous said...

Binti achana na mme wa mtu yatakuja kukupata mkubwa pamoja na hizo hela unazopewa hazitakusaidia chochote. take care of yourself madam.

Anonymous said...

Kama vipi chakachua tu

Anonymous said...

umeuliza maswali mawili la kwanza kama huyo jamaa ana mpango gani na wewe. mimi nafikiri ni vigumu kwa mtu kukutabiria hilo. lakini cha wazi kinachoonekana hapa ni kuwa huyo msichana wake wa miaka mitano kunakutoelewana kwa kiasi fulani ndio maana alikuja kwako, japo kuwa haina maana kama waliachana kubisa.Au inawezekana waliachana kabisa lakini kuna vitu vinamfanya asimtupe kabisa, kama vile watoto au hisani aliyowahi fanyiwa siku za nyuma na huyo mwanamke. Pia usisahau kuna wanaume wanapenda kuwa na zaidi ya mwanamke moja hata kama dini zao haziruhusu.
Hata hivyo fedha anazokutumia inaonesha anakupenda kwa dhati. kinachotakiwa hapa sio kugombana nae, hekima ya ziada inatakiwa. tafuta siku ambao atakuwa na amani ya kutosha kabisa na muulize kwa utaritibu sana nini hatima ya uhusiano wake na yule mwanamke. wakati ukimuuliza hili hakikisha unampa uhuru wa kutosha ili aweze kuutoa undani wake. Baada ya hapo wewe mwenyewe waweza amua au utaijua hatima yako.usikubali kuombwa msamaha tu,kuomba msahama wakati mwengine huwa kichaka cha kuficha makosa. Yaani mtu anaendelea na kosa akijua akiomba msamaha atakubaliwa.
Kuhusu kama uendelee nae au uachane nae mimi ninavyoona ni wewe ndio unaweza amua baada ya kuongea nae, na kupima faida na hasara ya uamuzi unaotaka kufikia.
Labda lingine la muhimu ninaloliona hapa ni suala la kuishi pamoja. Siku hizi ndoa ni dili usidhani kila kitu kitaenda chenyewe. Jaribu kumshawishi muanze maisha ya pamoja, hakikisha jambo hili linafanyika kwa haraka na kwa gharama ndogo kadiri itakavyowezeka. Ukifanikiwa kuishi nae hakikisha unakuwa chachu ya maendeleo yenu kama kuwa na nyumba maandaliza ya elimu kwa watoto na kadhalika. Wanaume mara nyingi wanapokuwa wanashuhulikia habari za maendeleo huwa wanasahau mambo mengine yasiyokua na maana.

Anonymous said...

Pole ma dear, but hukuweka wazi kama wameachana na huyo msichana au vipi? na hayo makosa anayoomba msamaha mara kwa mar ni makosa yapi ni hayo ya kuwa na msichana mwingine?na kwa mama yako alijitambulisha akiwa na nia gani as just a boyfriend au mchumba mean yuko kwenye process za kuchumbia?
Ombi kwa Dinahicious, my dear sijuii ni mimi tu au na wasomaji wengine ila ukweli ni kwamba nimemiss shule zako, plse tupe darasa siku moja moja as you were doing before thou haya maswali na majibu yanatusaidia but we need darasa mamii, thanks

Anonymous said...

Neno pesa, oh neno pesa ni neno la kawaida, lakini ukitafuta tafsiri yake hakika (hutajua, neno pesa neno pesa oh... (wimbo: Neno Pesa; mwimbaji: Ahmed Kipande; Bendi: Kilwa Jazz Band; miaka ya 1960's; kwa sisi vijana tunaopenda nyimbo zinazoitwa "zilipendwa").

Anonymous said...

Hebu weka e-mail yako hapa gerentii nitakusahaulisha huyo fala. Mmakonde-Mmanyema.

Anonymous said...

Dina usiitupe barua yangu hii kapuni. Ombi langu moja tu: Huyu dada atoe e-mail yake hapa nitamtafuta, ntam.... na nitamfanya amsahau kabisa huyo cheater wake. Lover boy.

Anonymous said...

dunia mzunguko huyo huyo si mwingine bali handsome boy fulani..bado hajaamua kuoa,,na hata akiamua hakuoi wewe wala yeye..anajua mwenyewe lini ataoa,,na si mwaka huu wala kesho wala keshokutwa,,ndugu yangu huyo kidume cha mbegu dah kama unabisha mgusie suala la kuoa tuone kama maandalizi yataanza..kuweni dada zetu ..penye nia panaonekana,,yanini kusugua kichwa kwenye moto kisa kuna vitambaa vya kujifuta ..kwikwi kwi kwi.!!

Anonymous said...

mdada huyo ni lover boy,,,ulivyosimuila hivyo umenigusa aisee,,maana hiyo system anaitumia kila mahali,,ni mgonjwa wa k,,,nitumie mail fanuem@gmail.com nitakkupa data zake vizuri,,

Anonymous said...

sasa bibie,mbona umesema ameomba msamaha,,,sasa huyo mwingine katoka wapi tena,,nilijua kampotezea,,baada ya kukubali kosa,,,au ndo umesamehe hewa,,na cheating inaendelea kama kawa,,kuwa na msimamo dada,,huyo atakuumiza sana,,na utajuta kupoteza muda,,na hizo pesa ni za kukulelea hiv positiv status tu,umwachee mwanao bila mama , embu songa mbele,,mapenzi gani hayo ya kupenda pesa kupita utu wako,kwani wewe huna riziki aliyokuandalia mungu mpaka ukajidhalilishe hivyo, kwa taarifa yako jamaa keshakusoma kuwa unamsamehe kwasababu ya pesa zake,,na usimuone mjinga,,atakutumiaaa weeeee ,,siku ikifika anataka kuachana na ukapera hawezi kuoa mpenda pesa loh..sie wanaume si wajinga, we umejifanya mjana kwa kujidai unasemehe kisa pesa,,ngoja nae azimwage,,si zipo,,ila subiria deadline m2 wangu utakonda ka mshumaaa..