Tuesday, 5 October 2010

Nashindwa kumuacha mume wa mtu-Nifanyeje?


"Natumaini wewe ni mzima na waafya. Mimi ni mwanamke wa miaka 24, naomba ushauri wako kama mdogo wako. Mimi nimetokea kumpenda mume wa mtu na nina amini ananipenda pia. Tumekuwa na mausiano kwa mwaka mmoja bila hata mke wake kujua na nina tamani sana kumjua mke wake.

Tatizo langu ni kuwa sijiamini kama huyu Mume wa mtu atakuja kuwa nami kama mpenzi wake wa kudumu, mimi binafsi nashindwa kumuacha kwasababu Jamaa mwenyewe ni innocent and very caring.
Naomba ushauri nifanye nini?."
Dinah anasema: Mie mzima wa afya namshukuru Mungu, Nashukuru sana kwa Mail yako na hongera kwa kuwa wazi pia kuwa na nia ya kuachana na huyo mume wa mtu lakini hujui uanzie wapi?
Ninaamini nia yako ni kuachana nae na labda ulipogundua kuwa ni mume wa mtu ulitaka kufanya hivyo lakini kutokana na hali ya kujali na upole anaokuonyesha unadhani kuwa ni mtu mwema na hivyo kuzidi kumdondokea kimapenzi. Ikiwa kama nia yako sio kuachana nae hakika usingekuja hapa kuomba ushauri na badala yake ungeendelea kivyako.
Uhusino wenu umekuwa kwa mwaka mmoja kwa vile mkewe hajui na wala hajahisi kuwa mumewe ana-cheat labda kwa vile anajali na amevaa ngozi ya kondoo hivyo mkewe anamuamini kupita kiasi na hivyo kutohisi kitu chochote kibaya.
Kama mkewe angejua au angehisi kuwa mumewe anagawa umasikini nje ya ndoa yao hakika angempa wakati mgumu sana na kupelekea Jamaa kuachana na wewe.
Sasa hebu tuambie kitu gani kinakufanya utamani sana kumuona mkewe? Ili umwambie kuwa mumewe ana-cheat (ni jambo jema japo ni ngumu kwa yeye kukuamini hasa kama mumewe atakataa na kudai kuwa wewe unamtaka) AU unataka kufanya ushindani ili kuzua ugomvi juu ya mumewe (sio vema kuumiza hisia za mwanamke mwenzio kiasi hicho).
Hisia za Mapenzi:
Kutokana na uzoefu hakika natambua kuwa ni ngumu sana kukabiliana na hii kitu kwani hupangi au kuchagua nani wa kumpenda, hisia za kimapenzi hujitokeza tu kwa mtu yeyote na wakati wowote, lakini kabla hisia hizo hazijaota mizizi (hazijakukaa sana) ni vema kuwa mdadisi kuhusu mtu uliempenda ili kujua ukweli kuhusiana na maisha yake ya sasa kimapenzi. Na mara tu baada ya kugundua kuwa amefunga ndoa ni vema kumkwepa.
Kutojiamini:
Ofcoz huwezi kuwa na hali ya kujiamini au kuwa na uhakika wa wewe kuwa mpenzi wake wa kudumu kwani huyo mwanaume sio wako na sio single ni mume wa mtu, siku yeyote ikiwa mkewe atagundua kuwa kajisahau na kuanza kurudisha yale yote ambayo labda mumewe anakosa na sasa kuja kupata kwako.
Vinginevyo, kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji ni kuwa, ikiwa Imani zenu za Dini zinaruhusu na mkewe wa kwanza akaridhia then utakuwa mke wa pili.
Matokeo yake:
Wee bado ni binti mdogo wala huitaji kujiweka kwenye matatizo makubwa kama kuharibu ndoa ya mtu na vilevile kuishi na hatia ya kuharibu maisha ya watoto ambao ni matunda ya ndoa hiyo. Kumbuka watoto waliozaliwa kama matunda ya ndoa hiyo wataumia kama atakavyoumia mama yao.
Utakuwa umewanyang'anya baba yao, utakuwa umewaharibia maisha yao kwani hakuna mtoto anataka kumuona mama yake anaumia (unajua watoto tulivyo karibu na mama zetu). Huenda hujui yote haya kwa vile hukulelewa katika mazingira ya ndoa (kama mmoja wa wachangiaji alivyogusia), mazingira tuliokulia husaidia sana kwenye maamuzi yetu.
Nini cha kufanya:
Achana na huyu mume wa mtu kwania anakupotezea muda wako na kukuzibia bahati ya kukutana na wanaume, kwani kuna vijana wengi tu wenye umri mkubwa zaidi yako lakini hawajaoa na pia wapo vijana wenye umri wako (24-29) ambao wako huru.
Kila la kheri.

44 comments:

Anonymous said...

kwa hivyo wanaume woooooooote walo jaa duniani huyo wa mwenzio ndio umemuona mtam,ehhee.sasa ngoja ajue halafu utaisoma namba vzuri,tafuta wako mpumbavu mkubwa.kudandia vya wenzie,

Anonymous said...

pole kwa kujidanganya, ujue wasichana wengi hua hatuna fikra kabisa, yn nasikia hasira sana ninaposoma huo uchafu wako, we unaona sifa kuchukua mme wa mtu? just imagine wewe kama ungekuwa na mme then mtu amchukue utajisikiaje? kuweni na huruma jamani. hicho unachokifanya sidhani kama uko sahihi then you are proud of it!!!!

Anonymous said...

Dada umeomba ushauri ufanyeje kwa yanayokusibu.
ushauri wa kwanza usijiingize kwenye matatizo maana siku hizi magonjwa ni mengi na hasa huu ugonjwa tishio sasa kwa kuwa na mahusiano na mume wa mtu ni kwamba unaongeza chain ya maambukizi na umesema kuwa humjui mke wake je vipi kama huyo mke wake ameathirika na wewe hujui, je ulichukua uamuzi wa kupima kujua kuwa huyo bwana kama mzima au la maana anaweza akawa anataka kukuambukiza ukimwi ndio maana anajifanya anacare. je unajua ana wanawake wengine wangapi zaidi yako maana kama mkewe hajui kama una mahusiano na mumewe ni rahisi kwako pia kutojua kama ana mahusiano mengine zaidi yako.
ushauri wangu kwako ni kwamba uachane na huyo mume wa mtu maana kimaadili hiyo ni mbaya labda kama mmepanga kuoana kama dini yako inaruhusu lakini kama hairuhusu ni bora uachane nae na utafute mtu ambae atakuwa wa maisha yako yote. Jitahidi kuwa mbali nae huyo bwana hata kama anacare kiasi gani kwani tayari ana mke wake na hivyo kwako kuwa nae kama wa kudumu itakuwa ngumu . Akikuchoka atatafuta mtu mwingine zaidi yako au atakuwa na wanawake wengine pamoja kuwa unamuona anacare kwako.

Anonymous said...

Atakuaje innocent wakati tayari anacheat na wewe. acha vya watu wewe tafuta vyako.

Anonymous said...

Naomba nikuulize swali kabla sijakupa ushauri, wewe na hyo mme wa mtu ni dini gani? Kama bwana ni muislamu na wewe upo tayari kubadili dini kuwa muislamu (kama siyo muislamu) uwezekano wa kuwa mtu wako wa kudumu upo. Maana uislamu unaruhusu mke zaidi ya mmoja. Hata hivyo hiki si kigezo cha kukufanya uwe na uhakika asilimia 100 kuwa atakuoa. Weye bado mdogo sana, achana na mme wa mtu tafuta wa kwako. Tamaa za kuishi maisha ya juu ndiyo zinakuponza mdogo wangu. Kwa nini usitulie ukaridhika na kidogo ulichonacho ukisubiria kupata wa kwako mwenyewe? Jiweke ww kwenye viatu vya mke wa hyo bwana, ungesikia mmeo anatembea nje ya ndoa ungefurahi kiasi gani? Mabinti wa siku hizi mna tamaa sana, na ukimwi huu mtaisha. Maana huna uhakika kama kweli huyo bwana hana mwanamke mwingine zaidi yako na mkewe, hujui kama mkewe naye ana mahusiano ya ziada na nani. Ukiunganisha huo mnyororo utaona ni jinsi gani unajiweka kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya UKIMWi. Tulia dada acha tamaa za vijisenti vya kupita

Reka1 said...

Mdogo wangu, mume wa mtu ni sumu.
hata kidini ni dhambi kuwa na mume wa mtu, sijui wewe mwenzetu ni dini gani?
Anyway just imagine wewe ndio mke wa huyo mume wa mtu, halafu siku moja unakuja gundua mumeo anakucheat Utajisikiaje? Acha tabia hiyo ni chafu mdogo wangu, muombe muumba akujalie akupe mume wako si wa wenzio. Naumia kwa sababu najua uchungu wa mume!

Anonymous said...

Very innocent? give me a break sister a man is cheating on his wife and you call him innocent? tafuta wakwako mbona we bado mdogo muonee huruma huyo mwanamke mwenzako na fikiri kama angekua mume wako halafu kuna demu anakula pembeni huku akijua ni mume wa mtu.

Anonymous said...

we dada achana na mume wa mtu tena ni dhamb kubwa unayoitenda hakika believe me or not unamsababishia maumivu ya moyo huyo mke wake jamaaa embu jifikirie ungekuwa ni wewe umeolewa then mumeo ana mtu mwingine we ungejisikiaje?kwakweli ni mbaya sana ila ujue kuwa ndoa yao imeandikwa mbinguni wwe anakutumia tu labda kama ni muioslamu labda akuoe ila kama ma dia umeingilia ndoa ya kikristo hiyo dhambi ni mbaya na ni laana unajitafutia,sasa wewe kama ni mwamnamke umetimia si utafute wa kwako jamnai ni nini kumganda wa mwenzio?ndo nyie mnaorogwaga hata msijielewe, kwa kifupi achana nae tafuta wa kwako

claire said...

poleee !
wewe unajua kuwa huyo ni mume wa mtu then unafikirikua kuwa siku moja aje kuwa mpenzi wako wa kudumu , kivipi ?

au umeplan kumroga huyo mwanaume ili amuache mkewe ?

skia dada muda na umri unakwenda bibi eeeh , so usipochangamka sasa kumtafuta mwanaume ambaye atakuwa wako si wa kudoea coz hapo wewe ni mdowezi wa mwanaume wa m2 alafu mbaya zaidi unajisahau unataka kulowea kabisa kwa kutaka kuweka makazi ya kudumu!

utarogwa mjini hapa , we huyo mwanaume anakuzingua tu coz angekuwa anakupenda angekushauri utafute mwanaume wako na wewe kuliko kuwa nae yeye coz ye anajua ana wife wake so hamtafika kokote , atakufanya wewe ni SPARE PART tu au CHOMBO CHA STAREHE au BIG G tu then ukiisha utamu anakutema jalalani ye anarudi kwa mkewe ! upo hapo ?

usidanganyike na hizo care na love nyingi nyingi hizo ni swagger tu !

then hata kama unavyo dai anakupenda but in reality huyo ni mume wa mtu sasa wewe jiulize una nafasi gani kwake ? au una future gani nae ? jibu ni hakuna zaidi tu ya wewe kumpa uchi tu !?

so bibi amka tafuta wako , mi naamini utapata tu na mwenye malavidavi yote utakayoyataka kuliko kugandana na huyo mwanaume kujipotezea muda tu !

byeeeeeeeeeee !

Anonymous said...

Kama ni Mwisalamu olewa naye, kama mkristo basi hapo toka haraka maana unapoteza muda ungali bado mtoto mbichi sana wakati kuna vijana wenzako wanakusaka sana.

usicchelewe kung'ang'ania mume wa mwenzako bibie, na akijua ni hatari,Na pia ni hatari kwako maana huyo jamaa anaweza kukuzalisha na hapo ukapoteza thamani yako kabisa.

Umesema unatamani kumjua mkewe,unamtaka umuombe akuruhusu?au unataka kumuona kama unamzidi uzuri ili uone kama huyo mume wake atamtaliki ili wewe uchukue namba?

Bibie miaka 24 ni mbichi kulikoni usipotezee muda wako hapo kupendwa kupo kwingi sana,lakini lazima ujue kuwa upendo wakati fulani ni upofu wa fikra na dhamiri.Ukijua kuwa ni mume wa mtu kimbia sana ili utafute maisha yako.

Pole lakini maana umeonja asali kuiacha ni noma sana. lakini kwa kuwa ni mali ya mtu huna budi kuiachia ili usijehatarisha ndoa ya mwenzio.

Anonymous said...

Sasa dada yangu hapo umesha sema ni mume wa mtu huoni htari iyo mbele yako ya kuharibu uhusiano wa watu? Miaka 24 bado naamini ukitulia unaweza ukapata yule mtarajiwa wako,hebu angalia usiwakolofishe hao waliopendana,kama ulikuwa unafanya ivyo basi tambua kuwa ni kosa,ukizingatia yeye ni mume wa mtu!

Anonymous said...

Dada yangu lazima utambue kwanza unalolifanya ni kosa kwa kuwa yeye ni mume wa mtu tayari;huoni kuwa unataka kuwaharibia uhusiano wao?Pia unasema sijui kama atakuja ishi nawe ina maana unataka aishi nawe kama mume na mke ila jawabu si unalo tayari kuwa yeye ni mume wa mtu !Umri wako bado hauja chelewa,kuliko kuwa na tumaini la kuolewa na huyo bwana wa mtu ni bora ukaanza tafuta wako kabla hakujachwa!
Usidanganyike na yeye kukujali kwa kukupa maitaji yako au kwa kuwa yeye ni mpole,lazima ufikilie je baadaye nini kitatokea kuolewa na yeye au ndio just passing time?
Hapo mimi naona hakuna kitu,ch muhimu ww kama umejua ni bwana wa mtu ni vema sana ukamwambia ukweli zeni kila mtu akachukua nia yake!

Anonymous said...

Sasa dada yangu hapo umesha sema ni mume wa mtu huoni htari iyo mbele yako ya kuharibu uhusiano wa watu? Miaka 24 bado naamini ukitulia unaweza ukapata yule mtarajiwa wako,hebu angalia usiwakolofishe hao waliopendana,kama ulikuwa unafanya ivyo basi tambua kuwa ni kosa,ukizingatia yeye ni mume wa mtu!

Anonymous said...

Angalia sana dada hivi ingekuwa kwa upande wako ww ndio unaechukuliwa mume wako ungejiskiaje achana muwe wa mtu anaweza akaja kuumiza moyo wako na ukawa unawachukia wanaume milel huyo mume wa mtu hakufai kama amemsaliti mke wake hata nawe wasalitiwa.

Anonymous said...

pole sister!! hongera kwanza umeliweka wazi hilo. dada jaribu na wewe kufikiria hisia za mwenzako unavyo umpemda hivyo na mkewe halali anampenda hivyo hivyo. jaribu kukaa naye mbali kwa sasa. Jaribu kutafuta mpenzi wako mwenyewe!! uanze kumpenda kama unavyo mpenda huyo wa watu jaribu kuheshimu hisia jaribu kufikiria taumia vipi siku akilijua hilo!! pole sana dad ndio mapenzi yalivyo. ila naamini ukikaa nae mbali mapenzi yatapungua wanaume wapo wengi tena wenye mapenzi kushinda huyo acha kuwa mtumwa wa mapenzi ambae sio wako tena huo ni ushauri wangu kwako.

emu-three said...

Swali kubwa la kujiuliza je kama wewe ungelikuwa ni mke wa huyo jamaa na huyo mkewe ndio wewe ungjisikiaje?
'Mke au Mume wa mtu ni kaa la moto, huwezi kulifutika kiganjani...kamwe! Mapenzi hayo ni ya `uwongo'
Ushauri wangu, achana naye, tafuta wako, au labda anaruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja sawa mshauri akazungumze na mkewe, vinginevyo unachezea `kaa la moto'

Anonymous said...

wewe ni mwizi na arobaini zako zitafika tu,,,huna dini kwani mpaka usijue kuwa kuiba ni dhambi alha

Anonymous said...

Kweli unaamini ni Innocent? Au maana halisi ya neno hili inakupa taabu kidogo? How can he be innocent na ana mahusiano na wewe na huku ni mume wa mtu? Mkewe nae unamtakia nini ndugu yangu? Unataka ujilinganishe nae? Ushauri wangu: Bado una nafasi ya kupata wako achana na mume wa mwenyewe unapoteza muda wako na usichana wako. Wanaposema mwanaume anatafuta pa kubadilisha mboga ndio hasa, na wewe umekubali kuwa mboga ya pembeni isiyoliwa hadharani

Anonymous said...

Kweli unaamini ni Innocent? Au maana halisi ya neno hili inakupa taabu kidogo? How can he be innocent na ana mahusiano na wewe na huku ni mume wa mtu? Mkewe nae unamtakia nini ndugu yangu? Unataka ujilinganishe nae? Ushauri wangu: Bado una nafasi ya kupata wako achana na mume wa mwenyewe unapoteza muda wako na usichana wako. Wanaposema mwanaume anatafuta pa kubadilisha mboga ndio hasa, na wewe umekubali kuwa mboga ya pembeni isiyoliwa hadharani

Angel said...

achana na mume wa mtu kile usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzako naamini ingekua wewe usinge penda mwanamke mwenzako akakufanyia uchafu unao fanya wewe
pili huyo hawezi kua nawewe maisha inamaana wewe huhitaji kuolewa na sikuzote utaishi mafichoni tu
shida za nini achana na huyo bwana mapema
sana ,machozi atakayo lia mke wake atakapo jua ukweli itakua laana kwako na kwa uzao wako binti
kua muungwana achana na mume wa mtu ,wewe bado mdogo utapata wakwako na utampenda zaidi ya huyo
. wewe subiri upate mimba uone kama atakupenda tena
tena atakukimbia hataangalia nyuma au hata asipo kukimbia lakini atatafuta mwingine mpya kamaalivyo kutafuta wewe ilihali ana mke wake nyumbani .tena hua na wasangaa sana nyie wa dada mnaojidai wajanja kutoka na waume za watu kumbe mmefanywa viosk vya kutulizia kiu tu kwa wapita njia ,wakati nyumbani wanayo mastoo ya vinywaji wanajisavia watakavyo ,nyie mkitoka hapo kitandani mwawaza alivyo kushikashika unapandwa na morali wakuushusha hakuna mwenzio akifika nyumbani anaanza kukaa mkao wa kunywa anakunywaaaaaaa akichoka analala hapo hapo wewe mawazo usiku mzima ,acha ujinga tafuta wakwako acha kufwanywa kiosk.utajuta maisha yako yote ,wape hata wa zazi wako heshima hivi mama yako akijua mwanae anatembea na mume wa mtu ndio maana haolewi atajisikiaje aibu!!!!!!! masikitiko ya wazazi wako ni laana tosha acha kuji laaanii tulia omba mungu utapata wa kwako
kama muislam basi halalisheni ili mwenzako ajue hayuko peke yake na ukamsaidie kumpikia huyo bwana na kumfulia sio mwenzako ahangaike kpasi wewe wajua kumega tuu .

Anonymous said...

Wewe mtoto unataka ufanye nini na mume wa mtu tena ulifanya makosa sana kukubali kuwa nae jiondoe mapema kwani unajizuia mwenyewe kupata mume wako. KWANINI MABINTI HAMTULII TENA UNAJUA KABISA NI MUME WA MTU TENA UNATAKA ANG'ANG'ANIE KWAKO UFANYE NAE NINI HUYO SIE WAKO achana nae upesi umwombe Mungu akupe mume wako halali. Acheni tabia ya kutembea na waume za watu jamani inauma ngoja na wewe uje ufanyiwe hivyo uone utamu wake. NASIKIA HASIRA MAANA SIPENDI HIYO TABIA

Anonymous said...

naquote "bwana mwenyewe ni innocent and very caring", binti fahamu huyo bwana kuwa na relation na wewe tayari amepoteza hizo sifa unazompa.mm nakushauri achana nae kwa sababu huwezi kuwa na uhusiano wa kudumu na mume wa mtu,fikiria kama ungekuwa ww mumeo anatoka nje ya ndoa ungejisikiaje? inauma sana,kuna msemo unasema what goes around comes around.ww ni msichana mdogo sana naamini una mambo mengi ya kufanya kwa wakati huu badala ya kuheng na mume wa mtu, ni nuksi unajiwekea kwani hata mungu hapendezwi na kitendo hicho.kuna wanaume wengi tu ambao hawajaoa unaweza kuwa nao hao na ukafunga ndoa lkn mume wa mtu? labda kama imani inaruhusu akuoe mke wa II,inawezekana anakwambia anakupenda lkn kumbuka hata huyo mkewe alimwambia hivyo hivyo wakati anamtongoza but now you can see yupo na wewe,wake up my sister.frank frm dar.

Anonymous said...

Dada nakupa pole sana. Ndoa na iheshimiwe na watu wote. Lakini inawezekana unafanya ufanyayo kwa sababu labda umelelewa nje ya ndoa. Unamwita huyo mzinzi mwenzio Innocent and caring. Anaweza kuwa caring ila Innocent to me, BIG NO. Tena una hatari. Mimi ni msomi lakini nikikujua unatembe na mume wangu tu nakutia ukichaa nakuhakikishia hilo! Kama si ukichaa utavuja wewe maisha yako yote. Siwezi kutumia bastora kwani ntafungwa na kuwahacha wanangu ila kwa mganga naenda kwa kuwa hakuna ushahidi. Cha mtu mavi ukikiona tema mate. Sasa ukute huyo mkewe house wife na mume ndo kitega uchumi pekee alichopewa na mungu na wewe unawaingilia. Subili kurogwa tu malaya wewe.

Anonymous said...

wewe mume wa mtu wa nini? huyo anabadilisha mboga tu hapo kwako, tena we mtoto mdogo, ndio uko kwenye umri wa kupata mwanaumwe wa kuja kutulia naye akuite mke baadae unahangaika na aliyeoa, afu ukifika 30s unaanza kulalamika mi hadi leo siolewi...achana naye huyo, tafuta wako maana anakupotezea muda tu na mkewe hamwachi kamwe!

Anonymous said...

Dada nakupa pole sana. Ndoa na iheshimiwe na watu wote. Lakini inawezekana unafanya ufanyayo kwa sababu labda umelelewa nje ya ndoa. Unamwita huyo mzinzi mwenzio Innocent and caring. Anaweza kuwa caring ila Innocent to me, BIG NO. Tena una hatari. Mimi ni msomi lakini nikikujua unatembe na mume wangu tu nakutia ukichaa nakuhakikishia hilo! Kama si ukichaa utavuja wewe maisha yako yote. Siwezi kutumia bastora kwani ntafungwa na kuwahacha wanangu ila kwa mganga naenda kwa kuwa hakuna ushahidi. Cha mtu mavi ukikiona tema mate. Sasa ukute huyo mkewe house wife na mume ndo kitega uchumi pekee alichopewa na mungu na wewe unawaingilia. Subili kurogwa tu malaya wewe.

Anonymous said...

uNATAMANI KUJUA JINA LA NYUMBA KUBWA EEH. Taja jina la bwanako utamjua mkewe. Wewe dada mdogo usitafute kijana mwenzio muanze maisha unatafuta wenye mali tayari eeh. Mteremko eeh. Kwa taharifa yako utahachwa soon and by the time he is finished with you hutapata hata wa kukupa 'hi'. Nani anataka kuoa kimada mzoefu. Nyie ndo wale wadada walokuwa wanachukuliwa na makonda wakiwa wanafunzi miaka ile ya 80s kwa ela ya chips wasijue kuna mijanaume ya maana inawasubili wamalize shule. Unababaika na ako kagari alikonako mme wa mtu. Uliambiwa wenye ma vogue walikuwa nayo wakati wanaoa. Utajiri unatafutwa na mume na mke ndo maana mnadoda mnaweka high standards wakati wenyewe si lolote si chochote.tafuta wako mama wa kushare ni wakushare tu. Na unayeumia ni wewe kwani kama ulivyosema mkewe hajuhi. Akija kwako anapiga bao moja kwa mkewe mawili, then full kumkumbatia usiku kucha. Wewe na hii baridi unakumbatia mto. Hallooo. Am sure wivu unakuuma ndo maana unataka humjue the wife anaefanya mume asilale nje instead akupe mgao once a week tena mchana kweupeee akitoroka kazini. Aah. Anampenda mkewe shosti analala na wewe pindi mkewe akiwa kwenye edhi, unamsaidia kupunguza nyege aaahh. Angekuwa hampendi si angemwacha. Hiloo. Usifanye mchezo na ndoa wametoka mbali ati.

Anonymous said...

eh my dear..you are too young to sleep with married men! yani at 23 already ushaanza kulala na waume za watu?sipo hapa kukuhukumu nachokuambia tu ni kuwa maadam wewe ni mwanamke unaetaka kuja kuolewa basi fikiria uko na mumeo alafu kuna binti huko nje ana uhusiano nae utajiskiaje?what comes around goes around. Hakuna ugumu wowote wa kumuacha mume wa mtu, muachie mwenzio mpenzi wake tafuta wa kwako bibi, hivi ukikaa unamuomba Mungu akusaidie alafu huku unajua unachukua mume wa mtu unajiskiaje?acha mdogo wangu kabisa huo mchezo

Anonymous said...

Salamu zangu wana blong hii!!
Dada Dinah natumaini hu mzima wa afya.
ushauri wangu kwa huyu binti anayempenda mume wa mtu ni
"achana naye" kwani hapo hakuna upendo wowote na sana sana anapoteza muda wake kwani mwisho wa yote mume wa mtu hurudi kwa mkewe.
Nashukuru.

Anonymous said...

wahenga walishasema MUME/MKE WA MTU SUMU shoga, binadamu tumetofautiana mawazo na fikra, huwezi jua mke wa huyo baba ikitokea akajua about your relationship with her husband unaweza ukaja jutia kuanzisha mahusiano with that man in the first place.

ninavojua mtu hawezi kumuacha mke wake bila sababu inayoeleweka kwani wewe hujui wameanzia wapi mahusiano yao mpaka ukakutana na huyo jamaa, na kumbuka siku hizi kuna magonjwa na wewe bado mbichi kabisaaaa achana nae endelea na maisha yako ili ujiepushie matatizo makumbwa ambayo yanaweza kukukumba huko mbeleni.

Anonymous said...

OF COURSE HAWEZI KUJA KUWA NA WEWE TENA IKIWA KAMA NI NDOA YA KANISANI. JE, JARIBU KUFIKIRIA INGEKUWA NI WEWE KUWA MMEO ANA MWANAMKE MWINGINE NJE, UKIWA KAMA MKEWE NA UMELIJUA HILO UNGEFANYAJE/UNGEJISIKIAJE?
KUMUACHA UNAWEZA NI KUJIENDEKEZA TU.KWANI UMEZALIWA NAYE?? ACHA UJINGA, MUACHE MARA MOJA KAMA JIBU LA SWALI HAPO JUU NI: "UNGEUMIA ROHO NA USINGEPENDA ITOKEE MUMEO AWE NA MWINGINE". PERIOD!

Anonymous said...

mdogo wangu hebu achana na huyo mume wa mtu, at 24 kwanini uamue kuwa na mume wa mtu? hakukuwa na mwingine zaidi yake? alafu unasema yuko inocent the way unavyomchukulia ndivyo wengine pia wanamchukulia. anamjali mke wake ndio maana hajakuonyesha usije mfanyia fujo. kuwa mwenzi wa maisha yako yote ni ndoto au wamaanisha amwache mkewe? anza kujichanganya na vijana wenzio utampata atakae kuwa wako na si wa mtu!

Anonymous said...

wacha ujinga ww, mume wa mtu anakupotezea muda tu hana jipya wala nn, hv unajisikiaje kuwa na mume wa mtu? huna uhuru nae, hawezi kulala kwako, yani just bushit tu, muache tafuta wako. shauri yako ucpomuacha kwa hiari utakuja muacha kwa kasheshe, ohooo...

Anonymous said...

km anakupa jando la uhakika na anajua kutombana tulia nae.kwani mwanaume kutombana na mboo ilo kwenda shule

Mama 2 said...

Hivi wewe!!! ndo kwanza una miaka 24 uko na mwanaume wa mtu! hao vijana wenzako ambao unaweza kutoka nao na kuwaintroduce kwa mtu bila wasiwasi utakuwa nao saa ngapi. Maana mume wa mtu bwana huwezi kumtambulisha hovyo kwa watu kama boyfriend wako mwenyewe, huwezi ukatoka naye outing peupe watu wanakuona. Wewe unakuwa wa kujificha siku zote. Hayo siyo maisha tafuta wako. Na ukirogwa ujifanye unazaa nae tu umekwishaaa! anatafuta dogodogo mwingine, maana nawe unakuwa huna tofauti na mkewe, majukumu yanaongezeka. Mume wa mtu waachie watu walioenda age na wameshajichokea na maisha, wanaishi kwa kubangaiza. Lakini wewe bado mdogo. Hakuna nyumba ndogo hata moja isiyoonyeshwa mapenzi, but yanakuwa ya uongo. Olewa naye uone kama hayo mapenzi yatakuwepo. ANAKUDANGANYA HUYOOOO!!! ANAKUPOTEZEA MUDA WAKO!!Ndoa tamu asikwambie mtu, kama mnaishi kwa amani. TAFUTA WAKO BIBI!!

Anonymous said...

yaani jamani mi riho inauma,kweli mme wa mtu halafu umeshafahamu kwa nini usimwache?unachofanya ni dhambi kubwa kwani una wadhulumu watoto wa hiyo familia.na siku mkewe akifahamu ndo utajua kama ni unasikia raha au utamu kuwa na mumewe achana nae

Anonymous said...

umefanya la maana sana kusema ukweli kuwa unatembea na mume wa mtu. ACHA HIYO TABIA MUME WA MTU/MKE WA MTU NI SUMU. Kuna dada nilishuhudia alionywa aache hiyo tabia hakuacha matokeo yake alitiwa TENDE LA MIGUU yote miwili akawa inavuja maji na usaha, kahangaika kote imeshindikana iliyobaki kamrudia Mungu ila matende yapo pale pale na bado yanavuja maji na usaha. ASIYE SIKIA LA MKUU HUVUNJIKA KUU ACHA HIYO TABIA

Anonymous said...

ww ni mtu wa ajabu,tena hujatulia kabisaaa!tatizo mabinti wengi mko after money,unafikiri dhiki ukiziendekeza ndo zitaisha?Napenda ujue kuwa huyo bwana ana mke anayempenda ww anakutumia tu na inawezekana mko wengi mnaodanganywa na bwana mmoja.Wewe ni mdogo bado ukitulia utapata mwanaume wa kuwa huru naye;kuwa makini mkewe akijua utaonja joto ya jiwe!

Anonymous said...

we mtoto jamani hivi hujui kuwamumewa mtu nisumutena kali inauwa, kama umejua kuwa nimumewa mtukwa nini usikimbie ukamwacha sasa unasema umenasaunampenda,hakika binti kam kweli weweunasali una Mungu wakoachan na mume wa mtu kabisa,sikubalianina wewe unaposema umeshindwa kumwacha kumbuka wat goes roundcomesround lazima utavuna tu ipo siku na weweukijakuolewa utaibiwa mumeo na usilie kumbuka utakuwa unavuna ulichopanda,
huna hata hurumahujuianaweza kuwa na watotohalafuweweunataka uchukue muda ambaohuyobaba angekaana mukewe nawatotowake,
kuwana aibubintihamnacha ushauriachana namumewa watu kunamagonjwa unataka kuumwa jamaniwatoto wasiku hizi hamna adabu kweli,

Anonymous said...

we mtoto jamani hivi hujui kuwamumewa mtu nisumutena kali inauwa, kama umejua kuwa nimumewa mtukwa nini usikimbie ukamwacha sasa unasema umenasaunampenda,hakika binti kam kweli weweunasali una Mungu wakoachan na mume wa mtu kabisa,sikubalianina wewe unaposema umeshindwa kumwacha kumbuka wat goes roundcomesround lazima utavuna tu ipo siku na weweukijakuolewa utaibiwa mumeo na usilie kumbuka utakuwa unavuna ulichopanda,
huna hata hurumahujuianaweza kuwa na watotohalafuweweunataka uchukue muda ambaohuyobaba angekaana mukewe nawatotowake,
kuwana aibubintihamnacha ushauriachana namumewa watu kunamagonjwa unataka kuumwa jamaniwatoto wasiku hizi hamna adabu kweli,

Anonymous said...

Ati nini???? Unasema jamaa ni innocent and caring???? Kama angelikuwa ni innocent asingekuwa anamsaliti mkewe na kama ni caring angeanza huo ucaring wake nyumbani kwake. Wewe kama unataka mchi vijana wenye uwezo wako wengi tu tena wengine wana vijisenti vyao. Sijui uko mji gani, ukitoa e-mail yako, kama wewe unafaa, nitakutafuta nikuchangakie barabara. Utamsahau huyo bwana wa watu. Busyshaft.

Anonymous said...

Unaufahamu usemi wa Kiingereza What goes around comes around? Tafakari.

Anonymous said...

Wewe nadhani bado hujapata mtu singo akakupiga mparago wa nguvu. Usijitie kuwa jamaa ni innocent na mashamsham mengine.

Anonymous said...

we ni ngono tu ndo inakusumbua na tamaa zake.we unadhani mwamke angefanya hivyo kwa baba yako ungekuwa na familia leo.Acha Acha! haraka sana.hilo pepo la ngono lipeleke kwa boyfreind wako.naamini ulikuwa naye be4 hujakutana na husband wa m2.

Anonymous said...

Dah....bahisi hata kulia kwa comment zenu...maana mimi niko kweny mahusiano na mume wa mtu ila ckujua wala hakusema...nampenda kufuru sasa nashindwa hata kumpa ushaur huyo dada. Naregret