Friday, 17 September 2010

Shukrani kwa Maoni, ushauri na Mawazo yenu, sasa nimejitambua!

"Nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipo mshukuru muongozaji wa blog hiimy sister DINAH, shukrani zangu pia ziwaendee wale wote ambaowalisoma, au kuchangia katika ujumbe wangu ulio rushwa katika blog hii pendwa tarehe 18/08/2010 (Bofya hapa).

Kwa heshima na taadhima nawashukuru sana tena sana, sababu amini msiamini mmenionesha mwanga. Wapi nielekee. Nakubali kusema kuwa nilipoteza muelekeo ila kwa mchango na mawazo yenu na ushauri wenu kupitia hapa nimefanikiwa kufanyia kazi yote kutoka kwa kila mdau.

Kulinganana majibu hayo sasa nimejitambua, nasema hivyo kwasababu nilijaribu kumuomba tukae chini nijue kipi kinamsumbua akashindwa kutokea mahali ambapo tuliekubaliana zaidi ya mara mbili that means kweli hana mapenzi ya dhati kwangu.

Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na masomo yangu ya Ualimu, kwa wale ambao walishindwa kufahamu kama ninasoma ama la. Mimi ni mwanachuo wa Diploma ya Ualimu mwaka wa pili sasa.

Dada dinah pamoja na wale wenye mapenzi ya dhati na nia njema ktk blog hii Mungu awabariki sana."

1 comment:

Anonymous said...

Ninashukuru kama umelielewa hilo. Manake angeendelea kukupotezea muda wako. Mungu yupo pamoja nawe atakusaidia na utapata mchumba/mke mwema na utamfurahia katika maisha yako yote.Kila kheri katika masomo yako.By ansncion