Nimegundua mume wangu kampa mimba mwanamke wa nje-Ushauri

"Habari dada Dinah, mimi ni moja ya wadau wa blog yako. Nieolewa na ni mama wa mtoto mmoja ana miaka 3+ na ninakaribia kupata baby no.2 panapo majaaliwa mwishoni mwa mwaka huu.

Mwenzenu nina matatizo ambayo naomba wadau wanisaidie kunipa ushauri nini cha kufanya maana nimejaribu kufikiria sioni njia ya kutatua matatizo yangu. Mimi na Mume wangu tangu tumejuana tumekuwa tukiishi kwa amani na upendo, lakini cha kushangaza hivi karibuni nilimuona kabadilika sana kiasi kilichonifanya nianze kuchunguza kulikoni?

Mbona mambo hayaendi sawa kama zamani! baada ya kuanza uchunguzi niligundua mume wangu kuna watu anawasiliana nao sana bila kutaka mimi nifahamu wanawasiliana kwa ajili ya issue zipi. Hapo nilijawa na wasiwasi zaidi nikaamua kutega baadhi ya number kwenye simu ili msg zikitumwa asizione kwenye inbox ila ziingie kwenye folder tofauti.

Nilipokuja kufungua lile folder nilikuta msg nyingi za mdada mmoja ambaye ni mpenzi wake na alikuwa akilalamika kuwa hamtumii msg wala kumpigia simu nakuwa amepunguza kumjali na yeye ni mjamzito na ameamua kuitoa hiyo mimba kisa hamjali sababu hampigii simu.

Nilipoona hizo msg nilitamani kufa hapohapo! maana sikutegemea kama mume wangu angekuwa na mwanamke nje ya ndoa yetu ambayo bado changa. Nikaamua kumuuliza mume wangu akasema hana mwanamke nje na hategemei kuwa na mwanamke nje ya ndoa.

Nami kwa kuonyesha kuwa hamna msg niliyoona nilikaa kimya kwa muda wa wiki mbili bila kumuuliza kitu. Baadae nikakuta msg nyingine ya huyo mwanamke akimuuliza mume wangu anaamuaje kuhusu ujauzito alionao?

Nikaamua kuhamishia ile msg kwenye inbox na kumuomba mume wangu aisome ile msg na anieleze kuna kitu gani kinaendelea. Chakushangaza mume wangu akasema haijui hiyo msg, basi nikamwambia tupige hiyo simu tukiwa wote nae akakubali yule dada alipopokea akaanza na maneno yanaonyesha wao ni wapenzi wa siku nyingi.

Mumue wangu akajidai kumfokea yule dada lakini haikuleta maana yeyote, nikaamua kuchukua ile namba na nikaipigia mimi mwenyewe nikimuomba tukutane kwani nina shida nae, yule dada akakubali lakini hakutokea na simu yangu hapokei tena.

Huku mume wangu hajawahi kulala nje ya nyumba yetu hata siku moja na siku zote yeye huwahi kurudi kutoka kazini kabla yangu maana mimi huwa narudi kuanzia saa kumi na moja na kuendelea na yeye hurudi kuanzia saa nane mchana.

Hapo naomba dada Dinah na wachangiaji wengine mnisaidie kimawazo, nifanyeje maana nimepunguza sana upendo kwake kila nikimuona mume wangu namuona kama ni muuaji maana kama ameweza kufanya mapenzi nje ya ndoa tena bila ya kutumia kinga si anataka kuiteketeza familia yetu?!!

Asanteni"

Comments

Unknown said…
pole dada mi nasikitika tu maana nami mume wangu kama wako...ukimuona huwezi kumzania lakini...yaani hata cha kuongea sina ila naomba nijuze na mimi jinsi ya kuhamisha messege kwenye simi kutoka inbox to another folder....nazani nami itanisaidia kwa mume wangu maaana utulivu zior kabisa
Unknown said…
pole dada mi nasikitika tu maana nami mume wangu kama wako...ukimuona huwezi kumzania lakini...yaani hata cha kuongea sina ila naomba nijuze na mimi jinsi ya kuhamisha messege kwenye simi kutoka inbox to another folder....nazani nami itanisaidia kwa mume wangu maaana utulivu zior kabisa
Anonymous said…
pole mama kwa masahibu hayo,inavyoonyesha huyo mwanamke hatakiwi tena,ila huyo mume kwa kuwa ame cheat,wakati ndoa yako bado changa,ipo siku ata cheat tena tu.huyo mwanamume hatotulia kabisa,na ushauri katika mambo ya ndoa ni mgumu,mateso unayapata wewe,na kila mtu atakupa ushauri tofauti,lakini uamuzi wa mwisho unao wewe mwenyewe,kama uendelee kumvumilia au uanze maisha yako upya.usiamue kitu kwa kuogopa jamii itakuona mbaya,hapana amua kwa kuwafikiria watoto wako,kwani mtoto ni mama,asikwambie mtu.
Unknown said…
pole sana mpenzi i know how you are feeling right now. Kuhusu ushauri kumchukia mumeo sio dawa bali ndio kwanza unazidi kuleta matatizo kwenye ndoa yako. Kama kweli unampenda mume wako punguza hasira rudisha upendo kama zamani ingawa ni ngumu kwani moyo huwa unauma sana ila hauna jinsi huyo ndio mumeo na baba watoto wako anza kusali kama ulikuwa husali kwani sasa hivi ndoa zina matatizo sana mpenzi bila kuomba mungu ni ngumu sana jitahidi usali na kumuomba mungu akupe moyo wa uvumilivu na kusamehe na pia umuombe mungu ili aachane na huyo mwanamke wake na nakuhakikishia hakuna mungu anachoshindwa ukimuomba kwa imani na inaweza ikachukua muda kidogo, ila usikate tamaa endelea kumuomba mungu sana kama mkristo unaweza kutafuta makanisa ya kiroho ukaomba wakusaidie kwa maombi na kukufundisha jinsi ya kuomba kama ulivyosema mumeo anawahi kurudi nyumbani na hajawahi kulala nje ya ndoa basi ujue ni ibilisi tu alimpitia na jifunze kutokagua simu ya mumeo kwani unajitafutia magonjwa ya moyo bure huyo ni mumeo ndio maana akakuoa na anarudi nyumbani cha msingi ni kumuomba mungu aachane na huyo mwanamke na asimjue tena. Ukianza kununa ataenda kwa huyo mwanamke au atatafuta mwanamke mwingine ili aweze kupoza machungu na matokeo yake anaweza kuhamia huko huko kabisa ukifanya mchezo. So omba mungu tena ukimaanisha na kuwa na imani isiyotetereka usifanye mchezo kabisa watoto wako wanahitaji malezi yako na ya baba yao. Kuomba mungu ndio dawa kwani huwezi kushindana na wanadamu wameshakutangulia lakini mungu yeye ndio mkuu na muweza wa yote hakuna anachoshindwa.

good luck
Anonymous said…
pole dada yangu
then huyo mwanamke asikumize kichwa wala huyo mumeo usimchukie kwa ajili ya hiyo issue achana naye mtoto unayemjua wewe ni yule uliyemkuta amezaliwa kabla ya ndoa,atakayeletwa baada ya hapo si wako huyo na una haki ya kumkataa, then huyo mwanamke ni malaya tu ukute anataka kuvunja ndoa yako ndugu yangu wanawake wa hivyo wapo wakiona mambo yako yanaenda vizuri ndani kwako watafanya kila mbinu wakuchafue ufanye uamuzi ambao si sahihi mimi imenitokea na nilimshitilia mbali mpaka leo nna amani na furaha na mume wangu. Achana naye malaya tu huyo ana lolote jipya angekuwa wa maana si angeolewa yeye.
Anonymous said…
mimi nakushauri tulia mdogo wangu wanaume wote ndivyo walivyo inatakiwa kuwa na imani tu.
emu-three said…
Mimi nakushauri bado uendelee kfanya uchunguzi wa kina, kwani meseji peke yake haiwezi kuhakiki dhana yako. Wapo watu wametumiwa meseji za uongo wakachukua hatua za haraka bila kutafiti na matokeo yake ni majuto!
Kama kweli mume wako ana mahusiano nje, basi itabidi umkalishe chini na ushahidi wako ambao umeshaukamilisha, akikana basi utajua kuwa jamaa sio mwaminifu, vinginevyo mwingine atakiri udhaifu wake na atakuomba msamaha.
Swali ni je kwanini alienda nje? tamaa, au kuna walakini katika mahusiano yenu? haya atayasawazisha dada Dinah
Anonymous said…
Yaani nakuonea huruma sana, kweli wanaume hawaeleweki, na unakuta unamfanyia kila kitu, with all Biblical/World definition ya mke mwema anayependa kujenga nyumba yake/familia na ndoa yake unafanya lakini cha ajabu bado haya majibwa(sorry I am generalizing) hawashikiki. Kweli sijui hata mtu atatoa wazo gani la kukusaidia zaidi ya... kwa upande wangu,kwa ajili sasa umeshakuwa mama na unamtoto tayari na unamwingine unamtarajia, inabidi ufunge/umeze hayo maumivu, uchungu mumeo anayokuletea ili uweze kupata nafasi ya kuconcentrate kwa watoto wako, yaani futa mawazoni kabisa maudhi hayo ili upate fursa ya kufanikisha salama mida yako ya kujifungua vizuri bila blood pressure na pia uweze kuwa mama mzuri kwa mwanao mdogo - yaani utu uzima ni jalala and you need to act as such. Mumeo inaonekana alivyokana wakati ulipomuuliza kuhusu sms na mkampigia simu huyo msichana pamoja na kabisa ukaona mumeo amefanya act wakati wanaongea basi hiyo ni dalili kuwa anaweza hata kuwa stubborn ukiendelea kumuuliza na pia atakuumiza sana moyo kwa labda majibu yake (nasisitiza hivi maana wewe sasa ni mjamzito, na hormone zako ziko everywhere rightnow) so you REALLY NEED TO UNDERLINE AND BOLD YOUR PRIORITIES HAPA - yaani hicho KINYANGARIKA cha nje kisije kikakufanye upoteze mtoto kwa ajili ya mawazo because you very well know that... SHE IS NOT WORTH IT AT ALL, na hata huyo mume wako ukifanya jitihada za kumuuliza kuhuzu hizo message na asipoonyesha kuomba msamaa na kuona kipi ni muhimu sasa hivi katika familia yake - then be an IRON LADY AND MAKE decision ya kuconcentrate na kulea mimba(siyo nakwambia uondoke ...hapana) lakini nakwambia msogeze pembeni halafu uconcentrate to what is really really important kwako wewe sasa hivi, kama ni kuishia kupata mawazo na kuhatarisha mimba yako na kutoweza kutake care ya mtoto wako mkubwa then be it, lakini kama unaona umuhumu ni kusimama as a STRONG WOMAN AND STRIVE FOR WHAT IS RIGHT FOR THE HEALTH OF YOUR SOON TO BE GOLDEN BUNDLE AND THE OTHER CHILD, THEN BE IT - Good luck!!
Anonymous said…
Dada pole sana! nakupa pole ya pili kwa sababu unaonekana ulimwamini sana mume wako kupita kiasi, sasa nisikilize, kwa taarifa yako hakuna mwanamume mwenye mwanamke mmoja, hiyo uiweke akilini kuanzia leo mpaka kufa kwako, ni kwamba imetokea tu akakuoa wewe ukawa mke wake kwa sababu ya mifumo ya jamii zetu, lakini ninachotaka kukuhimiza hapa ni kwamba, kwanza habari ya kushika shika simu ya mumeo utakuja kufa na presha bureee, na hakuna simu ya mwanaume isiyokuwa na message za wanawake awe ameoa au hajaoa.
Mpendwa, kwa sasa zingatia afya yako ili uweze kujifungua salama, na usife na presha, mbona mambo ya kawaida sana hayo dada yangu wewe unapaniki nini, ok wewe umemwamini na kilichokuaminisha zaidi ni kwa sababu mumeo anatoka kazini machana, ahaa asikudanganye mtu firauni ni firauni tu usinzi unaweza kufanyika hata saa moja asubuhi kabla hata mtu hajaingia kazini, na yeye anakuzuga ooh mke wangu nipo nyumbani tangu saa nanae mchana, hapo anakuwa ameshakufan yia timing na kujua ni namna gani anakufix.

na huyo dada uliyetaka kukutana naye ulikuwa una nia ya kufanya nini? sikiliza, lazima uwe makini na ujifunze kuishinda hasira yako, vitu kama hivyo sio vya kuendea kwa hasira kwa sababu kwanza huji huyo dada ni wa aina gani na hujui yeye ana mawazo gani kuhusu huyo mwanaume, imagine ungeonanan naye na akakupiga au akakujeruhi au hata akakufanyia kitu kibaya ukadhurika, ungemlaumu nani? najua inauma sana lakini siku nyingine fanya analysis ya kutosha ili uwe na evidence, na ikiwezekana umfahamu mbaya wako hata kabla hujataka kuonana naye uso kwa uso. Utapoteza maisha kwa sababu ya mwanaume nyang'au huyo. Watu wapo kwenye ndoa kukamilisha torati tu dada na sio mapenzi yaa kweli, wewe tulia madam ulishakubali kuwa mke wake, wewe tulia.
Anonymous said…
pole sana mi nina tatizo kama lako, mume wangu kampa mimba mwanamke, nje, mbaya zaidi hatujapata mtoto ktk ndoa yetu kwa miaka 5 sasa, moyo unaniuma cha kufanya sijui,,kuwaambia ndugu wazazi naona aibuu, yaani nipo nipo tu,tuone wadau wengine watashauri nini, nami itanisaidia.
Anonymous said…
pole sana dada! wanaume ni wa chafu sana ukichunguza sana utakufa na wanao wata pata shida just pray n kneel down ! ma ldia
Anonymous said…
Pole sana bidada kwa hayo yaliyokukuta. Lakini ukitaka ndoa yako iwe nzuri usipeleleze anachokula nyuki. wewe kula asali tu kweani UNGEJUA ALACHO NYUKI ASALI USINGEKULA. huyo ni mwanamke uliyebahatisha kumfahamu je usiowajua unafikiri wako wangapi? Maadam wewe umepewa heshima ya kuwa mama mwenye nyumba basi tulia mshukuru Mungu.....Kizito!!
Mdada said…
Pole sana, tuko wengi wenye tatizo kama lako. Mie naomba unisaidie jinsi ya kufanya msg isiingie kwenye inbox. Naomba sana.
Anonymous said…
Pole sana dada kwa yaliyokukuta. Kusema kweli hawa viumbe kwa jina la mwanaume si wa kuwaamini sana. Kusema kwali umedai kuwa mmeo hajawahi kulala nje hata siku moja, lkn ujue kulala na mmeo kila siku si kwamba hawezi kutoka nje ya ndoa. Unajua kuna wanaume ni mabingwa wa ngono ya chap chap, yaani ile lunch time ya kazini kwake anaitumia kula na kungonoka na muda wa kurudi kazini yy anakuwa wa kwanza.

kwa kweli cha muhimu kwako ni kukaa naye na kuzungumza nikimaanisha vunja ukimya. Kama akikiri kosa msamehe kwani hakuna malaika duniani. Inawezekana pia nawe una vijikasoro vilivyochangia yy kutoka nje ya ndoa yenu, lkn kwa sasa hivi ni kuelewana tu kwani SIKU HAZIGANDI. Msamehe, sahau yaliyopita na endeleeni kulea watoto wenu kwa pamoja. Cha muhimu zaidi mhimize kutumia kinga kama akizidiwa manake asijekuua.

Jambo lingine nakushauri uache kuchunguza simu ya mmeo, utajiua bure kwa presha. Ukimchunguza sana kuku hutamla hata kidogo.

Julie
Anonymous said…
Fanyeni kikao cha familia pande zote mbili. Kisha aulizwe waziwazi: Je, bado anataka kuwa katika ndoa au la? Na kama anataka kuwa katika ndoa, anataka ndoa ya aina gani? Kama amechoka na ndoa usimng'ang'anie. Lakini lazima akubali majukumu ya ulezi wa watoto. Watoto wasitumike katika mchakato wa wazazi kukumoana ili watoto wasije kuathirika kisaikolojia.
Anonymous said…
Dada pole ni mitihani ya kimaisha hiyo....Ndoa ni challenge sana ila vumilia..

Unajua huyo mumeo kitendo cha kumruka na kumkataa huyo mwanamke inaonesha mumeo bado anakuhitaji na kaupendo kwako kapo...Mimi kama mwanaume,kwa maelezo yako inaonesha mume wako aliteleza tu bahati mbaya..yaani kwa mumeo ni ajali kabisa hiyo...

Cha kufanya mumeo akubali kumtunza huyo mtoto..wewe jiimarishe kwenye familia na kama una watoto wako basi leo vizuri wala usikwazike..jitahidi kusahau mungu atakusaidia...huwezi jua mwanamke huyo alimpa nini mumeo hadi akabeba ujauzito wake ambao mumeo hautaki..
Ili kurudisha familia yako kwenye track na mapenzi onesha kuwa close na mumeo asije zama huko kabisa na mpende kama zamani..hii itamfanya kujirudi na kuunda upenda na familia imara tena...Hiyo mimba ni maji yameisha mwagiga na huyo kiumbe hana hatia so kubali tu...

kama unafanya kazi ongeza bidii na jitahidi kusahau machungu..wee unabahati mumeo analala home kila siku...Pia jaribu kuchunguza ni nini mumeo anamiss toka kwako..je unampa game kiasi cha kumridhisha?asikwambie mtu ngono tamu huimarisha uhusiano..am telling u!..kama hujui mapenzi jifunze..internet ipo!

Gluv

gluv100@yahoo.com
Anonymous said…
JAMANI DADA POLE SANA, LAKINI HAPA TUAMBIAE UKWELI, NDIO NIMESOMA MAONI YOTE KWA WALIOCHANGIA, LAKINI CHA AJABU HAKUNA ALIYEONGELEA UKIMWI NAONA TU USHAURI WA KUWA CLOSE NA MMEO JAPOKUWA HUYO HUYO MUME ANAWEZA KUMHATARISHIA MAISHA YAKE NA KUMFANYA WATOTO WAKE WAWE BILA MAMA KWA AJILI YA TAMAA ZAKE ZA FISI?, MI NAONA KAMA MWANAMKE NI LAZIMA UMWAMBIE MUMEO KUWA WEWE HUMWAMINI TENA UAMINIFU HUO UTARUDI TU AKIKUBALI KWENDA KUPIMA, NA UCHAGUE ZAHANATI/HOSPITALI UNAYOIAMINI. TUMESHACHOSHWA NA WATOTO YATIMA, NA HII KWA KWELI KWA WENZETU WANAUME NI FORMULA YA KULETA UKIMWI NYUMBANI NA KUSABABISHA YALE YALE....USIMWOGOPE KABISA MAMA HAPA (SINA MAMA UACHE KUMHESHIMU KAMA MUME LA) LAKINI USIMWOGOPE KUDAI KUWA KWA VILE HUMWAMINI INABIDI AENDE KUPIMA, NA AKIKATAA UANZE INTRODUCE CONDOM CHUMBANI KWAKO. NAJUA UTASEMA NDIO ATAHAMIA KWA HAWARA, SIO HIVYO DADA, YAANI HATA KAMA USIPOWEKA SHERIA ZAKO ZA KUKUTUNZA WEWE ILI UWEZE KULEA WANAO MPAKA UKUBWANI NI LAZIMA TU KATIKA SAFARI YENU YA MAISHA AANZE KUTOKA TENA NA TENA NA WANAWAKE WENGINE (AMESHAONJA ASALI HUYO) - NYUMBA NYINGI SIKUHIZI MWANAMKE ANAFANYA UAMUZI HUO ILI AWEZE KUTUNZA WANAE. WANAUME HAWA MARA NYINGI HAWAFUGIKI.
Anonymous said…
Pole sana shost wangu,mwanamke yoyote mwenye mahusiano na mwanaume kama una mpango wa kuachana nae, awe boy friend au mumeo basi shika simu yake na uwe unaifuatilia, ni lazma tafrani zitakuja tena zingine zinaletaka vifo.Lakini kama mumeo wampenda na unamwamini basi simu yake usiguse kabisa.Kwa shost tatizo lako hili litakuchanganya sana kama utaendelea kulifanyia ligi na kulifuatilia kwa undani, we ongea na mumeo msikilize anakuahidi nini baada ya kugundua mambo yake ya nje,kama anamsimamo na wewe na anaonyesha anakujali futa wazo la mwanamke mwengine anakuchukulia mumeo tena mjamzito.Wanaume walio wengi wanawanawake zaidi ya mmoja,tena shukuru mungu huyo wa kwako alifanya siri ila we umemchokonoa,ili uishi kwa amani na furaha tele acha kumfuatilia mwanaume,muweke mumeo kwenye sala zako za kila siku,mungu amuepushe na tamaa za wanawake wa nje na ndoa yako itakuwa salama.Mi pia yalinikuta ila kwa sasa nina amani ya ajabu huwezi amini.
Anonymous said…
Wakina dada mnapotoa comment zenu ..haina haya ya kuwachanganya wanaume wote..coz sisi pia tunawake zetu na tunawatreat vizur...wewe kama mumeo au mpenz wako kakukosea basi ongea kwa kumtaja mumeo sio kusema eti wanaume ndio walivyo....sio kweli kila mwanaume anamwanamke zaid ya mmoja...Je unaonaje pale mwanamke anapomsaliti mumewe kisha na wanaume tuanze kuwasema wote kwa ujumla?..kitu ambacho sio kizur mimi mwenyewe siwez kuwasema kuwa wanawake mna tabia flan coz sijawahi kuona hata siku moja mke wangu akinifanyia kitu nisichopenda kias cha kuanza kusema eti wanawake ........so be specific..kama umeumizwa bac omba ushaur
Anonymous said…
tafadhali mnaotoa maoni, haipendezi kumtukana huyo mwanaume, mpaka hivi tunavyojadili tumesikiliza upande mmoja tu hatujasikia upande wa pili hivyo hatuwezi kuanza kutukana kwani hata ukirtukana haisaidii kitu, lakini pia kama ni kweli huyo baba kafanya hivyo bado hatujui nini kilimtokea, siku hizi kina mama mnatumia nguvu za giza kuchukua waume za watu, yawezekana alifanyiwa hivyo au ni kweli ni tamaa zake, pia yawezekana alikosa hio huduma ndani ya nyumba akaamua kuitafuta nje, kuna baadhi ya kina mama hutumia njia ya kumnyima mume wake tendo la ndoa kwa ajili ya kushinikiza mambo anayoyataka, sasa kama hali ndio hio unategemea nini? kazi kwako dada Dinah tuweke sawa
Anonymous said…
duh, hivi kwani huyo dada kasema ni mjamzito? huyo anymous wa 3:23:00pm vp? soma vizuri kabla huhachangia.pls then bidada saidia namna ya kufanya msg zisiingie kwa inbox. mada ndefu zinaboa kusoma. just write short and clear and point guys. camon
Anonymous said…
Pole my dear, mara ya kwanza niliisoma hii post niliumia roho sana sana....i can put myself in your shoes and understand well how you are going through rite nao,
My dear kama hujawai kusali basi sali piga magoti umwombe Mungu kwanza akupe nguvu na hekima ya kukabiliana na matatizo yote sasa ivi halfu muombee mumeo aweze kukiri na kuomba msamaha then siku moja jitahidi uwe kwenye mood nzuri then mwombe mumeo mtoke mkakae sehemu ambayo unaona ni nzuri kwa mazungumzo ya aina hiyo umuulize tena taratibu mimi nna amini kwasababu utakuwa umeshasali lazima atakuambia ukweli...na kama akiendelea kukataaa (which i gave it ver small percentage)jaribu kuishi maisha yako mwenyewe sijakuambia utoke nyumbani hapana anza ku-concentrate kwenye vitu vinavyokufanya uwe na furaha na kumsahau yeye thou mnaishi nyumba moja, toka na marafiki, concentrate kwenye kazi/biashara yako, toka na watoto wako, kuwa mrembo tena mamii jitahidi kuwa mrembo sana sana uwezavyo...jaribu kumwonyesha kuwa awepo asiwepo wee maisha kwako yanakwenda kama kawa...nakuambia atajisikia vibaya na kuanza kujileta mwenyewe, usisahau kusali my dear Mungu akutie nguvu.
Polee...wish will help you more,nitakuombea na mimi
Anonymous said…
My dear, two wrongs don't make a right! Yes, what he did was wrong, and look, he's so much shocked he can't own up. This is the real time to LOVE him more!! Nothing beats true love.
Ok, so you get worked up and end the marriage...in other words you push him right to the arms of that other woman, or more.
Let the anger pass, talk it out and assure him of your love. Real love is divine an holy, it moves mountains.
About the other woman, that is his problem, please allow him to solve it himself (not with your help)
Finaly, check, for every wrong in a relationship/marriage, both parties have some responsibility ... own up to your wrongs, learn a lesson and ashame the devil, by emerging out of this better, stronger!! Best of luck!

I am Harry, from Kenya.
Anonymous said…
Pole dada ndio maisha ila mbona watu wengi wanachangia kwamba usichunguze simu ya mumeo wakati hao wanaume ikiita wao wa kwanza kusiliza unaongea na nani kwa wakati huo?

Jitahidi kulea mimba yako na uangalie maisha ya mbele ndivyo walivyo usiiumiesana coz ndio maisha utaachana na huyo na ukapata mwingine ikawa afadhali ya huyu ulie nae

so muachie mungu ila wanaume wanakeraaaaaaaa sa hao kaz kutuambia sie walimu wetu vipofu ila wao wa kwao wanaona mpaka nyeti za wanawake wa nje hawana hata haya utampaaaaaaa mpaka ubinuke sarakasi lakini akitaka kutoka atatoka tu wanaume hapana wala sio sababu ya style may be huko nje anapewa kifo cha maende tu na anaridhika.

Lea baby wako na kuwa tayari kwa kupata huyo mpya usijipe presha ukaja kufa sababu ya mume ukifa kesho yy arobaini hata afikishi anaishi namwanamke mwingine so dada kinachotakiwa ni uvumilivu tu.

Then kuwa busy na mambo yako wala usikae ukawaza coz itakuletea matatizo mengine najua inaumaaaaaaa sana coz yamenikua tena wangu mkubwa huyo wa nje mdogo wamepishana miezi 6 tu na nimekuja jua kipindi nataka kuolewa so ingekuwa ww dada si ungetaa kuolewa so ndio life styke yetu.
Anonymous said…
Pole dada unajua wanaume hata sijui niseme nini wanaume wote samahani. kwanini unapogundulika kuwa unacheat hutaki kukubali, unajua hakuna kilichofichika chini ya jua. Shemeji yangu mme wa dada yangu alikuwa anacheat sana kila mkewe akigundua anasema sifanyi na umenifananisha, alifanya uchafu mwisho wa yote kuna watu wakamstua na kumpa no za simu za huko anakocheat tena ni luchtime lakini alikuwa anaitumia vema, kupiga siku hiyo mchana kapokea mumewe kurudi nyumbani alikataa kabisa sie yeye ni sauti tuu labda zimefanana lakini hakuwa yeye, na kumnunulia zawadi juu, kufunika madhambi kwa mungu hakuna kilichofichika, Sasa mwanamme mgonjwa HIV posive sasa hebu niambie na kujidai kote yeye ni hafanyi hayo mambo kwa kweli mungu atusaidie sana sana, wanaume tulieni sihukumu lakini wanaume ni chanzo kikubwa cha kuleta magojwa majumbani hata kama wanawake wanaleta lakini kiasi kikubwa ni wanaume. SAsa wewe huyo mumeo alivyofanya hivyo amekumbuka hata kujilinda, au alijitosa tuu.kama walipima au ndiyo karukia basi anastuka liko magomeni, mbaya mno hakuna kitu kizuri kama wanandoa kuwa waaminifu.TUlia uzae mwanao usijipe pressure ukafa kabla ya wakati ndugu na hali yako muombe mungu akuvushe ni kipindi utapita na utashinda.
Unknown said…
mmh!!!!pole sana dada yangu,kutokana na maelezo yako,mi nahifkiri kwa asilimia kubwa sana uwo ni mchezo unaachezewa ili uachanishwe na lahazizi wao kipenzi ch amoyo wako,si unajua tena ndoa tena siku hizi mdogo wangu?kila mtu anaililia,hivyo kua makini,kelele za mlango zisiukoseshe kunywa maji,endelea kujivinjari kama kawaida na icho kinyangarika a.k.a kidubwana wewe achana nacho.right?
Unknown said…
mmmmmmh!!!!pole sana dada yangu ila ilo ni tego umewekewa thus kuwa makini sana cuz wajanja ni wengi siku hizi mtu wangu
Anonymous said…
mh! ple dada mi, hawa wanaume huwa nawaona wamezaliwa tumbo moja hawana tofauti hata kidogo, hawana umepunguza wapi wala umeacha nini? ninyi mnaochangia na hao wanaozaa na mahouse girl wao ambao hawajui lolote unataka kusemaje!!!hawa ni midubwana tu, asikuumize kichwa huyo.

Mimi naomba nikwambie MUNGU ANAWEZA YOTE, piga maombi kwa sana, kapimeni ukimwi kama nyote hamna endeleeni na furaha yenu ya ndoa, kwani NDOA NI AGIZO kutoka kwa Mungu huyo mwizi (malaya) hana lolote, anatapa tapa tu kwa kuwa anajua hana lake. TULIA, JAIMINI, JITHAMINI, ENDELEA NA MAISHA. Nakuombea kwa Mungu ujifungua salama dia!