Monday, 30 August 2010

Nina Ujauzito wa Miezi 2, je haya ni ya kawaida?

"Kwenu wadau wenzangu, Kwa mara nyingine tena naleta swali langu nahitaji michango yenu,
Mimi ni mwanamke nimeolewa na baada ya miezi 7 ijayo natarajia kuitwa mama. Tatizo lilonifanya nije kwenu kuomba ushauri ni kwamba tangu nimegundua kua ni mjamzito nimekua katika wakati mgumu sana mpaka inafikia kipindi nashindwa hata kufanya kazi.

Yaani napata kichefuchefu cha ajabu ila sitapiki, nakuchagua baadhi ya vyakula pia harufu harufu hizi za manukato au chakula mara nyingine zinanipa shida kweli lakini najipa moyo kwani najua haya ni mambo tu ambayo humtokea mama mjamzito pindi mimba inapokua changa.


Ila kubwa zaidi ni kwamba sijisikii kabisa kufanya tendo la ndoa na Mme wangu kitu ambacho naona kama vile nanyima haki yake, ila najitahidi sana kujiweka katika fikra za kimapenzi lakini nashindwa.


Namshukuru Mungu kuwa yeye Mume wangu ni muelewa, anaelewa nikimwambia ila sasa naona hali mbaya kwani ni wiki ya pili sasa sijisikii kabisa kufanya mapenzi. Nahitaji msaada wenu wa mawazo ndugu wadau, nahisi nitaipoteza ndoa yangu.

Ningependa kujua kua Je hali hii iliyonikumba baada ya kushika ujauzito ni kawaida kwa wanawake au ni tatizo lingine linanikumba?
Asanteni"

13 comments:

Anonymous said...

Niyakawaida kabisa jamani mimbaaa isikie kwa mwenzie tu.miye nilikuwa namtema mate mume wangu hadi taulo linalowa chepechepe nanilikuwa sina hamu ya tendo.ikiwa kubwa ndoutapenda kunanihi kila siku lkn kwa sasa kabebi bado kachanga

Anonymous said...

huwa ni hali ya kawaida kwa baadhi ya akina mama hasa wakati wa mimba changa kama yako, mweleweshe mumeo kwani ikifikisha mienzi 3au4 itaisha hiyo hali, ila nawe ujikaze ndo umama huo shosti.

Anonymous said...

Usijali mumy hiyo ni hali ya kawaida na wala si tatizo kwani mimba zinatofaitiana na hali kama yako huwatokea wengi tu.unachotakiwa kufanya ni kujiweka karibu na mumeo pia jitahidi kutengeneza hisia na hata kama huna hamu ya kufanya mapenzi basi jitahidi hata kumridhisha kwa njia nyingine ili asijiskie vibaya,hali ya kechefuchefu na kuchagua baadhi ya vyakula pia ni ya kawaida vumilia kwakuwa mimba bado ni changa mi mwenyewe hali hiyo ilinisumbua sana ila ilipofikia miezi 5 ya ujauzito ile hali ilipotea,so ucjali na usiogope unachotakiwa ni ku relax na usijibweteke bado unaweza kujichangamsha kwa vikazi vya hapa na pale huwa inasaidia pia.Mungu ni mwema atailinda ndoa yako mtumainie yeye na ondoa shaka kuhusu hilo.

Anonymous said...

Hiyo hali ni ya kawaida japo si kwa wanawake wote. Try to be close to ur husband, be open minded kwa kumueleza ukweli wa jinsi gani unajisikia. Mueleze kwa ukweli na kwa dhahiri kwamba awe mvumilivu coz hali kama hyo inatokana na mimba na si kuwa umetaka. Kwa jinsi hii mwanaume muelewa atakuwa close to you and he wl help u to be comfortable all time. Kama vipi mpenzi akitamani mchezo jaribu kumsaidia kwa kumfanyisha musturbation kwa mkono wako laini. Kwa jinsi hii atafikia kilele bila penetratioon. Be couragous woman and ur husband sud force himself to be couragous to u. Take care and be happy always.

Anonymous said...

Kawaida mama, ukifika mitatu yataisha.

Anonymous said...

Ni kawaida dada wala usijali kuna kipendi itafika hiyo hali itaacha na utaendelea na mambo mengine kama kawaida my dear usihofu coz kila mtu na inavyomjia na kumchukua ktk hali kama hiyo uliyonayo.

Halima Hamad

Anonymous said...

Hongera bibie..mbona hiyo ni hali ya kawaida, tena bora wewe hata kutapika hutapiki..mie nina ujauzito wa miezi sita..lakini mpaka dk hii natapika japo si kama ilivyokuwa ya miezi miwili...kwani wakati ujauzito wangu una umri wa miezi miwili nilikuwa natapika sana, kichefuchefu..mate ndo usiseme...ila tumetofautiana mie kwenye mambo flani aaaah mashallah kama kawa mpaka dk hii..mume wangu hajapata tabu kwa hili...CHAKUSHAURI usihofu hiyo ni hali ya kawaida kwa ujauzito hasa ikiwa changa..amini itaisha tu...al the best mamaa

Anonymous said...

mimba bado canga jamani subira ikifika miezi 4 huko tano mtafaidi zaidi na hali itabadilika tena wewwe unaonekana umepata hromones changes ile mbaya unahitaji kupumzika kwa kila kitu hali itaisha , mueleweshe mumeo kama msomi ataelewa !

Anonymous said...

habari dada, mimi ninawatoto wawili na kwakweli sijapitia hio situation yako, maisha yangu ya ngono yaliendelea kama kawaida. mimi naamini nikichonsaidia kikubwa ni daktari wangu wakwanza alieniambia "nikiweza kutoa kichwani mwangu kua mimba si ungonjwa then you I will be fine". kila la kheri mama mtarajiwa

Anonymous said...

Hongera mamito Mungu amekuzawadia kuitwa mama! hayo ni mambo ya kawaida kabisaaa ukiwa na mimba haswa changa na wala usiogope kwa kusema eti ndoa itapeperuka hapana, mimi naamini ndoa ni zaidi ya kufanya mapenzi, bwa'kaka hakukuoa kwa ajili ya mapenzi tu (thou huwezi ukalitoa)ni combination ya vitu vingi aliviona kwako thats why akapropose!
Mimi binafsi nilikua na hiyo nausea siku nzima, moods ndo usiseme na nilikosa hamu kabisaa ya kufanya mapenzi..ni mambo ya kawaida ongea na mumeo mshawishi na yeye awe anapenda kusoma soma hayo mambo ya mwanamke akiwa na mimba anakuwaje, kuna vitabu au hata akigoogle anapata. Mume wangu alikuwa msomaji mzuri ndo maana alikuwa anaelewa vizuri what am goin through...
Jitahidi hata wewe kuleta leta vitabu au kudownlod mambo hayo msome pamoja tena atakuwa anakusaidia sana coz he will kno what you are going trough rite nao,
Ni hayo tu narudia tena hongera mpenzi.

Anonymous said...

ya kawaida mie nilianza kufanyana na mume wangu nikiwa miezi 7 tena ya kujilazimishaaa ili njia kidg itanuke ni kitu cha kawaida kabisa kumbuka kile kichefuchefu ulichonacho na maharufu kweli huwezi stahimili kufanya tendo sasa ivi na nina uhakika mumeo atakwua muelewa

Anonymous said...

kawaida shost after hiyo hiyo miezi 3 itaisha utapeta tu, mwezio sahv ni 5 month napeta kama kawa

atupele mwasyeba said...

mamy minawewe hatuchekani ila wanasema tuwe na subila yatisha baada ya mieezi 4 paka 5 tuvumilie tu shosti ndo ukubwa