Tuesday, 13 July 2010

Ni mdada mwenye Elimu zaidi ya Mchumba, je haiwezi kuwa tatizo tukifunga ndoa?

"Dinah mdogo wangu, hujambo?
Mimi ni mama wa miaka 41, niliolewa na kukaa na ndoa kama miaka 10 hivi na kupata mtoto mmoja. Mwamaume yule akaanza vituko na hata akanza kulala nje yando ayetu. Nilivyoona karaha zimezidi nilimueleza kua nitahama nyumbani kwake lakini hakuonyesha kujali na wala hakunibembeleza ili nisihame.

Siku ya siku nikatafuta nyumba, nilipofanikiwa nikamueleza kuwa nimepata nyumba na nategemea kuhama, lakini hakuniomba nibaki. Nikajua hakua ananihitaji tena basi nikahama. Baada ya mda mfupi nikatafuta shule nikaenda nje ya nchi kusoma.

Huku nyuma yeye akafunga ndoa na yule hawara yake (sisi ni Waislam). Nikadai Talaka akaitoa bila ubishi. Nikaendelea na masomo na Mungu akanisaidia nikamaliza salama na sasa nimepata PHD yangu tayari.

Hivi sasa kuna wanaume wawili mamekuja wanataka kunioa, mmoja kaishia form two na mwengine form four, shida yangu ni kua viwango vyao vya elimu ni vidogo mno na ndio kitu pekee kinanipa hofu kuingia kwenye hayo makubaliano ya ndoa na mmoja wao, ingawa nahisi bado nahitaji kuwa na mume.

Naomba mnishauri wanablog, Jee mwanaume ukimzidi elimu sana na hata kipato haiwezi kuwa tatizo ndani ya familia? ili kuwe na amani ndani ya ndoa ya hivyo mtu ufanye nini? Nahitaji kufanya maamuzi kati ya mmoja wao. Nahitaji sana kuolewa kama Mungu akinibariki. asanteni wote".

38 comments:

Anonymous said...

Theoretically hakuna tatizo mwanamke kumzidi elimu mwanaume, however practically kuna tatizo. Na tatizo linaanza tu pale unapoanza kuhisi kuwa kuna tatizo kuwa na mume/rafiki ambaye una mzidi kielimu na kipato. Na kwa sababu wewe binafsi umesha aanza kuhisi hivyo basi tatizo limeshaanza.

Ni vizuri zaidi watu kuwa na elimu/ufahamu unaofanana ili kufurahia maisha. Hii ni kutokana na kwamba mume na mke pamoja na mambo ya kindoa husaidiana pia katika mambo mengine ya kikazi na kijamii. ili uweze kutimiza majukumu yako ya kila siku kama Ph.D holder ni lazima uwe na mwanaume ambaye anatambua na kuelewa kile unachokifanya.

Ushauri ni ingawa ka umri kameenda kidogo, you still have a good chance of meeting Mr. right. Tuliza ball

Anonymous said...

mimi sidhani kama elimu ina matter. upendo ndio kitu muhimu katika ndoa na mumtangulize Mwenyezi Mungu ktk familia yenu. nakutakia kila la kheri

Anonymous said...

kwa maelezo yako tu inaonyesha hao wote wawili hawatakufaa na ndoa haitadumu, elimu yako na ya hao wapenzi wako imetofautiana sana na hata mwenyewe unaonyesha hilo swala la elimu utali"mind" sana na litakusumbua.

na wewe na PHD yako itakuweje uingie kwenye mapenzi na mtu wa form two? ndoa si masuala ya ngono tu, kuna mambo mengi sana ya kushirikiana na mengi kwa kweli kwa dunia ya leo yanazingatia elimu. nashauri wote wawili uachane nao inshaallah mungu atakupa angalau mwenye digri,

Anonymous said...

I can assure you! mwanaume ukishamzidi elimu na kipato huwa hajiamini. Chochote utakachokifanya hata tu kuraise challenge ndogondogo za kawaida ataona ni kwa vile umesoma au atakuwa defencive na kuwa na inferiority complex kuwa 'kwa vile sijasoma ndo unafanya hivi....'. Ndoa inaweza kukosa amani. Sasa kwa mawazo yangu hata hiyo difference ya elimu ni kubwa mno. Bora angekuwa hata na masters ingekuwa gap ni ndogo. Amini usiamini mimi nilikuwa na mchumba ambae nikapata masters kabla yake na alikuwa na 1st degree, vurugu iliyokuwepo kati yetu siwezi kuisimulia. Kuna mambo nilikuwa naweza fanya kwa nia nzuri tu lakini utashangaa mtu anaiweka na usomi... Amani ikapotea nikaona sina future nae nikamuacha. Kwa bahati nikapata mume mwenye PHD, sasa mimi nikawa niko chini yake koz nina masters tu, naona arguments zentu nyumbani zinakubalika hazina ugomvi. Challenge ikitolewa una argue kwa points na si kwa ubishi usio na hoja na mnaelewana na kukubaliana. Sasa hiyo PHD my friend hata safari za kikazi zitakuwa ni nyingi, we sikilizia ugomvi utakaokuwa ukitokea. Kwa vile yeye hatakuwa na exposure ya kusafiri kikazi huenda hata akawa anafikiri unaposafiri hauko innocent. Kuna kuchelewa kutoka kazini simply because kuna kazi ya gafla imezuka na huenda inatakiwa labda mfano kesho yake asubuhi sana. so huwezi kutoka mapema hadi ikamilike. Sasa vitu vidogovidogo kama hivyo tu vinaweza kuiweka ndoa yako matatani. But mwishoni mwa siku uamuzi ni wako na unajua wewe unampenda nani zaidi na atakufaaje kimaisha. Ila huu ni mtazamo wangu.
Lucy

Anonymous said...

Pole sana dada angu kiukweli mwanume kama utamzidi elimu ndani ya nyumba ni ishu sana bora mwaume akuzidi wewe.Ila kikubwa mapenzi ya dhati na wewe kumuheshimu mumeo na kumuona kama na yeye kasoma basi maisha yataenda tu dada angu ila kama utamdharau kisa hajasoma hapo ndoa itakuwa hakuna.
TINA-MOROGORO

Anonymous said...

duuu! PHD na form II/IV jamanii?
na umri je isije ikawa unataka kuwa fataki wa kike?

well, vijana/wanaume wamekuwa wajanja sana haswa wakijua unakipato? fikiria mara 2 ndugu yangu, kwanza jiulize haya una watoto? kama unao au huna 41 unataka kuzaa? si utazalia ICU muhimbiliii teh teh ok then jiulize unataka mume wa nini hata kukera km wa kwanza? na nyie wamama wasomi mna matatizo yenu nyie mpaka hapo ushayaanzisha matatizo kabla ya ndoa kufungwa hilo lakutaka kujua tofauti zenu za kielimu ni tatizo pia ambalo utalijenga hata kwenye hiyo ndoa mchwara unayotaka kufunga
the thing is fanya mazoezi na kumrudia mungu wako mawazo ya ndoa za uzeen na watu wanao taka fortune zako achana nao sawa mama, hii huu ujumbe ufikirie mara 2.

RUDN said...

inategemea na makubaliano yenu na jinsi wewe utakavyokuwa unamtreat huyo mume wako unless otherwise sio tatizo

Anonymous said...

Wewe mwanamke wacha kupoteza wakati na maswali! Ni elimu yao unataka ama ni mboo na kutombwa kila siku? Ni kawaida kwa mwanamke wa umri wako kujihisi kuwa na mume, kwani katika umri wa 35 mpaka 45 ndio huwa yuapata hamu na nyege tele sanaa, yaani nyege kwa wingi! Chukua mboo ikutombe kila siku sawa sawa, wachana na mambo ya elimu yao, kwani si una elimu yako?

Anonymous said...

sasa phd yako itakuwa imekusaidiaje kwenda kuolewa na semi-illiterate ambapo thinking capacity,mtazamo na analysis ya mambo mengi ni tofauti?.Pengine secretely unadhani unashindana na Ex-husband. Mambo mengine hayahitaji haraka kiasi hicho.Jichunguze kuona ni kitu gani kilisababisha jamaa akakupiga chini kihasarahasara namna hiyo ili ujirekebishe.pengine ulikuwa mbishi asiyeshauriwa,au ulikuwa una kelele nyingi,au ulikuwa mchafu au mlalamishi tu asiye na shukrani.socialize huku unamuomba Mungu unaweza ukapata the right candidate.Ila usimpangie Mungu siku na saa.

Anonymous said...

Mimi binafsi nazungumza kwa uzoefu lakini pia kwa kuelewa nature ya vile wanaume na wanaweake walivyo hasa katika mahusiano ya ndoa. Bila kwenda kwa undani sana,ningekushauri kwamba hao jamaa hawakufai. Najua unaweza ukawa unampenda mmoja wao na wao pia wanakupenda lakini ndao ikishaanza na mihemsho ya kuoa na kuolewa ikaisha mkaja kwenye life realities mtakuja kutofautiana kifikra,kimaono, kimtizamo,na kwa ujumla vile ambavyo mnachukulia maisha na kujenga hoja zenu.

Hilo gap la elimu ni kubwa mno na sijui labda uwe an angel lakini mkishaoana utakuja mdharau mmeo bila hata wewe kujua au kupenda kwa sababu vile itakavyoanza its a process which will take time and before you know it, it is already there. Na tatizo ni kwamba kuirekebisha hii ni ngumu kwa sababy hao jamaa kwenda tena shule ni.

Ingekuwa rahisi kidogo kama mwanaume ndo angekuwa na elimu kubwa kuliko mwanamke. Naturally and this is a proven scientific and pyschological finding, women tend to prefer having a man who is at least slight clever/educated/smart/intelligent whatever you may call it.

I am talking about utopia theories here, this is a fact and although most people may be in denial at the beggining, they often find it too late when they finally come to terms with its implications and eventualities.

So if its advice you need from me, please dont do it. I know now its a bit emotional because you want to get married but think aloud for the sake of your future. Hata hivyo mtu kama ulishaolewa kwa hiyo im not expecting you to be overly excited about marriage and this puts you in a very good position for you us both your mind and heart to make decisions like these rather than been driven by emotions only.

Best of luck. If you would like to get more info/advice my contact email is Marchnov2008@ymail.com

Anonymous said...

Mama before you involve yourself to this you have to be very careful. As you said the first man did that to you for the men I know ambao wameoa wasomi mahusiano yao mara nyingi is worse. So plz my dear friend be careful.

Mwanaume ambae hajasoma/hana hela, akioa mwanamke msomi/mwenye hela huwa anatumia nguvu kudifence, so atakuweka kwenye wakati mgumu sana unasafari kikazi hataelewa ataona una mambo yako. Before you engage your self plz plz AMUA MWENYEWE.

Angel said...

mmm.dada yangu unapo kua katika mapenzi hua siku zote hakuna linalo shindikana ,yote yana wezekana ,lakini ukisha ingia katika ndoa ,kuna karaha mbali mbali ambazo zinahitaji uvumilivu wa hali ya juu. mimi kwa ushauri wangu hao wanaume sio wa hadhi yako ,watakunyanyasa kisa elimu yako ,ulio ipata kwa juhudi zako mwenyewe ,mimi ni mmama ambaye nimeolewa na mwanaume ambaye nimemzidi elimu yeye kaishia darasa la saba mimi ni form six na nipo naendelea kusoma natarajia mwaka huu kuanza diploma ,manyanyaso ninayo pata asikuambie mtu ,yani mkigombana kidogo tu utasikia kwa vile mimi sijasoma .yani hilo limekua fimbo ya kunichapia ,hua najiuliza hapo sijasoma je nikisoma kama wewe itakuaje ? please usijiingize utaumizwa tena mimi kweli nafikiria kutoka nduki maana maumivu yame zidi ,yani lazima kuna element alizo nazo huyo mchumba wako ambazo zita ku cost baadae .kwa mfano unaweza ukawa na kikao labda na madoctor wenzako au hata kazia ofisi zikakubana ukachelewa nyumbani,uki muambia utasikia siulikua na wasomi wenzio kweli kama inawezekana uache lakini kama umependa sana utavumilia .

Anonymous said...

Hapana dada yangu haiwezi kuwa tatizo kama mmependana naamini mtafika mbali point ya msingi ni wewe kutokuwa na dharau kwake!
Tuwasiliane kupitia kp21p@hotmail.com kuna issue nataka kukuuliza kuhusiana na masomo nje ya nchi.

Anonymous said...

Mimi wacha nikwambie - the saying inayosema apples with apples and pears with pears - si bure- kuna dada mmoja naye vile vile amesoma na kufanikiwa kuwa professior - na mume wake ni medical doctor - yaani wote wawili ni wasomi lakini jinsi huyu mume alivyokuwa anamundermine huyu mkewe professior - whatever she does au hata wakijadiliana kuhusu mambo ya familia, ndugu, watoto - the husband has to have the last say even if its he is making a wrong decision/choice na mkewe akimwambia uamuzi huu sio mzuri au waungwana anamwambia mkewe niondolee uprofesser wako hapa. Huyo mumewe akaanza kutembela na housegirl,yaani wala bila hata kuficha...baada ya muda mke akawa yamemfika na anataka waachane - alipoita kikao cha wanandugu -huyo mume akawaambia hao ndugu waliokuja kwenye kikao kuwa simtaki huyu mwanamke maana ananiletea letea uprofessor wake chumbani, yaani alimnyanyasa sana, japokuwa wameachana watoto walikuwa wadogo so baba alipata chance ya kuwaambia kuwa wasiwe wanamsikiliza mama kwa sababu anajidai kasoma, kasoma kuliko nani, mwanamke ni mwanamke tu, sio kila siku kwenda mikutanoni, mara kusafiri safiri, akatafute mwanamme atakayeweza kuvumilia-basi watoto wakawa jeuri, yaani jeuri sana kwa mama na baba wala hata hasemi neno.Yaani huyu mama katesema lakini jinsi Mungu si Athumani uprofessor wake umemfanya kakutana na watu wa level yake - yaani alidiscover kuwa alijichanganya badala ya apples with apples alikuwa amechanganya apple with a pear - my sister most men will find your profession extremely intimidating (haswa hawa mwenzetu - waafrika) watakuona very intimidating and though in the beginning it can be ok but after a long while or even from their own family members they can start kumshawishi to change his mind.

Tafuta level yako dada - apples with apples or pears with pears.

Anonymous said...

Tatizo ni ufahamu wao na si elimu! make ur own choice and pray!-martin

Anonymous said...

Hey Mdada mwenye PhD. Kwanza Hongera sana kwa kufakamia elimu hadi ukanyakua hiyo shahada ya uzamifu.

jambo la pili pole sana kwa kuchafuliwa maisha ya ndoa na mume wako hadi sasa inakupelekea kuingia mkenge na ndoa nyingine.

Tatu, kwa kiwango chako cha elimu ulichonacho sasa unahitaji kuwa makini sana.Kwa sasa hivi unatazamwa na jamii kama msomi mahiri katika uwanja fulani, hivyo jamii inategema sana kujifunza kutoka kwako.Kwa hiyo usifanye makosa hasa kama hayo yanayohitaji uangalifu na umakini zaid kuliko aidha kuwa na haja sana ya kuwa na mume.

Nne, nikija kwa hao wanaume, ninapata wasiwasi nawe kwamba tayari unavinjariwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja.Inakuwaje kuonyesha kama unakubaliana na watu wawili at a time licha ya kwamba labda hujaingia nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.lakini tayari inaweza kukupa dosari sana utakapokuwa umeamua kuchukua mmojawapo.

hata hivyo mimi ningekushauri kwamba tatizo la kuolewa na mtu aliyechini kielimu kuliko wewe linaweza kuwepo au kutokuwepo kwani itategemea sana jinsi wenyewe mtakavyochukuliana.Na hasa wewe ambaye ndiye kinara wa elimu unahitaji kujishusha sana na kujua namna ya kumchukulia mumewe hasa kwa mambo ya kifamilia na kinyumbani.lakini unapotoka katika lango hilo ukiwa nje ya hapo nadhan i utabaki kuwa mwenye PhD.

Jambo lingine ambalo naliona na mumewe kujiamini kuwa ninyi hamtaoana kwa sababu ya elimu bali upendo unaowaunganisha.Na najua hao wanaume wameishajua kuwa kuwa wewe ni msomi na ni wajibu wako kuwaambia bayana kuwa elimu yako imewazidi mno, na kwamba wanaionaje hiyo na watachukuliana nawe vipi?hapa nina maana wafumbuke MACHO na akili kwamba uwanja ulio nao utakuweka wewe kwenye nafasi nyingi ambazo hatimaye wanaweza kukwazwa kwazo kama hawajiamini.

Muhimu ni kujua hayo na kuweka bayana mambo yote.lakini mambo ya mume/mke na familia hayana shida mradi wewe msomi utajua namna ya kubadili mazingira kuwa sasa uko wapi na kwamba nahitaji kuwaje.

Kipato pia kitatofautiana, ingawa siwezi kusema wewe utakuwa na kipato kikubwa,maana inawezekana hao wanaume ni washika mapesa kwani kutokuwa na kisomo hakuna maana huwezi kushika nafasi zingine za kipesa.mfano wafanya biashara hivi.lakini hayo unayajua wewe zaidi wakoje hao wanaume.Penye upendo mambo mengine hujitenga mbali.

Kuna mwanaume ambaye alioa mke mwenye elimu ya kidato cha sita wakati yeye alikuwa wa darasa la saba.Baadaye huyo mwanamke aliendelea na masomo hadi nikawa naye hapa marekani kusoma PhD na tulipomaliza yeye mume wake akabaki hajiendelezi.Mke karudi bongo na kapata kazi za kimataifa.ndoa ikaanza kuteteleka kwani huyo mke kakutana na wanaume lukuki wa kufanana na kichwa chake.Kwa hiyo itategemea sana na wewe mama na wala siyo mwanaume.

Mwisho wewe kama msomi mwenzangu nakushauri uweke umakini sana katika kilichekecha hilo licha ya mashauri mbalimbali utakayoyapata hapa lakini jibu sahihi litakuwa ndani ya moyo wako.La muhimu uwe muwazi sana na hao wanaume na kaa na kila mmoja umweleze the whole situation ili ujue wanajiamini vipi katika hilo. ila nakuomba usiwatishie kwa elimu yako bali uwaeleze hali yako na wajibu wako kama msomi katika jamii.

nakutakia kila la heri dada na uitumie elimu yako vema.

Anonymous said...

mambo mdada!
mi nashauri kama unamapenzi ya dhati chagua mmoja ufunge ndoa dear.Elimu si tatizo but jaribu kuchagua yule mwenye upeo zaidi wa maisha ingawa ujasema hao wanaume wanafanya shughuli gani kwa sasa. kama hana kazi basi jaribu hata kumfungulia biashara ili nae awe nakipato chake si unajua wanaume wengi hawapendi kuonekana magolikipa? so chagua mmoja ujinafasi nae elimu si tatizo unaweza ukampata huyo mwenye elimu akakutenda tena! poleee!

Anonymous said...

mambo mdada!
mi nashauri kama unamapenzi ya dhati chagua mmoja ufunge ndoa dear.Elimu si tatizo but jaribu kuchagua yule mwenye upeo zaidi wa maisha ingawa ujasema hao wanaume wanafanya shughuli gani kwa sasa. kama hana kazi basi jaribu hata kumfungulia biashara ili nae awe nakipato chake si unajua wanaume wengi hawapendi kuonekana magolikipa? so chagua mmoja ujinafasi nae elimu si tatizo unaweza ukampata huyo mwenye elimu akakutenda tena! poleee!

Anonymous said...

Bibie hongera sana kwa kuchapa kitabu hadi Phd. Mimi ni mwanaume mwenye shule kama yako, kwa mtazamo wangu ninakushauri utafute kwingine. Kuoa/Olewa na mtu ambaye hajamaliza hata kidato sita na kupata walau ka-certificate au diploma ni kujitakia matatizo. Hawa jamaa huwa unaongea nao nini zaidi ya kutiana?! Labada kama wamekaa vizuri kifedha/bishara maana unaweza ukawasaidia jinsi ya kufanya au kushindana kwenye hii hali ya soko huria. Vinginevyo, perspective zenu ni tofauti mno. Kwa vile ulishaolewa nadhani utakuwa umeshajua kwamba kuoa/olewa ni jukumu kubwa zaidi ya kupigana mikasi. Wachache niliowanaona wenye gap kiasi hicho, wanaishia kulumbana kila siku, huyu anadai mwenzie hasaidiki kwasababu ya elimu yake ndogo na mwingine anasema ananyanyaswa na mwenzie kwasababu ya elimu yake juu na kipato kikubwa. Najua wanawake mkishanogewa na mshariba huwa hamuambili, kazi kwako kama umeshanogea na hiyo mboo, wewe ndio mwenye uamuzi wa kusuaka au kunyoa!!
Ni mtazamo tu!

Ni mimi Muti Mukavu aka MM

Anonymous said...

Hao ambao umewazidi kielelimu wanaweza wakawa na inferiority complex, na huenda ikawanyima raha kipindi chote cha maisha yenu, wewe unaweza ukawa sawa, ila mwanaume kwa vyovyote atakuwa hayuko ok.

Nways,Mimi pia natafuta mwezna na nna PhD labda tutaendana, au wasemaje. Ni mtazamo wangu tu.

Anonymous said...

Hapo ni wewe utakaeidumisha au kuiangamiza ndoa hiyo. Wanawake wengi wakishakuwa na elimu au kipato kikubwa kuliko waume zao,kuwaheshimu, kuwasikiliza na kutimiza majukumu yao kama mke wa mtu huwa ngumu. Ndio maana wanawake wengi wa aina hiyo waume zao hutembea na housegirl au huwa na nyumba ndogo.

Anonymous said...

Habari dada dina na wanablog wote, natumaini mu wazima wa afya napenda kuchangia mada ya huyu mdada kama ifuatavyo;
Kwa upande wangu sioni shida katika kutofautiana kielimu katika mapenzi ila tatizo ni kwamba wanaume wengi huwa na tabia ya kujishuku pindi pale mwanamke anapomzidi hasa kwa hivi vitu viwili
1. PESA
2. Elimu
Mimi binafsi na ndoa yangu ni mfano wa hayo ninayokuambia maana mim i ni graduate na mume wangu wa miaka minne sasa ni form six lever lakini amekuwa akitaka ubishani na kufuata atakalo simply nikijibishana naye anaona namdharau, imefikia mpka ameanza chuo kwa kutaka naye apate degree. pia mimi namzidi kimshahara kiasi cha kwamba nikifanya mambo yangu anaona natumia hela vibaya na anataka nimpe yeye iliaweze kupanga na anavyodai mipango ya kimaendeleo,ninachoweza kukushauri ni kumchunguza huyo umpendaye na muweze kuwekana wazi juu ya tofauti zenu na ni kwajinsi gani yeye anazipokea. Mapenzi hayachagui mamii ila inabidi uwe mwangalifu usije teswa nayo sababu tu yakuwa desparate take ur tym na uolewe na mwaume umpendsaye no matter what naumweleze mpenzi wako awe huru juu yako kama mkewe na yeye kama mume mambo ya elimu,vyeo na pesa yabaki nje ya mahusiano yenu yasiwakwaze, nakutakia kila la heri, E

Anonymous said...

Hongera kwa kupata PhD, My dia huo mpishano ni mkubwa sana, itakua ngumu mno kucop ktk ndoa, nina mifano miwili ya watu ambao ni degree level waliolewa na std 7, hazikudumu hizo ndoa. Thinking inakua tofauti sana. Otherwise itabid ujishushe saaana, hata mawazo ya maisha umsikilize yeye ili ajione nafasi yake kama baba wa familia ipo palepale. Jipe muda nae mchunguze uone kama mnacop, watu hawafanani, may b naexposure nzuri

Anonymous said...

inategema wewe wahitaji nn katika ndoa,.je waona wana uwezo wa kusongesha lfy yenu?mbona kuna familia zina maisha mazuri na wazazi hawajaenda shule kivile?nadhani wewe unatishwa na mitizamo yenu ya uchambuzi wa mambo, jaribu kutofautisha elimu yako na mahusiano na ondoa fikra kwamba wewe umewazidi hapo waweza fanya maamuzi sahihi.

maggie said...

Nimesoma kwa ufasaha maelezo yakokwanza pole kwa yaliyo kupata kwa mumeo ulieachana nae.

dada yangu kwanza napenda kukwambia kuwa mapenzi ni maua huota popote kama ulivyo amua kuwapenda hao mbwana wawili pamoja na elimu zao kuto fikia kiwango ulicho nacho wewe lakini moyo umependa, nakwambia hayo kwa sababu nataka uelewe kuwa kwa hali yoyote uwe na elimu usiwe na elimu,uwe tajiri au masikini utapenda tu, hivyo basi nakushauri kati yahao mabwana wa wili tafuta mmoja ambae unampenda zaidi funga nae ndoa usijali mambo ya elimu au kazi aliyo nayo kwa ni baadae kama una uwezo unaweza kumshauri ajiendeleze sio mbaya ila kikubwa ni upendo na maelewano ndani ya nyumba.
nacho kuomba kama utakubali kuolewa nae akiwa na elimu hiyo ndogo tafadhali usije ukamnyanyasa maana sisi wanawake sijui tuko vipi wengi wetu wakijiona tu wanauwezo kumzidi mumewe basi manyanyaso moja kwa moja mpaka mwanaume ananza kutafuta mwanawake nje ili kuepuka kero za ndani. nakutakia uchaguzi mwema na maisha mema pia katika ndoa mpya ijayo.

Anonymous said...

Achana nao kabisaaaa! Kama bado unataka furaha kwenye ndoa mwanaume ukimzidi chochote akakuoa ni shida na hata ndani ya nyumba itakuwa shida kama bado unataka mume Mungu atakupatia kwa wakati wake usije ukaishia kuolewa mara ya pili na yatatu. Wanaume wasomi wako wengi bora hata angekuwa na degree moja au la wawe wanakuzidi kipato kwa biashara laa sivyo utajijutia nafsi yako

Anonymous said...

Mboo haina elimu cha msingi ni kukubaliana na maelewano tu basi.
Mohdy

Anonymous said...

msomeshe kwanza huyo unayemtaka, akianza chuo ndo muoane lakini aendelee kusoma hata mkiwa ndani ya ndoa walau apate degree au masters yatosha

Anonymous said...

dd msomi pole sana na yaliyokukuta mm nakushauri usikubali kuolewa na wote hao 2 inavyoonekana una hamu ya kuolewa sijui kwa vile exhusband wako kaoa na ww ndio unaforce uolewe, ngoja nikwambie ndoa ni maisha siyo kwa yale unayoyaona leo huko mbele ya safari utakachoona ni maisha yenu mnayapanga vipi, mnaheshimiana vipi kila mmoja anawajibika vipi ktk familia sasa huo utanashati wake na au ametoka familia nzuri kiasi gani hutaviona wewe umewazidi uwezo, elimu itakuwa ngumu kuendana na men wengi unapowazidi hayo huwa na inf. complex hivyo itakuwa shida kwako na utajuta kama waliotangulia kuchangia ndoa nyingi ambazo mama kamzidi baba ktk elimu au uwezo hazidumu tena zingine zinaishia hata kuuana, my friend mwombe mungu akupe wa kiwango chako cha elimu na uwezo yule ambaye hutakuwa na wasiwasi naye yaani ukiona una amani naye 100% huyo ndiye mpango wa mungu mbona mungu ni tajiri wa vyote mwombe kwa kadri ya mapenzi yake mwambie mungu unataka mume wa namna gani atakupa tu usiogope na kukata tamaa kwa nn uende kuishi ndoa mbayo unamashaka nayo?. Hao ambao tayari ww mwenyewe unawasiwasi nao, tayari mungu anakupatahadharisha labda umeshindwa kuelewa tu usijiingize mkenge kabisa. unajua wanawake wanaweza kuishi na mume aliyesoma kumzidi yy sana na maisha yakawa mazuri tu lkn na mume uliyemzidi, ni tatizo kubwa mwanzoni hutaona tofauti ss kadri ck zinavyokwenda utaona tu ndio wengine ili akudhalilishe anaamua kutembea na hgirl au ndugu hapo home au hata jirani.

Anonymous said...

Mpenzi wangu wa moyo,
Kwanza hongera kwa kuwa muwazi.

Nitakuwa mfupi ( brief, ha ha ha ) kuwa hapo ni kitendawili. Better safe than sorry my dear.
Gap ni kubwa na kwa vile ni ndoa ya pili, vikishindikana, vitakutia doa na watu watadhani ni wewe una shida.
Yamenikuta so naongelea kwa uzoefu.

Kwa vile una watoto, kaa kimya usubirie wakati wa Mungu akupatie mtu 'mtayefanana ' naye.
That's too wide a gap na ina translate a lot katika maongeo, mafikira , maamuzi na perceptions.

Ndimi Mama Kiduku

Anonymous said...

Mpenzi wangu wa moyo,
Kwanza hongera kwa kuwa muwazi.

Nitakuwa mfupi ( brief, ha ha ha ) kuwa hapo ni kitendawili. Better safe than sorry my dear.
Gap ni kubwa na kwa vile ni ndoa ya pili, vikishindikana, vitakutia doa na watu watadhani ni wewe una shida.
Yamenikuta so naongelea kwa uzoefu.

Kwa vile una watoto, kaa kimya usubirie wakati wa Mungu akupatie mtu 'mtayefanana ' naye.
That's too wide a gap na ina translate a lot katika maongeo, mafikira , maamuzi na perceptions.

Ndimi Mama Kiduku

Anonymous said...

huu naona ni moto kwako dada maana kuingia ni rahisi lakini kutoka ni kazi ngumu sana lazima ufikiri vizuri kabla ya kuchukua maamuzi
kwamjibu wa swali lako tayari inaonyesha kuwa kuna walakini ndani ya moyo wako kinachokusuma nidesire to have sex na hapo upendo haupo.
inaonyesha hao wanaume hawakufai yawezeka hata wao wanalitambua hilo ila wanataka kukuchuna tu

it my comment, changanya na za kwako

Anonymous said...

mimi sijawahi olewa lakini nipo masomoni ndo kwanza natafuta degree, mpenzi wangu wa siku nyingi ameishia form four ina matatizo yake sito danganya lakini nadhani kama mnaelewana elimu yako haiwezi ingilia mapenzi yenu na mtangulize M Mungu atakujaalia, chagua mmoja alafu ona inaenda vipi i dont think you got anything to loose end of the day just go for what makes you happy i dont thnk your education level should determine who you with that would be so unfair kwa kweli and it will brake me cause my man is so nice to me, relationships have problems be it cause of levels of education or other wise its given..bless you.

Anonymous said...

Hivi nyie mnaomshauri dada wa watu aolewe na mtu ambaye hajasoma eti kisa mboo haina shule, ndoa sio mboo tu kuna zaidi bwana mbona kuna watu mafundi sana wa mapenzi lakini zinavunjika ndoa zao. Acheni kumdanganya mwenzenu ndoa sio lelemama bwana. ACHENI TENA UKUTE MWANAUME HANA ELIMU DU' KAAAZI KWELIKWELI SIO MWELEWA HATA KIDOGO, NAKWAMBIA UNAWEZA PIGWA HATA MBELE YA WAKWE KISA HUJATANDIKA KITANDA NA KUMFULIA CHUPI. WAKATI ULIKUWA KWENYE MKUTANO WA BUDGET YA MWAKA YA TAIFA, MMECHANGANUA MAMBO KICHWA KIMEJAA UMECHOKA SHUGHULI NYINGI OFFISINI. BADO KUNA ASSIGNMENT KIBAO. WAJAMENI HAELEWI KITUUUUUU

Anonymous said...

kila mtu na bahati yake mimi mwanamme anayetaka kunioowa anacertificate mimi nina Diploma Tatu tofauti, ila nafanya kazi namuhishimu sana na ananijali na kunishauri ila wote ni f4 kwa hiyo inategemea na mtu jamani ila pHD gapu kubwa sana mpendwa wang fikiria mara mbili tatu

JIBABA said...

Elimu si hoja Dada kikubwa Mapenzi kama unavyosema una umri wa miaka 41 ambao ni naona ni mkubwa sana, hivyo ni vyema ukafanya maamuzi ila si ya haraka kwani unatakiwa UMPIME huyo mwenza wako juu ya uelewa wa maisha, familia na mahusiano kwa ujumla wake.

Nashauri ni vyema ukamchagua Mume ambaye amekuzidi Umri ingawa si kigezo kikubwa sana lakini katika saikolijia ya maisha tunatambua kuwa UKUBWA NI BUSARA NA HEKIMA.

"EVERY WOMEN NEED A MEN" kwani utafiti wa kisayansi ulifanywa na WANABAIOLOJIA umebaini kuwa UPWEKE WA KIMAPENZI NI SUMU KWA WANAWAKE WALIO WENGI, fanya hima MAMA Mpate Mwenzio NA HATIMAYE UIREJESHE FURAHA YAKO YA MOYO.

Thanks.

Anonymous said...

Elimu c kigezo cha maepnzi mama!!unaweza ukampata mwenye elimu ya juu au zaid but mapenzi ziro ki2 ambacho ni kibaya maishani!!angalia kati ya hao wawili yupi moyo wako umeridhika nae then mfunge NDOA! elimu haina mwisho unaweza mkajadiliana taratibu na kwa hekima khs yy kujiendeleza kielimu,hilo linawezekana coz 2meona wengi wamejiendeleza ukubwani na sasa wana elimu ya juu zaid mama!!usisikilize maneno eti ooh!!mtachangia vp mawazo!!huo ni ufinyu wa mawazo pia!ZINGATIA!!

Anonymous said...

Elimu c kigezo cha mapenzi,upendo!!angalia moyo wako umempenda nan kati ya hao then fungeni ndoa,elimu haina mwisho mtashauriana taratibu na kwa upendo khs kujiendeleza kielimu kwa Mumeo!!wapo wengi wenye elimu za juu 2meona but kichwani MATOPE tu hakuna busara wala maarifa!na wanazingua tu ktk mahusiano!hao wanaoangalia elimu kwanza nawahesabu km wapo AFTER MONEY!! na c upeo au maarifa hiyo ni zuga tu!fuata moyo wako mama!olewa then mshauri kwa unyenyekev mumeo atakuelewa na kujiendeleza if da problem is Education!