Wednesday, 28 July 2010

Mume wangu aninyanyasa nakudai "mimba ikitoka utapata nyingine"...

"Mimi ni mama wa kitanzania ninaeishi na familia yangu UK, nimeolewa miaka 12 iliyopita na ndoa yetu imejaaliwa watoto wa wiwili na mwingine wa tatu yuko njiani. Mimi nilikuja UK kwa ajili ya masomo na kumuacha mpenzi wangu ambae sasa ndio mume wangu nyumbani Bongo.

Wakati naondoka tulikubaliana kuwa nikikaa kwa muda nimfanyie mpango ili na yeye aje huku kusoma, lakini kutokana na ugumu wa maisha kwangu kama mwanafunzi niliekuwa chini ya wazazi sikuweza kufanikisha hilo na yeye hakuwa na pesa za kutoshana kumleta huku. Basi tukaamua kusitisha suala la kusoma na kwavile tulikuwa tunapendana tukaamua kuwa yeye aje huku kama mwenza wangu na hivyo mimi nitaendelea na shule wakati yeye akifanya kazi ili kumudu maisha yetu.

Baada ya mimi kumaliza na kufanikiwa kupata kazi kwenye Bank na tukafunga ndoa mwaka uliofuata, maisha yakawa mazuri, mapenzi motomoto kama mke na mume na baada ya mwaka mmoja tangu tufunge ndoa nikajifungua mtoto wetu wa kwanza.

Baada ya kumaliza likizo ya uzazi mume wangu akaamua kuacha kazi bila sababu ya msingi, mimi haikunisumbua kwa vile kazi yangu ilitosha kutufanya tuishi maisha ya kawaida. Mtoto wa pili akaja, nikaamua kukaa chini na mume wangu ili tujadili maisha yetu ya mbeleni kwani familia inakua, mume wangu akaahidi kurudi kazini. Lakini hakufanya hivyo na sasa mtoto wa tatu yuko njiani.

Mume wangu amekuwa mvivu, hajali, hana umpendo na asie na ubinaadamu kabisa, natoka nyumbani asubuhi na mapema kwenda kazini, narudi jioni nikiwa nimechoka si unajua tena ujauzioto! nikifika nyumbani kitu pekee nahitaji ni kupumzika, lakini wakati napumzika utasikia mume wangu anauliza "leo hatuli humu ndani?" wakati yeye anatazama TV. Kwavile nakuwa nimechoka na sitaki ukorofi mwanamke nainuka naenda jikoni na kuanza kuandaa chochote cha haraka haraka ili nipate muda wa kupumzika.

Siku moja nikaamua kuzungumza na mume wangu na kumwambia jinsi ninavyojisikia kuhusiana na suala zima la ujauzito, masaa mengi kazini na kumuomba tusaidiane shughuli za ndani ili kuepusha matatizo kwangu na kwa mtoto alie tumboni.

Sikuamini masikio yangu pale mume wangu aliposema kuwa " wewe ni mwanamke wa kiafrika ni lazima uhakikishe nyumba safi, chakula kinapikwa na kuangalia watoto. Kwani kuwa na mimba ni ugonjwa? wangapi wanakuwa na mimba zinatoka na wanapona alafu wanashika nyingine na wanazaa? ikitoka hiyo utapata nyingine".

Dinah ghafla nikajisikia sina nguvu, nikanyanyuka taratibu bila kusema kitu nikaenda zangu kupumzika. Tangu siku hiyo nikaamua kuwa kila Juma Pili nitakuwa napika chakula/kuandaa chakula kingi kwa ajili ya wiki nzima ili watoto wangu na baba yao wasishinde njaa.

Sasa ndugu zangu nauliza hivi, kama hali imefikia hivi na watoto wetu hawajafikia umri mkubwa kuishi na mzazi mmoja nitakuwa nakosea kama nikimvumilia mpaka watoto wakuekue kidogo ndio nitafute ustaarabu wangu au nitengane nae sasa ili nisimpatie matatizo mtoto alie tumboni?.

Mimi binafsi hisia za mapenzi kwa mume wangu hazipo tangu aliponiambia kuwa mimba sio ugonjwa na mameno mengine yote, yaani namuona kama mtu tu pale asie na umuhimu wowote kwangu. Sina uhakika kama hali hii nikutokana na ujauzito, hasira au mapenzi yameisha?

naombeni msaada wenu wa kimawazo.

Mdau wa UK"

40 comments:

Anonymous said...

Nini? what a rubish? Kama alikuambia kuwa mwanamke ana wajibu wa kuhakikisha nyumba ni safi, chakula kimepikwa, na mimba si ugonjwa kwa nini na wewe kwanini usimuambie kuwa wajibu wa mwanaume ni kuhakikisha nyumbani familia inakula, watoto wanasoma, wanaishi vizuri na mahitaji yote yanapatikana sababu yeye (mume) ndo head of the family and bread earner! what a looser! yaani wanawake wakati mwingine huwa tunavumilia mengi... na wewe ni mfano mzuri koz umeamua kufanya kazi na kuondokana na mfumo wa kutegemea kila kitu kwa mwanaume. Sasa yeye badala akushukuru kwa bidii yako eti anakaaa chini na kuangali TV na kusubiri urudi ufanye kazi... POLE SANA my love. Nakuelewa si ajabu unakaa kimya ili kupisha shari na maisha yaendelee. kama kaamua kuishi kama looser basi akuheshimu na kuthamini mchango wako na asaidie kazi za nyumbani... Ingekuw amimi wala nisingehangaika kujiuliza. Ningeanza taratibu za kuachana nae mara moja. What do you have to loose. Koz kama sasa hivi unalea familia peke yako itakushinda nini ukiwa peke yako? Watoto ni wenu na atabaki kuwa baba daima... Ila kuishi kwa kero hiyo mi nisingevumilia

Anonymous said...

Pole sana aunty kwa yaliyokukuta.... hapo huna njia yoyote ya kufanya maana mimi sikuona sababu ya yeye kuacha kazi akitegemea nini wakati ndio kichwa cha familia? Wewe mwenyewe umemuendekeza kiasi cha kudhani wewe ni mama so u have to provide kila kitu,La muhimu kaa nae chini mueleze ukweli kuwa anavyofanya sio utu. Atoke hapo nyumbani akatafute kazi then muangalie maswala ya watoto... Ikishindikana hakuna kumpa hata senti tano za mshahara wako maana anazoea. mwanaume gani asiyeona aibu huyo, yuko nchi za watu then anataka kukaa kama kwao mrudishe tz huyo bwege, akome tena akome mara mia yeye hakuonei huruma kwa yote unayomfanyia, unalisha familia, unazaa utadhani wewe ni kiwanda?
Na kwanini umekubali kushika mimba nyingine wakati unajua mstakabali wa maisha yenu sio mzuri? Kazi hizo zina wenyewe leo upo kesho kimya inamaana utashindwa kusaidia hata ndugu zako kisa umeolewa na mume mvivu? Ndugu zake yeye nani anawasaidia?

Kama nikuzbe vibao wewe dada, anyway ni hayo tu kwa sasa nitarudi baadae

Anonymous said...

wou wou wou wou..ukisema kwako kwaungua kwa mwenzio kwatekekea nina matatizo kama yako japo yametofautiana ila wangu mie ana mdomo mchafu kama choo cha public,

Dia kwa sasa hivi una mimba hebu lea hiyo mimba kwanza halaf ukisha zaa....ulee watoto wako ukiwa na huyo mume hapo hapo mpaka watoto wako wakue..ondoa hiyo zana ya kusema huna mapenzi nae leo watoto wako muache na ujeuri wake usimueleze chochote, kingine ukumbuke kufanya vitu kwa ajili ya maisha ya watoto wako hapo baadae...baadhi ya wanaume sio watu..

Anonymous said...

Yani ww dada umeandika hii mail hata aibu uoni ndo tatizola wadda wakishaenda kuishi nje wanataka kujidai nao wazungu.Wewe dada unaonysha hata kitchen paty hujapewa namuunga mkono huyo mwanaume maana wewe dada ulitaka kumfanya mwenzako bishoke na majibu aliyokupa sawa kabisa wewe siyo wakwanza kukeba mimba usilete uchafu ndani kwako kisa eti ukifagia mimba itatoka wewe dada wa wapi mbona wa ajabu hivyo unatu aibisha wnawake wenzio kabisa yani.Hata kidogo watu wanatafuta wanaume wewe umempata mwanamme unamchezea sisi tunawasaka hao wanaotendwa na wake zao waje kwetu tuwafanyie kila ki2 uone kama atakutafuta nyooooooo usije kulia eti umeibiwa mume wakati weweni mvimu akipata mashapu wanaompeleka chooni kuoga akiwa mgongoni bibi hutomwona tena.
WASOMAJI SORRY KWA KUANDIAKA MAELEZO MAREFU YANI DADA HUYU AMENIBOA YANI HADI BASI
(TINA WA MOROGORO)

Anonymous said...

pole sana sana aunt kwa matatizo magumu tena kipindi cha ujauzito,umenigusa roho yangu manake hata mimi yalishanitokea kama hayo,to bad mi sikuwa na kazi niliyofanyiwa Mungu ndo ajuae.napenda kukuambia kwamba sio tu kwa ajili una mimba hiyo hali ya kutokumpenda itaendelea kila siku na itakutesa sana hivyo basi take action,kama vipi mtimulie mbali bila shaka uk kuna child benifit,ukijiandikisha kama single parent unacleam vitu kibao na utamudu maisha yako bila stress za kila siku,sasa huyo mume wa nini/ kazi unayo, usijitese bure dadangu mtimulie mbali!!!! anakwambia ikitoka utabeba tena!1 hell not

Anonymous said...

kwanza wakati anakuambia wewe ni mwanamke wa kiafrika unatakiwa kupika, usafi na kulea watoto ungemwambia na yeye ni mwanaume wa kiafrika anatakiwa akafanye kazi alete pesa nyumbani, hapo ulipo unafanya majukumu yake hapo si pa kupoteza muda mweleze anatakiwa akafanye kazi na ukiona bado hataki achana naye mapema watoto hawatakushinda kuwalea tena unamchomea kabisa arudishwe bongo akione cha moto.

Anonymous said...

hakupendi, fikiria maisha ya wanao, umpeleke marekani, umlishe, umpikie na kumzalia bado hakudhamini unachong'ang'ania kwake ni nini?

Anonymous said...

kaa dada pole sana yaani mtanisamehe mwanaume anaroho mbaya sana huyo. kazi ufanye umlishe umzalie watoto uumpikie sasa hapo uanaume wake upo wapi???very selfish. Mbaya unawatoto wadogo na anakuja mwingine ndugu unao? ita hata ndugu zake na useme umechoka kabsia hii ni unyanyasaji kabisa wa wanawake. hadi nasikia kulia kaa. Mimba si ugonjwa ila unahitaji kupumzika sasa yeye acheki tv wewe uhenyeke kwa kila kitu loooooooooooooo hata haya hana. mie naona ita washenga akalishwe chini akatafute kazi na kama hataki yeye ndio atake care ya nyumba watoto na kusaida vitu vidogovidogo jamani mnaishi Uk maulaya cha ajabu kikowapi kupika na majiko ya umeme na kwenda shopping kusafisha nyumba na vifaa vya mashine looo uvivu mtupu. Wahusishe ndugu zako jamani usikubali kuteseka!!

Anonymous said...

Unajua wakinamama wengi sana wanafanywa kuwaheshimu waume zao wakati hao wanaume hawana hata kiduchu cha heshima kwa mke wake. Mi nitakwambia hivi dada, yuko mumeo amesahau kama wewe ni mkewe na anakuchukua kama mtumwa vile, hana huruma,hisia au hata uchungu na wewe, yaani usote kazini uje nyumbani uanze kazi tena na yeye amejiketisha mbele ya tv halafu na labda usiku anataka haki yake.Mimi nakusihi ufwate hisia toka moyoni mwako, kama umeauwa kuendelea kuishi naye ndio hivyo hivyo watoto wako wataanza kujifunza mafunzo wanayoyaona kwa baba yako na kama hisia zako ni kuchukua ustarabu wako ambayo mimi kama ningekuwa kwenye hii situation ningefanya ni kwamba utapata utulivu wa akili na hamna stress/huzuni etc, na utaweza panga mipango yako kikamilifu na pia utaweza weka hata akiba kwa upande wa fedha manake huyo naona ameamua kuwa goalkeeper na dalili za kurudi kazini kama zingekuwepo ungekuwa umeziona.

Most times mambo yaianza na saikological tocha, anayekuwa tochad anadhani labda mambo yatabadilika yatabadilika na anaendelea kuvumilia na kukaa, watoto wanaokota yale yote mabaya ambayo wazazi wao wanafanyiana na badala ya kulea watoto kwa maadili mazuri unakuta watoto wanakuwa affected na maneno au mambo wanayonaona wazazi wao wanavyotendeana.

My advice to you is ....FOLLOW YOUR FEELINGS, kama utamvumilia basi be ready for a long haul of miserable family life na this time it will also affect your kids in a way bigger than you expect

Anonymous said...

Kwa kweli huyo mwanaume naweza kusema hana upendo wa dhati.katika kipindi cha ujauzito kama icho inabidi aonyeshe upendo wa dhati kwako ili ukuaji wa mimba uende vizuri;Pia hivyo vituko vyake anakuwa kama amesahau mmetoka wapi,mpo wapi na mnaenda wapi,na mnatakiwa kufanya nini hasa ktk kipindi hicho cha ujauzito.Pia ningesema huyo ni mwanaume wa kizamani sana ambaye anaona kila kazi ya nyumbani ni ya mwanamke.ebu aache tabia hiyo;ndoa ni kusaidiana bila kujali unafanya nini;kwani akipika atabadilika nini
?au akifanya usafi ndani ya nyumba atabadilika nini?Hakuna bali ni kujijengea heshima na utu ndani ya nyumba.Hapo kuna mawili 1.labda kuna sehemu anajishikiza anatafuta kisa tu akutimue,2.kapagawa kuja uk;
Nakushauri kuwa mvumilivu ,kaa naye chini tena,ongea nae kiupole,lea mimba yako,akiendela baada ya kujifungua chukua chako anza maisha yako kwanza hauna shida unakazi yako nzuri tu !kwa nini akunyanyase aka usikubali.

Dondidondi.

Anonymous said...

Mhhhh du!!

Hey mdada, mimi niko ughaibuni, kwa kweli kisa chako nimekisoma hata sijamwelewa huyo mumeo kama masimulizi yako ni kweli.Yaaaaani mumeo ughaibuni watu tunachakalika kiaina hata usingizi tunausamehe na hatuna familia wengine, lakini mumeo mwenye familia anafanya hivyo?? kweli nashindwa kuamini mimi!!!

Kama ulivyosimulia ndivyo kweli, basi huyo mumeo ni hatari sana. Yamkni ni vema arudishwe bongo, au huko Uingereza maisha ni mtelemko?? Hapa US sidhani kama hata siku mbili zingempita huyo, la sivyo huwezi kuishi na mtu wa namna hiyo kama mume na baba wa watoto wenu.

Mimi binafsi nakushauri usitengane naye jaribu kuvumilia na tafuta watu wenu wa karibu wakusaidie kumpa somo, naamini atarekebika.

Ukimwacha utajiingiza kwenye shida zaidi kwa usumbufu mwingi.Wewe mvumilie kwanza huku ukitafuta njia ya kumrekebisha taratibu.Huku ughaibuni watu wanatafuta kazi kwa udhi na uvumba yeye anaacha ili akae tu anaishi ulimwengu gani huyo?

Kama umepoteza hamu ya mapenzi naye, hilo si tatizo maana hata ukifanya mapenzi na mtu anakuudhi hayawezi kuwa mapenzi kwani mapenzi ni furaha na raha inayokamatisha kila kilicho ndani ya mwili wako.Kwa hiyo kama sehemu ya mwili wako inajeruhiwa hata ungefanya ngono hutafurahia hata kidogo. Hilo lisikusumbue litakuja lenyewe mambo yatakapojirekebisha.

Kila la heri mdada.

Anonymous said...

ungemwambia kwamba na yeye ni mwanaume wa kiafrika anatakiwa kufanya kazi na kuilisha familia sio kukaa nyumbani na kuangalia TV.

bmk
uk

Anonymous said...

Mimi nimwanaume mwenye familia ya mke nawatoto watatu, nakuonea huluma saana dada yangu,,yani utadhani una hali kama ya mke wangu anayokuanayo akiwa na ujauzito.Ok dada yangu hivi wewe ni mcha Mungu?Hili neno mume wako alilokutamkia ni neno baya mnooo!! na huyu bwana mimi nimeshindwa kumuelewa kabisaa!! kwasababu yeye yupo hapo UK kutokana na nguvu zako!! na anazidi kutofautiana na mke wake hivo??Ila mala nyingi matatizo ya mume na mke nivigumu kuyaingilia mtu wa pembeni na ikumbukwe kwamba hapa hujaonyesha chochote ambacho wewe umeshamuudhi!!je wewe hujawahi kumuudhi kwa lolote?kwasababu mimi nashindwa kuelewa jinsi gani anashindwa kukusaidia kazi za jikoni kipindi una upendo kwake namna hiyo,,Na kwa maisha ya ulaya mke na mume kusaidiana kwa kila kitu ni lazima,,mimi nipo hapa Amsterdam na mke wangu tunapeana zamu ya kupika hata kama hana tatizo lolote, na tunaenderea kuishi maisha mazuuri na watoto wetu watatu,,wala sioni tatizo lolote kwasababu hata kupika kwenyewe nilifika hapa ulaya bila utaalamu wowote wa kupika ,lakini mke wangu mwenyewe ndo aliye nifundisha polepole mpaka nika enjoy.Ushauli;NAKUOMBA CHA KWANZA USIINGIZE MAWAZO YAKUTENGANA NAYE KWAMATATIZO HAYO HARAKA,WATOTO WASIKUE BILA BABA YAO,,LAKINI KITU MUHIMU KAA NAYE MUELEZE UKWELI WAKO WOOTE KUHUSU YEYE NA HILO NENO ALILOTAMKA MBELE YAKO UMUELEZE KWAMBA LIMEKUUDHI MNO! KAMA UTAONA ITAKUWEA VIGUMU KUMUELEZA MTAFUTIE RAFIKI YAKE AU HATA NDUGU YAKE UMTUME KWAKE,,PIA UMUELEZE KUWA KAMA HABADILI TABIA HIYO YA KUTOKUSAIDIA MAMBO YATABALIKA .NA KAMA ATAKUA NA MAPENZI KWAKO LAZIMA ATAKUOMBA MSAMAHA.lakini usichukue maamuzi yakutengana mapema hivo bila hata ya kuyaongelea. ni hayo tu.

Anonymous said...

Dada huyu mumeo hana ustaarabu, kama unaweza kulea wanao mwenyewe hebu ondoka hapo tafuta sehemu uishi kwa maana huenda huyo mumeo anataka mimba hiyo itoke! na nashangaa sana mwanaume asiye fanya kazi ebu mweleweshe pia mwanaume wa kiafrica ndie anatakiwa awe mtafutaji nawe utunze nyumba na watoto kama alivyokuambia!

Anonymous said...

jamani jamani!!!!!!!!!!hii dunia tunaelekea wapi?????

mie napenda kusema huyo mwanaume hana maana kabisa hana upendo kwa mume wake, na umimi unamsumbua.

kaa nae chini mamy mweleze kilichoko kwenye moyo wako, asipojirekebisha ni bora uishi na wanao mwenyewe.

NB: kwani mlifunga ndoa??? na watoto wako wanaumri gani???

emu-three said...

Nilikuwa sijakisoma hiki kisa, wakati nilipopata kisa kimoja mitaani, naombeni muende mkakisome;
copy hii na paste kwenye browser yako,
http://miram3.blogspot.com/2010/07/siri-ya-mtungi-aijua-kata.html

Halafu jaribu kuunganisha na hili tukio, linawiana kidogo, lakini tofauti yake ni kuwa wewe uliyeleta kisa hiki ni mchapa kazi na mwadilifu katika familia yako wakati yule ni `mwovu' kama tukio linavyoonyesha.
Mimi kwa ushauri wangu kwako, kuna mawili, kwanza subiri ujifungue halafu uone nini cha kufanya, kwasababu ukiwa mjamzito unaweza ukawa na maamuzii yatokanayo na mimba, kuchukia, kukasirika, kutokupenda nk.
Lakini la pili kaa na mumeo usichoke kumshauri kuhusu swala zima la malezi ya watoto na uwajibikaji ndani ya familia. Mweleze wazii kuwa yeye ni baba, kama hataki kuwa baba, basi akubali wewe uwe baba yeye awe mama, kimajukumu. Nashindwa kumuelewa hapo anaposema `wanawake wanatakiwa kufanya hizo kazi, je humuulizi na wanaume wanatakiwa wafanye nini, kwani kimtizamo huo mwanaume ndiye alitakiwa akawajibike makazini, sasa yeye mbona yupo nyumbani.
Kuna kutokea kukosa kazi, na hii inaweza kuwa kwa mume au mke, na hapa ndipo tunatakiwa tuwe na hekima ya kuamua, kama mke ana kazi na mume hana, basi mume jitahidi kufanya zile kazi za nyumbani kama upo nyumbani, kuna ubaya gani, siku ukipata kazi mtasaidiana.
Nakuomba mlengwa usichukue maamuzi yoyote sasa, subiri ujifungue, hata kama unaishi kwa shida kama ulivyosema, wewe hakikisha kile unachokiweza unafanya kama hukiwezi na kitahatarisha afya yako acha, na utoe sababu kwanini.
Ni hayo kwa leo.

Anonymous said...

Sasa kama " wewe ni mwanamke wa kiafrika ni lazima uhakikishe nyumba safi, chakula kinapikwa na kuangalia watoto".

Je yeye si ni mwanamme wa kiafrika ambaye ni lazima ahakikishe anafanyakazi ya kumuingizia kipato na kuhakikisha familia yake inakula, inavaa na watoto wanapata elimu?

Anonymous said...

Hi wewe! yani nimepatwa na uchungu utafikiri mimi. Nakwambia mwanaume asipokua na kazi ni anatumia nguvu zake kukunyanyasa wakati wewe ndio unaemlisha. Sorry for what is happening to you. Omba Mungu atakuonyesha njia ya kutokea ili kuyanusuru maisha yako na watoto wako. Kwa upande wangu ningekushauri umwitie hata marafikiki zenu wa karibu ambao unaona wanabusara ili waweze kuongea nae awe anajishughulisha. Jamani haya maisha ni ya mwanaume mzima kukaa na kusubiri tu mwanamke afanyekazi. Je watoto anaozalisha anategemea nani awasomeshe. Pole mpenzi mtetezi wako yuko.

Anonymous said...

TINA WA MOROGORO UMENIKERA KUPITA KIASI TANGU HII BLOG IANZISHWE. WEWE INAONEKANA UMEPOTEA NJIA HUKUSTAHILI KUINGIA HUMU KWANI HUMU NI KWA WASTAARABU NA WALIOELIMIKA NA KUELIMIKA SIYO LAZIMA UFIKE CHUO KIKUU AU FORM SIX BALI NI KUWA NA HALI YA UELEWA WA MAMBO.

SIJAELEWA KABISA UMEKURUPUKA TOKA WAPI NA KUVAMIA MADA BILA KUELEWA CHOCHOTE NA LUGHA ZAKO CHAFU ZA KICHANGUDOA NA KISHANGINGI.

HATUTAKI WATU WASIYO WASTAARABU HUMU PLSE USIPOTEE TENA NJIA SIKU NYINGINE. WEWE UNADHANI KUNA MJINGA MWENZAKO YEYOTE ATAKAYESAPOTI HUO UTUMBO WAKO ULIOANDIKA HUMU?

KWANZA INAONEKANA HUJAWAHI KUZAA WALA KUOLEWA. KWA HERI

Anonymous said...

1st im sorry bt I hope my swanglish itaeleweka n da short forms,.I rily mix up hz lugha.
Pole sanaa Aunty,im a fan of ths blog bt huwa nasoma comment tu bt yaani leo I hd to comment cz of huyo 'Anonymous wa 12:56PM aka akathubuthu kabisaa kuachaa na jina ati Tina wa Morogoro,..jeez galfrnd kwenda kuminsult mama wa watu ati kisa wewe u hvnt had a guy mayb in a 100yrs ndo unasaka kwa udi na uvumba yatakushidaaaa n I mean t big tym...u will b a slave 2 any man n ni cz of ppl wit mentality lyk urs ndo maana Tz hatuwezi kuendelea cz da women don get deir rights at ol!!,.education haipo!!! obviously dada mie nimefunzwa na Mama n im stl very young yaani ndoa ni vry far away frm me bt najua Destiny's Child walisema u gota 'Cater 4 ur man'..kupika,kufua,cleanin n ol dat najua bt note ni u gota cater 2 a MAN...nt a MONSTER!!!!..cz definitely she is living wit a ungrateful freakin MONSTER yani km bado kuna watu ooh an african woman ni hivi n afrian man ni hivi i summarize n call it BULLSHIT,...trust me Im very cultural,..I cook 4 ma parents sawa sio housgal wala nini,so usianze mtoto wa kishua.bt dats cz dey treat me right n wit LOVE n will do da same 4 ma friends,aunties,n da superior 'future husband'..sio huyu negro cz
Obviously a man km huyo ambaye amesema mimba ikitoka utapata mingine yaani hiyo ni straight up 'He doesnt give a damn no let me sy he doesnt give a F**ck abt her' Tina hivi wewe unaelewa maana ya miscarriage au unasikia tuuuu...lyk da wy unasikiliza taarifa ya habari, people die okaay. yaani 1st routine ya huyu Anti work,den arudi kupika hapo hajataja mambo kibaoo lyk hata nani anawaogesha watoto wake,wavalisha n ol dat cz ts inhuman wat she is goin thru n den ur supportn it n da worst part da person treatn her lyk shit is her own husband wala sio Mama mkwe eeh?..

Anonymous said...

Nw im back,. ma advice cz rily nilikuwa na nchecheto na huyooo Tina
All I can sy is uamuzi ni wako ok lyk wengi walivyosema obviously if u rily love sum1 u gota give em a 2nd chance actually many chancess n u knw dey sy marriage z 4 better n 4 worse so divorce shuldnt b ya 1st option...
1)Communication-Talk 2 hm yaani km mliweza kureach ol dese 12yrs wit shida tel hm amechange,he aint da same guy u fell for, or married n definitely u want 2 b in a good relationshp acha mapenzi bt gud understanding wit da father of ur kidzz.,,,talk n tel hm..silence will kill you.
2)Children:I bliv da minute u give birth life aint abt u anymo ts abt da baby..so ur kids obviously u want dem 2 hv a good family,a great father n mother too...dey r nw ur life so if ur life is messed up..darling so is theirs..so u need 2 make it ol clear 2 ds God looser of a man n tel hm everytn frm why he left work,ur kids,future financial issues,his stupid pathetic old stone age mentality of African women wafanye nini??..i feel even sick tryn 2 write it down yaani in short ur life rit nw cz wewe ur nt in marriage ur in HELL,..marriage is great n beautiful n soooo km he rily rily loves you (n im talkin of Jack& Rose Titanic kinda o love,..hahahaa) n love is ol abt forgiveness den if he listens,..give it another try n pray 2 Almighty God akusaidie den u see..yaani akichange alaf akarudia tena hiyo tabia Mamaaaa beba kilicho chako n LEAVE..cz if he is a man lyk dat dey neva change hadi wanaingia kaburini..ts a FACT,n Im a WITNESS.
All da best.

Anonymous said...

Naweza sema ni kweli maana mimi niko uk pia wanaume wengi wetu wanakuwa hawataki kazi na wanategemea benefits na wengine wengi kukaa kula mirungi usiku kucha hata time na wake zao hawana,la pili nimeshawasikia wanawake wengi kulalamika kuhusu hii issue ya waume zao kutokutaka kazi na wengine hulalamika hata hawapati haki yao y kinyumba dakika moja mwanaume akikaa juu kamaliza ama anatoa povu tuu.Na kuna mwanamama hapa anasema asilalamike wao wanaume wanawatafuta na mwengine anasema hajafanyiwa kitchen party nafikiri hawa watu hawajui maisha ya uk yanakuaje ukiishi hapa ndio unajua na nampongeza mdau wa us kwamba maisha kwao ni magumu sana hapa ni chamtoto mdau wa uk

Anonymous said...

wewe Tina wa MOROGORO sijapata ona mwanamke kama wewe unaroho ya hurua wewe? mume wa kuangalia tv 24//7? mwanaumke ndio akulishe, kuzalie kukulelea watoto na kukupa kila kitu uanaume upo wapi sasa? au kusaidana? yaani hadi aibu kusome ushauri wako eti huyu dada amekuboa wewe ndio umeboa zaidi!! miaka hiii ni kusaida na kupendana kwenye ndoa sio kutesana kama watumwa

Anonymous said...

Ni vizuri ukaenda kumuona rafiki au ndugu wa karibu huko ambaye ni mtu mzima mwenye busara na ambaye mume wako ana muheshimu (hata kama mzungu)ukamuomba aongee na mume wako na hii iwe baada ya huyo rafiki ku take time na kukaa na huyo mume kwa few hrs kupata picha ili hata atakavyo comment iwe kwanza ni kama ameiipata from an observers point of view.....aunt agony

Anonymous said...

HEEEEE! HUYO TINA WA MOROGORO ANA AKILI NZURI KWELI? AU KWA VILE ANA SHIDA YA MWANAUME? ANATAKA KUOLEWA SIO? AU KAHABA TU. KWANI HAYO MANENO ALIYOONGEA SI MAZURI KAMA NI KWELI NI MWANAMKE ALIYEKAMILIKA KIAKILI. ANASIKIA MWANAMKE MWENZAKE ANAOMBA USHARU KWA YALIYOMKUTA, ANAMUONA WA AJABU? KUMBE AJIJUI KUWA YEYE NDIO WA AJABU. (UKIONA MWENZIO ANAVYOLEWA WEWE TIA MAJI)NADHANI UNA AKILI NZURI. HATA KAMA UNA SHIDA VIPI YA MWANAUME SI MWANAUME MWEMA HUYO. NDOA NI UPENDO NA KUWA KITU KIMOJA. NA UPENDO NI KUSHIRIKIANA KWA KILA JAMBO PAMOJA NA HILO TATIZO ALILOKUWA NALO HUYO DADA. KUSAIDIANA NA KUSHIRIKIANA KWA KILA JAMBO. KAMA WEWE UNAONA ETI ANASTAHILI HIVYO ULIVYOSEMA, MBONA HUYO MWANAUME ANASHINDWA KUYAFANYA YA WAJIBU WAKE? UMENIBOA KWELI WEWE TINA WA MOROGORO. NADHANI NIKUSAMEHE BURE KWANI LABLA UJUI JINSI GANI MIMBA ZINAVYOSUMBUA. NAKUOMBEA KWA MUNGU UPATE MIMBA NDIO UTAJUA MIMBA NI NINI. NA MTU AKIWA HIVYO ANASTAHILI AFANYIWE NINI. WEWE AUKO SAWA HATA KIDOGO.

POLE SANA DIA, HAWA WAUME WETU WA KIBONGO WENGI NDIO YAKO HIVYO. WANAKUPENDA UKIWA MSICHANA TU. UKISHAKUWA MAMA, NDIO MATATIZO YANAPOJITOKEZA. NA UKICHUNGUZA SANA UTANGUNDUA KUWA ANA NYUMBA NDOGO TU LAZIMA, NDIO INAYOMPA KIBURI HICHO. HATA MIMI HAYO MATATIZO NIMEYAPATA DIA, SAWA KABISA NA YAKO. NA SASA NINA WATOTO WATATU, MDOGO ANAVYONYA WATU WALISEMA KWANINI NIMEZAA MTOTO MWINGINE, 'BUT GOD KWONS' HUWEZI KULAUMU HICHO. LAKINI MPAKA SASA NIPO KWA SABABU YA KULEA WATOTO WANGU, AKILI KICHWANI KWANGU. KWANI NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIONYESHA HIYO TABIA NAJUA NAISHI NA MTU WA AINA GANI. VUMILIA DIA, UZAE MTOTO WAKO,NA JITAHIDI UWE NA AMANI UONE KAMA NI JARIBU TU, NA KILA JARIBU LINA MLANGO WAKE WA KUTOKEA NA USIONDOKE WALA USIMFUKUZE, ILA JITAHIDI SANA KUMUOMBEA KWA MUNGU, HIYO ROHO ISHINDWE. KWANI MTU WA KAWAIDA MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUACHA KAZI BILA SABABU. PIA WATOTO WAKO HAYO HAWAYAJUI, WATAKOSA UPENDO WA BABA YAO. MUOMBEE NA MUNGU ATAMBADILISHA KTK JINA LA YESU. 'AMEN' USICHOKE KUMUOMBA MUNGU NI PEPO TU, LINALOSABABISHA HAYO YOTE.

KWANZA NAKUPONGEZA KUWA MAMA MWEMA NA MPOLE KWANI UNAMTII MUMEO NDIO MAANA UNAAMKA NA KWENDA JIKONI KUANDAA CHAKULA. NA WAMAMA WACHACHE WENYE MOYO KAMA HUYO, MUNGU AKUBARIKI SANA.
NAKUOMBEA MUNGU AKUTIE NGUVU NA UJIFUNGUE SALAMA MPENDWA. USIONGOPE NA UTASHINDA TU.

Anonymous said...

We Tina wa Morogoro umalaya unakusumbua ndo mana huoni hata uzito wa hili swala unafikiria kuwa na jianaume mbwa kama hili ndani ya nyumba. Nchi za watu hizi wanakutumikisha kwa kila senti wanakulipa. Mtu kama unafanya kazi masaa nane , kumi au 12 unaweza ukakuta muda wote huo uko umesimama bila kukaa sasa pima ukiwa na mimba.Ningekuwa jirani mie ningemsaidia huiyu dada kumchapa huyo mwanaume viboko kwa kufanya haya anayofanya chefuuuuuu.

Kweli we Tina wa Morogoro umenichoshaaaaaaaaaaaaa sijui tatizo ni umalaya au elimu.... Mungu akusaidie dada lolote utakalo amua liwe ni uamuzi wa busara. We ukifanya uchunguzi utajua huyu bwana ana kimada nje na huyo kimada akili zake kama za Tina wa morogoro. If so don't waste ya time utakufa kwa presha bureeeeeee ukawaacha wanao wadogo. Mtimue aende huko kwa hao wanawake wa kiafrica watao mlea kama yai na kuchukuliana na domo lake chafu kama choo, mwenyewe atarudi kanyoka.

All the best sweet.Dinah mdau wa UK huyu chukulia hili swala serious umsaidie huyu dada kimawazo, if possible in person, this is not the way to live at all.

Anonymous said...

mdada pole sana kwa yanayo kusibu mana ningekuwa mimi nisingeweza kuishi na huyo mwanaume suruali hivi inakuwaje hata bado unamwita mumeo mimi ningemwita mwanaume uumee tu na si chochote coz me ninachoelewa baba ndiye kichwa(baadhi ya watu husema hivyo)ila kwako naona ni tofauti huyo ni mkia.
Cha kufanya kama unahela ya kutosha tafuta kila njia mrudishe Tz, akuepushe na hizo presha usije ukajifungua siku si zako mtoto wa watu. Kiukweli hana mapenzi kabisa na wewe chakufanya kama unaweza kulisha familia nzima basi jipunguzie mzigo kwa kumtoa mbio huyo mpenda vya bure
Good Luck
straw

bebegal said...

biblia Inasema Mwanume Kichwa cha nyumba na anatakiwa akupende sana na kula kwa Jasho lake . As well vivyo kwa mwanamke utamuheshimu mumeo japo si kwa mwanume kama huyo. Nakushauri ngoja ujifufungu salama na baada ya likizo ya Uzazi hatakuwa hajabadilika na usaidizi wa mtoto Mtupilie mbali kabisaa hakui koz atakufanya Utende dhambi kaa chini uongee nae tena kwa mara ya mwisho otherwise ashike ustarabu wake au analengo baya na wewe. haiwezekani Mwanaume asitambue yeye ni nani katika familia . haya maisha ni mafupi na umri unaenda soo asikupotezee muda na kukupa stress za kijinga you deserve to be happy my dear. muweke wazi hataki Aanze maisha yake watoto watakua tuuu.

Anonymous said...

Hivi wewe anony wa saa 12.56.00 ujiitae TINA wa MOROGORO nafikiri na wewew huna akili kama huyo kaka anaeletewa kila kitu na mkewe... Hivi umemuelewa muhusika concern yake? hajakataa kuwa hawezi fanya kazi na wala hadai asaidiwe kazi na mumewe kwa maana ya usawa na kwa vile yuko nje. Anasikitika kuwa mumewe kaacha kazi bila sababu za msingi na kuwa ni yeye pekee anaefanya kazi na kutunza familia. kwa upande mwingine halalamiki kuwa mwenzie hafanyi kazi isipokuwa anasikitika kuwa ni yeye pekee anaefanya kazi mwenzie yupo home kakaa tu and yet kwa hali yake anahitaji support ya kutokumfanya akapoteza nguvu nyingi na hasa ukizingatia kuwa katoka kazini anahitaji pia kupumzika kutokana na hali yake. Labda wewe TINA utuambie WEWE si mwanamke. Ni nani akiwa ktk hali kama hiyo hahitaji kupumzika? mbaya zaidi ni majibu ya kunya ya mumewe... HIVI SASA WEWE TINA UNATAKA KUTUAMBIA KUWA HUYO MUME KUKAA BILA KAZI NI SAWA? UNATETEA UZEMBE WAKE? Wewe TINA si umeshangaa huyo dada kudai asaidiwe kazi... NAKUULIZA WEWE TINA NA HUYO MUME KUKAA TU AKASUBIRI KILA KITU ALETE MKEWE NI SAWA? TINA, kama umejali uafrika sana, JE SI NI YEYE SASA MUME NDO ALITAKIWA KUHANGAIKIA MAISHA YA MKEWE NA WATOTO NA SI YEYE KULETEWA? TINA, Ukitoa argument uwe umetazama pande zote critically... NA WEWE TINA UMENIUDHI KWELI KAMA ULIVYOKUWA UMEMKASIRIKIA HUYU DADA KIMAKOSA!

Anonymous said...

pole sana dada yangu kwa kweli huyo mumeo anaonekana hakupendi na anaweza kuendelea hivo hivo we ukisubiri eti labda siku moja atabadilika..

na kama upendo umeisha kwa kweli huwezi kumlazimisha mtu anaonekana kukuchoka

ninakushauri jifungue halafu uangalie ustaarabu wa kuondoka maana hana maana kabisa huyo wala huruma

aibu sijui kaiweka wapi

Doreen said...

Dia pole sana mana ni maudhi matupu.Nachokuomba lea mimba yako mpaka pale utakapojifungua na uwakikishe hubebi nyingine. wala usiondoke mana watoto watapata shida. vumilia na ujitume km kawaida yani wala usione shida. somesha watoto wako na chakula mlishe mana ndoanachotaka. pia mkabithi bwana Yesu maudhi yote naamini atabadirika. usifikirie kuachana mana sio suruhisho. do it for ur children plz.

Anonymous said...

Mwalimu wetu Dina vipi u mzima? wiki ya 3 hii hapa kwako kimya tumukimiss sana sie wanafunzi wako usitusahau namna hiyo tunajifunza mengi hapa,weekend njema.

Anonymous said...

pole dear, kama unaweza kulea watoto mtimulie mbali hana maana katika maisha yako, Mungu atakusaidia utalea watoto bila shida. pole aunt,

Anonymous said...

Kweli nimeamini nijinsi gani wanawake tulivyoamka na kushirikiana kupendana watu mmetoa maoni mazuri yakutia moyo ila huyo changudoa tina wa morogoro kachemsha rudi shule tina huna point wewee tunakuombea mungu akupe mume wa dizani hiyoo ndoutajua kilichomtoa kanga manyoya.wewe unakaa morogoro gani mbona unatia aibu au ndo wale wateja wa makuti bar wewe.wanawake siku hizi nikupendana na kuheshimiana kusaidiana kuhurumiana tina jaribu kuwa mstaarabu umalaya tu unakusumbua wewe mdau norway

Anonymous said...

huyo dada wa morogoro jamani nipeni namba yake!!!!!
Nimpe mumu wangu mie.. wala asiende huko ulaya....aje huku mbezi ya kimara.. mume wangu mie naya ndio mshika remote na kuangalia tv the whole day.. mimi ndo wa kuhangaika kutafuta kila kitu cha ndani.. yeye kama anaona ni rahisi aje amchukue... kha.. dada amenikera huyo mpaka basi.

Anonymous said...

Jamani Tina wa morogoro msimlaumu yee ni baadhi tu ya wale wanawake wengi mjini ambao kazi yao ni kuingilia ndoa za watu na kuwafanyia full uswahili ili wasahau familia zao...kubeba mwanaume mgongoni wapi na wapi tena mwanaume asiye na mbele wala nyuma, mwanaume gani unakaa nyumbani unaangalia tv wakati mkeo yuko kazini..shaaammeee.. hii ndo kichefuchefu ya ze comedy kabisa..hivi kweli mwanaume kama huyo wawezaje hata kulala nae kwa kweli mi ningemuonea hata kinyaa kwani mapenzi yanaongezeka zaidi pale unapomuona mwenzako na yeye anajituma na anamchango kwenye familia...my dear pole sana akili kumkichwa angalia asije kuwa na mipango yake mingine anakutibua wewe akunyonye mpaka pumzi ya mwisho ufe kwa presha na mawazo yeye akaoe kwingine atafute kazi aanze maisha upya...wake up my dear.

Anonymous said...

Ashakum si matusi lakini huyo mumeo ni mshenzi... Badala ya talaka, jaribu mtengane kwa muda kuona kama atabadilika.

Anonymous said...

We Tina wa Morogoro, tangu blog yenu ya matusi, kashfa, uzandiki, ubaradhuli na ujinga, iliyokuwa ikiitwa 'zeutamu', ifungwe naona unatapatapa katika blog nyingine kutoa 'mchango' wako usio na kichwa wala miguu. Nakuarifu kuwa umekosea njia. You are in the wrong place baby. Sitakutukana, ila ntakupa ushauri wa bure: unahitaji msaada haraka sana. Nakutakia kila la heri.

Anonymous said...

TINA WA MOROGORO UNABOA INAONEKANA UJAOLEWA WALA HUWAJUI WANAUME WALIVYO NA KAMA UNGEKUWA NA HIZO TABIA NZURI UNGEKUWA NA WAKWAKO
MWANAUME ANATAKA KUKUFANYA KAMA BOA KISA WEWE UMEOLEWA YAMEPITWA NA WAKATI HAYO
KAMA SWALA LA KILA MMOJA KUWAJIBIKA NAYEYE MWANAUME ANGEWAJIBIKA KWA KKUTUNZA FAMILIA KULISHA NA KUWAPELEKA WATOTO SHULE SIO KUKAA KWENYE TV TU
SUBIRI UOLEWE UPATE MUME UYAONE UTAKUJA HADITHIA SIKU MOJA YAKIKUFIKA,
MAMA DORA

Anonymous said...

TINA TINA TINA nashindwa hata nikuambie nini realy u dosolve THE UTAM BLOG not this one fuck u UNAFANYA WATU WAANZE KUTUKANA HUMU