Wakwe hawataki niolewe na Kijana wao, nahisi nina ujauzito-Nifanyeje?

"Za kazi dada, pole kwa kazi ya kuelemisha jamii.
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 23 sasa, lakini bado sijabatika kuolewa japokuwa nina boyfriend ambaye nampenda sana ila tatizo limejitokeza hivi juzi alipoenda kuwataarifu wazazi wake kuwa anataka tufunge ndoa.

Wazazi wake wamekataa na kumwambia mke wa kwanza wa mtoto wao ni lazima wamkabidhi wao kama wazazi, baada ya mpenzi wangu kunipa habari hizo sikujua nifanye nini wala niseme nini kwake.

Yeye anadai kwamba ananipenda hawezi kuniacha, lakini nimvumilie kwa muda na ndani ya miezi miwili ili atimize mashariti ya wazazi wake kwanza kwanza ndio ajue nini cha kufanya, leo hii (Email imenifikia Dinahicius wiki iliyopita) ndio kaenda kuoa nami najihisi mjamzito ila yeye bado sijamwambia,

Naomba ushauri please, nifanye nini?"

Dinah anasema: Namshukuru mungu kwa sasa niko salama baada ya kukamatwa na Hay Fever na ndio maana nilishindwa kujibu swali lako mapema, samahani kwa hilo.

Pole sana kwa Mkasa unaokabiliana nao. Kwa kweli nashindwa kuamini kama kuna Makabila ambayo bado yanasisitiza/lazimisha watoto wao kuolewa na watu walioawachagua wao kama wazazi. Hili la mke wa kwanza atafutwe na wazazi alafu baada ya hapo ndio kijana aoe anaemtaka yeye ndio nimeliesikia hapa! Inasikitisha sana.

Nadhani kuna mawili hapa Moja, ni kuwa wazazi wanamlazimisha kufunga ndoa na binti waliomtafutia wao (Inanikumbusha wimbo wa Binti Kimanzi) kama kijana anaeheshimu wazazi wake na kuwaridhisha kwa kila hali ni wazi itakuwa ngumu kwake kutaaa matakwa yao (inategemea na Mila, Utamaduni wao na Uoga wake yeye kama mwanaume).

Baadhi ya wanaume hufunga ndoa za kulazimishwa na kuishi na wake zao ambao hawana hisia nao kwa muda bila kushirikiana nao kimwili na kuwapa vituko mpaka wake hao kuomba Talaka na baada ya Talaka jamaa huenda kufunga ndoa na yule ampendae ambae ni chaguo lake ambae aliendelea na uhusiano nae wakati yuko kwenye ndoa batili.

Kama hii ndio nia ya mpenzi wako then hakuna haja ya kuwa na wasiwasi as long as unajua nini kinaendelea na siku zote anakuwa kwako.....hii haikufanyi wewe kuwa the other woman bali unamsaidia kuridhisha wazazi wake. Kumbuka mke "mtafutwa" ndio the other woman....ukimsadia kufanya vituko ni wazi mwanamke yule ataomba Talaka mapema.

Pili, inawezekana kabisa kuwa huyu jamaa anashindwa kukuambia ukweli tu kuwa hataki kufunga ndoa na wewe kwavile sio "wife type", anakupenda sawa lakini haoni kama unafaa kuwa mke wake. Kuna wanaume wengi sana hasa Afrika wanatekereza zoezi hili, utakuna Girlfriend wake mzuri kwa kila hali na wamekua pamoja kwa miaka mingi lakini anaishia kuoa "kitu cha ajabu" (mwanamke ambae wala hawaendani) na baada ya ndoa jamaa ataendelea na Girlfriend wa zamani au kuwa na Girlfriend mwingine ambae wanaendana nje ya ndoa yake.

Hii ni kwa vile baadhi ya wanaume wa Kiafrika wanaamini kuwa mke ana viwango vyake tofauti na mpenzi mzuri alienae mwenye kujipenda, kupenda maisha, kujali na kujituma/jitegemea kiuchumi. Nadhani umewahi kusikia wengi wakisema Uzuri wa mwanamke sio sura bali ni tabia.....imani hii ndio inapelekea wanaume kuoa bila mapenzi au attraction na hivyo ku-cheat on their wives kwa kutokana wanawake ambao wanawavutia na pengine kuwapenda nje ya ndoa zao. Inasikitisha lakini ni ukweli.

Sasa, kwavile unahisi kuwa unamimba nadhani ni vema kama utamjulisha jamaa kuwa umeshika mimba, kama kweli anakupenda na anania yakufunga ndoa na wewe baada ya "kuridhisha wazazi" na anajali maisha ya mtoto wake atakaezaliwa mwakani hatoendelea na ndoa au hata kama ataendelea nayo na kufanya kama "Binti Kimanzi" kwamba mume hatoi ngono, hali chakula chake, halali nyumbani n.k basi itakuwa vema.

Lakini kama mjamaa yuko serious na mke "mtafutwa" na anataka ku-share kitanda na kum-treat kama mke then sahau kama alikuwa mpenzi wako, hakikisha anajua umebeba mimba ya mtoto wenu ili asaidie kwa matunzo na malezi ya mtoto hapo baadae.

Mtoto atakapozaliwa (Mungu akijaalia mwakani) utakuwa na miaka 24, bado ni binti mdogo na una nafasi kubwa sana ya kuweka sawa maisha yako na kumlea mtoto wako kwa mapenzi yako yote. Mungu atakujaalia na utakutana na kijana mwenye kujali ambae atakuwa mume mwema hapo baadae.

Ni vema ukajifunza kudadisi asili, mila na desturi za mpenzi wako mpya ili kujua taratibu za kwako. Hupaswi kumuuliza yeye mwenyewe bali zungumza/uliza watu wenye asili kama yake ili usirudie makosa.

Usijipe hofu kipindi hiki ambacho unakuza kiumbe tumboni, jaribu kutuliza akili na kumfiria zaidi mtoto wako huyo atakae zaliwa. Ingekuwa nchi zilizoendelea hakika jamaa wa huduma ya Afya wangekupa Ushauri Nasaha na kukupa nafasi kama unataka kuendelea kutunza mimba au kuisitisha ikiwa changa (mimba ya mwezi mmoja ambayo ni kijibulungutu cha damu kinakumbwa wa mbengu ya Apple na Kisheria nchi za Magharibi unaruhusiwa kutoa) kwa njia za kisasa na salama zaidi.

Kwa bahati mbaya Tanzania hatuna utaratibu huo japo kuwa watu wanatoa mimba kienyeji na kwa njia za kizamani ambazo ni hatari kwa maisha yako, hivyo nisingekushauri ufanye hivyo japo baadhi ya wachangiaji wamegusia hilo.

Nakushauri utunze hiyo mimba kama kweli ipo na lea mtoto wako kwa kusaidiana na baba yake.

Kila la kheri!

Comments

emuthree said…
Sasa ataenda kuoa huko kwa miito ya wazazi wake na wataaishi siku kadhaa na huyo mke kama mke na mume au, halafu atamuacha au. Au wewe utakuwa mke wa pili? Hujaiweka sawa hiyo, kwani nahisi wakiachana naye huyo kama ni swala la kuoa na kuacha atamuacha na uja-uzito kama alivyokuacha wewe. Na yeye ataleta malalamiko kama yako!
Hili ni swala nyeti linapogusa mila na taratibu ambazo mara nyingi wazazi wetu wanazidumisha. Hatuwezi kuwapinga sana, kwani wao wana mtizamo wao wa kudumisha mila zao. Lakini swali la kujiuliza ni je hawo watoto wao wanaowalzimisha kuoa kutokana na mila zao wataishi kimila zao?
Mimi kwa maoni yangu, ilikuwa mkae mjadili kiundani na hata ikibidi kuwashirikisha hawo wazazi au wazazi wako wakutane na wazazi hawo wengine wajaribu kuelimishana umuhumi wa ndoa kuwa ni makubaliano kati ya muoaji na muolewaji!
Lakini hata hivyo wewe na huyo ndio mlitakiwa mcheze karata yenu vyema. Na ungehakikisha unamfahamisha kuwa una ujazito wake kabla hajaondoka!
Haya ni yangu
Anonymous said…
kwa nini umeanzia section B,sasa huyo ameshakuacha na mzigo hiyo ndio njia ya kukuacha mtu unasema ameshaenda kuoa unategemea sisi tukushauri nini
siti said…
Dada pole sana kwa matatizo yaliyokukuta na matatizo yameumbiwa binadamu ila yanatofautiana kwa kila mtu.Pia ungekuwa makini sana katika mahusiano kwanza bila kubeba mimba yake japo inaweza kutokea bahati mbaya ni bora uzae ndani ya ndoa kuliko nje ya ndoa kwani hata jamii inakuwa vigumu kukuelewa.Na ninichokushari kama huyo mwanaume angekuwa na mapenzi ya kweli na wewe angezungumza na wazazi wake ukweli kwamba angependa kuoa mke aliyemchagua yeye na si wazazi wake kwani atakayeenda kuishi na huyo mke ni yeye.Na pia angewaambia ukweli kuwa ameshampata mchumba na sio kukubali aende kuoa then arudi kwako coz kama ni ndoa ya kanisani hawezi kumuacha tena.Hata mm yamenikuta kama hayo matatizo yako kwan mchumba wangu ni mzanzibar na wazazi wake hawataki aoe huku bara wanataka aoe hukohuko Zanzibar lakini ameongea nao na kuwaeleza ameshanipenda mm japo imechukua muda kuelewa na kunikubali mm niwe mkwe wao lakini haina jinsi na tunategemea kufunga ndoa August Mungu akipenda. kama huyo mwanaume angekuwa na msimamo basi hata wazazi wangemuelewa.
Ila kwa sababu ameshaoa ww mwambie tu ukweli kama una ujauzito wake ikiwezekana washirikishe na wazazi wako.
Anonymous said…
Bibie kama kaoa si ndiyo mwisho au unataka uwe mke wake wa pili??

Huo uja uzito toa mama maana mimi nionavyo huna usalama hapo ukishazaa ndo umejiharibia usichana wako vinginevyo ukubali ukewenza au utabaki nyumba ndogo.

Mhhhhh na ninyi wadada yaani hata kutumia kinga hamuwezi ili kujinusuru na mengi?mnaruhusu mtu anatumbukiza mkwaju wote bila tahadhali kweli katika enzi hizi za utandawazi?Na miaka 23 still very young.
Hapo huna ndoa kama wazazi wake wamemgomea.Kama umeenda shule vizuri basi zinduka wala usitegemee hiyo jali.Tena lazima uwe mjanja inawezekana mpenzi wako mwenyewe anakudanganya tu huyo aliyemwoa alikuwa naye muda mrefu hata kabla ya wewe kuanzana naye.Zinduka binti!!!
Anonymous said…
Open yours eyes bibie! Unataka ushauri gani hapo wakati jamaa kaenda kuoa? Unataka kuwa mke wa pili?

Usipoteze muda, kama alikuwa anakupenda angewakalisha wazazi wake chini akapangilia points zake vizuri na akatafuta watu makini kama wawili hivi wakampa support ya points wakati anaongea na wazaze wake; nadhani usingeweza kufika hapa ulipo. Kama una strong reasons hata kama wazazi ni 'waakoloni' kiasi gani utawafanaye wakubalianae na wewe. Lakini wakisema kuwa lazima tukutafutie mke na wewe ukainamisha kichwa chini kama kobe kaona nyoka, utaishia kuona usiyempenda!!!!!

Kama una mimba usiitoe, huu siyo mwisho wa dunia; tulia, jifungue na tunza mtoto wako. Cha msingi mueleze kuwa una mimba yake; if you are real sure kama niyake! Maana mpaka sasa hujamwambia na unadai unampennda; je hamuonani kila mara?

Pole! Lakini jifunze kusoma nyakati!!!!
Anonymous said…
Pole sana dada huyu mkaka hakupendi ametafuta tu sababu ya kukuacha, kuwa kama mbayuwai akili za kuambiwa changanya na zako.
Anonymous said…
Pole sana ndugu yangu, mm pia yalinikuta km yako. Nilimpata mchumba mwezi mei 2007 tukakaa mpaka mwezi wa 11 hiohio 07 akaoa m/mke mwengine akajidai eti kalazimishwa na wazee wake lkn nisijali mm nitakuwa wa 2 kwa vile dini yett inaruhusu. Na kweli januari 08 akaja akaleta posa nyumbani na mwezi ulofuatia akapata safari ya kikazi ulaya mwezi 1, aliporudi hakuja kusema lolote nyumbani akawa kimya tu. Mwaka jana disemba nikamfata nikamuuliza mambo yetu ya ndoa vp maana naona kimya na sijijui nipo kundi gani km bado nipo na yeye au ndo basi? Akanambia ningoje mpaka nimalize chuo miaka 3 kumbe alikuwa na lake mwezi ulofuata kaoa mke mwengine wa 2 mm nipo tu, na kinachoniuma zaidi ni kuwa yy ndo alonibikiri, sasa dadangu hapo nakushauri usipoteze muda wako kwa huyo mtu kwani hana mapenzi na wewe na wala asikudanganye eti utakuwa wa 2 kwani yatakupata km yangu. Dada endelea na maisha yako usingoje kuumizwa zaidi
Anonymous said…
Pole sana mdogo wangu huyo kaka hana maamuzi yake binafsi anaendeshwa na wazazi wake. Kwa kijana wa karne ya sasa anao uwezo wa kuelimisha wazazi na wakamwelewa, sasa huyo wa kwako naaona hana ubavu kwa maana hiyo hata akikuoa wewe atakuwa akiendeshwa na wazazi wake kwa kila jambo. Hiyo mimba sikushauri kuitoa kwa sababu hicho kiumbe kina haki ya kuja kuishi duniani labda mungu akipende zaidi akichukue, hata hivyo unajuaje mayai yako ya uzazi yako kiasi gani? unaweza ukatoa mimba na usizae tena, mifano iko mingi mi naujua wa dada mmoja ambaye alishauriwa na shost wake atoe mimba iliyoingia karibia na kufunga ndoa kwa sababu ilikuwa inamsumbua sana maswala ya kutapika na nini, alipoitoa hakupata mimba tena mpaka leo hii anajuta.Usiombe unapotafuta mtoto bwana hata kama huna mume unatamani umpate wa kukupa mimba na aachane na wewe ilimradi tu unamwanao.Nakuomba mimba ilee vyema zaa mtoto wako mengine muombe mungu atakujaalia.
Anonymous said…
Unadanganywa dada, mimi wakati naolewa sikujua ka mume wangu alikuwa na girl friend, tukifunga arusi yeye alikuwa ndo anajifungua.

Unajua alimdanganya hawezi kumuoa kwani wazazi wamekatalia na wamemchagulia mwanamke. Ila haya yote niligundua baadae sana nikiwa tayari niko ndani ya ndoa na nina mtoto tayari. Kweli kiliniuma sana kwani hata mimi ni mwanamke hivyo nisingekubali nimfanyie mwanamke mwingine kitu ambacho mimi sitaki kufanyiwa MAISHANI. Hawa viumbe kwakweli sijui wakoje NI WAONGO SANA WALA USIWAAMINI WANAUME KAMWE.

Huyo mwanamke bado wako naye analea mtoto ila mke wake ndio mimi japo sipendi haya maisha roho inaniuma sana kila nikikumbuka kuwa anahuyomwanamke NAUMIA MNO.

JAMANI WANAUME KUWENI WAKWELI.

HAKUNA CHA WAZAZI WEWE ZAA, LEA MTOTO WAKO KAA ZAKO KIMYA ILA ACHANA NA HUYU MWANAUME KABISA. USIWE UNAMUUMIZA HUYO MKE WAKE MAANA HAJUI KAMA MIMI NILIVYOKUWA SIJUI.
Anonymous said…
Katika pita pita zangu nikasoma hivi. Utajuaje kama mwanamme hana mpango nawe? Katika sababu alizotoa mwandishi anasema, pale mwanamme anawapo watumia wazazi wake kama kisingizio katika maamuzi yake kumbe ni yeye aliye amua kufanya hivyo. Huna haja ya kupoteza muda wako au kuendelea na mimba kwa usawa huo dada, kuendelea kujing'ang'aniza kwake ni sawa na kujifungia mlango katika anga lako la mapenzi.Kama unaona dhani kutoa mimba zaa endelea na hamsini zako, ila swala la kuolewa na huyo bwana sahau na futa katika mawazo yako.Mke wa kwanza kwake ndo aliye muheshimu kuliko wewe. In Jesus name, kwanini utake kuwa chaguo lake la pili? Hivi kweli umejishusha utu wako kiasi hicho?Leave him and acha kusikiliza sababu zake kwamba ni wazazi wake wamemshinikiza. Wewe kasha kutumia na anataka kitu kipyaaaaaaaaaaaaaaa.
Anonymous said…
katoe hiyo mimba uwe free,na uache tabia ya kubeba mimba kama sungura
By Felixs Wapps
Anonymous said…
Hapo ndio penye akili/hekima
Anonymous said…
shost pole sana kwa matatizo yaliyokukuta!! huyo boyfriend wako naweza sema hajaelimika! atakubalije kwenda kuoa mtu asije mpenda kisa wazazi wamesema? kila kitu kina nafasi yake, wazazi wana nafasi yao kwenye kutoa ushauri na yeye ananafasi yake katika kutoa maamuzi. shost me sifikirii ataoa then atamuacha akuludie wewe! hivi akimpenda huyo mwanamke kizima zima je unadhani itakuwaje? hapo ni kumuomba mungu ili akupe imani uweze kulea mimba hadi kujifungua na usishawishike na kutoa ni hatari sana.
Ila kingine ndugu msubili aludi umueleze juu ya mimba uliyonayo ili umsikie atasemaje. pole shost!!