Friday, 4 June 2010

Ex analazimisha nirudieane nae, nimekataa anatishia maisha yangu-Ushauri

"Habari dada Dinah! pole sana kwa kazi nzito uliyonayo ya kutusaidia kwa mawazo na kutuelimisha. Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 ni mwajiriwa wa Shirika moja hapa Dar.Nilipo kuwa Kidato cha 2, nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada mmoja, kwa ukweli nilimpenda sana.

Tulivyohitimu Kidato cha 4 kwa bahati mbaya mwenzangu hakuchaguliwa na mimi kuchaguliwa kwenda Kidato cha Tano, Wazazi wake waliamua arudie Kidato cha 3 Shule 1 ya Sekondari ambayo ilikuwa Wilayani na wakati huohuo mimi nilitakiwa kwenda kuendelea na masomo shule 1 huko Dar!

Kifupi ilikuwa siku ya majonzi kwetu kutengana kwani ndio ilikuwa mara yetu ya kwanza kuwa mbalimbali. Nashukuru Mungu nifanikiwa kumaliza Kidato cha 6 na mpenzi wangu alifanikiwa kumaliza Kidato cha 4! Mimi nilijiunga na Chuo Kikuu nae akaamua kwenda kujiunga na Chuo cha Ualimu.

Matatizo ya uhusiano wetu yalianza pale ambapo mwenzi wangu alimaliza na kupangiwa kituo cha kazi huko mkoa wa Tabora! kwani kwa kipindi chote ambacho tulikuwa mbalimbali tulizoea kupigiana simu angalau mara 3 kwa siku na hamna siku kupita hatujapigiana simu!

Baada ya yeye kupata hiyo ajira akawa hapigi simu hadi mimi nimpigie, nilikuwa naumia sana natabia ile mpya, siku 1 nikamwambia ukweli kwanini mimi ndio nimpigie simu na nisipopiga ndio siku hiyo hatuwasiliani? Akanijibu tena kwa ukali kuwa yeye kapelekwa huko(Tabora) kufanya kazi na wala sio kunipigia simu mimi.

Kwa kifupi yupo busy! Niliumia mno na jibu lile lakini kwa kuwa nilimpenda nilimuomba radhi kama swali lile limemuudhi, tukaongea mambo mengine tu. Baada ya miezi michache kupita, ghafla simu yake ikawa haipatikani.

Niliteseka sana ikabidi nimtafute dada yake ambaye yeye hakunificha aliniambia wazi kuwa mdogo wake(yaani mpenzi wangu) amefunga ndoa na anadai kaniacha mimi kwa kuwa sina future!

Nilihisi kuchananyikiwa nikawa kama siamini nachokisikia! Nilikubaliana na hali halisi japo iliniathiri kimasomo na ilinichukua zaidi ya miezi 6 kumsahau! Nashukuru nilimaliza Chuo na baada ya muda mfupi nilipata kazi nje ya nchi. Kitendo cha kuondoka Tz kilinisaidia kwa 90% kumsahau kabisa mwanamke yule na nimekaa huko miaka 4 nikachoka nikaamua kurudi Tz.

Niliporudi Tz nilianza kufanya kazi hapa nilipo(ilikuwa mwaka jana mwezi wa 8)!Mwezi February mwaka huu, asubuhi moja nikiwa kazini nilipokea simu kutoka kwa yule dada(Ex~girlfriend wangu) akadai kwa muda ule yuko Dar kaja kwangu kwani anamazumgumzo ya kina nami(kumbuka ni zaidi ya miaka 5 hatujaonana wala kuwasiliana).

Tukakubaliana, tukaongea mengi mojawapo ndio lililonileta kwenu ndugu zangu mnishauri, nalo ni:-Anadai kuwa kuolewa kule alilazimishwa na alikuwa hampendi yule mwanaume hata kidogo. Kwa kuwa alikuwa ananipenda mimi ndio maana ameamua kumwacha yule mumewe na kunifuata mimi!

Mimi nilimwambia ukweli kuwa; KWANZA ndoa ya Kikristo haina Talaka, PILI siwezi kuwa nae kutokana na ukatili alionifanyia! Wadau naomba ushauri wenu kwani sasa hivi imekuwa kero kwangu. Yaani mwanamke amekuwa akipiga simu na kutoa vitisho kuwa kama sitomkubalia basi atakunywa sumu nakuandika Waraka kuwa mimi ndio nimesababisha hivyo. Ili mimi nishikwe na Polisi na kutumikia kifungo kwa rest of my life.

Kwa ukweli mimi siwezi kurudiana nae hivyo naomba mnielekeze njia gani nizitumie ili niondokane na kero hizo! Kingine ni kuwa toka niachane na mwanamke huyu nimetokea kuwa chukia sana wanawake, sina hamu tena ya kuwa na mwanamke na ni mwaka 5 sasa sijawa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke!

Je hali hii ikiendelea ndio kusema sitooa tena na ukizingatia umri unaenda? Naombena msaada wenu ndugu zangu na akhsanten sana.
Collns H.M
Dar "

Dinah anasema:Kabla hatujapoteza muda, hebu chepuka kwenye kituo Cha polisi na ripoti vitisho kutoka kwa huyo Ex na waeleze sababu ya Mwanamke huyo kukupa vitisho hivyo, kisheria Polisi wanatakiwa kukulinda wewe kutokana na vitisho vya mwanamke huyo.

Kama anakufuata-fuata Ofisini au nyumbani kwako yeye atapewa barua kwa mujimu wa Mahakama kuwa haruhusiwi kukatiza karibu na wewe na akionekana eneo hilo (unapofanya kazi/ishi) polisi wanahaki ya kumuondoa kwa nguvu.


Sasa ikitokea kajiua atakuwa kajiua kwa matatizo yake mwenyewe na wewe utakuwa salama kwani Polisi watakuwa na maelezo yako yote. Hakikisha unapata copy (nakala) ya maelezo yako, jina na cheo cha Polisi aliechukua maelezo yako, muda (siku, tarehe na mwaka), na jina la kituo just incase polisi huyo atahamishwa au kupoteza ushahidi.

**********************************************************

Baada ya kutendwa na kuumizwa na mtu uliemuamini na kumpenda imekuwa ngumu kwako kuamini wanawake, sidhani kama unatuchukia wanawake wote bali hutuamini. Kuna hali fulani ya uoga wa mwanamke mwingine kurudia kilichofanywa na Binti uliempenda.

Kwa kawaida huwa nashauri mtu ajipe muda (kaa mbali na uhusiano wa kimapenzi) mpaka utakapo pona kabisa kihisia, kupona huko kunaweza kuchukua muda mrefu kuanzia miezi sita mpaka miaka saba. Urefu wa uponaji kihisia unategemea zaidi na muda wa uhusiano wenu.

Kama uhusiano...kwa Mfano: ulikuwa wa miaka miwili na zaidi kupona kwake huchukua muda mrefu pia. Kutokana na maelezo yako inaonyesha ulikuwa umepona lakini baada ya huyu mwanamama kuanza kukufuata fuata katonesha kidonda hivyo kukurudisha nyuma.

Hali hiyo ya "kuchukia" wanawake ikiendelea hakika hutoweza kuoa au tuseme kuishi na mwanamke unless other wise uamue kufunga ndoa na mwanamke ili kutimiza wajibu kitu ambacho ni hatari sana.

Ili kuepuka hilo wewe mwenyewe unatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kukaa mbali na huyo binti "machafuzi" ili uweze kuendelea na maisha yako mapya, hilo moja.

Pili, unatakiwa kurudisha imani juu ya wanawake, kwani si wanawake wote tunatabia chafu. Kuthibitisha hilo angalia wanawake wote kwenye familia yako je wanatabia kama ya Ex wako? Hapana! sasa hiyo inamaana kuwa kosa la mwanamke mmoja halibebwi na wanawake wote Duniani. Kurudisha kwako imani juu ya wanawake ndio njia pekee ya wewe kuwa karibu na viumbe hao na hivyo kudondokea mmoja kimapenzi.

Ni matumaini yangu maelezo ya wachangiaji yamesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya uamuzi wa busara ili uendelee kuishi kwa amani na hatimae kupenda tena.

Kila la kheri!

23 comments:

Anonymous said...

Ndugu yangu huo dada ameshakuona wewe mjinga na mshamba wa mapenzi hivyo anaweza kukuburuza vyovyote atakavyo, yaani nasikia hasira natamani kama ningekuwa karibu nawe nikupige vileee.

Wewe msomi mzima na mwanaume lijali iweje huo msichana asiye mstaarabu na tapeli mkubwa wa mapenzi aje kukusumbua kichwa chako kizembe hivyo? Hawezi kufanya kitu chochote kwani wewe ndio ulimtuma akuache?

Hebu zinduka mtoto wa kiume achana na huyo tapeli mkubwa tena mwenye roho mbaya sana, atakuja kukuumiza mara kumi ya alivyokuumiza mwanzo. Huyo inaonyesha amezoea kubadili wanaume kama nguo.

Alikuacha ati kwa kuwa huna kitu, sasa hivi mambo yamemuharibikia na kaona wewe mambo yako ameanza kukusumbua tena, lakini amini nakwambia kuwa huyo binti kamwe hana mapenzi ya dhati wala ya kweli kwako.

Kama yeye alilazimishwa kuolewa, kwanini hakukwambia ukweli tangu mwanzo tena kwa upole? Na badala yake akawa mkali kama kuku mwenye vifaranga why? Na kama alilazimishwa ninauhakika kabisa kuwa dadake angekwambia ukweli kuwa mdogo mtu kaolewa kwa kulazimishwa.

Huyo mwanamke ni hatari tena sana wala huna huna cha kujiuliza mara mbili hapo ni kumpiga chini tena bila huruma, siyo kwa kuwa unalipiza kisasi noo but hii ni kwa usalama wa maisha yako.

Mabinti wazuri tena waaminifu na wenye elimu nzuri wapo wengi tu tena wanatafuta wachumba makini kama nyie wenye mapenzi ya kweli. Mimi kuna wasichana wazuri na wasomi wenye elimu ya chuo kikuu wapo wengi wacha MUNGU nawafahamu, wakati wowote ukitaka msaada wa kutaka mchumba tuwasiliane mimi takusaidia bila matatizo yoyote.

Case yako imeniuma sana kupita kiasi wewe ni kijana mwenzangu, nami pia sijaoa ila ninamchumba wangu na muda mfupi sana ujao tutafunga ndoa kwa uwezo wa MUNGU mwaka huu. Kwa sasa niko nje ya nchi nafanya masters.

Tuwasiliane kwa email hii, themzushi@hotmail.com, jina la email wala lisikutishe kwani hii naitumia tu kwa dharura ila nikipata ya kwako takupa mawasiliano yangu yote.

Nakuombea sana ili MUNGU akupe ujasili ushinde haya majaribu na kumuepuka huyo binti kwani ni mtu hatari sana kwa maisha yako. Ila acha kuchukia wasichana wote kwani wapo wengi waaminifu sna na wenye mapenzi ya kweli wanaotafuta waaminifu na wenye mapenzi ya kweli kama wewe.

Anonymous said...

kimbia haraka polisi kajisalimishe huyo ana lake jambo alikukimbia sasa ameboronga anarudi kwako! kakangu usikubali kula makombo yaliyoachwa mezani,asingeutenda hivyo moyo wako,tena sio msitaarabu ana vitisho,mshamba.mapenzi hayalazimishi.

Anonymous said...

pole kaka kwa yalokupata.hapo dada hajakutishia maisha ila amejitishia yeye mwenyewe coz akinywa sumu yeye ndo atakae kufa sio ww.hata akiandika barua ww hujamshawishi kunywa sumu.bro just move on with your life.mkataa pema,paovu panamwita.bwana wake hakuwa akimpenda na sasa amechoka nae sasa amekuwa mfa maji aachi kutapatapa.mwambie anywe sumu kama anataka,hawezi kunywa huyo.wakunywa sumu hasemi.nakushauri ubadilishe number.usije ukamrudia huyo.ukifanya hivyo utakuwa kama mbwa kula matapishi yake.bro move on with your life.mpoteze.wala hajalazimishwa coz mbona hajakwambia ila alikata mawasiliyano.open ur eyez.msa25@mig33.com

Anonymous said...

mimi pia nashauri katoe taarifa polisi mapema ili akitimiza azma yake ya kujiua wewe utakuwa ushajitoa kwenye hilo sakata. Ila usikubali kurudiana nae sisi wanawake tunamatatizo yetu binafsi, mimi naamini alikuacha kwa sababu aliona huna future nae ye kashapata ajira wewe bado mwanafunzi akaona bora akaolewe na huyo bazazi wake alieona anamfaa kwa wakati huo sasa hivi anajidai alilazimishawa, huo ni upimbi we karne hii ukalazimishwe kuolewa na mtu usiyempenda mbona haifananii kabisa? kama anataka kujiua mwache ajiue manake hata biblia inasema kila nafsi itaonja umauti akianza yeye wengine tutafuata its just a matter of time, so usitetereke na vitisho vyake alale mbele.

kuhusu kutokuwa na mahusiano sidhani kama ni tatizo ila ni kwa sababu hukuwa tayari kufungua moyo wako kwa msichana mwingine kwa sababu uliumizwa

Anonymous said...

Kijana wangu,

Kwanza nakupongeza sana kwa utulivu wako ulionao kutojihusisha na mapenzi mengine baada ya kuparanganyika kwa penzi la kwanza.Umekuwa mfano mwema sana kwa wengine.endelea kuwa makini hivyohivyo ili usije fanya kosa.Na pia umempendeza hata muumba wako.

Pili nipende kukutahadharisha kabisa kwamba usijaribu kabisa kurudiana na huyo mjinga.Wewe huwezi ingia kuoa mwanamke ambaye aliolewa amechakazwa huko.Unayo nafasi nzuri ya kutulia na kutafuta mwanamke mwingine ambaye hajaingia ndoa yoyote.

Kurudiana na huyo ni kujichafua na kujiongezea uadui na watu pasipo sababu.Nasema hivyo kwa sababu ukirudiana naye huyo ujue alikuwa mke wa mtu na alikuwa ndugu wa watu hao,hivyo kumuoa wewe utajikuta unazungukwa na maadui.Ukirudi nyuma utakuwa nguzo ya chuma.Chukia kabisa hilo jambo.

Huyo binti anakudangaya anaposema alilazimishwa na wazazi kwani alimpata wapi huyo kijana?Kuna kulazimishwa miaka hii na mtu msomi tena mwalimu nani atamlazimisha kupenda pasipopendeka.Huyo aliona wewe hujaanza kazi na akawa amelaghaiwa na mtu huko Tabora ndo kaingizwa mitini.Iweje sasa wewe uoe mtu kakaa kwenye ndoa miaka 5 na upuuzi halfu leo akwambie urudiane naye.Mwambie atabaki kuwa rafiki tu lakini si mke.

Huko yamemshinda ndo maana anataka kurudi kwako.Kataa kijana utajuta muda si mrefu ukizembea hapo.Hivi wewe na akili yako tena msomi wa chuo kikuu unatishiwa kirahisi hivyo na kunyong'onyea hivyo?Hebu fumbuka macho unatuaibisha wasomi na wanaume wenzako.

Mabinti makini tena wasomi wapo kedekede unahangaika na mtu alieyolewa?Hiyo ndoa ilikuwa ya vichakani?katoa lini talaka?na kama katoa talaka unadhani kwako hatatoa na alikujibu vibaya huko mwanzo?Mapenzi kweli ni "upofu" kabisa si ya kuyafakamia!!!

SUCRE said...

Nadhani hakuna la ziada kama Dinah kashamaliza kila kitu hivyo basi ki
lichobaki ni utekelezaji tu wa hara
ka kabla halijatokea la kutokea na pia huyo msichana umuogope sana kam
a UKOMA na ikiwezekana ubadilishe n
a namba ya simu(mpya)fasta...Kila la kheri nakuombea na wala usithub
utu kuwa naye kwa ukaribu wa namna
yoyote ile.

Anonymous said...

Hayo ya Dina hayana upinzani! Na mimi ushauri wangu ni huo. kwani huyo mwanamke alikuwa anakimbizana na nini? Unafikiri kuwa yeye ni mwalimu, ilikuwa ndo mwisho? Wewe kama, usijali, ripoti polisi haraka iwezekanavyo, vinginevyo utajutia kuchelewa. Wanawake wanatabia kama hiyo.

baby said...

pole kaka, huyo dada hana lolote inawezekana ameshaona wewe mambo yako yanakua mazuri ndo anataka kukutishia, kama alivyokueleza da dinah nenda ukaripoti polisi na taratibu zote zitafuatwa. ukirudiana naye atakuja kukutenda zaidi ya mwanzo

pole sana kaka yangu

Anonymous said...

Da!!pole sana mtu wangu fata ushauri wa dina kwenda polisi nadhani ni mzuri na utakusaidia.

Anonymous said...

Kama Dina alivyosema nenda polisi kwa usalama wako wa baadae. Ndugu yangu wanawake wanatamaa za muda mfupi sana.akitangaziwa kuolewa anaona kwake ndio future kumbe hajui ngoma aichazayo. huyo usimkubali kamwe, kajichokea huko ndio anataka kujileta kwako, kasahau nini?

Anonymous said...

sawa kabisa Dinah ulivyosema, nenda polisi kamchukulie RB upesi na uwaeleze wanafamila yake kwamba humtaki kwa sabau hizo ulizo zieleza hapa.. mmh!nahisi huyo dada yake ni mshauri wake wa karibu, inawezekana kabisa kamwambia arudi kwako kwa gia hiyo ya kijiua ili umkubali,na wanavyoona upo singo ndo kabisaa anahisi anayo nafasi.. akisema tena anajiua we mpe go ahed, maisha yake yako mikononi mwake na sio kwako alaa!

asikuletee njaa zake huyo khee! kwani lzm kuwa na mtu.. maisha yamemshinda huko aliko olewa anajirudisha kwa nguvu inahuuu!!.huwezi kuishi kwa mashaka kisa huyo msaliti. 5yrs is a long tyme people change anaweza kuwa na tabia mbaya iliyomfanya aachike ndoani anataka akuletee wewe.

hapo kaka akifa hauko guilt kabisaa atakuwa kajiua mwenyewe kwa matatizo yake ya binafsi so we endelea na maisha yako bwana, usimwendekeze, akikupigia simu kata!akitaka mkutane usiende!akija kwako usimkaribishe km una mlinzi mwambie asimfungulie! hakikisha unampotezea mazima, if possible change ur mobile number..
km humtaki kweli kuwa serious ili ufanikishe zoezi zima la kumwondoa maishani mwako kabisaa..Lily ars..

Anonymous said...

daah kwanza pole sana kaka mhasirika wa mapenzi kama mie niliyoathirika, kwani nami nipo kwenye wakati mgumu wa kupenda kutokana na maswahiba yaliyonikuta, anyways, ya kuchangia ni mengi ila kama dada Dinah alivyokushauri ni vizuri ukaenda kituo cha Pilisi kutoa taarifa kuhusu kutishiwa usalama wako, pia hy mwanamke hakufai kwani hana msimamo kwani ni jambo la kuwa wazi kama kweli alilazimishwa kuolewa angekueleza tu vizuri mwanzo mwisho then umshauri ila kwakuwa alificha alipenda mwenyewe so sikushauri umrudie zaidi ya kulifikisha kituoni upewe ulinzi. ni hayo tu kwa leo. Naitwa Furaha wa DSM, furaha1984@yahoo.com

Anonymous said...

Nimependa ushauri wa Da'Dina.......Nenda kwanza polisi.Mengine yatafuata.

Anonymous said...

pole kaka yangu kwa matatizo hayo,pili fanya kama dada dina alivyo kushauri,huyo dada hana msimamo wa mapenzi karne hii hamna mtu anaye lazimishwa kuolewa na mtu asiye mpenda hasa katika miji hii iliyo endelea,huyo alikupenda mapenzi yale ya kitoto wakati ww uliingia miguu yote miwili,akajua wewe mambo yako hayawezi kuwa super sasa kasikia umeenda ugaibuni anachanganyikiwa anataka kurudisha mapenzi,hallo amechelewa kama daladala limejaa hata sehemu ya kukanyaga hamna imekula kwake.mwache ajiuwe kwa ujinga wake,na anaetaka kujiuwa huwa hasemi anakutisha huyo achana nae angalia maisha mapya asikuchoshe mototo wa mwanamke mwenzie.

Anonymous said...

KWELI KAZI IPO HUYO MDADA ALICHEZEA BAHATI KWELI WATU WENGINE WANATAFUTA WANAUME WA KUWAPENDA HAWAPATI ILA YEYE ANAICHEZEA POLE YAKE MIMI NI MSICHANA MWENZAKE ILA HAKUFAI TENA KAKA YANGU KUWA MAKINI,KAMA ALIVYOSEMA DADA DINA NI VIZURI UKARIPOTI POLICE KABLA HUJACHELEWA,PILI ANAONEKANA HAJATULIA HUYO KAMA ANAWEZA MWACHA MME WAKE NA NDOA YA KANISANI AMINI HATA KWAKO HATAKUWA MWAMINIFU HATA KIDOGO SABABU ALIKUACHA BILA TAARIFA NAKUSIHI KUWA MAKINI,NA UNA NAFASI YA KUPENDA TENA MBONA TUPO TOFAUTI SIO WANAWAKE WOTE WAPO HIVYO WENGINE WAMETULIA SANA HAWANA PAPARA ZA MAISHA PLIZ UTAKUWA UNAIDHULUMU NAFSI YAKO EMBU TAFUTA MSICHANA UOE,TATU MSHIRIKISHE MUNGU KATIKA KILA JAMBO ATATENDA,NINAKUOMBEA NAIMANI UTAKUWA SAWA TU,POLE SANA.

Anonymous said...

Pole sana kaka angu,ila kweli kumsamehe mtu aliyekuacha wakati wa shida leo unaraha ndio anakufata na mikwara kibao,ni kitu ambacho hata binadamu gani hakiwezi,hata shetani mwenyewe hatoweza kumsamehe.yani watu jamani sijui kwanini huwa tunajisahau hivi.me yalinikuta kama hayo nikamwambia huyo ex-boyfriend wangu tafadhali nakuomba usinikwaze nashukuru kanielewa.sasaivi ninasonga mbele na maisha yangu tena nataka niende mabali niepuke vita na walimwengu kabisa.wewe nenda police uwaambie story yote then kweli wakupe RB alafu uwe nayo kabsa kwa sababu atakuletea tabu isiyo na msingi bure,chakula kakiacha mwenyewe kisa kibaya leo kakiona kitamu?mwambie muda wake umeisha bwana.

Thanks
Karen

Anonymous said...

Kha! huyo dada kakumbwa na ule usemi usemao " Majuto ni mjukuu" na "ng'ombe akivunjika malishoni hurejea ngamani" hata hivyo pia kuna usemi usemao "usitukane mamba kabla hujavuka mto" na vile vile ule usemao "apandaye ngazi hushuka" na zaidi "mbio za sakafuni huishia ukingoni".

kaka yangu nakushauri wewe uwe imara kama mkuki asije akakusumbua huyo, wakati ule uliponyenyekea kwake na kumsaka kwa udi na uvumba, ukaumia moyoni, ukasononeka, ukateseka kwa sababu ya hisia zako za kweli, alikutupa na kukuona hufai, jamani mimi nina hasira sana! kaka dunia bado ni nzuri kwako na simama imara kama nilivyokushauri na chukua hatua za kisheria haraka sana, uwe makini sana wadada siku hizi wanaenda kwa sangoma, mkumbatie Mungu wako kwa bidii na tia bidii katika kusali na kuamini, huyo dada natamani kumuona mpuuzi wa aina gani huyo? nina hasira sana kwa sababu hata mimi nilifanyiwa vibweka kam hivyo na mwanaume mmoja, amini siku zote aondokaye, hurejea , mimi pia ananisumbua sana, lakini nimesimama, nimeshaenda polisi nina RB siku yeyote akileta pua mbele yangu, haki ya nanai ni segerea na kesho yake lazima ahamishiwe butimba gereza la mwanza, atupwe mbali anipishe mie na pilika zangu za maisha. kaka wewe tena hata akipiga simu usiiangalie mara mbili, dawa yeke huyo ni polisi tu. Pumbavu kabisa, amekosa akili.

Anonymous said...

Nimerudi tena, suala la kujiua na ajiue sasa hivi afe kabisa, kujiua kwake wewe kunakuhusu nini, mtu dunia imeshamshinda anakung'ang'ania ati kwa sababu huko alikoenda kwa mbwembwe kumemshinda, loooo, haki ya nani ww kaka usilogwe ukarudiana na huyo mdada, halafu achilia mbali mambo mengine, kuna kusamehewa lakini sio kwa mwanamke aliyekuwa na uhusianao na wewe akakukimbia kwa sababu eti hukuwa na future, na sasa ameona umekuwa na future ndio anajileta, huyo ni tapeli danganya toto, hajatulia wala hajuai anakoelekea, asikutishe eti atajiua, kwani akijiua wewe utapoteza nini shwain huyo, kama vipi niambie nimunulie dawa ya panya nimletee aondoke fasta, alaaa watu wengine wanaudhi sana.
yeye alikuwa anaitaka future na wewe ulikuwa bado mwanafunzi hiyo future ungeijengaje nakuuliza? au huyo ngumbaru hakujua kuwa kuna stage na stage pumbaf huyo, future yake si ndio hiyo alioipata huko alikoenda, aaaa naapa kaka ukirudiana na huyo mwanamke, wewe, itakula kwako! kila la heri, fikiri zaidi, ukipewa akili ongeza na za kwako.

Anonymous said...

Hey kaka mbona yako ni madogo tu mimi binafsi yaliisha nitokea hayooo ex boy frend wangu tulipotezana naye miaka takribani 11 from 1996-2007.nilikwisha msahau kabisa sina hata wazo.nikapata mchumba tukafunga ndoa tulikaa dar miaka 2 tukahamia nje ya nchi.kwaujumla maisha yalikuwa ni mazuri.baada ya kuhamia nje nilipata kazi banki niliwajengea wazazi wangu nyumba la kifahari nikawafungulia miradi mbalimbali.kwakweli mume wangu alikuwa nazo.siku yasiku yule x wangu akarudu kijijini alifiwa na dada yake ndoakaanza kuniulizia yuko wapi yule fulani akaambiwa yuko mamtoni mambo yake ni safi kaolewa na mwanaume mwenye uwezo sana naunavyoliona lile jumba ndolakwao ikamruka akili.akaanza kwenda kwa waganga kuniharibia maisha yangu mimi na mume wangu gafla bin vu nikaanza kumfikiria yule x hadi nalia yaani nilikuwa natamani nipaye nikamuone nilichanganyikiwa nikawa kama kichaa nilikwenda hadi kwao kumtafuta wakanipa namba zake za simu nikaanza kumtafuta.tulipoonana nikamueleza mimi nimeolewa.nimekuja tu kukusalimia akaniambia yeye bado hajaoa acha tu mkaka ni historia ndefu ile hali ilivyoendelea nikamtafuta mwalmu akatukosanisha ili ninusuru ndoa yngu huwezi amini siku hizi hanipendina hana mawasiliano na mimi ndoimekuwa salama kwangu kwahiyo kama alifunga ndoa ya kikiristo achana naye ila jaribu kumueleza taratibu najua bado unampenda jaribu kuwa muungwana usilipize yale aliokufanyia ilikuwa utoto halafu siku nyingine akipinga simu mpe mwanamke apokee halafu mwambie amuachie maagizo ataacha hatopinga tena bay

Anonymous said...

Pole mdogo wangu! Loh wanawake wengine wanatia aibu, yani kaacha mumewe aliyefanya akakuacha bila sababu za msingi, Huyu hakufai TENA MSHUKURU MUNGU ALIYEKUPA UAMINIFU NA UVUMILIVU HUO WENGI WANATAMANI KUTULIA LAKINI HAWAWEZI.

Naamini unawachukia wanawake kwa ajili ya kujeruhiwa tu na HUYU MWANAMKE FEDHULI TAPELI WA MAPENZI NA MWINGI WA TAMAA. Hakufai mwambie ka sumu anywe bwana hiyo haikuhusu nenda zako polisi kachukue RB.

Naomba Mungu akupe MKE MWEMA. Ndoa ni nzuri ka UTAPEWA ALIYETOKA KWA MUNGU. SAHAU YOTE ALIYOKUTENDA OMBA MUNGU NAYE ATAKUPA ATAKAYETIBU MAJERAHA YAKO YOTE.

NAKUPONGEZA NA KUKUSIFU KWA KUKUBALI KUONANA NAE BAADA YA MIAKA YOTE 5, YEYE KACHOKA. WEWE BADO UKO GADO, HANDSOME, UKO SINGLE AND I HOPE FINANCIALLY YOU'R OK TOO.

MTESE BWANA WALA USIMWONEE HURUMA KA SHETANI ANAVYOTESEKA BILA HURUMA KWA MUNGU NA ANAJUA MWISHO NI JEHANAMU TU ATAENDA.

PEOPLE HAVE TO LEARN.

Anonymous said...

he, makubwa hayo alisema ameenda Tabora kwa kazi na si kwa mawasilianao huyo alikuchoka baada ya kupata kipya sasa kipya hicho amekichoka anataka cha zamani tupa huko achana naye kabisa. Mkataa pema pabaya panamwita, si siri kaka yangu kuna wasichana wengi sana tena wametulia ila wana bahati mbaya kama wewe, natumaini mungu amekuanadalia mke mwema. Hata mimi nilishakumbwa na hayo ila namatumaini kuwa ipo cku nami nitampata aliye mwema.

Anonymous said...

Ndugu yangu, sidhani kama kuna jambo ka kutuuliza hapo. Nahisi huyo mshenzi ameshaanza kukuzungukia kwa masangoma, maana inavyoonekana unataka kuwa laini. Huyo si mtu wa kuhusiana nae tena-kwa namna yoyote ile. Hivi hujajua tu kuwa anataka kukudhalilisha? Sasa wewe mtu kashaolewa, na pengine kashazaa, utamuoa wa nini? Kwanza hiyo ndoa ya kwanza ataivunjaje? Au unataka kuoa mke wa mtu? Kwanza kwa lipi zuri alilo nalo huyo FALA,MBWIGA,MWENDAWAZIMU, IDIOT! Wewe na usomi wako ule makombo ya wanaume? Tena unajua kabisa yeye haji kwako-anafuata future yako. Mbinafsi, ana tamaa na ni fukunyuku huyo. Kama alikuwa anataka future kwa nini asijitafutie yeye kwa kusoma vizuri? Mtu mwenyewe mwalimu-tena nahisi wa primary. Halafu et anamkebehi mwanachuo "huna future". Sasa anajileta ili nini? Mwambie huli vyakula vilivyochacha! Tafuta mchumba wako, msomi, muelewa, mtu mzima kama wewe. Achana na hii dot.com generation inayofikiri maisha ni gari na club tu. HUyo akija sasa wewe ndio umtishe-mwambie una RB na akikusumbua unamkamata. Afterall, suicide ni kosa la jinai. Kwa hiyo akijiua wewe huna hatia. Hakuna sheria ya kukutia hatiani kwa hilo-mimi ni mwanasheria. Wala usitishike na hivo vishawishi vyake. Hiyo taarifa ya polisi ni muhimu ili akifanya huo upumbavu nyumani kwako au popote ambapo utaonekana uko connected iweze kukudefend. Vinginevyo move on na maisha yako na MPIGE MKWARA MZITO ambao unaweza hata ku-accelerate hiyo sumu anayotaka! Fala mkubwa huyo. natamani ingekuwa mimi-angejua kilichomnyoa kanga manyoya!

beeA-TARA said...

dah pole sana mtu wangu hata mimi mwenyewe kuna msichana nampenda sana na nilmekuwa nae na mahusiano zaidi ya mwaka sasa lakini hv juzi kabadilika sana mtu wangu na kuanza kupunguza heshima nimemfuatilia nikajua ana jaribu kujenga mahusiano wa wengine nimeongea nae kushusu hilo lakini anasema mimi na yeye its ovwer mabaya zaidi tunafanya ofisi moja, mapenzi amesema atanipa lakini sipo moyoni mwake kabisa inaniuma sana napomwona ila mi mwanaume nakula ngumu tu sijui hawa vipi ni kweli nampenda kuliko anything lakini haelewi lakini zamani alikua annipenda sana tatizo analosema ni umri kati yangu nae kanipita miaka miwili hivi mimi sijalishii lakini nampenda kufa jamani niambieni nifanye nini nimsahau?