Tuesday, 22 June 2010

Alinichumbia lakini akaoa mwingine, sasa ananisumbua, nimkomeshe vipi?

"Nawasalimu wote,
Mimi ni mdada mwenye umri wa miaka 33 hivi na nina mtoto mmoja wa miaka miwili na nusu. Nilitokea kupendana na kijana mmoja hivi wa kichaga ila kweli alichonitendea sitasahau. Ukweli mimi nilimpenda kutoka rohoni na sikuangalia ana nini ila nilisikiliza roho yangu na nikampenda, na kwa wakati ule niliamini pia na yeye alikuwa amenipenda kwa dhati.

Tulikaa muda wa kutosha na wote kwa pamoja tuliamua kuanza process za kuoana na kwa wakati huo nilikuwa na miaka 28, basi tulikubaliana kuona na mipango mbalimbali ilianza ikiwa ni pamoja na kunivalisha engagement ring.

Mimi nilishauriana na wazazi wangu na ikaamuliwa shughuli ya engagement ifanyike nyumbani kwetu, na ndivyo ilivyokuwa. Baada ya engagement nilisafiri kikazi nikaenda Nje na nilikaa huko kama wiki nne hivi, wakati wote huo nilikuwa nalazimika kumpigia mchumba wangu simu mara kwa mara kumjulisha hali.

Baadaye nilirudi Tz baada ya kazi iliyonipeleka huko kuisha. Kama mwezi hivi tangu nirudi nikagundua kuwa nilikuwa mjamzito, sikushtuka nilijua kisingeharibika kitu kwa sababu nilikuwa nimeshaweka mambo wazi.

Wakati huo nikaanza kupata tetesi kuwa huyo kaka ambae sasa ni mchumba wangu alikuwa ana uhusianao na mama mmoja aliyekuwa ameachika kwa mume wake akiwa na watoto watatu, hivyo huyo kaka alikuwa akiishi kwa huyo mwanamke, mimi sikuwahi hata kumshtukia kwa sababu pia mimi kazi zangu nyingi zilikuwa za kusafiri mara kwa mara.

Nilipofuatilia nilikuta ni kweli na ushahidi ni kuwa siku moja nilikamata wallet yake ikiwa na vyeti viwili vya angaza kimoja kikiwa na jina la huyo aliyekuwa mchumba wangu na kimoja kikiwa na jina la huyo mwanamke.

Kumbe walishakubaliana kuona, hata hivyo kulikuwa na picha ndogo ya huyo mwanamke kwenye wallet hiyo ya mchumba wangu. Nilipomuuliza alikana akasema sio wallet yake eti ni ya rafiki yake.

Niliendelea kukuza mimba yangu bila hata kupata msaada wowote kutoka kwake, na wakati huo ndio alikuwa akila maisha na huyo mwanamke aliyekuwa akiishi kwake na wakati huo huyo mwanamke alikuwa amemkabidhi Rav 4 ya Bluu, taratibu za kufunga ndoa na mimi zikawa zinapigwa chenga tu.

Kila nikimuuliza alikuwa hana jibu kamili, sasa na mimi nikaacha kumuuliza maana yake mtu mzima niliona kufunga ndoa sasa ni ndoto, siku moja kipindi cha Xmas huyo aliyekuwa mchumba wangu aliondoka na huyo mwanamke hadi nyumbani kwao Moshi kwenda kumtambulisha kwa wazazi wake hao hao waliomsindikiza kuja kwetu kunivalisha engagement ring ndio hao hao walimpokea huyo mwanamke na kukaa naye kwa muda wa wiki mbili.

Wakati akimpeleka huyo mwanamke kwao, nilikuwa nimebakiza wiki mbili tu kujifungua, Mungu akasaidia nikajifungu salama, na alikuja Hospitali, lakini hakutoa hata Shilingi moja na bili iliyokuwa inatakiwa ni 148,000.

Siku niliyokuwa natoka Hospitali alisingizia kuwa alikuwa anaenda Airport kumpokea rafiki yake lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameenda kwa yule mwanamke. Hiyo haikuwa tatizo kwangu, kama niliendelea kujitunza mwenyewe kwa kipindi kile cha Ujauzito bila yeye kujishughulisha sitoshindwa sasa.

Huyo mwanaume alikuwa akija nyumbani kwangu na kutoa maneno ya kashfa na alikuwa akikuta mtoto amelala anamuamsha, haikuishia hapo, maternity ilipoisha, nilirudi kazini kwangu, na ndipo aliponifuata na kuniomba msamaha huku akalia.

Mimi nikamsamehe kwa sababu niliona labda hatarudia tena, basi nikampa sharti la kuhama ule mji tuliokuwa tukiishi mwanzo tukahamia mji mwingine na akafungua bisahara zake huko ambazo kweli ilibidi nimuongezee mtaji, niliamini angetulia.

Lakini kumbe haikuwa hivyo, baada ya kuona bisahara imekolea akaanza ufuska tena, na kwa kuwa mimi nilikuwa nafanya kazi field zaidi, basi kila nikisafiri alikuwa anaoa, wanawake wa kila aina, pete ya engenement aliyonivalisha akaichukua akamvalisha mwanamke mwingine tena, ikawa ni vurugu tu.

Nikirudi nyumbani nakuta Condom zimetumika zimetupwa chini ya uvungu, na siku moja nilikuta condom saba zilizotumika zimetupwa bafuni. Kweli ni story ndefu na siwezi kuandika yote. Niligundua huyu mwanaume alikuwa akipenda hela zangu sana kwani kila mshahara ukitoka anautaka wote hata senti habakizi, usipompa ndani hakukaliki.

Basi nilioona hali inakuwa mbaya nikaamua kuachana naye nikatafuta kazi sehemu nyingine nikapata, nashangaa alikuja katika huu mji ninaoishi akaulizia watu hadi akapajua ninaposihi sasa ameanza kunitishia, mara ataniua, mara atanifanya hiki na kile.

Shida yake anataka arudiane na mimi na baada ya mimi kuachana naye biashsra zake zimeyumba, manake hana msimamo ni kuhonga wanawake tu hana kai nyingine, na mpaka sasa mtoto ana miaka miwili na miezi 4 hajui anakula nini, anavaa nini wala anaishi vipi.

Sasa naomba mnishauri nimfanyeje manake nimeshatamani hata angetoweka duniani tu, maana hana anachofanya cha maana zaidi ya kunikosesha amani, mpaka sasa nimeamua kuishi na mwanangu tu. Naombeni msaada, ni nini naweza kufanya ili nimkomeshe.
Asante".

23 comments:

Anonymous said...

Duuh pole sana kwa matatizo yote ya
liyokukuta na kwa haraka sana kwanz
a inabidi utoe taarifa polisi kuhus
u hivyo vitisho anavyokuambia ataku
fanyia then toa taarifa kwa wazazi
wako nao wajue nini kinachoendelea
kati yako na huyo MHUNI asiyejua ma
ana ya ubinadamu ni nini na usimfik
irie wala kuthubutu kuwa naye tena
katika maisha yako na hatoweza kuba
dilika hata kama utamloweka na OMO
kwa wiki 8-10.Nakusihi uendelee kuw
a na msimamo wa NO/NEVER kwake na a
kuache kabisa bila kukusumbua pia u
sifanye mzaha maana anaweza kukudhu
ru uwe makini na matembezi na hasa
usiku...Kwa ushauri zaidi na ukitak
a kumkomesha ili ahame yeye kwa huk
o ulipo nitafute nitakupa support t
hrough...a_flex05@yahoo.com
Pole sana kwa usumbufu/matatizo.
SINDBAD

Anonymous said...

mimi nafikiri kumu-ignore ni adhabu tosha, mueleze point black kuwa biashara naye imeisha (kama kweli lengo ni hilo), na akizidi kukusumbua utamfikisha mbele ya sheria!
jamani, uanaume siyo suruali peke yake na majukumu pia....

Anonymous said...

Wewe mdada unampa mshahara wako mwanaumeee mhhh pole sana mpenzi wanaume siku hizi wanaangalia sehemu yenye unafuuu wa maisha.kwakeli namshukuru mungu kuwafungulia nuru wanawake wengi wamesoma wanakazi nzuri lkn bado tunababaishwa na hawa watu wamiguu mitatu a.k.a wanaume halafu hujasema yale ya rav4 yaliishia wapi.ktk maisha yako mwanaume asiujue sana mshahara wako.utampa hela yeye anahonga.hata mimi yamenikuta hayo ili wakwangu alipewa gari na mwanamke halafu yeye akanidanganya kanunua balon tukaenda kwao+ kwetu.nikawa nimepata safari ya kuja nje hamadi za mwizi 40 napinga simu anapokea mwanamke sikugombana na mwanamke nikaomba kuongea na mwanaume huwezi amini alinikana mbele ya mwanamke wake.kwasasa nimeisha msahau.

Anonymous said...

aaaah pole sana dada yangu kwa mateso makubwa ya mapenzi, ushauri wangu ni mdogo tu dada yangu, ni vema ukaenda kutoa taarifa polisi ya kutishiwa kuuawa ili upate ulinzi, na pia ningeomba uachane naye kabisa kwakuwa tayari una kazi yako nzuri ambayo inakufanya uishi bila kutetereka na zidi kuomba Mungu akujalie kumtunza vema mtoto wako. magonjwa ni mengi hy hakufai kabisa dada yangu anachohitaji ni fedha tu kwakuwa ameshakujua u mtu wa aina gani kwahiyo anatumia namna yoyote ambayo anaona kwa vyovyote lazima umsaidie, kwahiyo dada yangu funga masikio endelea na maisha yako. Furaha DSM

Anonymous said...

KIUFUPI HUYO SIO MWANAUME WALA USIJARIBU KUWAZA KUMRUDIA WALA KUOLEWA NAE...HATA KUZAA NAE ULIFANYA KOSA ILA PIA SI KOSA MLEE MWANAO KATIKA MISINGI ILIYOBORA....

KUHUSU VITISHO VYAKE WAPIGIE SIMU WASHENGA WALOKUJA KWENU NA PIA WAPIGIE SIMU WAZAZI WAKE PAMOJA NAWAZAZI WAKO UWAELEZE HAYO MATATIZO KWAMBA YEYE HUMTAKI NA ANAKUTISHIA MAISHA YA KUTAKA KUKUUA...

BAADA YA HAPO NENDA KARIPOTI POLISI UWAELEZEE KILA KITU KAMA ULIVYOELEZA HAPA..IKIWEZEKANA ATAFIKISHWA KITUONI NA KUPEWA ONYO KWAMBA CHOCHOTE KITAKACHOMFIKA HUYU MWANAMKE NI WEWE NDO UTAKUWA WA KWANZA KUKAMATWA NADHANI KWA HAYO SIDHANI KAMA ATARUDI KUKUSUMBUA....

Anonymous said...

DADA NENDA POLISI KAMCHUKULIE RB YA KUWA ANATAKA KUKUUA ALAFU UONE KAMA ATASOGEA KWAKO TENE
BY;WAUKAE

Anonymous said...

Jamani aunty pole sana kwa matatizo unayopata kwa kweli dada kama mimi ningekuwa wewe tena nina uwezo wangu ningemkomesha huyu mwanaume mimi nina ushauri huu.1 kama unampenda rudiana nae ila hakikisha yeye ndo anachukua majukumu ya kulea familia kama alikuwa anajua account zako badilisha kila kitu and then umwambie kuwa wewe mwenyewe huna hela so hapo unaweza kumpima kama kweli anakupendea hela and cha pili sasa hivi kuna magonjwa kama tabia yake ni mbaya na humtaki tena nenda polisi mkatie RB kuwa anakutishia kukuua so ina maana chohcote kibaya kikitokea yeye ndo responsible ila sasa siwezi jua kwenye moyo wako kama unampenda and usimpe mwanaume roho yako kama ulivyosema wanaume ni wabaya sana mpe Mungu roho yako na ndie atakuongoza jinsi ya kuishi na huyu mwanaume.

Anonymous said...

Maisha mzunguko kweli, LAKINI kumbuka; Harry “In order to be walked on, you have to be lying down.”
—Brian Weir

Anonymous said...

wewee acha nushamba ushajua anachokufatia sio mapenzi ila biashara zimeyumba we mtimue kama mbwa fukuza wewe wanaume wapo wengi au hujiamini?istoke huyo kijana hana mapenzi ya kweli si kwako wala kwa huyo mama wewe mtimume mkomeshee tena mwambiee utamfunga

ha ha ha au umemzimi a na wewe mana mpaka umeandika humu inaweza kuwa bado unaupendo nae mana hiyo kazi rahisi tuu si hata ya kuomba omba ushauri fukuza marabuku! alaa unachelewa nini?eeenh au nikusaidie? sema kama hujui kumtoa ndukiii unaniuziiiiii

Anonymous said...

Pole mpenzi mimi nina bwana wa hivyo sema tofauti ni kuwa yeye hatoki kwangu hata akilala kwa wanawake lakini anarudi najua ni jinsi gani inavyouma,huyo mwanaume ana hasiri ya umalaya tu hata akimuoa mwingine atakuwa hivyo hivyo siokwamba akupendi ila jumalaya ni jadi yake mi ninachokuomba kama unampenda muombee tu atayaacha hayo yote unajua hakuna kinachoshindikana kwa Mungu, kama Mungu kakupangia kuwa nae atambadilisha tu.

Anonymous said...

Daaah pole sana dada angu kwa kweli una msalaba ambao si mda mrefu utautua tu.
Cha msingi wewe mtafute umwambie kila lililo la wazi na la kweli hakuna lisilo na solution wala usikate tamaa ndugu yangu sisi wanaume ni kama mapanya mda wote wanataka kuingia kwa shimo kama hatujaingia,pole sana vile vile muombe Mungu aakusaidia tu

Anonymous said...

KUSEMA UKWELI MIMI NI MWANAUME TENA MTU MZIMA WA UMRI KAMA WAKO INGAWA BADO SIJAOA ILA NINAMCHUMBA JAPO KWA SASA NIKO NJE YA NCHI KIMASOMO. NAPATA HASIRA NA MACHUNGU MPAKA NASHIDWA NIANDIKE NINI KWANI UNANITIA HASIRA SANA. NAONA HATA KAMA NIKIANDIKA USHAURI NI SAWA KAMA NAPOTEZA TU MUDA WANGU KWANI WANAWAKE AKILI ZENU MNAKUWA KAMA MMELOGWA, SIJUI MLIUMBWA MUWE WATUMWA WA MAPENZI AU NINI? MANAKE HATA TUKIKUSHAURI HAPA NAJUA UJINGA WENU WANAWAKE UTARUDI KULEKULE KUJIPELEKA TENA KWA HUYO MALAYA MCHAFU TENA ASIYE NA HESHIMA, MPENDA VYA BURE NA KULELEWA NA WANAWAKE, MPNDSA KUHONGWA MMMXXX#####""XX.

HUYO SIYO MWANAUME KWANI MWANAUME LIJALI HAWEZI KUBEHAVE KIS.....GE NAMNA HIYO. MWANAUME LIJALI HUJIHESHIMU NA NI MTAFUTAJI MWENYE KUPENDA KUTUNZA FAMILY.

HIVI KWA NINI UNAKUWA MJINGA HIVYO KIASI CHA KUSHINDWA HATA KUJITAMBUA KUWA UKO JEHANAMU NA WALA SIYO MAPENZI HAYO? NILIDHANI KWA MUJIBU WA MAELEZO YAKO NI MDADA FULANI MSOMI BUT USOMI GANI MPAKA WASHINDWA KUJITAMBUA NA KUJIAMINI?

HIVI KINACHOKUTIA HOFU MPAKA UKUBALI KUWA MTUMWA WA MAPENZI YA KISHENZI TENA KWA MWANAUME MSHENZI NA MCHAFU KAMA HUYO ASIYE NA HESHIMA KWAKO WALA KWA NGUDU NA WAZAZI WAKO NI NINI? AU HUO UMRI NDIYO UNAKUTIA WASIWASI KUWA HUTOPATA MWANAUME BORA MAISHANI MWAKO ATAYEKUPENDA, KUKUJALI, KUKUHESHIMU NA KUITUNZA FURAHA YAKO DAIMA?

UNAFAIDI NINI SASA KUISHI NA MSHENZI TENA MCHAFU KIASI HICHO? AU HUJIAMINI KAMA WEWE NI MZURI? AU UNASUBURI MPAKA AKUUE KWA UKIMWI NDIO UTIE AKILI?
HIVI WEWE HUNA NDUGU AU WAZAZI WA KUWASAIDIA HIZO PESA MPAKA MSHAHARA WOTE UNAUTOA KWA HUYO MALAYA MPENDA KUKULEWA NA WANAWAKE KAMA SHOGA?

HAPO HAMNA PENZI ISIPOKUWA ANAKUTUMIA TU WEWE KAMA MTAJI NA KAMWE HANA MAPENZI KWAKO HATA CHEMBE THATS WHY HATULII KATA KIDOGO. AMESHAKUONA WEWE NI MJINGA THATS WHY WAKUBALI KUMKABIDHI MSHAHARA WAKO WOTE HUYO MALAYA MKUBWA WA KIUME TENA MCHAFU. NAHESHIMU TU DADA DINAH BUT NINADUKUDUKU YAANI NATAMANI NIPOROMOSHE MITUSI YA KUFA MTU.

HIVI DADA ZETU NI MPAKA LINI MTAENDELEA KUTESEKA NA KUTUMIWA KAMA VYOMBO NA MITAJI KTK MAPENZI? KWA NINI HAMJIAMINI KIASI HICHO?

MIMI KABALA YA YOTE NAKUSHAURI SANA KAMA ANAKUTISHIA KUKUUA WE NENDA KAMRIPOT POLICE HARAKA SANA ILI UPATE RB NA ULINZI WA POLISI KWANI WACHAGA WAWEZA KUUA WAKATI WOWOTE KWA PESA, HUJALI PESA KULIKO UTU, MWENZIO KISHAKUONA WEWE MTAJI THATS WHY ANAKUTUMIA APENDAVYO KWANI AMESHAKUONA KUWA NI MJINGA.

MIMI UNANITIA TU HASIRA MPAKA NASHINDWA NIANDIKE NINI, UNAKUWA ZOBA KIASI HICHO KWA NINI LAKINI? YAANI NAONA UCHUNGU MPAKA BASI. WEWE KARIPOTI POLISI KUWA HUYO JAMAA ANATISHIA UHAI WAKO NA WEWE HUMTAKI TENA MAISHANI MWAKO, TENA IKIWEZEKANA HAMA HAYO MAENEO HARAKA BILA TAARIFA, NA HATA AKIJA KWA KULIA NA KUJIPAKA MAJIVU KAMWE USIMRUHUSU TENA AINGIE MAISHANI MWAKO HAKIKA SAFARI HII LAZIMA AKUUE KAMA SI KWA UKIMWI BASI HATA KWA NJIA YOYOTE ILE ILI AKUNYANG'ANYE KILA KITU, KUNA WANAUME WENGI SANA KWA NAMNA HIYO SIKU HIZI, NA HUKU UGHAIBUNI NDIYO BIASHARA YAO.

Anonymous said...

Usikirie kumkomesha wala kumdhuru itavyokuwa iweje ni baba ya mtoto wako.muhim usurudiane naye hata mtu akupigie vuvuzela usimsikilize hafaaaai anapenda pesa zao.muite uongee naye kwa kina kwamba ameharibu mara mbili na maonfezi hayo usiwe oeke yako kuwa na watu wahekima.mwisho toa ripoti polisi wajue maana hiyo kumtushia mtu maisha mvaya sana na mwenyewe alijue karipotiwa aache wazimu.wala usikate tamaa utapata mume mwenye mapenzi sio huyo jambazi wahed.hao watu wadizain hiyo matatizo sana

Anonymous said...

DADA ANGU POLE KWA MKASA HUO,
KANZA FUNGUA KESI KABISA MAANA ANAVYOKUTISHIA KUKUUWA UNAJUA KILA MTU ANA AKILI YAKE MWENYEWE,UWE NA RB YAKE KABSA,PILI HUYO SI MWANAUME WA KURUDIANA NAE MY DEAR HAWA WATU WANATABIA MBAYA,ME NILISHATOLEWA NA MAHARI KABSANA MWANAUME AKANIFANYI HAYOHAYO.NA SASA PIA ANANITAKA TENA,NIKAMWAMBIA KAKA TUSIKWAZANE NAKUOMBA SANA UNIACHE KABSA.KWAHIYO MAMA UAMUZI NI WAKO WEWE MWENYEWE UNAO NA USIWEUNAMRRUHUSU KAISA KUJA KUMWANGALIA MWANAO.

Anonymous said...

Dada pole sana na machungu ya dunia. Kitu cha kwanza karipoti police manake jinsi anavyokutishia tishia isije siku ikawa kweli. Na pia mtoto akianza shule waambie walimu wake hakuna mtu mwingine atakaemchukua toka shule bila idhini yako ni hayo tu dada. Mungu akusaidie. Huku kaka anatuaibisha kweli sisi wachaga - naore mbaka!!

Anonymous said...

Dada yangu kwanza nikupe pole sana kwa yaliyokukuta na yanayoendelea kukusakama yakisababishwa na huyo aliyekuwa mchumba yako!!! Natamani hata kumtukana lakini hapa si mahala pake sana sana ni ushhauri kwako. Kwanza elewa kabisa hapo hakuna mapenzi kabisa, yaani huyo mwanaume ni tapeli tena mzoefu, limbukeni tena aliyepitiliza na kazoea vya bure, tena hafai kwenye jamii yetu ya sasa. Na kwa ubabe wake inaonyesha ameshawahi hata kukupiga!! Anyway, cha msingi ni kuwa huyo mwanaume hakufai kabisa, hebu emergine anahongwa RAV 4, mara akifulia huko anakuja kwako, keshafanya hapo kwako ndo shamba la kuvuna asivyopanda. Dada kazi ni rahisi sana nenda kamripoti polisi kuwa anakufuata fuata na kukutishia maisha, na tena nenda ustawi wa jamii ukadai haki zako za kulea mtoto azilipe na anapaswa kuleta gharama na kumlea mtoto wenu ingawa ulizaa naye kwa bahati mbaya. Tena akikamatwa na polisi muandikishane kuwa asikufuate fuate na asaini kwa mkono wake kuwa lolote litakalokukuta baya sababu ni yeye. Azuiliwe kuja nyumbani kwako, na kama kumuona mtoto aende kuripoti polisi kuwa anataka kumuona mtoto wake, tena angalia huyo jamaa anaweza akukutoroshea hata huyo mtoto maana tunawaelewa wanaume hao!!. Ni hayo na nakupa pole sana kwa ufedhuli anaokuletea huyo mwanaume.

Anonymous said...

nauliza hivi kwani weh polisi haukujui????unajua unalea mtu hlf mwisho wa siku inakuwa mbaya anakujeruhi au kukuua ndio unaanza kujuta, peleka huyo mwanaume polisi haraka sana, shauri yako

Anonymous said...

Kwanza kabisa ripoti tukio la vitisho polisi na kwa ndugu zake hili ni kwa usalama wako.Pili toa taarifa kwa ndugu zake kwa vitisho alivyotoa.then uiachie sheria ichukue mkondo wake.Pia hongera kwa kuwa mvumilivu kwan vituko vyote ulivyovipata na bado ukaweza kumsamehe.Huyu mwanaume inaonekana hakuwa na upendo wowote kwan bali ni pesa zako tu ndo zilikuwa zinawaweka karibu.Mdau A town

Anonymous said...

NO noooooooh please no no no nina mengi ya kuandika lakini sina muda, ila nooo usimpe nafasi tena, hata aje kwambie yeye pope John Paul.

Anonymous said...

sikuwahi kuhisis kama bado duniani kuna watu wana mapenzi ya dhati kama wewe mdada umeiniacha kinywa wazi pale uliponieleza eti ulimsamehe baada ya kukuacha ukiabika na pete yako ya uchumba, yaani dah kweli duniani wasichana tunajua kupenda.
Sasa ni hivi ulifanya makosa sana ulipofikia hatua ya kumsamehe na nahisi bado unatamani kumsamehe ila nkikubwa ninachokushauri mdada nenda katoe taarifa kwenye vyombo vya dola, pili mweleze ukweli hata akiendelea
kukutishia nyau wewe fanya lililo sahihi kwa ajili yako na mtoto wako. NAkupa siri mopja hakuna kitu kizuri kama kuishi bila huyo shetani kwani naamini wewe ni binti mrembo ambae utapata tu mkaka ambae he deserve your love and affection na ambae naamini atakuheshimu kama mwanamke. Kwa jinsi ilivyo huyo ambae unamwita mchumba hafai hata kumpa jina hilo next time mwite jina lake tu. Mimi ningekuwa wewe ningeanza kumjali zaidi huyu malaika uliyenaye mana ndio zawadi tosha toka kwa Mungu achana na huyo asiye na haya, jalikazi yako mana kwa sasa ndio mumeo au mchumba wako achana kabisa kujiuliza ufanye nini nakupa ujanja ufuatao najua utakusaidia
1. TOA TAARIFA POLISI
2.NAJUA BADO YUKO MOYONI MWAKO SASA HAKIKISHA UNAMSAHAU KAMA ANA EXIST
3.JALI KAZI YAKO MANA NDIO MUHIMILI WAKO
4. USISAHAU KUMUOMBA MUNGU SANA AKUPE NGUVU
4.TULIA MUDA UKIFIKA UTAPATA MCHUMBA AMBAE MUNGU AMEKUANDIKAI SIO HUYO MROHO WA PESA.
NI HAYO TU
straw

Anonymous said...

Huyu dada mnapoteza muda wenu kumshauri,jamaa aliwekwa ndani na mwanamke,dada anakuta condom zilizotumika uvunguni bado anamuendekeza? Nionavyo jamaa ni mtombaji mzuri dada anashindwa kumsahau.Mwitie mwizi ebo!! ye si hajulikani mji huu?

Anonymous said...

God forbid!!mama tafuta sheria,na nenda polisi ujiwekee kinga...ili chochote kikikutokea basi ajulukane ni yeye tu na atashikishwa adabu

wanaume wengine zoba sana!

napendael said...

UKICHEZA ATAKUUWA DADA, UNA MTOTO TAYARI UNATAKA NINI, KAZI UNAYO MSHUKURU MUNGU, HAPO SONGA MBELE USIRUDI NYUMA KAZA BUTI TU.........