Friday, 28 May 2010

Tutadumu au ananipotezea muda tu-Ushauri!

"Habari dada Dinah! Pole na majukumu.
Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba ushauri kwenye blog yako. Mimi ni mwanamke wa miaka 25, nina mtoto wa miaka 3.

Kwa sababu zisizozuilika nimeachana na baba wa mtoto karibu mwaka na nusu sasa. Baada ya hapo sikujihusisha na mwanaume yeyote yule hadi mwanzoni wa mwaka huu nilipotokea kupendana na kaka mmoja.


Penzi letu limekua kwa kasi sana lakini from the beggining nilishamwambia situation niliyokua nayo kabla sijakutana na yeye. Mwanzo ilimsumbua kwasababu hakutegemea,but after few days aliniita tukazungumza na tukakubaliana kuendeleza mapenzi yetu kwa kuwa my baby sio kipingamizi.


Mtoto wangu namhudumia mwenyewe kila kitu after all mimi nakaa kwa wazazi wangu ila yeye anakaa peke yake. Kinachonipa shida ni hiki MOJA -nakosa amani pale ninapoona anawachangamkia watoto wa majirani lakini wangu hamchangamkii kivile. Huwa ananiambia niende nae kwake kwavile weekends nashinda kwake kwakua wote hatuendi kazini.

Dinah anasema: Natambua kuwa ungependa mpenzi wako amchukulie mwanao kama mtoto wake lakini hiyo itakuwangumu kidogo hasa kama yeye mwenyewe hana mtoto, kwamba hana uzoefu wa kuwa baba.

Nadhani ni mapema sana kwa mpenzi wako kuanza kujenga mazoea na mtoto wako nahivyo kupelekea mtoto huko kumuita yeye baba, vilevile huenda anaogopa kuzoeana na mtoto huyo kwa vile hana uhakika na uhusiano wenu kwa maana kuwa ikitokea anamzoea mwanao kama mwanae na siku moja mkaachana ni wazi ataumia sana na pia mtoto ataumia kwa vile hawatopata nafasi ya kuonana tena.

Sidhani kama anachuki na mtoto wako ila inaweza kabisa inampunguzia ile hali ya kujiamini kutokana na ukweli kuwa kunamtu mwingine alifanya mapenzi na wewe na matunda ya mapenzi yenu ni huyo mtoto. ngumu sana kwa mtu yeyote kumchangamkia mtoto ambae sio wake.

Kumbuka kuwa mmekuwa pamoja miezi michache tu, na katika kipindi hicho kifupi sidhani kama ni haki kwakwe mpenzi wako au mwanao kuzoeana. Unatakiwa kuheshimu hisia zake na wewe kupunguza hali ya kujishitukia.

Yeye kuchangamkia watoto wengine zaidi kuliko mwanao haina maana kuwa hampenzi mtoto wako, kumbuka hao watoto wa jilani hawahusiani na wewe, hawakuzaliwa na wewe, hivyo anavyowachangamkia haina uhusiano wowote na mwanao, anawachangamakia na kuwapenda kama watoto.

Kama ambavyo sote tunapenda watoto wote bila kujali wazazi wao ni akina nani, lakini linapokuja suala la mtoto wa Ex wa mpenzi wako kidogo inakuwa tofauti, na ukikuta mtu anaonyesha kumpenda mtoto/watoto wako ndani ya kipindi kifupi tangu mkutane ujue kuna kitu nahitaji kutoka kwako na njia pekee ni kujipendekeza kwa watoto/mtoto wako.


MBILI -Siku zote za weekend ninapopika chakula nikiwa huko kwake, after eating he never says thank you au chakula kizuri/kibaya yaani ha-comment chochote. Sometimes nikitoka kazini nikimnunulia kitu cha kuvaa au hata take away sababu yeye hapiki na anarudi usiku he never says thank you.

Dinah anasema: Hii ni tabia ya mtu ambayo imejengeka kutokana na mazoea (inategemeana na mazingira aliyokulia) au kasumba iliyojengeka kutokana na mfumo dume, kwamba chochote kinachofanywa na mwanamke ni haki yake au ni wajibu wa mwanamke nahivyo hakuna sababu ya kushukuru.

Kuonyesha shukurani ni kitu muhimu sana kwenye uhusiano wa kimapenzi, na asante hiyo sio kwenye chakula, zawadi, ngono tu bali kwa kila jambo unalofanyiwa na mwenzio, hata ile hali ya yeye mpenzi kukujali unatakiwa kumshukuru, lakini kwa baadhi ya wanaume wetu wa Kitanzania inakuwa ngumu kwa vile hawajui.

Wakati wanakua baba zao (wazee wa Mfumo Dume) hawakuonyesha shukrani wala heshima kwa mama zao na hivyo wao kama watoto wa kiume wakadhani kuwa ni kawaida. Hivyo wajibu wako hapa ni kuweka wazi suala hili ili ajue kuwa unayomfanyia sio wajibu wako na wala sio haki yake bali ni mapenzi na hali ya kumjali, ni vema akaonyesha shukrani, akakuambia kama chakula kizuri au kibaya ili ujue wapi pa kuboresha au nini cha kuongeza, nini ununue na nini ukiepuke n.k.

TATU - Nikivaa nguo nzuri au nikipendeza hanisifii, yaani hana ile kusifia chochote changu.
Sasa napata mashaka why he is like this?au mimi ndio na-complicate mambo? kwangu mimi nahisi kuwa tabia yake sio normal.

Dinah anasema: Tabia yake ni ya kawaida sana kwa wanaume wengi tu hapa Duniani, kama nilivyosemahapo juu tabia hujengwa na mazoea sasa kama mazingira aliyokulia yalikuwa ya mfumo dume kwamba mwanamke haeshimiwi wala hathaminiwi inakuwa ngumu sana kwake kujua nini aseme kuhusu mwanamke, anachojua yeye ni kuwa mwanamke yuko pale kwa ajili yake, ampikie, amsafishie nyumba, amjali na kumridhisha kingono.

Zungumza nae na kuweka wazi hisia zako, alafu siku hadi siku anza kumsifia yeye na siku akivaa ovyo mwambie ukweli kuwa hajapendeza na bora abadilishe avae hivi au vile....hii itamsaidia kuelewa umuhimu wa kukusifia unapofanya jambo zuri au unapopendeza.

NNE, according to him anasema ananipenda, kuhusu future yetu pamoja hatujawahi zungumzia in deep but tuliongea one day. Kutokana na kuachana na baba wa mtoto wangu, naogopa sana kuwa na mwanaume lakini ndio hivyo mtu huwezi kuishi mwenyewe milele na ninampenda sana mpenzi wangu huyu wa sasa.

Lakini tatizo ndio hivyo simuelewi au niseme ni mimi ndio ninacomplicate things na kukosa amani.
Asante na naombeni ushauri nifanye nini, tatizo, ni langu au mwenzangu? Je kuna uhakika wa maisha ya mbele kama wapenzi?."

Dinah anasema: Asante sana kwa ushirikiano na uvumilivu wako, nimejaribu kutoa maelezo kwa kila swali hapo juu na hapa nitakupa maelezo kwa ujumla. Melezo yako kwenye kipendele cha nne yameonyesha kuwa wewe ni mdada mwenye uwezo mzuri wa kuchanganua mambo, umegundua kuwa tatizo ni wewe na sio huyo mpenzi wako japokuwa na yeye anavijitabia fulani ambavyo vinaongeza uzito kwenye tatizo ulilonalo wewe kama wewe.

Baada ya kuumizwa na hatimae kuachana na baba mtoto wako, umepoteza ile hali ya kujiamini na pia umekuwa ukifanya vitu kwa tahadhari kubwa (unajishitukia) kwa vile husingependa kilichotpokea kitokee. Hali hii inakufanya utamani au utake uhusiano ambao ni secure na commited au hata ndoa. Ni hali ya kawaida kwa mtu yeyote alietendwa na kuumia sana.....sasa hili ndio tatizo lako.

Uhakika wa maisha ya mbele hakuna mtu anaujua hata mtunzi wa kalenda hajui lakini siku zote sisi kama wanadamu huwa tunajitahidi kumuomba Mungu atupe uzima na aongeze baraka ili mahusiano yetu yasimame imara. Pamoja na kumtegemea Mungu pia sisi wenyewe kama pea (wapenzi) tunatakiwa kufanyia kazi ili mahusiano hayo yaendelee kuwa mazuri na yadumu kw amuda mrefu.

Kwa maana ninyingene najaribu kusema kuwa, kama unataka uhusiano wako uendelee na uwe na afya njema ni vema ukajitahidi kugundua tofauti za hisia za upendo kwa mwanao ambae ni sehemu ya mwili wako na mapenzi kwa mwanaume ambae sio sehemu ya mwili wako lakini anaumuhimu kwenye maisha yako.

Jifunze namna ya kuzungumza na mpenzi wako, namna ya kuwakilisha hoja zako, kujua mipaka kati ya mtoto wako na mpenzi wakoa ambae sio baba wa mtoto huyo (epuka kumzungumzia mtoto unapokuwa na mpenzi wako) ukiwa unamzungumzia mtoto kwa mpenzi wako itakuwa kama vile unamzungumzia Ex wako. Ni ngumu lakini jitahidi.

Umekuwa na mpenzi huyu mpya kwa takribani miezi mitano, mimi nakushauri upunguze speed kidogo ili u-enjoy maisha yako kama mama lakini pia ni binti mdogo wa miaka 25, kwani inaonyesha unaharaka sana hali inayoweza kuharibu uhusiano wenu usipokuwa mwangalifu kwani jamaa anaweza kuingia mitini kwa vile unampeleka-peleka, kumbuka wanaume wanapenda amani, hawapendi kulazimishwa wala kusukumwa-sukumwa.

Pamoja na kuwa umemhakikishia kuwa Ex hayupo tena kwenye maisha yako lakiniukweli utabai kuwa ni baba wa mtoto wako na mtakuwa na uhusiano fulani kwa ajili ya mtoto wenu kwani huwezi ukamkataza mtoto kuwasiliana na baba yake au baba yake kuwasiliana na mtoto wake.

Sasa wewe kuwa na mtoto ni headache kwake tayari kwani anaweza kuhofia mambo mengi kama vile....itakuwa vipi kama siku moja ikitokea jamaa anataka kurudiana na wewe kwa kisingizio cha mtoto wenu? huenda anafikiri kuwa itakuwa rahisi kurudiana kwa vile tayari mnamtoto......umewahi kufikiria hili, kujiweka kwenye nafasi yake ili ujue ni vipi anajisikia?!!

Mpaka sasa anajua kuwa wewe unamtoto na amekwisha muona au huwa anamuona mara kwa mara, wakati unajaribu kuhimarisha uhuaino wako vema kama utapunguza mawasiliano kati ya mtoto nampenzi wako, unapokwenda kwake kwa ajili ya weekend usiende na mtoto, nenda peke yako ili mtumie muda wenu kama wapenzi wakati mtoto atakuwa na bibi yake.

Acha kucheza kamchezo ka "a little family" kwa maana kuwa mnapokuwa pamoja ninyi watatu basi wewe unapata amani kuwa ninyi ni familia, ni mapema sana kwa hilo...mpe muda Mpenzi wako.

Ni rahisi kwa watu kusema ukipenda Boga penda na Ua lake, lakini wanasahau kuwa upendo kati ya mtoto amabe sio wako na mpenzi unatofautiana, Upendo unahitaji muda, upendo huwa haulazimishwi, upendo ni hisia na kama hisia hizo hazipo hakutakuwa na upendo....suala muhimu ni kwa yeye kumchukulia mtoto wako kama watoto wengine tu hapo jirani na kuheshimu nafasi ya mtoto kwako kama mama yake.

Natumaini umenielewa,kama kuna mahali nimekuchanganya tafadhali usisite kuniandikia nami nitafafanua. Jaribu kutembelea Makala za nyuma na baadhi ya maswali ili uweze kujifunza zaidi namna ya kuishi kwenye uhusiano na kuufanya uhusiano uwe na maendeleo na hatimae kuwa wa kudumu.

Kila la kheri!

10 comments:

siti said...

kwanza pole sana kwa kuwa kwenye mahusiano yasiyo na maneno matamu kama asante,umependeza coz hayo ni muhimu na pia yanaboresha mausiano.kwa kukushauri kwanza dada unabidi ufanye uchunguzi kiundani zaidi ni kweli amekubaliama na amekupenda kiukweli hata kam una kabeby coz unaweza ukadhani uko kwenye mapenzi ya kweli kumbe yuko na ww kwa maslahi fulan.kama angekuwa na mapenzi na ww basi hata huyo baby angemjali km anavyokujali ww inatakiwa akubali boga na ua lake.
Na kuna wanaume wengine hawajui kusifia wala kusema asante hata km umemfanyia kitu kizuri inaweza ikawa ndio malezi yake au hulka yake inachotakiwa ww umwambie ila utumie lugha ya kimapenzi zaidi mfano dia leo nimekuletea chakula najua utafurah sana au leo dia nimevaa vizuri najua utanisifia na mbinu nyingine mfano wa hizo ili umueke sawa na ww uenjoy mapenzi yenye kubembelezana na kudhaminiana ww na yy.

Anonymous said...

Hey bibie!!

Kwa maelezo yako pale mwanzo kabisa umesema alionyesha kinyongo sana mara ulipomweleza kuwa katika uhusiano uliopita una mtoto.

Kama wewe zinakucheza vizuri hapo alipo unamsaidia tu kumsogezea siku zake hadi atakapopata wake wa kuoa.

Kibaya zaidi hamjaongea chochote kuhusu hatima na azima yenu ni nini katika mahusiano hayo?Naona wewe unaenda kwake hadi kumpikia na kumpa haki zote za meme/mke.Kwa ujumla umeenda kijumla mno kiasi kwamba yatakugharimu sana.

Kumbuka kwa mnajiri wa maelezo yako huwa unapenda kumpelekea hata mapochopocho kadhaa, hapo unazidi kuonyesha udhaifu kiasi kwamba anakuona unahangaika naye mno bila kujijua.

Mahusiano yanahit aji busara ya kutosha, yaani chukua muda mrefu ku-study mtu na kuelewa na kujua ni nini hasa unakitaka katika hayo mahusiano.Pia acha kubembeleza mahusiano kwani yanahitaji sana hiari na hulka ya kujituma kwa watu wawili pasipo kujiumiza.Ukiona mashaka kwa mwenzako ujue uhusino huo una walakini.

Kwa doa ulilonalo hilo tayari wewe unaweza kujishusha zaidi kama mwanamke wa kutumiwa tu.Jaribu kuchukua muda mrefu sana kuelewa mazingira ya mwanaume anayekuja mbele yako.

Wakati huu kwako wewe si wa kuendelea kujihusisha na mapenzi kwani umeyapitia hadi ukapata na mtoto.Kinachotakiwa sasa ni kjenga dhamira ya kuolewa na unapokutana na mwanaume usipoteze muda kuingia katika mapenzi bali lenga moha kwa moja katika uhusiano unaokupanpicha ya kuolewa.

Ukitaka kumjua mwoaji si kazi ngumu,bali inaonekana ngumu kwa sababu wanawake /wasichana hamnayo malengo mahususi ya jambo hilo.

Huyo mjamaa yako kusema ukweli hana bao nawe ila kwa sasa amekupata wewe wa kumtulizia mihemko yake.Lakini kukuoa wewe hilo sahau.Usipokubaliana na mimi utanikumbuka muda si mrefu.

Mdau USA

Anonymous said...

(1)Kitendo cha kuachana na mume wako kisikufanye ukawa insecure na kutetemekea kila mwanaume....kama analeta maringo na haonyeshi mapenzi kwa mwanao achana nae....AKIPENDA BOGA APENDE NA UA LAKE....(2) put your child first always......utapata mwanaume anayekupenda kiukweli na mtoto wako.....(3)You are still very young.....asikubabaishe....kwa mfanyia yote hayo mazuri, he thinks you are desperate and that is why he is taking you for granted.....RUN AWAY AS FAST AS YOU CAN!!!!!!

Anonymous said...

Acha kukomplicate ukweli anaufahamu kwani ukifanya kitu kibaya huwa hasemi kuwa hapa umekosea au kama hujapendeza au umevaa nguo mbaya huwa hasema duh hiyo ndo nguo gani?

kwa wastani mi sishangai kabisa ila sema wewe wapenda kuambia hivyo lakini yeye hana tabia hiyo ndo maana unaona kama hayuko normal.

kuhusu suala la mtoto kama kweli hajawai kuoa kabisa na hana mtoto kabisa hapo panatia shaka saana na sidhani kama kunaweza kuwa na future, anaweza kuwa anakutumia tu then muda ukifika anatimua so heads up

Anonymous said...

Ni bora haya mambo ungejaribu kukaa naye na kumuuliza taratibu na kwa ujanja kiasi, wewe ni mtu mzima utajua jinsi ya kumuuliza. Unajua kuna watu wengine huwa si watu wa kupenda kusifia sifia, kama usemavyo kutoa asante, kuna wengine hata kuonyesha wamefurahi pia ni shida(ingawa wanakuwa na raha moyoni). Kwa mtazamo wangu nadhani ni maumbile tu ya mtu aidha yaliyotokana na malezi au mambo yaliowahi kumsibu etc. Lakini kama nilivokushauri hapo mwanzo, ni vyema muongee naye ujue otherwise utaendelea kujiuliza maswali meeengi na usipate jibu sahihi hata moja katika maswali yako, maana mwenye jibu sahihi ni muhusika.

Asante

drchima said...

HI HOW U DOING
am frank speaking from experience he is just wasting yo time
am a gentleman i knw,
Tatizo ni mtoto hapo anajiona kama amesha yavaa majukumu kabla ya wakati,
if am not mistaken ndo anaanza maisha.Kinacho mfanya ashindwe kukushit ni kwa sababu amekuzoea thats it if you want to groove what i say kama nikweli anza ku complain utaona anakugeuzia kibao.
ni hayo tu m2 wangu

Anonymous said...

sorry dia, bt huyo mtu wako hana tru feeling na wewe yupo hapo kuvuta muda ampate mtu wake mwingine anayempenda aondoke!!

sio kawaida m/mme kutokusifia kabisaa kihivyo lzm wanasemaga (mama leo umenibamba, hiyo ndo inaitwaje?) hata km hawajui fasheni za wanawake kihivyo.

mpotezee kwa muda, mpunguzie manjonjo maana na we umekwenda fasta sana kwny hiyo relation ndo maana anakuignore anajua unampenda ki kweli anahisi akikuacha hutapata mtu mwingine..^-^ars.

Anonymous said...

MY MY DEAR
usipende kujipachika kitu ambacho kinamadhara na ww kweli mtu anakupenda kwanza cha kumuambia ni me nina mtoto ukimuona haeleweki kula kona fasta,usisubiri lolote.wanaume wa sikuhizi hawataki majukumu kabsa.na kweli kuna wanaume huwa hawajui kusifia wanawake kabsa,me nina mfano kabsa boyfriend wangu huna hana anachonisifia hata ila me nalipuka hasa,alafu akiona nipo sexy utasikia hiyo nguo sio nzuri na kwakuwa nishamjua namuambia me ndio napenda kwa sababu wewe sina ninchovaa au nachofanya ukanisifia,ananyamaza na me nina
mipango yangu koz nimemuona si mtu wa kumtegemea sana.kwahiyo mama usijipatie maradhi na dawa ya kuyatibu huna,toka mapema hapo ili usijejuta badae.yani hamna kitu kinaudhi kama mtu umependeza hakusifii,umepika chakula kizuri halikusifii,lipo tu wanaume wenzie ndio wakusifie.jikaze mama usijing'ang'anize kwa kuwa uliachana na mtu.

Anonymous said...

Habari dada Dinah!! na wapenzi wote wa blog hii.

Nawashukuru sana wote mlionishauri though ushauri unauma sana lakini ndio ukweli.

Sijui kama nimewahi sana ila kwa wale wote mliochangia hadi sasa,I have started work on it.

So far,nashukuru na wanaozidi kuchangia nipo tayari kuwasikiliza.

Asanteni sana.

docter said...

kila mtu na tabia zake ,,hasa malezi ya kiafrika sisi waume hujihisi kama ndio wamiliki,,so dada ,,asante na umependeza isikushugulishe bana nae huyo kijana mpaka ujue moja ,ila wewe kamata sukani ,,kumbuka mapenzi hayashauriwi ..from me docter lees