Tuesday, 11 May 2010

SmS imezaa Penzi linalonichanganya-Ushauri

"Shikamoo dada Dinah, pole na majukumu.Mimi nimfuatiliaji mzuri wa blog yako na nimeona niombe ushauri kupitia blog yako. Naitwa Angel nina miaka 23, ni mwalimu wa Sek├Ândari moja hapa Mbeya.

Stori yangu inaanzia hapa; Mwaka 2007 Septemba nikiwa nasoma Diploma ya Ualimu huko Dodoma, kunakaka mmoja alikosea namba kwa kutuma vocha kwenye namba yangu. Mimi bila hiana nikamrudishia ile vocha na kumpigia kumwambia kaka umekosea namba.

Basi kwa kuwa nilikuwa mstaarabu kwake, kesho yake alinipigia akaniomba niwe dada yake kwani watu hufahamiana kwa njia tofauti. Nilimkubalia natukaanza mawasiliano kama kaka na dada. Yeye alikuwa Mwanza.

Baadae 2009 mwanzoni akaniomba tuwe wapenzi na kwa kuwa nilikuwa sina boyfriend kwa kipindi hicho nikamkubalia, tukawa wapenzi ingawa badohatujaonana. Nikawa naongea na ndugu zake kama shemeji yao nae akawaanaongea na ndugu zangu.

Tuliahidiana mambo mengi sana ambayo tulipanga kuyafanya mara baada ya kuonana. Mara nyingi nilipenda kumuuliza je atanipenda the way nilivyokwa kuwa mimi kwani ni mnene na wanaume wengi hupenda wanawake wembamba akawa akinijibu alichompa Mola hawezi kukikataa kwani ameamua yeye hivyo hakuna kitakachotutenganisha.

Hatimaye mwaka huu mwezi wa Nne nilienda kwake Musoma alikohamishiwa kikazi. Nampenda zaidi ya mwanzo kabla sijamuona, siku mbili za mwanzo niliienjoy kuwa nae. Tatizo likaja akawabusy sana na simu yake akichat na wanawake tofauti tofauti, sms za mapenzi na nilipokuwa nikishika simu yake alikuwa mkali kweli akidai kuwa eti namchunguza.

Usiku akilala ndio nachukua simu na kusoma zile sms,asubuhi akienda kuoga akawa anaficha simu yake. Baada ya wiki kuisha nikaongea nae kumwambia anavyofanya sivyo kabisa na kama hanipendi aseme tu kwani tulishakubaliana kuwa endapo mmoja watu hajaridhika na mwenzie aseme tu kwa uwazi.

Akasema hayo ya kutonipenda nayasema mimi yeye hana mawazo hayo kabisa, kwa kweli hatukufikia muafaka tuligombana kweli usiku ule na nikamuomba kesho yake akanikatie ticket niondoke.

Kweli baada ya siku mbili niliondoka, Nilivyofika Mbeya siku mbili za mwanzo tuliwasiliana vizuri kabisa, baadae nikawa nikimtumia sms hajibu na nikimuuliza kama kuna tatizo anadai hakuna na anaomba tuache kuwasiliana kwa muda then atanitafuta. Nikamwambia kama anataka tuachane aseme tu , lakini hakujibu na alikata simu.

Kitendo hicho kiliniumiza sana kwani nashindwa kabisa kufundisha wanafunzi kwangu kila nikiwaza promise tulizopeana mwanzo na vituko anavyonifanyia sasa nashindwa kabisa ku-concentrate na kazi zangu.

Nampenda saaana tu ila nashindwa nifanyaje ili nijue anawaza nini kuhusu mimi na hisia zake kwangu zikoje?naomba ushauri.
Asante, Madam Angel-Mbeya"

Dinah anasema: Angel asante sana kwa ushirikiano, ni matmaini yangu kuwa maelezo kutoka kwa wachangiaji yatakuwa yamesaidia kwa kiasi fulani kujua nini cha kufanya ili kupana amani na hivyo iwe rahisi kuendelea na maisha yako.

Huyo mwanaume (kutokana na maelezo yako) hana mapenzi na wewe alitaka kukutumia kama anavyotumia hao wanawake wengine, na usikute anatumia mtindo huo wa kutuma sms kwenye simu za wanawake ili kuwapata kiurahisi kama alivyofanikiwa kwako.

Na mara baada ya kupata alichokitaka ndani ya siku mbili ulipokwenda kumtembelea alihamisha hisia zake kwenye simu yake, Mshukuru Mungu kuwa mwanaume huyo alionyesha wazi tabia yake ilivyo ukiwa nae karibu imagine ni mangapi anafanya ukiwa Mbeya?

Huyu mwanaume kama walivyo Players wote huwa hawataki kuonekana kuwa wao ndio chanzo ya uhusiano kufa ili wakiishiwa huko waliko waweze kurudi kwako na kuomba uhusiano wenu uendelee kwa madai kuwa wewe ndio ulimuacha lakini yeye hakufanya hivyo.

Player yeyote akiona uko serious na uhusiano atakuambia "nitakutafuta" kwa maana nyingine anasema "usinisumbue na nikihitaji huduma yako nitakuambia"......hii inamaana kuwa mwanaume huyo hakufai na ukiendelea kutegemea siku atakutafuta utakuwa unajipotezea muda wako bure na kujipa maumivu ya moyo juu ya mtu ambae hathamini utu wala effort yako kwenye uhusiano husika.

Najua unahisia kali za mapenzi juu yake na hii inaweza kuchangiwa na umri wako kuwa mdogo na hivyo unashindwa kutofautisha hisia za kikware (last) na zile za kimapenzi (love) zote zinafanana sana kwa kuanzia lakini moja hudumu na nyingine huisha....sasa alichokuwa nacho huyo mwanaume juu yako ni Ukware na sio mapenzi.

Vievile nahisi kuwa kutokuwa ulikuwa na matarajio makubwa/mengi juu ya uhusiano wako na mwanaume yeyote kukutaka kwa vile unahisi kuwa umekamilisha mahitaji kimaisha isipokuwa mume, kwamba umemaliza masomo, unajitegemea kwa kufanya kazi na kinachokosekanakwenye maisha yako ni mtu wa ku-share nae maisha yako.

Huna haja ya kujua anawaza nini juu yako kwani amekwisha liweka wazi hilo kuwa hakuna mwanamke yeyote anaemthamini na kila mwanamke kwake ni "sanamu" la kuchezea na fashion ikipita anatupilia mbali na kwenda kununua the latest one.

Badili mawasiliano yako ili asiweze kuwasilianana wewe, pia futilia mbali namba yake ili usishawishike kuwasiliana nae unapojisikia mpweke (we all have those days), jaribu kubadili mtindo wa maisha yako hasa kwa kufanya mazoezi mepesi nakubadili ulaji wako kama unadhani kuwa ukubwa wa mwili wako ni kitu ambacho kinakukwaza.

Kwa kufanya hivyo utakuwa umejiongezea hali ya kujiamini zaidi kama mwanamke mdogo, mrembo, alieenda shule na mwenye kujitegemea kiuchumi. Tumia muda wako mwingi kuongea/kujichanganya na watu wanaokujali nakukupenda (ndugu, jamaa na marafiki).

Hakikisha unajiweka busy na jitahidi ku-focus zaidi kwenye Taaluma yako ili usijepoteza kazi kutokana na utendaji wako mbaya unaosababishwa na mawazo juu ya mtu amabe hana umuhimu wowote kwenye maisha yako.

Mungu atajaalia na siku moja utakutana na kijana mwema, mwenye kuheshimu na kuthamini mwanamke, mwenye upendo wa dhati na kwa pamoja mkapendana na hatimae kufunga ndoa. Yote hayo yanawezekana kwani Angel wewe bado ni mdogo na una muda mwingi wa kujipanga upya na kufurahia maisha yako kama mwanamke anaejitegemea kabla hujajikita kwenye masuala ya kimapenzi na mahusiano nahatimae kuwa Mke na mama kwa watoto wako.

Kumbuka ukiwa mke na mama hutopata muda wa kufurahia maisha yako wewe kama Angel bali mke na mama kwa watoto wako.....maisha yako yatabadilika in good way, lakini itakuwa great kama utakuwa ume-enjoy uanamke wako kabla hujawa na majukumu mengine ya Mke na mama.

Kila lakheri!

35 comments:

Anonymous said...

Angel, pole sana na yaliyokusibu. Mimi jinsi nilivyoelewa hii story ni kwamba, kwanza wewe inaonekana ulimpenda sana ulipomuona, i mean baada ya kumuona tu, lakini kwa upande wake hakukupenda toka rohoni. Unatakiwa kujua kitu kimoja kuwa muonekano wa mtu huchangia kwa kiasi kikubwa kukuza au kupunguza upendo, hivyo naamini kabisa huyo mtu wako inawezekana muonekano wako hakuupenda ndio maana alishiondwa kuendelea kuwasiliana na wewe, na hata hivyo kuwasiliana na wanawake wengine ili hali wewe upo naye inaonekana ilikuwa ni mbinu ya kukukatoisha tamaa ili uondoke mapema umuache manake hakukupenda. Na kuna kitu kingine pia wanaume and may be wanawake pia wanakuwa na list of lovers kwa maana ya kufanya comparison na inawezekana hilo pia alikuwa nalo akijua akishakuona the he could compare with others in his list na kuona kama ni yupi analipa zaidi, haya mambo yapo, so inawezekana jinsi alivyokuona pia hukumvutia na hivyo hukuweza kuhit his heart as others in his list.
My dear this should not put you off, inatakiwa uwe mjasiri ujue kuwa si kila kitu unachopanga kinaenda kama kilivyo, we always plan for a lot of things but failure and success are always out of our control. Unachotakiwa kufanya ni kukubali matokeo hayo lakini cha muhimu zaidi hapa ni kutulia tuliiiiiiii, umepata somo kuhusu men do not rush kutaka kiplease roho yako, unaweza kuishia kuiumiza zaidi, tulia muombe Mungu akupe mtu mwema kabisa, na iam sure utapata. Na usiendelee kuumiza roho yako kwa kujuta saaana, will not help, endelea na maisha yako, wewe bado ni mdogo fanya kazi yako kwa bidii, and have determination kama kuendelea na masomo na kadhalika. U ngali mdogo sana kupoteza nyota ya maisha yako kwa sababu ya kicheche wa musoma, ila na wewe angel dont be easy hasa kwa myu usiyemjua, wenzio tunakodi watu ili kutupa habari nyeti za watu wanaojionyesha weupe kwetu, kumbe ni weusiiiiiii tiii.

Anonymous said...

Angel, pole sana na yaliyokusibu. Mimi jinsi nilivyoelewa hii story ni kwamba, kwanza wewe inaonekana ulimpenda sana ulipomuona, i mean baada ya kumuona tu, lakini kwa upande wake hakukupenda toka rohoni. Unatakiwa kujua kitu kimoja kuwa muonekano wa mtu huchangia kwa kiasi kikubwa kukuza au kupunguza upendo, hivyo naamini kabisa huyo mtu wako inawezekana muonekano wako hakuupenda ndio maana alishiondwa kuendelea kuwasiliana na wewe, na hata hivyo kuwasiliana na wanawake wengine ili hali wewe upo naye inaonekana ilikuwa ni mbinu ya kukukatoisha tamaa ili uondoke mapema umuache manake hakukupenda. Na kuna kitu kingine pia wanaume and may be wanawake pia wanakuwa na list of lovers kwa maana ya kufanya comparison na inawezekana hilo pia alikuwa nalo akijua akishakuona the he could compare with others in his list na kuona kama ni yupi analipa zaidi, haya mambo yapo, so inawezekana jinsi alivyokuona pia hukumvutia na hivyo hukuweza kuhit his heart as others in his list.
My dear this should not put you off, inatakiwa uwe mjasiri ujue kuwa si kila kitu unachopanga kinaenda kama kilivyo, we always plan for a lot of things but failure and success are always out of our control. Unachotakiwa kufanya ni kukubali matokeo hayo lakini cha muhimu zaidi hapa ni kutulia tuliiiiiiii, umepata somo kuhusu men do not rush kutaka kiplease roho yako, unaweza kuishia kuiumiza zaidi, tulia muombe Mungu akupe mtu mwema kabisa, na iam sure utapata. Na usiendelee kuumiza roho yako kwa kujuta saaana, will not help, endelea na maisha yako, wewe bado ni mdogo fanya kazi yako kwa bidii, and have determination kama kuendelea na masomo na kadhalika. U ngali mdogo sana kupoteza nyota ya maisha yako kwa sababu ya kicheche wa musoma, ila na wewe angel dont be easy hasa kwa myu usiyemjua, wenzio tunakodi watu ili kutupa habari nyeti za watu wanaojionyesha weupe kwetu, kumbe ni weusiiiiiii tiii.

Anonymous said...

Angela,

Uroda umeliwa, inatosha sana hapo wala usiendelee tena kumsubili huyo jamaa kiashakuacha njia ya panda.

Usicheze na wanaume kwani utachezewa sana.Ishara tosha umeishaziona tena si kwa kuambiwa bali kwa kuona na kusikia mweneyewe.Je unataka nini zaidi?

Kibaya sana mlipatana mapenzi na mtu huyo kabla hata hujamjulia na kumfahamu kwa undani.Mbaya zaidi umemfuata yeye mbali kule Musoma, huoni huyo jamaa amekutumia vilivyo.Tangu mwaka 2007 hadi leo ulidhani yuko pekee?

Tena una bahati kwa kuwa hukupata kipigo huko maana ungekutana na wake wenza huko.Usiwe na upendo usio na mbele wala nyuma.Mara nyingi nimeshangaa watu husema nampenda sana na huku analia naye.

Nakuomba binti zingatia masomo achana naye huyo jamaa utapoteza taifa la watanzania kwa kutozingatia kazi yako ya kufundisha sawaswa kisa unawaza juu ya boyfriend wako.

Huo unene wako usikupe hofu yoyote wala nini.Kuna wanaume tele wanaokupenda ila usiwe na haraka tena mdogo sana miaka 23 unababaika na huyo jamaa tena kisha kuingilia kimwili, wow!!

Naomba sana achana na mawazo juu ya mtu huyo.Mimi natoka Mbeya hivyo nakuomba usiwakoseshe wadogo zangu masomo kwa kuwaza mapenzi na huyo mpuuzi wako.

Nakutakia kila la heri na baraka katika maisha na kazi yako.

Anonymous said...

Wee dada acha upofu mtu kakuonyesha makucha makali bado unazinguliwa naye?? unataka nini zaidi na umejionea mwenywe huko?

Hivi wadada unakuwaje hayo mapenzi yanawafanya muwe vipofu kabisa?? yaani hamuwezi kuthamini utu wenu mnachezewa na ahadi za upuuzi na watu wapuuzi hivyo.Mwanaume kiashakutomba umemfuata na kufanyiwa vituko hivyo na bado unataka ushauri gani???

Jamani mimi mwanaume naumia sana kuona hivyo utafikiri hamjawa viumbe vyenye thamani sana kujidhalilisha kiasi hicho??

Jilindeni jamani hampo kama watu wa kuokotwa barabarani tu,jipe heshima. Sisi wanaume kazi kuonja onja tu hakuna lolote.e ona sana umemfuata hadi Musoma umempa penzi nono huku kesho anakufanyia vituko, na bado unakomalia hapo eti UNAMPENDA???hahahahahahaaaaaaaaa hapo unaniacha hoi bin hoi.Very young girl! please do not put yourself under fire.You still have a long journey to get into genuine relationship.Utawafundisha nini hao wanafunzi wako kama na wewe unapotea njia hivyo.Hakupendi huyo kakuonja basi imeishatoka hiyo.

Anonymous said...

Hahahahahahahahhh! Hivi hata 'nyakati' wewe teacher mzima huwezi kuzisoma? Ama kweli waliosema 'Mganga hajigangi' hawakukosea. Kweli mwalimu huezi ukajifundisha na kuelewa soma ambalo lipo mbele yako: nanukuru: 'ana wanawake wengi na message za mapenzi nilizisoma', pili 'tuligombana sana mpaka akanikatia tiketi kesho yake nikaondoka; tatu 'alisema tuachane kuwasiliana na akakata simu'.

Sasa unataka atoe tangazo kwenye redio kuwa ameaachana na wewe?? Mbona majibu yako wazi mwaliumu: 'hakupendi tena'! Siku ya kwanza hata mwezi haukuisha ulitolewa baruti; je ukiolewa si ndo utakuwa ukipigwa makofi kila siku!!

Fungua macho, angaza na uone! Huyo hakufai!! Kwani umeambiwa wanaume wameisha? Eti umeshindwa ku-concentrate kuwafunisha wanafunzi! Kwa kipi hasa alichokufanyia mpaka kinakuchanganya? Kuona message za wanawake zake? Kufukuzwa kabla ya kumaliza matembezi yako? Kukwambia tuache kuwasiliana? Au mie mwenzio ndo sielewi maana ya kupenda? Ama kweli....

Pole!!!

Anonymous said...

Hi Angel mwl mzuri, unajua wewe bado mdogo sana asikusumbue inavyoonesha huyo mtu wako hajatulia kabisa kabisa, sasa usipate pressure, tulia fanya mambo yako labda hajisikii tena kukupenda na mwanzo alikupenda lakini mlikuwa hamjaonana, fanya mambo yako kwa nafasi. kama ni wako atakutafuta, na ukiendelea kumfuatafuata atakuona unashida sana, jifanye hamnazo hata kama unampenda, tulia kimya jidai uko likizo na akili yako akikutafuta sawa asipokutafuta basi fanya mambo yako, kwa raha zako.

Anonymous said...

Usipote muda wako Angela, move on.

Anonymous said...

pole sana dada nachokushauri huyo mwanaume sio mwaminifu na hakupendi kama anakupenda asingechati na wanawake wengine usiku wa manane halafu ukimuliza anakua mkali alitaka tu kukutumia halafu basi achana nae kabisa muombe mungu utapata mwingine na ikiwezekana badilisha namba ya sim kabisa ili msiwasiliane tena

Anonymous said...

huyo hakufai ni mchafuzi tu achana nae kabisa muombe mungu utapata mwingine

Anonymous said...

huyo hakufai ni mchafuzi tu achana nae kabisa muombe mungu utapata mwingine

Anonymous said...

achana nae mpuuzi huyo asiyejua thamani ya mnwanamke utapata mwingine

Anonymous said...

Mimi naona huyo mwanaume hana mapenzi ya dhati kwako,nadhani baada ya wewe kwenda huko musoma kumfuata ametimiza mahitaji yake yakufanya mapenzi na wewe kisha anataka kuingia mitini,jambo la msingi ukae ukijua kuwa huyo kaka hana tena mapenzi na wewe,pia kama umeshaona yuko bize na wanawake wengine ni wazi kuwa huyo kaka ni play boy,nakushauri uachane nae mapema acje kukua kwa ukimwi..MOM

Barafu said...

Wewe naona bado una mambo ya teenage. Huyo ni playboy flani, na huo ndio mchezo wake. Kwa taarifa yako tu ni kuwa keshawanasa wengi tu kwa mtindo huo, na anaendelea nao. Ni fataki mwenye ubunifu wa hali ya juu. Na kama hukutumia condom siku hiyo, wahi haraka kapime ngoma, zingatia ushauri utakaopata na ujiepushe kabisa na mitego hiyo. Umejifunza, usirudie tena mdogo wangu.

Anonymous said...

Jamani mdogo wangu sijui ni kuambie nini kuhusu hawa wanaume ndotiketi hiyo jamani.japo moyo haukubali piga moyo konde mdogo wangu najua maumivu yake yameshanikuta mimi miezi miwili sasa nilishindwa kula nikashindwa kulala mpaka nyumbani kwao nilikwisha tambulishwaa.ama hakika mwanaume ni rafiki yako kwenye shuka tuu.kwahiyo angalia ustarabu mwingine utakufa kwa preshaa wkt mwenzie anakula

Anonymous said...

dad huyo kaka hana mapenzi na wewe nikwambie ukweli, inawezekana mwanzo alikua akikupenda lkn baada ya kukuona nadhani type anayoitaka sivyo ulivyo dada yangu, hata mimi ilitokea kuna kaka alikuja kazin kwangu long time then tukabadilishana namba, though sikua makini sana kwani hata sura sikuishika, after kama 7 months tukawa tukichat then akaniomba tuwe wapenzi, sikuwa na hiyana lkn siku tulipokutana kweli sikumpenda kabisa yaani sikufeel chochote juu yake lakini ilibidi nimwambie ukweli kuwa sijampenda, alinielewa japo aliumia sana kwani yeye alikuwa kanipenda toka moyoni, sasa huyo jamaa yako anakosea ni bora angekwambia tu mapema kuliko kukuficha. take it easy najua mapenzi yanaumiza sana lkn inabidi ukubaliane na ukweli. pole sana

Anonymous said...

Pole sana mdogo wangu kwa hilo lililokupata, naelewa unavyojisikia, kwani hata mimi nimekutwa na janga kama hilo, hivi nipo kwenye process za kupona majeraha ya moyo kwani nimeona ni bora tu niachane nae na niumie kwa muda kuliko kuendelea kung'ang'ania maumivu ambayo hujui mwisho wake lini.

Wanaume wa dunia ya leo wengi ni waongo, wahuni, hawana huruma kwa sisi wanawake, wanatutumia na kutuumiza kupita maelezo bila kujali.

Nakushauri achana nae usisubiri akutamkie wanaume huwa hawasema kwa maneno bali kwa vitendo, hayo anayokufanyia maana yake ndo hiyo kwamba hakuhitaji tena. Najua sio rahisi kuachana na mtu ambae wewe bado unampenda hata kama ameshakuonyesha kwamba yeye hakuhitaji, na ndo hasa hicho ambacho huwa kinatutesa wanawake wengi kwani hatuko rahisi kuachilia kwa ajili ya upendo

Ukiendelea kusema umfatilie au uvumilie Nakuhakikishia litakalo kuja kukukuta utatamani utafute sumu ufe.

Nakutakia kila la kheri na Jitegemeze kwa Mungu atakupa AMANI NA FURAHA na zaidi atakuletea yule alie muandaa kwa ajili yako

Anonymous said...

pole sana dada kwa yalokukuta the same story happen to me few years ago unajua mmnapokuwa na mawasiliano bila ya kumit unajenga picha ya uyo mtu so mnapokutana na kugundua ni tofauti na vile ulivyofikiria unapoteza muelekeo uyo mwanmme alipokuona na kukuta upo tofauti na alivyokuwa anafikiria alipoteza upendo wake wa kujidai kwako dada think aanza kukubali kuwa he is not that into you na anza kufocus your future apo hapana tena uhusiano kama mlisex think kapime na ucomfarm afya yako epuka mapenzi ya simu or internet

USTAWI WA JAMII said...

pointi ya msingi ni kwamba mlifanya uchaguzi pasi na kuelewa upeande wa pili ukoje sasa basi kitu kilichotokea ni kuwa nduguyo ni mgonjwa wa kuchat na sasa yuko kwenye hit point ya kuchat na mtumwingine huo ndio ukweli hivyo kwasa huna chako hapo. na kwa upande wa mapenzi ni kuwa kiukweli kabisa wewe sio aina ya mwanamke anayo ipenda na ndio maana ukaona yote yaliyo tokea aombi msamaha na aoni kama anakosea hii inamaanisha kwamba hata akikukosa hapotezi.

Anonymous said...

Dada, mimi sitaki kukuumiza zaidi, lakini mbona naona kama umeshajionea vyakutosha. Wewe ukiona dalili za mvua kimbia ukachukue mwavuli maana itamwagika tu. Yaani hana hata ustarabu anakwambia wazi wazi mkate mawasiliano, atakutafuta (yaani inaama akiwa tayari kuona kama bado anakupenda au bado unafaa....ni yeye ataamua kukutafuta?) Hebu jiulize yaani anajali hisia/feelings zako huyo jamani?. Mimi naona wala usiumie, utapata wako tu na ni Mungu atakupa, wala usisononeke maana hawa wa aina hiyo ndio hao hao hata kama mkikamilisha ahadi zenu mkaona mambo yatakuwa mabaya zaidi - dada usije ukafa na gonjwa ukijiona - huyo jamaa bado anataka kusample huku na huko - kimbia!!.

Anonymous said...

Huyo kaka hana mapenzi na wewe, hakutaki, jikaze uendeleee na maisha yako.....akufukuzae hakwambii toka!

Paul Akwilini said...

DADA USHAURI WANGU NI KWAMBA HUYO HAKUPENDI. INAONEKANA ALIIPENDA SAUTI YAKO NYORORO KWENYE CM AKADHANIA NI BONGE LA MREMBO FLANI HIVI. ALIVYOKUONA IKAWA TOFAUTI NA ALIVYOTARAJIA. NAKUSHAURI MFUTE KICHWANI MWAKO KABISA HUKU UKIMUOMBA MUNGU AKULETEE MCHUMBA KUTOKA KWAKE. PIA SIKILIZA NYIMBO NZURI ZA KUKUPA MATUMAINA KAMA WA MSANII CHAMILION-NK.

Anonymous said...

My dia Angel wewe bado mdogo sana ua only 23 u can still find someone who will cherish u! Wanawake tumekuwa na tabia moja siku zote tunatafuta excuse ya yale mabaya ambayo wanaume tunaowapenda wanatufanyia. Ushauri wangu get out of dat relationship mwanaume au hata mwanamke akisema kuwa tuache kuwasiliana kwa muda then ntakutafuta he wants out (meaning hapo alikuwa anakwambia he wants his space)inawezekana kuwa huyo hajaridhishwa with de way u luk en wateva bt dat shudnt bring u down am sure there is a guy out there ambaye will cherish en luv u kwa jinsi ulivyo. So i suggest u moveon en worry not u wil get thru dis wit tym!!!!!

Gise said...

Madam Angel...! ukwl ni kwamba, huyo kaka hakuwa anakupenda hata chembe, yani ni tamaa zake tu ndo zilikuwa zinamfanya akawa anawasiliana na ww sana kabla hamjaonana live, na alipokuona tu basi hakuvutiwa na ww na ndio maana ameamua kukuonyesha kuwa hakutaki, sasa sikia ww ni mwl embu weka hisia zako za kike pembeni na kaza roho msahau na mfute kabisa ktk maisha yako.
Najua ni vigumu lakn embu jitahidi mpendwa manake kunakoelekea ni kubaya zaidi, atakuumiza sana, dalili ya mvua ni mawingu,
my dear watch...! huyo jamaa sio yani,, atakuumiza sana Teacher.

Anonymous said...

dada pole sana. kwa ushauri wangu naomba uanze maisha mengine huyo kaka umtoe moyoni mwako,sina hakika kama umri wako unakurusu kucheza na wakati.inaonesha wazi huyo kaka hana mpango na wewe kuna kitu alikuwa anataka toka kwako na ameshakipata.so....!we jaribu kucheki mtu mwingine atakae kupenda...

Anonymous said...

HAKUPENDI HUYO,HEBU ACHA UJINGA,SHIKILIA KAZI YAKO. NA USHUKURU KUJUA TABIA YAKE MAPEMA,UTAMPATA MWINGINE MWENYE MAPENZI YA KWELI,HUYO NI MBABAISHAJI.

Anonymous said...

Mmhhhhhhh Binti wewe!!!

Umeumizwa na kugalagazwa kwa sababu ya wema wako wa kumrudishia credit jamaa aliyoituma kwako kwa makosa!!

Wema wako umekufanya umekufanya uwe mtumwa wa mapenzi na mtu ulimtendea wema!!

Wema wako na uaminifu wako umekuingiza kwenye mapenzi yasiyo salama.

Uaminifu na wema wako umekukimbiza hadi kumfuata jamaa kule Musoma pasipo kujali usalama wako?

Wema wako ulio adhimu sana miaka hii katika jamii ya sasa unataka kukuingiza kwenye mkenge wa kuambukizwa virusi?Je ulipofika Musoma kweli ulipima kabla hamjaingizana kwenye majamboz na jamaa huyo?Naamini mlifakamiana bila hata kujijali maana ulijipeleka mikononi mwa simba aliyejeruhiwa angekuachaje kukurarua pasopo huruma na uko kwenye kiota chake?Mwenyewe umesimulia kuwa siku mbili ulipofika mambo yalikuwa murua!!! Siku ya tatu uchungu ulianza kuota makeke na ncha kali za misumali.

Uaminifu na wema umeanza kukuliza machozi na kukukosesha raha na hata kuwakosesha wanafunzi wako haki yao kufundishwa kwa umakini na wewe.Jamani binti nakuonea huruma kuwa umechimba shimo ambalo unajitumbukiza mwenyewe.

Kwa upendo na huruma nakushauri usiendelee na mapenzi bubu kama hayo.Umeliwa uroda inatosha kwani ukiendelea naye utanyofolewa jicho ns kukufsnys kipofu kabisa.

nakutakia kila la heri na mwamini Mungu katika maisha yako,msiba wa mapenzi bubu ni mkubwa mno hivyo be careful usipatane na mtu kwenye mitandao na kumfuata mbali kabla hujamjua kwa ukaribu na mahali palipo salama.

Anonymous said...

hapo mbona majibu unayo wewe mwenyewe.Labda mimi nikukumbushe tu hayo majibu: 1. Nikuwa huyo jamaa hana mpango na wewe ila alitaka tu akuvue chupi na aweze kulinganisha Kuma yako na za hao wasichana wengine ambao uliona sms zao, au ubize aliokuwa nao katika simu yake akichat nao. 2. Wewe lengo lako akuoe, yeye lengo lake akutombe tu akuache. 3.Unajua mwanaume akishamtomba mwanamke na kumkojolea shahawa zake basi anamwona huyo mwanamke hana maana, hivyo kwa kuwa wewe ulimvulia chupi, tena hakutumia hata condom, yaani alipima vema Kuma yako, na pengine ndo imejaa maji yaani inakinaisha hata wakati wa kutomba.Wewe si umesema "MNENE KWA UMBO" ni dhahiri una maji mengi ndo maana kakumwaga au huna mvuto. 5. wewe tulia tu hapo shule fundisha ipo siku utampata wa kukuoa dada yangu ila tu nakuomba usifanye tena kosa la kumvulia mwanaume chupi hadi mkapime au tumia kondom, au hadi uone mipango ya ndoa imekamilika. Ninayo mengi ya kukushauri na ujanja wa kutumia kuwapima wanaume ambao kweli wanania ya kuoa au laa, kama hutojali basi unaweza kunikontact kwa e-mail hii: na kisha tukaongea mengi zaidi. Pole sana mdogo wangu, bado ninaimani utampata tu mkweli wa kukuoa, ila huyo achana nae kabisaaaaa! KAZI NJEMA!samahani kama nitakuwa nimekukwaza kwa maneno makali yasiyo na tafsida lakini nilikuwa naelezea hisia zangu, maana hawa wanaume kwa kweli wanatuumiza sana sisi wanawake! am sorry dear.

Anonymous said...

mimi naona mdogo wangu wala usijipati mapresha bure na wewe bado mdogo huyo mwaume hakupendi anashidwa tu kukuambia kwani akufukuzae akuambii toka bado ujachelewa utapata tu wako wakukupenda bado mdogo take care

Anonymous said...

mimi naona huyo mwanaume hakupendi kwani akufukuzae akuambii toka wewe bado mdogo sana usjipatie mapresha kwa mtu asiyekujali tulia umtoe mawazoni kisha uombe mungu akupatie wako wamilele bado ujachelewa kabisa take care man

Anonymous said...

Mpendwa dada yangu kwa ufupi huyo kaka akupendi,kwasababu kwanini akataze usisome msg kwenye cm yake,pili ww mwenyewe umesoma msg ukakuta za wasichana tofauti2,uoni kama huyo kaka si muaminifu?ushauru mm naona achana nae atakusumbua akili yako ushindwe kufanya kazi zako vizuri na kwa ufanisi,muombe mungu akupe wa kupendana nae.kwa kuwa asilimia kubwa ya vijana cku hizi si wa kweli wengi wamekuwa matesta wa mapenzi,

Anonymous said...

Achana na huyo mwanaume ni taperi na hakupendi.Alitumia mbinu hiyo akupate, then akutumie tu. piga moyo konde na msahau kabisa, ipo siku wako wa kweli atapatikana. pole sana.

Salaam.

MiE said...

ivi inakuaje watu mnapanga future kupitia upepo? mie siwezi tongoza dem kwa staili iyo, uyo mchz inaonesha ndo zake izo, package iliuza kuliko contents ndo maana mchz aliboreka baada ya kuufungua, nakushauri kabla hujaumia zaidi fanya uamuzi wa kumwaga...achana na msongo wa mawazo kwamba wanamm wanapenda madem wembamba,kuna maturbo yanachetua mbaya.

Anonymous said...

huna haja ya kuendelea kupenda mahala usipopendwa,utaishia kufa na presha buree.

Anonymous said...

Helo Angel mapresha ya nini sister??mapenzi yalianza tangia enzi za Adam na Eva kutendwa kupo nakutaendelea kuwepo.Ila naomba nikwambie mshukuru mungu kakuepushia kitu kikubwa sana hata kama ulimvulia chupi potelea mbali,je hao wake zake kama ulivyosema uliona sms zao/zake wangekutoa reception si ungeumia zaidi.Ujue mungu kakuandalia mume mwema zidi kuomba ipo siku utaandika kwenye blog hii kuwa"Nakushukuru dada Dina kwa ushauri wako mungu kanipa ubavu wangu"mwisho najua wewe ni mwalimu umri wako bado mdogo ingawa foolish age ulishapita tumia hata elimu uliyo nayo kung'amua mambo mfuate mchangiaji mmoja amekusema sana tena sana lakini mwishowe kakupa bonge la ushauri kuwa you have to select the man whom you know well not through internet /phones.Kaza buti fundisha hao madogo hivi mmeo wa dhati yupo njiani anakuja na utaifurahia ndoa yako hayo yoooooteeee ni mapito dada yangu!!!!!!!!!!

happy said...

Dada pole sana!
Huyo mwanaume hakukupenda ila alikuwa anakutamani tu ss keshakuonja na hakutaki tena.Pia ww ni mtu mzima usikubali kusex na mtu kabla hujamchunguza tabia yake coz ahadi za kwenye simu mara nyingi zinakuwa si za kweli na ukizingatia hamjawahi kuonana kabisa kwa sababu kama angekuwa amekupenda ni wazi kuwa angeendelea kuwa na mapenzi ya dhati na ww.Ninachokushauri tulia muombe Mungu atakupa mwanaume ambaye hatouumiza moyo wako tena.