Thursday, 13 May 2010

Nimegundua Mpenzi alizaa kabla, sina amani-Ushauri

"habari dada dinah na pole kwa kazi ngumu ya kuelimisha jamii, mimi nimekuwa mfatiliaji wa hii blog yako kwa muda mrefu na leo nina swali , Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 21 sijaolewa ila nina mchumba ambae ana malengo mazuri na mimi lakini dada nina tatizo moja.

Mchumba wangu huyu tangu niwe na uhusiano nae ni mwaka umepita sasa, kwa kweli ananipenda na mimi nampenda tena sana tu na ananihudumia kwa kila nitakacho yani kama mke wake. Huwa hanifichi kitu! lakini nimekuja kugudua kuwa yeye ana mtoto mmoja wa kike na ni mkubwa, kwanza alikataa kuniambia kwa kudai ni mapema mno baada ya kumbana akaniambia kweli kuwa anamtoto ambaye alizaa na mwanamke mmoja kabla ya kuwa na uhusiano na mimi.

Alidai kuwa anamuhudumia yule mwanamke sababu wazazi wa yule binti wamembana ahudumie, pia amesema yeye anampenda mtoto tu na sio mama yake kwani hakutaka kuzaa nae ila ilikuwa bahati mbaya!

Sasa dada mimi Moyo wangu umeingia chuki sana baada ya kusikia hivyo lakini mwenyewe anadai anampenda sana mtoto wake kuliko kitu kingine, mimi hapo ndio sielewi je anampenda kuliko mimi?

Dada naomba ushauri, huyu mwanaume nampenda na ndiye anayenisomesha Chuo mpaka sasa na huduma zote ananipa ila tatizo ni chuki iliyoniingia ghafla nashindwa kuelewa ni kwa nini naomba msaada wako! kwani nataka nafsi iwe na amani."

Dinah anasema: Asante sana kwa mail na uwazi wako, Habari ni njema sana tu namshukuru Mungu. Vipi wewe? pole kwa kutokuwa na Amani moyoni. Kuna mchangiaji kafafanua vema kuwa hisia hizo sio chuki bali wivu nami nakubaliana nae kani ni ukweli.


Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke/mwanaume yeyote mwenye mapenzi, unapogundua mpenzi wako anazungumza na Ex wake na siku zote huwa tunawakataza wapenzi wasiwasiliane na Exes.....sasa ndioitakuwa Ex ambae wametengeneza mtoto pamoja kama sehemu ya mapenzi yao....mmh?!! Ni ngumu sana tusichukulie juu-juu tu.

Mchumba wako ni Kaka mwema, ni kweli anakupenda na amedhihirisha hilo kwa kutokuambia mapema kuwa anamtoto ili asikupoteze, muda ulipofika kaweka wazi kila kitu na hata kusema kuwa anahudumia mama mtoto wake. Hii yote inaonyesha kuwa Mchumba wako ni mmoja kati ya wanaume wachache waaminifu, wakweli na wawazi.....Mshukuru Mungu kwa hilo.

Nadhani kinachokuumiza zaidi ni Mchumba wako kumhudumia mama mtoto wake na sio mtoto, kama Mchumba wako hana uhusiano na mwanamke huyo ni wazi hapaswi kumpa huduma yeyote yule mwanamke bali mtoto wake tu.

Mtoto huyo ametengenezwa na watu wawili, yaani yeye na huyo mwanamke hivyo wote kwa pamoja wanatakiwa kukusanya nguvu na kumhudumia mtoto wako sio Mchumba wako kumhudumia mwanamke huyo kwa kisingizio cha mtoto kwani mwanamke huyo hamhusu kwa sasa.


Wazazi wa yule Binti wanachokifanya sio haki na kisheria hakitambuliki, Mchumba wako anatakiwa kuhudumia mtoto wake tu na si vinginevyo. Ukipenda unaweza kuongea na Mchumba wako sasa au kusubiri mpaka mtakapo funga ndoa wewe na mume wako (waakati huo) itabidi mjipange na kwenda kuonana na wanasheria wanaojihusisha na masuala ya watoto na familia (zamani walikwa pale Mnazi mmoja) huko watampa ushauri na nyaraka zinazoelezea haki yake kwenye maisha ya mtoto wake na sio mama wa mtoto huyo.


Alafu mchumba wakoa naweza kuwakilisha ishu hiyo Mahakamani (Mahakama ya Wilaya na omba kuonana na Hakimu moja kwa moja, Hawana matatizo kabisa) na ajieleze huku akiwakilisha yote aliyopewa kule kwenye kitengo cha Sheria kinachojihusiaha na maswala ya watoto na familia ili wazazi na huyo mama mtoto waambiwe kuwa kisheria Baba mtoto (mchumba wako) anatakiwa kuhudumia mtoto wake tu na kwanini, pia Hakimu atasema wazi ni kiasi gani kitatolewa na baba kwa mwezi kwa ajili ya mtoto.


Ni kweli anapenda mtoto wake na upendo huo ni tofauti na alionao kwako, mtoto wake ni damu yake hawezi kuikimbia unless otherwise DNA test iseme vinginevyo. Wewe ni mpenzi wake na anakupenda sana tu pia anampenda mwanae kuliko kitu chochote....hiyo haina maana kuliko wewe.

Mchumba hajui namna gani ya kuwakilisha maelezo kwako ili kukuhakikishia kuwa anakupenda zaidi ya mtu yeyote hapa Duniani lakini pia anampenda mtoto wake kuliko kitu chochote hapa Duniani. Katika hali halisi hawezi kulinganisha upendo wake kwako na kwa mtoto wake kwani ni hisia za upendo za aina mbili tofauti ndani ya moyo wake.

Kama kweli unampenda huyo jamaa na unakwenda kufunga nae ndoa inakubidi ukubali mzigo alionao, kwa maana kubali kuwa kuna mtoto aliezaliwa kabla wewe hujamjua Jamaa na hivyo mtoto huyo ni sehemu ya familia yenu.

Waswahili wanasema ukipenda Boga penda na ua lake, lakini wanasahau kuwa upendo haulazimishwi. Unaweza ukapenda lakini usipendwe hivyo suala muhimu ni kuchukulia mambo kama yalivyo na kujengeana heshima ili kuishi kwa amani.


Huitaji kumpenda wala kumchukia mtoto huyo bali mchukulie kama ambavyo utamchukulia mtoto yeyote utakaekutana nae, hakuna haja ya kujilazimisha au kujipendekeza ili uwe kama "mama yake" kwani kwamwe huwezi kuwa mama yake, hakikisha Mchumba wako hamlazimishi mtoto huyo kukuita wewe "mama" akuite atakavyo yeye as long as hakutukani...MF anawezakukuita jina lako au Antie, lakini ikitokea mtoto kajisikia kukuita mama that will be fine.


Mthamini kama mtoto wa Mchumba wako, mpe ushirikiano wako kila atakapohitaji bila kuwa na hisia zozote mbaya juu ya mama yake as long as Mchumba wako anaweka kila kitu wazi kama anavyofnaya sasa, hakikisha anaendelea kukushirikisha kila anapofanya mawasiliano na mama mtoto wake huyo.

Kamwe tena ni marufuku kumwambia mchumba wako kuwa ni vema mtoto ahamie kwenu kwani siku zote mtoto wa kike anapenda kuwa na mama yake, kitendo cha kumtenganisha na mama yake hata kama ni kwa nia njema bado mtoto anaweza kukichukulia vinginevyo na hivyo mtoto huyo kuathirika.

Ni vema mtoto akaamua mwenyewe kuja kukaa nanyi moja kwa moja au kukaa kwa muda mfupi kila baada ya miezi kadhaa n.k. ili kujenga uhusiano mzuri na pia kupata nafasi ya kufahamiana.

Nini cha kufanya: Kwa vile mchumba wako kaweka kila kitu wazi, unachotakiwa kufanya ni kuacha kuhoji kuhusu upendo wake kwa mtoto wake au hata kujilinganisha kwa kusema kuwa "najua unampenda mtoto wako kuliko mimi", badala yake anapomzungumzia mtoto mpe ushirikiano na ikiwezekana ushauri wa kujenga na sio kubomoa ikitokea kaomba ushauri kutoka kwako. Hiyo Mosi.

Pili, Ondoa shaka juu ya uhusiano wa mchumba wako na mtoto wake, chukulia uhusiano wake huo na mtoto wake ni mfano mzuri kwako kujua yeye ni baba wa namna gani na atawapenda vipi watoto wako mara baada ya kufungandoa.

Tatu, hakikisha unaulizia mtoto mara kwa mara ili kujua anaendeleaje hii itampunguzia mzigo na itampa furaha akijua kuwa wewe pia unajali kuhusu mwanae.

Nne, zingatia masomo yako ili ufanye vema kwenye mitihani yako ambayo ni ndio msingi wa maisha yako ya baadae kama mwanamke anaejitegemea.

Ni matumini yangu kuwa maelezo ya wachangiaji na haya yangu yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuelewa zaidi njisi ya kukabiliana na wivu ulionao kati yako na mama mtoto wa Mchumba wako.

Nakutakia kilala kheri kwenye Masomo yako, Uchumba wenu na maisha yenu ya baadae kama mke na mume.

30 comments:

Anonymous said...

pole sana kwa kugundua kuwa mpenzi wako ana mtoto...ila naomba nikwambie mapenzi mchumba wako aliyonayo kwako na aliyonayo kwa mtoto wake ni tofauti sana hayafananishwi na hivyo sio sahihi wewe kusema kuwa anampenda mtoto wake kuliko wewe...jiamini mrembo acha kugombania mapenzi na mtoto.pia kama kweli unampenda huyo mpenzi wako basi mpende na mwanae afterall it happened before you why do you hate him?people make mistakes in life and he is only human.lakini kwa jinsi mail yako ilivyo nahisi hutaweza kukaa kwa mapenzi na huyo mtoto kwa upendo kama itatokea mkafunga ndoa so kuliko ukamtese mtoto wa watu bora utafute mwanaume asiye na mtoto.pia omba mungu akusaidie uondokane na roho hiyo ya chuki kwani mapenzi ya kweli overcomes such things easily.pole sana

Anonymous said...

we mdada hicho ni kitendawili! japo mtoto alizaliwa kabla ya uhusiano wenu lakini mara nyingi sana watu huwa awaachanagi,tena ukizingatia bado anatoa matumizi kwa huyo dada aliezaa nae, ni wazi kuwa wanamawasilianio na baya zaidi uezi jua kama wanakumbushiana.hapo fata moyo wako wanaume waliozaa nje wengi wana matatizo sana na huyo binti anaependwa kuliko kitu chochote siku ukiolewa uletewe umlee ndo utaona rangi zote

USTAWI WA JAMII said...

kitu imekuingia sio chuki sema ni wivu ulionao juu ya huyo jamaa kwani ulikuwa napicha nyingine kichwani mwako juu yake hivyo kwa namna moja au nyingine ameyaparaganyisha matarajio na mipango juu yenu. cha kufanya kaa tulia jipange upya na ikubali hali na usisahau kumpenda mtoto wa mwenzio kama mwanao kwani ni njia pekee itakoyo mfanya mshikaji aongeze mapenzi kwako. NARUDIA TENA sahau, jipange upya na kuwa karibu sana na mumeo na huyo mtoto then utanipa majibu. maana iko hivi "UKITAKA KUISHI KWA AMANI KUWA KARIBU NA MTU UNAYE MCHUKIA"

Anonymous said...

Ohaaaaaa, binti pole sana, mimi nampongeza huyo mwanaume kwa kuwa wzi kwako mapema kabisaaa kabla hajakuoa, hii inakupatia nafasi ya wewe kufanya uamuzi sahihi kabisa ama kuendelea naye ama kuachana naye. Ila naona kama sula la yeye kuwa na mtoto limekuumiza sana sana, sasa nakwambiaje sikiliza roho yako, ikiwa suala hilo limekupa kichefuchefu amua moja, chapa lapa, manake kama huwezi kumpenda mwanae sasa huwezi kumpenda milele, na kama bado anahudumia mtoto huko aliko na mama yake, kwa taarifa yako mavi ya kale hayanuki, hawezi kumhudumia mtoto aache kumhudumia mama hasa kama yule mama hajaolewa na bwana mwingine, akili unazo za kukutosha, ukipewa akili na mtu mwingine, ongezea na za kwako. Mbayuwayu!

mamasudi said...

habari wanablog wote.

kwakweli dada umenisikitisha sana baada ya kusema huna amani baada ya kugundua mpenzio ana mtoto!!!!

kama kweli unamapenzi naye unatakiwa umpende na huyo mtoto wake kwani ulimkuta naye. na anavyosema anampenda mtoto wake sio kwamba hakupendi ila ni anakutaadharisha mapema uelewe kuwa anampenda mtoto wake nawe umpende.

kama unataka kujua kweli huyo mwanaume anakupenda onyesha kama unamjali huyo mtoto wake lakini ukionyesha haumpendi naye anaweza akabadili mawazo. hakuna mtu asiyempenda mtoto wake hivyo jitahidi uwe na mapenzi kwa wote. UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE. Ingawa alichelewa kukuambia msamehe na muendeleze penzi lenu kama mnapendana.

Anonymous said...

Soma shule wewe usiwe mjinga hivyo!!!

Kama anakutimizia matumizi na kukulipia ada unalalama nini na ameishakuambia kuwa ana mtoto??

Mbona jambo dogo hilo kimbembe cha nini na una habari yote na yeye amekiri?

Wewe unadhani mtu anazaa na mtu halafu waachane hivi kirahisi bila kuongelea mambo mengi ya mtoto.Iwe isiwe lazima hao wakutane ingawa kweli jamaa ana upendo na wewe ndo maana anakugharimia mambo yote hayo.

Usilalamike kijinga hivyo, sasa unataka amwache mtoto asimhudumie?

Wewe komalia shule na ongeza love kwa jamaa ili uweke wigo wa kutosha kumzingira jamaa siyo kulalama.

Anonymous said...

Ndio anampenda kuliko ww,utaki ampende mtoto wake alafu nani ampende,hata ungekuwa ww lazima ungemuweka mtoto wako kwanza then ndio afuate mwanaume best,hapo unatakiwa uchague ila usitake aache kumpenda mtoto wake itakuwa umeharibu sana,na ukitaka ufanikiwe na ww umpende huyo mtoto bidada,asante

Anonymous said...

Sasa dada yangu wewe unataka amchukie mwanae? ila mimi naona huyo kaka anakupenda sana ndio maana akaamua kukuendeleza kielimu ingekuwa hakupendi asingeamua kukusomesha,hilo lakusema kwanini hakusema kwaanzia mwanzo miminaona aliogopa urafikiwenu utaingia dosari sasa wewe usijali hilo bali pia uchunguze km hawashirikiani na huyo mzazi mwezake kimapenzi maana maradhi ni mengi siku hizi

Anonymous said...

huyo mwaume anakupenda sana ndio maana anakusomesha ingekuwa hakupendi asingeangaika nawewe mbona asimsomeshe huyo mzazi mwenza? huoni kwamba anakupenda wewe usijali hiyo ya kutokuarifu km ana mtt labda alikuwa anaogapa ukijua usiano wenu utaisha.Ilachunguza km bado niwapenzi maana maradhi ni mengi siku hizi.

claire said...

mimi kwanza nakupa pole kwa mshituko uliopata lakini kitu nachokwambia kuwa huyo mwanaume wako ni mtu mzuri ndio mana kakubali kuwa ana mtoto , angekuwa hakupendi angekuficha , na suala la mwamaume kuwa na mtoto siku izi ni kitu cha kawaida na haliusiani na mapenzi yenu kama mnaelewana . hapo cha msingi wala usibabaike na wala kuwa na wasiwasi kuwa huyo mwanaume anakudanganya , aaah wapi ?

kingine ni kwamba tena wala usijaribu hata siku moja kumuuliza eti kati yako na mtoto wake nani anampenda ? skia nkwambie mdogo wangu , upendo wa yeye na mtoto na wewe na yeye ni vitu vwili tofauti sawa ? so wewe una nafasi yako kama mwanamke wake na mtoto ana nafasi yake sawa mama , umenipata ?

wewec cha kufanya ni kumpenda tu zaidi na pia huna budi kumpenda mtomto wake pia , si unajua ukipenda boga upende na maua yakke ?

na kumrekebisha pale anapokosea pia kama anakitu kingine ambacho ukijui mwambie akueleze kwani mambo ya kufichana fichana yamepitwa na wakati siku izi !hayo ndo mapenzi sawa !

tena ujitahidi kumzoea pia mtoto umchukulie kama mwanao pia , akiona humnyanyapai mtoto wake basi hilo dume litakupenda zaidi na zaidi , but ukuleta mdomo mdomo wa kumtenga mtoto hapo ndoa utaisikia kwenye bomba la mvua tu kwani mwanaume ataona kama humpendi mtoto kwa wakati huu je ukuingia kwenye nyumba si mtoto atakuwa anashindia mkong'oto ? ataogopa mwenzangu !

ila usishingwe tu kumchimbia mkwara japo wa kiutani utani kuwa unaomba huyo mtoto awe ni yeye tu asije akazalisha mtoto mwingine tena yani kaba mpaka Penalt !

NB: MWANAUME KUWA NA MTOTO SIKU IZI NI KITU CHA KAWAIDA KAMA AMEZALIWA KABLA YA UHUSIANO , WANAITWAGA WATOTO WA MAJARIBIO !

MI NAAMINI ANAKUENDA HUYO BWANA !

Anonymous said...

swala la bahati mbaya kwa kuzaa kabla ya ndoa ni kitu cha kawaida na wengi aliooa au kuolewa utakuta mmoja alishazaa. kwa hiyo ni vema ukamuelewa kama alivyokueleza kuwa ilikuwa ni bahati mbaya.

swala la wewe kuumia kwa kuambiwa kwamba mpenzi wako anampenda sana mtoto wake, hilo naona ungeliacha kwani mtoto ananafasi yake na wewe unanafasi yako.

la msingi baada ya kuona, mchukueni mtoto iwapo mtabarikiwa kuzaa watoto wengine wakue wote katika nyumba moja na umpende kama mtoto uliyemtoa tumboni mwako.

Kinyume na hivyo wewe mwenyewe unayomaamuzi ya kusuka au kunyoa.

Anonymous said...

bora huyo uliyemkuta tayari kazaa na amekuambia ilikuwa bahari mbaya, kuliko uolewe na mtu ambaye hakuzaa, baadaye anakuletea katoto ka miezi 6 wakati firt born wako ana miaka 10.

Anonymous said...

Hi dada

Pole kwa yalikukuta ila acha roho ya kwanini kumbuka ya kwamba ww unapata pia msaada kutoka kwake ss chuki ya nn kuwekeana na mtoto wa mwanamke mwenzio na iweje uulize km kweli ww ndio unapendwa zaidi or mtoto na kumbuka ya kwamba mtoto aliemzaa huyo bwana wako ni mtoto qake na ataendelea kumpenda so ipo siku saa dakika anaweza kuja kukumwaga kwa upuuzi wako usio na kichwa wala miguu.

Unachotakiwa kufanya ni kumpenda huyo mtoto km wa kumzaa ww coz ww si ndio msaada mkubwa kwa huyo bwana na anakusomesha na kila kitu so roho ikuume kwanini na kumbuka ya kwamba isingekuwa rahisi kukwambia kipindi ambacho mlianza uhusiano coz wanawake tuna hasira za karibu mno so kama kakwambia ukweli hakuna aja ya kukaa na jaka la moyo ndani ya nafsi coz taka usitake ndio hivyo mtoto yupo na aanhudumiwa km ww na hawezi kuacha damu yake sababu ya kwako ww so be careful coz kuna wenzio wanatafuta nafasi km hiyo hawaipati ngóoooooooooo ktk dunia hii ya ss.

Mie binafsi hapa nilizaa na mume wangu ila tulikuwa atujafunga ndoa nimeolewa mwaka jana july 09 na nimeaa nae aug 06 so nilishawahi kumkuta na msg kwenye simu kuwa mtt kaishiwa pampers na mambo mengine mengi tu na kila nikimuuliza alikuwa ananikatalia kuwa ana mtoto ila hakuna siri chini ya jua kipindi cha vikao ya send off yangu ndio nimekuja jua kuwa kweli ana mtoto coz huyo mwanamke alinipigia simu akaniambia kila kitu huyo aliezaa nae so ingekuwa ww si ungekufa hapo hapo.

Kuwa mvumilivu bado ujaolewa so kuwa mpole mpende mtoto km nafsi yakoooooooooo ili upate kula zaidi kuliko uwe na chuki mtt ana kosa

Anonymous said...

Shosti pole,Hivi huyo mtoto wewe anakuzuia nini?kama ulivyoeleza kwamba huyo kaka anakupa kila kitu unachotaka,japo huyo mtoto yupo.shauriro wenzako wanataka hata wenye watoto watatu lkn hamjali,ndugu yangu ngoja nikudokeze jambo,shika shikamana upate raha zako wenzako wanakesha kwa waganga kutafuta bahati hizo ww unataka kuipiga teke.acha akili ya kitoto sasa ww ili umchanganye vizuri huyo kaka mpende sana huyo mtoto kwasababu ndio mboni ya jicho lake alafu utaninipa majibu,hivyo unavyopewa si vitu fanya hivyo upewe vitu, watu wako wa karibu watajiuliza umeenda kwa mganga yupi?unajua wasichana wengi mnakosea wenyewe alafu baadae mnaenda kuwafaidisha waganga bila mafanikio,mm na utuuzima wangu ningekutana na mtu kama huyo nisinge fanya faulo.

Anonymous said...

Acha utoto,mbona mambo ya kawaida hayo m2 ameshakuambia anakupnda na hana tena mahusiano na huyo,ww unataka nn?...amchukie mtoto wake?..ukipenda boga na ua lake best.

Paul Akwilini said...

POLE SANA DADA. LAKINI UJUE NA WEWE SIKU AKIKUPA MIMBA NA HATIMAYE KUZAA MTOTO, NA WEWE UTAKUWA HUPENDWI BALI MTOTO NDIYE ATAPENDWA. MWOGOPE SANA MCHUMBA ANAEKUAMBIA MANENO KAMA HAYO MAANA HATA HUYO ALIYEZAA NAE ALIKUWA ANAPENDWA NA KUPENDA KAMA WEWE. KWA USHAURI WANGU HUYO HAWEZI KUWA MUMEO HATA SIKU MOJA NA USIJARIBU KUINGIA NAE KWENYE NDOA. SIKU NAWE UKIZALISHWA, ATATAFUTA MWINGINE NA WEWE UTAWEKWA KANDO KAMA HUYO ALIYEKUTANGULIA.

Anonymous said...

Dada nakushauri kwa kuwa ameshaliweka wazi hilo kwanza mpende huyo mtoto kama unavyompenda baba yake yan huyo mchumbako.Na ikibidi ongea nae mkishaungana kindoa mchukue huyo mtoto ili mawasiliano kati ya huyo mchumbako na huyo mzazi mwenzie yatapungua.Nahis tatizo ni hiyo huduma atoayo na mawasiliano na huyo mwanamke aliyezaa nae.

Anonymous said...

POLE SANA NDUGU YANGU, MWANAUME MWENYE MTOTO NJE KWA KWELI INABOA SIKUFICHI NI THROUGH EXPERIENCE, MTOTO WAKE ATAKUSUMBUA KULIKO UNAVYODHANI NA HUYO MWANAMKE ALIYEZAA NAYE NDO ZAIDI, MAANA ATAKUWA NA UCHUNGU WA KUTAMANI ANGEOLEWA YEYE, UTAISHI MAISHA MAGUMU.MIMI SINA CHOICE SABABU NIMEJUA WAKATI NIMESHAOLEWA LAKINI NILIJIAPIZAGA SITAKI OLEWA NA MTU MWENYE MTOTO NJE, BUT ALIKUWA HAJANIAMBIA, MAUMIVU YAKE YASIKIE KWENYE BOMBA.AT LEAST HAUJAINGIA KATIKA KIFUNGO CHA MAISHA MAKE UP YOUR MIND, NDOA NI MILELE, USIJE KUFA KWA PRESURE NA SONONEKO LA MOYO KWA HASIRA, KUROGANA NA MAGOMVI YASIYOKWISHA WHILE U HAVE OPPORTUNITY TO SAVE YOUR SELF FROM THIS. KUWA MAMA WA KAMBO SI MCHEZO, MIMI INGAWA NIMEMWAMBIA SITAKI KUKAA NA HUYO MTOTO SABABU HAUKUNIAMBIA NA ALIJUA ANGENIAMBIA NISINGEKUBALI KUOLEWA NAE, SITAKI KUWA MAMA WA KAMBO. MAANA NINAJIJUA SIWEZI MAANA NINA HASIRA SIWEZI LEA MTOTOT WA MTU HALAFU LAWAMA KILA LEO, UNAJIKUTA UNAPATA UGONJWA WA MOYO.KISA?

Anonymous said...

Sasa hivi mnapendana sana unaweza ukasema hamna shida ananipenda ,na ameshakuambia anampenda sana mwanae na anamhudumia mpaka na mama yake,ina maana hilo ni jukumu la milele, ukishaolewa miaka 2/3/5 mapenzi yakianza kulega maana ipo hiyo, ndo utajua maharage si mboga ni kiungo cha makande ,huyo mtotot wa kambo na mama yake watakavyokuumiza moyo wako.ukisema mtoto ukae nae ili mumeo asiende huko kwa mzazi mwenzie uhakikishe huyo mtoto unamlea kama malaika ili mama yake asimuharibu na yenyewe ni subjective anaweza huyo mtoto asikupende, maana lazima ampende mama yake kuliko wewe.ukisema mtoto abaki na mama yake, mumeo ataenda kumuangalia mwanae walau mara moja kwa wiki hasa wikiendi ambapo unatamani ubaki nae mumeo atakwambia anaenda kumuona mtoto, hapo ndo penye shuguli, kule akienda anamtega, na anaweza akamtia mimba tena hii imeshatokea kwa wengi.ukisema uende nae kumuona mtoto huyo mwanamke anaweza akasema hakutaki ukanyage kwake.yaani jamani maumivu ya mtotot wa nje msikiege tu yanawakuta watu, it is terible, kama una uwezo wa kuepuka mama,please do that wakati una opportunity

Anonymous said...

mtoto wa nje kabla yandoa afadhali u can think twice but usiombee mtotot wa nje ndani ya ndoa, maumivu yake hayabebeki. but mwisho wa siku mtoto wa nje, lakini tutafanyaje na wanawake siku hizi wanajibebesha mimba bila kuolewa kila kukicha, na hao wanaume waliowapa mimba ndo hawawataki wanasema sio wife material, wanakufuata wewe, na walivyo wabaya wanakusubiri ufall in love,ndo mtu anakuambia ana mtoto ,inauma sana. pole sna but u still have chance ya kumake ddecision, whatever decision ujue mtotto wa nje ni kero, ni msalaba, u will carry it all your life.

Anonymous said...

wanaowaharibu hao watoto wa nje ni mama zao, afadhali uoewe ukute watoto ambao mama yao kafa, ukiwapenda vizuri watakupenda na kukuheshimu,nadhani wanawake tuliozaa nje na hatukuhatika kuolewa na hao waliotuma mimba, tusiwatwike mzigo hao waliolewa na wazazi wenzetu, hasira za kupigwa buti ukamuachi mwanamke wa watu aliyeolewa, na kumtumia mwanao kumkosesha raha mwanamke mwenzio, kama una hasira haukuolewa na aliyekupa mimba, please deal with it, ullitakiwa kabla haujafanya mapenzi bila kinga utafakari na hilo pia. any way my dear, pole sna kama umeanza kusikia chuki ghafl kwa huyo mwanaume sabau ana mtoto nje, take that as a relief and start a fresh, if u can

Anonymous said...

Jitaidi kuondoa iyo chuki uliyonayo coz mtoto hanamakosa yeyote pia alizaliwa kabla ya uhusiano wenu kama mchumba'ko amekuomba msamaha kwa kukuficha huna budi kumsamehe na kumpenda mtoto kama wa kwako ila kama anaendelea na huyo mwanamke alozaa naye hapo ndo shuhuri.Pia inaonyesha huyo mwanaume anakupenda manake anakusomesha ata kukuoa bado! unatakiwa ushukuru kwa ilo. Hayo mawazo yako ya kikatili juu ya mtoto futa kabisa mdogo wangu coz mchumbako akigundua anatakuona umfai

Anonymous said...

embu acha wivu wa kishamba je akiiacha huduma kwako utajisikiaje,halafu unaonyesha una roho mbaya san,kumbuka siku zote damu nzito kuliko maji.
hapo ajakuoa chuki hivyo akikuoa si ndo utawatimua ndugu zake kama mbwa wakija kumsalimia.
punguza chuki na wivu usio na maana hela zake we unazitolea macho si vizuri hivyo dadaangu

Anonymous said...

Kutokana na maelezo yako, huyu mwanaume anakupenda, anakuheshimu na anakuthamini. Kupata mtoto ni baraka, ninamsifu kwa kumjali mtoto wake, inaelekea ilikuwa vigumu kwake kukueleza mwanzoni kuwa anamtoto hatahivyo amekuwa muwazi kwako.

Lazima uelewe mapenzi anayokupenda huyu mwanaume ni tofauti na mapenzi anayompenda mwanae, pia uelewe wewe na mwanae ni watu wa muhimu sana katika maisha yake. Kama kweli unapanga future na huyu mwaume inabidi umsupport katika malezi ya mtoto, support yako inaweza kuwa kumsaidia kuchagua vifaa vya mtoto, ana plan gani juu ya malezi ya mtoto n.k.

Fikiria ni watoto wangapi wanaozaliwa nje ya ndoa ambao hawapati malezi na wanaishia kuwa watoto wa mtaani? Ukiwa na kisirani utampa huyu mwanaume wakati mgumu sana.

Anonymous said...

samahani ila we dada una roho mbaya, utakuja jua dhamani ya mtoto utakapozaa au utakapokua unamtafuta.
mimi nikiwa na umri kama wako nilikua na bf niliempenda kuliko hata uhai wangu ila nikajua ana msichana amempa mimba na alikua mkubwa kuliko mimi,niliumia ila nilisamehe.just imagine angekua kampa mimba akiwa na wewe tayari si ungekufa wewe!
nachotaka kukushauri ni kuwa muelewa,coz hata wewe unaweza kuja pata mimba na uachwe then akatokea mwanaume akupende,walah asipompenda mwanao waweza kufa kwa kihoro.
mapenzi si uchawi,ukitaka penzi lishamiri we waweza kuwa mganga wako mwenyewe, mpende huyo mtoto,mjali kama mwanao,mpende huyo mwanaume wako,na kuwa mwema.

Anonymous said...

Kama roho yako haina amani achana naye, mana kama unakaa naye vile unamtumia kipesa trust me hun it will come to hunt you. Ila kama un anampenda kwa dhati basi huna budi kuukubali umama wa kambo, kwani sio watoto wote wa kambo wakoforofi. Unacho takiwa ufungue moyo wako na umpokee huyo mtoto bila kuwa na ile roho huyu ni mtoto wa kambo lazima jeuri na nitamwonyesha. Muhimu give her time to adjust without forcing her to see you are not bad mother and you love her. The child and you both need time.

Anonymous said...

Kama anakupenda na wewe unampenda na amekwambia alishaachana na yule mwanamke wewe tatazo lako ni nini?

Inaonekana wewe huna mapenzi kwake ya kutoka moyoni ila inafuata huduma tu! Na kwa uhakika asingekuwa na uwezo (kiuchumi) usingempenda!

Unataka amchukie mtoto wake? Damu ni nzito kuliko maji au hujui!!!! Kwa taarifa yako ni kweli anampenda kuliko wewe! Kwani bado hamjaoana na bado hujaanza kuitwa mkewe so think very careful before you open that mounth of yours!

Mie naona hata ukiolewa utampataabu mateso huyo mtoto ambaye hana makosa au utasubiri umalize chuo na upate kazi na useme 'kwaheri siitaji tena huduma yako'

Mhh, dunia hii!

Anonymous said...

mhh pole ila one thing uelewage kabisaaaaaaaaaa, mtoto na baba yake bwana usije ingilia. mapenzi anayo feel kwako ni tofauti na anayo feel kwa mwanae, na raha zaidi ni kuwa mapenzi ya baba kwa mtoto hayapotei kamwe, hata mtoto abehave vibaya gani - unconditional love... ila kwa mahusiano ya mapenzi kama ujuavyo leo ivi kesho vile..so never ever compare yourself na mtoto that is teh cardinal rule. ila ukitaka mkae kwa amani mpende mtoto kama wako na muombe Mungu akusaidie juu ya hilo la sivyo ukijiona huwezi then we sahau pia ndoa kwa mwanaume yeyote yule.

kwanini nasema hivi, coz leo wamkataa mtoto wa boyfriend, haya mkaachana. kesho ukapata mume mzuriiiiiiiii, ya dunia mengi dada, akateleza kidogoooooooo akapata mtoto nje ya ndoa, haya niambie utavunja ndoa?

utawakimbia wangapi? jifunze kusihi na hii hali ya uncertainity.... sishabikii waume za watu kuzaa nje ya ndoa hapana ila this is what happens most times. tena waume wengine huzaa hata na wanawake watatu / wawili tofauti huku ana ndoa yake. so my dia, sikushauri umwache, ukimbie etc. mi nakushauri umuombe Mungu akupe moyo wa kukabili mambo tofauti yaliyo na challenge kwenye relationship yoyote ile utakayo kuwa nayo.

Mama Trina - GPM

eva said...

Mleta mada kwa kweli inabidi ujihoji kabisa nafsi yako kama uko tayari kupambana na misukosuko. Watoto tunawapenda lakini siku ukigeukwa mama utapata presha. Mie mwenyewe yamenikuta nikampokea akiwa na miaka 13 katoka kijijini kwa bibi mzaa mamaye mazingira magumu ile mbaya. Nimemlea kwa upendo bila ubaguzi, nimemsomesha mpaka chuo lakini alivyokujanibadilikia kwa kweli namwachia mungu. Mawasiliano ni yeye na mama mzazi huko alikoolewa, mei dharau. Kwa hiyo mamy kama unampenda mchumba wako jitahidi kumpenda hata mtoto wake, akija kubadilika, basi umwachie mungu.

Anonymous said...

pole sana. mimi swali langu ni dogo tu kwako, kwani huyo mchumba wako kuwa na mtoto kunakuadhiri nini? je ingekuwa wewe ndo mwenye mtoto ungemchukia mwanao? tafadhali kaa tafakari na kubaliana na yote mungu ndo anayetoa watoto uwezi kujua huyo uliyenayo ndo akaja kukusaidia huko mbeleni au usipate mtoto mwingine zaidi ya huyo. Kaa chini mwombe mungu sana akusamehe maana hujui unalolofanya na kuwaza dhambi.