Friday, 2 July 2010

Ex ananirudisha nyuma kihisia, nami nataka ndoa-Ushauri

"Dada Dinah na wasomaji wote, Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22, nina mchumba wangu tunapendana sana na hivi karibuni tunatarajia kuoana.

Tatizo langu kubwa ni hivi, kabla ya huyu mchumba wangu nilikuwa na boyfriend ambaye nae mwanzo tulipendana sana ikaja kutokea hitilafu katika mapenzi yetu kwani alikuwa na mahusiano na mwanafunzi nje ya uhusiano wetu. Kabla ya kuchukua uamuzi nilijaribu kukaa nae nikamweleza ni jinsi gani naumia juu ya tabia yake aliyoianza.

Ilionyesha kuwa alinielewa na tukaendelea na mapenzi yetu kama kawaida, baada ya muda tena nikaja kuona sms ya yule yule mwanafunzi aliekuwa akitembea nae akimtaka aende kwake, kwakweli nilishindwa kuvumilia.

Nikaongea na Dada zake kwani yeye hana baba wala mama hao dada zake na kaka zake ndio walezi wake, japo kua mama yake mzazi amefariki hivi karibuni akiwa ananitambua kama mkwe wake mtarajiwa.

Dada zake walikaa Ex wangu na kuongea nae kwa kirefu zaidi, akawa kama ameelewa lakini baada ya mda mfupi mambo yakawa yale yale, basi dada zake wakaniambia kua wamejaribu kumuonya lakini hawaoni msimamo wake ni upi! Basi nikajitahidi kwenda nae hivyo hivyo, baadae nikachoka nikaamua kumwacha aendelee na mambo yake.

Sasa huyu Mchumba wangu ambaye nimeamini kuwa ananipenda labda aje abadilike hapo baadae nami nampenda pia lakini kila nikikutana nae njiani yule Ex ananiambia kua anaomba turudiane kwani amejifunza na amejua umuhimu wangu.

Anadai kila mwanamke atakae mpata anakuwa nae siku chache tu baada ya kugundua kua anamwanaume mwingine, na mimi nashindwa kumsahau kabisa na kila nimwonapo huyu Ex mwili wangu wote unasisimka.

Sijajua nifanye nini ili niweze kumsahau kabisa japokuwa alinitenda lakini nahisi kama kuna hisia zimebaki, naombeni ushauri wenu wadau japo kua najua wengine wataniponda hilo sinto jali zaidi nahitaji ushauri ili nijue njia ya kumsahau huyo Ex ili niweze kufunga ndoa kwa amani na Mchumba wangu wa sasa.

Asanteni
Mwanablog"

Dinah anasema: Hey asante sana kwa mail yako. Kutokana na maelezo yako inaelekea kuwa wewe umeingia kwenye uhusiano mpya muda mfupi tu baada ya kuachana na Ex wako hali inayosababishwa wewe kushindwa kuelewa hisia zako.

Ikiwa tayari umechumbiwa na mwanaume unaempenda na yeye anakupenda kwanini upoteze muda na huyo mwanaume ambae anakuja kwako kwa vile tu kila mwanamke anaekua nae anakuwa sijui na nini? Mwanaume anakuja kwako na kutaka mrudiane kwa vile anakupenda sio kwa vile wanawake wengine anaokua nao wanakuwa na tatizo fulani!!! hii ni sababu tosha ya wewe kuhama mtaa kabisa achilia mbali kubadili njia ili usikutane nae.

Nini cha kufanya ili umsahau Ex: Kama inawezekana basi hamisha makazi, ikiwa haiwezekani basi tafuta namna ya kumkwepa kama ulivyofanya mara tu baada ya kuachana. Hilo Mosi.

Pili, hakikisha unapotoka unakuwa na mchumba wako au mtu yeyote anaejua uchumba wenu kwa sababu za "kiusalama" kwamba jamaa likikuona na mtu mwingine halitopata nafasi ya kuongea nawe kuhusiana na hisia za kale.

Tatu, epuka kukaa mwenyewe kwani kunaweza kukufanya uanze kukumbuka yaliyopita, hakikisha akili yako inafanya kazi kila wakati kwa kufikiria mambo mengine muhimu kama vile kazi/masomo, maisha yako ya baadae na nini ungependa kufanya baada ya kuolewa, mipango ya ndoa yenu, aina gani ya gauni, rangi, ukumbi, wageni n.k.

Nne, jitahidi kuzungumza na mpenzi wako kwa njia ya simu kila siku kabla hujalala hii itasaidia kutokuwaza Ex, ukizungumza nampenzi wak kuhusu hisia zenu za kimapenzi na jinsi mnavyopendana ndio yatakayotawala akili yako mpaka utakapo pitiwa na usingizi.

Nakutakia kila la kheri kwenye kumsahau Ex na hatimae kufunga ndoa namchumba wako.

13 comments:

Anonymous said...

Move on we dada, ukikosea stepu ujue utakosa yote. There is nothing there btn you two but guiltiness and what ifs.Wanasema penzi la zamani halifi ila kidonda ndugu nacho hakiponi vilevile. Alisha kuumiza pamoja na maneno yake matamu ukirudiana naye ndo atakuona mjinga zaidi, kuwa umwemwacha mtu aliyetaka kukuoa umeenda kwake atakunyanyasa mbaka uone moto. Wanaume sio waaminifu ni marachache sana kubadilika.Utaishia kuumizwa tu na kufa na wivu na ghubu kwa tabia chafu atakazo fanya.
Don't look back, move on......

Anonymous said...

,unajua mtaka mawili moja humponyoka dada acha papara>

claire said...

he pole kwa mchanhanyiko uloupata bibi wewe !

skia nkwambie we hebu jifikirie huyo bwana ulienae saivi ni unampenda kiukweli toka moyoni au ulikuwanae tu kwavile ulikuwa single ?

wewe jifikilie tu mwenyewe unataka nini , unamtaka nani ndo ambaye kiukweli kakuingia toka moyoni yani ongea na moyo wako hapo !

unajua nakwambia ivyo kwa sababu wewe ndo muhusika mkuu wa maamuzi yako kwa kuwa hapa tunaweza tukachoooooonga but mwisho wa siku ukweli unao mwenyewe , sawa mama ?

wewe jifikirie ukiwa na huyo bwana wako mpya unakuwa na furaha toka moyoni au unajidanganya tu hapo ?

coz mi naona huyo bwana mpya huyo, hukumpenda , na kama ulimpenda basi kwa kumreplace tu yule wa zamani but si wewe kama wewe amekuingia kumoyo ndo mana unapomuona moyo unakusisimka coz mapenzi kwake yamekujaa tele tena kupita huyo wa sasa , kwa mtazamo wangu .

sasa wewe cha kufanya ni kufuata wapi unataka kwenda , kama wa kwa sasa au wa zamani nani amekubamba .

wewe navokuona una uchu wa ndoa mapema , angalia tu usije ingia kwenye ndoa then ukaja kujutia baadae kwa kuwa huyo aliyekuoa hukumpenda ki ukweli ukweli then ukataka kutoka , itakuwa too late na hakuna atakae kuelewa sawasawa, ndo hapo watakuuliza ulikuwa wapi wakati wa uchumba kufanya haya maamuzi.

skia kama ni kugombana utagombana sana tena sana tu kwani hakuna uhusiano ambao hapa duniani wakaishi bila kugombana .

NB: USIJE UKAINGIA KWA NDOA BILA MAPENZI KWANI UTALIA BILA KUPIGWA UKAJIONA MTUMWA KAMA SI MFUNGWA KABISA !

SO SEMA NA MOYO WAKO UNAMTAKA NANI ?

T CHAO !

Anonymous said...

Mambo yako mwanablog mwenzetu

Mie kwa ushauri jaribu kumsahau hakuna kinachoshindikana coz kumbuka km kumuonya ulimuonya na hata ndugu zake walimuonya na akusikia ss leo iweje aone umuhimu wako wakati hapo mwanzo ulikuwa unamwambia abadilike na hakutaka??

Jarib kufikiria maudhi yake ya hapo mwanzo mpaka mlipoachana kweli unataka kidonda cha moto wakati maumivu umeshajiwezea yanakwisha my dear.Kama umeshapata mwingine achana nae coz una company ingine ya mtu mnaependana haihusu ukitana na huyo ex wako huko njiani.

Mie binafsi yalinikuta na niliweza kuyamudu dada hakuna kinachoshindikana chini ya jua tuliweza kuacha kunyonya maziwa ya mama yetu sembuse kuja achana na mwanaume tena sio mchumba hawara tu,kuwa na msimamo mpende akupendae asiekupenda achana nae mwache na hao wanafunzi wake.

Frm Mama chuu

Gise said...

We dada ww, Wanaume hawabadiliki hata cku moja, yani mkia wa fisi haumbanduki fisi hata siku moja, angalia usijiharibie bure kwa huyo machumba wako, huyo ex ni mchafuzi tu na atazidi kukuumiza walah nakwambia, weka hisia zako za kujifanya unamkumbuka pembeni forget abt him endelea na maisha, kila la heri

Paul Akwilini said...

DADA ENDELEA NA HUYO MCHAMBA WAKO MPYA ACHANA NA WA ZAMANI. HUYO WA ZAMANI ANAKUONEA WIVU KWA VILE UMEPATA MWINGINE NA HUWA ANAWASHWA AKIKUONA NA HUYO MPYA KWA MAANA ANAWAZA JINSI MTU MWINGINE ANAVYOKUMEGA. UKIAMWACHA HUYO MPYA SHAURI ZAKO.

ANGEL said...

unajua tatizo letu wanawake hatuna msimamo ndio maana hata huyu mwanaume anakusumbua akijua kua wewe ni dhaifu unaweza ukarudia matapishi
hebu tujitahidini kua na msimamo .huyo hawezi badilika na sio kwamba anaachana na wanawake kwavile wana wanaume wengine ila yeye ndio kicheche sasa anaona angalau wewe ulikmvumilia ,usifanye makosa ya kurudia matapishi .nitakupa ushuhuda mmoja mimi nilikua na mpenzi ambaye tulidumu kwa muda wa mwaka mmoja alikua kurya na mimi ni mpare ikatokea kua kaka zake wawili walioa wanawake ambao sio kurya wote wakaacha sasa wazazi wake waka mwambia asije akaoa kabila lingine yani aoe kurya. nilimpenda sana ila sharti moja lilikua no sex before marriage kwahiyo kwakipindi chote hatuku sex ,alipo ambiwa hivyo hakuniambia akawa ananitafutia mtego iliani nase nikisha mpa tu aniache ,nilikua na msimamo sana hakufanikiwa na baada ya muda akaniambia ukweli kua wazazi wake wame mwambia asije kuoa mke ambaye sio kurya ,niliumia sana lakini nilijipa moyo kwavile hakuni tomba .nikaachana naye nikamuona kama kaka yangu ,hadi leo nimesha olewa nina mtoto lakini hakomi kunitaka nimpe aonje angalau siku moja lakini sinahuo mpango .namuona kama wanaume wengine wala siwezi kumpenda tena muda wake umepita .wanaume ni ving'ang'anizi kua makini

Anonymous said...

oh pole sana we dada.Just follow ur heart,usifuate ushauri ambao hawatakuwepo kutest reality ya maisha yako.
Mimi najua kama kweli mtu unamfill mpaka unasisimka tis true he has invested in part of ur brain.Waweza jilazimisha kuwa mbali nae lakini y? just listern ur heart,sometimes ni kuchananyikiwa tuuu.
Anyway,wewe ndo unaeweza kupima kwa 7bu hata huyo mpya(mchuchu) si kwamba ni malaika kuwa ukiwa nae upo paradiso ambako hakuna mkosaji,take time to weigh na uone vipi na huyu mme2b yupoje ukute ndo kicheche dada angu ila hujamjua tu. Kumbuka usemi huu "all men are polygamists" sijui kama kuna kuna research ilipruvu hii but ni suala la kupeana ujuzi tu kuwa haipendezi na kama vigezo vyako vipo kuwa anakufill kweli atakuthamini tuu. Usije uza cow kununua goat. Kila la kheri kwenye iyoo dillema,hope utakuja na conclusion ya ukweli. Lastly,STEP IN DA NAME OF LUV!
J
J

Anonymous said...

CHEATER NI CHEATER TU HATA UFANYEJE?KAMA MTU ALIKUWA CHEATER/SI MWAMNINFU KABLA HAJAKUOA AKIKUOA NI ZAIDI, HAYO MANENO MAZURI ANAYOKUAMBIA SASA NI KWA SABABU ANAKUTAKA KWA SASA BUT MAISHA NI MAREFU KULIKO UNAVYODHANI.HAFAI KABISA HUYO EX WAKO, ILI UMSAHAU WEWE KUMBUKA TU MABAYA ALIYOKUTENDEA, UTASHIKWA NA HASIRA NA UTAMSAHAU. AKIKUOA HUYO EX NDO UTAJUA MAANA YA NYUMBA NDOGO NI NINI, MAUMIVU YAKE NA YANAYOWAPATA WANAWAKE WENZIO HUMU KTK BLOG WAKILALAMIKA KUHUSU NYUMBA NDOGO KTK NDOA ZAO.

Anonymous said...

dada yangu nakushauri badili hata njia anayopita huyo ex
usijekujidanagajya kuwa mwanaume anabadilika
hawabadiliki hata siku moja
huyo mwanaume anakuona unapendwa na unapendeza sana sasa anataka akuharibie
Tangu lini mtu akitapika anarudia matapishi yake?
au huwa mtu akitapika anasafisha na kutupa matapishi yale na kuendelea na kula chakula kingine ili ashibe zaidi
so pia kwenye mapenzi maisha ni kusonga mbele na hakuna kurudi nyuma
hisia zipo na iwapo utaziendekeze unaweza kurudia matapishi, so ondoa hisia zote juu yake na usimpe nafasi huyo ex za kukukaribia
mpe nafasi zaidi huyo mpya na kila unapojisikia hisia na ex mwite huyo mpya
nakutakia furaha njema na mapenzi mema

Anonymous said...

ooh... sema na moyo wako na uendelee na maisha yako. huyo bwana hata kama bado unayo hisia naye basi jitahidi uachane naye. anakuona unafaa ss kwa kuwa si wake tena wkt ulipokuwa wake akuona kiasi gani ww ni muhimu ktk maisha yake. mpe mapenzi mchumba mpya in fully n no turning back!

Anonymous said...

Acha upuuzi huo wewe binti.Hivi ninyi kina dada mna nini??

Inawezekanaje ukarudisha hisia kwa mtu aliyekutenda kivile?Upendo gani huo usiyo na macho wala mawazo maelekevu??

Yaani nimeona vituko vingi humu blogini kwenu mabinti mnalilia mapenzi butu kabisa.Mnalizwa bado mnang'ang'anyia wanaume hao vipi ninyi?

Wewe umepata mtu anayekupenda na uko salama naye na umechumbiwa, eti bado unarudi kuweka mazungumzo na bedui yule aliyekutenda ukatendeka!!Hata kuomba ushauri humu ni kama mnatupotezea muda.Ni afadhali kama usingekuwa na mchumba mwingine ingeleta maana.

Kosa si kosa ukirudia kosa utakosea haswaaaaaaaaaaaaaa.Nani kwakuambia tunarudia kuyala matapishi tuliyotapika? Ukila hali yako itakuwa mbaya kuliko hata ulivyokuwa mwanzo.Chunga sana.

Achana naye wala usirudie tena kuweka maongezi na mtu huyo na ujue unamwibia huyo mchumba wako na akibaini utajuta kuzaliwa.Mkamata mbili yote humponyoka.

Anonymous said...

mwanaume hata sikumoja habadiliki kama aliweza kukucheat mwanzo basi hata kama ukirudiana nae lazima atakucheat jitaidi umpende huyu mchumba wako wa sasa cz m sure anakupenda sana achana na ex wako kabisa