Sunday, 25 April 2010

Ushuhuda!!

"Habari Dinah,
Mimi ni yule mwanamke niliyetuma ujumbe kuhusu msg tata niliyotumiwa na mwanamke kuhusu mume wangu na namna mume wangu alivyomisbihave. Nashukuru Mungu kwani ile siku nilichanganyikiwa sana lakini zifuatazo ni step nilizopitia nataka na wanablog wengine wa D’HICIOUS wasome nao ikitokea wana shida kama mimi wafanyeje.Pia nashukuru wachangiaji wengi kwa comments zao nyingi zikielekeza vizuri . Mtarejea maelezo yangu ile siku, mchana nilimtumia msg mume wangu nikamwambia majibu aliyonijibu asubuhi na mwenendo wake ni dhahiri kuwa anamwanamke mwingine na nikamwambia kuwa kama hatajirekebisha na kutulia na familia yake Mungu wa mbinguni atakwenda kumpa adhabu hapa hapa duniani.Huwezi amini alituma msg ya kushuka na kuniomba kabla sijarudi home tukutane mahali tulivu tuongee. Akanambia kuwa yeye hana uhusiano na mwanamke mwingine isipokuwa anaomba msamaha kwa yale aliyosema akidai aliropoka kwa vile mie nilimfokea na kumwambia lazima kuna kitu anaficha.Anasema hakupenda ile tabia na ndio ikamuipress aseme vile, tukarekebisha tofauti zetu na amezidisha mapenzi zaidi ya yale ya mwanzo. Anawahi kurudi kama kawaida, muda mwingi tunazungumzia mipango ya maendeleo yetu.Namshukuru Mungu kwani nilikuwa nimeanza kufikiria kuondoka zangu maana maneno yale yalikuwa mazito.

Ushauri: Ndoa inahitaji uvumilivu, kuna mambo yanarekebishika, unaweza kuamua kudivorce kumbe ilitokea bahati mbaya. Tuvumilieni. Nawashukuru sana kwa mawazo yenu."

2 comments:

Paul Akwilini said...

hongera dada kwa kuweza kuongea na mwenzako na kumaliza tofauti zenu. maana kwa mwanamke mwingine asingeweza kwenda hata kumsikiliza mume wake badala yake ungeweza kudhani labla angekudanganya zaidi,lkn sivyo. mume wako mpe hongera na bado anaipenda ndoa yake. pia ushuhuda wako ni ushauri kwa wale wote waliopo kwenye ndoa na wale ambao hawapo kwenye ndoa, siku wakikutana na masahibu kama hayo wasije wakapanik na kujikuta wanavunja mahusiano. wajue kwamba ndoa inahitaji uvumilivu mkubwa tena sana na sio rahisi kama wanavyofikiria. mungu awabariki.

Anonymous said...

Dada Mungu akubariki ,nawewe ongeza upendo mara dufu kwa mumeo,usimkatishe tamaa kabisa.Hivyo alivyoanza nawewe koleza kabisa.Ninaimani ndoa yenu itaendelea kuimarika zaidi na zaidi.