Tuesday, 20 April 2010

Uongozi wa Dini umenaharibu, je niendelee kumsubiri?

"Hi Dinah!
Naitwa a.k.a Doctor nikiwa hapa Dar. Nina mpenzi ambae anasoma Chuo kimoja hapa nchini, mwanzoni tulipendana sana hadi ikafikia tukapanga tuoane atakapomaliza masomo yake mwaka 2012.

Lakini alipoanza tu Chuo 2009, wiki mbili zikapita akakata mawasiliano ghafla! Nimeonana naye tena mwezi uliopita baada ya kurudi kutoka Chuo na akasema anataka uhusiano wetu uishe kwani anataka kusoma na amechaguliwa kuwa kiongozi kwenye kikundi cha Dini.

Hivyo anahitaji muda mwingi wa kufanya shughuli hizo. Kwa kweli simwelewi kabisa huyu binti, maana siku nyingine ukimpigia simu ili kupanga mihadi ya kuonana anakuja vizuri tu, siku nyingine ukimpigia simu ananikatia.

Yaani simwelewi au nimpige chini kabisa, nitafute mrembo mwingine maana nahitaji binti wa kuishi naye ifikapo 2011 au 2012. Naomba maoni ya wadau. Nipo katikati ya bahari na sijui wapi pa kuanzia!!!!!!"

Dinah anasema: Doctor asante kwa ushirikiano wako, kuzungumzia na kukubaliana kuwa siku moja mtafung andoa sio tiketi ya mtu kubaki na wewe, kama kweli uko serious unatakiwa kuchumbia kwa vitendo (jitambulishe kwao nakufuata taratibu zote) nadhani huyu Binti ameamua kuzingatia masomo yake kwanza bila kuchanganya mapenzi na wakati huohuo kaamua kubadili mtindo wa maisha yake na kumtumikia Mungu ktk hali halisi ni jambo jema sana hasa ukilichukulia kwa upande mwingine.

Mf: Badili kabao wewe uwe kaka wa huyo binti, kwambatufanye ni mdogo, hivi angekuwa na mpenzi ambae wewe kama kaka unaona kabisa kuwa "jamaa" ataharibu maisha ya kimasomo ya mdogo wako hata kama atamuoa (which sio guarantee as hajachumbia kwenu)......alafu kwa bahati nzuri mdogo wako huyo wa kike kachaguliwa kwenda Chuoni na ghafla akaamua kuachana na "jamaa" ili azingatie masomo yake Chuoni.....ungejisikiaje kama kaka?!!


Kama nia yako ni kufungandoa mwakani au mwaka unaofuata haimfanyi huyo Binti kutaka kuolewa muda huo pia, lakini kama mlipokuwa pamoja na mkajadili suala la ndoa muda huo na alipojiunga na Chuo/Uongozi wa Dini akaomba uhusiano wenu ufe ni wazi kuwa Imani yake ya Dini kama zilivyo nyingine zote hasikubaliani na mahusiano ya kingono kabla ya Ndoa.

Mimi nadhani ni vema kuheshimu uamuzi wake na kumpa muda ili azingatie masomo yake(huenda atabadili mawazo), usijenge hasira/chuki na ikiwezekana endeleza urafiki na mawasiliano ya mara kwa mara mpaka utakapokutana na mwanamke ambae atakuwa tayari kuolewa na wewe kipindi ulichojipangia bila kuwa na majukumu ya Kimasomo wala Dini.

Kila la kheri.

12 comments:

Anonymous said...

Wewe Acha uzembe huyo Kisha pata Bwana we achana naye anza maisha mapya,

Tafuta mtu wa kuoa oa anza maisha mapya huyo umeshampoteza kabisa nakushauri msahau kitu kizuri ni kwamba kakuambia kabisa kuwa uhusiano wenu ufe sasa bado unataka nini?

Take new life mkuu.

boniphace said...

Bwana Doctor
pamoja na kuwa hujaeleza vizuri uhusiano wenu ni wa muda gani, na mmekuwa close kwa vipi, au hiyo plan ya 2012 ilianzishwa na nani hasa, wewe au yeye. Lakini kwa uzoefu wangu na hao viumbe, it seems obvious to me kwamba hapo umeliwa brother.
Amesema anataka uhusiano wenu UISHE, hilo hakika ndilo lengo lake, lakini sababu si ya kweli. Uongozi wa dini unatumika kama kinga tu ya kukuweka mbali na kutoonyesha udhaifu wake hata akuache, ni watu wangapi viongozi wa dini lakini wana familia na wanaparticipate vema kwenye masuala ya kijamii? Na ninyi mlikuwa na "vision" njema kabisa, ya kufunga ndoa, hivyo si kwamba hamkuwa na nyuma wala mbele. Kama angekuwa na mpango wa kweli na wewe, dini isingeweza kuwatenganisha. Niko convinced kwamba amepata mtu mwingine, na si hivyo tu bali hakuwa na mapenzi ya dhati kwako, maana kwa tabia za wenzetu, kama angekuwa anakupenda hasa lakini ameshawishika kwingine, angeweza kuanzisha uhusiano mwingine huku yuko nawe.
Kwa ufupi nashauri ujaribu kumsahau na kuganga mengine. Warembo wapo wengi, ingawa mapenzi ya kweli ni ngumu kuyapata, lakini uvumilivu ni mwanzo wa mafanikio. Nahisi kama utaumiza moyo wakati mwenzio amesha-make up mind yake. Kama una vyanzo waweza kuchunguza huko chuo kama mwenendo wake ukoje, ili tu kujihakikishia ninayokwambia, ya kwamba ameshakuwa mwingi wa habari.
Wasalaam,
B

Anonymous said...

hapo kaka ujaelezea vizuri coz atujui ww una elimu gani?na km elimu yenyewe ni ndogo funga kilicho chako hakuna mahusiano hapo ni kupotezeana muda tu.Coz wasichana jamani wakiwa chuo wanabadilika sio sababu ya kuchaguliwa yy kuwa kiongozi wa dini ndio akatishe mahusiano yenu kipo kitu tu jaribu kukaa nae na kumuuliza kulikoni je zile ahadi zetu zote ni hewa or ndoto za alinacha?usipoteze muda wako kwa mtu ambae abebeki kwa shuka wala taulo na wax mmwageeeeeeee chini asubirie hao viongozi wenzie wa dini

Anonymous said...

Please kaka, tulia na umwombe mungu,
usiwe na papara kumpiga chini sio solution. waweza enda pengine ukajuta
mbona ni fahari kama ameamua kumtumikia mungu,?huoni mungu anakupenda? yawezekana mungu anakuhitaji pia wewe kupitia huyo dada. na mungu akawawezesha kuwa na familia nzuri yenye baraka,upendo na amani. fahamu ni vijana wa leo tunaoharibu maadili na kwenda kinyumena mapenzi ya mungu muumba wetu. hivyo yawezekana mungu ameweka hofu juu ya kushirikiana kabla ya agano takatifu la ndoa. please mke mwema mtu hupewa na bwana vivyo hivyo mume pia. kuwa karibu na mungu au kuishi maisha safi ndiyo msingi wa aman, upendo,na baraka kwa sisi wanadamu. omba utapata jibu. asante.

Anonymous said...

Hahahaaaa! Hakika umenipa raha sana unaposema " sijui nimpige chini huyu binti?". Kwa taarifa yako huyo binti ameshakuacha kwenye mataa. ndo maana ukimpigia simu mara nyingine anaikata. ameshapata mjanja huko chuoni, na anapokuambia anakazi nyingi za dini nadhani anajaribu kukueleza kistaarabu kuwa kwake sasa huna nafasi. Nakushauri ndugu yangu kama ulikuwa na mpango wa kuoa anza sasa mapema kutafuta mwingine kwa kumshirikisha Mungu. Teh, teh, tehe.

miram3 said...

Kuna usemi usemao uishipo hapa duniani, unatakiwa kujiandaa pia, kwa maisha ya baadaye. Ndio maana wengine hujitahidi baada ya kazi lazima wafanye ibada, lakini ajabu wengine hukazania upande mmoja tu. Kwa mfano wengi wetu tunajibidilisha na kutafuta maiisha ya kidunia sana kuliko ya baadaye.
Hili kwangu naona ni kasoro, tufanye kotekote, kwani yote ni yetu
Cha ajabu kuna watu hawataki hata KUOA AU KUOLEWA?
Swali langu ni hili je kama wote tungefanya hivyo dunia kungekuwa na watu? Kuna kisa kizuri nilitaka kuwapa, lakini naogopa mtasema nimeanza visa vyangu, nitakiandika kwenye blogi yangu.
Ushauri wangu kwako, mpe muda, shaurianeni kwa mapana, lakini usimlazimishe, najua watu kama hao sio rahisi kubadili nia yao, kwani wameamua kujiandaa kwa maisha ya baadaye! Ila kwa muona wangu mwingine jaribu kuangalia uwezekano mwingine wa kutafuta rafiki wa matilaba yako baada ya muda uliompa kwisha , kwani upendo na ndoa ni nusu ya maisha yetu!

Paul Akwilini said...

sasa si ameshakuambia kwamba mahusiano yenu yaishe? wewe ndo umepigwa chini. mimi nakushauri kwamba tafuta mwingine maana inavyooneka ni kwamba yeye amepata mwingine na hilo la yeye kuwa kiongozi wa kikundi cha dini, haliwezi kuvunja uchumba, mapenzi au uhusiano. kwani kiongozi wa dini hawezi kuwa na mchumba na mwisho wa siku akaolewa au kuoa? labda kama ni padre au sista kwa kanisa katoliki. mwisho pole sana kwa hayo yaliyokupata. labda ni mpango wa mungu na ipo siku atakuja kutoka kwake endelea kuwa mvumilivu huku ukimuomba mungu mweza wa yote.

Anonymous said...

Dada Dinah kazi yako ni nzuri lakini unachelewesha sana kupost comment za wasomaji, unajua haileti raha kuitembelea site alagu unakuta imenuna wiki nzima, Changamka kama huna visa vipya vya kutupendishia kila siku basi achia comment zishuke daily

boniphace said...

Namuunga mkono anonymous contributor aliyegusia kuchelewesha kwa comments kurushwa.

Dina please try to work this out, ni ukweli inaondoa raha kabisa!

Thanks, B.

Anonymous said...

Hili la kuchelewesha comments zetu linatukera wengi tu. Sasa Dada Dina hii blogu inakuwa kubwa tafuta njia au msaada wa kufanya mambo yawe fast fast. Wote tunapenda kusoma blog hii kila baada ya masaa kadhaa lakini saa zingine unakuta mambo hayapostiwa.

Anonymous said...

KUWA KIONGOZI WA DINI CHUONI HAKUMFANYI MTU AWE BUSY KIASI CHA KUSHINDWA KUWA KATIKA MAHUSIANO, KWANI HATA WACHUNGAJI WAKUBWA WALIO BUSY KULIKO MAELEZO KAMA KAKOBE NA WENGINE BADO WANAWEZA KUFANYA VYOTE KWA WAKATI MMOJA KUMTUMIKIA MUNGU NA KULEA NDOA ZAO KWA MAPENZI YA DHATI KABISA.

WAKATI NIKO CHUONI TULIKUWA NA KAKA MMOJA ALIKUWA KIONGOZI MKUU WA UKWATA ALIKUWA BUSY SANA NA MAMBO YA DINI MPAKA TUKAWA TUNAMWITA KAKOBE AU BABA MCHUNGAJI, LAKINI BADO ALIKUWA NA MPENZI WAKE TENA WALIKUWA MFANO MZURI SANA KWA WAPENDANAO NAYE YULE DADA TUKAWA TUNAMWITA MAMA MCHUNGAJI, BAADA YA KUMALIZA CHUO WALIOANA.

SASA HUYO MDADA NI ULIMBUKENI TU NDIO UMEMZUZUA KAFIKA CHUO KAKUTANA NA WATOTO WA MJINI WAJANJA ZAIDI YAKO SO WAMEMPAGAWISHA MPAKA ANAKUONA WEWE HAUNA MAANA, MIMI NAKUSHAURI TU UMSHUKURU MUNGU NDUGU YANGU KAKUEPUSHA MAPEMA NA HILO BALAA KWANI YAONEKANA BINTI ANATABIA YA KUKOSA UAMINIFU NA KUTOKUWA NA MSIMAMO, SASA ANAWEZA KUJA KUKUUMIZA ZAIDI BAADAYE MKIWA KWENYE NDOA TAYARI.

TULIA UTAPATA MWINGINE MZURI ZAIDI NA MWENYE MSIMAMO NA MAPENZI YA DHATI KWAKO, ATAKAYEKUPENDA WEWE KAMA ULIVYO HATA KAMA UNAELIMU YA DARASA LA SABA. UNAJUA KUNA WANAWAKE WENGINE WANAMSIMAMO HATA UMUHONGE TRENI AU NDEGE KATU HUTOBADILI MSIMAMO WAKE. MSAHAU TU HUYO BINTI NDUGU TAFUTA USTAARABU MWINGINE, MABINTI WAZURI WAPO TENA WENGI MNOOO.

Anonymous said...

OHH!!LALAA!!ME NADHANI MSHKAJI SIO MTOTO WA MJINI,UNAJUA ASILIMIA 95 ZA VIBINTI VIFIKAPO CHUO KIKUU HUDATA NA KUPAGAWA KABISA!!
YANI UKIWA NA GIRL FRIEND WAKO SECONDARY AKIINGIA CHUO TU JIANDAE KWA LOLOTE LILE MAANA WALIO WENGI AKIFIKA CHUO TU!!LAZIMA ATAFUTE WAKUMPA GOOD TIME.
ME YAMESHANIFIKA HAYO!!AMKA KAKA AU UMELISHWA LIMBWATA?YANI UMELROGWA KWA MSEMO MWENGINE!!DINI HAIMFANYI MTU AVUNJE UCHUMBA BALI ANGEKUHARAKISHA NDOA!!ANGALIA SAA NYENGINE UNAMPIGIA ANAKUJA AKIWA NA MJANJA WAKE ANAKATA SIMU!!WEWE NI SPEA TYRE SUBIRI AKISHAACHWA UTAMUONA ANAKUJA KWAKO NA KUJIFANYA ANAKUPENDA