Wednesday, 28 April 2010

Unene wa Mikono unanikosesha raha...nitaipunguzaje?

"Habari dada dinah pole na kazi ngumu uliyo nayo ya kuielimisha jamii. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mada zako ila sijawahi kuleta swali leo nimena na mimi nijitokeze kwa swali ili nipate msaada.

Nilikuwa sijajua tatizo langu nilipeleke wapi, nilisoma mada ya mazoezi na nikaona tu tangazo la jinsi ya kupunguza mikono minene kwa wanawake lakini sikuona maelezo ya kutosha ya nini hasa mtu anatakiwa kufanya.

Nilijitahidi sana lakini sikuona, naomba msaada wako wa maelekezo ya kufanya hayo mazoezi ya kupunguza unene wa mikono, kwani ni tatizo linanikosesha raha na ninashindwa hata kuvaa nguo za mikonoo mifupi au wazi kutokana na unene wa mikono yangu.

Mimi bado ni mdogo naomba msaada wako dada dinah, nategemea majibu yatakayo nipa furaha na nakuomba samahani kwa usumbufu."

Dinah anasema: Habari ni njema tu mdogo wangu, hujambo wewe? Asante kwa mail yako, sasa unaposema wewe bado mdogo unamaanisha ni chini ya miaka 21? Ni kweli kuna mazoezi ya kupunguza unene wa mikono kama unene wa mikono hiyo umesababishwa na unene wa sehemu nyingine ya mwili wako.

Mf kama sehemu nyingine ya mwili wako ni nyembamba lakini mikono pekee ndio minene basi utambue kuwa hili ndio umbile lako lakini kama sehemu ningine za mwili wako ni nene kama vile mapaja, kifua, kiuno, makalio n.k. ni wazi kuwa unene wa mikono utapungua ikiwa sehemu nyingine za mwili wako zitapungua yaani mwili wako ukipungua basi na mikono nayo itapumngua kwani ni sehemu ya mwili wako.

Inawezekana kabisa kuwa umeridhika na unene wa sehemu nyingine za mwili wako isipokuwa mikono....kumbuka huwezi kupewa/pata vyote hivyo kama unapenda maeneo mengine yabaki kama yalivyo itakubidi ukubali unene wa mikono yako na kuipenda kama ilivyo.

Kama asili yako (umbile lako) ni juu mkubwa ni wazi mikono yako itakuwa mikubwa tu, lakini bado unaweza kuifanya ipendeze nakuvutia na ukubwa wake sio unene tena kwani ukifanya mazoezi ya kupunguza unene/mafuta ukubwa wa mikono yako utakuwa umejengwa na misuli zaidi ya mafuta.....hivyo basi miko yako itakuwa firm na kujirudi kiasi nahivyo wewe unaona kuwa imepungua.

Ukiniambia umri wako then nitakuelekeza namna ya kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya mikono yako ili kuepuka ukomavu, mana'ke ukifanya mazoezi haya wakati bado mwili wako unabadilika (chini ya miaka 21) ni wazi yatakufanya uonekane mkomavu.

Nasubiri jibu kutoka kwako...
Asante.

5 comments:

Anonymous said...

Kwanza kabisa hujatoa maelezo kamili kuhusu huo unene unakuwaje?

Pili kama ni unene ulioambana na ukubwa wa vidole pia huwezi fanya mazoezi na unene huo ukapungua kwani
unene wa namna hiyo ni ugonjwa mabao unaitaji matibabu ya kitaalamu zaidi

lakini kama ni unene wa mikono usioambana na vidole au miguu then hilo ni suala jingine ambalo utapewa ushauri zaidi namna ya kuupunguza

NB Kama huo unene umeambana na vidole basi nenda hospital kwani hilo ni tatizo la homorne utatibiwa.

Paul Akwilini said...

ina maana umenenepa tu mikono bila sehemu nyingine za mwili kunenepa? kama ndo hivyo basi utakuwa ni ugonjwa. madokta msaidieni.

Anonymous said...

unataka kupunguza mikono kwa sababu gani, mbona wengine tunapenda sana wanawake wenye mikono minene, hasa kama ni laini hivi

Anonymous said...

Mimi nilikuwa naomba utueleze kidogo kuhusu uzito wako (body weight)hii ni kutokana na kama ukifanya mazoezi na kuangalia unachokula matokeo yake mwili mzima utapungua which will include mikono yako, japokuwa kwa wakati mwingine haitafikia kiasi unachotaka basi inabidi uendelee kukazania kufanya mazoezi 'husika' ya sehemu ambazo ni ngumu zaidi kupungua,mfano wengine wanalalamikia makalio/mapaja, au tumbo au kama ulivyosema mikono. Nakutumia link ya kukick start your diet/weight loss

http://www.think-slim.com/2008/04/pierre-dukans-protal-diet/

Anonymous said...

Akafanye pushup tu mikono itakuwa sawa