Thursday, 29 April 2010

Nini jukumu letu kwenye ndoa?, hebu tuwekane sawa!

"Dinah pole na shughuli hizi za kutuelimisha, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Inaonekana ndoa nyingi zina matatizo ya ajabu na sasa Dinah inabidi utoe mada mpya zinazowafanya wanandoa wajue majukumu yao, huenda mwanaume unakuwa hujui kwa nini umeoa tuelekezane hapa tujue majukumu yako na familia yako.

Mke ajue kwa nini ameolewa na amsaidie mume wake kwa kiasi gani maana inaonekana wanawake wakisaidia sana nayo ni tabu pia sasa tuishije katika ndoa zetu ili kupunguza haya matatizo?

Tuongeaje na wapenzi wetu ili tusigongane? pia imeonekana kuwa wanaume wa sasa wana tabia za kununa na hapo inakuwaje? zimekuwapo kasumba kuwa wanawake wakiwa na uwezo kiuchumi ni shida ktk familia lakini mjue kuwa wanawake wengi sasa wana kazi nzuri au sawa na wanaume je tusiwaoe?

Hebu tupeni na uzoefu nyie wanaume wenye wanawake wanaowasaidia sana hapo nyumbani muwe wawazi bila kuweka ile ya uanaume au kuona aibu. Mimi kwa kifupi nimeona wanawake wengi wakiwa msaada mkubwa kwa familia ikiwa baba ana upendo na anamjali mkewe na akiwa mwaminifu hapo matatizo hayapo.

Mie nayashangaa haya matatizo ya ndoa kila siku humu mpaka naona kama ni shida kuoa, nioe mwanamke wa aina gani du!"

Dinah anasema: Shukrani sana kwa kuwakilisha hili suala, hakika hali iliyopo hivi sasa inakatisha tamaa sana. Ndoa zimekuwa zikifungwa kwa kasi ya ajabu na zinavunjika haraka kuliko ilivyokuwa miaka ile ya bibi na babu zetu, mama na baba zetu. Watu wengi wamepoteza imani na baadhi hawaheshimu wala kuthamini ndoa.

Matatizo yanayosababisha ndoa nyingi kuvunjika yanatofautiana kwa kiasi kikubwa(nitaelezea jinsi ninavyoenda mbele), vilevile sababu zilizowafanya hao wanandoa kufunga ndoa pia zinatofautiana(nitaelezea jinsi ninayoendelea).

Sababu kuu ya kufunga ndoa ni mapenzi, japokuwa enzi za babu na bibi zetu hali ilikukuwa tofauti kutokana na mtindo wa maisha wakati ule na vilevile mfumo dume, wanawake na wanaume wengi walifunga ndoa bila mapenzi, yaani mapenzi hayakuwa sababu ya wao kutaka kushi pamoja bali Familia zao, umri, kuepuka aibu, kufaidika kiuchumi kutoka familia tajiri, ndoa n.k.

Ndoa hizo zilidumu kwa muda mrefu kwa sababu ya watoto, kuepuka aibu, kuachika ni kama kufukuzwa kazi kwavile enzi zile ndoa ilikuwa kama sehemu ya ajira, kwamba mwanamke kuolewa ni mwisho wa matatizo. Sasa ukiachwa ni wazi kuwa familia "watakufa njaa" na wewe hutoolewa tena kwani jamii ilikuwa inaamini kuoa mwanamke alieachwa ni mkosi.


Kutokana na maisha tunayoishi sasa wengi tunapata nafasi ya kupendana kwanza kabla ya kufunga ndoa, lakini baadhi hufunga ndoa kwa sababu zilizowafanya bibi na babu zetu kufunga ndoa which kwa maisha ya sasa ni sawa na kujipa kifungo/mateso ya maisha kwani ni ngumu sana kuishi na mtu usiempenda maisha yako yote.

Nitakuja kumalizia hili midaz........

12 comments:

Anonymous said...

da we kaka nimekufurahia sn,kweli da dina tunaomba utupe somo kuhusu hii inshu,maana mi mwenyewe nataka kuolewa lkn kila nikiona matatizo ya wanandoa kwakweli naishiwa hamu kabisa ya ndoa yenyewe,maana naona ndo itakuwa yaleyale.tunakutegemea sn da dina kwenye hili.

Anonymous said...

Nakubaliana na sister. lakini ni vizuri zaidi tukipata kujua matatizo ya kila mmoja wetu. hivyo itakuwa tumejifunza practicaly. maana ukipata mhadhara tuu bila ya mifano hai inakuwa hujajifunza kitu lakini kwa kusoma matatizo mbalimbali hapo tunapata hisia kamili. na kuona vipi wenzetu wanavyoweza kusaidia katika matatizo hayo. nionavyo mimi mwendo huu ni mzuri zaidi. lets hear other views

Baba Watoto said...

Asalaam Aleykum Jamiah(Amani ya Bwana iwe kwenu nyote)

Si muongeaji sana lakini ni muumini mkubwa wa FAMILIA(ndoa) huumia sana pale ndoa zinapokuwa na matatizo au zinapovunjika kwani huamini kuwa ndoa ni mustakbar wa mwisho kwa mwanadamu au hata kiumbe chochote kilicho hai. kwani kuvunjika kwa ndoa ni chukizo kubwa wacha kwa wanadamu wenyewe hata kwa muumba aliewaleta hapa duniani kama ambavyo Qur'an au Biblia zinavysema kuwa JAPOKUWA NI HALALI KUACHANA LAKINI CHUKIZO KUBWA MBELE YA MUUMBA.

Asili ya ndoa imeanza mwanzo kwa wazazi wa kwanza ADAM NA HAWA hawa walikuwa na JOB DISCRIPTIONS zao kwa kila mmoja kutokana na majukumu yao ya asili ambayo yalitokana na maumbile yao pasipo kuangalia muuingiliano wa majukumu.

Mfano Baba alikuwa(na ataendelea kuwa)Mtafutaji wa chakula (Lunch-seekers)na mlinzi wa familia wakati Mama alikuwa ( na ataendelea kuwa)mtengenezaji wa nyumba (home-maker)mtunzaji wa Familia.

Majukumu hayo yalidumu na yaliheshimiwa na kila mmojo kwa nafasi yake na kama mmojo alimsaidia mwenzake ilikuwa kwa utashi wake lakini kwa FAIDA YA FAMILIA na kuzidisha MAHABA na MSHIKAMANO(kutulizana) katika familia.
Kutokana na kila mmoja kuwa na majukumu yake kama kuwinda(kuleta mkate wa kila siku)au kulea watoto.
kila mmoja alithamini na kuyaenzi (APPRECIATIONS)majukumu ya mwenzie kama ya kwake pia kila mmoja aliheshimu nafasi ya mwenzi wake kutokana na umuhimu wake katika familia.

Waliweza kuliwazana, kufurahishana na hata kutokuelewana katika mambo mbalimbali lakini walikuwa wepesi kuvumiliana na hasa MWANAMKE kwani kutokana na MAJUKUMU na UZOEFU wake wa kutunza familia( hasa watoto) alikuwa ana uelewa mkubwa katika elimumalezi na ameumbwa hivyo(yuko Humble) huwezi mbadili pamoja na mabadliko ya teknolojia.

Kinacho sumbua kizazi cha sasa (ningependa kukita cha DOT COM)yaani kuanzia miaka ya 60s mpaka leo

Anonymous said...

yaani kweli dinah tuandalie,mi mwenyewe cjaoa ila nikiangalia wadau wanavyolalamika huwa nawaza mara mbili..............

Anonymous said...

Asante mdau kwa kuleta mada..nilishaomba kwa dada dina atupatie huu uwanja maana haya matatizo yaliyomo kwenye ndoa zetu ni balaa,to be honest mm nimeoa na ndoa yangu ina miaka mi5 now,amani hakuna,upendo hakuna basi tu tupo for the sake of our daughter,ukweli ni kuwa wote tunampenda sana mwanetu..niliwahi kukaa chini sana na kufikiria what the hell is the coz for all of these,maana ndoa kwa sisi waislam tumeambiwa ndo unapopatikana utulivu ati,sasa mbona hivi kulikoni? i come to realize jambo kuu moja
"Kuachana na manual tuliyopewa na mwenyezi mungu(maandiko yake)kwa jinsi alivyotutaka tuishi katika huu ulimwengu"...jamani tutake tusitake mungu anatujua vizuri sana ss wanadamu na matakwa yetu kuliko ss tunavyojifahamu nae bila kusita akatuwekea misingi ya kukidhi matakwa yetu lakini katika nyakati hizi hakuna tunachokifata..eti tunajua sana,unaweza kuijua NOKIA kuliko mtengenezaji wake? kwa sasa kwa kweli mungu tumekuwa tukimshilikisha tunapohitaji tu kuuthibitishia umma mafano kwenye kufunga ndoa na misiba lakini on how to find a wife/husband neh,kwenye namna anavyotutaka tuishi kama mke na mme ney..sasa hapo tunategemea nn,maumivu tu. kimsingi kwenye dini yangu kuna sifa za wanawake wa kuolewa na wanaume wa kuoa nazo ni mwanamke(dini yake,mali yake na uzuri wake) uzuri unaozungumziwa hapa ni ule unaoonekana kwa muoaji,amerithika nae? sio ule uzuri wetu wa kupita majukwaani(beauty are on the eyes of the beholder)mwanamke aijue dini yake na si kwa kuwa baba na mama ni waislam na yy ana jina la kiislam basi ana dini la hasha,na kama haijui ni wajibu wa mme kumfundisha mkewe dini,walah mke akijua dini ni utamu nyie jamani...pia sifa za mme(dini yake,uwezo wa kumtunza mke,ukamilifu katika uanaume wake)...sasa hapa mara nyingi tukiangalia ndoa zetu hili la mme na mke kuifahamu dini zao na kuzifata huwa ni chini ya 5%...hapo lazima ndoa iyumbe wadau..kwa kujua kwetu tukajiwekea sifa za waume tunaowataka(outgoing,handsome,rich)..sifa za wake zetu(mlimbwende) nafuu kwa wanaume naweza sema wako kidogo waangalifu(mara nyingi utawasikia sio kila mwanamke ni wa kuoa tu,wengine wa kutoka nao out na kula gud time,even tho thy'r wrong kwa upande mwingine) hutakiwi hata kutoka nao..au akitaka kuoa anaachana na girlfrnd wake wa longtme na kuoa mtu mwingine kabisa huku mkimshangaa mbona hawaendani,upendo ni kitu muhimu sana kwenye ndoa lakini upendo unakujaje? manafanyaje kuufanya usipotee na mkaendelea kupendana milele? hapo ndo inakuja manual ya allah,huu upendo wa kukutana mitaani na kuanza kutamaniana kwanza halafu tunajidanganya tunapendana ndo chanzo cha matatizo(wengi huchanganya upendo na kutamani,love and infatuation). Tukirudi kwenye maandiko dini zetu zote

Anonymous said...

(DINAH HAPA HTML INAGOMA KUPUBLISH SO UTANIUNGIA,COMMENT YA MWANZO ILIISHIA "dini zote mbili" HII NI MWENDELEZO )zinasema mme ampende mkewe na mke amheshimu mmewe,hapo tunaona mme ndio mwenye upendo,yampaswa kumpenda mkewe as a result mke ameumbwa kureturn ule upendo in a special way ambayo wanawake huisi pia wanawapenda wanaume,hii concept ni trick kidogo kwa wadada kuielewa,lakini nafsi ya mwanamke imeumbwa kupenda nafsi inayomtendea mema ndo maana mwanamke humchukia kabisa mwanaume fulani lakini mwanaume kwa upendo(matendo mema atakayokuwa akimtendea bint)humfanya bint taratibu abadili msimamo na ghafla humpenda jamaa aliyekuwa akiapa hamtaki,na hivyo hivyo pindi mwanaume anapokuwa amempenda mke na mke akamuheshimu na kumtii isipokuwa kwa jambo lililoharamishwa upendo wa mme huzidi mara dufu na hapo ndo utulivu unapopatikana ndani ya ndoa,kinyume chake ni haya tunayoyasoma humu kwa dina..so talking thru experience mm baada ya kuona utulivu hamna nilikaa chini na kuliangalia sana nini tatizo na nikagundua sina dini na mke wangu pia,nikamuweka chini bi mkubwa tukaliongea kwa kirefu na kukubaliana kuanza kuisaka elimu ya dini,dini yetu sisi ni mpaka ujifunze ndo utaweza kuitekeleza, tumeanza kuisaka elimu ya dini na alhamdulillah tunajitahidi kuitekeleza na tunaona matunda yake,japo hatujafika lakini njia tumeiona now tuna amani na harufu ya mawada tunaanza kuisikia,lakini wadau tukisema twende tunavyojua sisi wallah tuombee tuwe tumepatia(kama majibu ya kuchagua,waweza patia jibu huku ulikuwa hujui) la hasha ni machungu na kuendelea kuwaonea huruma wanaoingia,na kingine ndugu zangu tuache sana haya mambo ya kuiga kila kitu kutoka ughaibuni,yapo mazuri tuyachukue lakini hebu tuwaangalie hao tunaotaka tuishi kama wao,kila kukicha ni divorce tu,mtu anamiaka 35 kishataliki mara tatu..kuna cha kuiga hapo? naomba niwaachie wadau wengine wachangie

Anonymous said...

wadau in short and clear majukumu ya wana ndoa yako kwenye maandiko ya mwenyezi mungu,tumrejee anasemaje kwenye hayo na tutaona utulivu tulioambiwa unapatikana kwenye ndoa,kamwe tusikae tunasema nampenda ananipenda that's all..ndoa ni zaidi ya hapo,kuna nyakati upendo hutoweka inabidi muwe na msingi mwingine unaowashikilia na kuwawezesha kurudi kwenye msitli msingi huo ni dini na si watoto kama tunavyofanya siku hizi,watoto wanaweza kutufanya tuwe pamoja lakini hakuna utulivu,tumrudie mwenyezi mungu baba wa mbinguni atuambia nini majukumu yetu kwenye ndoa....

Anonymous said...

Mimi binafsi naona,majukumu ya ndoa yanatokana na wanandoa wenyewe watakavyopanga maisha yao yawe,hakuna formular ktk ndoa za siku hizi.
Ingekuwa zamani tungesema,jukumu la mama ni kukaa nyumbani na Baba ni kufanya kazi,sasa hivi mambo ni tofauti mwanamke na mwanamme wote wanachakarika kutafuta riziki ya kila siku wote kwa pamoja.
Familia nyingi zinatofautiana,utakuta mama anafanya kazi lakini Baba ndo anafanya kila kitu,mama pesa yake,aah! kwa raha zake anaamua azifanyie nini,lakini hapo hapo wengine mama ndo anaefanya majukumu yote ya kifamilia.NDO MANA NASEMA HAKUNA JUKUMU MAALUM SIKU HIZI.Labda lile lililowafanya muungane ndo mnaloambiwa msinyimane ni jukumu la kila mmoja.

Anonymous said...

Habari Zenu,
ni swali zuri sana kaka alilo uliza...ingawa sijaolewa ila nayaona around me na kwa kweli bado nazidi kujiweka kwenye bado bado nisubiri kwanza. kwa observation yangu kutokana na environment niishio,kwa kweli naona ndoa zimekuwa adhabu sana. nakaa kwenye flats zenye nyumba thelathini,na bahati nzuri au mbaya nyumba nne tu ndio hatujaoa/kuolewa. ila i'm telling you, yes we have our lonenlyness at times but we are the ones who are happy. haipiti siku mbili jamani, mume wa huyu kamfumania mkewe na smses au simu, au mke kamfumania mume na house girl wa nyumba flani,au mume hana kazi tena mwanamke ndio analisha familia anakua anamchoka mumewe wanaanzana visa vya hapa na pale. nashindwa elewa amani kwenye ndo zetu za siku hizi imekwenda wapi?viapo wanavyokula watu wakiwa wanaoa/kuolewa kwa kila mtu na imani yake, huwa wanaelewa uzito wake?maana yake? au ndio tuseme, we are just human,nobody is perfect? ila if we are, and we know nobody is perfect then why cant we make the imperfect perfect? kila mtu anasahau jukumu lake nadhani because of what is going on around us, a lot of stress, makazini,watoto,majukumu...kwaio mwisho wa siku mtu anakuwa so loaded inside mpaka inapelekea ku affect hata relationship yake. nadhani pia kwa upeo wangu,inafika stage watu wa kenye ndoa hawacommunicate kabisa,wanaishia kuwa room mates sasa. because hamna mtu mwenye time tena na mwenzie coz ya what i have mentioned above. na pia ukiangalia ndoa zetu za siku izi sie vijana za kuji show off ndio kabisaaaa,napenda kuziita"u have attitude,i have attitude. you have money, i got money, you have good brain,so do i" ndoaz...hamna wa kujishusha,hamna wa kumsikiliza mwenzie kila mtu anasauti,anajua zaidi...! nadhani clear communication iwe set kwa kila mtu na partner wake,what do u expect from me and i to you. despite of our busy working life, lets try to put some time for us and also for ourselves (yes, even lovers need a holiday)...fullfill your goals in your marriage and your personal goals too coz sometimes kuto fullfill personal goals nadhani zinapelekea mpaka ku block kuelewa majukumu yetu kwenye ndoa. haya ni mawazo yangu tu,shukria.

Me-Myself & I.

Anonymous said...

Dada dina mimi kwa upande wangu naona uanzishe mdahalo wa hizi mada za ndoa kwasababu kila mtu kwa karne hii ana matatizo yake katika ndoa,kama mm sijapata yale matatizo kama ya wenzangu wananyolalamika. kwahiyo nikisoma hizi email zao naumia sana yaani nachanganyikiwa najaribu kuamishia kama ingekuwa mm ingekuwaje,mm naona uanzishe kipind cha live kama cha oprah na watu wengine wanao fanya hivyo uko majuu,mm nadhani ingesaidia kwa wale ambao wanamatatizo katika ndoa zao.kiukweli mm mume wangu anakipato cha kawaida tu,mwanzo nilikuwa naumia sana kwanini niko na mtu kama huyu mwenye kipato cha chini.nikajaribu kutoka nje ya ndoa lkn sikuwa huru na huyo mwanaume mapenzi yetu yakawa yakificho pesa yenyewe hanipi kwakweli nilijuta niakaona nimetenda dhambi pasipo faida,sasa nimeamua kubaki na mume wangu ananipenda japo hana uwezo nipo huru hata nikienda nae viwanja,japo ukosefu wakipato pia uchangia kukosa hamu ya kutiana,lkn mungu ananisaidia nafurahia mapenzi na nimekaa nae nakumueleza majukumu yake na namshukuru mungu anayatekeleza kwa uwezo wake na mm yakwangu nayatekeleza siku zinaenda tunafurahia ndoa yetu.nina mengi ya kushauri lkn muda wa kuandika sina,anzisha hicho kipindi na mm nitakuwa mshiriki katika hicho kipindi,

N.J

Anonymous said...

mimi nadhani majukumu yote ni ya kushare kwa kizazi hiki kila mtu ana wajibu ktk familia si kwamba kwa sababu wewe ni mwanaume basi huwezi kubadili dipper au huwezi kwenda sokoni na kwakuwa wewe ni woman huwezi kubadili flat tyre so ktk ndo kila mtu ana haja ya kujituma na kingine we need to learn to accomodate each other and communicate more never pile up staff
thanks

Anonymous said...

hii mada ni nzuri sana, kweli ni vizuri tuelimishane, maana me nna mchumba lakini naona ananikatisha tamaa, anaonekana too demanding, anataka hela zote ninazopata nimpe,nimfanyie kazi zote za ndani, nikisema nimechoka au nikichelewa kidogo mfano kupika ataongea mpaka kero,nampenda ananipenda lakini hizo kero zinanitia wasiwasi mpaka nasema, hii itakuwa ndoa au utumwa.ana msemo wake anapenda kuusema kuwa "unitunze"