Thursday, 15 April 2010

Nataka kuacha Mpenzi lakini naonea huruma watoto wangu-Ushauri

"Mambo vipi dada Dinah
Pole na kazi na hongera sana kwa kazi hii ya kutoa ushauri.
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 32 kwa sasa ninaishi na mwanamke ambaye ninae kwa miaka nane sasa na tumebahatika kupata watoto wawili mmoja wa kiume na mmoja wa kike.

Mwanzo wa maisha ki ukweli tulikuwa tunaishi vizuri tu lakini kadri miaka inavyozidi kwenda mambo yamekuwa yanabadilika na tatizo kubwa naweza sema limekuwa sugu, nasema hivyo sababu ni tatizo la muda mrefu na nimejaribu kuliongelea lakini naona hakuna mabadiliko yoyote na hakuna sababu za msingi anazotoa .

Dada Dinah huyu mwanamke swala la kunipa unyumba kiukweli limekuwa ugomvi yaani hataki na hatoi sababu za msingi kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Sasa nimechoka sana na nafikiria mambo mengi sana moja kubwa ni kuachana naye lakini nikifikiria watoto wangu nakosa raha.

Nafikiria katafuta mwanamke wa nje ambaye tutatimiziana hayo mambo hapa pia dada naogopa sana UKIMWI, siku chache zilizopita nilifikiria kupiga punyeto na nilivyofanya hivyo kwa kiasi fulani ilinipunguzia hamu lakini nitaendelea kufanya mapenzi na mkono wangu hadi lini?

Dada naomba ushauri nifanyeje?
Asante
J.M. KURASINI."
Dinah anasema: JM mpendwa asante sana kwa ushirikiano. Sasa kaka yangu umekaa na huyo dada miaka 8 na kakuzalia watoto wawili bado hujatangaza ndoa na inaonyesha huna mpango huo, yeye kama mwanamke hiyo hamu ya kungonoana na wewe kila utakapo ataitoa wapi?

Kama mwanamke hasa wa Kibongo hapo umemharibia maisha, kwanza kazaa watoto wawili (hakuna mwanaume atataka kuoa mwanamke mwenye mzigo), pili amekuwa nje ya "soko" kwa muda mrefu na hivyo itakuwa ngumu sana kwake kujiingiza kwenye masuala ya kimapenzi na mtu mpya.....miaka nane sio mchezo!

Kitu kikubwa ni kuwa umempotezea hali ya kujiamini na inaelekea wazi kabisa wewe huna hisia za kimapenzi nae (kwenye maelezo yako hakuna mahali umegusia kumpenda) tena bali uko nae hapo kwa ajili ya Ngono ambayo sasa huipati na inakufanya utake kutoka nje na watoto. Kinachokuzuia kutoka nje au kumsaliti ni UKIMWI, vinginevyo unekuwa na kimada.

Huyu dada kisheria ni ana haki zote kama Mkeo kwa vile mmeishi pamoja zaidi ya miaka 2, lakini hiyo haitoshi mpaka hatua zote kijamii zitakapofuata na kufunga ndoa kama wanavyofunga wengine.......kama alivyogusia mchangiaji, hicho ni kitu pekee huyu mdada anakitaka kutoka kwako.

Inaelekea alifanya yote ili kukufanya utangaze ndoa lakini hukufanya hivyo, akaamua kushika mimba mara mbili na kufanikiwa kuzaa wewe bado huna habari na ndoa, amendelea kuishi na wewe na sasa ni miaka nane (muda mrefu kuliko wanandoa wengi) lakini wewe ndio kwanza una-demand Ngono badala ya kutafuta tatizo ni nini hasa.

Huyo ni mwanamke, na ndoto ya mwanamke yeyote ni siku moja kufunga ndoa na mwanaume ampendae, huenda kwa wanaume hili ni suala la kijinga lakini kwa mwanamke ndoa ni kitu muhimu sana kwenye maisha yake.

Nini cha kufanya: Rudisha hisia za mapenzi kwenye uhusiano wako (kwani inaonyesha wewe umejisahau na yeye amekata tamaa kama sio kachoka), Muonyeshe huyu mama ni namna gani unampenda, onyesha kuwa bado unavutiwa nae japokuwa amezaa watoto wawili kwani mwanamke anapozaa mara mbili na zaidi mwili wake hubadilika.

Hivyo "Kisaikolojia" anaanza kuamini kuwa havutii tena na vilevile uke wake hauko vile ulivyokuwa awali na hivyo kujishtukia kuwa hatoweza kukuridhisha (anaweza kuwa na aibu pia), sasa kwa vile wewe hujui au hujali unadhani yeye anakunyima lakini ukweli ni kuwa humpi ushirikiano na wala huonyeshi kuwa bado unavutiwa na umbile lake.

Fanya yale yote ambayo ulikuwa ukimfanyia mwanzo wa maisha yenu kama wapenzi, unapohisi kutaka ngono usimuombe kama vile "haki yako" au "jukumu lake" bali itake ngono kwa kuonyesha mapenzi, kwa kumshika nakucheza na mwili wake, jitahidi kumfanya ajisikie kuwa anapendwa.....akielekea endelea lakini akigoma basi usimlazimishe na badala yake muulize kwa upole na upendo tatizo ni nini?

Usilalamike, bali tafuta ukweli kutoka kwake....."kitu gani nakosea mpenzi", " asali wa Moyo kwanini hutaki tufanye mapenzi?"....."naomba uniambie kama nimekosea nijirekebishe".....alafu mmwagie misifa (kulingana na kile unachokipenda na una uhakika anajua kuwa ni kweli).

Jinsi siku zinavyozidi kwenda ongeza kuonyesh amapenzi kisha tangaza ndoa(ndani ya mwezi mmoja), mchumbie mama watoto wako na mfunge ndoa. Nina kuhakikishia utaona mabadiliko na kila kitu kitakuwa sawa mara tu baada ya huyu dada kuwa na uhakika kuwa mnakwenda kufunga ndoa.

Hakikisha unafunga ndoa kiukweli,
Kila la kheri!!

13 comments:

Anonymous said...

Asante dada Dinah kwa kutupa nafasi kusaidiana kimawazo.

Kaka yangu pole sana kwa matatizo katika uhusiano wako na mpenzio.
Unyumba katika ndoa ni matokeo ya mawasiliano mazuri kati ya wapendanao.Jaribu kuongea na mpenzio na kujaribu kupata ufumbuzi wa kiini cha matatizo.Swala la kuachana ni mapema sana.Naamini kama ukimuuliza kwa upendo na kuwa na mazungumzo na mpenzio katika hali ya utulivu utaweza kufahamu kiini cha matatizo na kuweza kupata ufumbuzi wa unyumba.Pia usisahau kumtanguliza Mungu katika yote haya ili akupe hekima na busara ya kutatua matatizo katika uhusiano huu.

Anonymous said...

kaka kosa lako bado hujalijua?????????!!!hata ningekuwa mi ndo huyo mwanamke wako ningefanya ivoivo........umeshamzalisha watoto 2 na bado hutaki kufunga nae ndoa miaka yote hiyyo 8 mnaishi tu kama mahawara....muoe na tatizo litaisha ye hawezi kuwa mjinga tu kila siku kwa kumuweka ndani km kimada..ni hayo tu

Anonymous said...

Pole sana kaka yangu na pia nikupe pongezi kwani wewe ni kati ya wanaume wachache sana wa bongo ambaye unajali wanao na unajali magonjwa ndiomana hujatafuta kimada na unasita kuachana na mkeo hata umediriki kupiga punyeto nawakati una mke pole sana na Hongera kwa uvumilivu na utu ulionao Mungu atakuzidishia.
sasa ushauri wangu kwakweli kaa na mkeo kwa upole kabisa na upendo mweleze jinsi unavyompenda jinsi ulivyofikiria kuachana naye na kutafuta kimada lakini ukashindwa kwaajili ya upondo ulionao kwake na kwa familia wasije pata tabu wanao au kuleta magonjwa mwelezee jinsi gani unateseka bila kufanya mapenzi hadi kudiriki kufanya punyeto
nina hakika ukikaa naye kwa upole na kumwelezea hisia zako zote hizo kama kweli anakupenda atakuelewa.
unajua wanawake wanahitaji kubembelezwa usimwendee kibabe mbembeleze

Anonymous said...

Pole bro,nina tatizo kama lako yani hiyo kitu inatesa sana akili.nimefikia mahali nimejiuliza maswali magumu 1.labda simtii mtu wangu vizuri,jibu nakuta hapana kwasababu ikitokea nikapata nafasi huwa namfikisha kileleni fresh.2.labda anatiwa nje,hili linanipa wasiwasi 3.labda anamatatizo ya kusikia hamu,mbona nikipata nafasi ya kumtia anafika kileleni.kwakweli mpaka sasa hivi nipo kwenye wakati mgumu wa maamuzi nifanye nini,nje kuna uwezekano wa ngoma,kumuacha nafikiria mtoto wangu,kubembelezea mapenzi najisikia kuwa namtongoza upya mke wangu,halafu inapoteza ladha kila siku kuwa unabembeleza halali yako.adhabu mbaya ni hiyo ya kupiga punyeto wakati una mke,mimi imesha nichosha maana inanipotezea kumbukumbu sana.dada dina tusaidie mawazo yako inachanganya sana.

Anonymous said...

Pole bro,nina tatizo kama lako yani hiyo kitu inatesa sana akili.nimefikia mahali nimejiuliza maswali magumu 1.labda simtii mtu wangu vizuri,jibu nakuta hapana kwasababu ikitokea nikapata nafasi huwa namfikisha kileleni fresh.2.labda anatiwa nje,hili linanipa wasiwasi 3.labda anamatatizo ya kusikia hamu,mbona nikipata nafasi ya kumtia anafika kileleni.kwakweli mpaka sasa hivi nipo kwenye wakati mgumu wa maamuzi nifanye nini,nje kuna uwezekano wa ngoma,kumuacha nafikiria mtoto wangu,kubembelezea mapenzi najisikia kuwa namtongoza upya mke wangu,halafu inapoteza ladha kila siku kuwa unabembeleza halali yako.adhabu mbaya ni hiyo ya kupiga punyeto wakati una mke,mimi imesha nichosha maana inanipotezea kumbukumbu sana.dada dina tusaidie mawazo yako inachanganya sana.

Anonymous said...

Brother tafadhali nenda kwa wazazi na uwaeleze ukweli ili huyo mwanamke aeleze chanzo cha kukataa. Lakini kwa sisi waislamu hilo sio tatizo kakuwa unamwambia 2 kama kazi inamshinda akupe ruhusa uwowe mwanamke wa pili ambaye atamsaidia kazi inayoshinda yeye.
He he he he, bro acha ujinga huo wa kutafuta mwanamke wa nje mbona hayo mambo yalishapitwa na wakati, kwanza wa2 wote wenye kufikiri waliachana na hayo mambo tangu cku nyingi labda wajinga 2 ndio bado wanafanya. Kwanza kwenda nje ya ndoa ni Haram Zaburi, tauraat, Injil wal furqan vyote vimekataza jambo hilo, sasa wewe unataka kufanya nini sasa? Ushauri wa bure ni kuwa fuata tartiibu za kutatua tatizo hilo.

Anonymous said...

mdogo wangu ndio ukubwa huo. Mimi nakushauri usimwache mke. Baba na mama wanapokuwa pamoja katika malezi ya watoto basi watoto hao hukua vizuri.
Ushawahi kumwuliza tatizo ni nini? Inawezekana kabisa ana tatizo na kama unavyojua si binadamu wote ni wawazi kabisa masuala ya ndani ya miili yao hata kama wewe ni mume na hutakiwi kufichwa chochote. Pili inawezekana anapata taarifa zako hata kama si za kweli kuwa unarukaruka. Inamwia vigumu sana kukubali kitu cha namna hiyo. Ile hali ya usaliti ndio inayomfanya labda akose hamu ya kukupa unyumba. Inawezekana kabisa anapojaribu katika hali ya mashaka matayarisho ya mwili wake yanakuwa si mazuri na hivyo kupelekea maumivu wakati wa kungonoka.
Keti naye tena mlizungumze na ikishindikana mkutane na watu wazima ili wawasaidie.

Anonymous said...

UNAJUA TATIZO LA WANAWAKE UKIMUONYESHA KUMPENDA TU BASI ATAKUSUMBUA USHAURI NI HUU INGAWA ITAKUGHARIMU ACHANA NAE TAFUTA MWANAMKE ATAKAYEKUTIMIZIA HAJA ZAKO WATOTO UTAWALEA SASA UTAFANYAJE NA RAHA YA KUCHIMB KISIMA UINGIE MWENYEWE

Anonymous said...

Muombe ruhusa ya kuoa mke wa pili kwa kuwa hupati unachohitaji. akikuruhusu basi jua hana mpango na wewe anza kufikiria jinsi ya kulea watoto kwa njia nyingine

Anonymous said...

pole sana ndugu yangu, naomba swala la kuachana nae lifutre kabisa, hakuna ndoa isiyokuwa na matatizo japokuwa yanapishana.

nakuomba kama ujafunga nae ndoa anza kufanya maandalizi sasa na utimize amri ya Mungu, usiendelee kuzini na mwenzio na watoto unamzalisha na yeye anapenda kuingia kanisani bwana, na uhakika atabadilika.

kae nae faragha, ongea nae kwa mapenzi na mbembelezee akuambie tatizo ni nini??

na kama ulikuwa huna utaratibu wa zawadi fanya hivyo sasa, toka nae out, tafuta muda angalau kwa wiki mara 2 toka na familia yako, mwonuyeshe upendo kwa vitendo na uhakika kila kitu kitakwenda sawa

mwisho endelea kuwapenda watoto wako sababu hakuna atakaeweza kuwapa mapenzi anayowapa mama yao HAKUNA, penda familia yako na palipo na upendo na Mungu yuko., nakutakia kila la kheri

Anonymous said...

Wadau,

Mimi namuunga mkono anonymous namba 2, Kaka nadhani hujafahamu nn unachokitafuta katika mapenzi, dada huyu utatest hadi lini? kama uzazi anao nn unachosubiri kumuoa? huenda dada huyu ameona ww unamtumia kama chombo cha kujifurahishia na kukutengenezea viumbe tu. haoni kama hayo ni mapenzi, kama kweli ww unampenda kwann usimuoe??

Nakushauri muoe binti huyo na utaona vitu atakavyokupatia, kwani siku za nyuma alikuwa anakunyima unyumba?? angalia pia penzi litakapohama kwa asilimia 100% kwako akapata mtu mwingine atakayemuonyesha penzi na kumuoa itakugharimu sasa. wanawake huwa haturudi nyuma tukihamisha penzi ooooooohhhhh!

Anonymous said...

napenda kujiunga na mchangiaji mwezangu, ya kwamba amuoe huyo binti kwani si mke wake japo wamekwisha zaa watoto,,,ajaribu kumwambia swala la kufunga ndoa kama atakubali..akikubali anze taribu aone kama atabadilika,,naamini lazima atajiskia furaha na yeye kuwa mke halali wa ndoa hata mbele za mwenyezi MUNGU...

Anonymous said...

pole sana kaka ndiyo maisha, ila vunja ukimya mweleze juu ya hilo kuwa unataka kuoa mke wa pili kwa sababu hakutimizii haja zako. na kama hatosikia tafuta rafiki lkn kabla ya kufanya chochote mwombe mwende mkapime.