Wednesday, 14 April 2010

Nahisi naibiwa, je niamini hisia zangu au?-Ushauri

"HABARI DADA DINAH,
POLE SANA KWA KAZI NZITO YA KUELIMISHA JAMII.
MIMI NI MWANAMKE MWENYE UMRI WA MIAKA 29 ,NINAMPENZI WANGU SASA YAPATA MIAKA MIWILI TANGU TUANZE MAHUSIANO, ILA NINAHISI KAMA VILE YUKO NA MSHICHANA MWINGINE.

HUWA HAPENDI NIENDE KWAKWE AKIDAI KWAMBA ANAHOFIA WADOGO ZAKE ANAOISHI NAO, MARA NYINGI HAPENDI TUWEPAMOJA MFANO WIKIENDI MUDA MWINGI ATASEMA YUKO NA RAFIKI ZAKE.

YAANI NAHISI KUNA JAMBO ANALOLIFICHA NA NAHISI ANAMWANAMKE MWINGINE ZAIDI YANGU, DADA NAOMBA USHAURI JE NIAMINI HISIA ZANGU AU NIFANYE NINI?
MAGDALENA
DAR ES SALAAM"

Dinah anasema: Magdalena mpendwa, dalili ya kwanza kabisa kuwa mtu anakupenda ni kutumia muda wake mwingi na wewe, kutambulishwa kwa ndungu, jamaa na marafiki zake ni dalili ya pili kuwa kafika kwako, kuwa wazi na huru kuwa na wewe au kukuonyesha kwa watu wake wa karibu ni dalili ya tatu, Mpenzi kutokuthamini mtu mwingine yeyote (rafiki zake) bali wewe na kama kuna shughuli/sherehe basi utakuwa wa kwanza kujulishwa na kushirikishwa kabla ya rafiki na jamaa wengine.

Haya yote hufanyika kwenye hatua za mwanzo kabisa za uhusiano wa mtu yeyote, miaka miwili ni mingi sana kwa mtu kuendelea kukufanya wewe "mpenzi wa siri" kwa wadogo zake.

Natambua suala la yeye kukutambulisha au kukupeleka nyumbani ili kuepuka vishawishi kwa wadogo zake hasa kama wako kwenye umri wa kushawishika (kubalehe), wanaweza wakadhani kuwa na girlfriend/boyfried na kumpeleka nyumbani ni kawaida kwa vile kaka anamleta wake hapa.

Lakini vilevile inawezekana anahofia wadogo zake kuuliza kuhusiana na mwanamke mwingine ambae labda wanamfahamu, ili kuondoa utata jamaa inabidi akatae wewe kufahamu nyumbani kwake n.k.

Mpenzi anapokuwa na tabia ambayo wewe unadhani kuwa sio kawaida au hajawahi kuwa nazo kabla hukupa maswali na hofu, vilevile kama unabahati pia unaweza kupata hisia fulani ambazo huwa zinawatokea watu wachache, zinajulikana kama "the sixth sense" inakuwa kama "maono fulani hivi", kama kuna kitu kinatokea behind your back you just know.

Lakini kabla hujakurupuka na kumshutumu mtu kuwa anafanya maovu, unatakiwa kufanya uchunguzi wa karibu ili kuwa na uhakika ili kufanya uamuzi wa maana.

Nini cha kufanya:Punguza ulalamishi kwamba usimuulize wala kulalamika kuhusu tabia yake ya kukukwepa na punguza mawasiliano na huyo Boyfriend wako. Ikiwa unajua mahali anapoishi basi fuatilia kwa karibu ili kujua nini kinaendelea pale nyumbani, je kuna mke(mwanamke mwingine n.k.).

Badilisha mtindo wako wa kimaisha kwa kuwa mwanamke mmoja anaevutia kuliko kawaida, hakikisha unajipenda na kujijali zaidi, vaa mavazi yanayokukaa vema kulingana na umbile lako (usilifiche) ili uvutie zaidi.

Ukiomba kuwa nae mwisho wa wiki na yeye kudai kuwa anakwenda kutumia muda wake na rafiki zake, kuwa calm na muulize kwa upendo ni wapi huko anakoenda? ukijua kona anazopenda kutembelea basi ibuka huko bila yeye kujua, ukifika hapo mahali endelea na starehe zako lakini hakikisha kuwa amekuona.

Baada ya kufanya haya utakundua ukweli na hivyo itakusaidia kufanya uamuzi wa busara ili uweze kuendelea na maisha yako hasa kama kweli ni cheater na pengine kukupa nafasi ya kuweza kukutana na mwanaume atakaejali hisia zako, atakae kuthamini, kukupenda kwa dhati, mwanaume atakae kuweka wewe juu/wa kwanza kabla ya rafiki zake.

Ikiwa umegundua kuwa ni mwanaume mwema lakini hajui namna ya kumpenda mwanamke then itakubidi umfundishe, umuelekeze namna ya kujali na kuthamini mpenzi, kuweka wazi hisia zako na kumwambia ni namna gani unapenda kutumia muda wako mwingi na wewe. Mueleze kuwa hupendezwi na siri na usingependa uhusiano wenu uwe siri, ungependa "Dunia" ijue kuwa ninyi ni wapenzi.....ukianzia na wadogo zake, ndugu, jamaa na marafiki.

Kila la kheri kwenye umauzi utakaoufanya kutokana na matokeo utakayo yapata.

8 comments:

Anonymous said...

mh!jamani,mimi naic kama una data na ma bf!!tuwasiliane kupitia ma email marcolucanna@yahoo.com.plz

Anonymous said...

mimi nahisi unaibiwa kwani kama ana mapenzi ya kweli ni lazima angekutambulisha kwa nduguze na hata hao marafiki anaodai yuko nao kwani kuna ubaya gani hao marafiki zake wakikujua na unatakiwa kuwa makini kwani wanaume wengi ni macheater asije akakupotezea mda.take care

Lisa said...

Shosti na mimi nipo kwenye balaa kama lako, tena afadhali wewe unajua anapokaa, mimi hata hajawahi kunionyesha anapoishi na tuna mwaka sasa, madai yake si vizuri kwenda kumtembelea kwa kuwa anaishi na ndugu zake hawatamuelewa, yeye ndo huja kwangu tu kwa vile mimi naishi peke yangu. Kwa kuwa nampenda nimekubalina na hali hiyo hivyohivyo japo siipendi na huwa inanifanya nihisi kwamba pengine ana mwingine.

Ila najipa moyo kwamba alie wangu ni wangu tu na asie wangu hata akisema anitambulishe kwao kama sikupangiwa hatakuwa.

Kila la kheri nawe

Anonymous said...

Mmmhh....fumbua macho mdogo wangu unaibiwa,huyo shemeji sio mkweli anakudanganya, achana naye asikupotezee muda ila nakushauri kaa peke yako utulize akili utafakari unatoka wapi na unakwenda wapi, mungu atakubariki utampata shemeji mwingine mwenye upendo wa dhati, pia naomba uwe mwangalifu katika kuchagua usije ukaruka majivu ukakanyanga moto, pole kwa yote

Anonymous said...

Siku hizi kila kitu kwa evidence,hayo ni mawazo yako tu.inawezekana yakawa ya kweli au si kweli.wewe fanya uchunguzi wa kutosha,utakapogundua ni kweli basi utaamua kusuka au kunyoa.Ila inavyoelekea huyo hana mapenzi ya kweli kwako,watu wanaopendana hawawekeani mipaka.

Anonymous said...

Pole sana, Mdogo wangu huyu bwana hakufai hata kidogo achana nae, na wala usimwambia chochote wala usimgusie tena kuhusu kwenda kwake wala week end kumwambia mtoke wote kaa kimya. hapo utakuwa unamuweza na ww akikwambia nakuja kwako mwambie leo sipo naenda kwa dada au mtajie sehemu yoyote ile. umuone atasemaje maana huyu ni mshenzi hana lolote atakuwa na mtu tu huyu ana kupotezea muda.

Nakwambia hivyo kwa kuwa mm wakati msichana yalinikuta km yako siku hyo nikamuondolea uvivu nikamwambia wazi, tena km ww ni jasiri mwambie km hutaki nijue unakokaa na wewe usije kwangu.

Hapo ndio utagundua km kweli anakupenda au anakupotezea muda.

Anonymous said...

DADA unaibiwa live!!!!
Mi yamenipata hayo, hakuwahi kunipeleka kwake kwa madai hayohayo kwa miezi nane, nami kwa upuuzi wa kufuata mapenzi nikamwamini si nikawa namshirikisha kwenye madili yangu?
Asiniibie anasubiri nini!!!! milioni 20 za kununulia gari akapotea nazo kwa madai ya kunisaidia kununua na kulitoa bandarini kwa sababu niko busy... inaenda mwezi wa sita huu sijui alipotelea wapi ingawa nshatoa taarifa polisi....

Kimbia fasta dada, usije lia kama ninavyolia!!!!

Anonymous said...

kijana kwanza nitangulize pole sana...huondugu yangu unaojiongopea kua ni utamu wala sio utamu, na hii yote kwa sababu tigo haina kwa kazi hiyo na kutoa utamu bali ina asili ya kutoa mavi tubasi na si jinginelo,sema tu wewe kwa vile ibilisi kakutawalia na akakupambia kwa utamu na wewe ukaingia kichwa kichwa eti ukajifanya wahisi utamu! sio utamu wewe! kwanza hebu muogope mungu wakotena mtake radhi kwa tendo hilo ulokua ushafanya jitahidi utubie na usirudie tena,na tena usijiongopee kumuomba mkeo tigo,usije ukamuingiza ktk ibilisi aliekua kishakuingia wewe,na kama utaona huwezi zaidi kua mende kupenda choo ni bora mkeo ukampata talaka huwenda mungu akampa mume mwema kwani wewe tayari ibilisi kishakuozesha yani umeshaoza labda ubadilike,kwani kuna maradhi mengi yanayopatikana sawa mwanamume au mwanamuke kwa kwenda kinyume na maumbile. hata wewe ni bora umuone doctor akushulikie kabla maradhi hayajakufumukia,kwani baada ya kupata bao ktk tigo kuna vijidudu ambavyovinakua ktk mavi vyarudi ndani ktk ubookwani ule mlija wa uboo hua unatanuka ili shahawa zitoke asa vile unavosinyaa basi unafyonza vijimavi ambavyo wewe hotohisi kitu, kwa hiyo upo hatarini kija na ili kusafisha uo uboo wako waja fanyiwa oparetion na kupasuliwa kama kiazi,isitoshe wewe kwanini wafanya jambo ambalo mola kakemea ktk dini zote nadhani wote twajua sogoma na gomoro waliangamizwa kwa sababu hiyo ya kupenda kumavi,,, nakuonea huruma ndugu yangu lakini usijali muda bado unao maadamu bado wapumua na milango ya rehema bado iwazi yakusubiri wewe ulopotea.
ni mie ndugu yako M.I.MGODOKA.Egy