Nifanyeje? Tuna VVU Binti wa kazi adai Mimba ni ya Mume wangu?

"Hodi wenyewe, mama nanihii upo?’ ilikuwa sauti ya mama mmoja alikuja kuchota maji. Mimi nilikauka kimya, siunajua tena siku ya Jumatatu unatakiwa uwe kazini lakini kwa vile bado nipo kijiweni, sikupenda majirani wajue hili.

Mama watoto alikimbilia nje na kumkaribisha huyu mgeni ambaye hakutaka kuingia ndani zaidi ya kuchota maji na kuondoka. Yule mama alimuuliza mama watoto wangu kama anataka mfanyakazi, niliguna moyoni, nikijua nini jibu atakalopata.‘Kwa hivi sasa sihitaji, inagwaje kweli ni muhimu ningekuwa naye, kwasababu nashindwa kufanya shughuli nyingine au kutoka kwa vile sina mtu wa kumkabidhi majukumu’ mama watoto alimijibu.

‘Sawa, lakini huyo ni mtoto mzuri kitabia, ingawaje hawa watoto wa nyumbani unaweza ukawaamini sana lakini wakafanya jambo ambalo hutazamii. Yaani mimi hapa nilipo natamani duniani inimeze kwa tukio lililotokea kwangu, kisa cha mfanyakazi wa nyumbani’ Huyo mama akaamua kukaa kwenye ngazi za nyumba yangu ili aweze kumhadithia mke wangu.

Nilikuwa dirishani kwahiyo maongezi yao nilikuwa nikiyasikia vizuri, na kwa vile Yule mama hakujua kuwa nipo aliongea kiundani mambo yake, kama unavyowajua akina mama wakiamua kuongelea swala Fulani kwa mtu anayemuamini.‘Ndiye unayetaka kuniletea mama?’ mke wangu aling’aka.

"Hapana sio huyo, huyo wangu namuandaa aende kwao kalikoroga mwenyewe’ Yule mama alisema , na kabla mke wangu hajamuuliza vizuri alianza kuhadithia kisa ambacho kilinifanya nishituke na kuamua kukiweka hapa ili wale wenye nia njema wachangie na huenda iwe fundisho kwa wenye wafanyakazi wa nyumbani.

Binti huyu niliye naye nilimchukua akiwa mdogo, alipomaliza darasa la saba. Tuliishi nae kama binti yetu, na kwa vile alikuwa na adabu , mchapakazi mzuri niliamua kumsomesha Sekondari hadi kidato cha nne. Hakufaulu, lakini tulikuwa na malengo ya kumsomesha zaidi.

Lengo hilo lilikwama kwasababu mume wangu kibarua chake kiliota majani, ikawa mimi ndiye mhudumiaji wa familia. Kama unavyojua kipato changu ni kidogo nisingeweza kumsomesha na kuilisha familia, kwahiyo tukakubaliana kuwa asubiri hadi mume wangu atakapopata kazi.

Siunajua maeneo ya huku kwetu kama unafanyakazi ili uwahi kazini inabidi uondoke saa kumi na moja alifajiri na kurudi nyumbani ni kuanzia saa mbili za usiku. Hili halikuwa tatizo kwasababu mume wangu alikuwa katika mkumbo huo kabla hawajampunguza kazini kwao.

Na pia yupo huyo binti ambaye tulimchukua kama mfanyakazi wa nyumbani na bado tunaendelea kumlipa licha ya kujitolea kumsomesha na kumpa huduma zote kama mtoto wetu. Lakini kama walivyosema wahenga, kuku wa kienyeji hafugiki, na kweli kwa hili sidhani kama nitahitaji mfanyakazi wa nyumbani tena.

Wakati mwingine nawashangaa sana hawa waume zetu, sijui akili zao zikoje. Unajua ninakuhadithia hili sio kwasababu nimjinga wa kutoa siri za mume wangu nje. Hapana, lakini lilotokea inabidi nimhadithie mtu ninayemuamini ili anipe ushauri.

Naujua ushauri nasaha nimeshaupitia, lakini huu sasa ni mkali zaidi. Wiki kama mbili zilizopita nimepata kalikizo kadogo nikaona nishirikiane na familia kujifanyia miradi midogo midogo na hapo ndipo nilipogundua kubwa kuliko.

Mfanyakazi wangu huyu wa nyumbani ni mjamzito nilipomuombana aniambie ni nani aliyempa hiyo Mimba, alikataa katakata, hadi nilipomwambia na mrejesha kwao kijijini ndio akanitajia. (Nitamrejesha kwao ingawaje hataki lakini kwa hali ilivyo sitaweza kusihi naye tena).

Nilishindwa kuamini kuwa Mume wangu ndio mwenye mzigo huo yaani hadi sasa siamini mbaya zaidi nilipomuuliza Mume wangu nae alikataa kakataa kabisa sasa sijui nimuamini nani? hili linawezekana kweli?.

Isingekuwa mimi na mume wangu tumeathirika na VVU ningefungasha virago vyangu ili kumuachia nafasi, manaake kaona simfai mpaka anatembea na Msichana wa kazi, lakini kutokana na tatizo letu tunahitajiana hasa kwenye kumlea mwanetu ambae pia aligunduliwa kuwa ameambukizwa.

Tuliamua kupima baada ya mtoto wetu kuwa anaumwa mara kwa mara, alipopimwa akaonekana ana Virusi vya UKIMWI hivyo na sisi tukalizimika kupima na majibu yakawa hayo kwamba wote tunavyo.

Sio siri kuwa mimi na mume wangu na mtoto tumeathirika, sasa sikutegemea kuwa mwenzangu anaweza kukosa imani na kudiriki kutembea na mfanyakazi wetu ilihali anajua kuwa anamtataizo haya ya kiafya.

Mume mume wangu kakataa katakata na kusema huyu binti kaumua kumpakazia ili asiondoke hapa nyumbani. Je nifanyeje ili kuupata ukweli? Japokuwa namuamini sana mume wangu na tangu tuoane naye hajawahi kunisaliti au kunidanganya. Sasa mimi nachanganyikiwa sijui nishike wapi? Nisaidie ushauri, nifanyeje?" Akamaliza huyo Mgeni mchota maji.


Kwa haraka haraka Mke wangu akamuambia Mgeni wake kuwa afuate Sheria, kwamba amshitaki na huko kwenye vyombo vya Sheria atapata ukweli na ushauri huo ulimfanya Yule mama ainuke na kwa hasira akaaga huku akisema‘Nini?, nimshitaki mume wangu?kwaheri" aliaga mama huyo!

Je ingetokea kuwa huyu mama kaja kwakokutaka ushauri ungemsaidiaje? Ungemshauri vipi?
Asanteni.
M3.

Comments

Anonymous said…
Hatua ya kwanza huyo binti akapimwe kama ana VVU.Mana kama kweli katembea na mumeo lazima litakuwa bayana, haitakuwa vyema kumuondoa huyo binti wa watu kimya kimya bula kujijua kama ana hilo tatizo.Mana huko mbele ya safari atakako kwenda ataendeleza maambukizo ya hatari.Kma huyo mwanamme kafanya ngono na binti mdogo bila kinga huku akijijua tatizo lake kweli si salama na anatakiwa kushitakiwa kabisa.Binafsi ningejua kafanya kitendo hicho ningemshitaki na hata kama unasema wewe una mwamini mume wako VVU viliingiaje ndani ya nyumba yako? Ahitakiwe kabisa huyo bwana na inavyoonekana hayo mahusiano yalianza toka zamani.
Anonymous said…
jambo la msingi angeenda kwanza kumpima huyo binti na kujua hali yake kama ameambukizwa ama laa,kama atakuwa ameambukizwa hapo inabidi sheria ifuate mkondo wake kwani huyo mume atakuwa amefanya jambo la kinyama na anastahili adhabu kwani atakuwa ametenda dhambi kutokana na kuijua hali yake kiafya.jambo la pili huyo mama anapaswa amsaidie huyo binti kwakuwa mimba ameipatuia nyumbani kwake hata kama sio ya mume wake,kumrudisha kijijini atakuwa hajamsaidia bali atakuwa amemuongezea tatizo katika maisha yake,afanye utu amsaidie.
Anonymous said…
MMh! HICHO KISA CHAKUTUNGA, M3 WEWE TU KILA SIKU UNAKUTANA NA VISA. SIJUI MNAOAMINI CHANGIENI.
Anonymous said…
arika! jamani mbona huyo mume kamuua mtoto wa watu jamani!! Mungu atusaidie yaani hii mambo ni full noma, mtu anajijua kaadhirika bt still anasambaza kwa makusudi.
haya hebu mpelekeni huyo mwana wa watu kwa doc kwanza ili mpate uhakika kama nao au la! if so ndo aanze dozi na mapema kumlinda huyo kiumbe alie tumboni.kumrudisha kijijini haitasaidia ilhali haujui hali yake ya kiafya..
she made a mistake kutembea na mumeo bt huyo mumeo ndo wakulaaniwa kabisaa maana yeye anajijua afya yake ni mbivi(mbaya).kuna watu wanaroho za shetani kabisaa na huyo mume ni 1wao. hii ishu imeniumiza sana moyo wangu.. so sad.. poor girl..
lily Ars.
Anonymous said…
Kuna mchangiaji mmoja kasema M3 ni mtoa visa vya kutunga, huenda iakawa hivyo au ni kweli, na wote hapa tunatakiwa kusimamia katika kuelimishana, kuwa kama kitu hicho kimetokea tutasaidiaje!
Visa kama hivyo vipo vingi, tunaviona na tumekutana navyo. Na naungana na wachangiaji wa mwanzzo kuwa ni vyema kwanza huyo binti akapimwa na pia sheria ichukue mkondo wake.
Anonymous said…
eti unamwamini mumeo??

hapana duh! au mmepataje ukimwi siyo kwanjia ya ngono?

kama unamwamini so wewe ndo uliuleta ukimwi ndani ya nyumba?
kama ni hivo usimlaumu mumeo kwani alikuwa anatafuta njia ya kujifariji!

sijui nikushangae au nikuulize swali?

inakuaje mwanamke unakua siyo mwaminifu ndani ya ndoa unatafuta nini huko nje ambacho ndani hukipat?

mama mi naona jilaumu wewe na siyo mumeo maana umesema unamwamini mumeo means kwamba wewe ndo sio mwaminifu.

cha msingi msaidie huyo msichana pamoja na kiumbe kilichopo ndani ya tumbo kwanza kampime na kama kaathirika msaidie huyo mtoto mtarajiwa asiambukizwe
Anonymous said…
mi naona hicho kisa kinakuhusu wewe na wife wako na sio kusema yule mama. mi nakushauli huyu msichana akapimwe virus vya ukimwi.kama akikutwa ameambukizwa. apewe dawa maalum ili kuzuia maambukizi kwa mtoto atakayezaliwa.thatz important. ..sana
Anonymous said…
Kazi kwelikweli, kwa hayo na mengine mengi msikose kumtembelea
M3, kwenye blog yake ya
http://miram3.blogspot.com/
Anonymous said…
uyo baba si mwaminifu.angekua mwaminifu ukimwi umetoka wapi?akashtakiwe uyo.