Wednesday, 24 March 2010

Nahisi Mtumwa ndani ya ndoa yangu!-Ushauri

"MAMBO DADA DINAH,
POLE NA MAJUKUMU YA HAPA NA PALE PALE. NAOMBA SANA MY DIA UNISHAURI MAANA NIKO NJIA PANDA. JAMANI MWENZENU MIE NIMECHOKA SANA NA MAISHA YA KUKWARUZANA NA KUPIGIANA KELELE KILA WAKATI NA MUME WANGU.

MUME WANGU NI MTU ANAEPENDA KULAUMU SANA NA KITU KIDOGO KIKITOKEA KINAKUZWA KINAKUA KIKUBWA HASA, HATA UKIOMBA MSAMAHA HAELEWI. IMAGINE MIMI NAFANYA KAZI ARUSHA NA NINAISHI MOSHI KILA SIKU ANATAKA NIWE NAENDA NA KURUDI KWAVILE NAMPENDA NIKAKUBALI INGAWA NACHOKA SANA.


MARA NYINGI NAFIKA USIKU KWENYE SAA MOJA AU MBILI USIKU NA NINAKUA NIMECHOKA KWELI, WAKATI MWINGINE HATA MUDA WA KUANGALIA MAZINGIRA YA NYUMBANI SINA.

BASI AKIKUTA HATA GLASS ALIOACHA ASUBUHI CHUMBANI ATAONGEA MANENO MENGI SANA MARA OOH "WEE MWANAMKE HUJUI WAJIBU WAKO" UKIMWOMBA MSAMAHA BADO ATANUNUA.

KWA KWELI MIMI SIMUELI, KWA KIFUPI YEYE ALISHAISHI NAWANAWAKE WAWILI TOFAUTI MMOJA KWA MIAKA 4NA MWINGINE KWA MIAKA 10 ANAWATOTO 4 LAKINI WALISHINDANA NA HAWAKUFUNGA NDOA MIMI NDIO NILIEFUNGA NAE NDOA NA TUNAISHI NA MTOTO MMOJA WA KWAKWE.

YAANI HATAKI MTOTO AULIZWE KITU AGOMBESHWE ANAONA KAMA VILE ANAONEWA YAANI MIMI SIJABAHATIKA KUPATA MTOTO NA MUME WANGU HUYU INGAWA NINA MTOTO MMOJA KUTOKA UHUSIANO WANGU WA AWALI.

MATUMIZI NDANI YA NYUMBA KUTOA NI KWA SHIDA SHIDA UKIMWAMBIA AACHE HELA YA CHAKULA MARA ASEME AMESAHAU UKIMPA LIST YA VITU VYA KUNUNUA BADO ATADAI KASAHAU.

ANANICHOSHA KWAKWELI, WAKATI MWINGINE NAAUMUA KUFANYA MWENYEWE TU KUEPUKA KERO HANIHUDUMII CHOCHOTE KAMA MKEWE, NIFANYAJE JAMANI NA HUYU BABA?

MIMI NA MIAKA 29 YEYE ANAMIAKA 42 LAKINI VITUKO NAVYOFANYIWA NAHISI KAMA MTUMWA, MARA AJITENGE NA MWANAE YAANI KILA NALOFANYA ALIONI YEYE NI KULALAMIKA TU.

JAMANI EMBU NIAMBIENI KOSA LANGU NINI NA NIFANYAJE? SAMAHANINI KWA KUWACHOSHA ILA NILITAKA MPATE PICHA HALISI."

Dinah anasema: Mambo ni mazuri tu mdada, namshukuru Mungu. Shukrani kwa ushirikiano wako. Mumeo ni Mbahili/mchoyo, mlalamishi, mkorofi, hana huruma, hakuthamini, mvivu, sio mwelevu, hajali na mbinafsi hizi ni baadhi tu ya tabia ambazo mtu yeyote alie na akili timamu hawezi kuzivumilia.

Yaani unasafiri kutoka Mji mmoja kwenda mwingine kila siku na bado anakusimanga kuwa hujui wajibu wako? Wala sikulaumu kwa kuchoka mdogo wangu.

Huyu mwanaume anasumbuliwa na "mfumo" dume uliochanganyika na hali ya kutokujiamini kwa vile wewe ni mdada unaejitegemea kiuchumi, pia inawezekana ameathirika kisaikolojia kutokana na uhusiano wake na wanawake Mf mama yake, mama wa kambo, bibi, wapenzi wa awali n.k. Hali hiyo ndio iliyomsukuma kukulazimisha wewe kusafiri kila siku kutoka Arusha kwenda Moshi kwa kufanya hivyo anahisi kuwa ana-control juu yako wewe kama mwanamke.


Nijuavyo mimi maisha ya ndoa ya siku hizi ni kusaidiana sio kwa vile tu mwanamke unauwezo wa kiuchumi sawa au zaidi ya mumeo basi ndio iwe sababu ya kuchukua majukumu yote kuanzia ujenzi wa nyumba/kodi mpaka shughuli za nyumbani....ni sawa na kuwa single mama mwenye watoto na mume.

Hakika unampenda mumeo lakini vilevile unamuogopa, kwa sababu hata kama unampenda mtu huwezi kukubali kufanya kitu ambacho unajua wazi kitahatarisha afya na maisha yako, pamoja na kuwa unampenda unatakiwa kujiamini pia kuwa na msimamo na kumpa challenges mumeo sio kila akisema wewe ni "ndio bwana"......"nisamehe mume wangu" hata kama kosa ni lake!


Tabia za mumeo zinaweza kubadilika ikiwa wewe mwenyewe utasimama imara na kutaka mabadiliko, akijua wazi kuwa anayofanya ni makosa na ukampa nafasi ya kujirekebisha atafanya hivyo hasa kama anakupenda na anataka ndoa yenu iendelee. Lakini kabla ya kumtaka abadilike unatakakiwa kujua historia ya maisha yake.


MF; Kama mumeo aliwahi kuishi na mama wa kambo na mama huyo wa kambo kwa namna moja au nyingine alikuwa akimnyanyasa yeye kama mtoto pia mama huyo wa kambo alikuwa akimtawala baba yake (baba mkwe wako) then itakuwa imejiweka wazi kuwa Mumeo anakuwa na tabia hiyo kama sehemu ya kujilinda dhidi ya "mwanamke" kwa kifupi atakuwa ameathirika kisaikolojia.

Na suala la kujitenga na mtoto wake pia linaashiria "maumivu yake ya kisaikolojia" kwa vile wewe sio mama wa mtoto huyo anadhani kuwa utamfanyia vile alivyofanyiwa yeye na mama wa kambo, hivyo chochote utakachokifanya kwa vile tu wewe sio mama mzazi basi inaonekana ni uonevu hata kama unafanya hivyo kumsaidia au kumkanya mtoto.


Nini cha kufanya: Chukua likizo ya uhusiano, nenda kwa wazazi/ndugu ukatulize akili kwa siku mbili-tatu au hata wiki mbili. Utakaporudi utakuwa tayari kujaribu na kuweka mambo sawa ili ndoa yenu iendelee au kuimaliza.

Sasa, kwa vile wewe ni mdogo kwa mumeo (kibongo bongo huna nguvu) itakuwa ngumu kusikilizwa, hivyo jaribu kutumia watu wazima (wazee) unaowafahamu nakuwaamini, itakuwa vema kama watakuwa wale waliowafungisha ndoa.

Hawa watawapa ushauri na kuwapatanisha ninyi kama pea ili muishi kwa amani na upendo kiimani zaidi na sio kivitendo kwa maana kuwa maelezo yao hayatomfanya mumeo kubadilika kwa vitendo lakini itatoa nafasi kwako wewe kama mwanamke mdogo (kwa mumeo) kuweza kuwakilisha hoja zako za kutaka mabadiliko kirahisi.

Zungumza na mumeo kwa uwazi, weka hisia zako zote ili ajue kuwa anayokufanyia yanakuumiza na yanakusukuma nje ya ndoa yenu kitu ambacho wewe usingependa kitokee. Mwambie ni jinsi gani unampenda, unamheshimu na kumthamini.

Weka wazi hisia zako kwa mtoto wake, kwamba huna nia mbaya na unamjali kama unavyomjali mtoto wako.....kama historia yake inahusisha mateso ya mama wa kambo, itakubidi umhakikishie kuwa wewe sio kama wanawake wengine wenye roho mbaya.

Sema, kamwe hutomtesa wala kumnyanyasa mtoto wake, utamsaidia kila atakapohitaji msaada wako, utamfunza ili awe mtoto mwema na mwenye adabu kama unavyofanya kwa mtoto uliemzaa. Hutombagua wala kumnyanyapaa.

Mueleze ni kiasi gani unachoka kusafiri kutoka mkoa hadi mkoa kila siku, na kwa pamoja mtafute njia ya kuodoa kero hiyo (sio kuacha kazi tafadhali), ni mmoja wenu kuomba uhamisho ili kumfuata mwenzie.

Zamani kisheria ilikuwa mwanamke anamfuata mume siku hizi hata mume anaweza kumfuata mke, angalieni nani kazi yake inalipa zaidi na hivyo mmoja wenu kutafuta kazi nyingine huko ambako mwenzie analipwa vizuri zaidi (kamwe usikubali kuacha kazi) hata akikupa choice kazi au yeye, mama chagua kazi kwani wee bado mdogo na kumbuka unajukumu lingine hapo ambalo ni mtoto wako kutoka uhusiano wa awali.

Acha uzembe wa kukubali kila anachokisema mumeo, mpe challenges, pia sahau suala la kuomba misahama isiokuwa na sababu, omba masamaha pale tu unapojua kuwa umemkosea.

Ukifanikiwa hapa, njoo tena ili nikupe mbinu za kumfanya ajifuze kukusaidia shughuli za ndani unapokuwa kazini......ukimjulia mwanaume vijishughuli vya ndani sio deal sana kwake, sema tu sisi wanawake huwa tunawazoesha vibaya hawa wanaume ktk harakati za kuwakosa ili watangaze ndoa.

Mara wanapofunga ndoa nasi tunagundua kuwa hatuwezi kufanya yote, kazi Ofisini, kazi za nyumbani, kupika, kuwa mbunifu ili kumridhisha kingono, kuweka vionjo ili mapenzi yasifubae, kuangalia, watoto n.k Jamani eeh maisha ya sasa ni Tofauti, mwanamke huwezi kufanya yote hayo peke yako!

Natumaini wachangiaji na maelezo yangu yatasaidia kwa kiasi fulani ktk kufanya uamuzi,
Kila la kheri!

19 comments:

Anonymous said...

duuuuuu pole sana Dada yangu kwa yanayo kukuta.Nakuonea huruma sana ma wewe bado binti mdogo sana usingetakiwa kusulubika na huyo mbaba mtu mzima na watoto wa4 aliyeshindikana na wanawake2 pole sana my dia.Ila umeshafunga ndoa huna budi kuvumilia mana uliapa kuwa naye katika shida na raha.Cha msingi mkalishe chini mweleze kwaupole kabisa jinsi unavyompenda na kumjali umweleze na kero unazozipata juu yake.kama anakupenda atakusikiliza ila ujue kama anatabia yakulalamika ataacha taratibu hawezi acha kwa maramoja kuatu unamwambia direct ila kwa upole pale anapokosea.unajua watu wengine wanafanya vitu vya ajabu lakini hawagundui mpaka uwaeleze

Anonymous said...

Pole dada kwa kuwa mtumwa wa ndoa kwa kweli hii stori inanipa nihisi inawezekana wewe ni Niwa na huyo mumeo ni Meena kwa kuwa mambo yote uliyoeleza kuhusu huyo mumeo yanaangukia kwa huyo bwana niliyemtaja na vilevile kuhusu wewe yanafanana na ya huyo dada niliyemtaja.Kama ni kweli nijulishe ninaweza kukusaidia maana aliwahi kuwa rafiki yangu wakati nikiwa Arusha na nafahamu tabia yake pamoja na kwamba kwa sasa sina mawasiliano yake.Kama sivyo naomba unijulishe then nitakupa ushauri wa nini cha kufanya maana matatizo yako yanafanana na hayo wa hao watu niliokutajia

Anonymous said...

Dinah pole na shughuli hizi za kutuelimisha, naomba nitoke nje ya mada kidogo. Inaonekana ndoa nyingi zina matatizo ya ajabu na sasa Dinah inabidi utoe mada mpya zinazowafanya wanandoa wajue majukumu yao, huenda mwanaume unakuwa hujui kwa nini umeoa tuelekezane hapa ujue majukumu yako na familia yako. mke ajue kwa nini ameolewa na amsaidie mume kwa kiasi gani maana inaonekana wanawake wakisaidia sana nayo ni tabu pia sasa tuishije katika ndoa zetu ili kupunguza haya matatizo. tuongeeje na wapenzi wetu tusigongane. pia imeonekana kuwa wanaume wa sasa wana tabia za kununa na hapo inakuwaje. zimekuwapo kasumba kuwa wanawake wakiwa na uwezo shida ktk familia lakini mjue kuwa wanawake wengi sasa wana kazi nzuri au sawa na wanaume je tusiwaoe hebu tupeni na uzoefu nyie wanaume wenye wanawake wanaowasaidia sana hapo nyumbani muwe wawazi bila kuweka ile ya kiume.Mimi kwa kifupi nimeona wanawake wengi wakiwa msaada mkubwa kwa familia ikiwa baba ana upendo na anamjali mkewe na akiwa mwaminifu hapo matatizo hayapo.Mie nayashangaa haya matatizo ya ndoa kila siku humu mpaka naona kama ni shida kuoa, nioe mwanamke wa aina gani du!

andrew said...

Dada if pocbo achana nae utazeeka mapema mwaya na hizo shida,ukiniuliza mimi nitakuambia hakupendi,hivyo 2..!!

Anonymous said...

Pole sana mdogo wangu, si vizuri kukukandamiza kwa sababu unatafuta ufumbuzi wa kuishi na huyo bwana kwenye ndoa yenu. Ila kitu kimoja nadhani ulifanya haraka kuolewa naye, kwanza ungechunguza ni kitu gani kimewaondoa hao wake zake wa awali, pili ukiona mwanaume ameachana na wanawake aliozaa nao, wakakubali kuacha watoto na kuondoka zao ujue huyo bwana ana matatizo makubwa. Nakupa pole sana tena sana maana huyo bwana hutakaa umbadirishe tabia yake ndo hivyo alivyoumbwa na ndo maana wenzako wakamshindwa !

Anonymous said...

Pole dada waswahili walisema mfupa aliyoushinda fisi ww hutauweza!!! Huyo bwana kwanza inaonyesha anagubu na kwa mtaji huo hawezi kuishi na mwanamke yoyote ww mvumilie ukichoka timua tena bado mapema mana hapo inaonyesha unapoteza nae muda tu, ukizingatia bado una umri mdogo tu miaka 29 bado mbichi bibie, na isitoshe hujazaa nae mtoto hata mmoja na mfano mzuri unao hata kuacha pesa ya matumizi issue, je ukija kuwa na familia shost si ndio itakuwa balaa.

Kaza buti mtafutie sababu utimue zako maadam una mtoto wako bora ukamlee mtoto wako.

Ni hayo tu shost wangu, pole sana

Anonymous said...

Dada pole sana kwa matatizo ktk ndoa yako.La msingi hapo ni kua mvumilivu na unatakiwa umzoee coz inawezekana ata hao wenzako wawili walishindwana nae sababu ya gubu lake so kwakuwa ww umeshafunga na ndoa basi huna budi kumvumilia na kumchukulia kama alivyo tupo wengi wenye matatizo ndoani lakini ukisema uachane nae utampata mwengine ambae ana matatizo zaidi ya hayo so jaribu kumpotezea tu la muhimu ni kutomjali.chichi

Anonymous said...

dada yangu huyo ndo mumeo na inavyoonyesha ana gubu na ndo maana hao wenzio wawili walishindwa so kwakua ww umeshafunga na ndoa jaribu kumzoea coz ndo mumeo huyo,dawa usimjali basi utamzoea sababu unaweza ukaachana na huyo ukampata mwengine ambae ni tatizo zaidi ya huyo.saada linga.

Anonymous said...

Dada haya mamabo yameanza leo?I mean ghafla tu?Ama?WAKATI WA UCHUMBA HAYA HUKUYAONA?AMA ULIKUWA UNAYAFUNGIA MACHO?KWENYE NDOA NI MUHIMU KU-SHARE VIIKAZI VYA NDANI PIA...NA KAMA UNAVYOONGEA KITU KIDOGO KAMA KUONDOA GLASS...ANAPASWA HATA ASILALAME KWANI NI RAHISI ANGEMALIZA KUNYWA ANACHOKUNYWA AKINYANYUKA AKAIPELEKA YEYE MAHALA PAKE...KAMA AMBAVYO WEWE UMEPITIWA KUITOA NAYE PIA ANAWEZA KUPITIWA.MWANAMKE PIA NI BINADAMU KAMA YEYE...LAKINI NAHISI HAPO NDIPO WANAUME WANAKOSEA...KWAMBA YEYE MUME BASI HAWEZI ONDOA GLASS?

Anonymous said...

wewe mdada mdogo tu utakufa mapema sana yaani kusafiri kila siku Moshi tu Arusha back and forth?? Ni kazi gani hiyo hata inalipa nauli hiyo mama?

Huyo mumeo kweli chizi na so crazy halina huruma kabisa.Jamani fanyeni tafiti kwanza kabla hamjaolewa ni mtu wa namna gani anataka kukuoa.Mtu kaachana na wake wawili,kisa??

Wewe mama kwa kweli mimi nashindwa kupata ushauri wa maana hapo, maana naona ni full wivu tu wa mumeo. Muhimu ni kumuomba Mungu ambadilishe huyo mumeo aweze kuwa natabia nzuri ya kukuhurumia.

Anonymous said...

Pole sana kwa mikwaruzo katika ndoa yako.Jinsi ulivyoelezea kuhusu ndoa yako inaelekea unampenda mumeo ingawa haoneshi penzi kwako.Sifahamu uhusiano wako na Mungu ukoje lakini cha muhimu muombe Mungu sana kuhusu Mumeo.Maombi yako yatambadilisha Mumeo.Mimi nimeoa na nina mtoto mmoja.Nilikuwa na matatizo katika ndoa yangu lakini Mke wangu alikuwa mvumilivu sana na akamlilia Mungu anibadilishe na Mungu akamjibu sala zake.Sasa hivi ndoa yangu ni nzuri sana na ninampenda sana Mke wangu.Ukishamlilia Mungu pia omba akupe hekima ili uongee na mumeo kuhusu mawasiliano yenu katika ndoa yenu.

Anonymous said...

dada pole sana, ndoa ndoano! uvumilivu ni muhimu ila naona hapo kwako hamna mapenzi ya dhati, mlioana bila kuwepo na nia ya dhati kwani kina mmoja alishakuwa na uhusiano wa awali. kwa umri wako kama unaona kero zaidi achana na huyo jamaa! tafuta maisha yako.

Anonymous said...

Pole sana Dada.Mimi nakushauri upunguze hasira,tena uwe mpole kabisa kanakwamba hakuna chuki yoyote baina yenu.Muombe mumeo mkae chini muelewane ili akueleze yale ambayo hapendi wewe uyafanye,na wewe utapata nafasi ya kumueleza mapendekezo yako,Wote mkiwa juu,ugomvi hauwezi kuisha,na pia hatakama unachoka kazini,jiahidi na majukumu yako ya ndani uyafanye.

Anonymous said...

Pole sana dada, mimi nashindwa kukuambia chochote maana mimi naishi maisha kama yako, hivi shosti nina mpango tu wa kusepa! better to stay alove deliver unhappy, nimeolewa 2006 niko na mtoto 1 na my huz, lakini sina furaha kabisa, mume wangu kanizidi like 10 years, nahisi nina presha sasa ingawa naogopa kucheck, moyo wangu unaenda mbio kila wakati, sijapanga hata kuzaa naye tena, ana mahasira kama kifaru. I tried to chat with pastors lakini most of them wananiambia people like that will never change, nimeshamwombea hadi nikagombana na Mungu wakati mwingine. Ila solution iliyopo sasa, naomba kibali kwa Mungu either niachane naye au ananisaidia kumrekebisha, I gave God 2 option. Kwa sasa dada yangu naomba fanya kazi yako ndo iwe mumeo, achana naye, na wala usimwaze kabisa, mimi niko na 29 years kama wewe, lakini nimeshakomaa vya kutosha because am seeking a many advices kwa watu tofauti. All the best, mimi ni mchaga na mume pia ni mchaga.

Anonymous said...

huna tofauti na mimi my dear wangu chakula na matumizi anatoa ila akijisikia ananisimanga umekaa tuu kazi kula,watoto wake bora kuliko mimi kinachoniuma zaidi mpaka watoto tuliozaa hawathamini kama anavyowathamini wale aliozaa awali,haipiti siku bila kusemana ovyo na unyumba nanyimwa yaani mambo ni mengi siwezi kusimulia ila navuta subira na kujitahidi kumuweka sawa lkn nikichoka naachia ngazi,ila mwenzako nimegundua jifanye huna time nae kama vile umechoshwa na tabia zake atajirudi lkn kama msimamo ni uleule jaribu kushirikisha wazazi

Anonymous said...

Wee dada wewe hiyo tabia ya kujifanyia mambo mwenyewe yeye ni baba wajibu wake ni kulea familia, Pili ulitoka wapi na baba wa miaka 42 wewe mtoto mdogo wa miaka 29? Ulishasikia kakaa na mwanamke miaka 10 na mwingine miaka 4 vikawashinda wewe ndio kikakupeleka nini?

Jamani mie naona watu wengine wanapashwa tuwatukane hasa na sio kuwapa ushauri.
Jenga maisha yako angalia maisha yako wewe na ya huyo mwanao achana na huyo Mzee.I wish ungekuwa karibu yangu wewe dada nikuzabe makofi. Mchaga gani wewe uliyezubaa kaaaaah vitu vingine vinaudhi sana jamani. Publish Reject

Anonymous said...

nijuavyo mimi na haka kauelewa kidogo ka dini ni kwamba.. kwenye mahusiano yoyote yale mwanaume kazi yake ni kupenda na mwanamke kazi yake ni kutii...
Sasa jiulize kama huyo mumeo alikupenda/anakupenda kweli?nawe mara yako ya mwisho kutii alichokwambia(naomba nieleweke si vyote vya kutii but inakupasa umweleze kwa nini unanona sio busara kutii anachokwambia)

Ni rahisi sana.. fanyeni mawasiliano yenye kufaa, mwambie unachofikiria na pia umsikilize anachofikiria na mfikie mwafaka...

Ikishindikana hapo mama waeza kimbia fasta.. bado u mdogo mno kuyabeba hayo..

Anonymous said...

mmmmmmh!pole mwaya hope one day our lovely GOD ll give you a good solution for your problem.Keep on praying my dear maana amna aliye bora kila mtu anamapungufu yake ila yanatofautiana.My self i ll also pray for you dear, cha msingi ni wewe kuwa mkweli kwa mumewako na wala usimfanyie baya am sure kama ni binadamu aliyekamilika na mwenye hekima akiona wewe u mwema kwake ataona aibu na kujirudi.Pia usipende kubishana naye let him talk talk hapo utapunguza ligi.

Anonymous said...

Jitenge naye anza maisha yako mwenyewe