Tuesday, 2 March 2010

Mke asikiliza wambea na sasa tunaishi ki Juma na Roza

"Habari za kazi Dada Dinah na heri ya mwaka mpya.
Mimi Naitwa Emmi nipo Iringa nimekuwa mpenzi sana wa blog yako hasa kwa ushauri na maoni mbalimbali yatolewayo humu.

Mimi nina mke nimeoa miaka mitatu iliyopita na tumejaaliwa mtoto mmoja wa miaka miwili sasa. Shida yangu sister ni kwamba mke wangu anapenda sana kusikiliza maneno ya mitaani. Mimi ni mnywaji wa pombe kiasi lakini yeye hanywi na aliniruhusu kunywa isipokuwa nisizidishe kiwango na hilo nalizingati sana.


Sasa yeye akiambiwa tu umbea kuwa mmeo ana wanawake wengine basi akirudi kutoka huko atokako hunijia kama Mbogo na hataki kusikia cha mtu, yaani ananitukana sana lakini mimi kwa sababu nampenda na pia kujali sana uwepo wa mwanangu huwa simlipizi kwa kutusi zaidi ya kukaa kimya.


Ila kuna wakati nilimwambia aachane na hao wambea kwani watambomolea nyumba yake lakini anabisha. Kwa sasa imefikia hatua hataki kukaa na mimi na anatafuta kila sababu ili nimfukuze ila mimi ni kimya nasubiri uamuzi wake.


Jamani nipeni ushauri juu ya huyu mwanamke, je nimuache au niendelee kukaa kimya huku yeye akiendelea na matusi yake ndani ya nyumba? Kwani kwa sasa tunaishi kama kaka na dada yaani kila mtu ana chumba chake, nafikiri umenielewa.
Nitashukuru sana kwa ushauri wenu Wadau.
ahasante!!! Manuel"

Dinah anasema: Manuel asante sana na heri ya Mwaka mpya! Unajua ndoa inajengwa na watu wawili ambao ni mume na mke. Huyo Mke asingesikiliza maneno ya watu na angekuamini kama ungekuwa unakunywa pombe na yeye akiwa pembeni.


Lakini kwa vile huwa hayupo unapokwenda kulewa anahaki zote za kuwa mkali nakukubali anachoambiwa na Mashoga zake ambao baadhi huenda ni walevi nahuenda huwa unafanya nao utani au wao wanakutania wewe kupita kiasi na pengine umewahi kuwtaongoza bila wewe kujua kutokana na pombe na hivyo kuhisi kuwa unaweza ukawa na mwanamke wa nje na hivyo kupeleka habazi ambazo hazina uhakika kwa mkeo.

Unajua tena Mji wa Iringa ni mdogo na usikute watu wanajuana na wanajua unanywea bar gani na huko bar huwa unakaa na kina nani......kama marafiki zako hawajaoa au wameoa lakini sio waaminifu kwa wake zao ni wazi baadhi ya watu wanaweza kuhisi kuwa hata wewe unafanya kama wanavyofanya watu wote unaokunywa nao Pombe hapo kilabuni/baa.

Ni kweli marafiki zake (Wambea) wanaweza kutunga na kum-feed maneno mkeo ili kuharibu ndoa yenu nahivyo wao kuwa huru kutoka na wewe....yote yanawezekana.

Tatizo hapo sio mameno ya wambea, tatizo hapo ni kuwa Mkeo anahisi upweke ndani ya ndoa yenu, ni wazi kuwa humpi muda wa kutosha kwa vile muda mwingi unautumia ukiwa kazini na kilabuni. Unaporudi nyumbani unakuwa na kilevi kichwani hivyo sio wewe kwa asilimia zote....sijui unanielewa hapa?!!

Sasa kutokana na upweke huo ambao unaweza kumfanya afikirie mengi mabaya na hata kuzaa wivu mkali ndio unaomfanya asikilize na kuamini kila anachoambiwa na marafiki zake kwa vile wako pale kwa ajili yake na wanaonyesha kumjali, kumsikiliza na kumpa ushauri.....hata kama ushauri ni wa kubomboa bado atawaamini kwa vile Saikoloji yake inaamini kuwa "wanamjali, wanamsikiliza na kumthamini" zaidi kuliko wewe.

Ninachokiona hapa sio "umbea" bali ukosefu wa mawasiliano na wewe kushindwa kuzingatia nguzo muhimu iitwayo "Maelewano" Mf: wewe ni mnywaji ili asikunyime kile unachokipenda kutokana na pombe amekubali kuwa endelea kunywa lakini sio sana.....mkeo ame-complimise hapo!

Je! wewe umekubali kitu gani ambacho labda wewe hukipendi lakini kwa vile ni mkeo mpenzi na hutaki kumnyima raha ya kufanya jambo alitakalo ukakubali aendelee kufanya jambo hilo....SIDHANI!


Unatakiwa kumshukuru Mkeo kwa kukuamini na kukuruhusu uendelee kunywa pombe lakini usizidishe. Mkeo sio tu anakupenda bali pia anajali afya yako kwani sote tunajua Pombe sio nzuri kwa afya zetu.

Sasa kwa vile ameruhusu uendelee kunywa haina maana uende kilabuni kila siku na badala yake unaweza kunywa ukiwa nyumbani na hivyo yeye kupata muda wa kuwa na wewe. Unaweza kabisa kufurahia Bia ukiwa na familia yako sio washikaji kila siku.....wewe ni mume na baba hivyo jaribu kuzingatia majukumu yako kama Mwanaume wa kisasa.

Ukimya wako ndio unamfanya mwanamke huyo kuzidiwa na hasira na ndio maana hatakaki hata kuwa karibu na wewe, sio hivyo tu inawezekana anaamini kuwa umetoka nje ya ndoa na hataki kupata maamubukizo ya HIV (kitu ambacho hata mimi nampongeza) incase ulitereza nje kiukweli.

Nini cha kufanya: Watu wengi hukimbilia Talaka, lakini tukumbuke kuwa Talaka sio suluhisho la matatizo na mkikimbilia Talaka ni wazi hutomkomoa yeye mkeo au rafiki zake bali mtoto mliemleta hapa Duniani. Mtoto wenu ndio ataumia japokuwa ni ngumu sana kwa ninyi wazazi wake kuona maumivu yake Kiakili, Kimwili, Kisaikolojia na Kihisia.

Tafuta muda mzuri, ukiwa umetulia kiakili na zungumza na mkeo, Omba msamaha kwa kutokuonyesha kuwa unajali (hii itamlainisha na kumfanya akusikilize vema), mhakikishie ni kiasi gani unampenda na ni muhimu kiasi gani kwenye maisha yako.

Mwambie kuwa yote anayosikia kutoka kwa rafiki zake sio kweli na ili kumthibitishia hilo basi uko tayari kwenda kuangalia afya yako (vipimoo vya HIV)...majibu yakitoka safi ni wazi itampa amani moyoni na hivyo kuanza kulala kitanda kimoja na mume wake (wewe Manuel).

Weka wazi yote yalioujaza moyo wako kutokana na tabia ya mkeo ambayo ni wazi imesababishwa na unywaji wako wa Pombe.

Kumbuka Ndoa inajengwa na Nguzo 3, (1) Zote ambazo ni kwa mujibu wa Imani za Dini zenu, alafu kuna zile mbili za kidunia/kabila (inategemea unatoka wapi) ambazo ni (2) Uhusiano wa kimapenzi (3) Uhusiano wa kingono.

Uhusiano wa kimapenzi nao una Nguzo tano muhimu ambazo ni Heshimiana, Thaminiana, Shirikiana, Sikilizana/Elewana/kubaliana na mwasiliano (kuna topic inazungumzia kwa kirefu )sasa wote wawili mnatakiwa kuzingatia hayo ili kuimarisha uhusiano wenu wa kimapenzi.

Pia ongeza muda unaotumia kuwa na mkeo, badala ya kuzungumzia masuala kuhusu maisha na mtoto hakikisha mnazungumza kuhusu ninyi wawili kama wapenzi kitu ambacho kitawasaidia kuw akaribu zaidi na hata kuboresha uhusiano wenu wa kingono.

Punguza unywaji wa pombe kwa maelewano kuwa nae apunguze marafiki wasiokuwa na mpango, badili utaratibu wako wa kwenda kunywa pombe kilabuni na badala yake nunua chupa/kopo za pombe na kunywa huku mkeoyuko pembeni.

Kila la kheri!

8 comments:

Anonymous said...

Heeeeee kumbuka kuwa penye wengi pana mengi.Huko kilabuni unakoenda kunywa ndiko unakowakuta hao wambea wanaenda kummwagia radhi mkeo.Unajua hata ukicheka na mwanamke tu wanapeleka habari kwa mkeo.

Mimi nakushauri kama unataka kuwa salama na mkeo achana na pombe kabisaa au agiza nywea home.Hakuna njia nyingine kwenye michanganyiko ya watu wengi hasa kwenye mapombe haku na jema hata kidogo.Kimbia kabisa maeneo ya vilabuni.Kama kweli unampenda mkeo basi pombe si kitu cha kushikamana nacho.Tafuta kitu kingine mbadala badala ya pombe.

Kila mwanamke atakuwa hivyo tu amini usiamini hakuna anayetaka aibiwe.Hata kama kwa sasa hunywi sana lakini ipo siku utazidiwa.Mwambie mkeo kwamba umeacha pombe kwani ndicho chanzo cha kutokuaminiana ndani.Kwa sasa ukitoka ulikotoka wewe chonga hadi home na msaidie mkeo kazi hapo home panga kazi mbali mbali mwende pamoja jioni mkafanye mambo yatakuwa mswamo kabisa.Usimwelewe vinaya mkeo hali ya pombe si salama kabisa vinginevyo na yeye awe anakunywa mnaenda wote.

Pole dogo lakini achana na pombe ili unusuru ndoa yako.

Anonymous said...

mhh!hapo pagumu kaka,ila km unampenda mkeo tafuta njia mbadala muweze kutatua tatizo lenu.kusema kumuacha huo ni udhaifu labda km kweli naww unakimwanamke huko unapoenda kunywa pombe,na baada ya kuyaweka sawa mambo yenu hakikisha naenda wote huko unapoenda hata km hanywi pombe hiyo kidogo itasadia au sio lazima uende bar mbona unaweza hata ukanunua na kunywa kwako!ukiwa mnaongea na mkeo kuliko kungangania kwenda baa matatizo mengine unayasababisha we mwenyewe.kikubwa ktk maamuzi yenu mumuangalie mtt wenu ambaye bado mdogo na anayehitaji malezi ya wazazi wote 2.ni hayo

Anonymous said...

Pole kaka kulingana na maelezo yako mimi nadhani si kwamba anasikiliza ya wambea labda yeye kapata mtu mwingine ndio maana anatafuta sababu ya wewe kumfukuza.ushauri kaa na mkeo muongelee masuala yenu na umpe nafasi ya yeye kueleza kile kilicho moyoni mwake unajua unapotoa kilicho ndani unapunguza maumivu na pia ajue kwamba nyumba haijengwi na watu wa nje bali nanyi wawili na ndoa ina mlango wa kuingia tu hakuna wa kutoka. Pia mweleza ubaya wa kutoa maneno machafu(matusi) mbele ya mtoto kwani ubongo watoto ni rahisi sana kukata vitu kwa hiyo asije akampiga mtoto pindi atakapokuta mtoto wake akitukana, neno la Mungu linasema mlee mtoto katika njia inayofaa naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. pia jenga mazoea ya kutoka naye hata kama hanywi pombe yeye atakunywa vinywaji laini ila atakuwa nawe hivyo kueposha maneno ya watu

mamaB said...

Pole kaka manuel. Mimi naona huyo mkeo labda amesahau msemo usemao Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake mwenyewe. Maneno ya kuambiwa ukiyasikiliza sana yatapelekea kuharibu ndoa yako, afterall hujapata ushahidi kama mwenzi wako anafanya kitu kibaya ni bora achunguze kwanza pia na wewe kaka badili tabia uwe nae mkeo karibu, onyesha kumjali hiyo itamfanya akuamini hata hao magossip wakimwambia kitu akifananisha na the way unampenda haweziwaamini.

Jinyenyekeze muanze upya ukurasa wa mapenzi.

Anonymous said...

Inavyoelekea huyo bi dada anapalia nyumba yake moto sasa itakapoungua ibaki gofu ndo atakapoisoma namba kwa nyuma wakati hao mashostito wanaompa umbea wanamla kisogo na kumuona punguwani kwa kuharibu ndoa yake wakati wao wapo na wapenzi/waume zao wanakula bata tu.

Kaka mi naona ndoa yenu bado changa hamna haja ya kuachana au na wewe kumshushia varangati, ila sio siri na sisi wanawake tunamidomo michafu jamani yani mtu anaweza akakushushia mitusi mpaka unajiuliza hivi na huyu kazaliwa na mwanamke mwenzangu ama? halafu saa nyingine upeo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana, inabidi tubadilike mambo yakusikiliza mashoga na umbea yamepitwa na wakati, uwe na shoga ambae mnakaa na kupanga vitu vya maendeleo, shoga wa kupiga umbea wa kazi gani anakuchosha tu na maneno yasiyokuwa na staha.

Ushauri wangu kwa sababu hali ni tete itisheni kikao cha wanandugu kila mmoja wenu aeleze matatizo yake, ninaamini mtasuluhishwa na ndoa yenu itakuwa shwari na mapenzi motomoto.Pole kaka ndo mitihani ya ndoa hiyo, wenyewe huwa tunaapa for better for worse, sasa vumilia tu hiyo worse but you shall overcome majaribu kaumbiwa mwanadamu.

shamim a.k.a Zeze said...

UJIO MPYA WA DARHOTBOARD 'DHB FORUM'

ULISHAWAHI KUWA MEMBER WA DARHOTBOARD ' DHB FORUM' SASA NI WAKATI WA KUKANDAMIZA UPYA TENA BAADA YA DHB KURUDI KISASA ZAIDI

HIVYO BASI UNAITWA KAMA ULIKUWA MEMBER INGIA KWA JINA LAKO LILE LILE AU LA JIANDIKISHE UPYA, TUANZA MAKAMUZI UPYA.

WAPI MASAKI,BABY KIBAKI, MSJACQUE,LIVECAT,MC ZOBIZOBI,GAIZKA,BIMKORA,DUMISANE,GEEQUE,MALIWAZA.MALISAK,FUNZADUME,NAILA,JANNY,LUCKY ONE,DR MUATHU, DINAH,MCHAICHAI,MADOIDO,PAPAK,TZKWELI,MTOTOWA MJINI NA WENGINEO WEEENGI NI WAKATI WAKUJUMUIKA UPYA NA KUANZA KUSOGOA KAMA KAWA

BOFYA
http://www.darhotwire.com/forums

KARIBU SANA

DHB TEAM

*****Madam nirushie hiyo plz kijiweni kwako maana najua wana wa mapenzi na mapendi washinda huku

zeze...udelete post sio upost

Anonymous said...

ukisikiliza wembea siku zote mtagombana.kama huyo mwananmke anakupenda kweli mwambie asisikilize watu otherwise hakupeni pole sana ndugu?mdau

Anonymous said...

Ndugu yangu chanzo cha kuvunja ndoa ni wewe mwenyewe. Kwanza hujaonyesha kujali tatizo linalomkabili mkeo, kama ungekuwa ulionyesha kujali basi hata hzo pombe ima ungeacha au ungenywea nyumbani. Vipi kaka try to analyse what makes ur wife not to trust u, then keep away frm that. Amiin nakwambia kilaji kinawatoa wa2 wengi kwenye nuru na kuwapeleka kwenye kiza, ikiwa wataka mkeo basi acha pombe na ikiwa wataka pombe basi kubali mkeo aondoke, kila m2 anahisia na cku zote m2 anaekupenda lazima aumie hasa akisikia habari za usaliti awe amethbitisha au laa. Mwisho wa yote ni kwamba chunguza pia mwenendo wa mkeo, kulikoni anakomalia kuondoka kuliko kutatua tatizo????? Take care bro that is bitter sweet of mariage.
Mwatima