Kwanini wanaume mnapenda kuterekeza Familia zenu?

"Habari yako Dinah, pole na majukumu. Mimi ni mama wa miaka 40 sasa nina watoto 2 lakini nimetengana na mume wangu kwa miaka mitano sasa. Uniwie radhi kwa hii habari ni ndefu sana ila nataka kushare na wamama na wababa kwa ajili ya kile kinachotokea ktk maisha ya ndoa unapobainika udanganyifu kwa mmoja wapo.


Tumekuwa kwenye ndoa kwa miaka 11 mpaka nilipoamua kumuacha mume wangu January 2006, kwa muda wote tulioishi pamoja tulipitia maisha magumu na ya wastani na tulikuwa tunasaidiana sana. Nilikuwa nampenda mume wangu kwa dhati, akiwa hana kitu nilifanya kwa niaba yake na sikuona tatizo.

Mwaka 2002 mume alipunguzwa kazini na kwa maelezo yake hakulipwa hela ya maana, mimi nikaona sio tatizo nilikuwa na kipato cha kutuwezesha kuyamudu maisha ya familia yetu kwa furaha, hapo tayari nilikuwa nimenunua kiwanja maeneo ya Tegeta.


Mume alikuwa hayapendi maeneo hayo ya Tegeta hivyo hakujishughulisha hata kukiona hicho kiwanja. Muda mwingi mume wangu alikuwa anabaki nyumbani mimi nikiwa kazini. Hapo nyumbani tulikuwa na msaidiza wa kazi na watoto 2.

Wakati huo mtoto wetu mkubwa alikuwa anasoma darasa la 2 na mdogo alikuwa chekechea, nilikuwa na akiba niliokuwa naitunza kwa ajili ya kujenga lakini tukajadiliana tukaona bora tununue gari ili mume wangu awe na shughuli kwa kutumia hivyo gari. Mume wangu alitafuta gari nikalinunua na yeye akawa analitumua kama tax. Tatizo likaanzia hapo.

Naomba niwaambie hivi mimi ni mama mwaminifu ninamwamini Mungu katika kweli yote sikuwahi kumfikiria mume wangu vibaya au kama angaliweza kuwa na mwanamke mwingine au kutembea na house girl nilikuwa namwamini sana na nilikuwa bize sana nikidhani namsaidia mwenzangu kumbe wapi.


Gari lilianza kunionyesha mambo, mume akawa hataki kufanyia kazi akawa anazunguka nalo tu, asubuhi naulizwa hela ya mafuta, matengenezo mpaka nikajuta kununua hilo gari. Nikaamua kuwaambia ndugu zake waongee nae.


Walipoongea nae yeye akasema hawezi kuendesha taxi kama nataka ninunue fuso ndio atafanya kazi hiyo, hilo likaniwia gumu nikachukua gari nikampa dereva mwingine. Jamani! wakati mimi ninahangaika kutafuta pesa za matumizi na kusomesha watoto kumbe mwenzangu kaanzisha uhusiano na dada wa nyumbani ndio maana hata kazi hataki kufanya ila mimi nilikuwa sijui kinachoendelea.


Mwaka 2003 tulianza kujenga na yeye ndio alikuwa anasimamia ujenzi ila cha moto nilikiona, tunapanga bajeti ya site vizuri namkabidhi pesa akirudi jioni ana shoti laki 2 au laki inategemea na wingi wa pesa utakayompatia lazima apunguze materials bila sababu mpaka nikaanza kumchunguza.

Hapo tulikuwa tunaishi Kinondoni kumbe bila mimi kujua alikuwa kampangishia mwanamke chumba huko Gongo la Mboto. Tukaanza kukorofishana maana ukiweka hela ndani yeye kazichukua hata simu anabeba.

Alivyojua kuwa najua habari za huyo mwanamke akaanza kusema mimi nataka kumwacha kwasababu hana kazi, oh sababu unajenga na mambo mengi mabaya kwa kweli. Tulisuluhishwa lakini hakuwa tayari kuacha tabia ya wanawake wa nje na mimi nilimchukia sana kwa tabia zake ndicho kilichotutenganisha mimi na huyo mume wangu.

Tulipoamua kutengana aliniambia niondoke na watoto niliondoka nao na wanasoma vizuri tu kwani niliamua kuwapeleka Boarding School ili wasiadhirike na kutengana kwetu japokuwa wakirudi likizo Mume wangu anakuja kuwaona lakini hawasaidii kwa chochote hata chupi hawanunulii.

Kwa sasa anafanya kazi nzuri tu lakini hataki kuwasaidia watoto. Mwaka huu kabla watoto hawajarudi Shuleni waliniomba sana nimsamehe baba yao na nilifikiri sana nikawaita wazee na nikawaambia kuwa nimemsamehe kilichotushangaza ni kwamba yeye hajakubali kusamehewa anachotaka ni nyumba niandikwe kwa jina lake kwanza na gari ninalotumia nimpe au niliuze ndio atarudi.

Kwa masharti hayo mie nimesema basi na kila mtu aishi peke yake maana naona mwenzangu anawivu na nilichonacho ambacho kimsingi ni cha familia yetu, nimeogopa masharti yake maana anaweza kutufanya tuanze kupanga tena.

Kinamama ninachotaka kujua ni hiki; Kwa kina mama hivi waume zenu nao wakijua kuwa umejua anachokukosea na kutengana huwa wanawasusia familia?

..... na kina baba naomba kuwauliza mpaka lini mtawatesa wake zenu kwa kuwasusia familia zenu?

Samahani sana Dinah usilitoe jina langu.
Nina hasira sana na wanaume na ninawachukia kwa kweli."

Dinah anasema: Asante sana kwa maelezo yako uliyoyapangilia vema kabisa. Maelezo ambayo hakika yanatia Moyo wote waliopatwa na matatizo ya kindoa, Inaonyesha kuwa hata sisi wanawake tunaweza kusimama Imara na kuhakikisha watoto wanapata maisha bora hata kama baba yao hataki kusaidia.


Hongera sana kwa kutumia muda wako mwingi kuhakikisha kuwa familia inaendelea kula na kuishi mahali bila usumbufu wowote, lakini kujituma kwako kumezaa tatizo lingine ambao ni hali ya kutokujiamini kwa mumeo.

Mwanaume yeyote hapendi kulishwa na mwanamke, kwa maana ya kuwa na mwanamke mwenye nguvu kiuchumi. Huyu mwanaume atahisi kuwa unamdharau hata kamahufanyi hivyo bado atadhani kuwa unamdharau kwa vile tu hana kazi au hata kitu.

Mwanaume huyu atatafuta namna nyingine ili ku-gain ile hali ya yeye " kuheshimika" nakuwa in control na ndipo sasa anakwenda kuanzisha uhusiano na mwanamke mwingine na ili kurudisha hali ya kujiamini na nguvu as a man akatumia pesa za kujengea nyumba kuhonga, akatumia gari kufanyia shughuli zake nyingine na sio kazi ya kubeba abiria.....hii yote ilikuwa inamfanya ahisi kuwa bado ni MWANAUME out there!


Lakini kitu ambacho wanaume sio tu mumeo ni wote, huwa wanakisahau au hawajali ni kuwa unapoamua kufanya uchafu nje na kuharibu ndoa yako atakae umia sio Mkeo bali ni watoto ambao hakika hawana hatia na hawakuomba kuzaliwa na nanyi bali uamuzi wenu ndio umesababisha uwepo wao hapa Duniani.


Ndoto ya Mtoto yeyote Duniani ni kuwaona baba na mama yake wako pamoja, na mtoto huyo hatopenda kuona mtu mwingine anaingilia uhusiano wa baba na mama yake. Inasikitisha unaposhuhudia watoto wanatamani ndoto hiyo itimie lakini mzazi mmoja anaendelea kuwa mbinafsi na kutokujali matakwa, hisia na haki ya watoto hao.


Mumeo hapendezwi na maendeleo yako kiuchumu na anahisi kuwa humueshimu tena kwa vile alikuwa hana kitu napengine hata aliwahi kudhani kuwa kuna mwanaume mwingine anakupa hizo pesa za kujenga nakufanya mambo mengine ya kifamilia na kimaendeleo.....wanaume wengine ni wanadhana potofu sana, wanadhani mwanamke huwezi kufanikiwa kimaendeleo unless kuna mtu unamtumia.

Yeye kutaka Gari iuzwe na Nyumba iandikwe jina lake ni wazi anataka ku-gain power au control kama mwanaume. Hakuna dalili za yeye kutaka kuendeleza penzi ili kuwa na maisha bora kama familia.

Kama unahisia za kimapenzi juu yake, kwamba bado unampenda na yeye anakupenda na ungependa ndoa yenu ifufuliwe then ni vema wote wawili kushirikiana na kupata ushauri wa kitaalamu zaidi na baada ya hapo mali zote ziandikwe majina ya watoto kama alivyogusia mmoja wa Wachangiaji nami nitaongeza maelezo yangu kwenye hili kama utakuwa tayari.


Lakini kama unataka kurudiana na Mumeo kwa vile tu watoto wanataka kuwa na baba yao karibu then nakushauri utafute Mwanasheria wa masuala ya ndoa (unaweza tu kwenda Mahakamani ukaeleza nia yako na wao watakupa ushauri wa nini cha kufanya) ili kumtaliki mumeo Kisheria ili asije kukupa matatizo baadae, pia Talaka itakusaia wewe kuwa huru na kuendeleza maisha yako.

Nikijibu swali lako kama mwanamke: Inategemea na asili ya Mwanaume, mazingira aliyokulia, uzoefu wake, maisha ya wazazi wake n.k., ila wanaume wa Kibongo kuterekeza familia zo ni kawaida sijui wamerogwa?

Hata kama baba yako alikuwa mchafuzi au alimterekeza mama yako haina maana kuwa na wewe "urithi" hayo, jitahidi na uwe tofauti, kuwa baba bora kuliko alivyokuwa baba yako. Muonyeshe baba yako kuwa alichokifanya sio Uanaume ni upumbavu na wewe ni mwanaume na unafanya kinyume kabisa na lichokifana.

Wanaume wa kibongo wenye t abia ya kuterekeza Familia zetu kwa sababu ya Vimada mnatakiwa ku-MAM UP!

Ninyi wanawake (Vimada) kama unajua kabisa jamaa anafamilia yake kwanini ukubali aiterekeze? Kwanini unakubali mwanamke mwenzio ateseke? Hebu fikiria ingekuwa ndio wewe umeterekezwa ungejisikiaje?

Wanawake wote mnaopenda kunyatia/kubali waume za watu mnatakuwa ku-WOMAN UP nakujifunza kusema "SITAKI kuharibu maisha ya watoto wako"....utakuwa umesaidia watoto hao kuendelea kuwa na wazazi wao wote wawili. Jifunzeni kujitegemea na kuendesha maisha yenu bila kutegemea kubebwa na wanaume wa watu.

Dada tafadhali kama utaamua kuendelea na ndoa kwa vile bado mnapendana basi hakikisha afya yake ni safi na unasimamia hapo kwenye mali kuwa ni za watoto, vinginevyo atakumsikinisha (kukufanya uwe masikini) huyo mwanaume.


Kila la kheri mwanamke wa Shoka!

Comments

Anonymous said…
Pole sana dada kwa yaliyokukuta. Nafikiri tabia kama hizo ni kwa baadhi ya wanaume na siyo wote. Nafikiri yaliyokukuta ni kutokana na kuolewa na mtu ambaye hukuwa umemchunguza vizuri. wanawake wengi wanatumbikia kwenye matatizo kwa sababu ya kukimbilia kuolewa bila kujiridhisha na tabia za wenza wao. ukweli ni kwamba hiyo tabia alikuwa nayo siku nyingi ila inawezekana wewe ndo ulikuwa hujajua tu.

Nafikiri uamuzi uliofanya ni wa busara. Kaa kivyako, na usimfikirie kabisa.
Anonymous said…
Hauko peke yako mimi nefunga ndoa na nina watoto 2 sasa wakati ninamtoto mmoja nilipojua mume wangu anatoka na mtu ndio alizidi kuwa mkali nyumba ilikuwa haikaliki mimi hasira juu na yeye anakuja juu zaidi ilikuwa balaa badala yeye kuomba msamaha yaishe na alivyokuwa anaonekana kwa kweli ni kama alikuwa hataki kumuacha huyo mwanamke nilipata maudhi mno yani nilikonda kwa kujiuliza kwa nini anifanyie hivyo mimi ilihali mume wangu alikuwa ananipenda sanaa nilijiuliza maswali mengi mpaka niliposhauriwa niwe mvumilivu ndipo taratibu kama mwaka mzima wa uvumilivu na vituko alikuja kutulia na amini usiamini yeye sasa ndio anajisikia vibaya kuliko mimi kwa aliyonifanyia... ila kuna kitu bado mpaka leo huwa kinaniumiza kwanini aliamua kufanya hivyo?? labda simridhishi au ni nini!! hivi kwa nini hawa wanaume wanaumiza wake zao kwa wanawake wa nje mm pia nisaidieni jamani, lakini dada omba mungu sana huyo ni mume wako fanya vyovyote muishi pamoja japo kila mtu na chumba chake. nyumba na gari andika jina la watoto then gari fanya tax kwa muda mpaka mabo yatulie nadhani inachukua muda kwa hawa wanaume wetu kuamini nafasi yake bado ni ileile kwako ndio maana wanakuwa hawajiamini kama wanaweza samehewa
Anonymous said…
Mshirikishe sana mungu dada mumeo atabadilika, jaribu kumueleza kwa nini ulitengana naye na mueleze ajiamini kuwa wewe unampenda ila matendo yake ndio yanayofanya matatizo yote yatokee, lakini kubwa mshirikishe mungu pekee na pia ufuate moyo wako unavyojisikia juu yake. kama hujisikii kuwa nae pia sikushauri.. hakikisha unachofanya kinatoka moyoni kwako ili usijekujuta sana baadae, pia jaribu kusamehe.
Anonymous said…
Pole sana na yaliyokukuta, mungu ni mwema na atakulipa kwa kadiri ya moyo wako ulichokitoa kwa mumeo. Ndoa ina misukosuko mingi mojawapo ni kama hilo la baba kupoteza kazi. Ambacho unatakiwa kujua si kila mwanaume ni wa staili ya mumeo. Binafsi niliwahi kuwa bila ya kazi kwa takribani mwaka mmoja na katika kipindi hicho ndio nilijua huyu mke wangu ndiye haswa niliyepewa na mungu. Kwani alinisuport kwa hali na mali mpaka nikapata kazi nzuri zaidi. Nilikuwa nikikaa nyumbani pamoja na kabinti kangu na msichana wa kazi huku yeye mke wangu akienda kazini. Sikupata hata mara moja kufikiria anything si tu kwa huyo house girl wala mwanamke mwingine yeyote yule. We have about 8yrs of marriage blessed with a daughter and a son, I never cheat on my wife. I trust her as much as she trust me. Pole sana na matatizo ndio dunia ilivyo.
Anonymous said…
Hapo tunadanganyana mamaangu. We umesema mtoto wako wa kwanza yupo darasa la pili na wa pili yupo cheke chekea, kwaakil ya kawaida hao watoto ni wadogo na uwezo wao wa kufikir si mkubwa kiasi cha kumuombea msamaha baba yao. . . Unataka kutuambia watoto pia wanajua chanzo cha ugomvi wenu? Sema wewe ndiye ulieamua kurudiana naye baada ya kuona amepata kazi nzuri. Sor 4 dat, ni hisia zangu na ninaziheshimu!
(kc21p@yahoo.com)
Anonymous said…
Mada yako imenitonyesha sana machungu niliyopitia. Ni hivyo hivyo, nilipogundua kuwa mume wangu anatembea,alinifanyia vituko wewe, basi yakanishinda nikaamua kuwachana naye - na kilichonisukuma haswa kuamua kumwacha ni kuwa, tuna watoto watatu, ndoa miaka 9 na kwa upande wa familia yake yaani ukimwi umewaathiri saana, ndugu zake (yaani shemeji wawili walikufa na ugonjwa huo na wake zao) sasa watoto yatima nikaletewa mimi. Kuangalia dada mtu (yaani wifi yangu)ambaye ni wa kwanza katika familia ya mme wangu walikuwa na watoto 7 - watoto 6 wa kike wakafa ha huu huu ugonjwa akabaki mmoja. Yaani nilivyoangalia hivyo halafu wanangu bado wadogo na tabia ya mumewangu ndio kwanza hajifunzi somo, nikaona chakufia - kikachukua watoto wangu, kwa bahati nzuri nilikuwa na biashara ambayo ilikua inanisaidia saidia, basi tukaamua kutengana. Yeye kidogo anaangalia watoto lakini haswa anataka turudiane eti amejirekebisha.

Dada wacha nikwambie - ukishaona moyo wako umesita katika uamuzi fulani - hata kama familia yako yote itakusihi vinginevyo - wewe shikilia uamuzi wako - nimeona sana tu, wasemavyo wahenga - chui hawezi jibadili madoa doa yake hata kidogo. Kwa hivyo kaa utunze wanao na kama Mungu atataka mrudiane atakuonyesha ishara - Usisahau watoto hawatabaki watoto kwa muda mrefu, watakua na kuwa na maisha yako, wewe utayaangalia maisha yao na kuzidi kujuta tu au hata kufa mapema kwa machungu.
Anonymous said…
Yaani we dada umenikumbusha machungu....
Mwenzio nilisamehe mpaka nikachoka, hawabadiliki ng o. wangu hakubadilika alirudia na kurudia na kurudia nikasema basi kwaheri, nna amani sasa niko mwenyewe na wanangu wanaishi. Kama vipi mpotezee tu.
Anonymous said…
pole sana mama
kwakweli nimesoma na nimesikitika sana kwa hilo lililokukuta na kabla ya yote nakuombea kwa mungu akusaidie akupe akili,fikra,hekima na uwezo wa kutambua zuri na baya
mimi mchango wangu ingawa sijaingia kwenye ndoa lkn nimeweza kutoa ushauri mwingi sana kwenye maswala ya ndoa kitu ambacho kinanifanya mpaka leo nishindwe kuoa kutokana na hizo kesi
USHAURI mi nafikiri huyo mumeo kwa sasa ameathirika na mfumo dume na bado ajatambua nini maana ya usawa kwa wote so ni vigumu sana kumbadilisha na hata ukimbadilisha atakusumbua sana kwavile tayari ameshakuwa na kitu moyoni mwake so its very difficult to accept it
2.somesha watoto watakuja kujua siku moja nani ni mkosa katika hili najua kwa mtazamo wangu tu kuwa awapendi nyie kuishi maisha hayo na kweli sisi km watoto tunakua na msongo wa mawazo unapokuta wazazi wametengana so jaribu mara nyingi kuwapeleka kipindi cha likizo kwa jamaa zako hili km vile mjomba,babu na wengine maana wakija hapo kwako unawatengenizea maswali mengi sana
3.kutoa matumizi na tabia ya mtu lkn kwa ninavyojua mimi ni proud sana kwa mwanaume na hasa huyo wa kwako anayependa mfumo dume kuwasaidia watoto hili aonekane kuwa yuko fiti hasa kipesa kwa watoto
4.jitaidi sana maisha yako usiwe mtu wakupenda kufuata ushauri hasa kwenye mambo ya ndoa maana ushauri mwingi unaweza kukufanya uchanganikiwe watumie sana wale wawili walikuwa mashaidi wako ktk ndoa yaani wasimamizi km mulichukua tu bila kuangalia aina ya mtu basi mi nashauri mfuate mshenga
wako
jm
Anonymous said…
sio wanaume wote wako hivyo nafikiri huyu kazoea kulelewa hakufai huyo wala usimsamehe masharti gani hayo ya wewe kuuza gari na nyumba kuandikisha jina lake achana nae tuza watoto wako
Anonymous said…
Du Hiyo ni kali sana, kwanza kabisa nikupe pole kwa yote aliyokutenda mwanaume mwenzangu, kimsingi amekosea sana kukuacha mwanamke mpiganaji na mpambanaji wa maisha kama wewe, sikusifii ila nasema kweli kwa mujibu wa maelezo yako!!!

Huyo bwana anavyoonekana hana mapenzi na wewe wala watoto wake au ulimbukeni wa maisha ndio unafanya awe hivyo. Kwa mwanaume makini anapokosea kwanza huomba radhi na kutafuta njia za kusamehewa na sio afanyavyo yeye, ana bahati kubwa hajijui tu kwanza amesamehewa pasi na kuomba radhi then yy analeta mbwembwe eti oh hiyo nyumba uliyojenga na gari andika jina langu, anasahau hoja ya msingi kuwa ninyi ni mke na mume mliotengana ambao mnahitaji kuwa pamoja tena!
Dada yangu usiingie mkenge kwa kukubali kuandika jina lake kwenye mali zako ulizochuma kwa jasho lako wakati yeye anakwenda kuhonga huko kama anapenda kuwa na nyumba ajenge yake na gari pia anunue la kwake, usidanganyike eti huyo hata akikubali kurudi muishi wote ukadhani anakupenda yy anapenda mali tu (TAPELI) Ukijichanganya na kumpa nafasi ya kukuingia utabaki kulia na kusagana meno atauza mali na kukuacha kule ulikojitahidi na kuondoka mpaka sasa umefika hapo ulipo!
Kwa kuwa haonekani kukupenda ameshashikwa na wengine wewe mshukuru Mungu na muombe yy akupe faraja kwa hakika atakupa wala usiwe na shaka mamangu!!

Kuhusu suala la kutuchukia wanaume wote hapo unakosea aunt usifuate ule msemeo wa zamani kuwa akioza samaki mmoja ndio wote wameoza hapana ni yy tu jamaa na ulimbukeni wake, pia usiseme kuwa hutapenda tena kwa kuwa binaadamu tumeumbwa kupenda na kupendwa pia hivyo nawe usije ukaikatili nafsi yako omba Mungu upate atakayekufariji na kukujali wewe na watoto wako, pia kwa standard ya maisha uliyofikia maisha bila mume pia yanawezekana aunt! Asikusumbue mtu ambaye hajui nini anataka na nini thamani ya mke na watoto!!! Since yy ndie biological daddy wa hao watoto inatosha kuwa hivyo endelea na maisha yako aunt kuwa jasiri mungu atakuongoza vema wala usitie shaka juu ya hilo!
Nikutakie kila la Heri!

Ndimi Uncle Sam!!!
Anonymous said…
na kweli ndio hawa wanaotufanya tuwe manunda au beijing wanavotuita wao now!!khaaaa iyo eti uandike jina lake na uuze gari?kiboko,,,yani mama ulifanya vizuri tu
Anonymous said…
POleeeeeeeeeeee sanaaaaaaaaaa dada yangu!!

Mimi nikiwa mwanaume, nakusihi usituchukie wanaume,ila mchukie huyo mumeo aliekufanyia upuuzi huo.

Dada hakuna mwanadamu aliemkamilifu kwa asilimia mia.mambo ya vurugu na usaliti yako kwa wanaume na hata wanawake.Ninayeandika hapa ni counselor nimeshughulikia masuala mengi sana ya jinsi yako ambayo mengi yamesababishwa na wanawake.Sikatai kuwachukia wanaume,ila nakuomba usiwajumlishe wote hivyo.Wako waaminifu na wenye huruma sana huwezi kuamini.Wako wanaume wanaotawaliwa sana na wake zao utadhani hakuna mwanaume katika familia hiyo.

Cha msingi dada kwa kuwa umesema wewe ni mcha Mungu sana, nakusihi uendelee kumwomba Mungu na kumtumaini sana ili aendelee kukuonyesha yale yaliyo ya utukufu wake zaidi.

Nakaamini kabisa kwamba sisi wanaume wengi ni wasumbufu na wahalifu.Iko misingi ambayo kina mama wanahitaji kujikita nayo wawapo katika ndoa au familia.Licha ya maelezo yako ya kina ,lakini hatuwezi kumhukumu mumeo kwani hatujui yaliyo ya upande wake.Kutelekeza familia kwa wanaume kunatokana na jinsi wewe mwanamke utakavyokuwa na mawasiliano na huyo mumeo.Kuna uwezekano kwamba mawasiliano yasipokuwepo si rahisi huyo bwana aje hapo kirahisi.najua maelewano hayapo lakini mawasilino kuelezana habari za watoto wanahitaji nini, na wanafanya nini ni muhimu.

hata hivyo nakupa pole sana dada,vumilia kwani huo ni msalaba wa ndoa.Kuna kuyumba na kuna kuyumbishwa.Lakini wewe simama katika mhimili wako imara ili uendelee kutunza watoto wako wasome.

Masharti ambayo mumeo ameyaweka ili murudiane hayana msingi.Hapo huyo mwanaume anatuaibisha hata sisi wanaume wenzake hasa kufuatana na hayo uliyoyasimulia jinsi ulivyomfanyia.Lakini jipe muda,ugonjwa huja haraka lakini kuutibu unachukua muda mrefu.

Ninakuombea Mungu azidi kukupa uvumilivu na kutowachukia wanaume, kwani utafanya kosa ukiwajumlisha wanaume kihivyo kwa sababu ya kosa la mumeo.
Anonymous said…
Pole sana mama mwenye tatizo; ila nakuomba kwanza usiwachukie wanaume wote kwani wapo wanaozijali sana familia zao kama wewe ulivyofanya. Vile vile ukumbuke kuwa wapo pia wanawake wasiofaa kuitwa wanawake lakini bado wanabeba jina hilo zuri la kuitwa ‘mwanamke’. Tatizo si jina, yaani mwanaume au mwanamke, tatizo ni jinsi gani kila mtu anamchukulie mwenzake pamoja na familia nzima. Fikiria, wewe mwanaume au mwanamke unapata raha gani au unajisikiaje unapomuona mwenzako ana patashida au taabu au watoto wanapata taabu; mara leo wakalale kwa baba mara kwa mama? Unaweza ukakuta chanzo ni kitu kidogo tu; ‘kutoka nje ya ndoa’. Kisa? Natafuta tofauti, you wouldn’t see that difference if you cannot find it in your our ‘coordinates – mke/mme’! Unatafuta kitu ambacho hukijui! Kama unakijua basi zungumza na mwenzako ili kama kilikuwa kinapugua basi kiongezwe. Au kama mwenzako alikuwa hafahamu/hajui basi aweze kuelewa. Tumekulia familia tofauti; so we cannot be the same. Ni vema watu tukabadilika, na kumuona mwenzako kama ni mwili wako, kama vitabu vyote vitakatifu vinavyoainisha: Wawezaje kuchukia mwili wako?
Tatizo la kuterekeza familia au migogoro kwenye ndoa litaisha tu, pale kila upande (mwanamke na mwanaume) utakuwa tayari kuvaa moyo wa upendo, kuvumilia, kuheshimiana, kusamehana, kushirikia na kuwapenda watoto. Ni vema vile vile kujiweka kwenye nafasi ya mwenzako yaani kama ambavyo wewe usingependa kudanganywa basi na wewe usidanganye!! Lakini pia tukithamini maisha ya baadae ya watoto wetu, baasi kila kitu kitafanyika kwa manufaa ya kujenga familia. Ni dhahili kwamba hata mme au mke anapokuwa mbali na mwenzake hatafikiria kwamba ‘je mwenzangu anaweza kufahamu habari zangu’; bali atajiuliza je; hili jambo nalotaka kulifanya lina faida kweli kwenye familia (yaani watoto)?

Nadhani upendo wa kweli amabao unaambatana na kumuogopa yeye aliyetuumba ndo tutamaliza matatizo haya kwenye familia zetu. Mama pole, kama tatazo la mume wako lake ni gari na nyumba kuwa kwenye jina lako basi viandikwe jina la watoto, after all, what we posses in our family belongs to our lovely kids.

Naomba kuwakilisha!
Anonymous said…
kc21@yahoo.com. Soma vizuri huo mkasa utaona kasema mtoto alikuwa darasa la pili mwaka 2002 sio sasa hivi. Na dada huyo mumeo achana nae, sababu kama yeye mtu wa karibu hivyo akuonee choyo na wivu kwenye jambo unalohangaikia watoto wenu, kama hiyo nyumba na gari, sisi watu wa mbali tufanye nini? Inshaallah Allah. s.w atakujaalia kila la kheri.
Anonymous said…
nikisoma hii message kichwa kinaniuma, as tuko wengi, na sasa back to beer nipoze machungu!
Anonymous said…
pole sana dada uyo mwanaume anataka akurudishe nyuma kimaendeleo na tayari kakususia watoto kama inawezekana kaa na watoto wako na usimsahau mungu maana hiyo ni michomoko ya shetani na kumbuka kuwa hao wanawake zake ndio wanamshauri upuuzi huo na kumbuka ipo siku atarudi kwako ata kimsahaa zaidi mie naona cha muhimu ni kusali sana na endelea na shughuli zako achana nae anakupotezea muda.
Anonymous said…
Pole sana dadangu kwa yote yaliyokupata. Mimi naomba tu nikushauri kuwa kamwe usithubutu kukubali kuandikisha mali yoyote uliochuma kwa jasho lako kwa jina lake kamwe usije thubutu maana unakuja kujuta maishani, kumbuka haya ni maisha siyo kila siku utakuwa na uwezo huo wa kutafuta so hizo unazopata leo zitakusaidia baadaye wewe na watoto. Suala la kumsamehe mumeo hiyo inategemea na moyo wako but amini moyo ukiutuma hufanya vile upendavyo wewe, but kwa mtazamo wangu wa haraka haraka huyo mwanaume hata nia njema na wewe kabisa ila lengo lake ni kutaka kukufirisi then akufanye uwe mtumwa kwake coz amejaa mfumo dume sana tena wa kizamani sana hata babu zetu hawakuwa hivyo. Fanya yote unayojisikia kufanya but kamwe nasisitiza usithubutu kuandikisha mali kwa jina lake au ushauri wowote wa wewe kuacha kazi ili uwe mama wa nyumbani utatani kufa siku moja kama siyo kujuta, mimi ni mwanaume japo sijaoa but nimeshuhudia matatizo mengi sana ya namna hiyo. Mungu na akusaidie sana kukupa hekima na msimamo thabiti na ujasiri.
Anonymous said…
Dada pole sana.but umekosea kwa kusema unatuchukiya wanaume.sasa je sisi wanaume tutakupa ushauri gani na unatuchukiya?mie ningekushauri ututake radhi kwa niaba ya wanaume.better umchukie mume coz sio wanaume wote wenye tabia mbaya kama ya mumeo.mustayoo@yahoo.com
Anonymous said…
jamani wanaume wamezidi nyie acheni, pole dada we somesha watoto mungu yu pamoja nawe
Anonymous said…
Ha! Pole sana dadangu kwa machungu uliyoyapata. Kwanza ningependa kusema kuwa kila mtu ana reasons zake zinazomfanya atende mambo anayotenda. Lakini kulingana na yale uliyoyasema, nadhani mumeo ana shida ya self-esteem; yaani hajihisi kuwa mwanaume. Nitafafanua zaidi.

Wataalamu wa kisaikologia husema kuwa "primary instinct" ya mwanaume ni kuwa "provider for his family", naye mwanamke ni "care giver". Ukizangatia hayo, si vigumu kuelewa tabia ya mumeo.

Kama ulivyosema, mwanzo wa tatizo hili ni pale mumeo alipoachishwa kazi nawe ukamnunulia gari ili afanye bishara ya taxi. Jambo la kwanza ni kuwa mumeo alikuwa na huzuni maanake hakuna mtu anayefurahia kuachishwa kazi. La pili ni kuwa kazi ya taxi haikumfurahisha pengine kwa sabau ni la kiwango cha chini mno ukilinganisha na kazi yake ya awali. La tatu ni kuwa 'ego' yake ilishushwa hadhi kwani yeye hakuwa "bread winner" wa fimilia tena. Basi, ili apaunguze huzuni moyoni na ajihisi mwanaume tena, aliwakimbilia wanawake wengine (wanaume wengine hukumbilia pombe) hadi akampangishia mwanamke mwengine nyumba kwa vile alimpata wa kumtegemea na ku-boost ego yake.

Mwisho, nadhani uamuzi wako ni wa busara sababu ukiiandikisha nyumba kwa jina lake na ukimpa gari basi utakuwa "at his mercy". Na inaonekana mumeo hana maturity ya kuelewa kuwa cha muhimu ni familia yenyewe sio gari ama nyumba. Pia, inaonekana kuwa hana upendo na uaminifu kwako ama kwa watoto wenu kwani angerudi hata kama nyumba haijaandikishwa kwa jina lake. Mungu akubariki.
Anonymous said…
pole saaana dada yangu kwakweli inaikitisha kuona upo katika hali hiyo,
kwanza; nisingependa useme kila mwanaume ni mbaya coz ya kutendwa na mumeo.
pili;unajua kama wapenz wawili mlikuwa mnapendana kwa dhat mmoja kuja kubadiika ghafla lazima kutakua na sababu iliyomfanya abadilike ghafla ila kwa hapo ni ngumu jua coz tunasoma maeleza ya upande mmoja i mean ww tu hatuja msikia na yeye,
tatu;kuna tabia flan wakina dada wanazo ila sijui wewe mfano mdada akiwana kipato den mumewe kalost huwa na vidharau flan na kumnyima mume nafas yake hapa ulikosea kitu kimoja kama mliweza kudiscus pamoja wakati wa kununua gari na mkakubaliana pia mlitakiwa wakati wa kununua kiwanja mngefanya hivyo pia mununue sehemu wote mngeipenda imagn yy angefanya hivyo nadhan hata ww ungechukia hapo umemuonesha dharau na umemnyima haki yake.
nne;unajua dada hata kama unakuwa bussy wanaume pia tunahitaj muda wakukaa na wake zetu,hili wote munajua hata sisi kama tunakuwa bussy sana na wake zetu wakiwa loose home easy kuwana mawazo ya ajabu.....nimesema hii ni kwa faida ya wote
tano;USHAURI...kwakuwa yy anataka kila kitu kiwe kwa jina lake hapo usikubaliane nae kwa kuwa tayar ameshaonesha udhaifu alionao kuanza kutembea nje ya ndoa,

mwisho;ni vizur kwa wapenz kutoa dukuduku lako lililomoyon kwa mpenz wako ili ajue kama unamkosea kuliko kuamua kuanza na tabia zisizo faa.
asante,
by; mfalme
Anonymous said…
Kwanza nakupa pole ya dhati kwa makubwa yaliyokupata. Kweli kazi ipo, duh! Pili napenda kusema kwamba wewe na huyo mumeo wote ni waajabu sana. Kwanini nasema hivyo? Tukianzia kwako: Hivi ulipokuwa unaolewa na huyo bwana ulikuwa umeielewa vyema Job-Description(i.e. Majukumu) ya MUME ndani ya nyumba? Nadhani hukuielewa na ndio maana ulianza kufanya mambo ambayo alipaswa kufanya mumeo(ofcoz mengine ni ya kimaendeleo) tena kwa furaha kabisa, ukidhani unamsaidia mumeo au ndio kuonesha mapenzi 'ya dhati' kumbe ndio ulikuwa unaangamiza ndoa yako kabisa. Lazima tukubali kwamba majukumu ya mke na mume ndani ya nyumba ni TOFAUTI. Ni jukumu la kwanza kabisa la mume kufanya kazi(kwa bidii!) ili kukidhi haja ZOTE za Msingi za familia yake. Mke ni MSAIDIZI wa Mume katika kupanga mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya kifamilia na pia ni MTENDAJI MKUU wa shughuli zote za nyumbani(it's Kind of old fashioned, but that's Godly fact.) Kama nyumba ingekuwa Serikali basi Mume ni RAISI na Mke ni WAZIRI MKUU. Sikuhizi imekuwa kawaida kabisa kusaidiana na hata kubadilishana hizo nafasi mbili(ndio maendeleo yenyewe hayo au?) Wote mke na mume tunafanya kazi na kuchanganya kipato na kupanga pamoja, na mwenye kipato zaidi ndiye anakuwa PRESIDENT. Technically it sound right... But fact ni kwamba hii inawaathiri sana wanaume wengi kisaikolojia na pia kuwafanya wabweteke na kuona "Hata nikikwama, WIFE atarekebisha mambo." Kumbe mambo huwa hayaendi hivyo katu. Mume ni kichwa cha nyumba, hivyo anapaswa kuiongoza na kuihudumia familia yake na kufanya maamuzi yote ya msingi ya kimaendeleo, na pia hana nafasi kabisa ya kuwa Careless! Women and Children may be allowed to be Careless, but not MEN. Sasa Ujinga wa mumeo ulianzia hapo: Alipoona hana kazi na wewe unauwezo wa kufanya hili na lile, yeye akaanza kubweteka. Hakujua kwa kubweteka kwake na kukaa nyumbani baada muda kutamuathiri yeye mwenyewe kisaikolojia na pia maneno na mambo mengi ya kipuuzi yangeanza kumjia(aidha kutoka kwa ndugu zake, rafiki zake, majirani, house girl au sometimes toka kwako wewe mkewe...maana wewe sio Malaika, lazima umewahi kumjibu vibaya au kuongea kwa mtu au watu juu ya ujinga wake...wanawake wengi hufanya hivyo kwa nia ya kutaka 'msaada wa mawazo' bila kujua kuwa hao watu si wote wenye nia njema.) Nionavyo mimi, matatizo halisi ya mume anayelelewa na mkewe huanzia hapo...jamaa alijiona hana mamlaka ndani ya nyumba(mamlaka halisi huletwa na uwezo wa kiuchumi) na akaanza ku-suffer inferiority complex na kuuona UANAMUME wake unakuwa tested(which is true, if u have failed to provide for and take care of your family, then your maleness is in question.) Hapo ndipo akaanza kufanya mambo yanayopaswa kutarajiwa kabisa kwa mume mpumbavu anaye-suffer inferiority complex kwa mkewe, yaani kutapanya pesa kwa makusudi, kutembea na house girl au wanawake wa nje...akidhani hiyo ni njia muafaka ya kuudhihirisha UDUME wake.) Dada yangu, ungekuwa na akili nzuri ungepaswa kulitarajia kabisa hilo, maana linatokea kila siku kwa watu wote kama mumeo. Pia huyo jamaa ni mjinga kupitiliza, kiasi kwamba alipoutambua udhaifu wako kwake, ameona akuchezee hata ulipojaribu kumrudia tena(na ungerogwa kumpatia hivo vitu, basi ungerudi peke yako nyumba ya kupanga, na hapo kwako angehamia mke mdogo!) Huyo bwana hana mapenzi na wewe kabisa, nina imani hata hamu ya kungonoka na wewe ilimuisha kabisa kipindi kabla hata hamjatengana. Mwanamume mwenye mapenzi kwa mkewe hawezi kuanza tabia za kudai mali za mkewe as if yeye ndiye kaolewa na huyo Mke. Mwisho...Kuna sababu nyingi za kumfanya mume amtaliki mkewe, lakini HAKUNA sababu yoyote ya msingi ya kumfanya mume aitese au kuitelekeza familia yake. Ni MPUMBAVU tu huyo Mumeo. Hebu tafuta mwanamume mwenye akili timamu uolewe naye, nadhani mtaishi vizuri maana sasa umeutambua ujinga wako na utakuwa umejifunza kutokana na makosa. Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. My take.
Anonymous said…
Pole sana. Mwanamume kama ni mwanamume kweli hawezi kuwatelekeza watoto wake. Bahati mbaya kuna wanaume wengi wamaofanya hivyo. Mwanamme mwenye kuatelekeza watoto wake SI mwanamme bali na mse*** na amejiweka katika ngazi ya unyama. Ahmad.
Anonymous said…
Pole sana dadayangu kwa yaliyokukuta. yaani maelezo yako yananipa picha kuwa ulikuwa unamsaidia sana mumeo kiasi kwamba yeye akajiona kama mwanamke na kutokana na hilo wewe ulikuwa huhitaji chochote kwake na kwa sababu ya uanaume yeye anahitaji mtu wa kumsumbua ndio maana akaanza kutafuta wanawake ambao wanamwona yeye ni msaada. mwanaume anataka kusumbuliwa, nataka nguo ya sikukuu, nataka pesa ya saluni na kila kitu mwanaume anachotakiwa kukifanya kwa mwanamke ndicho pekee kilichokuwa kinamfanya awe mwanaume. Mwanamke kama wewe unahitaji mwanaume anaejua kupenda na anaejali sana maana wanawake wengi hawapo tayari kubeba majukumu makubwa ya familia, mimi ningetamani kuwa na mwanamke kama wewe, mke wangu anafanya kazi lakini hanisaidii chochote jamani hivyo wengine wamejaliwa na bwana lakini hawajui.Pole na hongera sana kazana kusomesha watoto wako watakusaidia baadae.