Thursday, 25 March 2010

hivi kusamehe ni ugonjwa? kila akicheat mie nasamehe tu-Ushauri


"Pole na kazi dada dinah,
mimi ni mwanamke wa umri wa kati nina boyfriend wangu ambaye hadi sasa tuna kama miaka 2 na nusu. Nilikutana nae wakati yupo mwaka wa mwisho Chuoni. Wakati huo mimi nilikuwa nimeshaanza kazi.

Nilimvumilia hadi akamaliza Chuo na kufanikiwa kupata kazi Benki akapangiwa kituo cha kazi Wilayani hapa hapa kwenye Mkoa huu tunaoishi. Wakati nakutana na huyu bwana alikuwa ndio ametoka kuachana na demu wake wa chuo, ila kipindi hicho pia niligundua kuwa ana demu mwingine ambaye alikuwa anasoma Chuo mkoani Arusha.

Nilipomuuliza inakuwaje akaniambia huyo mtu ni kama wameachana kwani kwa umbali waliokuwa nao asingeweza kuwa nae tena na ndio maana alikuwa na mahusiano na yule demu wa chuo, Basi nikaamua tu kuendelea nae nikijua atakuja kubadilika kwani tangu mwanzo nilihisi jamaa yangu ana utulivu.

Matatizo yalianza wakati alipoitwa kwenye interview ya kazi, kumbe kule alipoenda alikutana na msichana aliewahi kuwa nae kipindi wanasoma. Kwa maelezo yake ya awali aliwahi kuniambia kuwa yule dada ndie msichana ambae alimpenda sana kuliko wasichana wote aliowahi kuwa nao ila walipotezana.

Sasa aliporudi tu nikagundua mabadiliko kwa mtu wangu, kwanza kwenye simu yake alikuwa ameweka jina langu lakini nikakuta kaweka jina la kwanza la huyo dada, pili nikakuta msg za mapenzi akimwambia huyo dada kuwa yeye ndio mkewe aliepangiwa na mambo mengine yanayoumiza sana moyo.

Mbaya zaidi mimi mwenyewe hajawahi kuniambia maneno kama hayo tangu nimfahamu, basi nikamuuliza kwasababu jina nililolikuta ni kama la mtu yule ambaye alishaniambia je ni yeye ndie amekutana nae huko kwenye interview?

Akaniambia hapana ila huyo ni mtu mwingine ambaye amemkuta hiyo sehemu anafanya kazi Benki na akaomba msamaha kuwa ni bahati mbaya na hatarudia tena. Siku ya mwaka mpya wa kuingia mwaka 2009 tulibadilishana line kwa bahati mbaya. Ya kwake aliiweka kwenye handset yangu basi wakati tupo kwenye mkesha mida kama ya saa 5 nusu hivi.

Nikapigiwa simu na mdada sasa kwa kuwa nilisahau kama line iliyokuwepo haikuwa ya kwangu, nikapokea huyo dada akaniambia anaomba kuongea na mwenye simu, nikmjibu anti simu ni yangu akan'gan'gania nimpe mwenye simu.

Nikakumbuka nikampa simu huyo boyfriend wangu, akaangalia tu no akakata simu alafu akaitoa line na kuitupa simu yangu kwenye moto. Ukweli kile kitu mmii kiliniboa sana nikaamua kuondoka kurudi nyumbani.

Kesho yake akaniomba msamaha na kuahidi kuninunulia smu nyingine, pia ndio akaniambia ukweli kuwa yule dada aliepiga simu ni yule mwanamke wake wa zamani na ndiye aliekutana nae kwenye intrview. Nikamuuliza sasa itakuwaje?akaniambia kuwa yale yalishapita na hawezi kuniacha kwani ananipenda sana.

Nikamuuliza tena nitaamini vipi asemayo? akampigia simu yule dada mbele yangu na kumwambia kuwa hawezi kuwa nae tena ana mtu mwingine hivyo huyo dada aendelee tu na maisha yake.

Nikasahau kabisa dada dinah kuhusu huyo dada na kufungua ukurasa mpya na mpenzi wangu, Ikaja kipindi cha valentine mwaka huo huo, tulikuwa Dar basi huyo dada akapiga simu usiku wa saa kumi wakati bado tulikuwa tumelala, nikaamka na nikapokea mimi akanijibu kwa jeuri kubwa kuwa kwa nini napokea simu zisizonihusu?

Nikamwamsha boyfried wangu kama mara ya kwanza akakata simu, tukagombana sana siku hiyo akasema anamshangaa huyo dada kwa nini bado anamfuata wakati yeye hampendi! basi akanidanganya nikajikuta nimemsamehe dada dinha.

Sasa kilichonifanya niombe ushauri kwa wadau ni hiki,ulipofika mwezi wa 7 nikapata ujauzito nikamwambia mwenzangu inakuwaje mimi naona wakati wa kufunga ndoa umeshafika kwani sitaki kuzaa nje ya ndoa.

Huwezi kuamini alikataa eti yeye hayuko tayari kwa ndoa hivyo mimi nizae tu na yeye atalea mtoto ndoa bado sana, nikamwambia naona sitaweza kuendelea kufanya mapenzi na yeye tena kwani hayupo tayari na mimba nitatoa siwezi kuzaa nje ya ndoa tena hasa ukizingatia siku za nyuma nilishazaa nyumbani wazazi wangu watanielewaje?

Basi tukawa na ugomvi mkubwa kwa kweli na sikwenda kumtembelea tena kama kwa miezi 2 hivi na hata mawasiliano yakawa hafifu sana. Sasa nahisi kipindi hicho ndio alikitumia kufufua tena mahusiano na yule dada.

Siku moja nikatumiwa msg na rafiki yangu kuwa anamuona mtu wangu na mwanamke nyumbani kwake je nimeachana nae?kama naweza niende nikahakikishe mwenyewe! Kweli nikapanda gari nikaenda nikamkuta huyo dada nyumbani kwake, sikumuliza kitu huyo dada nikamfuata huyo bwana ofisini kwake nikamuuliza akanijibu kuwa yule ndio yule dada niliekuwa namsikia mwanzo.

Nikamwambia vipi kuhusu mimi? akanijibu kuwa yeye hajui na majibu mengine ya kifedhuli tu, siku hiyo nililala guest da dinah,baada ya hapo alikuja nyubani kuniomba msamaha nikaamua kumsamehe, ila tatizo ni kwamba amekuwa sio mwaminifu kwani siku ya valentine nilimkuta tena na mtu mwingine akimlalamikia kuwa hamuelewi bora aachane nae kwani haoni faida ya kuwa nae.

Nikamuuliza ila majibu yake bado hayaeleweki na hataki kabisa tuachane, naomba ushauri kwa wadu nifanyeje?

Dinah anasema: Pole sana kwa usumbufu unaoupata Mdada, maelezo yako yanafanana sana na ya Binti mmoja wa Kikoloni nilikuwa na-share nae nyumba nilipokuwa Chuoni. Binti alikuwa na Bf ambae alikuwa anamtreat kama unavyofanyiwa wewe. Wakati mwingine wanawake aliolala nao jana yake wanampigia simu yule Binti (my housemate) nakuwambia kuwa walichokifanya na jamaa, binti anakuja kwangu na kulia.

Lakini kila nikimpa ushauri wa kuweka miguu yake chini na kumpa ukweli jamaa, binti anaomba kuonana na jamaa, ile njemba imefika tu inaanza kumfokea, wanagombana wee kisha wanaishia kufanya ngono as unasikia kukurukakara zao huko chumbani.....akitoka hapo naenda kuchovya kwingine....kesho yake binti anasamehe.

Nikachoka kuliliwa nikaamua kumwambia ukweli kuwa, jamaa yako anajua kuwa wewe unampenda kwa dhati na anauhakika wa kusamehewa kwa makosa na uchafu wake wowote atakaoufanya, kitu ambacho mwanamke mwingine yeyote hawezi kufanya. Ili kumuonyesha kuwa unathamani kubwa kuliko anavyodhania mtose bila kumwambia.

Nikamwambia kuanzia sasa mchunie, badili mawasiliano, badili kitasa cha mlango, anza kujichanganya na watu wengine, ndugu,jamaa na marafiki yaani keep busy na maisha yako......... Hivi ndivyo nitakavyo kuambia na wewe Binti mrembo.

Mwanaume akikutenda kwa kuwa na wanawake wengine kabla hamajafunga ndoa na ukamsamehe ni wazi ataendelea kufanya hivyo akijua atasamehewa tena na tena, sasa unachotakiwa kufanya hapa ni kutoka Nduki (achana nae) kabla hujapewa HIV.

Huyu mwanaume hakuthamini, hakupendi, hakuheshimu na hana mpango wowote wa kuishi na wewe maishani mwake, Mshukuru Mungu kuwa aliweka wazi hilo mapema pale uliposhika mimba, katika hali halisi siku hiyo ndio ilitakiwa kuwa mwisho wa uhusiano wenu.

Hataki muachane sio kwa kuwa anakupenda.....ni kwasababu anajua wazi hakuna mwanamke yeyote hapa Duniani ambae anaweza kusamehe unayomsamehe wewe, uko hapo ili kutumiwa kama back up! na si vinginevyo. Mpe buti la meno huyo hakufai kabisa.

Wachangiaji wamesema mengi mazuri na haya yangu kwa namna moja au nyingine yatasaidia kum-buti huyo looser!
Kila la kheri.

20 comments:

Anonymous said...

kusamehe ni kuzuri sana pale inapotakiwa na pale ambapo kosa halirudiwi tena, dada open ur eyes unadanganywa na kuchezewa nakuonea huruma muda wote huo anakufanya mjinga unasubiri , natamani ningekujua nije kukutoa huko , una ugonjwa wa mapenzi , unahitaji tiba fungua macho kimbia , utapata mwanaume mwingine hivi kwa nini mtu akuumize hivo akuchezee , na huoni jamaniiii ni nini kinawapata akina dada wake up , usikubali kunyanyaswa , if he is not the right man wait u will get the right man , usipopendwa utapendwa pengine dada.

Anonymous said...

Dada, fumbua macho uone na fungua masiki0 uweze kusikia ujumbe anaokupa huyo boyfriend wako! Kwa nini unahangaika na mtu asiyekupenda kwenye zama hizi za gonjwa la ukimwi? Hata nyakati hujui kusoma; ama kweli binadamu tu watu wa ajabu?? Yaani wewe endelea kufumba macho; utajikuta kaburini!

Kwanza mimba ulitoa ua ulizaa? Kama ulitoa unayodhambi kubwa!!!

Anonymous said...

Pole mwana! Mhhhhhhhhhhh ama kweli yaani sipati picha kwa story hii!!

Mimi kama mwanaume nashindwa kuuelewa uvumilivu wa huyu dada. Kama ulivyosimulia ndivyo ilivyo kweli, nakushangaa inakuwaje uendelee kumvumilia kiasi hicho kama vile yeye amekuoa? Yaani pamoja na vituko hivyo bado unasamehe? au umefuata vifungu vya biblia kusamehe saba mara sabini?

Kwa jambo kama hilo hakuna msamaha kama huo.Kwanza hapo uko gizani mno.Kumbe ulizaa mwanzoni nje ya ndoa, na bado unarudia kufanya kosa lilelile la kutombwa bila hata kinga? Hivi ulifikiri hizo shahawa zitaingilia mlango mwingine?

Hata unaposema hutaki kuzaa nje ya ndoa, je kutombwa nje ndoa ndiyo halali?Mbona unachezea maisha yako hivyo dada?Je una wasiwasi kwamba hutapata mwanamue mwingine ukiachana na huyo jamaa ambaye anakuchezea usanii hivyo?

Je tukushauri vipi dada wakati jibu lipo wazi kabisa?Kuna cha kukushauri wakati mambo yako bayana mno wala huhitaji kuuliza mtu.Jamaa amekukataa kukuoa na bado unajua ana mademu kibao.

Nakushauri kimbia haraka sana nenda tu kazae huyo mtoto wala usitoe kwani uliyataka mwenyewe ukiua kiumbe hicho damu itatakiwa mikononi mwako.Ulifanya kosa na bado unarudia kosa lilelile?

Kina dada jamani hivi bado hamjafunguka akili katika dunia ya utandawazi hii?Kama umechukua na mimba si ajabu na gonjwa kakwambukiza.

Anonymous said...

dada!
mimi ni mwanamke na nimesha wahi kupata mkasa kama wako way back nikiwa bado cumpus kwa wanaume wawili tofauti wangu nilidhani nina nuski na nilipoteza faith in life kabisa but from all that experience nimefifunza kuwa mwaume mtumzima hashindwai kufanya maamuzi hivyo basi kama anaendele na mambo ambayo anjua si mema basi ameamua na huwezi kumzuia maana utamfunga kengele? mimi nili take time out kama mwaka bila ya kuwa na mahusiano baada ya hapo nimekuta na kijana wa kawaida tu tunapenda na kusukuma gurudumu la maisha pamoja.
mwisho, jibu la tatizo lako unalijua ila wewe unaogopa tu mrembo.

de'victorious said...

Achana nae coz hakupendi nakupa live dada coz yamewahi kuntokea kama hayo na huwa hawaachi hata akikuoa akakuweka ndani ataendelea hvo hvo cha msingi mu ignore fany amambo yako.....achana nae atakuja kukufanya kitu kibaya huyoo hutokaa uamini......achana nae jamani atakutesa tuu huyo,.....

Anonymous said...

binti pole kwa yalokukuta,ila nakushauri uchukue ustaarabu wako utaambulia magonjwa buuure,kama yeye alikupenda amini yupo atakayekupenda na kukuthamini zaidi ya huyo,embu anza naq life yako mama isitoshe una kazi .wanaume wapo wengi,tulia

Anonymous said...

hey hey hey mdogo waku wakeup!!!

maisha siyo ya kuchezea, huyo mtu wako sio mwaminifu na wala sio mkweli, angalia UKIMWI upo na unamaliza binadamu siyo mchezo

kwanza ujatuambia ile mimba bado unayo au uliitoa???

kama unayo gagamala uzae maisha yatasonga na kama ulitoa mwombe Mungu wako msamaha na usirudie tena, kumbuka kutumia zana unapokutana na mwenzio.

achana na huyo mwanaume atakuua bila sababu, mwombe Mungu wako akupe mume mwema aliekupangia kuwa wako.

Lisa said...

Pole dada, ila kwa mtazamo wangu huyo hakufai na wala hana mpango wa kukuoa.

Najua si rahisi kumuacha hasa kama unampenda sana, ila akili kichwani mwako, chagua kusuka au kunyoa, nionavyo mimi huyo atakuliza kila siku na mwisho wa siku hata kuoa vilevile.

Anonymous said...

nakushauri achana nae kwani haelewi anachotaka! USIPOTEZEE MUDA WAKO KWAKE KAMA HATAKI KUPROPOSE NOW ACHANA NAE. Kuna mwanaume utakutana nae na atakupenda na kuheshimu maamuzi yangu mama.

Anonymous said...

Mh, pole mwana dada inavyoelekea huyo mwanaume ni muhuni tu wa mtaani, na bado ana akili za kivulana za kutamani tamani tu wasichana. Muda wake bado wa kuseto kama mume (kama unavyotaka wewe awe mumeo) haujafika. Bado ana mambo yale ya kubadili wasichana. So minakushauri achana nae, na kama hiyo mimba bado ipo wala usiitoe maana ndo ilivyopangwa iwe hivyo maadamu amesema mtoto wake atamtunza usijali. Hata kama atashindwa kukusupport katika kumtunza utajitahidi mwenyewe kumsaidia mwanao. Pole sana shoga yangu ndio walivyo wanaume wengine anataka akutumie tu then akuache kwenye mataa. Ushuri wangu achana nae na msamehe lakini usirudiane nae tena!!

Lily.

Anonymous said...

Nakumbuka wimbo wa

akufukuzae...
hakuambii toka,
utaona mambo yamebadilika e!
.....
Jamani mimi kina dada wengine kwa kweli nawashangaa sana... Hivi unataka uone nini tena ndio uthibitishe kuwa huyo jamaa anakuchezea na kwamba hana mapenzi na wewe? yaani uone msg, usikie simu za mwanamke usiku na akuthibitishie kuwa anaempigia ni mwanamke, akudhalilishe kwa majibu yake, akupe mimba asiwe na commitment ya kuwa mume, umkute mwanamke mwingine kwake akupe majibu ya kifedhuli... na bla bla bla


Yaani hapo bado unatuuliza swali la ufanye nini? Nafikiri si kila mtu ana common sense. Ungekuwa nayo hata usingeruhusu mimba iingie. Kwanza na kumuona hana uaminifu bado unakwenda nae pekupeku...

BIG POOLE kwa kutokujionea huruma. jamani wanawake tujipende tusionekane kama tuko desparate sana kutaka kuolewa. Mtu anakubabaisha achana nae. Anza maisha upya. Pyuuu

Anonymous said...

My love sasa unasubiri nini hapo? au haya maradhi yaliyojaa? jamani hivo bado wasichana tuna akili ya kudanganywa kitoto tu? lol too sad! achananae mkimbie huyo utampata tu wa kwako mwenye mapenzi na utajilaumu kwann umechelewa kwa huo mhasherati!
Be strong nothing impossble acha kujiliza, futa vumbi anza safari mpya mama! kila la kheri

Anonymous said...

Pole sana, ila nakushauri uachane na huyo bwana maana kama si ukimwi utakufa kwa pressure. Inaonekana unampenda sana huyo jamaa ndo maana anakufanyia hivi anajua utasamehe tu kama kawaida yako, pia nadhani hataki kufunga ndoa nawe kwa kuwa umeishazaa huko nyuma. pia hujaeleza kama bado una hiyo mimba au umeitoa. Atakusumbua sana na utakosa raha ya ndoa kama kaanza kukuambia maneno mabovu hivyo. Pia ana kichaa kidogo sasa hiyo simu kwanini aliitupa motoni !

Anonymous said...

usilazimishe kupendwa wakati hupendi dada yangu nakuonea huruma sana sababu unapmenda ila yeye hana habari achana naye kabisa utazidi kuumia m.mungu atakujaalia utapata mwingine, kwani huyo kaka hajatulia hivyo hajakuoa akikuoa utaumia zaidi ya hapo, kama unafanya kazi kuwa busy na kazi yako mdogo wangu wanaume hawasadifiki,

Anonymous said...

kwani unachotafuta kwake nini?

Anonymous said...

Dada nashukuru umekuja na swali lako wakati mzuri sana. Huyu kaka kasha kuambia hataki kuwa na wewe ila wewe ndo husikii. Mie nilikuwa na mtu karibu kwa muda wa mwaka, tukiwa kitandani anasema ananipenda ila tukikutana nje ananitambulisha kama rafiki yake na anasema hawezi kumwambia mtu i love you na hayuko tayari kuwa kwa mahusiano. Unadhani nilisikia kuwa anasema ananihaji kwa ngono tu wala nikawa nasema labda hataki watu wajue uhusiano wetu mbaka pale nilipo mkuta na mwanamke live.Kumuuliza anataka tuachane anasema hapana ila hawezi kuahidi kuwa yule mdada mwingine niliye muona naye atamuacha, upo hapo? Huyo kaka hatakaa abadilike kamweeeeeeee hata upite msamaha wa rahisi wewe wahi zako mbele utapata mtu anaye kupenda kwa dhati na ambaye hata kuletea vituko vya madharilisho kiasi hicho.vunga vilivyo vyako mapemaaaa, mwenzio nimefunga vyangu ilimradi nina heshima yangu kuliko kujiletea magonjwa bureeeeeee.

Anonymous said...

Bi dada,penda unapopendwa.nikupe siri moja ya mwanaume,as long as atakuwa hajapata wake wa moyo,hizo ndo dalili za mwanaume msela haswa,na kwa kuwa wewe unatafuta ndo mkimbie kama ibilisi.muda wake wakutafuta mke ukifika atakuwa ameshakuchoka na utaona kifaa kipya kinaingia na utajuta misamaha yako,Nilichogundua kwako ni kwamba uko sensitive si ajabu ndo maana jamaa anaogopa kesi za labda utajiua,at the same time ukweli haufichiki,uzalendo unamshinda lazima atoke nje.maana unakae nae bila ridhaa yake...hajasetle.KWA KIFUPI WE NI KIKANGANGANIZI.ILA MESSAge alishadeliver kwako mara kibao kuwa hakutaki ,we unazidelete kwa kisingizio cha msamaha.KAMA HUMUACHI HUYO JAMAA KUANZIA DAKIKA HII KWELI UMEJICHOKA.lucy

Anonymous said...

Wewe!! Wenzio huwa wanasamehe na kusahau kabla hata ya kuombwa samahani!! Na m2 kama huyo usikubali kurudiana naye, we mradi ushamsamehe kwa aliyokutendea basi inatosha huna haja ya kurudiana naye. Huo mchezo wa kuigiza unaofanya utalia kilio cha mbwa mdomo juu cku ukiambiwa hilo jamaa lina ngoma, utadata mi nakwambia. Mkimbie huyo jamaa ni nyoka mkali mwenye ngozi ya kondoo

Anonymous said...

MDOGO WANGU,,MI NAKUOMBEA KWA MUNGU AKUFUNGUE MACHO..EBU KASIKILIZE ULE WIMBO WA JAY DEE, BINTI AMKA UBADO MREMBO..

Anonymous said...

khaa!! huyu kwl kajaaaliwa uvumilivu, ningekuwa wa kiume ningemuoa bureeeeeeee!