Wednesday, 10 March 2010

Alinitenda na rafiki yangu, sasa niko Ughaibuni anitaka tena-Ushauri

"Habari za kazi dada dinah, Mungu akubariki sana kwa kuanzisha uwanja huu wa ushauri kwa watu wenye matatizo, kwa kweli kupitia Blog hii watu mbalimbali tumeweza kuelimika. Nami kama walivyo tangulia wenzangu kuomba ushauri nami naomba ushauri wako na wachangiaji wengine wote kutoka na tatizo hili linalonisumbua.

Mimi ni mwanamke nilikuwa na mwanaume naishi nae kwa bahati nzuri tukabahatika kupata mtoto mmoja, mapenzi yetu yalivunjika baada ya mpenzi wangu huyo kutembea na rafiki yangu mpenzi. Mwanzo wa mapenzi yao nilikuwa naletewa taarifa na watu wa karibu yangu lakini kutokana na kumuamini sana huyo jamaa na rafiki yangu nikawa napuuza nikijua ni maneno ya watu tu.

Lakini siku moja ndipo nilipokuja kupata ukweli baada ya kuzikuta msg za mapenzi kwenye simu yake. Mimi katika kupata ushahidi nikatumia zile msg dada yangu, baadae mpenzi wangu alipokuja kujua kuwa nimegundua hakuonyesha hata dalili ya kuomba msamahaa na siku moja tukagombana sana mbele ya mama yake mzazi kuhusiana na suala hilo na katika kunionyesha ujeuri akazungumza mbele ya mama yake kuwa hawezi kumwacha huyo rafiki yangu.

Mimi sikuona sababu ya kuendelea kuwa nae ikabidi niondoke. Baada ya hapo akaamua kuhamia kwa huyo rafiki yangu na kuishi nae kama mke na mume, Mungu si athuman nilikaa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu bila mpenzi wala rafiki wa kike kutokana na jinsi nilivyotendwa.

Baada ya hapo nikapata rafiki wa kiume ambaye alionesha kunipenda na kutaka kunioa lakini kwa vile nilishatendwa nikawa makini, huyo rafiki wa kiume nimefahamiana nae kwa muda wa miezi mitatu tu nikapata safari ya nje ya nchi na kipindi chote cha miezi mitatu sikuwahi kufanya nae mapenzi.

Rafiki huyu wa kiume aliniambia kuwa anataka kunivisha pete ya uchumba kabla sijaondoka, lakini hadi naondoka hajatimiza ahadi yake nami sikutaka kumkumbusha. Sasa baada ya kuwa huku nje yule mwanaume wa kwanza ameanza kunibembeleza eti turudiane na kwamba yeye alifanya vile kwa bahati mbaya.

Huyu rafiki yangu mpya nae ambaye tulipanga kufunga ndoa nitakaporudi nae amepata safari ya kwenda nje kulinda amani kwani yeye ni Mwanajeshi na tangu alipopata taarifa hizo za safari hajagusia tena nia yake ya kunivisha pete ya uchumba, hadi sasa nashindwa kujua la kufanya, sina uhakika kama huyu mpya anania ya kweli nami au nirudiane na yule wa zamani ambaye kwa watu wa karibu wananiambia kuwa bado wanaendelea na yule rafiki yangu.

Naombeni ushauri wenu ndugu yangu na wachangiaji wengine kwani nimechanganyikiwa. Watinga"

Dinah anasema:Tubarikiwe wote Watinga, asante sana kwa ushirikiano wako. Huyo baba mtoto wako hafai kabisa na futa wazo la kurudiana nae kwani hakukuheshimu na wala hakukuthamini sio tu kama mpenzi wake bali mama wa mtoto wake na akakutenda na rafiki yako.


Kama ulivyosema mwenyewe alipogundua kuwa umejua uchafuzi wake bado hakuonyesha kujutia makosa yake, hakuomba msamaha na badala yake alionyesha kiburi. Mimi binafsi naamini kuwa kama mtu anakupenda kwa dhati kamwe hawezi kukuumiza na ikitokea mnashindwa kuelewana kwa sababu zozote zile na mmoja wenu kutaka kuondoka.


Lazima mtu huyo (mkosaji) atapigania penzi lake kwa kuomba msamaha, kujutia makosa na kuahidi na kuhakikisha anabadilisha mwenendo wake na ikibidi kuwekeana "sheria" hasa kama wewe ulietendwa unataka kuendelea na uhusiano. Uamuzi uliochukua ni wa busara hasa ukizingatia hamkuwa kwenye ndoa hivyo hakukuwa na suala la kupoteza muda kujiuliza shold i stay...should I go?


Siku hizi nasikia wanaume wa wetu wa Kibongo wanapenda sana kutumia wanawake kiuchumi, akijua tu umefanikiwa kimtindo au uko nje (as wanaamini kuwa Ulaya = kupata senti kiurahisi) basi Exes wengi hujaribu sana kujipendekeza kwa kujidai kuwa wanataka kuoa au kurudiana na wewe kwa vile wanauhakika ulikuwa unawapenda hivyo utakubali haraka kurudiana nao. Lakini ukweli ni kuwa hawana nia na wewe bali wanataka kukutumia nahuko waliko wanaendeleza mahusiano na wanawake wengine.


Muda uliochukua kupumzika (kuwa nje ya uhusiano) unatosha kabisa kwa wewe kuwa tayari kujaribu tena uhusiano wa kimapenzi japokuwa, lakini miezi mitatu ya kuwa kwenye uhusiano mpya ni mapema sana kwa wewe na yeye kupeleka uhusiano huo kwenye level ya juu ambayo ni uchumba kuelekea Ndoa.

Huyu Mpiganaji huenda anania njema sana tu na wewe lakini baada ya kutumwa kwenda kulinda amani huenda imeingilia mipango yake hasa ukizingatia kuwa wewe uko Ughaibuni. Kuna mawili-matatu huenda yalikuwa yanasumbua akili yake Moja ni kukuchumbua na yeye kupoteza maisha by doing that atakuwa amekuumiza sana kuliko akijifia bila kujicommit kwako kama mume wako wa baadae.

Pili huenda amepoteza ile hali ya kujiamini baada ya wewe kwenda Ughaibuni, amekuwa na wewe kwa muda mfupi sana hivyo ni rahisi kwako wewe kama mwanamke kubadilisha mawazo mara baada ya kukutana na wanaume wengine Makini huko Ulaya.


Kama unampenda kiukweli huyu Mwanajeshi basi mimi nakushauri uendeleze urafiki ambao ni a bit special kwa vile mnapendana kimapenzi hii itawasaidia sana wote wawili kujua nini mnataka out of uhusiano/urafiki wenu na Mungu akijaalia kila mtu akamaliza shughuli zake huko aliko na kurudi Nyumbani basi mtaungana na kuwa full time wapenzi na hata ndoa kama mtapenda iwe hivyo.

Hapo hakuna cha kuchanganyikiwa wala nini, ni uamuzi tu. Kama unataka keep urafiki na Mpiganaji au achana nae uanze upya pale utakapo kutana na mtu mwingine aliekua na kutulia kiakili.

Natumaini ushauri wa wachangiaji na nyiongeza ya maelezo yangu yatakuwa yamekusaidia kufanya uamuzi wa busara.

Kila lililo jema!

20 comments:

Anonymous said...

Huyu mpya hana msimamo achana nae. Tulia kwanza ujue unataka kufanya nini. Na huyoo wa mwanzo aliyekuacha kwa sababu ya rafiki yako si mwaminifu na hujui nakuletea nini kiafya. Sidhani kama sasa hivi akikurudia ndio atakuwa kabadilika. Kwa kumuonyesha kwamba wewe si wa majaribio usirudiane nae. Mi ningemuuliza wakati ule uliniona sifai, iweje sasa ninafaa? kuwa na msimamo mtu asiku take for granted kwamba you will always be there kwa ajili yake. Akikutenda tena unaweza ukatamani kunywa sumu sababu utajiona ni mjinga sana baadae.

Anonymous said...

Achana naye huyo hana mapenzi ya kweli kwani atazidi kukuumiza. Tulia Mungu atakupa mwingine. Kuhusu huyo mjeshi kuwa na subra labda ana nia lakini kuwa makini wanaume wengi ni matapeli. jane. Arusha

Anonymous said...

mambo vipi dada yangu? pole sana kwa matatizo yaliyokupata, kwa kweli sio siri nakupongeza haswa kwa moyo wa ujasiri ulionao kwani ingekuwa mimi ninaependa kisasi duh zijui ingekuwaje, kikubwa ninachokushauri hebu tulia kwani mpaka hapo Mungu bado hajakuandalia wa kukuoa kwani yule wa kwanza kama kaweza kutembea na rafiki yako kipenzi ipo siku atatembea hata na ndugu kwani tabia haina dawa na wala haibadiliki ipo kama ngozi, nakushauri achana nae kabisa yaani haukufai hata kwa bahati mbaya amini usiamin anajifanya anakupenda sasa hivi kwa sababu mambo yako yapo safi,kama kaweza kukuumbua mbele ya mama yake ipo siku atakuumbua mbele ya halaiki ya watu, na huyu mwanajeshi wewe kauka tu umsikilizie kama kweli atakuwa ameandikiwa kwa Mungu ili awe wako basi atakuwa tu na kama sio basi Mungu atakusaidia tu na utampata.

Anonymous said...

Dada pole kwa yanayokusibu. Kwanza nakupa precaution kuwa waogope sana wanaume wote kama nyoka mwenye sumu kali. Wanaume wengi wanatabia ya kuja kwa kujivika ngozi ya kondoo na kumbe ni mbwa mwitu wakali kabisa. Maneno yao ya mdomoni mara nyingi c kilicho ktk nyoyo zao.
Ushauri wa bure ni kuwa mkimbie huyo man anayejivika ngozi ya kondoo kwa kusema at anakupenda tena, kumbuka hata kabla hajakutenda alikuambia hvo hvo kuwa anakupenda na hato kutenda, lakini hatimaye alikutenda. Jambo la msingi kabisa ambalo napenda kukuhusia ee dada yangu ni kuwa, USIOGOPE WALA USIVUNJIKE MOYO kwakuwa furaha yenye nuru i mbele yako yaja nawe hujuwi, uvumilivu wako ndiyo silaha yako. Usikimbilie kuolewa kwakuwa ndoa yaweza kuwa ni pepo ya duniani ama ni shimo ktk mashimo ya kuzimu/jahanamu. Badala ya furaha unaweza kuwa m2 wa kulia kila cku.
Usiwe na wasiwasi wala usiwapapatikie hao jamaa, just wait, mpenzi hapatikani kwa manati, mpenzi wa kweli yu aja mwenyewe tena Mungu atakuongoza na atakuonyesha wala huhitaji kumsujudia m2 ili akupende, ujue kuna miji2 yapenda kuabudiwa ndo ikuwowe, mishetani hiyo.
Tatizo tunalazimisha ndoa za haraka na wapenzi wasio na mapenzi ya kweli. Ipo cku utampata mpenzi wa kweli na utafurahi na kulia machozi ya furaha na kumshukuru Mungu. Utajisemea mwenyewe laiti ungalijuwa kama huyu ndiye mpenzi wa kweli basi ucngethubutu kuhangaika na kuingia ktk mapenzi yenye utata, na ungelimsubiri for the last days. Ba bye dada.

Anonymous said...

Huna sababu ya kuchanganyikiwa! Usikubali kurudiana na huyo mzazi mwenzio! Lazima atakuliza tene na mara ya pili itakuwa kubwa zaidi!

Anonymous said...

Hivi kwanini sisi wanawake ni wapumbavu sana...kwani dada hauoni ukweli uko wapi hapo?kwanini tukipenda tunakua kama vipofu au makondoo.tena afadhali hata kipofu jamani...Huyo katembea na rafiki yako bado tu unamtaka,mpaka atembee na dada yako ndio ujue kua hakufai...si huyo mwanaume wala rafikiyo wa kuchekewa,wasamehe ila usiwape nafasi, SALI NDUGU YANGU MUNGU ATAKUPA YULE ALIEKUANGIA UWE NAE MAISHANI.

Anonymous said...

Achana na huyo wa zamani, hata mkirudiana hutaweza kumuamini 100%,atakusumbua tu, na isitoshe ushasema bado yupo na huyo mwanamke wake ( shoga yako wa zamani) sasa kwako anataka nini kama si kukunyanyasa tu...huyo wa pili ana majukumu mengine, hata hamjajuana tabia, mtafunga ndoa vipi? cha maana tulia utapata wa kwako , Mwenyezi Mungu atakujaalia, Muombe Mungu and go and meet new people.

Anonymous said...

Huyo wa mwanzo wa nini? Mtu alikutenda tena katembea na rafiki yako wa nini tena? Ningekuwa mie wala tusingekuwa na mawasiliano kabisaaaaaa maana alikufanyia ushenzi wa hali ya juu.

Anonymous said...

Je huyo jamaa yako(Mumeo wa kwanza) alikuwa wa ndoa kamili yaani iliyofungwa kanisani,msikitini au bomani?

Nitatoa ushauri wangu mara utakaponijibu swali langu.

So Much said...

Dada mimi nina swali moja dogo tu,yanini umrudie huyo wa zamani?!kwanini alikuacha?!sasa umabadilika umekuwa malaika ama?!Amka kuwa na msimamo.Muonyeshe wewe ni mwanamke thabiti na unajiamini.Achana na wote hakuna mwanaume hapo.Huyo wa zamani mwambie wewe ni yule yule hakuna ulichobaidilika kusema wewe sasa sasa ni malaika.
So Much

Anonymous said...

dada mbona majibu unayo mwenyewe, hakuna mwaume hata mmoja mwenye mpango na wewe kati ya hao wanakudanganya, fight for your own life pamoja na mtoto wako. Mwanaume mwaminifu atakuja subiri usiwe na haraka

Da Fai

Anonymous said...

acha ujinga, achana nao wote, hakuna muoaji wala mvalishaji wa pete ya uchumba. kaa tulia zidi kumomba mungu atakupa mume bora, hao wote mabwege, na hilo limwanaume lililokuwa linatembea na rafiki yako anataka akurudie kwani umebadilika nini? acha ujinga huo, endeleza maisha yako lea mtoto wako.

Anonymous said...

dont you dare kurudiana na huyo mwanaume wako wa kwanza if he is capable kutembea with your best friend atakuja kukuumiza vingine vikubwa zaidi, mamii mie yamenikuta bt hakufanikiwa kutembea nao coz my friends aliniambia tena mie alikuwa anawataka rafiki zangu wawili na wote wakaniambia, cn u imaging inavyouma nikapiga moyo konde nikachapa mwendo kila cku ananililia eti anataka turudiane tena anakuja na gia anataka anioe nimemkimbiza, na huyo mwingine asikuchanganye wanaume wapo na bila sisi wasingeishi so jua kwamba yupo wakwako anakuja nakushauri live your life,enjoy coz your beautiful my dia life is too short,have fun with your gals,mens are so..........yaani achana nao kabisaaa

Anonymous said...

Mhhhhhhh kweli nimeiona hasira ya wadada hapa imewaka maana kelele zilizopigwa kuchangia ushauri hapa ni babu nene hasa.

Kumbe wadada ni wachangiaji sana pale tu wanapoona anayelalamika ni wa jinsia ya kwao.Lakini akilalamikiwa wa jinsia ya kwao wanafyata mikia.

Pamoja na hayo nami kama mwanaume ningekushauri dada utulie wala usipaparike na mwanaume yeyote hapo.Huyo mjeshi endelea tu kuwasiliana naye na hatimaye utaona reaction yake itakuwaje.Lakini cha msingi usiharakishe kusaka mwanaume utaingizwa mkende maana watu wakijua stori ya mtu kama yako ni rahisi kukuingizia gia ya kukuwin soon.

Kina dada msikasirike mno na wanaume, kwani hata ninyi wapo wasumbufu na wasanii kwelikweli, tena usiombe mdada akufanyie ujeuri mwanaume utajiua kabisa kwani huwa wajeuri hasa.Ni humuhumu kwenye blog hii tumeshuhudia wanaume wakilalama na wapenzi wao kuwa hawaeleweki.

Kila la heri huko ughaibuni dada kula dafu za huko sijui uko ughaibuni ya wapi tungetonyana labda mambo yangeiva hukuhuku.

Anonymous said...

Du!! wadada wakali humu jamani,kina dada mbona mmekasirika sana?? mwenzenu atakosa mwanaume!!

Kuna mdada umekashfu sana wanaume, nakuonea huruma, bila shaka wamekuchakza sana.Pole sana dada,ndiyo dunia hii ya utandawazi. ukibeza wewe wengine wanasema nimpate wapi na lini!!

Anonymous said...

SASA WEWE UNANCHEKESHA USHAAMBIWA KWAMBA HUYO MZAZI MWENZIO BADO ANAENDELEA NA RAFIKI AKO,HLF ETI UNAOMBA USHARI UMRUDIE AU HEEE.....achana nao wote ishi maisha yako utapata mwingine...tena hyo mzazi mwenzio ndio usimfikirie kabisaaaa....chonde chonde....ukimkubali huyo mzazi mwenzio...utarudi hapa kuomba ushauri....

Anonymous said...

pole bibie kwa yote yalokupata. Mimi nasema labda kama kuna maelezo mengine umetuficha, but kama ni hayo tu tena ya ukweli basi huna haja ya kupoteza muda wako kwani hakuna mkweli hapo wote hao ni matapeli, uwe na subira utapata wa kwako aliye mwaminifu na mwenye mapenzi ya dhati, mpe Mungu nafasi atakuonyesha aliye wa kwako ambaye utafurahia naye maisha ya ndoa yaliyojaa mapenzi ya dhati milele mpaka kifo.

Chaoga said...

huyo wa pili kuna uwezekano mkubwa sana ana nia nzuri na wewe ila tu kutakuwa na kitu kidogo tu hapo kinawatenganisha na hasa nahisi itakuwa wewe kutokana na maumivu uliopata kwa mzazi mwenzio hukumuonyesha asilimia 100 ya upendo huyo mlinda amani wetu. na huyo mzazi mwenzio usirudi kamwe kwake kakudhalilisha kwa mashosti zako....

Anonymous said...

jambo la msingi unatakiwa uwe na msimamo wako kama msichana sio unakurupuka tu katika kufanya maamuzi,halafu unaonekana bado unampenda huyo mzazi mwenzio,angalia maisha yako mtunze mwanao,halafu unaonekana sana una hamu ya kuolewa tulia mungu atakusaidia.

Anonymous said...

Wewe bado unampenda?