Sitaki kuudhi mke na Familia yangu, nitaachaje?-Ushauri

"Habari dada Dinah, Mimi nijiite Elly. Umri wangu sasa ni 34yrs, naishi scandinavia countries.
Leo ndio mara yangu ya kwanza kuandika humu japo kwa suala la kupitia mana nyingine najikuta nimerudi kama mara mbili kwa siku kuona kama kuna jipya.

Ni ukweli nisiouficha kuwa nimekuwa nikijifunza mengi kupitia hapa.
Nimeona niandike humu kwani naamini kwa ushuri wanaopewa waliopitia hapa kuomba ushauri kwa kweli naona wanasaidiwa. Kwani wengi wa watembeleji wa humu ni watu wazima.

Kifupi Dinah, mie nimekuwalia mazingira ya dukani tangu nikiwa Primary hadi Secondary, kipindi hicho chote cha kuuza duka kuna wateja hasa Arusha , Mererani na Mbeya ambako nimeuza duka nyakati tofaui (sio yangu ni ya kaka zangu) wakinunua sigara basi wana kuambia "niwashie" na mimi kuwawashia kama kawaida. Tangu kipindi hicho basi ndio mwanzo wa kujua sigara.

Sikuwa mvutaji yule wa viile, Ila pale ninapohitaji kuchangamka kama wanywa pombe ama wala ndumu, mie steam zangu ni sigara moja nachangamka.Tabia hii nimekuwa nayo kwa miaka 17 sasa. Miaka sita iliopia nilifunga ndoa na tumejaliwa mtoto mmoja ambae nilimuacha Bongo kwa miaka 3 sasa na mwanetu ana 4yrs.


Wakati wa kudate na ma wife hakuwahi gundua kuwa mara nyingine huwa navuta sigara, nasema mara nyingine maana kama nilivyotangulia kusema mie nilikuwa sivuti kila siku.
Pamoja na kutokujua ila kati yetu kuna kipindi fulani tuliambiana what I like and don't.

Yeye cha kwanza ni uvutaji na pombe, katu hatopenda wala kutamani mwenzie atumie. Pombe kweli Sijawahi kutumia kwani ladha yake tu inatosha kuninyima raha ya kunywa. Tabu yangu tangu nimekuwa huku Ughaibuni, Unajua tena kutimiza ndoto kwanza naona sio kama nilivyotarajia.

Maana nilitegemea ningeweza kuileta family huku ktk kipindi cha 1 year kitu ambacho kinaonekana ni kigumu hivyo napigana pengine kupata mtaji nirudi ku-join family ama kama yeye atapaa skuli basi aje. Ila hili sio ilionileta hapa ktk blog.


Sasa kipindi chote cha 3years nimekuwa nikivua takriban sigara 10 kwa siku, ila cha ajabu siwezi vuta waziwazi hadi nikiwa mwenyewe hivyo hata marafiki hili nao hawajui. Dinah sigara siipendi na sipendi kuwa mvuaji bali najikuta tu navuta.

Nimejaribu kuacha nimeshindwa, najua hata wife akijua japo nitajitutumua ka kidume ila ukweli hili litanipunguzia heshima nilionayo kwa mke wangu na jamii ya kwatu ambao hakuna hata mmoja mvutaji, sijui nimetokea wapi maana huu si utoto tena kwa umri huu.


Tafadhali msinishambulie jamani bali mnipe ushauri kama kuna mwenye kujua mbinu yoyote ya kuepukana na sigara.
Shukrani sana kwa ushauri mtakao nipa maana nitaufanyia kazi"

Dinah anasema: Elly asante sana kwa ushirikiano wako pia uvumilivu. Inapendeza kuona watu wamechangia uzoefu wao kuhusu matumizi ya sigara, mimi binafsi nitakupa ushauri wa uhakika wa kuacha "habit" yeyote mbaya inaweza kuwa kujichua, kutokuoga, ngono na watu tofauti kila siku (ngono zembe) kula sana, uvivu, kujamba, kutumia psa ovyo, kunywa pombe n.k

Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa mtu anaweza kuzoea kitu fulani na kukitumia kitu hicho kama "kiondoa" mawazo au kwa case yako kukuchangamsha, mazoea hayo yanaweza kujenga tabia na tabia ikazaa tatizo liitwalo addiction kwa kitaalam.

Kama huko Ughaibuni ni pande za Uingereza, basi nafurahi kukuhabarisha kuwa NHS wanatoa huduma ya bure na baadhi hupewa malipo fulani ili waache kuvuta sigara, hivyo basi unaweza kufanya mawasiliano na wahusika ili kupata msaada wa kitaalam zaidi na support ili uache kabisa kuvuta Sigara.

Vinginevyo ni kujiwekea mikakati mwenyewe ya kujaribu kuacha tabia ya uvutaji, natambua kuwa ni ngumu sana kuacha kufanya jambo ambalo umelizoea ghafla, hivyo ni vema ukaanza kupunguza kiwango unachovuta kwa siku.

Mfano badala ya kuvuta kumi kwa siku kama ilivyo sasa, jitahidi na uvute mbili, jinsi ambavo siku zinakwenda unazidi kupunguza siku za uvutaji...Mf; umeweza kuvuta kila siku sigara mbili sasa anza kuvuta sigara moja kila baada ya siku mbili, endelea kubadilisha the habit, na sasa punguza na vuta moja kila baada ya siku nne.

Utajikuta unavuta moja kila baada ya wiki na baadae itakuwa moja kila baada ya wiki 2, alafu utajikuta unavuta moja kila baada ya mwezi na hatimae utasahau kama umevuta au laa!...haina maana ukaitafute bali jipongeze kwa kufanikiwa.

Hii haitochukua siku mbili au mwezi mmoja bali ni miezi kadhaa hivyo kuwa mvumilivu na kuwa commited kwenye mkakati utakaojiwekea, kumbuka ni wewe pekee mwenye uwezo wa kujizuia kuvuta sigara.

Wakati unaendelea na mkakati wako wa kuacha kuvuta sigara, jaribu kubuni kitu mbadala utakachokuwa unakitumia kujiliwaza au kuondoa mawazo kila unapojisikia mpweke, mwenye huzuni, unapoikumbuka familia yako.....unaweza ukatumia senti unayonunulia sigara kumi kununua kadi ya simu/muda wa kutosha ili kuzungumza na watu ambao ni muhimu kwako au kwenye shughuli zako au zile unazotaka kwenda kuzifanya Nyumbani.

Kwa vile uko mwenyewe huko Ulaya ni wazi kuna wakati unapata upweke sio wa kimapenzi tu bali hata ule wa marafiki, ndugu na jamaa, maisha ya Ughaibuni ni tofauti sana na hapa nyumbani kutokana na Tamaduni zetu kutofautiana.

Unaweza ukajikuta unaishi ili kufanya kazi badala ya kufanya kazi ili uishi, yaani yanakuwa ya upweke sana kwa vile hakuna ile " kujichanganya" kama hapa bongo, kwamba ukitoka kazini kila mtu anakwenda kwake na maisha yake kivyake.

Ni matumaini yangu utachukua ushauri wa waungwana wengine na sehemu ya maelezo yangu na kufanyia kazi kamaulivyo ahidi.

Kila lililojema.

Comments

Anonymous said…
Mdogo wangu, unastahili sifa kabisa kwa jinsi unavyojali uhusiano wako na mkewe ikiwa ni pamoja na famili yako pia.

Ni wazi kabisa kwamba ukishazoea kitu kuacha kazi inakuwa kibarua kikubwa sana. Hata hivyo maandamu umeanza kulivalia njuga swala hilo naamni safari yako imekolea na punde utafanikiwa.

Jambo moja ni kuchukia kitendo hicho kabisa na kujiona kinakuangamiza kabisa kiafya, kifikra, kisyosyolojia na hata kisaikolojia.Kwa minadhiri hiyo basi ndugu yangu weka mkakati na jikane mwenyewe na chukia kuvuta.

Jambo la pili hebu anza kutafuta kitu kingine mbadala ambacho unaweza kufanya ili uchangamke.Ukikipata hicho ndicho mara utakapokuwa unawaza sasa ungevuta sigara unazamia kwa kitu hicho.Kwa mfano chai hivi, au pipi au kitu chochote cha kutafuna hivi. Pia unaweza hata labda kufanya mazoezi ya kukimbia au ukaenda gym kwa huko uliko ni rahisi kutafuta mahali au sehemu yenye gym kwa wepesi zaidi.lakini gym ya haraka ni kujikipu bize sijui unasoma huko au unabeba mabox?unaweza kuweka ratiba nguvu inayoweza kukufanya hata kukumbuka sigara ukashindwa. Lakini cha muhimu chukia kabisa uvutaji na muone mkeo kama yuko hapo anakuangalia na anakasirika.
Anonymous said…
kwanza kabisa muombe mungu kweli kwa kumaanisha aondoe kiu ya sigara hakuna kiu ambayo mungu hawezi kuondoa sigara ni mbaya mno mno leo nimezika mjomba yangu tatizo ni sigara za mda mrefu na aliacha mika 15 iliyopita, mdogo amepata ulemavu wa kidole kwa sababu ya sigara nikotin ni mbaya ukiona kiu ya sigara tafuta kitu mbadala ambacho kitazuia kiu ya kutaka kuvuta, hali ni mbaya kaka bora umeliona kutaka kuacha .
Diana
Anonymous said…
Kaka tumeingia choo cha kike, maana mi mwenyewe nina miaka 10 since started smoking na nimejaribu kuacha lakini nimeshindwa, hivyo sigara haina dawa, dawa yake ni kuvuta mpaka tufe.
Anonymous said…
Afadhali kaka yangu umeliona hilo mapema na nakupa hongera sana kwa kuijali familia yako na afya yako pia hujasema uko nchi gani exactly kama upo Uingereza nenda NHS yeyote ile unapata cancelling free in charge na wanasaidia mpaka mtu anaacha kabisa nasikia hadi siku hizi ukienda kuomba ushauri tu unapewa na hela juu kwa hiyo bro kama upo Uk nakusihi sana nenda bila kusita utajionea mwenyewe wish u best of luck!!!!
Anonymous said…
Mkeo mwenyewe ndiyo kinga mahususi ya kuacha sigara, kwa sababu umemuacha mbali ni vigumu kujikontro maana hakuna unayemuona kwa karibu kukukataza, you are free to smoke.Kwa hiyo kama ulivyosema mwenyewe ni bora utafute namna ya kuungana na familia yako itakuwa msaada mkubwa kukupunguzia adha hiyo ya uvutaji sigara.

Mtu asikudanganye ni rahisi sana kuacha kitu mradi tu umekichukia kama ni hatari kwako na kwa familia yako.Naamini maadamu umeanza kuliona jambo hilo hatari na athari zake utafanikiwa tu.

Kama wewe ni mkristo uone kuwa pia kikristo haifai kuhangaika na sigara kwani inaharibu hekalu la Mungu ndani yako.Ubarikiwe sana kutafuta uaminifu kwa mkeo na familia yako.
Anonymous said…
Pole sana ndugu yangu! Jaribu kutumia chewing gums zenye nikotini. Zinapatikana kwenye maduka ya dawa. Hizi zipo zenye kiwango tofauti cha nikotini, kulingana na kiwango cha uvutaji. Unachotakiwa ni kumueeleza mfamasia kuwa unavuta hadi sigara 10 kwa siku, then atajua ni ipi inakufaa. Kwa hiyo basi ukijisikia kuvuta sigara, unatoa moja na kutafuta....slowly utapunguza idadi ya sigara kutoka 10 hadi 0 kwa siku.

Hizi zinasaidia tu, kutpunguza hamu ya kuvuta, kwa kukupa stimu kidogo ambayo inafana na ambayo ungepata kama ungevuta sigara. Hata hivyo zitakusaidia tu iwapo unania ya kuacha kuvuta.

Mimi zilinisaidia kidogo, maana niliweza kupunguza idadi ya sigara....mpaka nilivyokuja kupata msichana ambaye alikuwa hapendi nivute sigara, ndio niliweza kuacha kabisa.
BK said…
Ngugu yangu nikupongeze kwa kuwa katika mwelekeo sahihi,
mim i nilivuta kwa zaidi ya miaka 25, na mzee wangu alivuta tangu nilivyo sijui lini kwani napata akili yeye anavuta.

kwahiyo ninapoandika sasa yeye havuti na mimi sivuti - njia pekee pamoja na ushauri mzuri ulioupata toka kwa waungwana wengine naweza kusema kwa kifupi tu NI WEWE

Ili kuacha ni lazima uwe na sigara wakati wote lakini uwe na utash (comand) au sijui niseme (will power to resist temtation )ujizuie kutovuta kwa nguvu zote hatakama iweje - labda mfano rahisi kwa hili ni kwa wale wanaofunga kwa sababu za kidini ukishamudu zoezi hili kwa wiki moja basi ujue kama kweli ni nia yako kuacha hutarudi nyuma na inakuwa rahisi sana baada ya hapo

ila niseme na niweke anagalizo siku tatu za kwaza ni ngumu kupindukia na ndizo za kujitahidi na kuweka nadhiri hasa.

kama nilivyo kuambia mwanzo kutokuwa nazo jirani inamaana kuwa unazikosa ila kama ukiwa nazo na ukamudu kujizuia kuvuta basi utakuwa uko salama na hata kama utakumbwa na msongo wa mawazo kiasi gani utamudu kujizuia

inawezekana ni uamuzi tu - na uamuzi lazima uwe wa kwako kwani kitu kidogo kama sigara kwanini kiendeshae maisha yako

kunywa maji mengi wakati wa hamu kuu kuna saidia sana na hakuna madhara

naamini kama mimi na mzee wangu tume mudu sioni kwanini wewe usiweze