Friday, 12 February 2010

Sijui nini cha kuongea nae, yaani nakuwa-blank-Ushauri.

"Da Dinah happy new year! Blog yako imenisaidia sana kwa mambo mengi ambayo nilikua siyajui na yale nilo kuwa nayajua nimeweza imarisha zaidi, shukrani sana na pia kwa wote wanao changia watoa msaada mkubwa pia.

Da Dinah mimi nipo nje ya nchi kwa ajili ya masomo boyfriend wangu wa miaka minne sasa yupo Bongo, tumesha kwaruzana sana kwa ajili ya mahusiano yetu lakini nampenda kweli huyu kaka. Hilo si swali langu lakini just to give you an insight.

Mwaka jana mwishoni nilikua Bongo kwa likizo fupi na nilimtambulisha kwa Mama yangu Mama akampenda na yeye alikwisha nitambulisha kwao muda kidogo japokuwa mama yangu alikuwa anamsikia lakini hatukuwahi kukaa sote.

Niliporudi masomoni tukawa tunaendelea kuwasiliana vizuri tu sema siku hizi anakuja mpaka mtandaoni tunaongea lakini ukweli sijui nini cha kuongea nae, does that make sense?? Yaani na baki kucheka na kukumbushia yalopita madogo madogo na yanayo endelea huku kiasi nitaongea nae kuhusu nini kingine jamani online?

I love the idea that we chat but I've never done that with him so am blank! niwe naongea nini online? msaada dada yangu mpendwa...asante. M"

Dinah anasema: M heri ya mwaka mpya nawe pia, naona sasa mwaka ndio unachanganya...nimekuwa napata shida sana kuandika 2010 na hivyo nikawa naishia kuandika 2001, ila sasa nimezoa...anyway!

Uhusiano wa mbali ni mgumu sana na wengi huishia njiani, lakini njia pekee ya kufanikiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu aliye mbali ni mawasiliano. Kwa bahati nzuri vijana wa sasa tumekuwa na Teknolojia na hivyo kuturahisishia sana linapokuja suala la mawasiliano.

Natambua wakati mwingine inaweza kuwa ngumu sana ku-keep maongezi kwa vile yeye hajui nini kinaendelea huko uliko na wewe hujui nini kinaendelea huko aliko, sio hivyo tu pia sisi wanadamu tunatofautiana kuna baadhi yetu tunapenda kuzungumza na wengine sio wazungumzaji.

Kama wewe ni mzungumzahi basi mazungumzo huja yenyewe yaani jinsi unavyoongea ndivyo ambavyo "topics" zinazaliana basi mnajikuta mnapiga soga mpaka mmoja wenu anaamua kuaga(hela imeisha n.k).....na wengine ni wa kimya kwamba akikupa habari anazodhani kuwa ni muhimu basi maongezi yameisha, utabaki kuuliza maswali nkupewa majibu mafupi.

Unaweza ukawa unazungumzia tofauti ya tamaduni za huko na Nyumbani, ukazungumzia sinema, habari za kisiasa, maisha kwa ujumla, mipango ya maisha yenu ya baadae, ni namna gani unakabiliana na masomo, leo Chuoni kulitokea nini, amekula nini, nani alipika (kama bado anaishai kwa wazazi), n.k.

Ukiwa unapa stori za huko uliko ambazo zinavutia na kuozungumzia mipango ya maisha ya hata yale maisha mlioishi miaka minne iliyopita......yaani unachanganya maongezi. Ili kumfanya na yeye aongee basi wewe unamuulizia habari za hapo nyumbani na watu mnaofahamiana nao n.k.

Pia mnaweza kuzungumzia ngono na hata kuifanya ngono kwa kutumia simu. Hii itawasaidia sana kupata zile kuwa karibu zaidi kihisia na hivyo uhusiano wenu kutotetereka.

Natumaini maelezo ya wachangiaji na nyongeza yangu yatasaidia ideas za kuendeleza maongezi na mpenzi wako.

Kila la kheri.

12 comments:

Anonymous said...

nashukuru kujua kumbe tuko wengi tofauti yako na mimi ni kwamba mimi ni mwanaume girlfriend wangu yuko bongo na mimi niko nje hali kama hiyo inanipata sana sina jipya zaidi huwa namwambia nakupenda au nakumiss au sikuzingine natunga tu story za kitoto sijui ninmeota niko bongo mara hili kweli ni shida mapenzi ya simu na email magumu jamani maoni ya wengi yatatusaidia wengi.

Anonymous said...

kaka/dada jaribu kupisha cku mbili ,tatu halafu ukija uje na jipya kweli ni magumu sana lakini si lazima kila cku m chati hata salaamu tu inatosha leave your sms then 2morrow another issue or day after 2morrow.

Anonymous said...

jamani na mimi pia am in a long distance relationship, i agree with you gal kabisa kabisa, hata mimi tulikua twachat na mchumba kwenye net, inafika saa huna cha kusema, mnabaki, mnaanza kukumbushiana ya zamani, au basi tu mnaanzisha kitopic chenu mnakiongelea weee, mpk mtosheke, mfano km mimi mwenzio naongea, basi huwa namuongesha mpz wangu weee, yani ata km nimeishiwa cha kuongea, basi ntaanzisha 'sex chat' yani ilimradi raha tu, unajua mnapokua mnachat ol the tym, ni sawasawa na mngekua nyumbani, i mean mume na mke, c mnaongea, mkichoka mnaangalia lbd movie, u can do the same with ua love even if mko mbali, me and my love huwa twatumia skype, where u can share screens, kwaiyo kama mmeishiwa maneno ya kuongea, basi unaeka movie, afu unashare screen yako na mpz,...yani wala usipate headache my dear, just be a little creative, mapenzi ni ubunifu sweetheart, yani tena mkiwa mnachat frequently, wala husikii uzito au ugumu wa long distance re'ship, utaona kama mpenzi uko nae karibu, mana kila kitu mwatoshelezana kwenye simu au kwenye net, kuna topic dada dina, alifundisha jinsi ya ku-do na mpenzi aliembali, my dear it works, we have tried that with my bf several times, na huwa twapata raha,...basi ndo akirudi hivi, mkikutana weeeee, usipime, ni EXPLOSION ya ajabu, raha jamani,

Anonymous said...

nyie mnaosema hamna cha kuongea,ina maana hamuongei kuhusu future yenu?? vipi mngependa maisha yenu yawe mkishakuwa pamoja? maybe mnafikiria kuwa na watoto? wangapi? n stuffs like that..au hata hamuwezi kusema tu-save some money ili hao wapenzi wenu wawatembelee huko mliko?? ni aibu kusema eti huna cha kuongea na mpenzi wako.then maybe you aint that into him/her!!!

Anonymous said...

Hello Jamani asilimia kubwa ya sisi ambao tuna ma girlfriends au ma boyfriends huongea unachoongea nae....sasa mtaongea nini zaidi ya
1. nakupenda
2. nimekumisi
3. unakumbuka siku ile kulikuwa na ....
4. unamkumbuka ......
5. hivi jana ulisemaje ....
6. nikija tuta ....
n.k

Angelikuwa ni mke au mume wako basi ungeongea nae vitu kama hivyo bali na vingine kama
1. mjomba alikuja, akasemaje .....
2. kwanini usienda kusalimia ....
3. nyumba imefikia wapi, maana ulisema .....
4. watoto wanaendeleaje
5. inamaana umetoa mchango laki 3, kwanini lakini baba ....
n.k

Lengo langu ni kutaka kuonesha maongezi hutofautiana na level ya relationship.....
wengine huongea na ma boyfriend au ma girlfriend wao mambo ya kitoto kabisaaaaaa. Ndio hivyo siku inaenda, na muda unasogea muwe pamoja mrudipo nyumbani TZ...

Uhusiano wenu unamalengo ya kuishi pamoja!!!!!? kama ndio, basi mnaweza kuongea na kuchati mambo ya kitoto na ya future. Ya future kama expectations...........

Anonymous said...

na mimi nina distance relationship huu ni mwaka wa 3,kipindi chote cha miaka 3 kila siku tunawasiliana either kwa simu,or text msgs,or email or chat. Kwa kuwa ni kila siku ya mungu s.times kweli cha kuongea lakini kwa kifupi japo salamu au maneno ya mapenzi tu au even sex on the phone.Kwa kweli na enjoy mno. Kama mnapendana maongezi yatakuja tu.

Anonymous said...

Pole sana wadasha wa mahusiano ya mbali.Naelewa fika jinsi yalivyo na surubu.

Mimi ilikuwa hivyo, lakini nilikuwa mjanja sana,nilikuwa najitahidi sana kupanga muda, yhaani niliweka kuongea naye kwa simu kila baada wiki mbili,na kuchat au kuandika mail nilikuwa siandiki au kuchat naye mara kwa mara.
Hasara za kuchat mara kwa mara, ni kufikia kiwango cha kuongea mambo yasiyofaa au kukwaruzana katika vijambo kadhaa.Hivyo pata muda wa kutosha bila mawasiliano ili umsahau na utakapowasiliana naye unakuwa na jambo la maana kuongea.

Jambo lingine Jaribu kuandika chini ni nini utaongea na huyo mpenzio siku mkikutana kwa simu.Panga mambo hata mawili matatu ya maana juu ya safari ya mahusiano yenu. Usiongee na mchumba/mpenzi wako ili mradi tu kujifurahisha, hapo ndipo unakaukiwa kabisa maana huna plan yoyote.

Mshirikishe hata jinsi unavyoendelea na masomo, na nini hasa unakifurahia unaposoma huko na nini unakiweza na nini kinakupa shida ili yeye awe mtu wa kukupongeza na yamkini kukutia moyo.

Jitahidi kuwa na hamu kujua mambo mengi yanayohusu upande wake na familia yake.Inawezekana hapo mlipo hamjui hata kaka na dada zenu kwa kila mupande.

Muuliza swali umedokeza kwamba mnakorofishana mara kadhaa, jambo kama hilo huwa linatokea sana hasa kwa sababu mko mbali, au huwa hamna jipya la kuongea zaidi ya yale ya utoto na yamkini mnayoyakuta mitaani au online. Ni muhimu muwe wabunifu na kujua hakika ni nini mnataka hasa katika mahusiano yenu.Kama mpo tu kimachomacho hivi bila dira yoyote mbeleni basi si rahisi upate cha kuongea na mpenzio.Kumbuka msilalie zaidi kwenye ufanyaji mapenzi kama ilivyo kawaida ya wapenzi wengi, zaidi sana lalia juu ya nini unakichuchumilia katika longolongo hilo la mahusiano, naamini utakuwa na mengi sana ya kuongea na mpenzio.

Kuna wakati mimi msichana wangu nilikuwa namuacha hata kwa mwezi mzima sijaandikiana wala kumpigia simu lakini nikiwa nimempa taarifa kwamba sitakuwa na nafasi yoyote hadi muda fulani.Hiyo ilikuwa inanipa nafasi ya kutosha kummiss na kuvuna mengi ambayo yatakuwa na maana kuongea naye.Na yeye alikuwa nankuwa na hamu kulikoni.Na tulikuwa hivyo kwa miaka minne na hatimaye tukamaliza mambo sasa tuko wote ughaibuni anakula shule na yeye.

Kila la heri jamani.

u cab try to ask abt her family one after the other
9kwa unaowajua) kujua wanaendeleaje,ask her abt her day,talk abt kitu ambacho ungependa mfanyia/fanyiwa kama mngekua karibu,talk abt ur future plans,funny enough u can make love/share love stories thru phone/webcam if privacy inakubali...

Anonymous said...

This distance love thing ina matatizo yake mengi ambayo ni ngumu mno kujua kama hayuko serious na maisha yake. Wapo wanaotumia kupanga mambo ya maendeleo kwa walioolewa na wale waioolewa na wapo wanaotumia ku-control kila kitu wenza walichonacho.

Kwa mfano unataka kujua leo kama mpendwa amekula nini, sawa ni vizuri kujua alichokula kama anakaa mwenyewe. Unajua kabisa huyo mpenzi wako anakaa na watu wengine kwa mfano unaanza kuulizia, zamu ya nani kupika, anajua kupika, sijui ana hiki ana kile....that's rubbish. Jaribu kutafuta muda wa kuwa unaongea nae probably thrice a week, ukikosa kazi za kufanya ndo kila siku unaanza kuuliza vitu visivyokuwepo.

Naandika hizi kwa sababu kuna relationship naijua binti yuko Tanzania mwanamume yuko Europe, kwa kuangalia hata uwezo wake wa kufikiria + elimu aliyonayo binti anataka kujua kila single details za watu wengine wanaoishi na mpenzi nyumba moja. Mpaka wakinunua vitu anataka aambiwe wamenunua nini.

Angalia yasije kukuta kama ya huyo binti ambaye hata shule yake anaacha kuconcentrate kwa kuwa kila muda anawasiliana na mpenzi wake mpaka saa 9 za usiku bongo.

Anonymous said...

Dada dihah mimi ni mpenzi sana wa glob yako lakini nashindwa kupost issue yangu nifanyeje?

Anonymous said...

poleni sana ndugu zangu. hata mi nilisha kuwa na long d/rship. ilikuwa bomba tulichat na kuongea mengi,tulipanga mengi but at last mwenzangu alivyorudi alileta mbwembwe kadhaa na kuleta sababu zisizokuwa na kichwa wala mguu. tuliachana kimiujiza.realy it was very pain fully 2 me coz milimwamini na kidhani ndo angekuwa mtarajiwa.nawaombea mungu na nyie yasiwakute kama yangu maama long drship ni 50/50 wapendwa. na kama ndo nakosa hata cha kuongea hapo nina mashaka>ni mawazo tu msinune