Friday, 29 January 2010

Nataka kuchumbua ila majibu yake mmh-Ushauri.

"Naitwa Michael miaka 25 ni mara yangu ya kwanza kwenye libeneke kuomba ushauri. Kuna binti anaitwa Joy ana miaka 23 ambaye ningependa awemchumba wangu, lakini nakuwa katika wakati mgumu kutokana na majibu anayonipa nikiwasiliana naye kupitia simu. Wakati huu hatukuwa karibu.

Majibu anayonipa hasa kwenye story za kawaida tunazopiga yanaonyesha uelekeo wa yeye kunikubali lakini nikimuuliza kuhusu mimi na yeye kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ananiambia muda wake wa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi bado, na nikimuuliza lini atakuwa tayari kasema "ni katika kipindi cha miaka 3 ijayo".

Nilimuahidi kumsubiri lakini akakataa kwa kisingizio kuwa asingependa kuniumiza wala mimi kumuumiza yeye.Tumekuwa karibu sana katika kipindi cha miezi 3 ya mawasiliano kupitia simu kiasi cha yeye kuniambia mambo mengi kuhusu familia yake na mengine yangehitaji mtu wa karibu sana kuyajua.

Mambo kuhusu boyfriend wake wa kwanza na jinsi walivyoachana, sifa za mume ambaye anamhitaji na zote ziliniangukia.Nilipomuuliza kama ananipenda na kunihtaji alisema ananipenda lakini kunihitaji hakuwa na jibu kamili.

Sasa wakati mgumu nilionao ni je niendelee kumbembeleza au nimuache? nikitaka kufanya hivyo roho yangu inasita kwani kwa jinsi anavyokuwa mgumu ndio nazidi kumpenda. Nifanyeje? Michael"

Dinah anasema:Mike hebu kuwa mkweli, unauhakika ktk umri wa miaka 25 uko tayari kumuoa huyo binti au ni gia tu ya kumpata kimapenzi? Kama kweli unauhakika na unania ya kumchumbia na kuja kufunga nae ndoa nasikitika kusema kuwa yeye kwa sasa hayuko tayari kwa ajili hiyo na amekuwa wazi kwako, kuwa anakupenda lakini hayuko tayari labda baada ya miaka 3...hapo uamuzi ni wako ku-take risk na kumsubiri au kuendelea na maisha yako.

Uamuzi wa kumsubiri unaweza kukupa matokeo mawili tofauti moja ni chanya au hasi, kwamba akawa nawe kama mpenzi/mchumba au akawa na mtu mwingine....ndio maana nikasema take risk.

Kitendo cha huyu binti kukuambia vitu vingi ambavyo wewe unadhani anapaswa kuambiwa mtu wa karibu zaidi kama vile mpenzi, ni kwa sababu anakuamini kama rafiki yake. Inawezekana kabisa hata upendo alionao ni wa kirafiki na sio wa kimapenzi na ndio maana anakosa jibu unapomuuliza suala la yeye kukuhitaji wewe kama mpenzi.

Katika hali halisi ni Binti mdogo ambae tayari amewahi kuwa kwenye uhusiano, kama mpenzi aliyekuwa nae alikuwa ndio mpenzi wake wa mwanzo ni wazi kuwa itamchukua muda mrefu kidogo kama hajaingia kwenye uhusiano mpya na mwanaume yeyote sio wewe tu.

Kutokana na maelezo yako nahisi kuwa huyu binti bado anahisia na yule ex, hisia zinazomfanya ashindwe kufanya uamuzi kwa vile hana uhakika kama bado anampenda yule au la! Inawezekana pia kajiwekea hiyo miaka mitatu kuweza kujua hisia zake ziko wapi.

Kitu ambacho kimepelekea yeye kukuambia kuwa asingependa kukuumiza au wewe kumuumiza, pale ulipoahidi kumsubiri ndani ya miaka mitatu ambayo kwa mujibu wake ndio atakuwa tayari kuingia kwenye uhusiano.

Nimependezwa na uwazi wa huyu Binti, kajaribu kuwa mkweli ili kukusaidia wewe kufanya uamuzi na kuendelea na maisha yako lakini wakati huohuo uendelee kuwa rafiki na mtu wake wa karibu.

Mimi nakushauri umuache (kwani kubembeleza kukizidi huwa kunaudhi sana) lakini endelea kuwa pale kama rafiki, msikilize, mshauri, msaidie na yote muhimu kwa marafiki. Ukionyesha kuwa umeheshimu "msimamo" wake lakini bado unaendeleza urafiki ni wazi atakuwa comfortable na wewe na pengine baada ya hiyo miaka mitatu wewe ukawa the one.

Kila la kheri.

7 comments:

Anonymous said...

Da Dinah sasa naona huyu anatafuta mbinu za kuongoza. Sasa anataka binti wa Kitanzania amkubalie kirahisi rahisi halafu akikubaliwa angekuja hapa kuomba ushauri, mbona kanikubali haraka hivyo je ni malaya, amewakubalia wangapi, na mambo kibao. kijana kwanza we bado umri unakuruhusu kufanya mambo yako mengi ya kimaisha, kama ni mapenzi mbona unamwarakisha hivyo. Hata mie mwanaume sikubali kirahisi mwanamke anenihitaji kiuchumba wa kuwasiliana ndani ya miezi mitatu,. kabla ya ndoa wasichana wengi maana ni kama kumi na mmoja hivi waliwasilisha maombi ya kuaka uchumba, ambao wengi nilifahamiana noa kwa miaka kama miwili kwa wakati tofauti na tumekuwa kama marafiki wa kawaida sana majibu yangu mengi kwao yalikuwa ni kama ya huyo mdada, maana nilihiaji muda wa kujiuliza na kukubali nafsini mwangu ni yupi kati ya marafiki nilionao anafaa kuwa wangu wa maisha, na ukumbuke wakati wa kufikiri haimaanishi umefunga milango ya kupata marafiki wapya. nao walifikia idadi nioikumbuka kwani nilikutananao mikoa tofauti. Hivyo ndani ya miaka minne wa kufikiri kuwa na family ndio nikampaa huyo wa ubavu, na wengine uzuri hakuna aliewahi kuwa nami kimahusiano zaidi ya frindship. maana huyo unaempapatikia ndani ya miezi mitatu akikubali utataka utombanenae baada ya 3months utamwona hakufai ama yeye akuone hufai.
ushauri wangu soma vizuri tabia ya mwensio kabla ya kuamka neno uchumba.Ningekuelewa kama uauambia unachohiaji kwake ni ngono ili pengine baadae ikiwakolea na mkaona mnaendana kitabia basi muoane. Ila sio vizuri kungonoka na sana kabla ya ndoa maana ukija bahaika kumpata ambae hajawahi utamwona mshamba mwisho wake nyumba ndogo.

Jeff said...

Mkomalie 2 mwana kama vipi coz maduu cku hizi wanazuga wagumu huku ukizingatia waoaji wenyewe ndo kama nyie c wengine tunachapa 2 then 2nasepa. Big up kwako dada dina..@

Anonymous said...

Achana na kumsakama binti huyo kwani anaonyesha anajitunza na ndiyo maana amekupa miaka mitatu.Hiyo tu inaonyesha kwamba hayuko tayari kuingia kwenye sokomoko la mapenzi sasa.Mimi nampongeza kwani bado ana muda mzuri wa kujifunza mengi na kujiendeleza katika mengi kwa ajili ya maisha yake.

Wewe usijidanganye kwa kusema anakupenda, ndiyo maana huwa hakupi majibu ya masuala mengine ukimuuliza.Huyo binti ana hekima sana.Tatizo la sisi wanaume tunakimbilia kutomba tu hatuna hata subira mradi ukishapatana na msichana macho yote yanaangukia kutomba tu wala hatuna nafasi kutafakari mambo.Na huyo binti analijua hilo ndiyo maana anajihami na mikwese hiyo.

Kama utakuwa mvulivu basi msubiri usiwe na haraka ya kuanza uchumba au mahusiano ya kimapenzi maadamu yeye amekwambia kuwa anakupenda lakini hayo mengine ameweka stop/period wala usimgasigasi mwache aendelee kutunza heshima yake hadi hapo muda wake utakapowadia.

Mabinti wengine igeni mfano wa huyo dada kwani sisi wanaume pima zetu zimelalia kwenye kuma tu bila hata kujali future na matazamio ya wadada wengi ambao wanataka wenzi wa kujenga nao maisha.

Anonymous said...

Kaka nakupongeza kwa wazo lako, kitu cha kufanya huyo msichana anaonekana kweli anamisimamo.
Ni wasichana wachache sana wenye misimamo ya namna hiyo tena umemwambia kuwa unataka kumchumbia, wangekuwa wasichana wengine wenye kukurupuka angeshakubali.
Pili kipindi mlichojuana na kufahamiana kama ulivyosema mwenyewe cha miezi mitatu ni kifupi sana kama unataka mke na ndio maana naye anawasi wasi nawe kwani siku hizi kuna utapeli mwingi mno wa kimapenzi, kuna baadhi ya wanaume wakitembea na msichana siku moja basi anakuacha hakurudii tena, japo hujatueleza sababu za rafiki yako kuachana na mpenzi wake wa zamani, inaonyesha kwa vile alishang"atwa na nyoka, kila jani nilimgusa anahisi kuwa ni nyoka.
Cha muhimu unachotakiwa nawe uwe mvumilivu kwake, usiwe na papara ili asije kujua kuwa wewe pia ni wale wale, wahenga husema mvumilivu hula mbivu.
Mara nyingine kama wewe ndio umeanza kumpenda yeye itachukua muda yeye kukupenda, atakuwa anavutwa na wewe kidogo kidogo kutokana na upendo wako utakaomuonyesha na itafikia wakati atakubali.
Suala la kuoa na kuolewa linahitaji maandalizi mengi na sio kukurupuka.
Umri wako na wake unawaruhusu kusubiriana, msije mkabebana leo haraka haraka baada ya miaka miwili mkaachana, haitakuwa na maana.
Usikate tamaa mapema, huyo ndiye mke mwema na bora kwako, komaa hapo hapo, rakini nenda taratibu usiwe na papara. ni ushauri wangu

Anonymous said...

Pole mshkaji kwa challenges unazozipata. Kwa mawazo yangu huyo binti anakupenda ila ni mjanja sana, anajaribu kukupima udhaifu wako juu yake si unajua hawa viumbe wanatujua udhaifu wetu wanaume. Nahisi anataka kuelewa kuwa unampenda au unamtamani?, uchumba wa siku hizi kwa kiasi fulani ni usanii na bila shaka anajua kisa fulani kuhusiana na uchumba.Ni bora umvumilie so long anajua lengo lako iko siku atakutamkia mwenyewe what to do.

Anonymous said...

Kama hakusema kuwa anakuhitaji basi huna bao.Kupenda ni kitu cha kawaida tu kila mtu anaweza kusema nakupenda kumbe anapenda kula ngoma tu na wala si upendo wa kweli hasa.Hivyo jamaa yangu usipoteze muda kummendea huyo binti kwani ana msimamo mzuri tu kwa ajili ya nafsi yake.

Usinendelee kumgasigasi achana naye kwanza kama atakuwa na haja na wewe utamuona hapo baadaye atakuja mwenyewe,lakini ukiendelea kumsakama atakuona juha tu wewe.

Nampongeza huyo binti kwa msimamo wake na jinsi anavyowasiliana nawe kukuonyesha kuwa anajali ubinadamu na utu wa mtu ndiyo maana anashare tu habari zote hizo ulizosema.Lakini hilo halikupi waranti kwamba ndiyo anakupenda la hasha huo ni urafiki tu wa kawaida kutia STORI.

kAMA UNA KIHELEHELE CHA KUTAKA BINTI WA KUTOMBA HUNA BUDI KUANGALIA PAHALA PENGINE SIYO HAPO UNAPOHANGAIKIA KWA SASA.

Anonymous said...

Usikate tamaa mtaka cha uvunguni shariti uiname.so kaza boti.