Mpenzi karudi Ulaya na kukata mawasiliano je nimeachwa?

"Dada Dinah pole na hongera sana kwa kazi nzuri.
Mimi ni msichana wa miaka 28, Naomba ushauri kama ifuatavyo. Nina mpenzi wangu wa muda mrefu nampenda sana, alikuwa Ulaya kwa miaka 3 na tulikuwa tunawasiliana vizuri sana.

Akarudi hapa bongo kurenew Visa yake na tulikaa pamoja vizuri kipindi chote hicho, siku moja nikamuuliza je vipi kuhusu maendeleo ya uhusiano wetu? akasema kwa sababu kazini kapewa wiki tatu tu za kuwa hapa Bongo hatutaweza kufanya lolote.


Akaniahidi kuwa ikiwa atanyimwa kibali cha kurudi huko Ulaya basi tutaendelea na mambo yetu na akifanikiwa kuongezewa muda basi ataenda Ulaya halafu atanitumia mwaliko, akaniambia nimsaidie kusali apate kwa sababu akikosa itamchukua muda mpaka atafute kazi hapa Tz.


Mimi nikasali, na kweli Mungu akatusikiliza alivyoenda Ubalozini akapata Visa na akarudi zake Ulaya, November mwishoni 2009, tukawasiliana siku tatu tu, mara mawasiliano yakakata nikamtumia sms nikimuuliza vipi mbona siku hizi kimya sana? hakujiibu, na mara akawa hapokei simu na wala hajibu email wala sms kwa mwezi sasa.

Hapa nimebaki nashangaa nini kinaendelea tena?wakati tulikuwa ok kabisa. Kinachoniuma ni kwa nini hataki kuongea na mimi? kwa nini hapokei simu?na ni kwa nini hakuongea nami kuhusu mipango yake alipokuwa hapa?
Nifanye nini?naombeni ushauri.
Pne"

Dinah anasema:Asante sana kwa mail yako na pole kwa maumivu ya moyo na hofu kuu uliyonayo juu yampenzi wako, isije kuwa mpenzi wako kapatwa na masahibu makubwa huko aliko. Hebu kwa kuanzia tu ili kupata amani moyoni, check na ndugu au jamaa zake wa karibu kujua kama Mpenzi ni mzima huko aliko alafu tunaendelea na mengine nikirudi......

Mungu apishe Mbali!

Comments

Flav said…
Pole sana Dada
Inaweza ikawa mwenzako kapata matatizo.
maana hata mie mpenzi wangu yupo nje ya nchi ila sasa tuna mwezi hatujawasiliana.nimejaribu kufatilia kweli nimekuta kapata matatizo na yupo ndani(Selo.ivyo tafuta njia sahihi ya kupata jawabu la kukidhi.
Anonymous said…
pole sana mpendwa.

inaelekea huyo mtu hakuhitaji na anakutumia tu kwanza kitu kipi kilichomfanya akate hayo mawasiliano na wewe kimtindo huo?

pili hebu fikiria kwani mlishawahi kukorofishana na yeye kwa siku za hivi karibuni?

huwezi jua kapatwa na nini ila jaribu kuwasiliana mpe muda zaidi ila ukiona kuwa haeleweki jaribbu kujitune kivyako na uendelee na maisha yako.

yeye si kitu na wala haongezi kitu kwenye maisha yako naamini kama ukimsahau unaweza kusonga mbele na ukafanya mambo mazuri zaidi tena kuliko ulivyokuwa naye yeye.

ninachosema ni kwamba foget about him and take your own business ili maisha yaende vizuri my dia.

popote ulipo unatakiwa ujiamini sana tu naamini utasonga zaidi na zaidi.
Anonymous said…
pole sana mpendwa.

inaelekea huyo mtu hakuhitaji na anakutumia tu kwanza kitu kipi kilichomfanya akate hayo mawasiliano na wewe kimtindo huo?

pili hebu fikiria kwani mlishawahi kukorofishana na yeye kwa siku za hivi karibuni?

huwezi jua kapatwa na nini ila jaribu kuwasiliana mpe muda zaidi ila ukiona kuwa haeleweki jaribbu kujitune kivyako na uendelee na maisha yako.

yeye si kitu na wala haongezi kitu kwenye maisha yako naamini kama ukimsahau unaweza kusonga mbele na ukafanya mambo mazuri zaidi tena kuliko ulivyokuwa naye yeye.

ninachosema ni kwamba foget about him and take your own business ili maisha yaende vizuri my dia.

popote ulipo unatakiwa ujiamini sana tu naamini utasonga zaidi na zaidi.
Anonymous said…
Kuwa mvumilivu kidogo maana huko ulaya usisikie tu watu wanaishi huko..vijana wengi wanateseka tu ila basi wanapenda kuishi huko.
Subiri kidogo ukina kimya tafuta mwingine,mbona wako wengi shostie.
Anonymous said…
mh dada pole sana ndugu yangu, lkn hapo kuna mawili
1. mtu wako may be ana matatizo yamemkuta
2. anaweza kua na mtu lkn anashindwa aanze vp kukwambia

lkn usikate tamaaa keep on trying lkn unapaswa kua mvumilivu usiwaze sana usije pata magonjwa ya moyo bure, hata kama kakuacha take it as a part of life
Anonymous said…
holahola dada.Mimi nikiwa huku uhaibuni naweza kukueleza mambo yafuatyo:

Kwanza huyo jamaa inaelekea 'Kafulia" kwa sababu hiyo bills zimegonga mlangoni kiasi cha kumfanya jamaa ainame kubeba box isivyo kawaida ili kumudu hizo bills na hivyo kukosa kabisa muda wa kuwasiliana na wewe.Huo si utani jamaa wengi wakija bongo kutoka huku na wanaporudi hutawaona hadi hata miezi sita itapita au hata mwaka wakijaribu kukaba shingo madeni.Naamini alipokuja huko alitumia vilivyo na aliporudi huku alikuta bills zimejazana akazamia maboxini.

Pili, huyo jamaa amekueleza kuwa ana kazi huku na hivyo ana amashaka kama anaweza kusota sana akija huko bongo bila kupata kazi.Nadhani ana kausanii kidogo kazi gani anayo huku, maana kama ni mtu amekula shule vizuri huku aseme atakosa kazi huko nina wasiwasi naye, kazi anayoisemea bila shaka ni ya kubeba box tu.

Tatu, inawezekana ana mwingine huku, na huko ana wewe hivyo akija bongo ni mfalme na akirudi ughaibuni ni mfalme.Sidhani kama ana future yoyote nawe dada ukipata mtu nenda naye usijechelewa eti unamngija aliye ughaibuni.Hata hivyo endelea kufanya utafiti zaidi kuliko aidha kukurupuka na haya tusemayo wengine.
Kwa kuwa hujatueleza kuwa yuko nchi gani basi labda pia naweza kuwa bias mno maana mimi niko USA hivyo siwezi kubaini hasa mahali alipo jamaa kuna nini na mambo kadha wa kadha.

Naamini ulimkaangizia sana jamaa alipokuwa huko akala na wala hakusaza.Lakini panua macho ikiwezekana vaa miwani ili uone vema kulikoni.
pie said…
hi.
thnk ushauri wa dina upo, poa, chek na ndugu na rafiki zake wa karibu, kama anamawasiliano na hao wengine wewe ndo hakujibu basi jua ndo basi tena sio wako tena..so tafuta mwingine wa ukweli...........
gud luk
pie
Anonymous said…
Mambo ya Ulaya waachie walioko huko dada, mtu asije kukudanganya hasa katika masuala ya mahusiano, wakija bongo wanakamua utafikiri zimejaa kumbe kaputi tu.Sasa huyo amekudanganya kuwa ana kazi halafu kakata mawasiliano.

usipoteze muda naye weka mipango yako ya kimaisha vizuri kama atatokea basi ni vema kama ndo kayoyoma usiwe na punic yoyote wewe jiweke kivyako kukabili situation yoyote itakayojiri.
Amos Bwire said…
Lolote linawezekana dada. Maybe kapata 'mzungu wa kuzugia',ama kapata matatizo ya ugonjwa au kuswekwa selo, or maybe 'kazi' zimemzidia kiasi kwamba hata handset yake kaitupa(kaiuza) kimtindo. Kwa lolote kati ya hayo yaelekea msaada wako haukuhitajika kwake...hivyo sioni haja ya wewe kuchachawa na kwenda kuuliza ndugu na jamaa zake. Duh, hayo mambo sio yenyewe kabisa, ni kujitia aibu na kujidhalilisha especially pale utapokuta ndugu zake wanaongea naye kila siku, au weshatuma mtu huko ulaya kwenda kumtoa selo au kumuuguza jamaa(mh hili nalo nenoo!). Mapenzi yanajengwa na watu wawili tu, sio na wazazi, mawifi, mashemeji wala marafiki. Kama wewe ni wa muhimu kwake basi lazima angekujulisha kinachoendelea kwake maybe hata before hajawajulisha ndugu zake. Binti songa mbele na maisha yako, achana na hayo maigizo, it's 21st century, men love independent women. My take.
Anonymous said…
Nashukuru sana kwa ushauri wenu, mpenzi wangu alipiga simu kusema kuwa yeye yupo kimya kwa sababu mambo yake hayaendi vizuri kidogo kwa hiyo hajajua km niende kule au la. Mimi nikamuuliza ndio akate mawasiliano na mimi wakati watu wote anawasiliana nao?akasema anafanya hivyo kwa sababu anahisi nitaulizia mipango yetu wkt yeye bado anaangalia situation. Mimi kinachonishangaza ndio asiwasiliane nami? hata salamu?nikamwambia kwa nini tusidiscuss mimi na yeye kuhusu hiyo issue ili tujue la kufanya akasema tutaongea. Hajapiga tena na wala hawasiliani na mimi kwa email, sms wala simu,nikimwandikia sms kumtakia hali hajibu, wala email. Mimi naona mambo ya ajabu,naanza kuwaza mengine nahisi kama sio mkweli. Sijui la kufanya nampenda sana najitahidi kufuata ushauri wenu wa kukaa kimya na kuendelea na yangu nashindwa. Hii hali inaharibu utendaji wangu wa kazi yaani ananichanganya sana.