Monday, 30 November 2009

Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza lakini....-Ushauri

"POLE DADA DINAH KWA KUTUELIMISHA SISI, MIMI NAITWA KHALID J. WA ARUSHA NINA MIAKA 19 NAPENDA KUKUPA HISTORIA YANGU YA MAHUSIANO, tangia nizaliwe sijawahi kufanya mapenzi na msichana yeyote yule lakini huwa na fanya punyeto mpaka leo hii lakini huwa nasikia raha sana nikifanya punyeto.

Siku moja nimekaa na rafiki yangu akawa ananiadithia jinsi mtu akifanya mapenzi anavyojisikia utamu kuliko asali mimi nikatamani kufanya ngono ili na mimi nisikie utamu huo. Nikatafuta demu tukanyonyana denda baadae nataka niingize mboo nikashangaa niemwaga shahawa na mboo ikasinyaa ikakataa kusimaa.
NAOMBA UNISAIDIE NINA TATIZO GANI?"

Dinah anasema; Kharid, asante kwa ushirikiano na uvumilivuo wako. Hata hivyo natumai maelezo ya wachangiaji wangu yatakuwa yamekusaidia kinamna. Wewe bado unakua nakilichotokea ni kitu cha kawaida kabisa ambacho huwatokea wanaume wengi kwa sababu mbali mbali na moja wapo ndio hiyo kuanza ngono kwa mara ya kwanza.

Kujipa mkono au kupiga nyeto ni kitu kizuri na salama zaidi kuliko kutafuta mwanamke kwa ajili ya kungonoka tu. Ila unatakiwa kufanya nyeto ikiwa tu umeshindwa kabisa kujizuia sio kila siku mpaka uwe addicted....unatakiwa kujiwekea limit.

Ikiwa kwa kumfikiria mwanamke au maumbile yake huku ukijipa mkono ulikuwa ukifanikiwa kufurahia na hata kumwaga, sasa ukiwa na mwanamke halisi pale sio ndio utamaliza kabla hujaanza! Hilo basi ndilo lililokutokea....ulikuwa too excited na wakati huohuo ulikuwa na hofu kwa vile ulikuwa hujui nini cha kufanya bila kusahau aibu ambayo ndio iliongeza hali ya kutokujiamini na hivyo ukashindwa kabisa kusimamisha tena.


Ni vema kujijengea mazingira mzuri kabla hujajiingiza kwenye mahusiano ya ngono moja kwa moja. Ktk umri wako ilikuwa ni muhimu kusubiri na kuendelea na nyeto yako na kama ungemdondokea binti katika harakati za kuutambua ujinsia wako na ungeshindwa kabisa kuzuia hisia hizo basi ungerafikiana na binti huyo.

Kwenye kipindi hiki ungekuwa na hisia fulani za Ukware (be in lust)....kipindi hiki sio rahisi kuwa na Mapenzi (be in love) japokuwa unaweza kudhani kuwa you are in love lakini sivyo. Ni kipindi cha ukuaji, hakika ni kigumu sana na kinachanganya kweli kweli.

Urafiki huo ungekusaidia wewe na yeye kutambua ujinsia wenu kwa kubadilishana mawazo, kuongea, kutembea, kucheza pamoja, kujifunza, kubusu nakushikana na sio lazima mngengonoana(mfanye ngono) mpaka muda utakapofika na ninyi wawili kukua kidogo nakufikia miaka 21.....angalau.

Ngono katika umri wako haina maana yeyote, utasikia raha kwa sekunde 60 alafu itakuwa basi. Ningependa uzingatie masomo zaidi (kama uko shule) na muda ukifika basi utaikuta ngono inakusubiri na utaifanya sana na yule mmoja utakaempenda na yeye kukupenda na wote kwa pamoja mtajifunza mengi zaidi na kugundua kuwa Ngono ni zaidi ya ngono ukiwa na umri mkubwa.

Kila la kheri.

Sunday, 29 November 2009

Nataka kubaki juu, hatupati muda wa kufurahia ngono....

Hujambo mpenzi mtembeleaji wa kona hii? Haya ni maswali matatu kutoka kwa watu watatu tofauti. Asante kwa ushirikiano.

Mosi-"Dada dinah pole na kazi ngumu but keep it up 4 the gud job. Mimi naswali dogo tu jamani, hivi hiyo Ky jelly yauzwa kwenye ma-pharamacy????? na pili kirefu cha ky kipo na kama ndio je nini au ni jina tayari kama lilivyo? samahani kwa ushamba".

Dinah anasema: Asante sana. Ndio KY Gel (Jelly) inapatikana kwenye maduka ya madawa. Sina uhakika na kirefu cha K-Y nimejaribu ku-check na Johnson & Johnson ambao ndio wategenezaji Orijino wa KY-Gel nao wanadai kuwa K-Y haina maana yeyote na hainakirefu japokuwa ni jina la bidhaa yao hiyo maarufu na inayoendelea kuwa maafufu baada ya watu kuanza kuitumia kama kilainisho kwa ajili ya kungonoka.
Shukrani kwa ushirikiano.

************************************************************************


Pili-"Jamani kweli mambo mazito nimeona ila nami ninashida. Mume wangu hupenda sana kunilalia juu wakati wa kufanya mapenzi, yaani kifo cha mende. Nikiomba nimlalie yaani mie niwe juu yake anasema anakubali lakini tena ananigeuza halafu yeye anakuwa juu! nifanyeje ili nibaki juu bila kugeuzwa na kulaliwa?!!"

Dinah anasema: Mumeo anapenda ile hisia ya yeye kuwa mtendaji mkuu (being in control) na mkao wa yeye kupata hisia hiyo ni yeye kuwa juu yako au nyuma yako (mbuzi kagoma, kumbi-kumbi n.k). Vilevile inawezekana kabisa kuwa yeye kuwa chini inamfanya atake kumaliza mapema na yeye hataki kukuacha "solemba" hivyo basi anaamua kukugeuza ili kukupa raha wewe kabla yake.

Sasa kwa vile wewe pia unapenda kuwa in-control ni vema basi mkawasiliana na kukubaliana au kupena zamu, kwama "mimi naanza juu mzunguuko wa kwanza, alafu wewe utakuwa juu mzunguuko wa pili".

Kungonoka kwa mtu na mume wake ni fun na sio mashindano. Hivyo basi ganyeni maelewano na kisha furahieni uumbaji wake Mungu.

Kila la kheri.
****************************************************


Tatu-"Ahsante sana kwa mafunzo yako mimi nauliza hivi, mpenzi wangu (mwanamme) anafika haraka yaani anakojoa kabla mimi sija-enjoy. Je nifanyeje au tufanyeje?"

Dinah anasema: Wakati wowote unakaribishwa lovey, Mwambie "mpenzi naomba leo unisubiri mpaka nitakapokuambia nakojoa/jakuja/namaliza/ nafika n.k ndio na wewe umalize".

Kuna uwezekano mwenzako hajui kama wewe umefika au bado labda kwa vile humpi ishara au huonyeshi dalili. Kama unapiga kelele ili afurahie lakini sio kelele za wewe kufurahia ni wazi kuwa yeye atakuwa akudhani kuwa umefika sikunyiingi, kumbe masikini hata robo ya safari hujafikia.

Jaribu kuwasiliana nae kuhusiana na suala la wewe kutofika kileleni, vilevile jifunze namna ya kuita kilele mwenyewe pia jitume badala ya kumuachia yeye akufanye mapaka ufike, hakikisha wakati anaendelea na mchezo na wewe pia unakata kiuno kwa ajili yako sio kwa ajili yake (kuna tofauti hapo), pia jiweke katika mikao ambayo itakurahisishia wewe kufika haraka zaidi kama vile wewe juu kwa kukaa na kulala.

Vinginevyo mwambie mpenzi aanze na katerero ya uume au ulimi kabla hajamuingiza Abdalah kichwa wazi kunako. Kumbuka, ili kufurahia ngono wote wawili mnatakiwa kuwasiliana kwa uwazi.

Kila la kheri.

Saturday, 28 November 2009

Ndoa na Kaka wa kambo (step Brother) ni sahihi?

"Mimi ni msichana wa miaka 23, nina kaka yangu baba mmoja na mama tofauti. Yeye ananipenda na mimi nampenda na tumekwisha wahi kufanya mapenzi mara kadhaa. Yeye ameahidi kuwa atanioa. Sisi ni Waislamu, je ni sawa tunachokifanya kama sio sawa tufanyeje?"

Dinah anasema:Inasemekana na kuaminika kuwa Kibaiolojia na Kiuumbaji ( Mungu alivyotuumba ) mtu na ndugu yake hawawezi kutamaniana, ndugu kwa maana ya kuwa mmechangia damu ya mzazi mmoja. Lakini ndugu wengine kama Binamu, wapwa n.k. wanaweza kutamaniana na hata kupendana kwa vile hawachangii damu moja bali wazazi wao ndio wanaochangia damu.

Pia inasemekana watoto waliochangia sehemu moja ya damu (kama wewe na kaka yako wakambo) wakitamaniana ina maana kuwa uwezekano mmoja wenu sio toto halisi (Kibaolojia) wa baba. Yaani huenda wewe baba yako ni mwingine na sio huyo unaeamini kuwa ndio baba yako au kama wewe ni mtoto wa huyo Baba basi kuna uwezekano kuwa huyo kaka yako sio mtoto wa kweli wa Mzee wenu (mama zenu ndio wanajua ukweli halisi ktk hili au mfanye vipimo vya DNA kujua ukweli).

Kwenye jamii yeyote ile Duniani bila kujali Imani zao za kidini mtu na kaka yake waliochangia damu hawaruhusiwi kuwa wapenzi achilia mbali kufunga ndoa na kuzaa, kwa baadhi ya nchi za Ulaya ndugu kupendana ni kosa la jinai.

Kama hisia za mapenzi ni kali sana miongoni mwenu (which sio kawaida kwa ndugu) basi ni wazi kuwa ninyi sio ndugu na hivyo mnapaswa kuanza mikakati ya kutafuta ukweli kuhusu baba yenu na njia pekee ni either kuongea na mama zenu ili kuwapa ukweli halisi au kufanya DNA test.

Namna ya kupata ukweli:
Msikurupukie mama zenu na ku-demand bali mnahitaji kuwa na mipango nakujua namna za kupata ukweli bila wao kujua kama mmekwisha wahi kungonoana, mana'ke wakijua tayari mnamahusiano mtarushiwa shutuma na mtashindwa kujitete na wao kina mama watakuwa saved kutokana na "kutokujua baba yako au baba wa kaka yako".

Wewe na yeye kwa nyakati tofauti na kila mtu kivyake zungumzeni wazazi wenu wa kike......mwambie "mama mimi nahisi kama vile huyu sio baba yangu! Sina mapenzi wala hisia za baba na mtoto, unadhani kuna uwezekano kuwa huyu sio baba yangu?"......atakupa jibu, hakikisha majibu yake sio ya kusita na wala haonyeshi mshituko pia ukali lakini kama atashituka, kuwa mkali na kusita ujue kuna walakini.

Mwambie kwa kusisitiza kuwa " nataka kujua ukweli kwanini napata hisia hizi, hivyo nitaenda kufanya vipimo vya DNA ili nijue kama kweli huyu ni baba yangu"......mpe muda!

Sisemi kuwa huo ndio ukweli kuwa huyo Mzee sio baba yenu halisi bali kuna uwezekano mkubwa sana kuwa ninyi wawili sio ndugu! Nadhani mmoja wenu huyo sio baba yake mzazi bali ni baba mlezi (alisingiziwa au mama alikuwa hana uhakika na aliyem-mimba).

Kumbuka kuna asilimia kubwa ya akina baba ndani na nje ya ndoa nchini Tanzania wanalea au walilea watoto ambao sio wao. Ili kujua ukweli, ni mama pekee anatakiwa kutoka msafi au kufanya vipimo vya DNA.

Vinginevyo Ni mwiko kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote ambae mmechangia damu. Toka kwenye uhusiano huo mara moja na usirudie tena.

Kila la kheri!

Friday, 27 November 2009

Wangu hakojoi, hata akienda masaa 2-Nini tatizo?

"Mie tatizo langu tofauti kidogo, Mpenzi wangu hakojoi yaani anaweza akaenda wee mpaka hata masaa mawili lakini haachii uji. Saa nyingine tunafanya mapenzi mpaka tunachoka tunaacha lakini hakojoi sasa sijui hili linasababishwa na nini? nisaidieni jamani "

Dinah anauliza:Mmekuwa pamoja kwa muda gani na Je huwa wote mnafika kileleni? Kumbuka kilele cha mwanaume au yeye kufurahia tendo sio lazima amwage uji a.k.a cream anaweza akafurahia na kufikia mshindo bila kumwaga!!

Naona umehsindwa kunipa jawabu ndani ya wakati ili niweze kukupa maelezo ya uhakika zaidi, hata hivyo nitakujibu kama hivi:-

Mwanaume kuchelewa kumwaga ni kawaida kabisa as long as anapata utamu (kuna dalili za mwanaume kusikilizia utamu au hata kufika kileleni na kilele cha mwanaume sio wakati wote kinaambatana kutoa manii). Wewe kama mwanamke hupaswi kuwa na shaka kama unaona dalili hizo.

Lakini kama haonyeshi dalili zozote zaidi ya kutokwa jasho na kuonyesha kuchoka basi ni wazi kuwa anahitaji msaada wako ili kufanikisha hilo linalokutia mashaka wee Binti mrembo!

Isije ikawa wewe hujui namna ya kumhamasisha wakati anaendelea kukufanya, hebu jaribu kumpa mikono, kish ampe mdomo kwa muda mreefu kabla hamjaanza kufanya mapenzi na wakati mnaendelea kungonoana jipinde na myonye chuchu, nyonya shingo, toa sauti za kuonyesha unasikia raha (hakikisha ni za kweli), mtie ulimi sikioni wakati anaendelea na mchezo, papasa makalio yake namshike-shike taratibu na kwa mahaba sehemu mbali mbali za mwili wake.....vilevile jaribu kuwa mbunifu na tafuta mkao utakao mfanya apate raha bin utamu.

Kitu kingine muhimu unachotakiwa kuzingatia ni kujua mikao maalum kwa ajili ya mwanaume pia kutokuonyesha kuwa umechoshwa na ufanyaji wake, hakikisha tendo hilo linakuwa la kufurahia na jaribu mikao tofauti ili kukuondolea "hali ya kuchoka".

Kila la kheri!

Thursday, 26 November 2009

Ni wakati wa kutumia Mkuyati huu?-Msaada!

"Hello Dinah,
Mimi mwanaume wa miaka 29, napenda nitumie fursa hii kutafuta suluhu ya tatizo langu. Miaka kama mitano hivi iliyopita nilikuwa na uwezo wa kumtomba mwanamke hata bao saba. Lakini siku hizi uwezo wangu umepungua sana, yaani naweza nikaingiza mooo kumani lakini dakika 2 tu nishapizi halafu nakuwa kama na mzingua ninayekuwa nae.

Mbinu nyingi zinazoandikwa hapa na kwingineko hata mpenzi wangu sometimes amejaribu sana kutumia maujuzi mbalimbali lakini wapi. Japo nimejaribu mbili, kwakweli nilikuwa nafikiria kama kuna uwezekano hata wa kupata kitu kama ni viagra, au mkuyati nisaidieni niondokane na hii fadhaa. Muga"

Dinah anasema: Muga, jinsi mwanaume anavyokua uwezo wake wa kungonoka unapungua, MF-Kama ulikuwa na uwezo wa kuondoka mizunguuko nane kwa siku ulipokuwa early 20s sasa kwenye late 20s utaenda mizunguuko michache. Kwa mujibu wa maelezo yako ni kuwa Miaka mitano nyuma ulikuwa unapiga bao tano, lakini sasa huchukui dakika 2 umemaliza, Je pamoja na kumaliza kwako mapema unaweza kwenye mizunguuko mingapi au kupiga bao ngapi?

Wewe umejaribu mbili, yeye kajaribu maujuzi kibao......maujuzi gani hayo? Mbinu za kumsaidia mwanaume asimwage haraka haziko nyingi hivyo na kwa kifupi sio ujuzi ni vitu vere vere rahisi na straightfoward!

Unatakiwa uwe umejaribu yote yaliyosemwa hapa na kujitahidi kwa kila uwezalo kabla hujakubali kuwa umeshindwa kabisa kujizuia kumwaga haraka na sasa unataka Dawa. Kwa kawaida ukiwahi bao la kwanza mabao mengine yanayofuata huchelewa hata kama ni kwa dakika kumi, haiwezekani kabisa kila mzunguuko wewe uchukue dakika mbili tu.

Mazoezi, wewe na mpenzi wako kuwa watundu na kugundua mikao gani inakuhamasisha kuliko na ile inayokuchelewesa, Pia unatakiwa kuendelea kujifunza namna ya kujizuia kila unapokaribia (jifunze ku-control akili yako).....haitochukua siku mbili au miezi 3, inachukua muda mpaka akili yako kuzoea namna ya kujizuia. Wakati unaendelea na hayo tafadhali jaribuni kufanya mapenzi ndani ya maji, vilevile tumia mpira (condom), hizi ni moja ya mbinu ya kumchelewesha mpenzi "kucheka mapema".

Wewe huitaji kutumia Mkuyati na dawa nyingine kama hizo, kwani kazi ya dawa hizo ni kusaidia uume kusimama sio kuzuia kumwaga, sasa kama wewe unauwezo wa kusimamisha kwanini ujitafutie matatizo mengine ya kiafya?.

Kila la kheri!

Tuesday, 24 November 2009

Nimefumania, nikangonoka nae same day, mimba yangu?-Ushauri

"Mambo vipi Dinah,
Mimi naitwa D niko Moro, ninampenzi wangu ambaye nampenda sana ila kunashida moja imeanza kujitokeza nayo sio ya kawaida. Ni miaka minne sasa tangu niwe nae kimapenzi na matarajio yetu ni kufunga ndoa mara baada ya kumaliza masomo yake.

Miezi kadhaa iliyopita tabia yake imekuwa ikibadilika na siku moja nilikamata sms za wanaume wawili kwenye simu yake, sms hizo zote zilikuwa zikimtaja yeye kama mke yaani kila mmoja kamuita mkewake, niliumia sana kwani hiyo ilikuwa first time kumfuma tangu niwe naye.

Wiki iliyopita nimemfuma akiwa na moja ya wale wanaume ambao nilifuma sms zao wakitoka gesti asubuhi na mapema ambapo usiku huo wote simu yake ilikuwa haipatikani, nilimbana kwa kuuliza maswali kadhaa akakiri kuwa alikesha na yule jamaa na nilimsamehe kwa kuwa sikujua cha kufanya kutokana na upendo wangu kwake.

Baadaye nilifanya naye mapenzi siku hiyohiyo niliyomfuma kwa kuwa nilikuwa sijatombana naye kama mwezi mzima na hivyo ikaniuma kuona jamaa anakula kilaini wakati mimi na msubiri amalize skul.

Sasa leo nimeona dalili za mimba kwake, matiti yake yamevimba na anadai chuchu zinawasha na tumbo limekuwa likimuuma mara kwa mara, nahisi nitabambikiwa mimba muda si mrefu, hebu nisaidieni jamani mimi bado nampenda lakini hali inazidi kuwa tete.
Nifanyeje? D"

Monday, 23 November 2009

Mikono mikubwa kuliko mwili....nitapendeza gauni la Harusi?"Pole kwa kwa ngumu dada Dinah.
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 tatizo nililonalo ni kwamba, mikono yangu ni minene kuliko mwili.

Nina umbo zuri, sura nzuri lakini mikono imezidi. Nahofia siku ya harusi yangu sintapendeza, kwa kawaida huwa sivai nguo za mikono mifupi au midogo. Nimekaribia kufunga ndoa na wasi wais wangu ni mikono, je kuna namna yeyote ya kuipunguza au hata kama kuna dawa yoyote unayoijua ya kupaka naomba unisaidie au kama kuna mazoezi yoyote ya kupunguza mikono. Mpenzi wangu huwa ananiambia huna mikono minene basi mimi sipendi, wakati najua ni minene"Dinah anasema: Hey mtarajiwa, hongera sana na kila la kheri ktk maandalizi ya kufunga ndoa. Hakika suala la kutafuta na kupata gauni litakalokupendeza kutokana na umbile lako sio kazi rahisi, hata hivyo shukrani kwa wabunifu wa mitindo yanguo za kufungia ndoa kwani wanabuni kutokana na maumbile ya watu.Ukubwa wa mikono itakuwa ni sehemu ya umbile lako na hivyo sio rahisi kuifanya iwe midogo au miembamba, pamoja nakusema hivyo kuna aina ya mazoezi ya kuifanya mikono yako kuwa "firm" na hivyo kuonekana minene lakini haijajitokeza kwa nyuma au kwa chini (kama mbawa), tafadhali kama utakuwa tayari mimi kukuelekeza namna ya kuzoezika basi usisite kuniandikia.Vinginevyo mimi nakushauri uchague Gauni ambalo litaficha mikono yako (angalia picha hapo juu), usifuate trend kwamba kila mtu anavaa gauni bila mikono basi na wewe utake hivyo (mara nyingi huwa too common) na badala yake nenda kwa a classic one lakini inayoendana na umbile lako.


Kila la kheri na furahia siku yako ya ndoa.

Sunday, 22 November 2009

Ndoa inanishinda, wanangu wadogo-Nifanyaje?

"Hello dada Dinah, pole kwa majukumu mpenzi.
Mie ni mwanamke wa miaka 29 na nina watoto 2 na nipo kwenye ndoa kwa miaka 4 sasa. Tatizo langu Dada Dinah ni kubwa, naomba msaada pamoja na wanablog wote.


Mume wangu ni mfanya biashara na mie ni mfanyakazi nilieajiriwa na Institution moja kubwa tu hapa ninapoishi, sasa mume wangu hafanyi lolote katika ndoa yetu, namaanisha hajihusishi na matumizi au manunuzi au gharama zozote za kifamilia jamani.


Kila kitu naachiwa mie, kuanzia bills, matibabu, mavazi ya watoto na garama nyingine zangu kama mwanamke. Kila ninapojaribu kumuelewesha anadai hali ni ngumu, lakini hata kama ni ngumu yeye kama mwanaume si anapaswa kufanya any means apate at least chochote haiwezekani ufanye kazi then ukose hata hela ya kununua chupi jamini!

Dinah anasema: Nafikiri mume wako kapoteza hali ya kujiamini kutokana na kuoa a powerful woman, mwanaume yeyote duniani hawawezi kabisa ku-keep up na mwanamke anaejituma na kujiweza kiuchumi. Hudhani kuwa anadharauliwa na kutawaliwa na mwanamke hivyo atafanya kila awezalo ili aweze kupata zile hisia za kuwa yeye bado ni wanaume kamili na wakati mwingine atakaka kuonyesha hilo kwa mwanamke ambae atamtegemea kiuchumi.


Yaani hata ukijaribu kuwasiliana kikawaida tu kuhusiana na masuala yenu ya ndani kama watu wengine kwenye mahusiano mwanaume huyu either atadharau na kutokukupa jibu muafaka or ataibua mzozo bila sababu ya msingi ambao utakufanya wewe ushindwe kumuelewa na kwa hasira unaweza kulipuka na kusema maneno makali yenye ulalamishi kutokana na kutokupata ushirikiano wake.


Ili kuepusha mwanaume asipoteze hali ya kujiamini kama mwanaume wewe mwanamke mwenye nguvu kiuchumi kuliko yeye unatakiwa kuendelea kumuachia sehemu yake kwenye familia kama baba, pamoja na kuwa labda wewe ndio utakuwa mtoa pesa haina maana ndio uwe mfanya maamuzi pia, ulipaswa kuhakikisha kuwa unampa nafasi ya kufanya maamuzi makubwa kwenye familia yenu ndogo.


Natambua wakati mwingine unaweza kufanya maamuzi makubwa mwenyewe ukidhani unamsaidia mumeo as kasafiri au anashughuli nyingi, lakini kumbuka sisi wanawake tunachukulia mambo tofauti sana na wanaume.

Humsaidii mwanaume kwa kufanya maamuzi ambayo yeye anadhani ni jukumu lake, unatakiwa kumshauri na kumpa ushirikiano lakini sio kumsaidia kwa kutenda, yeye atahisi kuwa unachukua nafasi yake na hatopendezwa kabisa na hilo.

Pili ana mahusiano nje ya ndoa na hili nina ushahidi wa kutosha baada ya kusoma sms ktk simu yake akimuagizia mwanamke guest na chumba namba Fulani amkute, kuuliza tu ilikuwa ugomvi mkubwa hasa na akaamua kuweka password kwenye simu yake.

Dinah anasema: Ofcoz lazima awe mkali kwani anajua kabisa kuwa amekosa na hayuko tayari kuacha kutenda kosa hilo. Kuna uwezekano mkumbwa huyu mumeo anapoteza senti zake huko nje ya ndoa yenu katika harakati za kutafuta "heshima" kama mwanaume.

Wanawake hao wa nje ni wazi kuwa wanamtegemea kiuchumi au hata kama hawamtegemei basi kuna heshima fulani wanampe kwa vile yeye ni mtoa pesa/offers kwenye mihangaiko yao ya kujistarehesha, kitendo cha mumeo kukusaliti kunampa hali ya kujiamini yeye kama mwanaume kwa vile ndio mfanya maamuzi ya matumizi ya pesa zake na sio huyo Hawala.

Tatu Sina hamu yoyote ya mapenzi na yeye tena, sio tu kwa sababu ya ulevi na harufu ya pombe kunikosesha hamasa pia kule anapolewa huwa hajitambui kabisa na wakati mwingine. Kingine anatumia tumbaku basi kinywa chote kinakuwa na harufu.

Mume wangu anatoka asubuhi kwenda ktk shuguli zake akirudi hiyo usiku haogi anajitupa kitandani kama mzoga bado atataka mfanye mapenzi jamani hiyo hamasa itatoka wapi ndugu zangu, na hapo wala hakutakuwa na maandalizi yoyote zaidi ya yeye aingize uume wake tu na akojoe basi.

Dinah anasema: Inaelekea ninyi hamna mawasiliano mazuri kama mke na mume, wapenzi na wazazi.Inaelekea kila tu anafanya mambo yake kivyake na kufanya maamuzi kivyake. Kutokana na maelezo yako hapa nadhani huyu bwana anasumbuliwa na masumbufu ya akili ( stress, au some sort of depression).

Kama biashara haendi vema na yuko hatarini kuipoteza kutokana na matatizo ya kipesa ni wazi kuwa anamawazo mengi kiasi kwamba anaamua kuwa mlevi ili kuficha/sahau yanayomsumbua na kujiachia/kutojijali tena kwama haoni sababu ya kufanya hivyo kama atapoteza biashara na kuanza kumtegemea mkewe kwa kila kitu.

Kwenye suala la kufanya mapenzi ningekupa ushauri kama angekuwa hana kimada, kwa sasa nenda kaangalie afya yako ili kujua kama hajakuambukiza Vijidudu vya HIV, ikiwa huna Mshukuru Mungu. Kisha anza harakati za kukusaidia kufanya uamuzi wa busara.*******

Wakati mwingine nafikiria hata kutafuta mwanaume mwengine wa kunipa raha lakini naogopa dada Dinah kwani watoto wangu bado wadogo na nisingependa waanze kuona wazazi wana tofauti kwani wanahitaji malezi ya baba na mama bado.
Plz naomba msaada wako dada Dinah, na samahani kwa msg ndefu.
Ni mimi Dada Line."

Dinah anasema: Asante dada Line, majukumu yanakamata kweli lakini ndio sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Aisee pole sana kwa yote unayokabiliana nayo, yaani kwa kifupi wewe ni single mum with a husband yaani kwa kifupi huyo mume hana umuhimu wowote kwani hakuna mapenzi, ushirikiano wala support!

Ni matumaini yangu maelezo na ushauri mzuri kutoka kwa wachangiaji utakuwa umekufumbua macho na kukuwezesha kuanza harakati muhimu za kuokoa ndoa yako kama sio kuiua kabisa. Kwa haraka haraka unaweza kudhani kuwa tatizo ni kumbwa, lakini kutokana na uzoefu wangu tatizo hili sio kubwa kiasi hicho kama utatulia na kuangalia nini hasa kinaweza kusababisha yote hayo yanayotokea baada ya miaka 4 ya ndoa.

Nina uhakika kuwa mlipokutana na kukubaliana kufunga ndoa mumeo hakuwa hivyo alivyo hali kadhalika wewe hukuwa hivyo ulivyo, lakini jinsi miaka inavyozidi kwenda wote wawili mnaanza kujisahau na kila mmoja wenu kumlaumu mwenzie "kimoyo moyo" as nimegundua kuwa uhusiano wenu sio wazi na hauna mawasiliano ya kutosha.

Kwenye ulimwengu wa sasa huwezi kuvumilia na kukaa unasali/omba Mungu akusaidie mumeo abadilike bila wewe mwenyewe kuchukua hatua kwa vitendo, Mungu anakusaidia akiona na wewe unajituma, unajitahidi kumuonyesha mumeo njia njema kwa vitendo na hapo Mungu nae ataona kuwa una nia ya kuokoa ndoa yako.

Kule kwetu (nitokako mimi) huwa tunaambiwa kuwa, linapotokea tatizo kwenye ndoa wewe kama mwanamke ndio unatakiwa kuhakikisha ndoa inasimama. Ikiwa mtaachana basi Makungwi(Shangazi/Bibiz) watakulaumu wewe kwa kutokuzingatia mafunzoa yao, ndio maana kila baada ya muda unatakiwa kwenda nyumbani kutoa ripoti na kama kuna tatizo/mapungufu basi unaelekezwa namna ya kutatua n.k.........

Hivyo basi kabla mwanamke uliyefundwa hujaanza kurusha lawama na malalamiko unatakiwa ku-review uhusiano wenu na kutumia mbinu na njia zote ulizofundwa kufanikisha hilo. Anyway!

Mimi binafsi siamini katika Talaka kwa mtu unaempenda na yeye anakupenda unless otherwise mumeo anatishia uhai wako na watoto pamoja na kusem ahivyo sitokushauri uvumilie bali nitakuambia tafuta muda, nafasi na mood ya kuzungumza na mumeo na wote kwa pamoja mshirikiane kuokoa ndoa hii kwa faida yenu na watoto.

Nikirudi nita-share hatua muhimu za kufuata ili kusaidia wewe na mumeo kusimama tena kama wapenzi.

Thursday, 19 November 2009

Sina hamu na mume wangu Kingono-Ushauri

"Mambo dinah, iko hivi mume wangu alikuwa akicheat. Baada ya kuchunguza nikabaini na yeye amekili kuwa alikuwa anatoka nje ya ndoa yetu. Tatizo langu ni kwamba nimeishiwa hamu ya kufanya mapenzi na mume wangu, yaani sina hamu hata kidogo.

Najaribu lakini akili yangu haiwi pale, sifurahii wala sina ile kulalamika kwa mahaba wala kumpa yale mapenzi motomoto naomba msaada wako plz. Jamila (mrs) Hans."
Dinah anasema: Mrs Hans, mambo ni shwari kabisa hapa, asante kwa kujali. Pole kwa unayokabiliana nayo, kabla sijakupa maelezo tafadhali soma topics za zamani kuhusu cheatng kwa kubonyeza hapa, hapa , hapa na hapa kwa majibu niliyompatia mwenzio aliyepatwa na same tatizo. Ofcoz kila issue iko tofauti na nitakuja kukupa ushauri kutokana na maelezo yako.
Nimatumaini yangu sehemu ya maelezo hayo yamesaidia kwa kiasi fulani kukabiliana na tatizo lililojitokeza kwenye ndoa yako. Kama ulivyoona kwenye moja ya Topic zangu ni kuwa baada ya kutendwa kuna hatua za kufuata ili kuponyeka. Huwezi kusema "nimekusamehe mume wangu" kisha wewe na yeye kutegemea kuwa kila kitu kikarudi kama vile zamani. Sio rahisi.
Kabla ya kuendelea na ndoa na hata kusamehe unahitaji kujua kwanini hasa mumeo aliamua kusaliti wewe na ndoa yenu? Nini hasa kilimpeleka huko nje.......angalia kama mnaweza kubadilisha jambo/mambo ili kuzuia hilo lisitokee tena (najaribu kusema angalieni uhusiano wenu kwa undani ili kugundua nini kimepungua na kwa pamoja as a team rekebisheni).
Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa umefanya uamuzi wa kuendelea na ndoa baada ya mumeo kukusaliti na hivyo basi ni wazi kuwa umemsamehe na unajitahidi kusahau ili kujenga hali ya kumuamini tena. Hili linapojitokeza kwenye ndoa au uhusiano wa kimapenzi huwa linaumiza sana hisia na linaweza kukufanya wewe uliyesalitiwa kufanya maamuzi ya haraka kutokana na maumivu vilevile hasira.
Lakini ni vema kukumbuka kuwa huwezi kufanya uamuzi wa busara wakati unahasira having said that sina maana kuwa ku-cheat ni sahihi na uamuzi wa busara ni kubaki kwenye ndoa...la hasha! Uamuzi wa busara unaweza kuwa ni kubaki au kutoka kwenye ndoa hiyo, suala muhimu ni kufanya uamuzi huo ukiwa umetulia kiakili, kihisia na kimwili.
Baada ya tukio kubwa na la kikatili kama hilo kutokea kwenye ndoa na wewe kuamua kusamehe ili ndoa yenu iendelee, itakuchukua muda mrefu kabla hujaanza kumtamani mumeo kingono, hata kama unahisi hamu ya ngono kuna uwezekano mkubwa akikugusa au ukimuona tu nyege zote zinarudi zilikotoka.
**Baadhi ya wanawake hulalamika kuwa wanapojaribu kufanya mapenzi na waume zao hupatwa na hisia za wanaume hao kufanya wafanyao kwa mwanamke mwingine hali inayowa-put off nahivyo kushindwa kuendelea na tendo.
Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa aliyetendwa, mumeo anapaswa kulijua hilo na kukupa support na kukuhakikishia uaminifu wake kwako, kuongeza mapenzi ya hisia kwako na vitendo (sio kimwili), kuongeza mawasiliano n.k.
Wakati hayo yanaendelea kutoka kwa mumeo, wewe jipe "therapy" kwamba acha kutopoteza muda na kuwaza juu ya ngono na mumeo au namna ya kumridhisha na badala yake jaribu kufurahia maisha katika mtindo mwingine (ikiwezekana badilisha mtindo wako wa maisha) hali itakayokufanya ujisikie vizuri wewe kama mwanamke, utajiongezea hali ya kujiamini, utahisi kupendeza na kuvutia vilevile usisahau kujiongezea maujuzi (review maisha yako ya kingono) ili ujue wapi panahitaji up to date.
Najua unaogopa atatoka tena kama usipompa ngono, lakini na kuhakikishia kama utakuwa unapendeza, unavutia, unaonyesha furaha, unaonge nae bila chuki wala kinyongo LAKINI ngono hapati, itamfanya ajishtukie (hakuna kitu wanaume wanaogopa kama kutombewa wake zao) hivyo basi hatokwenda nje, atataka kujua ni nani hasa anakupa furaha na kukufanya upendeze hivyo yaani ka jinga vile atagundua kuwa anamwanamke bomba na hivyo kuongeza mapenzi kwako hali itakayosaidia wewe kuanza kuwa comfortable kuanza kufanya nae mapenzi.
Ikiwa baada ya muda (miezi michache) hujapata hamu yakutaka kungonoka na mumeo basi wote wawili mtahitaji kupewa Ushauri kwa pamoja ili kila mmoja wenu ajue wajibu wake, ikiwa mumeo hajui ni kiasi gani kitendo chake kichafu kimekuathiri kiakili, kihisia, kimwili na kisaikolojia na nini anapaswa kufanya ili kusaidia uponaji wako.
Kama hakuna mawasiliano ya kutosha kati yenu (kwamba wewe una deal na yote haya peke yako as if ndio mwenye makosa) ni wazi kuwa muda wa ku-heal utakuwa mrefu kuliko kawaida na ndoa inaweza kuharibika as wewe hutokuwa mwenye furaha na amani na yeye anaweza kuamua kuendelea na mchezo wake mchafu akidhani kuwa humjali anymore au kuna mtu anamsaidia nje.
Kama kuna mahali hujanielewa au unataka maelezo ya ziada, tafadhali jisikie huru na usisite kunitafuta.
Nakutakia kila la kheri!

Wednesday, 18 November 2009

Sitaki kumpotezea muda na nimekuwa honest,lakini hanielewi-Ushauri

s"Dada Dinah, ni mara yangu ya kwanza kukuandikia lakini nimekuwa nafuatilia sasa blog yako hii na kwa kweli ni kitu ambacho tunakihitaji sana kwani inasaidia sana kufumbua matatizo mbalimbali ya kimapenzi.

Sasa mimi nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa mbali kwa muda wa miaka mitano hivi, kutokana na mimi kuwa nje ya nchi. Katika kipindi chote hiki tumekuwa katika mawasiliano ya mara kwa mara ambayo kwa kweli yamesaidia kuweka live penzi letu.

Sasa kwa jinsi mambo yalivyo ukiwa nje ya nchi ni kwamba mambo yanaweza kuwa unpredictable sana, kwani kutokana na mambo yanavyokwenda sioni kama nitaweza kurudi nyumbani hivi karibuni, kwa kuzingatia hilo na pia kwa kuzingatia kwamba umri unakimbia sana mimi nina miaka 31 na mpenzi wangu ana miaka 30 nikaona kuwa itabidi kuchukua maamuzi mazito.

Kwahivyo nikamwambia mpenzi kuwa mimi naona kuwa ni vizuri kama kila mmoja wetu akaamua kumove on ikitokea kuwa atapata wa kumfaa ili isije ikafika kesho na kesho kutwa tukaza kupeana lawama kutokana na ukweli kuwa labda nikarudi nyumbani tukakuta kuwa hatuwezi kuishi pamoja sababu labda wote wawili tumebadilika sana kwani tumekuwa mbali mbali kwa muda wote huu kufikiria kuwa tungeishi pamoja.


Nilipomueleza hivyo mwenzangu aliumia sana na ikawa akinitupia lawama mimi kuwa eti labda nimepata mwingine na ndio maana naamua kumtosa, lakini kwa ukweli ni kuwa mimi nilikuwa naangalia picha nzima kwamba tusiwe tunapotezeana wakati kwani umri wetu ndio unakimbia.

Kwa jinsi mwenzangu alivyo react ni kwamba hakubaliani na hilo na kwakweli ameumia sana kitu kilichonifanya nijidoubt labda uaamuzi niliochukua si sahihi kwani imefikia mahali inaniumiza kichwa sana. Ukweli ni kuwa I do care for her lakini inabidi mara nyingine uangalie jinsi hali halisi inavyokwenda katika maisha.

Sijui wewe na wadau wengine mnaonaje kuhusu swala hili, naomba msaada na mawazo yenu wote. Ahsante sana na samahani kwa mail ndefu kama hii, tuendelee kuelimishana katika swala zima la mahusiano"

Dinah anasema:Asante kwa kuniandikia, nadhani kosa ulilofanya hapa ni kufanya uamuzi ulioegemea upande mmoja tu (upande wako peke yako) bila kumuhusisha yeye (mpenzi wako), umefanya uamuzi kisha ukampa matokea....yaani hamkuzungumza na wote wawili kukubaliana kumaliza uhusiano au kutafuta namna nyingine ili uhusiano wenu uendelee.

Mwanamke yeyote mwenye mwanaume Ulaya anatarajia Big, sasa unapomuibukia na kumaliza uhusiano ktk mtindo huu, kidogo inakuwa ngumu kuamini, kuelewa na kukubali.

Kumbuka mko kwenye uhusiano na kama walivyogusia baadhi ya wachangiaji, inawezekana katolea nje wanaume wengine wengi tu kwa ajili yako kwa vile aliamini kuwa siku moja mtakuja kuishi pamoja.

Mimi nakushauri, uzungumze nae na umpe picha kamili ya maisha ya huko uliko. Kwasababu, watu wengi hapa nyumbani hawajui ni kiasi gani maisha yanaweza kuwa magumu huko Ughaibuni (ugumu interms of kutoruhusiwa kutoka nje mpaka wakurudishie kitabu chako, unaweza ukasubiri milele*).

Ukiweka wazi ni nini hasa kinakuzuia wewe kusafiri au hata kurudi nyumbani kwa sasa na hujui lini utaweza kufanya hivyo, akikuelewa ndio uanze kuzungumzia suala la uhusiano wenu. Hakikisha unampa nafasi yeye kukuambia msimamo wake na nini hasa anataka out of uhusiano wenu....msikilize kwa makini. Kisha mpe maelezo kutokana na matarajio yake au atakayo out of uhusiano huo.

Weka kila kitu wazi, kama kuna uwezekano wa yeye kukufuata uko nini afanye na kama hakuna mwambie kwa uwazi kabisa kwanini haiwezekani, kwa sababu kibongobongo wapenzi hutegemea sana kupandishwa majuu lakini hawajui urahisi na ugumu wake.....sasa mpe hali halisi.

Hakuna uwezekano wa kukufuata na huna mpango wa kurudi Bongo sasa:
Mwambie hali halisi kuwa, umri aliofikia wanawake wengi hupenda kuanza kujiandaa na ndoa, kuanza familia n.k. na wewe ungependa kufanya hivyo lakini unasikitika kuwa hutoweza kutimizia hayo kutokana na umbali na mambo yanavyokuendea huko uliko. Muombe radhi kwa kumpotezea muda kwani mipango haikuwa kama ulivyotarajia.

Akikubaliana na wewe, ahidi kuendeleza urafiki na wasiliana nae kila upatapo muda. Akiendelea kutokukuelewa na kukutupia lawama then punguza mawasiliano kama sio kuyakata kabisa.

Kila la kheri!

Tuesday, 17 November 2009

Anataka nifanye Masters pia niwe msiri-Ushauri

"Mpendwa dada Dinah. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 naishi jijini DSM. Nimekuwa nikifuatilia na kusoma mambo mbalimbali na ushauri wako na comments za washirika tofautitofauti. Nimeona bora nije na hii yangu ambayo kwa ukweli inanichanganya kichwa.

Ninae boyfriend kwa hapa nitamwita X mwenye miaka 26, nimekutana nae chuoni mwaka 2006 nikiwa naingia mwaka wa kwanza na hadi sasa tumeshadumu miaka 3. Tulikuwa darasa moja huko chuoni ila yeye kwa sasa anaendelea na Masters ambapo kwa mimi plan ni next year ndiyo niisome hiyo masters kwani sikupenda kuunganisha.

Mwanzo alipoanza kunidate alikuwa mtu mzuri sana, muda wote alikuwa karibu na mimi na tulipoanza mahusiano mambo yalibadilika kidogo japo aliniambia kuwa yeye ni busy person. Tulikuwa tunaonana kwake siku za weekend tu tena mchana. Siku za kawaida na hata kama ni darasan ni salaam tu basi then kila mtu na muda wake.

Nilipomuuliza alinijibu kuwa yeye ni mtu anaependa privancy hasa kwenye mambo yake ya binafsi kama mahusiano. Tuliendelea hivyo japokuwa alinitambulisha kwa baadhi ya marafiki zake wa chuoni na hata wa kazini kwake akiwemo Boss wake. Kitu ambacho kilinishangaza katika usiri wake ambao ulikuwa ni chuoni tu, kwani tukishatoka chuoni alijitahidi kuwa close na mimi.

Mara moja moja tulipokuwa darasani alikuwa anakuja kukaa na mimi na mda mwingine hapana, japokuwa darasa zima lilikuwa likikujua kuwa tunadate na walikuwa wanatushangaa tunavyoact kama hatujuani.


Hapo ndipo mambo mengine yakaanza, akaniambia anataka watu wachanganyikiwe kwamba wasiwe na uhakika kama tunadate kweli au la. Akawa akiulizwa "mkewako mzima?" anawajibu "sina mke mimi" na baada a hapo anawaacha kwenye mataa na kuondoka.


Kitu kingine ambacho kiliniuma sana ni kuwa hata kwenye party za chuo kama za darasa ambazo ni za usiku alikuwa haongozani na mimi, bali na marafiki zake 3 wa kiume na msichana mmoja. Ndani ya party anakaa na hao watu ila mda mwingi anatoka nje na kurudi


Wakati party inaendelea msg zake kwangu haziishi kutumwa kuwa nisijali nivumilie na niact kiutu uzima. Ukicheza mziki na mkaka anakuja kukutoa na kuniambia nijiandae tunarudi nyumbani. Kwa maana hiyo party ndio inaishia hapo.


Siku zilienda mara nyingine alikuwa na mikutano ya kikazi mpaka saa sita za usiku ndio anaweza kuniambia anatoka kikaoni, nilikuwa najiuliza ni kazi gani usiku? Nijuacho mimi ni kuwa anafanya kazi kwenye makampuni 2 ambayo kote kuwili alinipeleka.

Hatimae nikaja kusikia tetesi kwa watu wengi wa darasani kuwa X anafanya kazi ya upelelezi, tena na hivi alikuwa anasafiri sana kwenda nchi tofauti na hamna anayemuaga zaidi ya mimi tu basi mi ndio nikawa nasumbuliwa "vipi mumeo kaenda kufanya upelelezi?" na maswalimengine mengi.

Siku moja nikamuuliza, akaniambia "kazi zangu zote mbili unazijua haya ya upelelezi sijawahi kukuambia na wala siyajui ndio mana nikakwambia watu wambea sana wanaongea mno, wewe nisikilize mimi na si wao".

Kwa kweli haya yote yalinisumbua sana kichwa changu na mara kwa mara niliongea nae ila jibu lake ni kuwa eti nahitaji kumwelewa na tupeleke mahusiano kiutu uzima na si kitoto. Basi kwa vile nilimpenda nikaka kimya.

Ilimradi mapenzi niliyapata, nikiumwa yupo,nikiwa na shida ananisaidia, akiwa less busy naenda kwake na hata nikitaka kulala huko yeye sawa tu, pia yeye alikuwa anakuja kunitembelea nilikokuwa naishi na wakati mwingine analala. Marafiki zangu walimjua na aliwajua vizuri japo alikuwa ananiambia nisiongee nao kila kitu kuhusu mapenzi yetu kwani hataki umbea.


Siku moja nikamuuliza hivi una mpango gani na mimi wa mbeleni? akanijibu "nataka usome hadi masters mana kamwe sitaoa mwanamke asie na masters" na akaniambia kwa yeye ana plan ya kumaliza masters na kuendelea kusoma na ana mpango wa kuoa mwaka 2015 ila kwa sasa nijue tu kuwa sisi ni wapenzi mungu akipenda basi tutafika mbali.


Ila akaniambia ukitaka tuwe wapenzi zaidi inabidi ujifunze kuwa privancy person hiyo ndiyo sheria yangu,ukianza kuongeaongea sana mambo yetu na mengineyo tutaishia hapo.

Kwa saa tupo mbalimbali na huwa nafunga safari kumfuata chuoni na ninakaa nae siku tatu au mbili kisha narudi kazini. Mambo si rahisi kwa huu umbali ila najitahidi kumtembelea na hata mapenzi ya simu yanachukua nafasi kubwa zaidi kama nikiwa nimekosa kisingizio cha kuomba ruhusa kazini, maana kazi nazo si kila mara uombe ruhusa.

Basi mara nyingi mimi ndio nikawa nampigia simu kila siku jioni, inaweza kupita hata siku mbili kama sijapiga basi tena. Siku moja nikamwambia sipendi hiyo tabia kwa nini hapigi simu?akanijibu kuwa huwa anasahau kuweka credit basi nikamwambia "kama hunipendi uniambie kuliko kunipotezea muda".Tukaagana.

Kesho yake yeye akapiga simu ila sikuchangamka kama siku nyingine.Siku iliyofuata usiku akanitext "hujambo umeshindaje?usiku mwema", mimi nikamwendea hewani tukaongea vizuri tu mwisho nikamwambia "i love u",akanijibu "me too".


Nikamuliza "una uhakika?" akanijibu "sina budi ya kurudia kitu kwa miaka yote 3 tuliyokuwa pamoja hujakua tu?kua basi tuwe na mapenzi ya kiutu uzima" na akaniambia "kusema i love u kila siku haimaanishi ndo unapendwa naweza nikakuambia hivyo na bado nisimaanishi. Kwa kweli sikumwelewa, akaniambia mwisho tukagombana bure na yeye hataki hilo litokee bora tulale,basi tukaagana.

Huyu ndie mwanaume ambae ninae dada Dinah kwa miaka 3 sijapata jibu ni mwanaume wa aina gani huyu na kama kweli ananipenda na ana mpango na mimi. TAFADHALI NAOMBA UNISAIDIE KWA USHAURI NIFANYAJE.
Na washiriki wengine nahitaji maoni yenu tafadhali.

Ni mimi dada F"

Dinah anasema: Dada F, shukrani kwa ushirikiano na uvumilivu wako as nachukua muda mrefu kujibu kutokana na uwingi wa majukumu mengine ya kikazi na maisha. Nimefurahishwa na maelezo yako ya kina na kumfanya yeyote kuelewa picha nzima bila kuwa na maswali.....hongera kwa hilo.

Suala la Ushushushu sio muhimu sana as long as wewe unajua kazini kwake, na akitoweka siku zote huwa anakuambia kuwa anasafiri hivyo huitaji kujipa hofu na mimi binafsi sina uzoefu na masuala ya wapelelezi. Nitakupa maelezo kuhusiana na issue ya uhusiano wenu wa kimapenzi ambayo naamini yatafungua macho yako kwa kiasi fulani.

Mimi binafsi ninaamini kuwa sisi wanadamu lazima tupitie hatua sita za maisha ya kimapenzi na mahusinao. Ila tatizo la wengi huwa tunakurupuka na kutaka/kutegemea jambo fulani kabla ya wakati.

-Uzoefu/kutambua ujinsia wako kwanza (hapa unakuwa kwenye umri mdogo so jaribu kufurahia maisha na kupata uzoefu zaidi wa kimaisha na wakti huohuo unazingatia masomo/kazi, sio lazima ungonoke).

Pili:-Unapenda na ku-commit (hapa utakuwa mkubwa kiumri na umetulia kiakili).

Tatu:-Chumbia na Ndoa (kuwa na uhakika wa kuishi na huyo mmoja tu maisha yako yote).

Nne:-Familia(Uamuzi au kukubaliana kuzaa).

Tano:-Kufanya uhusiano wenu wa kimapenzi na ndoa kusimama Imara.

Mf-ninyi wawili bado wadogo, mnapendana sana tu (kutokana na maelezo yako bado mko hatua ya kwanza)...ila wewe unategea au unataka zaidi ya unachokipata kutoka kwenye uhusiano wenu, huenda ungependa siku moja ufunge ndoa na huyo mpenzi X hasa ukizingatia kuwa owte mnafanya kazi na mmeshakuwa pamoja kwa muda mrefu. Lakini yeye hayuko tayari kufanya hivyo kwani anachotaka yeye kwa sasa ni kurekebisha maisha yake na wakati huohuo kuongeza Elimu.

Kitu ambacho sisi wanawake huwa tunakikosea ni kuharakisha mambo, labda kutokana na " msukumo" kutoka kwa jamii inayotuzunguuka kuwa ukiwa kwenye uhusiano baada ya muda fulani basi lazima uolewe au hata kuzaa.

Lakini katika hali halisi tunatakiwa kujua nini hasa wapenzi wetu (wanaume) wanakitaka kutoka kwenye uhusiano husika na je ni hatua gani hivi sasa uhusiano wetu upo? kabla hatujaanza kurukia/harakisha hatua inayofuata kama sio kuziruka zote na kwenda hatua ya mwisho.

Sasa ninachokiona hapa ni wewe kutaka commitment na kuhakikishiwa nafasi yako, wakati yeye bado anajaribu ku-have fun. Kweli anakupenda lakini hiyo hamfanyi yeye kuwa na uhakika kwa 100% kuwa wewe ndio mke wake.......anahitaji muda.

Kwenye suala la wewe kuwa msiri, mimi sioni tatizo kwani naelewa kuwa kuna baadhi ya watu wanaaibu sana yanapokuja masuala yao ya kimapenzi.....yaani hawapendi kujionyesha wa watu wengine kuwa wao ni wapenzi. Sasa kwa vile mpenzi X ni mmoja kati ya hao watu ni vema wewe kuheshimu takwa lake hilo.

Nini cha kufanya: Jiulize nini hasa unataka out of the relationship with X, mawasiliano yenu yako bomba kama wapenzi, unapewa mapenzi yake yote, mnaonana kila mnapohitajiana, anakujali, kila mtu yuko huru kwenda kwa mwenzie, mnaoneana wivu (which ni dalili nzuri) X anaonyesha ameji-commit kwako.......nini kingine unataka?

Kama ni ndoa ndio utakayo ni wazi hutompata kwa sasa kwani yeye anadhania takuwa tayari akiwa na miaka 31 (2015) which wanaume wengi ndio hupenda kujipangia hivyo kuanzia 31-36 wawe wamefunga ndoa, huamini by that time wanakuwa somehow wamekamilisha "mipango" yao kimaisha.

Hivyo hapo kuna maamuzi 3 tofauti;
(1)-Endela na uhusiano huku ukimsubiri tumia muda huo kwenda kufanya hiyo Master yako au

(2)- Endela na uhusiano, furahia maisha yako na chukulia kila siku kama inavyokujia (mkifunga ndoa poa isipotokea ndoa poa).

(3)-Toka kwenye uhusiano ili kupata utakacho kwenye uhusiano mwingine (kama unaharaka sana na maisha ya wawili).

Nakutakia kila la kheri.

Friday, 13 November 2009

Mume ni mwema lakini hataki kazi wala hatoi Unyumba-Ushauri!

"Habari mpenzi,
nimevutiwa sana na blog yako, kwa kweli ina story za kusikitisha na ukweli kuhusu maisha. Mimi ni mwanamke niliyeolewa naona nina matatizo ambayo nimekaa nayo kimya kwa muda mrefu bila kujua nimwombe nani msaada.

Nimejaribu kuongea na Mama yangu mzazi lakini nimepewa ushauri wa kuvumilia, nimejaribu kuongea na Mama mkwe wangu ushauri ni huo huo sasa sijui labda nipate ushauri toka kwa watu wengine sasa.

Story inaanza hivi; tumependana na mume wangu bila kuwa na kasoro, baada ya mwaka wa uchumba tukafunga ndoa Kanisani. Baadaya ya kuoana tu mungu akanijalia ujauzito nikazaa mtoto wa kike mwaka uliofuata, basi ilikuwa ni furaha tu.

Baada ya miaka miwili nikajaliwa mtoto wa pili wa kiume sasa, basi nayo ilikuwa heri. Sikuwahi kugombana na mume wangu wala kukosana kwa aina yoyote, maisha yalikuwa ni matamu haswa kwani ni msikivu kweli kweli. Chochote ukimwambia anafanya hata kupika hata kufua nguo zangu za ndani.....duuuh hadi wengine walikuwa wananiambia nimempa limbwata.


Basi baada ya kuzaa mtoto wa pili nikashangaa mwenzangu hana time na mimi si kwamba halali nyumbani laah anakula na tunalala wote, watoto anaangalia na matumizi yote anatoa lakini penzi kitandani hakuna, basi ikapita miezi kadhaa bahati mbaya kazi yake aliyokuwa anafanya ikaharibika.

Akawa hana kazi lakini hatukukata tamaa ya maisha tulianza kutafuta tukisaidiana maisha na tulikuwa na miradi yetu midogomidogo ilikuwa inatusaidia. Lakini bado pamoja na yeye kushinda nyumbani tu labda akihangaika kuomba kazi huku na huku mimi nikirudi kutoka kazi hana time ya kufanya mapenzi ila kuongea tunaongea vizuri na hatugombani hata siku moja.

Nikapata woga wa kumuuliza mwenzangu kama ana tatizo maana naona jogoo huwa anasimama kama kawa hasa wakati wa asubuhi lakini hajawahi kunitamkia ananitamani au kunitaka kuwa anataka tufanye mapenzi, mhhhh nikaja nikaona hii kweli kali.


Miezi sita ikapita hatujagusana ila tunakaa vizuri sana kula wote, kulala wote na kushare vitu vingine tu kama kutoka out n.k. Sasa limekuja suala la kazi, kila ninapomuombea kazi kwa watu na kuitwa kwa ajili ya mahojiano hapati. Juzijuzi nilimuombea kazi mahali nifanyapo kazi na akaitwa lakini akakataa kwenda akadai yeye hawezi kwenda kufanya kazi mahali ambapo mimi nafanya kazi.

Hapo mhh sikumuelewa nikajaribu kumueleza vizuri kuwa hatutakuwa ofisi moja ila jengo moja hakukubaliana na mimi . Sasa dada dinah, mtu kama huyo unamfanyaje?

Mwaka mzima umekaa ukishikilia familia na ukisali Mungu ampe kazi, ukimvumilia na kumpenda ingawa hakupi unyumba bila sababu maalum, sasa na kazi hataki kufanya anachagua badala ya kufanya yoyote for the sake of the kids, je nifanyeje? tafadhali naomba msaada hapo kama ni wewe ungefanyaje?-Magy"

Dinah anasema: Mpendwa Magy asante sana kwa ushirikiano na uvumilivu as nimechelewa kujibu, lakini natumaini maoni na ushauri wa wasomaji umesaidia wakati unasubiri kutoka kwangu.

Nitakupa maelezo na ushauri katika sehemu mbili, moja kuhusu kutokufanya Mapenzi na pili suala la yeye kugoma kufanya kazi sehemu moja na wewe.

Kwanini hafanyi mapenzi na wewe lakini anasimamisha!!
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mwanume apoteze hamu ya kufanya mapenzi, kumbuka hamu na nguvu ni vitu viwili tofauti tena kwa wanaume kusimamisha pia kuko kwa aina mbili kusimamisha kwa vile wako tayari kungonoka na kusimamisha kwa vile ni sehemu ya ujinsia wao kwa maana kuwa kuna aina mbili za mwanaume kusimamisha:- (1)-kutokana na mawazo ya kingono (2)-kutokana na kuwa stimulated kwa kushikwa au kuguswa na kitu kama vile shuka, chupi, mkono n.k


Mfano ni mwanaume kusimamisha asubuhi, ile haina maana kuwa anataka ngono japokuwa inaweza kufanyika ngono kama akikuona ukopembeni na ukamvutia then akapata mawazo ya kingono on top of msimao ambao ulisababishwa na mzunguuko wa damu wakati kalala......


Hivyo basi yeye kutokufanya ngono na wewe haina maana anamatatizo ya nguvu za kiume. Nadhani tatizo kubwa linaweza kuwa moja kati ya haya :-

Mosi, Hofu ya kuachishwa kazi (katika hali halisi unapewa taarifa mapema kuwa utapunguzwa/fukuzwa kazi), sasa ile hofu ilisababisha msongamano wa mawazo (stress) na hivyo kupoteza hamu ya kungonoka.

Pili, mabadiliko ya mwili wako baada ya kujifungua mtoto wa pili (Chunguza hapa), na jitahidi kurekebisha.....jipende na hakikisha unavutia zaidi, fanya mazoezi ya misuli kuanzia ya ulimi mpaka ya Uke.

Tatu, hapati attention ya kutosha kutoka kwako kama mpenzi labda kwa vile wewe huna muda as una-deal na watoto bila ushirikiano wake kutokana na stress.......(peleka watoto kwa bibi yako au kwa ndugu yeyote mnae muamini) mara moja kila baada ya wiki 2.

Nne, Yeye kuwa muanzilishi wa kutaka/kufanya ngono kitu ambacho huwa kina udhi/kera na kuchosha na hivyo mtu anaamua kutokufanya kabisa......(Kuanzia sasa usisubiri yeye aanze, anzisha wewe). Hii itamfanya ajiamini na kuhisi kuwa anavutia pia anafurahi kuona kuwa mkewe sio Gogo, pia mara moja kwa wiki mfanyie mumeo jambo litakalo mfurahisha, pagawisha na kumridhisha kingono).

Nini chakufanya kwa ujumla: Mumeo anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwako, ushirikiano huo sio wa kumtafutia kazi au kumsukuma atafute kazi (kitu ambacho anakijua wazi yeye kama mwanaume) kwani kwa kufanya hivyo unamfanya apoteze ile hali ya kujiamini kama mwanaume na pia unasumbua Ego yake kwani yeye kama mwanaume kamili najaua kuwa ni wajibu wake kuwa provider kwa familia yake, sasa unapo-take over nakujaribu kumtafutia kazi inaweza kuchangia kumfanya azidi kuhisi kuwa yeye ni useless.

Natambua unafanya hivyo katika harakati za kumpa ushirikiano, kuonyesha uko pale kwa ajili yake na tayari kumsaidia mumeo kwa faida ya watoto wenu, yote haya wewe kama mwanamke ungefurahi kuyapokea kutoka kwa mumeo kama ungepoteza kazi......lakini sio mwanaume. Mwanaume anapewa ushirikiano kivingine.

Huyu mumeo anamengi sana akilini mwake hivyo hakuna nafasi kabisa ya kuweka mawazo ya kingono (kama unawajua wanaume vema utanielewa ninachokisema hapa). Sasa ili kumsaidia arudie hali yake ya kawaida unatakiwa kufanya kazi ya ziada......


Mf: kuongea nae vizuri, kumshauri/kumpa matumaini, kumshirikisha kwenye maamuzi (japokuwa hawezi kuchangia kwa sasa), kuonyesha unampenda na kuvutiwa nae zaidi sasa hana kazi kuliko alivyokuwa na kazi(anzisha ngono, cheza na mwili wake na kuwa mtendaji mkuu), kuonyesha kuwa unaweza kusimama wewe kama mama bila kuonyesha stress au kuzidia (anajua kuwa unazidiwa lakini sio lazima umuonyeshe au kulalamika kwani itamuangamiza kiakili), usionyeshe kukerwa na yeye kutokuwa na kazi, kumpa matumaini kuwa kazi ni kazi tu as long as senti zinaingia n.k.


Kwa kufanya hayo niliyogusia na mengine ambayo baadhi ya wachangiaji wameshauri hakika mumeo atakuwa comfortable na mawazo yanaweza kupungua na hivyo kuanza kupata nafasi ya kufikiria ngono akilini mwake na hata kuanza kuona kuwa unamvutia tena.


Kufanya nae kazi Jongo moja: Ukiachilia mbali matatizo mengine yanayoweza kujitokeza kwa kufanya kazi sehemu moja (unless otherwise Taaluma zenu zinafanana na mnawekeana mipaka vinginevyo sio nzuri/afya kwa uhusiano wenu wa kimapenzi.


Kama nilivyogusia hapo juu, kwa baadhi ya wanaume kusaidiwa na wake zao ktk mtindo wa ku-take over kama ulivyofanya wewe huwapotezea hali ya kujiamini na kuhisi kuwa "wameolewa" achilia mbali mwnaume huyo aende kufanya kazi Jengo moja na mkewe ambae ndio actually kamtafutia hiyo kazi na usikute kazi yenyewe ni ya kiwango kidogo kuliko mkewe........hapo haji mtu!

Uless kuna matatizo mengine kwenye ndoa yenu ambayo hukutaka kuyaweka hapa, lakini tatizo lako sio kubwa kiasi cha kutishia uhai wa ndoa yenu. Hakikisha unafanyia kazi ushuri uliopewa na nina kuhakikishia kila kitu kitakuwa safii na Unyumba utaupata lakini kwa sasa jitahidi ku-initiate ngono kila unapojisikiwa kutaka kufanya hivyo, usisubiri yeye akufuate au akuombe!....ni mumeo huyo hivyo unamfanya atake kufanya kwa kutumia uanamke wako au yeye anakufanya wewe utake kufanya kwa kutumia uanaume wake.

Kama ingekuwa mimi ningefanyaje: Mimi kama Dinah, kwanza kabisa ningekubali mabadiliko na kujaribu kubadili mtindo wa maisha yetu kama familia ili ku-save. Ningeonyesha mapenzi kwa mume wangu kuliko mwanzo, ningehakikisha namuondolea stress kwa kutumia mbinu mbali mabali za kumkanda na kuongea nae bila kulalamika wala kuonyesha kuwa nimezidiwa na majukumu.


Kila wakati ningemfanya aone kuwa niko nae sambamba ktk hardship na sio yake peke yake bali yetu sote. Ningempa support na kumshauri kuhusiana na kazi/biashara (sio lazima kuajiriwa) kwa kumpa mawasiliano au kumuonyesha sites/magazeti lakini sio kwa ku-take over na kuingilia Ego yake.


Ningemshawishi kwa maneno na vitendo kuwa kufanya mapenzi kunasaidia kuondoa au kupunguza stress, nikifanikiwa basi nitahakikisha namfanyia mambo hadimu ambayo najua yanaondoa stress hata kwa masaa mawili (which itamfanya anitake kingono mara kwa mara).

Kwa vile naelewa kuwa kipindi hiki cha hardship kinamfanya mume wangu kushindwa kutumia akili yake kufikiria/taka ngono na kusimamisha, basi ningetumia njia ya kumsisimua kwa kufanyia kazi mwili wake na kuhakikisha akili yake ime-relax kabla sijaanza zoezi zila la kumsisimua kingono.

Nakutakia kila lililojema!

Sunday, 8 November 2009

Sijawahi kushika Mimba, lakini natokwa maziwa-Ushauri

"Hi dada Dinah,
Pole kwa kazi ngumu unayoifanya ya kuelimisha jamii,
Mimi ni msichana wa miaka 26 napenda jua kama kuna sababu zinazoweza
kumfanya mwanamke akatokwa na maziwa kama hana mtoto na wala hajawahi kubeba wala kutoa mimba? na dawa yake ni ipi?
Nitashukuru sana ukinijibu kupitia blog yako
Naitwa F.K"

Dinah anasema: FK, shukrani kwa ushirikiano na asante kwa kunipa pole. Mimi binafsi sina utaalam wa kitibabu hivyo itakuwa ngumu kidogo kukupa jibu la uhakika as tatizo lako ni la kitibabu zaidi.

Kama unatumia aina yeyote ya dawa za kuzuia mimba au uliwahi kutumia inaweza kuwa ni moja ya sababu. Vinginevyo inawezekana ni mambo ya homono. Ila kwa ushauri mzuri wa kitibabu tafadhali, tembelea Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake.

Kila la kheri!

Sunday, 1 November 2009

Mtarajiwa kanikataza kutumia Vizuia damu na Kidole, eti....

"Pole kwa kazi nyingi D!
Mimi leo nina tatizo kama ifuatavyo, mume wangu mtarajiwa amekuwa akilalamika kuhusu vitu vifuatavyo:-
Tampax-Amenikataza kutumia pad za kujiingizia ukeni kwa madai ya kwamba zinatanua uke,
hivyo ilibidi niache na kuanza kutumia pad za kawaida tu.

Dinah anasema:Inasemekana kuwa Matumzi ya Tampax zinahusiana na matizo ukeni kwa wanawake ikiwa zinatumia mara kwa mara, wataalam wanshauri zitumike marachache sio hivyo tu bali pia inasemekana kuwa bidhaa hiyo inasababisha uke kubadili uhalisi wake ila sidhani kama ni upana.

Samahani Mimi binafsi sijwahi kuzitumia bidhaa hizo hivyo kwa vile siamini katika kuingiza vitu ambavyo sio asilia(vitu kama toys, tampax, dawa za kuzuia mimba n.k) hivyo sitoweza kukupa jibu kutokana na uzoefu ila kutokana na hadithi za kweli za baadhi ya watu ninaowafahamu.

Tampax zinatengenezwa kwa kutumia fibers ambazo ndio zinanyonya damu, inasemekana fibers hizo hubaki ukeni na kujikusanya na baada ya miezi/mwaka ukeni na zinaweza kusababisha matatizo ya kiafya na maambukizo ukeni. Tatizo kubwa linalosabishwa na matumizi ya Tampax ni TSS (Toxic Shock Syndrom), hili linaweza kuwa serious na hata kupelekea kifo.


Vidole-Hivi karibuni tulikuwa wote bafuni na akaniona jinsi ninayojisafisha ukeni kwa kujiingiza kidole, akashangaa sana na kuniambia hivyo pia ni vitu ambavyo vinachangia sana kutanua misuli ya uke!!!!!! Hajawahi niona ninavyojisafisha kwani hatuishi pamoja na kutokana na ubusy wa maisha basi huwa tunakutana wikiend kupanga mambo yetu ya ndoa.

Dinah anasema: Nadhani mpenzi wako anahitaji kutembelea blog hii, ili ajifunze mambo kuhusu wanawake na maumbile yao. Kuna vitu vinavyoweza kusababisha K kuwa pana na vyo ni:

Mosi, Utoko ukiachwa ukeni ndio inasemekana (kwa mujibu wa Dr wangu) kuwa unasababisha uke kupanuka. Inasemekana wanawake wengi wa kiafrika wana K zilizokaza kwa vile wanautamaduni wa kuondoa utoko kila siku tofauti na wale wa magharibi ambao wana K pana/kubwa.

Vilevile mwanamke ukianza ngono katika umri mdogo wakati mwili wako bado unakua/badilika basi harakati za ukuaji hu-ignore K yako ambayo kwa wakati huo itakuwa pana nahivyo utakapo kuwa mtu mzima utakuwa na K kubwa na ukadhani kuwa ulizaliwa hivyo lakini ukweli ni kuwa hakuna mtu anazaliwa tayari kapanuka K, hii ni ya pili.

Je Dinah ni kweli kujiingizia vidole kunaweza kuwa kunatanua misuli ya uke?
nimekuwa nikifanya hivyo tangu nimekuwa binti na bila ya kufanya hivyo najiona kama sijakamilika vile.

Naomba ushauri wako pamoja na wadau wengine wote ambao watapenda kuchangia chochote..
Love, Fatner!"
Dinah anasema:Niambie Fatner, asante na nimekwisha poa aisee. Sasa rafiki nimeamua kukujibu hapo juu kutokana na kila point uliyogusia. Pole kwa kuhisi kuwa baadhi ya wasomaji wanakushambulia. Kama wangekushambulia hakika mimi ningewaambia wasifanye hivyo na hata kuhariri comment zao.

Ukweli ni kuwa hawajaku-attack bali wameshangazwa na hali ya kujiamini kwako na uhuru mbele ya mpenzi wako which ni kitu kizuri ila kama kimepitiliza kidogo hihihihihihi....skia mimi ni mmoja kati ya wanawake wachache wanaojiamini, niko huru na muwazi kama unavyoona ninavyofanya kazi yangu hapa lakini tangu nimekuwa mtu mzima na kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi sijawahi kuruhusu Mpenzi mume wa mimi aone ninavyojiswafi uke wangu wala ninavyobadili kizuia damu (Pad).

Hata kama tunaoga wote, siku zote nitakuwa wa mwisho kumaliza kwani mimi kama mwanamke nachukua muda kidogo bafuni ili kujinafasi na kujisafisha vilivyo bila haraka.

Ni matumaini yangu basi utakuwa umechukua maelezo ya wachangiaji wengine in possitive way.
Asante kwa ushirikiano na tafadhali mtumie link ya jinsi ya kujiswafi uke mpenzi wako ili apate Elimu ya uanamke ambayo itamsaidia kufurahi tendo even more.

Kila la kheri.