Friday, 25 September 2009

Kwenda mwendo mrefu ni kaiwada?-Niwekeni sawa!


"Hallow sister dinah. Mimi ninauliza kwamba, kwa mwanaume anaeweza kufanya ngono kwa muda wa dk45 mpaka saa moja ndio amwage na hilo likitokea basi hawezi tena kurudia tendo la ndoa kwa muda huo. Je huyu tumuweke katika kundi gani? hii ni sawa, kawaida au anamatatizo?
FIGO WA ARUSHA"
Dinah anasema: Figo asante kwa uvumilivu wako, nilijaribu kuzuia mail yako kutokana na Mfungo mtukufu. Hongera sana kwa kuwa na uwezo wa kwenda mwendo mrefu ni hali ya kawaida kabisa japokuwa sio wanaume wote waliojaaliwa hivyo.....mshukuru Mungu.
Kwa kawaida mwanamke akiandaliwa vema na kuingiliwa ukeni anafika kileleni baada ya dakika 20-30 sasa kama wewe unaondoka dk 45 mpaka saa moja ni wazi kuwa mpenzi wako atakuwa more than happy hasa kama na yeye kajaaliwa au anaujua vema mwili wake na namna ya kujituma na kuita Kilele (anaweza akaenda kileleni zaidi ya mara mbili).....kumbuka hapa sizungumzii kilele via Kisimi bali maeneo mengine ndani ya uke.
Furahia maisha yako ya Kingono na ongeza ubunifu zaidi ktk kumshika na kumbusu wakati unaendelea na mwenzo wako ili kumfanya mpenzi asiwe bored au kuchoka kama sio kuwa mkavu ukeni hii itampa raha zaidi na zaidi.
Hongera sana!

Wednesday, 23 September 2009

Kuiba kumekwisha na mood imekwisha-Ushauri!


"My dear I so love your blog, I'm pretty new to it lakini dah! umenikosha na umewezesha mambo ndani kuwa mazuri zaidi. Ninatatizo moja of late na nadhani kupitia blog yako waweza nijibu.

"Mimi na mpenzi wangu we've been together for 10 months, tulianza kwa kuiba kwani wote tulikua tunawapenzi tofauti na mambo ya kuiba yakatushinda tukaona tuwe pamoja. Sasa sijui sababu tulianza na moto sana (or that's just what I want to believe).


Of late, yeye akitaka mimi nakua sijisikii kabisa au wakati mwingine nataka lakini I wouldnt feel like getting it on with him, hili tatizo lanikosesha raha kabisa na najua yeye anakosa raha pia but ni mpole na mnyenyekevu kweli ataniuliza kuna tatizo gani but I'll just say am not in the mood.


Please help me dinah, I trully am crazy about this guy na sipo tayari kumpoteza but I cant fake it with him sasa nifanyeje? Hope to hear from you soon.

Sandy"
Dinah anasema: Shukrani kwa kuipenda Dinahicious. Zile hisia, shauku, hamu zinazoupata mwili wako bila wewe kuweka any effort mara tu baada ya kukutana na Mpenzi mpya huisha ndani ya mwaka mmoja mpaka miwili.
Baada ya hapo wewe na yeye kwa kushirikiana mnatakiwa kuweka an effort ili kuendelea kupata msisimko ule ule au zaidi kila mara mnapokutana, mnapokuwa pamoja na zaidi na muhimu ni kila mnapofanya mapenzi.
Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa kuna vitu ambavyo vinasababisha wewe kujisikia hivyo. Inawezekana kabisa mtindo wenu wa kimaisha vilevile kunauwezekano kuwa mpenzi huwa anafanya vitu ambavyo havikusisimui au vinafanywa kimakosa kama sio ulivyozoea kufanyiwa awali..........hali inayoweza pelekea wewe kuishiwa hamu au kuwa na hamu lakini hujisikii kufanya nae huyo mpenzi wako.
Hii haina maana kuwa huna mapenzi nae, inaonyesha unampenda kutokana na ubora mwingine ambao Mungu amemjaalia na kama ulivyosema mwenyewe usingependa kumpoteza. Kwa maana hiyo basi ni vema wewe kama mwanamke na mwenye kumhitaji huyo mpenzi wako huna budi kuwajibika ktk hilo ili kuokoa uhusiano wenu.
Nini cha kufanya kwa kuanzia: Mosi, Fanya uchunguzi kwenye maisha yako ya kingono na mpenzi wako huyo. Mf; (1)-Nini ulikuwa ukimfanyia mpenzi wako miezi 3 ya mwanzo mlipokutana?
(2)-Nani alikuwa kiongozi kwenye ngono?
(3)-Nani alikuwa muwazi wa nini anakitaka kingono?
(4)-Mlikuwa mnajadiliana au kuambiana mahitaji yenu kingono ktk mtindo gani?
(5)-Nani ana uwezo mkubwa/mdogo? nakadhalika.....
Pili,Fanya uchunguzi wa namna mnavyoendesha maisha Mf; (1)-Kama wote mnafanya kazi ni nani anafanya masaa mengi au siku nyingi zaidi?
(2)-Nani mfanya maamuzi makuu? N.k
Tatu, Chunguza mzunguuko wako wa kingono ambao unakwenda sambamba kabisa na ule mzunguuko wa Hedhi.
Fanyia kazi hayo kisha njoo uniambie umegundua nini? Hiyo itanisaidia mimi kukupa maelezo ya nini cha kufanya kila siku za maisha yako kwenye uhusiano wako wa kimapenzi ili uwe bora na wenye afya.
Nasubiri majibu.......

Monday, 21 September 2009

Je anaweza kumsamehe Ba'Mkuu?-Ushauri.

"Dada Dinah mie nakuja tofauti kidogo. Nimekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Kijana mmoja kwa mwaka na nusu sasa. Nampenda na pia nadhani yeye ananipenda kwani huwa ananifanyia yote ambayo mimi nahisi ni kwaajili ya mapenzi yake kwangu.


Kipindi cha mwaka tumeishi pamoja baada ya yeye kuja na idea ya kusave ili tufunge ndoa mwakani, maana yake huku tunakosihi maisha ni ghali sana. Kwa vile ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuishi na mwanaume nyumba moja nikamuomba mpenzi ahamie kwangu badala ya mimi kuhamia kwake na akakubali.


Nilifanya hivyo kwa vile nilikuwa naogopa kunyanyaswa kama uhusiano wetu hautofika mbali. Namshukuru Mungu tangu tumeanza kukaa pamoja maisha yamekuwa mazuri ukiachilia migongano ya hapa na pale na kupishana kwenye baadhi ya mambo. Tumefanikiwa kusave kiasi cha kutosha kwa ajili ya kufunga ndoa kuanza maisha kama mke na mume.

Kitu cha kushangaza Mpenzi wangu hajawahi kuzungumzia wanafamilia yake, mwanzoni nilidharau tu kwa vile sikutaka kumkorofisha japokuwa kuna donge linanikaa rohoni nikitaka kujua kwanini hazungumzii familia yake wala kunitambulisha kwao kwa simu!

Huwa nafikiria vitu vingi sana juu ya mpenzi wangu huyu lakini kwa vile nampenda huwa najipa moyo maisha yetu ya ndoa ni kati yangu mimi na yeye na sio watu wengine. Siku moja nikaamua kukaa nae chini na kuuliza kama utani tu.

Mpenzi wangu alicheka alafu akaniambia, alikuwa anasubiri mpaka baada ya kufunga ndoa ndio aniambie ukweli kuhusu maisha yake lakini kwa vile nimeuliza basi atasema na lolote nitakaloamua basi ataliheshimu. Akaendelea kuwa yeye hana ndugu wala wazazi na alilelewa na baba yake mkubwa ambae alimtesa sana.

Nilimuonea huruma sana na nikatamani kumkatisha lakini pia nilitaka kujua mwisho wa story yake. Mpenzi wangu ilimbidi atoroke pale nyumbani na kudandia treni kwenda kijijini ambako kulikuwa na bibi na babu yake, alipelekwa shule na kufanikiwa kufaulu na kuendelea na Sekondari lakini baada ya tu ya kumaliza kidato cha nne Babu akafariki Dunia.

Maisha yalikuwa magumu kwani bibi hakuwa akifanya kazi na wala hakupokea msaada kutoka kwa baba mkubwa. Akaamua kuacha shule na kuanza kufanya kazi ya kulimia watu mashamba ili aweze kupata hela ya kula yeye na bibi.

Baada ya miaka michache kupita bibi nae akafariki na yeye akabaki mkiwa, hivyo akaamua kurudi Dar ili kutafuta kazi na kwa bahati nzuri alipata kazi kwenye Ubarozi fulani kama mlinzi. Akajiandikisha Chuo cha ufundi lakini masomo ya jioni na kujilipia mwenyewe. Alifanikiwa kumaliza na kufaulu, akiwa na kiu ya kwenda Chuo Kikuu aliomba Udhamini kutoka kazini kwake kwani gharama za masomo zilikuwa juu sana.

Boss wake baada ya kusikia historia ya maisha yake na kugundua kuwa hana ndugu akamdhamini akasome nje ambako ndio tumekutana. Baada ya kuniambia yote hayo nilijisikia vibaya na kujuta kwanini niliuliza, nilimuonea huruma mwanaume mzima kutoa machozi.

Nilipomuuliza kwanini hakuwa wazi tangu mwanzo? akasema hakutaka niwe nae kwa kumuonea huruma kutokana na maisha yake ya zamani bali niishi nae kwa vile nampenda.

Je! Ni sawa kama nitamshauri mpenzi wangu amsamehe baba yake mkubwa na kurudisha uhusiano?"

Dinah anasema: Nimepitia ushauri na maelezo ya wachangiaji na wamegusia vitu muhimu ambavyo natumaini umevifanyia kazi. Nakubaliana na imani yake kuwa hakutaka umuoenee huruma kutokana na hadithi ya maisha yake ya zamani ambayo inauzunisha na alitaka umpende.

Kuna watu wanajenga mahusiano na hata kufunga ndoa na kuendelea kubaki kwenye ndoa kwa vile wanawaonea huruma na sio kuwa wanawapenda. Nikirudi kwa past yake nadhani naungana na wote waliosema chunguza ili kujua ukweli na kama kuna ndugu (watoto wa baba Mkubwa'ke) basi unaweza k uanza kuzungumza nao bila kuwajulisha wewe ni nani (unaweza kujifanya ulisoma nae n.k) ili kujua ukweli wa mambo.

Kama asemayo ni kweli basi heshimu uamuzi wake wa kujiweka mbali na Mzee huyo (kama bado yupo hai) lakini jitahidi kutafuta namna ya yeye kurudisha uhusiano na watoto wa mzee huyo aliyemnyanyasa ili kuepusha watoto wao na wenu kuja kutengeneza mahusiano ya kimapenzi n.k si unajua Dunia ni ndogo hii.

Mimi binafsi sina uzoefu sana na matatizo ya kifamilia lakini nashukuru wasomaji wamekushauri vema kabisa.

Kila la kheri!

Sunday, 20 September 2009

Wapenzi 2 waniweka njia panda-Ushauri

"Pole kwa kazi kubwa unayoifanya na kutusaidia sisi wanawake, mimi ni msomaji wako mzuri na bila ya kupoteza muda. Nilipata ujumbe kuwa rafiki yangu amelazwa na nilipopata nafasi jioni nilipitia kumjulia hali.Nilikuta rafiki amekonda mpaka nikaogopa kwa kweli nilipomuuliza nini zaidi akasema vidonda vya tumbo! Kisa? manake inaonekana una mawazo sana, akaanza kunieleza ukweli sasa kwani siku zote nilikuwa sijui maisha yake ya kimapenzi ( anao wapenzi 2) wala hatukuwa karibu na kupata muda wa kuyaongelea mambo hayo.Katika maisha yake baada ya kutendwa na aliyekuwa bf wake wa kwanza, alidondokea kwenye penzi ambalo hakutarajia, huyo tumuite (P) alikutana naye kazini kwake. Huyu P yeye sio Raia wa Tz na walikuwa wakiishi pamoja.

Wakati huo rafiki yangu alikuwa akifanya kazi ya kawaida tu kwani elimu yake ni ya chini ( kwa sasa hafanyi kazi kwani alipata matatizo ya kiafya yaliyopelekea Operation na alipopona nafasi yake ikiwa haipo tena)

Huyo P alikuwa anajua siku moja atarudi zake kwao na kumuacha yeye aendelee na maisha yake, hivyo alikuwa tayari kwa hilo. P hakuwahi kumshirikisha ktk mambo yake yoyote yale yanayohusu maisha yake.

Rafiki yangu alijitahidi sana kumuhudumia P kama mpenzi wake, lakini alikuwa anajibiwa kuwa yeye P kaja Tz kikazi tu na si kutafuta mke. Mwaka wa 2 ndani ya maisha yao pamoja akakutana na kijana mtanashati wakiwa wanafahamiana tangu utotoni.

Family zao zinafahamiana huyu sasa tumuite (K) wakabadilishana namba za simu, wakawa wanawasiliana kama kawaida hadi siku moja K alipomualika rafiki yangu kwa ajili ya dinner nje, ktk maongezi K akaonyesha amempenda rafiki yangu kimapenzi.

Lakini rafiki yangu akawa muwazi kwa K kuanzia maisha yake na mahusiano ya mtu aliyekuwanaye ambae ni P, alikuwa akifanya kazi nje ya Dar kwa miezi 3 ndio anarudi Dar na likizo anakaa wiki 1 Tz then wiki 3 kwao kwani likizo yake ilikuwa ni mwezi kila baada ya miezi 3.

K akakubaliana na kuanzisha mahusiano japo rafiki yangu ana mtu mwingine, lakini kwa kuwa P alikuwa haeleweki kwani wakati wowote anaweza kuondoka na kwenda kwao, kama ujuavyo kazi za mikataba za watu hawa.

Ingawaje mambo ya kula, kuvaa pamoja na kodi na nyumba havikuwa na tatizo kwake tatizo lilikuwa kwenye sex, rafiki yangu alikuwa hafurahii hasa pale anapomwambia P style hii naumia au vyovyote vile ambazo hafurahii. P alikuwa hamsikilizi badala yake atamwmbia shhhhhhhhhhhhhhhhh! shut up, too much complaint from you!

Hali hii ikawa inamnyima raha sana rafiki yangu, kwani pamoja na kujaribu kuwa anamuelewesha lakini P alimchukulia rafiki yangu kama mtu asiyejua kitu akawa anampuuza tu. Sasa alipokutana na K mambo yakawa tofauti akawa anafurahia sex kwa kuwa K alikuwa anamsiliza na kumjali zaidi pale anapohitaji kusikilizwa.

Mpaka sasa wana miaka 5 na P kwenye uhusiano na wakati huohuo anamiaka 3 na K ambae kwa sasa yuko nje akimalizia masomo yake). TATIZO LINALOMKOSESHA RAHA Rafiki yangu ni hili:- P muda wake wa kuondoka umefika lakini ktk hali isiyotarajiwa amumwambia waende wote wakaishi huko kwao, kitu ambacho hakukitegemea hata siku moja kitatokea.

Yeye kwa sasa anampenda sana K na anafurahia sana wanapokuwa pamoja kuliko P, lakini K aliwahi kumcheat na rafiki yangu alipogundua aliumia sana na akaamua aachane na K kwa shingo upande.

Baada ya wiki 2 K alimfuata na kumuomba msamahama na kuahidi atorudia tena kitu ambacho kwa uchunguzi wake aligundua kuwa ni kweli ameshaachana na yule msichana kabisa, lakini anahofia K kutokana na umri wake kuwa sawa na yeye yaani 28yrs.

Je hatomsumbua tena huko mbeleni? kwa kuwa na wasichana wengine? kwa ufupi rafiki yangu hajui pa kushika, aondoke na P ingawa hana mapezi naye akaanze maisha mapya ya kujilazimisha mbele kwa mbele au abaki Tz afanye mpango wa kwenda kusoma ili aungane na K?


Kama mimi nilivyosaidiwa na wewe Dinah pamoja na wadau wengine kwa mawazo yenu basi na imani hata yeye utamsaidia pia. Pole kwa maelezo marefu D!
Gina"

Dinah anasema:Gina shukrani kwa mail yako nakwa uvumilivu pia. Mwanzo nilishindwa kujizuia kuhisi jamaa P alikuwa akimnyanyasa rafiki kwenye uhusianoo huo, lakini baada ya kugundua kuwa huyo Rafiki sasa ana miaka 28 ni wazi alianza uhusiano na P akiwa na umri wa miaka 22 (ndio kwanza kamaliza ukuaji) na kuunganisha uhusiano wa pili na K akiwa na miaka 25 (amekuwa mwanamke).

Nitakujibu ktk mtindo tofauti kidogo kwa kufuatia vipengele nilivyovipata ambavyo naamini vitasaidia mhusika kufanya uamuzi wa busara.

(1)Matarajio makubwa-Nina wasiwasi Rafiki alikuwa akitaka kuolewa na kwenda kuishi nje ya Tz (ndoto ya wadada wengi sana wa Kiboongo) lakini P wakati huo hakuwa na mpango huo kama ilivyo kwa vijana wengi wenye kiu na maisha, yaani wanaweka nguvu, akili na mawazo yao yote kwenye kusaka hela na sio kutulia na mwanamke kama mwanamke. P alisema "nimekuja kikazi na sio kutafuta mke" hili ni jibu ambalo limekosa swali, yaani Mpaka P kusema hivyo inamaana kulikuwa na ombi/swali kuhusu commitment.

(2)Ukosefu wa mawasiliano-Rafiki na P hawakuwa na uhusiano wenye mawasiliano mazuri au niseme uhusiano wao ulikosa ngunzo muhimu kati ya zile tano iitwayo mawasiliano. Huenda wote walikuwa hawajui kutokana na umri wao mdogo au kutokutilia maanani.

Kutokuelewana-Kuna uwezekano mkubwa P alipokuwa akiambiwa "unaniumiza" wakati wa tendo alidhani rafiki anataka kumkwepa kingono, kwanini nasema hivyo basi? unapotambua mtindo au mkao fulani unakufanya ujisikie uncomfy mara zote wewe mwanamke una-take over na kumpa mpenzio mkao/mtindo unaojua kuwa utawafurahisha wote wawili bila maumivu yeyote......jamani mikao na mitindo iko zaidi ya 200, sio lazima ufanye yote lakinic hagua ile unayodhani inakupa utamu bila discomfort kwa pande zote mbili.

Mwili kuwa tayari-Wakati mwanamke anamaliza safari ya mabadiliko ya mwili wake, kuutambua mwili wake na kujua wapi panasababisha raha bin utamu kwake as an individual sio rahisi. Mwanamke anaaza kufurahia nakujua utamu wa ngono ndani na baada ya miaka 23.

P hakumpa nafasi ya kukua na kutambua mwili kama mwanamke lakini ni wazi kuwa walikuwa wanapendana na ndio maana rafiki mapaka leo hii wana miaka mitano pamoja, kitu kinachoashiria ukuaji kwa pande zote mbili.

Rafiki ameanza kufurahia tendo kwa vile sasa amekuwa MWANAMKE japokuwa Kisaikolojia anadhani kuwa K ndio anaempa au kusababisha raha hiyo. Kwa bahati mbaya rafiki alikuwa ameamini na kukubali (Kisaikolojia) kuwa P hamjali na akifanyacho ni kumuumiza, lakini akiondokana na hilo atafurahia wakati wake na P.

Alikata tamaa-Inawezekana, Baada ya kugundua kuwa P hana mpango wa kufunga ndoa kwa vile labda hakuwa tayari kipindi kile wanakutana, Rafiki akawa nae kama "spare tairi" kutokana na masuala ya kiuchumi.

Ubinafsi-Rafiki yako sio mwaminifu na amefanya kosa kubwa kwa P. Alipogundua kua P ham-treat vile atakavyo au hakumpa alichokifuata ni vema kuachana nae na kumpa nafasi ya kukutana na watu wengine kuliko kumcheat kwa miaka 3.

P kuwa tayari-Miaka mitano inatosha kabisa kwa kijana yeyote kuwa tayari kufanya uamuzi wa kutulia na mwanamke mmoja. P anadhani kuwa mpenzi wake ni mwema, mvumilivu na sio push kwani alipogoma "kuoa" inawezekana baada ya "nimekuja kikazi na sio kutafuta mke" ni wazi kuwa rafiki alionyesha kukubali na kuridhika na ndio maana akaendelea kuwa nae. Baada ya kumaliza muda wa kuishi nchini huenda amegundua kuwa hawezi kuendesha maisha huko kwao bila mpenzi wake ambae ni wazi anampenda.

K -Alikuwa na wewe kwa vile ni muoga wa majukumu kwani licha ya kujua kuwa rafiki anauhusiano na P bado alikubali kuanzisha uhusiano, sio hivyo tu bali pia amemtenda rafiki. Mwanaume anaekubali kuiba mpenzi wa mwenzake huku akijua, ni dalili ya kwanza kuwa hafai......

Rafiki-Rudisha imani na mapenzi yako yote uliyoyagawa sehemu 2 kwa P, jifunze nguzo zote muhimu za kuimarisha uhusiano (zinapatikana hapa) na mambo mengine mengi. Ikiwezekana kuwa karibu sana na wataalam ili kupata msada ktk maisha yako ya kimapenzi na ngono.

Wapi pa kushika-Nenada na P kwa sababu kuu mbili na nitayaelezea kwa kifupi lakini uwazi na ktk hali halisi.

(1)-Jamaa anakupenda ila tatizo lilikuwa umri na kutokujua nini hasa maana ya kuwa na mtu kwenye uhusiano wa kimapenzi. Jamaa ameonyesha kuwa anajua wajibu wake kama mwanaume kwani kila akienda huko alikokuwa akienda kikazi anarudi kwako, alionyesha kuwa anakujali kwa kukurekebishia na kukutimizia vitu basic lakini muhimu ambavyo wengi hukimbia.

Hakuna mtu aliyekamilika hivyo usikute yeye P mapungufu yake yamelalia kwenye ufanyaji wa tendo la ngono which unaweza kurekebishika ikiwa wote wawili mtashirikisha wataalam na kushare na watu wengine wenye uzoefu.

(2)-Kuondoka na P itakusaidia wewe kusafisha macho kama utatumia akili pia kama unamalendo. P ni mtu unafahamiana nae na mmekuwa pamoja kwa miaka 5 kama wapenzi hivyo unamjua vema huenda hata familia yake unaifahamu hivyo mtu asije kukutisha kuwa jamaa atakuua ukifika huko kwao (si unajua wabongo na roho zao mbaya). Kama unahofu hiyo jiunge na social networking yeyote na tafuta marafiki wa kitanzania waishiao huko incase of anything utajuwa wapi pa kujihifadhi.

Kata mawasiliano na K, teketeza kila kilicho chake kuanzia sura yake akilini mwako mpaka mawasiliano (namba za simu na email add) zake kwani huyu anaweza kuharibu hapo baadae.

Nakutakia kila la kheri.

Thursday, 10 September 2009

Natokwa na Usaha-Ushauri

"Hello dada Dinah.
Mie ni kijana wa miaka 28. Nina tatizo moja ambalo nashindwa kujua chanzo chake ni nini.
Natokwa na maji maji yanayooneka kama usaha kwenye uume wangu.Hii imenitokea kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.


Nafikiri labda chanzo chake ni punyeto niliyokua napiga kila siku, mke wangu,tokea amepata mimba alikua na heavy morning sickness kwa hiyo sikutaka kumsumbua na tendo la ndoa. Sasa ikawa kila siku napiga punyeto.


Mwezi uliopita nikaanza kutokwa usaha, uume ukawa unauma na sometimes nikikojoa nasikia uchungu. Nikaenda hospitalini wakanipa dawa. Nikatumia dawa lakini sikupata nafuu nikarudi tena yaani ni mara tatu lakini bado usaha unatoka ila maumivi yameisha.


Hii siyo sexual disease,maana sikufanya mapenzi, ni hali imenitokea ghafla. Hospitalini walisema njia ya mkojo ina tatizo wakasema ninywe maji mengi ili niweze kukojoa kwa wingi, nimefanya hivyo lakini sioni dalidali za kupona.
Naomba ushauri wenu.

Raymond,UK."

Dinah anasema:Nafikiri tatizo lako Raymond ni la kitibabu zaidi. Magonjwa ya ngono sio lazima yapatikane kwa kufanya ngono ovyo bali unaweza kupata maambukuzo kutoka kwa mkeo, maambukizo ambayo husababishwa na uchafu au kutokuijali sehemu hiyo vema vilevile matumizi ya vifaa ya kuzuia damu ya hedhi (Tampax etc).

Vilevile kuna maambukizo ya magonjwa ya ya Zinaa amabyo hudumu mwilini kwa muda mrefu na huwa hayana dalili na unapoanza kuona matokea kama usaha au maumivu ujue tatizo limekuwa kubwa.

Kwa vile uko Uingereza naamini kabisa ulikwenda kwa GP na sio Daktari bingwa wa magonjwa ya Kiume ambae utamuona ikiwa huyo GP ataku-refer kwake. Hivyo fanya hima na kumuomba GP afanye hivyo ili ukatibu hilo tatizo.

Mimi kama Dinah sitoweza kukupa jibu la uhakika as sio Mtibabu. Pole sana kwa tatizo lako na kila la kheri huko kwa Daktari.

Saturday, 5 September 2009

Mume to be anuna kwa vitu vidogox2-Ushauri

"MAMBO VIPI JAMANI?
MIE NI MDADA WA MIAKA 29, NATARAJIA KUFUNGA NDOA HIVI KARIBU MUNGU AKITUJALIA TUNA MUDA WA MIAKA 6 SASA NA TUNAISHI PAMOJA KWASASA YAANI DADA TATIZO NILILO NALO NI HUYU MWANAUME ANAPENDA KUNUNA KWA VITU VIDOGO YAANI UKIKOSEA KITU KIDOGO ANANUNA NA ANAWEZA KUONGEA MANENO YA KASHFA MPAKA NAOGOPA YANI MIMI HATA SIJUI NIFANYAJE JAMANI ANAWIVU SANA YANI NIKIPIGIWA SIMU AU KUTUMIWA MSG KOSA UNAKUTA KANUNA MARA HANIAMINI YAANI MPAKA NAKEREKA YANI NI VILE BASI TU EMBU NISHAURI DADA NIMFANYAJE HUYU MTU JAMANI MAANA ANANIKWAZA MPAKA BASI."

Dinah anasema: Mambo poua tu mdada, hujambo? samahani kwa kuchelewa kujibu. Binaadamu tumeumbwa tofauti hali kadhalika ninyi wawili ni tofauti sana kitabia, kimalezi hata matakwa yenu ni tofauti natumaini hilo unalifahamu.


Huyu mchumba wako inawezekana hajiamini hali inayopelekea yeye kushindwa kukuamini wewe hasa unapopokea sms au hata kupigiwa siku, mara nyingi mtu mwenye au alikuwa na tabia chafu kupitia simu au hata Internet huwa anakereka "Kisaikolojia" (kwa vile anajua ndio zake au zilikuwa zake yaani anauzoefu fulani hivi ) na kuumia balada ya kuuliza kwa upole na upendo "ni nani huyo ulikuwa unaongea nae" au "nani amekutumia ujumbe.


Mmekuwa pamoja miaka 6, mnapendana na mnakwenda kufunga ndoa ili kuishi pamoja maisha yenu yote hivyo basi ni vema kuanza kurekebishana sasa. Natambua kila mmoja wenu anavijikasoro ambavyo havirekebishiki so u live with them na viji-habit vyake ambavyo vinarekebishika ikiwa mhusika atakubali kuwa anavyo na vinamkera mpenzi wake.

Nini cha kufanya:
Ni ngumu sana kuwakilisha issue hiyo kwake (Kwa wanaume wengi lawama zote anabeba mwanamke) hivyo unapaswa kutumia UANAMKE wako kuandaa namna/mazingira ya kuwakilisha issue, unaweza kutumia mapenzi ya hisia na mwili, unaweza kumromantisha (kumfanyia kitu romantic), unaweza kubadili mwenendo kwamba kila unapopokea sms unasoma kisha unamuonyesha au unaifugua karibu yake ili aione, na kama ni simu basi hakikisha unamhusisha.....MF-unaulizwa simuni, "unafanya nini" unaweza kusema nipo tu hapa na Mchumba/mwenzangu/mume wangu tunapumzika. N.k

Vilevile kama unajua kuna vitu vidogo vidogo vinamuudhi na vitu hivyo wewe ndio unaevisababisha basi unapaswa "kupumzika" yaania cha kuvifanya. Baada ya muda (wiki nne mpaka miezi 2) unaweza kuwakilisha tatizo lako kwake kwa upole na upendo, hapo hatoweza kukurushia lawama zozote kwa vile tayari ulimhusisha kwenye txts msg na simu unazopokea na ukaacha vile vitu vidogo vidogo vinavyomfanya anune.


Kule kwetu tunapofunzwa huwa tunaambiwa kuwa mwanamke ndio pekee mwenye uwezo wa kubomoa au kujenga nyumba yako (not exactly ila wanatumia hii ili wewe mwanamke ujue nafasi yako na kuwa mwangalifu kwenye uhusiano ili kupunguza matatizo), Pia kumbuka maisha ya kimahusiano na ndoa sio lelemama, yanahitaji kufanyiwa kazi kila siku.


Bibi yangu aliwahi kusema kuwa "kukitokea tatizo ndani ya ndoa jiangalie wewe kwanza na jirekebishe kabla hujaomba mwenzio ajirekebishe"RIP........alitumia kuomba rather than kumtaka mwenzio ajirekebishe.

Usitegemee mabadiliko ndani ya siku au wiki moja bali muda zaidi kwa kuwasiliana, kushirikiana, kukumbushana na kuongozana.

Kila la kheri ktk kuweka sawa hili na kwenye kufunga ndoa.

Thursday, 3 September 2009

Nahisi naibiwa-Ushauri

"Nafikiri upo salama na unaendelea vizuri na shughuli zako.
Mimi ni mvulana 24, nina girlfriend ambaye tumeanza mahusiano yetu tangu tukiwa form One katika shule moja huko Kibaha mwaka 2002.

Tumeanza mahusiano ya kimwili tukiwa kidato cha tatu mwaka 04 kipindi hicho mwenzangu akiwa na miaka 16, nami nikiwa na miaka 19, nilifurahi sana siku hiyo kwani nilikuwa nakata utepe wa mpenzi wangu .

Tangu hapo ilikuwa kila baada ya mwezi tunakula goodtym mpaka tulivyomaliza kidato cha 4. Matokeo yalipotoka mimi nilichaguliwa kuendelea na kidato cha 5 ktk shule ya Azania mwenzangu hakupata nafasi na pia familiya yake haikuwa na uwezo wa kumsomesha zaidi.

Huku tulipunguza mambo flani kwakuwa elimu ilikuwa ngumu ukilinganisha na ile ya O-level, lakini tulikuwa tunawasiliana kama kawaida na mambo flani ya kizidi tulijiburudisha. Baada ya kumaliza kidato cha sita 6 mwaka 08 nilipata nafasi ya kuendelea na Elimu ya juu katika chuo cha Uhasibu Tanzania Institutes of Accountancy (TIA) tawi la mbeya.

Tangu nijiunge na chuo kila nikikutana kimwili na mwenzangu naona tofauti na nilivyozoea awali kwani sasa ukipiga goli moja tu mambo yanabadilika uke wake unakuwa na maji na mda mwengine naona kama size imeongezeka.

Sielewi kabisa dada inakuaje, najiuliza au ameshaanza kugawa mali yangu?. Nikimuuliza anasema kwamba hiyo ni kawaida kwa msichana kuna kipindi huwa inatokea hivyo, nashindwa kuelewa ukizingatia sijawahi kuingiliana na msichana mwingine zaidi yake nami ndiye niliye fungua mlango wake.

Naomba unisaidie dada angu kwani naogopa asije kuniuwa na Magonjwa. Sasa nafikiria kuachana naye lakini nashindwa ukizingatia nimemzoea, nimvumilivu na tumefanya mambo mengi ya hatari ila kwa hili nashindwa kuvumilia na roho inaniuma sana, huwa najiuliza kwanini size iongezeke wakati mi ndo mfunguzi wa uke wake?.

Naomba unisaidie kwa hili dada Dinah ili nijue ukweli wa mambo ili nifanye uamuzi sahihi.Ahsante!!
HO"

Dinah anasema:Mie niko salama kabisa hapa "naholideika" tu kimtido sehemu sehemu. Asante kwa mail yako na kunivumilia pia as nilikuwa "nabizika". Sasa wewe HO rafiki yangu ulianza uhusiano wa kingono yeye akiwa na miaka 16, ni mtoto na mwili wake ulikuwa bado unajengeka.

Wakati mwili wake unaendelea na mabadiliko ya ukuaji mlikuwa mnaendelea kula good tyme kama ulivyosema mwenyewe hiyo inaweza kuwa sababu ya kwanza. Sababu ya pili nadhani hakuwa akifika kileleni alipokuwa mdogo, sasa amekuwa mdada (mwanamke) anapata kusikilizia utamu na hatimae kukojoa......tuanze na sababu ya kwanza, sawa?

Sababu za Ukuaji:-
Hivi sasa huyu binti atakuwa na miaka 21 kama bado nakumbuka hesabu vema, umri ambao mwili wa mwanamke unakoma kukua yaani yale madadiliko kutokana kuvunja ungo yanakuwa yamekamilika na sasa anakuwa mwanamke kamili yaani mwili wake uko settled...umetulia.

Kwavile alikuwa akingonoka mara kwa mara akiwa ktk kipindi cha ukuaji mwili wake ukatend kukubali mabadiliko ya kingono yaliyosababishwa na uume wako na kuendelea kufanyia kazi sehemu hiyo kama ilivyo, sasa baada ya kuwa mwanamke wa miaka 21 ni kawaida kabisa kwako kugundua mabadiliko kama hayo na kwa kifupi wewe ndie uliyesababisha.......wazazi huwa wanasema acha kuharibu watoto wa wenzako that is what they mean.

Sababu ya kutofikia Mshindo (sitokwenda kwa undani kwa sababu ya Mwenzi mtukufu):-
Jinsi mwanamke anavyofurahi tendo ndivyo ambavyo ute unaongezekana na anapofikia mshindo(kilele) basi mwanamke huyu huzalisha ute mwingi zaidi hali inayoweza kusababisha yeye na wewe mtiaji kuhisi kama vile uke umepanuka kimtindo.

Ndio maana huwa nashauri wapenzi wanaokerwa na hili kubadilisha mkao/mdindo au kumpa muda mwanamke huyo apumzike (sio lazima utoke, unaweza kubaki ndani bila kufanya kitu) mpaka mwanamke huyo atakapo kuwa tayari kuendelea na ute utakuwa umepungua au unaweza kumfuta na kujifuta uume wako kisha mkaanza upya.

Mwisho kabisa napenda kukuhakikishia kuwa binti huyo hakuchezi shere na hata kama angekuwa kifanya hivyo wala usingegundua kwa kumtia, sio rahisi hasa kama anaotoka nao wanauume wenye ukubwa kama wakoa u chini ya hapo.

Ondooa hofu na endelea kupiga kazi kwa bidii.

Kila lilojema HO.

Tuesday, 1 September 2009

Je ni kawaida au huyu wangu kazidi?-Ushauri

Habari dada!
Hongera kwa kazi nzuri unayoifanya kwa kusaidia kwa ushauri kwa watu wanaohitaji msaada,
nikiwa mmoja wapo ya wanaperuzi wa blog mbalimbali nimeona niombe ushauri kwako.

Mwaka huu ulipoanza nilipata mchumba ambaye wakati tunakutana mimi nilikuwa nimeajiriwa na yeye akiwa bado so unakuta tulipokuwa tunatoka out I had to share cost with him ili asijione ni mzigo kwake.

Aunt huyu Mchumba kwangu namwona ni mtu wa ajabu maana anaweza akaniita sehemu na kuagiza vitu na bill inapokuja ananirushia mpira mwanzo nilidhani kwa sababu hana kazi but now amepata kazi lakini bado anafanya the same.

Kama juzi tulitoka na rafiki zake bill ilipokuja akalipa chakula na kunirushia mpira bill ya vinywaji, kisa alijua siku hiyo nimepata pesa Ofisini. Kwa shingo upande nikatoa na kulipia vinywaji. Aunt hii sio mara ya kwanza there are time nilifiwa na ilinibidi kusafiri kwenda nyumbani (Kijijini) wakati msiba umetokea ilikuwa kama 3 days before birthday yake.

Niliporudi kama 2 dayz baada ya siku yake huyu Mchumba akawa ananikumbushia zawadi yake bila hata huruma kwamba nilitumia pesa kusafiri kwenye msiba tena wala yeye hakunipa hata shilingi kwa ajili ya safari.

Jamani eti hii ni kawaida au huyu wangu kazidi?
MJ"

Dinah anasema:Habari ni njema tu MJ, asante kwa mail na kwa uvumilivu as nimechelewa kukujibu. Ni matumaini yangu wachangiaji walisaidia kwa kiasi kikubwa kupitia michango yao.

Mh huyu wako kweli kazidi, mwanaume gani anashupalia zawadi ya b'day? Kwanza wanaume muhangaikaji (au tumuite a real man) huwa hawajishughulishi sana na kumbu kumbu za kuzaliwa kwake kwa kupata zawadi au kufanya party bali kutafuta mikakati ya kijiweka sawa kimaisha kwa vile umri unakwenda mbele na majukumu yanakwenda kuongezeka.


Kwa kawaida wanawake tumezoea kuangaliwa na kujaaliwa kiuchumi na wanaume hata kama tunasenti zetu wenyewe kutokana na shughuli zetu, sio kwa sababu ya mfumo dume, la hasha! ni kutokana na matakwa yake Mwenyezi Mungu, kwamba mwanamke atazaa kwa uchungu na mwanaume atakuwa mtafutaji. Tumekuwa tukiona hayo kwa macho, mama na baba wote wananya kazi lakini ni baba pekee ndiye anaefanya kila kitu kinachohusu manunuzi au pesa.


Kwa baadhi ya wanaume kumjali na kumtunza mwanamke kiuchumi ni sehemu ya UANAUME, kwamba asipofanya hivyo Ego yake inaumia na pengine kujiona useless. Lakini siku zinavyozidi kwenda mambo yanabadilika wenyewe tunaita maendeleo au usawa.


Nasikitika kusema sehemu kubwa ya jamii inalichukulia suala la Usawa tofauti kabisa na lengo au dhumuni la kuwa sawa, kwamba pamoja na kuwa tunatofautiana kijinsia sote tuna haki sawa ya kupata Elimu, Kulipwa mshahara kutokana na uwezo wa kikazi/cheo, kukataa/kukubali/kupinga au kufanya maamuzi, haki ya kuongoza kisiasa, kiuchumi au hata kingono, haki ya kutaliki n.k. Hii yote ni katika kuondoa mfumo dume ambao ulikuwa unakandamiza wanawake wengi Duniani.


Sasa baada ya wanawake kujua haki zao na kuwa na sauti baada ya ule mkutano wa Beijing, wakabadilika na kuwa sio sawa bali ni kujiamini kupita kiasi hali inayopelekea wao kuonekana au kuwa wajeuri. Hii imesababisha wanaume wengi hivi sasa kuwa wachunaji, ndio wapo wanaume wengi siku hizi wanatumia wanawake kiuchumi, wanafanya exactly what women used to do or are doing which katka hali halisi is wrong na haijalishi wewe ni mwanamke au mwanaume, huna hali ya kumtumia mwenzio kiuchumi na badala yake unatakiwa kushirikiana nae.

Nini cha kufanya: Unahitaji mawasiliano ya haraka sana ikiwa unampenda na unataka kuendelea na uchumba wenu ili baade mkafunge ndoa na kuishi pamoja kama mtu mmoja, usipojitahidi na kuweka mambo wazi sasa ni wazi kuwa ndoa yenu haitodumu au haitokuwepo kabisa kwani huyo sio mwanaume ambae mwanamke yeyote angependa kuolewa nae unless unataka kuolewa ili kuondoa "mkosi".

Tafuta siku nzuri na andaa mazingira mema ili uweze kuzungumza nae, hakikisha huna hasira na wala suiongee ktk mtindo wa ku-demand mabadiliko. Mwambie mpenzi mchumba wako kuwa unampenda na ungependa siku moja muishi kama mke na mume ( kwavile tayari mmechumbiana tayari), lakini kuna vitu vichache vinavyoweza kufanya hilo lisitokee.

Sema kwa uwazi, kuwa sio kwamba ulisahau kumnunulia zawadi bali mambo yaliingilia hapo kati na ikabidi usafiri kwa ajili ya shughuli za kifamilia hali iliyopelekea wewe kutokuwa na senti. Mueleze, kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi watu wanashirikiana kwa kila jambo na kila hali hivyo hukutegemea yeye ku-demand zawadi ya b'day bila hata kujali hisia zako baada ya kufiwa.

Orodhesha kuwa (kama nilivyo panga ili uweze kutoa your point mwisho), ili uhusiano wenu uwe bora unahitaji viungo vitano muhimu:-
(1)-Kusikilizana/kuelewana.
(2)-Kuheshimiana/thaminiana.
(3)-Kusaidiana.
(4)-Kuaminiana
(5)-Kushirikiana, "tunatakiwa kuonyesha ushirikiano huo kimapenzi, kimwili na kiuchumi".

Endelea kwa kusema kwa upole na upendo ukimuangalia machoni, kuwa unaamini ktk ushirikiano na kusaidiana kiuchumi na sio kushindana au kuwa tegemezi. Malizia kwa kusema sisi ni wachumba hivi sasa, tunatakiwa kuanza kujiandaa na maisha yetu ya baade kwa kuanza kushirikiana. Ongeza, ungependa kuanzia sasa tushirikiane na kukubaliana nini tunakwenda kufanya kabla ya kukifanya.

Mf: Kabla hatujatoka out ni vema mkapanga mnaenda wapi? mtakaa kwa muda gani? watu mtakao kutana nao huko walialikwa na ninyi au wakwenda wenyewe? na mtatumia kiasi gani?

Akikubaliana na wewe basi hakikisha unaangalia mabadiliko na wewe kuwa mstari wa mbele kuhakikisha ushirikiano huo unakuwepo (inaelekea yeye hajui ) so wewe sasa unajua hakikisha unakuwa a leader lakini sio in a kijeuri way bali loving way.

Akibisha ua kuwa mkali na hataki kukusikiliza ua hata kukuelewa basi tambua njemba hiyo inakutumia kiuchumi ili kuonekana ina hela Mpe buti la meno kisha anza upya na utakutana na mtu mwenye kujali na kukupenda kwa dhati.......si unajua mtu akiwa limbukeni wa kulipwa mshahara, anataka Dunia nzima wajue anajua kuzitumia (kumbuka hakuwa na kazi b4).

Nakutakia kila la kheri.