Sunday, 30 August 2009

Acha wale too wet! Mie yangu ni baridi-Ushauri

"Habari yako dada Dinah,
Pole na kazi za kuelimisha jamii,
Tatizo langu ni hili: nimeolewa miaka 3 iliyopita na nimefanikiwa kupata mtoto mmoja, natumia dawa za uzazi wa mpango sasa basi wakati wa kufanya mapenzi mume wangu anasema kuwa "K" yangu haina joto kabisa kama zamani na anasema kadri siku zinavyokwenda lile joto joto la ndani ya K linaondoka sasa ni miezi zaidi ya 4 tokea tatizo hilo litokee.

Je nifanyeje kurudisha hali ya ujoto ndani ya K yangu? je, hii inasababishwa na family planning? naomba please please uiokoe ndoa yangu maana tunapoelekea sipo kabisa.
nitashukuru sana iwapo nitapata ufumbuzi wa hili.
Ahsante na Mungu akubariki!"

Dinah anasema:Kwanza kabisa napenda kuomba msamaha kwa uchelewaji uliosababishwa na shughuli nyingi za kikazi, pili nasema asante sana kwa uvumilivu wako.

Tatizo la mabadiliko ya uke wako linaweza kusababishwa na uzazi (inategemea umejifungua lini?) hilo mosi, na pili basi inawezekanakana kabisa kuwa ni madawa ya kuzuia mimba ndio yanayosababisha mabadiliko ya uke wako.

Nadhani mumeo anashindwa kuelezea namna uke wako unavyo-feel kila anapokuingilia, inawezekana kabisa kuwa anahisi umaji-maji umeongezeka ambao mara nyingi huwa ni wa baridi kwa vile sio ule ute asilia unaotokana na nyege ni maji yanayosababishwa na matumizi ya madawa ya kuzuia mimba.

Nini cha kufanya: Kuna vitu 2-3 hivi unahitaji kuvifanya ili wote wawili kufurahia tendo lenu la ndoa. (1)-Badili aina ya kinga ya kuzuia mimba na hakikisha inakuwa Condom kwani hii ni kinga pekee ambayo haimbadilishi mwanamke kimaumbile wala kiHomono na haisababishi maji-maji. Lakini kabla ya kufanya hivyo unatakiwa kumhusisha mumeo ili asije kushangaa inakuwaje mnatumia Condom.

Natumaini itakuwa rahisi kwake kukubali kutumia Condoms since yeye ndio aliyelalamika kuwa K yako ni baridi vilevile hiyo ni kinga pekee itakayo saidia Uke wako kuwa na joto atakalo.


(2)-Sina uhakika muda gani umepita tangu umejifungua, vyovyote ilivyo jaribu kufanya mazoezi ya kukaza misuli ya uke, Misuli ya Tumbo( ambayo yanasaidia sana kuboresha tendo la ndoa), kaza misuli ya mapaja na makalio kila unapokuwa unafanya mapenzi na mumeo (licha ya kufanay K ibane kinamna pia itasaidia kufanya mapaja na makalio yako kuwa firm).


(3)-Angalia vyakula unavyokula, hakikisha unapika vyakula kiasilia zaidi yaani kibongo-bongo na epuka vyakula vya kupasha moto. Ninaposema uache kula ready-made au fast food sio ili upunguze mwili wako tu, bali pia ni kupunguza chumvi ambayo inaongeza maji yasiyohitajika mwilini ambayo yana uhusiano mkubwa sana na maji mengi ukeni.

Kila la kheri.

Sunday, 23 August 2009

Wake zetu na Tigo, utamjuaje kuwa anataka?-Msaada

"Za sahizi dada yangu, kuna comment niliiona kwenye mambo ya kutafuta mtoto kama sikosei, kuna mtu alisema anataka watu wakiri kuhusu tigo then nikaona kuna dada mmoja kakiri, alafu kuna mtu anaitwa Emu 3 akasema ilishaongelewa so we have to reffer back.

Nikafanya hivyo but kwa kukalashia tu. Kilichonifanya niandike hapa tena ni kwamba mimi nilikuja Bongo wiki chache zilizopita but nimerudi tena huku nje ya nchi kutokana na ishu ambayo ilinileta Dar kutokamilika kutokana na iyo mnaita Tigo.

Nilikuja kwenye sherehe za ndoa ya rafiki yangu kipenzi ambae alimuacha mchumba wake huko na amekaa nae 3yrs. Ilibaki week ndoa yao ifungwe, tukiwa Exim Bank na rafiki yangu tuna chanja, akapokea sms kutoka kwa fiancee but imekuja bahati mbaya na ilikuwa imeandikwa hivi " ULIVYONIFIRA LEO SITASAHAU" sorry kwa maneno makali.

Sikufichi dada yangu rafiki yangu amelia kama mtoto, na anasema ye katika miaka mitatu hajawahi hata siku moja kumla Tigo mchumba wake lakini kama angejua kuwa mpenzi wak anapenda kuzunguukwa basi angeweza lakini hakudhania.

DINAH hii tabia ya Utanzania while tunataka tuishi kama Wazungu utatu cost zaidi, tafadhali tusaidiane, yaani hata mimi nimechanganyikiwa kwasababu sijawahi wala sijui dalili za mwanamke mpenda Tigo, sio tu niko confused pia nimekuwa na uwoga hata kwa mpenzi wangu.

Yaani hivi ninavyosema jamaa karudi kubeba box na ndoa imevunjika. Ndugu wanamuuliza anawaambia muulizeni Ann ambae ndioa likuwa mke mtarajiwa, lakini msichana anashindwa kujielezea wala kudanganya kwasababu jamaa still anao ushahidi.

Sasa baada ya hapo nikakumbuka it was good to be true, na ishu ya yule mdau kuwa watu wakiri jinsi ya kufanya na madhala, the better way hasa kwa wanawake. Mimi nina wasi wasi kuwa even my girl is doing the stuff. Nina mpenda sana na kama ataniambia ukweli itabidi nianze tu kumfanya kinyume na maumbile.

Ningeomba wanawake watusaidie tutajuaje kuwa wanataka iyo kitu, DINAH THIS IS VERY SERIOUS, NDOA NYINGI NA NYUMBA NDOGO ZINAONGEZEKA KWA HII KITU, kama nakumbuka kuna mtu alisema kwenye comment kuwa yeye ananyumba ndogo just because of the TIGO na anajuta kwasababu inam cost.

DINAH PLZ JARIBU KUSAIDIA MAMBO MAGUMU NI BORA TULE TIGO WAKE ZETU WENYEWE.
JUNIOR ."

Dinah anasema:Junior sio rahisi kumjua mwanamke kuwa anapenda hili tendo, mzoefu kwenye wa tendo hilo au hata kutaga Tigo unless yeye mwenyewe awe wazi kwako kuwa hicho ndio kitendo atakacho. Tatizo hapa sidhani lilikuwa Tigo, nafikiri hakuwa muaminifu kwa Mchumba wake ambae sasa ni Ex.


Tigo imekuwa maarufu sana sio hapa nyumbani Tanzania tu bali hata Nchi nyingine Duniani, Tendo hili sio rasmi linatumiwa sana na Teenagers kama njia ya kuzia mimba, baadhi ya Makabila hulitumia tendo hili kutunza Bikira zao mpaka watakapofunga ndoa.

Baadhi ya watu wanaamini kuwa ni dhambi lakini wakati huo huo tukubali kuwa mtu anapoamua kufanya tendo hilo ni matakwa na chaguo lake na hatuna budi kuheshimu ikiwa atasema adharani kuwa anashiriki tendo hilo batili.


Pea (Couple) nyingi zinasumbuliwa na tatizo la mawasiliano, kwamba watu wanapata shida sana kusema kwa uwazi ni nini hasa wanataka kwenye uhusiano wa kimapenzi na ule wa kingono, hao wanaume wanaofuata Tigo nje ya ndoa zao wengi huofia kudhaniwa Mashoga (kwani O zote zinafanana) na wake zao au kuachwa ( kwa Dini ya Kiislamu mume akitaka Tigo unatakiwa kumtaliki).


Natambua watu wengi wana-find very hard kuzungumzia masuala ya kingono na wapenzi wao, lakini ili kuepuka matatizo madogo madogo ambayo ni serious kwenye mahusiano yetu ya kimapenzi tunapaswa kujifunza kuwasiliana kwa uwazi.

Sasa ili ujue kuwa mpenzi anataka Tigo au pengine hajawahi kufanya lakini angependa kujaribu basi ni vema kuulizana maswali ktk mtindo wa kuongea/wasiliana....Mf kitu gani cha ajabu umewahi kufanya kingono?____atakujibu, kisha unaweza kuuliza tena umewafi kufanya Tigo?____atakupa jibu, from there utajua kama ni mtu wa Tigo au lah! Hivyo yaani.

Mawasiliano haya yaliyo mara nyingi hufanywa siku za mwanzo kabisa za uhusiano wenu kabla mtu hujajikita kwenye Uchumba, unajua kabisa unachumbia mtu mwenye tabia gani Kingono, kwamba mtundu, mtundu kupita kiasi, asiye na mipaka kwamba yuko tayari kufanya lolote-popote, wa kawaida lakini anapenda kujifunza n.k.

Imani yangu kuhusu Tigo inabaki pale pale kuwa ni tendo batili na linamadhara makubwa kwa afya yako mwanamke hapo baade ikiwa linafanyika mara kwa mara.

Kila la kheri!

Wednesday, 12 August 2009

Unapompa mdomo mumeo/mpenzi usisahau hapa...na hapa!

Habari ya sasa mpenzi msomaji, mchangiaji na mtembeleaji wa D'hicous. Kama nilivyojieleza kwa baadhi yenu mlioniandikia ni kuwa kwa sasa nimebanwa (busy) kweli na shughuli za kikazi hali inayosababisha kukosa muda wa ku-dinahicious-ika na we hapa.


Sasa kwa vile nashindwa kubebesha maswali kutokana na ufinye wa muda wa kuyajibu ni heri yaendelee kuwepo huko (saved) na nitakapokuwa less busy which inatokea wiki ijayo basi nitayaachia ili tuendelee kusaidiana na kukumbushana vitu muhimu kuhusiana mahusiano, mapenzi na ngono.


Kwa vile mie sio choyo (wengi mmetambua hili by now) napenda kukumbusha (kama unajua) na kukufunza (kama ulikuwa hujui) kuhusu kona muhimu za kuzingatia unapomshukia mume/mpenzi wako. Natambua wengi mmeambiwa na wanawake wenzenu kuwa kichwa cha uume ndio mahali pekee pa kuzingatia na kupafanyia kazi kiufundi ili kumpa utamu kiumbe huyo uumpendae.


Si hivyo tu bali hata mwanaume wenyewe ambae ndio mpenzi/mume wako anaweza kukuongoza au kukwambia ubaki hapo kichwani muda mrefu zaidi huku mikono yako ikifanyia kazi pumbu na "shina" lakini kama wewe ni mtundu (kama mimi ofcoz hihihihi) utagundua kuwa linapokuja suala la kunyonya uume kumbuka kuna kona 3 muhimu unatakiwa kuzifanyia kazi ili kupata matokeo mazuri.


Vinaitwaje? sijui as nimekuwa nikijaribu mara kwa mara na kupata matokeo mazuri, ila najua vilipo. Bila shaka unaujua uume ulivyo, kwamba kuna kichwa, jicho, shingo alafu mwili na makalio (pumbu).


1)-Pale jichoni kwa chini kidogo kama unaelekea pumbuni ukipafanyia kazi vema kwa kutumia kidole ambacho kitakuwa kinaute unaojitokeza pale mpenzi atapata raha. Vilevile wakati unanyonya unaweza mpagawisha mpenzi wako lakini unapaswa kuwa mwangalifu usiingize ncha ya ulimi wako kwa ndani kwani anaweza kuwa uncomfortable kwani ni too sensitive kimtindo.

2)-Kwenye uume ukiangalia vema kwa nyuma chini kidogo ya jicho pia nishingoni (pale kwenye ring) ilipokatwa ngozi/gozi/mkono wa sweta yaani pale panapotenganisha kichwa na Shaft kwa nyuma lakini..... enhee hapo hapo, unapomnyonya uume mpenzi wako basi hakikisha mdomo unafunika na kufanyia kazi kichwa wakati huohuo ulimi ufanyie kazi hapo mahali nilipokuambia(kama sio atakaza misuli ya miguu na matako, atakunja vidole vya miguuni au kukushikilia kichwa basi atatoa sauti fulani hivi zinazokuambia "ooh ni utamu please endelea").


3)-Ukishikilia uume vema ukiwa umesimama, angalia kwa nyuma utaona kijimshipa fulani well sio mshika lakini ni kama mshipa ila mnene kiasi (wakati mwingine hauonekani) lakini kumbuka kama unaujua uume vema basi haitokuwa shida kuona kona hiyo hataka kama kijimshipa hicho hakijatokeza.


Ushikilie vema Uume kisha uangalie vema na ugawanye mara mbili (nusu) kwa kuangalia/kwa macho na pale kati kati ndio kipele chenyewe nakizungumzia. Sasa panyonye mahali hapo kuanzia chini ya kichwa kuelekea chini kwenye pumbu....hakikisha ulimi unapitishwa pale wakati midomo (lips) zina funika zile nusu mbili za Shaft.

Umenielewa au bado?

Unakumbuka zile aina 5 za kunyonya uume?? unapozifanya usisahau hapa.....na hapa.

Nakuhakikishia mume/mpenzi hawezi kuchomoka nje kufuata ngono ikiwa unanzingatia machache ninayokupa kupitia D'hicious, Akitoka basi atakuwa kaenda kutafuta mengine, lakini sio Ngono.

Psst! Hii ilikuwa moja ya Topic kwenye kipindi cha Dinahicious live ndani ya Bongoradio wiki iliyopita.

Kila la kheri!

Wednesday, 5 August 2009

Dating online bila ngono, Mume kagundua-Ushauri

"Habari za leo Dinah, Mimi ni mama Samirah wa Briton-UK nimefurahishwa na kipindi chako leo (12 -07-09). Cheating inaweza kutokea ikiwa owte au mmoja wenu anakuwa bored na hapewi attention.

Mimi nimeolewa miaka 25 iliyopita na nina watoto wakubwa tu, lakini kutokana na shughuli zangu nyingi za kikazi sikuwa na muda wa kuipa Ndoa yetu attention na matokeo yake tukawa tunaishi kama mtu na flatmate wake.

Mimi nikienda kulala mume wangu anaendelea kufanya shughuli zake kwenye Comptuter au kuangalia TV, yeye akiwa amelala mie nakuwa macho nikifanya shughuli zangu. Maisha yetu yakawa hivyo kwa muda mrefu sana.

Ikafikia wakati nikawa nakosa the attention kutoka kwa mume wangu lakini yeye akawa hajali kabisa, mwishowe nikaamua kujiunga na dating site ya wanandoa ambao wako bored (nilipewa habari na co-worker hapa kazini). Huko nilikutana na wake kwa waume na wote ni wanaume na wake zao nyumbani.

Nilikuwa muoga lakini baadae nikawa nafurahia attention kutoka kwa wanaume hao kupitia emails na hatimae nikaamua kukutana nao moja baada ya mwingine na nilikuwa nafurahia sana jinsi walivyokuwa wakinijali na kunipa the attention na sifa lukuki nyingine hata mume wangu hakuwahi kuniambia.

Kwakweli nilibadilika na kuwa mwanamke mwenye furaha sana na nikabadilika kimavazi kwani zile sifa zilinilevya ukizingatia wengine walikuwa wakiniambia nikivaa magauni ya hivi napendeza zaidi na umbile langu linaonekana vizuri zaidi, basi mie nikawa nanunua nguo kwa mitindo hiyo ili kupendeza zaidi kwa nje na kujisikia vizuri kwa ndani.

Pamoja na kukutana nao hao wanaume kwenye dates sikuwahi kushawishika kufanya nao ngono, siku zote niliishia kuongea kuhusu maswala ya kimaisha, matatizo ya ndoa zetu, wale wanaume waliokuwa wakijaribu kutaka kwenda zaidi ya maongezi mara nyingi nilikuwa siwapi nafasi ya kukutana na mimi tena na wala sikuwa nikiwajibu.

Kwa bahati mbaya Rafiki wa Mume wangu alijiunga kule na ndio ukawa mwisho wa maisha yangu ya ndotoni kwani aliliona profile langu na moja kwa moja akaenda kumueleza mume wangu. Mume wangu alikasirika sana na tukagombana sana siku hiyo, lakini mie nikamuambia mume wangu kuwa yeye ndio chanzo kwani alikuwa akiniona kama vile fenicha ndani ya nyumba, nimpikie, nimfulie, nimuandalie mahali pa kulala na yeye anachofanya ni kula, kulala, kwenda kazini nakurudi.

Mume wangu akaondoka kwa hasira huku akisema tunahitaji kupeana nafasi na atakuwa Hotelini, mume wangu tangu atoweke hapa nyumbani hajaongea na mimi bali watoto wake wetu tu ndio anaongea nao na huenda kumtembelea huko hotelini. Watoto wetu hunipa habari baba yao anaendeleaje.

Dinah mdogo wangu, mume wangu nampenda sana japokuwa alikuwa nakasoro zake na kweli nilijibu kwa hasira nikidhani kuwa atakubali kosa na kunipa nafasi nimueleze ukweli wa ile dating site, lakini hakunipa nafasi hiyo.

Namtaka mume wangu kuliko nilivyokuwa nikimtaka mwanzo, sasa ni heri niwe nae nyumbani na sipati attention kuliko kukosa vyote. Yeye simuoni na attention haipo mara saba zaidi.

Naomba wanablog na Dinah mnipe ushauri ili mume wangu arudi nyumbani."

Dinah anasema: Habari ni njema tu Mama Samirah, asante kwa mail yako. Natambua pea nyingi sana hujisahau au niseme husahau kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi ndani ya ndoa yao mara wanapozingwa na shughuli nyingi za kikazi.


Kutokana na maelezo yako nimegundua makosa mawili, Mosi ni uamuzi wako wa kumsaliti mumeo na kwenda kukutana na wanaume wengine, haijalishi kama uliwapa mwili (ngonoana) au la! Muda ulioutumia kwenda kutafuta, kujiandikisha na hatimae kuwa unakutana na hao wanaume nje ya ndoa yako ndio muda ambao ulipaswa kuutumia kurudisha romance ambayo ingeokoa ndoa yako.


Pili ni kumsukumuzia mzigo wa lawama yeye mumeo wakati unajua kabisa kuwa wote wawili mlijisahau au mlikuwa mnategeana au oengine mlikuwa mnadhani kuwa mmekuwa wazee kupeana attention kama wapenzi.

Badala ya kumuambia kuwa yeye ndio chanzo ulitakiwa kumuomba msamaha kwani wewe ndio uliyemtenda mwenzio, hata kama alikuwa hakupi attention bado alikuwa anakuheshimu na kukuthamini na kutumia muda wake nyumbani.


Ni wazi kuwa Mumeo amehama hapo nyumbani baada ya kugundua kitendo chako ili kupata nafasi ya kufukiri kabla hajafanya uamuzi kwa faida yake na watoto wenu, sasa unachotakiwa kufanya ni kama ifuatavyo:-

Mosi, ni kuomba msamaha kwa kumsingizia kuwa yeye ndiye aliyesababisha wewe kuibua tabia chafu na kumsaliti. Kama alivyoshauri mmoja kati ya wachangiaji, unaweza kutumia Kadi, Emails au barua (kizamani) ambayo actually siku hizi ni more romantic kuliko emails na Kadi. Hakikisha unaandika maneno yako kutoka moyoni na sio kuCopy na kuPaste kisha unaPrint.

Pili, kubali kuwa ulikuwa mjinga, mbinafsi na mwepezi kushawishika kirahisi na kufanya ulichokifanya, jutia kosa lako na kubali lawama zote ikiwa atazitoa juu yako (kumbuka you want him back ukianza ubishi utakuwa unamuongezea hasira)

Tatu, wakati unakili kuwa wewe ndio wa kulaumiwa, tumia nafasi hiyo kusema ukweli kuhusu kile ulichokuwa unakikosa lakini pangilia maneno ambayo hayatamfanya ajisikie alikuwa kajisahau (again, kumbuka wewe ndio unamtaka Mume asikutaliki hivyo kuwa mwangalifu), Mf: badala ya kusema kuanzia sasa tupeane attention.....unaweza kugeuza kibao na kuahidi kuwa utajitahidi kugawa majukumu na muda wako kati ya kazi na yeye n.k

Nne, kamwe usizungumzie wanaume wangapi umekutana nao na wapi mlikuwa mkikutana au nini walikuwa wakikuambia. Lakini ikiwa atataka kujua kama ulifanya ngono nje ya ndoa yenu basi sema ukweli (hapa umesema hukukutana nao kimwili) mhakikishie hilo kwa kusema wazi hisia zako juu yake, namna unavyomthamini kiasi kwamba huwezi kutoa mwili wako kwa mwanaume mwingine yeyote, sema hakuna mwanaume yeyote anaestahili mwili wako bali ni yeye mumeo na mengine yote ujuayo kuhusu kumfanya mwaname ajisikie Safiii!

Tano, mpe muda wa kufikiri mara baada ya kumuomba msamaha na kumueleza ukweli. Usilazimishe aje nyumbani haraka na badala yake muonyeshe namna unavyompenda kwa vitendo zaidi (kumbuka ahadi ulizompa), hakikisha yote uliyosema unayafanya kwa vitendo.

Kuwa mvumilivu kwani haweza akaamua kukusamehe na kusahau hapo hapo, atahitaji muda. Pia kumbuka kuna mtu wa tatu hapo anahusika ambae ni rafiki yake. Huyu rafiki (inategemeana na urafiki wao) anaweza akajenga au kubomoa ndoa ambayo tayari inaufa.

Hivyo basi, kama unauhakika kuwa huyu rafiki ni wa Damu basi unaweza kumtafuta huyu Bwana na kumueleza ni jinsi gani unampenda mumeo na watoto, ni namna gani ungepeda ndoa yenu iendelee kuwepo. Mwambie ni vipi unajisikia vibaya kwa kitendo ulichokifanya kwa rafiki yake ambaye ni mumeo, Weka wazi hisia zako za kimapenzi kwa mumeo mbele ya huyu bwana.

Hii itasaidia sana kufikisha ujumbe kwa mumeo ambao utajazaia yale uliyokwisha mueleza mumeo, hasa ukizingatia yeye ndiye aliyepeleka ujumbe wa dating site.

Baada ya hapa, watumie watoto ili kupata date ya familia ikiwa ni pamoja na baba yao, watoto siku zote wanapenda baba na mama kuwa pamoja hivyo haijalishi ni uchafu gani umefanya na utawaumiza lakini kama nia ni kurudiana watoto watasaidia kwa kiasi kikubwa sana kufanikisha hilo.

Kwa sasa nikuachie hapa ili ufanyie kazi Ushauri wa wachangiaji wengine na ule kiasi niliokupatia live kwenye radio siku ya Kipindi.

Kila la kheri.

Tuesday, 4 August 2009

Nafasi ya Wife, Unapogundua mtoto si wako-Ushauri

"Mie nafurahia sana jinsi unavyosaidia watu sijui ni kipaji au ulisomea haya mambo ya kushauri watu. Leo na mie natoa uzoefu wangu wa maisha ya ndoa naamini kuwa utasaidia wanablogu hii na wasomaji wengine kuwa makini na wapenzi wao.

Mie nimeolewa miaka saba iliyopita na tumebarikiwa kupata watoto wawili. Wakati tunachumbiana na mume wangu aliwahi kuniambia kuwa alizaa na mwanamke mwingine na waliachana miaka michache kabla hajakutana na mimi.

Ukweli sikujisikia vizuri kuwa na mwanaume aliyezaa na mwanamke mwingine lakini alinihakikishia kuwa haikuwa wazo lake kuzaa na yule mwanamke ila mwanamke yule alijilengesha ili Mume wangu asimuache wakati ule wako pamoja. Nilijitahidi kumuamini lakini bado nyuma nilikuwa nasumbuliwa na maswali kibao.


Mume wangu hakuwa akijihusisha sana na mwanamke yule isipokuwa kama mtoto anahitaji mahitaji muhimu ambayo yule mwanamke hawezi kutimiza au kama mtoto anaumwa, basi mume wangu akiwa kwenye heka heka za kumshughulikia mtoto wake mimi nilikuwa naumia sana nikifikiria mambo mengi ya kimaisha na uhusiano kati ya watoto wetu na mtoto huyo wa nje ya ndoa wa mume wangu.


Siku moja nikamuomba mume wangu amlete mwanae hapa nyumbani ili ajenge uhusiano na wanangu, lakini mume wangu alikataa kwa madai kuwa ni mapema kwake kufanya hivyo. Nilimuelewa na nikaheshimu uamuzi wake. Siku zikapita na sasa inakaribia mwaka mume wangu hajagusia lolote kuhusiana na mtoto wake huyo wala mama wa mtoto huyo kama ilivyokuwa zamani.

Juzi juzi hapa basi tukapata wageni kutoka upande wa mume wangu, kwa bahati nzuri tunaelewana sana na tunaongea mambo mengi tu kuhusu maisha. Mmoja kati ya mawifi zangu akagusia kuhusiana na mtoto wa nje wa mume wangu akaniuliza kama najua kuwa mume wangu alizaa nje. Mie nikajifanya kuwa sijui ili nipate umbea zaidi manaa yake wao walikuwepo na kaka yao na huyo mwanamke kabla mimi sijatokea kwenye maisha ya kaka yao.

Wifi yangu alizungumza mambo mengi ya kutisha na kusikitisha kuhusiana na uhusiano wa kaka yake na mwanamke aliyezaa nae. Kilichonitisha ni mwanamke yule kwenda kwa mganga ili mume wangu wakati huo alikuwa bwanake wafunge ndoa.

Wifi alinisimulia harakati zote walizozifanya mpaka kumpeleka kaka yao kwenye maombi na kufanikiwa kumtoa kaka yao kwenye maisha ya mwanamke yule na mwaka jana wakaamua kufunga safari na mtoto yule mpaka Afrika ya Kusini na kufanya vipimo vya DNA na kugundulika kuwa mtoto yule kumbe hakuwa wa damu wa mume wangu.

Baada ya maelezo hayo nikakumbuka safari ya mume wangu kwenda Afrika kusini kwa wiki moja na aliporudi alikuwa kama mgonjwa mie nikadhani ni uchovu wa safari. Pia nikagundua kwanini mume wangu alikataa kumleta mtoto yule pale nyumbani na kwanini siku hizi hazungumzii kuhusu huyo mwanamke wala mtoto wake wa nje.

Nashukuru Mungu nimejua ukweli kuhusu lakini nasikitika na kushangazwa na kitendo cha mume wangu kukaakimya kipindi chote cha mwaka mzima bila kunieleza lolote juu ya DNA au kuniambia tu kwa kifupi kuwa yule mtoto sio wake. Kwanini ananichunia kuhusu suala hilo wakati mwanzo alinihusisha?

Je itakuwa sahihi kama nitamuuliza? Kama ndio je nitaanzaje kuuliza ili aseme mwenyewe badala ya yeye kuja kugundua kuwa dada yake ndio aliyetoboa siri kwangu?

Mwenzeni hapa nilipo sielewi nini cha kufanya pia namuonea huruma mume wangu kwani najua kabisa anaumia na kujuta ndani ya moyo wake kutokana na muda alioupoteza kwa mtoto yule.
Mrs Mwilima, Dar es Salaam."

Dinah anasema:Mama Mwilima shukrani zikufikie kwa ushirikiano wako. Mimi binafsi sidhani kama ni sahihi kwa wewe kumuuliza mumeo kitu ambacho hakipo tena kwenye maisha yake. Hata mimi nahisi kuwa Dada mtu ambae ni wifi yako alitumwa na familia ya mumeo kukueleza wewe ukweli huo ktk mtindo wa siri, hii inawezekana ni ktk harakati za kuzuia mumeo kuumia zaidi kwa kujibu maswali mengi zaidi kutoka kwako kama mkewe (una haki zote za kujua kila kitu kuhusu mumeo).

Nini cha kufanya:Sahau kuwa mumeo alikuwa na mtoto kwani imejulikana sio wake, hivyo hakuna sababu ya kushupalia kitu ambacho hakipo tena na badala yake zingatia hali ya sasa ya mumeo. Natambua mumeo anahitaji muda ili kupona maumivu hayo (mwaka mmoja hautoshi kuponya maumivu yaliyowekwa kila siku ndani ya miaka yote aliyoishia kidhani mtoto ni wake), na wewe mkewe ndio mtu pekee utakaefanikisha uponaji wake wa haraka ili wote kwa pamoja muanze kuishi maisha yenye furaha na amani kama zamani.

Mpe ushirikiano mumeo, muonyeshe mapenzi ya kihisia zaidi na kumjali ktk kipindi hiki kigumu cha kukabiliana na masumbufu ya Kiakili na Kisaikolojia usikute hata Kiuchumi kwani Miaka yote hiyo alikuwa akipenda, kujivunia, kujali na akihudumia mtoto wa mwanaume mwingine akidhani ni wake.

Wewe pia unatakiwa kuwa mvumilivu kwani kipindi hiki mumeo anaweza akawa na hofu juu ya watoto wenu hao, inawezekana kabisa akawa anajiuliza mara nne-nne kama kweli ni wake au analelea mtu mwingine?

Ukiona hali yake inaendelea kuwa hivyo basi nakushauri wewe na wanafamilia kushirikiana na kumtafutia msaada wa Therapy ili kukubali ukweli, kusahau yaliyopita ili aweze kuendelea na maisha yake.

*****Haya mambo yapo sana na yanasikitisha lakini ukweli unabaki pale pale kuwa mama ni mtu pekee anaejua baba wa mtoto, Mtu unapoambiwa "huyu mwanao/mwanangu" Kisaikolojia watu wanaweza kuona mtoto kafanana sana na wao au babu, bibi, baba, shangazi yake n.k. lakini ukweli ni kufanya hiyo DNA Test kama unawasiwasi.

Kila la kheri Mrs Mwilima.

Monday, 3 August 2009

Namna ya kubadili mwenendo wa maisha yako kingono

Kutokana na uwingi wa shughuli (busy) nimeshindwa kutoa maelezo kwa maswali yaliyokwisha kuwa published hivyo basi siwezi kuendelea kuruhusu maswali mengine mpaka hapo nitakapoyajibu yaliyopo mapema wiki hii.

Sasa basi sio mbaya kama nikiwakumbusha haraka haraka kuhusiana na namna ya kubadili maisha yetu ya kingono pale unapohisi msisimko umepungua kwenye ndoa yako au hata mahusiano uliyonayo ya kimapenzi.

Kabla sijaendelea napenda kukuweka sawa, uhusiano wa kimapenzi ni tofauti na uhusiano wa kingono japokuwa kuna kutegemeana. Wapo wanandoa wanaendelea kupendana japokuwa hawana uhusiano wa kingono (hasa kama mmoja wao anamatatizo ya kiafya).


Lakini ukweli ni kuwa kama uhusiano wako wa kimapenzi sio mzuri basi uhusiano wa kingono hautokuwepo au ukawepo lakini hautokuwa ukifurahia kama vile unapokuwa mwenye mapenzi hali kadhalika uhusiano wa kingono ukiwa mbaya uhusiano wa kimapenzi unaweza kuharibika hivyo basi mahusiano yote mawili yanapaswa kuboreshwa.


Sote tunatambua kuna kujisahau, kuna kuzoea sana jambo na matokeo yake kuwa rotine ambayo inaweza kusababisha ule msisimko wa kufanya tendo la ndoa au mapenzi kwa wale ambao bado mpo mpo kwanza.

Hali hii inapojitokeza inaweza kabisa kusababisha mmoja wenu kutafuta namna nje ya uhusiano wenu na ndio maana wakati wote mimi huwa nakumbusha wote tulio kwenye mahusiano kuwa wabunifu, watundu na wadadisi ili kuendelea kufurahia mahusioano tenu ya kimapenzi na yale ya kingono.


Kitu cha kwanza unapaswa kukubali kuwa kuna vitu huwezi kuvibadili kuhusiana na uhusiano wako wa kingono na mume/mke/mpenzi wako hivyo basi huna buni kujifunza kuishi navyo, hapa nitakutajia baadhi na vingine unavijua mwenyewe (inategemeana na mpenzi wako0.
  1. Umbile na Rangi ya Nyeti zake (kubwa, ndogo, pana, nene, ndefu n.k)
  2. Uwezo wake wa kungonoka (mdogo au mkubwa)

Nini cha kubadili:-

  • Hakikisha ngozi yako mwilini inakuwa yenye afya na laini, huitaji mafuta ghali ya ngozi kamahuna uwezo huo na badala yake paka mafuta ya Nazi au yeyote ya maji kwani hayagandi mwilini alafu kunywa maji kwa wingi, achakunywa pombe.

  • Badilisheni ile rotine ya kushika/tomasana kwa kutumia mikono mikavu na badala yake paka mafuta kidogo ambayo hayana harufu au yenye harufu muipendayo ili kuongeza ulaini pale unapomshika-shika mpenzi wako, mshiko huo utaongeza msisimko fulani mwilini.
  • Pamoja na kuwa unajiswafi uke wako ili kuondoa Utoko pia ongeza ulaji wa mziwa ya mtindi asilia ili kuondoa harufu ya shombo hasa kama hapo ulipo kuna shida ya maji, sikutumia uache kujiswafi na ule Mtindi! la hasa ninachojaribu kusema ni kuwa ikiwa unajiswafi mara moja kwa siku kutokana na ukosefu wa maji Ulaji wa mtindi unasaidia kupunguza harufu hivyo hutohitaji maji mengi kujiswafi jioni kabla ya kulala....sijui umenipata pata hapo?!!
  • Itumie technologia ipasavyo hivyo basi Ibua tabia au jifunze kuzungumzia ngono na mpenzi wako kwa kubadishana barua pepe au SMS kama unajiamini na huna aibu basi unaweza kuongea moja kwa moja via simu.

Usianze kutafakari na kujiuliza utaanzia wapi? Unaweza ukazungumzia kitu mlichokifanya juzi ktk lugha ya uwazi zaidi, tumia maneno ambayo ktk hali halisi ni matusi au yanakaribia matusi lakini ni vitu ambavyo mnavifanya kama wapenzi.

Nitarudi kuja kumalizia......asante kwa ushurikiano!