Monday, 20 July 2009

Nataka kuwa a Good perfomer kama zamani-Ushauri

"Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 na nina tatizo kama la mwenzangu aliyetangulia linalotokana na Punyeto. Nilianza kupiga Punyeto nikiwa na umri wa miaka 16, katika kipindi hicho alijitokeza mwanamke aliyekuwa akifanya kazi kama nilliyokuwa nikiifanya kwa kipindi hicho ya uuzaji wa dagaa.

Akaniambia "kuna mtu nataka kuwa naye kimapenzi lakini naokopa kumwambia kwa sababu ni mdo kwangu"nikamuuliza ni nani huyo? akajibu "ni wewe mwenyewe" hapo nikakosa jibu. Siku zilivyo songa mbele akazidi kunipa promises za kukutana kwake kuni ana mambo ya kuongea na mimi ya husuyo kazi, ila kwakuwa nilikuwa na mashaka na promises zake siku zitimiza.

Siku moja alikuwa ametoka Kigoma ikaonekana atakuwa na mizigo mingi nikamsubili Station. Tulivyofika kwake akanipa zawadi aliyoniletea nikaipenda na kufurahishwa nayo. Kisha akaniambia"naomba unisubiri nioge twende wote sokoni, sikuwa na kipingamizi nilikubali na kumsubiri.

Alivyoingia chumbani alitoka amevaa kanga yaani maumbile yote yalikuwa yanaonekana akafika anakaa kwenye miguu yangu, usema ukweli baada ya kumuona maumbile yake ya matamanisho faster Mtambo uliinuka papo hapo. Aliponikalia nikahisi kwamba anataka Matibabu, sikuchelewesha nikamrudisha chumbani na kuanza mchezo.

Mchezo ulichukua kama masaa 2 hivi hadi akadai kuzidiwa, baada ya hapo tuliendelea na mapenzi na alinikubali kwa msukumo ila alikuwa ananizidi miaka 12. Baadaye nilisafiri kuelekea Kibondo huko niliishi bila mpenzi. Mpenzi wangu alikuwa punyeto na baada ya hapo nikasafiri tena kuelekea Marekani na sasa nilipata mpenzi ila ikifika wakati wa mahusiano ya kimwili siwezi kufanya hata 5 minute.

Nimesoma Makala nimegundua tatizo ni nini. Sasa je kuna uwezekano wowote wa kuweza kuwa na nguvu za kuweza kumtosheleza mwanamke kama zamani?

samahani AUNT kwa msg yangu ndefu yenye maswali
machache

Ninafurahi nipatapo Makala za Kiswahili
Please naomba unijibu
nakutakia kazi njema"

Jawabu: Asante kwa ushirikiano. Mwanaume anafika kileleni kati ya Dk 3-15 tangu tendo kuanza hivyo basi wewe hauna tatizo kabisa, lakini pia wapo wanaofika kileleni ndani ya dk20-saa moja. Hii inatokana na jinsi wanavyo tune akili zao.

Nikijibu wasli lako, Uwezekano wa kumridhisha mpenzi wako upo tena kwa kiasi kikubwa hasa ukizingatia wewe bado ni mdogo. Jaribu kufanya mzoezi ya kwenda mwendo mrefu bila kumwaga/maliza. Nikiwa na maana kiuwa kila mara unapofanya mapenzi na mpenzi wako jaribu kujizuia usimwage (soma mbinu kwenye link hapo chini), ukishindwa leo usikate tamaa, endelea kurudia mara kwa mara na siku moja utaweza.

Kwa vile sasa unampenzi basi ni vema ukaacha ile tabia ya kujichua mara kwa mara japokuwa najua sasa imekuwa mazoea lakini natambua unaweza kabisa kuachana na Nyeto. Baada ya muda utaweza kwenda dk 15, itakuwa 20 ambayo nadhani inatosha kabisa kwa mwanamke kuridhika na uume ndani ya uke wake.

Sasa wakati unaendelea kujifunza kujizuia ni vema kama utabuni njia nyingine za kumridhisha mpenzi wako. Bofya hapa kupata mbinu za kuzuia kumaliza/mwaga haraka, tafadhali soma kwenye maoni na sio the actual topic (wakati huu nilikuwa nikijibu as comment).

Kila lililojema.

Wednesday, 15 July 2009

I want a baby, tarehe gani nzuri?-Ushauri

"Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 22, nina mchumba wangu na tunaishi pamoja. Sijawahi kutumia njia yeyote ya kuzuia mimba mara zote huwa natumia tarehe, Sasa nashangaa tarehe hizo nikifatilia kulengesha ili nipate mimba sipati!

Nimejaribu kuuliza watu mbalimbali kila mtu ananifundisha tofauti kabisa, mwingine anasema ukimaliza hedhi ndio unapata mimba wengine sio hivyo!

Kwahiyo Dada Dinah tafadhari kama ulivyosaidia wengine na mimi nisaidie pia dada yangu. Nielekeze tarehe maalum ambazo nikilengesha mimba naipata kama hapa nilipo nimemaliza Hedhi na tarehe 23 mwezi wa Sita ndio nilikata hedhi,sasa nilengeshe lini ili nipate mimba?

Dada naomba unisaidie na unielekeze jinsi ya kulengesha kupokeamimba.Mimi kama mdogo wako nitashukuru sana,japo najua upo busy sana kwakazi ya kuelimisha jamii lakini nitashukuru sana zaidi ya sana kamautanijibu kupitia hii email address yangu kama usipopata mda sawa pianijibu kwa njia yeyeyote dada yangu mpenzi.

Wako mdogo Jane Tarimo
Dar es salaam."

Dinah anaomba ufafanuzi:Tafadhali niambie mzunguuko wako ni wa siku ngapi kwa maana wa kawaida wa siku 28, mzunguuko mfupi kwa maana ya siku 27-29 au Mrefu wa siku 27-35. Pamoja na mambo mengine nitakayokuelezea hii pia itanisaidia mimi kuelekeza tarehe gani hasa ni za kutegea ili kushika mimba.

Monday, 13 July 2009

Boyfriend anataka ngono, lakini mie naogopa-Ushuari


Hi,
Dada Samahani mimi ni msichana wa miaka 23 Sijawahi kufanya mapenzi ila nikiwa na umri wa miaka kama 6 tulikuwa tunacheza mambo ya kitoto.

Kwa sasa nimepata Mpenzi ila kinachonisikitisha anataka tufanye mapenzi ila mimi siko tayari nifanyeje.

1. Naogopa kupata Mimba kwa sasa

Dinah anasema:Sio kitu kizuri kuzaa nje ya ndoa na labda baadae kuwa mama wa watoto wenye baba tofauti hasa kama huyo Bf hatofungandoa na wewe. Vilevile sio vema kuwa mama kabla wewe mwenyewe hujafahamu maisha yako yamesimama wapi, kwamba huja-settle au kukamilisha malengo yako kama mwanamke.

2. Naogopa kupata Ukimwi


Dinah anasema: Kweli hali sasa inatisha sana kwani sio tu kuwa maambukizo ni mengi zaidi kuliko miaka kumi iliyopita bali pia hivi sasa tuna kizazi kilichokwisha ambukizwa, kwa maana kuwa walizaliwa na VIRUS au waliambukizwa wakati wa ukuaji wao kutokana na ukosefu wa elimu juu ya kuishi na walioathirika na virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Hivyo basi ninyi mnaokua miaka hii ambao wengi mlizaliwa miaka ya mwishoni mwa miaka ya 80 mnakuwa kwenye hatari kubwa ya kuanza uhusiano na watu waliokwisha ambukizwa na wazazi wao kabla ua baada ya kuzaliwa, hivyo basi mnatakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kujikita kwenye masuala ya mahusiano ya kimapenzi na hata ngono.

Hili tatizo ni kubwa na haijalishi wether uko nje ya ndoa au hujaanza kabisa ngono au umefunga ndoa, wote tunapaswa kuishi kwa taadhari na kujenga mzoea ya kuangalia afya kabla na baada ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi na ngono.

3. Naogopa kama naweza kumpa na anaweza kuniacha na naogopa kutendwa kwa sababu naona marafiki zangu wanavyotendwa na wanavyoumia.

Dinah anasema: Sio mara zote mpenzi wa kwanza ndio anakuwa mume hasa kama wote wawili "hamjakuwa" kiakili au hamjakamilisha malengo yenu kimaisha kama individuals. Hivi kama uoga wako ni kuachwa mara tu baada kutoa mwili wako kwake basi ni vema ukaliweka wazi hilo kwa mpenzi wako huyo.

Umri ulionao ni mdogo sana kuanza kufikiria suala la kutendwa, kwani vijana wa umri huo wengi bado wanajaribu kupata uzoefu kwa kujihusisha na mahusiaono tofauti na baadhi hawapendi kuwabaki na mpenzi mmoja kwa muda mrefu kwa vile hawako tayari kufunga ndoa, wanachokifanya ni ku-have fun na kupata experience.

Mwambie kwa kujiamini kabisa kuwa, "nitakuwa tayari kutoa mwili wangu (kufanya ngono) kwa mume wangu" kwa maana kuwa utafanya ngono utakapofunga ndoa, sasa kama yeye ametualia/kua kiakili, yuko tayari kukufanya wewe mkewe na anakupenda kweli basi atavumilia na siku moja kufunga ndoa na wewe ili kufurahia "ua" lako.

Akitoka baruti au kubembeleza umpe sasa na atakuona ujue hayuko tayari kuwa na wewe kwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja na nusu. (hii itasaidia kuokoa muda wako na vilevile utakuwa umenusuru kuumia kwani hutokuwa umengonoka nae).4. Nasumbuliwa na kutokwa na uchafu Mweupe kwenye sehemu zangu za siri mzito nifanyeje kwa sababu hii hali inanikera sana.

Dinah anasema: Huo uchafu unaitwa Utoko, ni asili kwa mwanamke yeyote anaekaribia na aliyevuja ungo (Balehe) kutokwa na ute huo mzito wenye rangi nyeupe. Kwa vile wewe bado hujajiingiza kwenye uhusiano wa kingono basi unatakiwa kuwa mvumilivu na kuwa msafi kwa kutawaza/dha kila unapokojoa, badilisha chupi mara tatu-nne kwa siku au mara tu unapoona Utoko huo kwenye chupi.

Utakapo anza kufanya ngono au utakapofungandoa na kuanz akungonoka basi utapaswa kuwa unajiswafi (Hapo juu kulia unaweza kutafuta topic inasema "jinsi ya kuswafi ume" au "Utoko" ili kufahamu vema zaidi).


5 Je nikiwa tayari kumpa huyu mpenzi wangu penzi mambo gani ambayo nitazingatia.

Dinah anasema: Utakapokuwa tayari kutoa mwiliwa kwa mpenzi wako huyu, njoo hapa nitakueleza kwa undani na kwa uwazi kabisa.6. Je nitajitayarisha vipi naomba ushauri wako kwa sababu huyu jamaa tuko naye huu mwaka na nusu na nimemwomba anipe muda wa mwezi mmoja tena.
Nashukuru sana Dada yangu.

Dinah anasema: Mwezi mmoja hautoshi kwa wewe kufanya uamuzia mbao utabadilisha maisha yako milele, kitendo cha wewe kufanya ngono bila kuwa tayari (kufanya ili kumridhisha BF) kitakufanya ujute na hutoweza ku-undo kilichokwisha tokea. Pia napenda utambue kuwa mwaka mmoja na nusu sio muda mrefu sana kwenye uhusiano kupelekea ninyi wawili kufanya ngono.


Kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa hauko tayari kufanya ngono kwa sasa na pengine unahitaji muda zaidi ya mwezi mmoja. Ikiwa kweli huyo Bf wako anakupenda basi hakika ataendelea kukusubiri hata kamani miaka 5 au hata mpaka mtakapofunga ndoa au utakapokuwa tayari kufanya hivyo.


Kumbuka ni wewe pekee mwenye mamlaka juu ya mwili wako, ni wewe pekee mwenye nafasi kuu ya kuchangua maisha yako ya kingono na sio mwanaume no matter how much u love him or he loves u.

Mara utakapokuwa tayari kuchukua uhusiano wenu kwenye hatua nyingine basi utahitaji kuwa na uhakika kuwa unachokwenda kufanya ndio kweli unakitaka na kamwe hutojutia, hakikisha unatoa mwili wako kwa mtu ambae mnapendana, mnaaminiana na mmepima afya kwa maana ya kuangaliwa kiuchunguzi kama hamna magonjwa yeyote ya zinaa ikiwa ni pamoja na kubwa lao UKIMWI.

Siku ya siku ikifika njoo nikupe maelezo zaidi ya nini ch akufanya, lakini kwa sasa zingatia na fanyia kazi ushauri uliopewa na wasomaji wa D'hicious.


Dinah anadokeza:Tafadhali usim-attack binti huyu mdogo, mpe ushauri utakao msaidia kama vile ambavyo utamfanyia mdogo wako ikiwa atakuja kwako kwa ushauri. Asante.

****Shukrani za dhati ziwafikie wachangiaji wote, tuendelee kushirikiana.
Binti muuliza maswali nakutakia kila la kheri ktk kufanyia kazi ushauri uliopewa na hatimae kufanya uamuzi wa busara.

Sunday, 12 July 2009

He's too busy kuwa na mimi, nampenda-anipenda-Ushauri

"Hi dinah,

Mimi ni msichana wa miaka 27, nina mpenzi ambaye tulianza mahusiano yetu tangu 2007. Tulipoanza mapenzi yetu yalikuwa motomoto, tulionana mara kwa mara na tulielewana vizuri tu. Ilifikia mahali na kunitamkia kwamba ifikapo October 2009 tutafunga ndoa.

Kwa kweli nilifurahi sana, kwasababu ni mtu ambaye ananijali sana. Chakushangaza kadri siku zinapozidi kwenda amekuwa bize sana na promises zimekuwa nyingi. Tunapopanga kuonana au kutoka out mara nyingi hatokei, nikimtumia sms anaweza asijibu kabisa, then baadaye anatoa sababu zisizokuwa za msingi na kusisitiza kwamba bado ananipenda sana.

Isitoshe sijamuuliza kuhusu ahadi aliyoitoa ya ndoa maana naona kama nitamforce. Kwa kweli naumia sana moyoni kwa sababu hana muda na mimi yuko bize kupita kiasi, lakini anadai ananipenda.

Sitaki kumjibu vibaya wala kumtamkia its over kwasababu nampenda nataka aje kuwa baba watoto wangu lakini ananiumiza kwa sababu ya the way he treats me. Naomba ushauri wako kwasababu kuna kitu kimenikaa moyoni nashindwa hata la kufanya.

Nimejitahidi kukaa kimya lakini wapi bado ananipigia simu na kunitumia sms bado kuwa bado
ananipenda. Sasa najiuliza mapenzi gani haya wakati mtu mwenyewe hana muda na mimi, muda wote ni wakazi ambayo anafanya hapahapa Dar.

Ni mimi mdau,
mery."

Dinah anasema: Hello Mery, asante kwa mail na ufafanuzi kuhusu umri wa mpenzi wako ambao hakika ni umri ambao vijana wehu huanza kutulia kiakili (anakaribia miaka 31). Nakubaliana na wewe kwenye swali la "mapenzi gani haya wakati yeye hana muda na mimi?".

Kutokana na tabia yake (kwa mujibu wa maelezo yako) kuna mawili-matatu yanawezekana:-
(1)-Inawezekana ni kweli anashughuli nyingi za kikazi zinazomzuia kukutana na wewe.

(2)-Vilevile kuna uwezekano mkubwa tu kuwa anaendesha maisha kivingine na anakuweka wewe kama spare tire incase huko aliko hakutokwenda atakavyo.

(3)-Hana mpango wa kuwa na wewe tena ila hajui namna gani ya kumaliza uhusiano hivyo anafanya hivyo ili wewe ukate tamaa na uchoke kumsubiri na hivyo u call it a day.

Kwanini basi nimedhania hivyo? Kwa sababu huyu bwana alikutamkia kuwa atakuoa au mtafunga ndoa mwezi wa Kumi mwaka huu lakini hakuchukua hatua zozote zinazoendana na matamshi yake Mf-Kujitambulisha kwenu na kupewa utaratiubu wa kufunga ndoa na wewe na hatimae kuanza maandalizi...mwezi Octoba sio mbali na nijuavyo mie maandalizi ya kufunga ndoa hasa kwa kufuata taratibu za kijamii Tanzania huchukua muda mrefu.

Kwenye uhusiano wenu kuna ukosefu wa mawasiliano, kwa maana kwamba hamzungumzii maisha yenu kama wapenzi kwa uwazi, wewe unadhani kuzungumzia ahadi yake ni kama kumlazimisha na yeye huenda anahisi kutokuzungumzia kwako suala la ndoa ni dalili kuwa huna mpango wa kuolewa nae au hauko tayari.

Unajua, kuna tofauti ya kati ya kukumbushia jambo ktk mtindo wa kuzungumza na kukumbushia jambo hilohilo ktk mtindo wa kudai/lazimisha (demand).....napata picha hapa kuwa hukujua tofauti hizo na wewe ukadhania kuwa kukumbushia ni ku demand yeye afunge ndoa nawe.

Nini cha kufanya: Kwa unampenda mpenzi wako na unaamini kuwa na yeye anakupenda lakini kwa bahati mbaya hatujui ni nini hasa kinasababisha yeye kuwa hivyo alivyo, fuata haya nitakayokueleza ili kupata ukweli utakao kusaidia kufanya uamuzi wa busara....

Naja midaz....

Saturday, 11 July 2009

Maji meupe ukeni, natumia Condom kwa kila tendo-Ushauri

"Habari dada DINAH.
Mimi ni msichana wa miaka26, nilianza mapenzi nikiwa form 2 lakini sasa ndiyo najuta. Nikiwa form 2 nilipata mpenzi ambaye alikuwa mkubwa sana kangu kwa umri na ndiye aliyenitoa bikira yangu.

Baada ya miaka 2 nikaanza kutokwa na majimaji sehemu za siri nikaenda hospital wakaniambia nimeambukizwa ugonjwa wa zinaa wakanipa dawa lakini majimaji meupe yakawa bado yanaendelea kutoka kuanzia hapo sikuweza kufanya tendo la ndoa bila Condom niliogopa kumwambukiza huyo mtu niliyekuwa naye.


Lakini dada dinah huyo mtu aliyenitoa bikra tuliachana nikapata kaka mwingine ambaye analengo la kuniona sasa dada tatizo ni kwamba tangu nikiwa form 2 hayo majimaji meupe ndiyo yalianza kutoka hadi leo ni miaka kama 7 bado yanatoka.

Nikienda hospital Dokta akinipima sionekani tatizo ila yanakuwa yananiwasha sana na kuna wakati natoka vipele. Nimetumia dawa kuanzia nikiwa form 2 hadi leo hii ila hayajaacha kutoka. Huyu kaka anayetaka kunioa nampenda ila sipendi kumuambukiza ugonjwa niliyonao? Sasa nifanyaje naomba ushauri.

Na je uwezekano wa mimi kubeba mimba upo?nampenda kweli huyu mchumba wangu na napenda anioe ila sasa nitafanyaje?nisaidie nipo katika wakati mgumu"

Dinah anasema:Pamoja na kuwa uliambukizwa Gonjwa la zinaa ambalo hujasema jina lake nadhani pia hujui Utoko ni nini. Ikiwa Daktari aligundua kuwa unatatizo na anakupa dawa ni wazi tatizo hilo lilikwisha hivyo hakukuwa na sababu ya wewe kuendelea kutumia dawa zile miaka saba baadae.

Hebu niambie kwa uwazi, maji hayo meupe yakoje? Kama maziwa yenye uzito wa cream (Utoko) au meupe kama maji ya yaliooshewa mchele (ugonjwa), meupe kama maji ya kunywa na yanatereza (ute unaojitokeza ukiwa na nyege au ukikaribia hedhi/yayi likiwa linapevuka) au meupe na yakiwa chupini huwa ya njao au kuna ukahawia kwa mbali na uzito wake kama cream(Ugonjwa).......ukinipa jibu hapa itanisaidia kukupa maelezo ya kutosha.


Sasa, hiyo hali ya muwasho na kutokwa na vipele kwa haraka haraka nadhani huenda inasababishwa na matumizi ya Condom (inategemea unatumia aina gani). Ikiwa unatumia Condom zilizotengenezwa kwa mpira wa Latex (Condom nyingi Bongo miaka ya 90s zilikuwa zikitengenezwa kwa aina hiyo ya mpira na actualy unaweza kabisa kusikia harufu ya mpira unapozitumia) hizi sio nzuri kwa watu wenye allergy.


Pamoja na kusema hivyo zipo Condoms za latex lakini hazina allergy lakini ili kujua hilo unapaswa kuzinusa, na ikiwa hazina ile harufu ya mpira basi ujue hazitokupa tatizo. Vilevile kuna Condom ambazo ni non-latex na wengi wanazipenda kwani hata material yake ni laini lakini imara na hazina harufu yeyote.


Hizi zimetengenezwa kwa kutumia Polyurethane na zinapatikana kwenye maduka Makubwa ya Madawa kila kona Dar es Salaam,hakikisha unasoma maelezo kabla ya kununua....usitegemee maelezo ya Mhudumu wa Duka la madawa (wengine hawajui au hawajali).

Kuhusu suala la wewe kupata mtoto hapo baadae nadhani lipo ikiwa Mungu atapenda iwe hivyo kwani tatizo ambalo labda ungehofia limetibiwa miaka saba iliyopita.

Nakutakia kila la kheri na Hongera sana kwa kuzingatia matumiz ya Condoms.

**Oh hey....Nipe maelezo kuhusu rangi na texture ya maji maji meupe yakutokayo ukeni ili niweze kukupa jawabu la uhakika ili uchukue hatua za haraka kwenda kuonana na Daktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake.

Wednesday, 8 July 2009

Boarding School imeniharibu, Mpenzi kakimbia-Ushauri

"Mpenda dada na wana blog wote, wasalaam!
Sitakukupotezea muda mwingi naomba sana unisaidie shida yangu hii kwani nahisi dunia yote nimebaki peke yangu!!.

Kifupi mimi ni Kijana mwenye umri wa miaka 29 Elimu yangu ni ya Chuo kikuu japo bado sijabahatika kupata kazi. Nilisoma shule ya Bweni ya wavulana pekee kuanzia Kidato cha kwanza mpaka cha sita.

Nilipokua shule tangu kidato cha kwanza nilifundishwa au kuiga tabia yakupiga punyeto (Masterburation) na ilikua ni tabia ya kawaida kabisa pale shuleni na kutokana na hilo hakika sikujua kama ina madhara yoyote.

Niliendelea kupiga punyeto kuanzia Kidato cha kwanza mpaka Kitado cha sita mfululizo na nikawa addicted kabisa. Baada ya kujua madhara yake niliamua kuacha kabisa tabia hii na hili nimeliweza.

Nilipofika chuoni niliingia kwenye uhusiano na msichana ambae nilmpenda sana na tulipendana sana. Baada ya kupima afya zetu na kukuta wote ni wazima wa afya, tulipanda siku tukaenda kutembea Zanzibar na siku hiyo ndio natuliamua tufanye mapenzi kwa mara ya kwanza.

Cha ajabu mimi mboo yangu ilisimama vizuri tu, nilipoingiza tu mboo kwenye K yake na kupampu mara mmoja nikamwaga hapo-hapo na mboo ikasinyaa!! Nilikaa muda wa zaidi ya saa mmoja ndio mboo ikasimama tena na nikajaribu kufanya tena sikuchukua zaidi ya dakika 3 nikamwaga tena!!

Hili tatizo liliendelea kujirudia mara nyingi sana katika uhusiano wetu na mpenzi wangu alikosa raha na kulalamika simlidhishi katika mapenzi. Baada ya muda akanichukia na mapenzi yakapungua na mwisho akaomba tuachane na akaniaacha!!.

Nimekaa mwenyewe muda mrefu sana na najihisi mpweke sana pia sina raha. Je naweza kupata mtu wa kunipenda katika hali hii na kuyaelewa matatizo yangu na kuangalia jinsi ya kunisaidia?

Je naweza kupata tiba ya tatizo hili? kwani hata Uume wangu umesinyaa na umekua laini na ukiamka asubuhi inakua imelala tu!1, naomba msaada wako,na Je kuna mwanamke yoyote atakuwa yuko tayari kunipenda kwenye hali?
NAOMBA MSAADA WENU WADAU.--Kulwa John"

Dinah anasema: Kulwa asante sana kwa mail yako ya uwazi kuhusu tatizo lako, kwa sasa hebu soma Makala hizi kwa kubonyeza hapa kisha hapa zinafanana kiasi na suala lako.

Nitarudi kwa ushauri zaidi....

Thursday, 2 July 2009

Can't marry me lakini anataka mtoto nami-Ushauri!

"Hakika wewe ni mwanamke jasiri..
Mimi ni msichina wa umri wa miaka 28 nimekuwa ktk uhusiano wa kimapenzi huu mwaka wa tano sasa, lakini sielewi nini cha kufanya mpaka sasa. Mpenzi wangu ni mchanganyiko wa rangi kati ya mweusi na mwarabu kwa baba.


Tunapendana tena sana tu, wazazi wake wanamwambia kuwa muda wa kuoa umefika atafute msichana aoe lakini si msichana aliyekuwa nae, thats means mimi, Alipopata habari hizo aliniambia japo roho yangu iliniuma sana lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kumwachia yeye aamue..


Ndipo baada ya mwezi mmoja aliponiomba kuwa anataka kuwa na mtoto na mimi, nilifurahi kwani napenda niwe na mtoto naye pengine hata awe mume wangu, akadai kuwa tutakapokuwa na mtoto itakuwa rahisi yeye kuwa karibu na mimi siku zote na pengine kuwa wote kabisa na hata kama ataoa ni kwa kuwaridhisha wazazi wake tu kwani yeye chaguo lake hasa ni mimi. Nikamuambia naomba muda nifikirie kwanza ili kama kufanya maamuzi yawe sahihi

Dinah sasa hapo ndio sijui nini cha kufanya:

Nafikiri niachane naye tu lakini nampenda na roho inauma sana hata ukizingatia tumevumiliana kwa mengi na pia huwa sipendi kubadili mahusiano hadi hapo inapobidi. Nahofia pindi atakapo oa, je ni kweli ataweza kuwa karibu na mimi?

Hasa atakapokuwa na huyo mkewe? Au ndio nitaishia kupata tabu na mwanangu tu? Maana si unajua mtu akishakuwa na mke tena hasa hawa wenzetu waarabu bila shaka huyo mkewe atakuwa mwarabu pia. Naomba ushauri wako ambao utanitoa hapa kigazini nilipo."

Dinah anasema: Pole kwa unayokabiliana nayo. Haya hutokea sana kwenye jamii nyingi tu za Kiafrika na sio Waarabu peke yao. Kabla sijaendelea naomba nikuulize swali.....hao wazazi wake wanajua kuwa wewe ni mpenzi wake?

Unayokumbana husababisha wanaume wengi kuamua kuoa mara mbili, ndoa ya kwanza kulidhisha wazazi na ya pili ni kwa mapenzi yake na hufanya siri bila wazazi wao kujua. Hapo hutafuta visa kama vile kunyima tendo la ndoa, kutorudi nyumbani mapema, kutokua chakula kipikwacho nyumbani, kutoongea nao, kutotembea nao n.k.

Hali inayopelekea mke huyo aliyechaguliwa kuomba Talaka, na hili likitokea Bwana anakuwa huru kutangaza ndoa nyingine ambayo tayari alikuwa ameshafunga sambamba na ile ya mke wa "kutafutiwa" na wazazi.

Huyu bwana inaelekea hata yeye amechanganyikiwa kama wewe ulivyochanganyikiwa na kweli anakupenda ndio maana anatumia njia ya kuzaa na wewe ili usijekuwa na mtu mwingine na akakukosa. Lakini, pamoja na nia yake njema bado utakuwa umezaa nae nje ya ndoa pia utakuwa ni Kimada na sio Mke pamoja na kuwa wewe ndio ulikuwa wa kwanza kuwa nae ktk uhusiano wa imapenzi.

Wewe hukupaswa kumuachia mzigo wote yeye peke yake ili afanya uamuzi (kosa kubwa ulifanya hapa), Wote wawili mlipaswa kulijadili suala hilo zito na kufanya maamuzi ya busara hasa ukizingatia mmekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.


Kitendo ulichokifanya kimemrahisishia yeye kufanya uamuzi logically zaidi na si kihisia na ndio maana akaja na suala la kukumimba ili aendelee kuwakaribu na wewe bila kuangalia hiyo itakuathiri vipi wewe Kihisia, Kimwili na Kisaikolojia.


Natambua ulipomuachia jukumu hilo ulitegemea yeye kukuambia kuwa hajali wazazi wake wanataka nini, atakachofanya ni kufunga ndoa na wewe, hata ikiwezekana kuhama mahali hapo na kupotea kabisa lakini awe na wewe............mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na mwenye kujali hisia za mpenzi wake hakika angefanya hivyo na sio kuja na suala la kuzaa na wewe lakini kuoa anaoa mtu mwingine.


Nakubaliana na ufikiriavyo, kwamba ni heri muachane tu. Ikiwa hili ndio utakalo basi fanya haraka iwezekanavyo kabla hujapoteza muda zaidi. Natambua inauma sana......maumivu hayo ni ya kawaida kwa yeyote anaeachana na mpenzi wake ampendae, iwe kwa kugombana au kwa kuelewana bado maumivu ni yale yale lakini kutokana na tofauti zenu kubwa inabidi iwe hivyo.

Kuzaa nae ni sawa sawa na kuzuia baraka na bahati kutoka kwa wanaume wengine wazuri out there, sio wanaume wote watakuwa tayari kulea mtoto wa mwanaume mwingine na si dhani kama huyo bwana ataendelea kuwa karibu nawe the way anaahidi sasa. Kama kweli anataka kuzaa na wewe basi mfunge ndoa as simple as that!

Ukimuacha kabla yeye hajafanya hivyo itakuwa vema kwani utamuonyesha kuwa wewe ni mwanamke mwenye msimamo, unajiamini na unajua unataka nini maishani mwako. Unataka kuendesha maisha yenye amani na furaha, unataka kuthaminiwa, kushehimiwa, kupendwa na siku moja kuolewa na kuwa mama, sio kuwa mama na wakati huo huo Kimada.

Miaka 28 bado unamuda mzuri tu wa kukutana mwanaume mwenye kujali hisia zako, atakaepigana kwa ajili yako bila kujali ni nani hasa anataka kujiingiza kwenye maisha yenu ya kimapenzi.

Mungu akujaalie ktk maisha yako na siku moja utafunga ndoa na mwanaume mwenye kufuata Moyo na kufanya uamuzi yeye kama mwanaume kamili na sio kuamuliwa na Wazazi wake.......
Kila la kheri!